Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA NOVEMBA 14, 2017

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dk. Tulia Ackson akitoa majibu ya miongozo  mbalimbali  ya wabunge  wakati  wa Mkutano wa tisa wa kikao cha sita  cha  Bunge hilo leo Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk Ndugulile  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge  wakati wa Mkutano wa tisa kikao cha sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dk. Harrison Mwakyembe  akisoma kauli yake kuhusu fursa kwa wasichana kujipima uwezo katika riadha ili waweze kuiwakilisha nchi katika mashindano yajayo ya kimataifa ya Jumuiya ya Madola, Olimpiki, All-African games na mengineyo leo Bungeni mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiteta jambo na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso wakati wa Mkutano wa tisa kikao cha sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe.Dk. Mary Mwanjelwa wakati wa Mkutano wa tisa kikao cha sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Dodoma.
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.


TRA YAONGEZA UFANISI WA UKUSANYAJI KODI YA MAJENGO

$
0
0
Serikali imesema mapato yatokanayo na kodi ya majengo yanayokusanywa na Serikali yameongezeka baada ya jukumu hilo kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ikilinganishwa na ilivyokuwa chini ya Halmashauri.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Bukoba Mhe. Wilfred Lwakatare (CHADEMA), aliyetaka kujua Serikali inazipa Halmashauri ushauri gani wa kitaalam wa hatua za kuchukua ili kuziba pengo la kibajeti.

Katika swali hilo Mhe. Lwakatare aliuliza kuwa Serikali haioni kuwa uamuzi wa kuipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kukusanya kodi hiyo ya majengo ni kuzidi kuipa mzigo mkubwa ambao hawatauweza.

Dkt. Kijaji alisema kuwa baada ya makusanyo yatokanayo na kodi za majengo kuanza kukusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA katika Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji 30, yalipanda hadi kufikia Sh. bilioni 34.09 mwaka wa fedha  2016/2017 ikilinganishwa na Sh. bilioni 28.28 zilizokuwa zimekusanywa na Serikali za Mitaa mwaka wa fedha 2015/2016.

“Makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la asilimia 20.6 ya makusanyo halisi yaliyopatikana kutoka Halmashauri husika kabla ya kodi hiyo kuhamishiwa TRA hali inayodhihirisha kuwa, TRA imefanya kazi nzuri katika kukusanya mapato ikilinganishwa na kiasi kilichokusanywa na Halmashauri hizo 30 katika mwaka wa fedha 2015/16.”. alisema Dkt. Kijaji.

“Katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18 Julai hadi Septemba, TRA, ilipangiwa kukusanya kodi ya majengo ya kiasi cha Sh. Bil 11.9 na kufanikiwa kukusanya kiasi cha Sh. Bil. 13.2 ikiwa ni ufanisi wa asilimia 111”.  Aliongeza Dkt. Kijaji.

 “Hatua ya Serikali ya kukasimu jukumu la ukusanyaji wa kodi za majengo kwa TRA, haikulenga kuzinyang’anya Halmashauri vyanzo vya mapato bali ni kuimarisha ukusanyaji wake”. alisema Dkt. Kijaji.

Aliongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kunakuwepo ufanisi katika ukusanyaji na matumizi ya kodi zote zinazokusanywa ndani ya Serikali na kwamba Halmashauri zote zinapata mgao wa fedha kwa kuzingatia makisio ya bajeti zao na makusanyo ya mapato yote ya Serikali.

Aidha, Dkt. Kijaji alisema kuwa Serikali inatambua kuwa kodi ya majengo imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa mapato ya Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji katika kutekeleza mipango na utoaji wa huduma na maendeleo kwa wananchi.

Katika swali la nyongeza Mhe. Lwakatare alihoji kwa nini Serikali isichukue maoni yake ya baadhi ya majengo makubwa yatozwe kodi na TRA na yale madogo yatozwe kodi na Halmashauri kwa kuwa kumekuwa na changamoto kwa TRA katika ukusanyaji wa kodi hiyo na kuwatumia Maafisa Watendaji wa Kata katika kukusanya kodi hizo ambao wameajiriwa na Halmashauri.

Akijibu swali la nyongeza Dkt. Kijaji amesema kuwa Serikali na Bunge lilipitisha sheria ya fedha kwamba kodi ya majengo ikusanywe na TRA kwa lengo la kuimarisha ufanisi wake katika ukusanyaji na matumizi.

“Serikali itaendelea kusimamia sheria hiyo na kuhakikisha lengo la kuchukua kodi hiyo linafanikiwa na wananchi wanapata huduma stahiki”. aliongeza Dkt. Kijaji.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)​

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.

Katika mkutano huo ambao unazikutanisha sekta Serikali na Sekta binafsi kutoka nchi wanachama, Makamu wa Rais alisisititiza kuwa pamoja na kuelekea kwenye kujenga Afrika Mashariki ya Viwanda ni muhimu viwanda hivi vitumie malighafi zinazozaliwa ndani ya Afrika Mashariki.

Makamu wa Rais alisema kujenga uchumi wa viwanda uendani na maboresho ya sera ya viwanda ili itoe uwanja mpana wa kuajiri vijana wengi zaidi.

Makamu wa Rais alihimiza kuwa Viwanda vitakavyojengwa viende sambamba na kilimo kwani kwa pamoja ndipo tunaweza ona mafanikio na ukuaji wa uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa Ujumla.

Makamu wa Rais alimalizia kwa kusema kuwa Serikali na Sekta binafsi zinawajibu kushirikiana katika kuandaa mazingira mazuri ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.

MDAU MUGANYIZI BISHEKO ACHUKUA JIKO

$
0
0
 Mdau Muganyizi Bisheko na mkewe Bi. Brenda Ngowo pamoja na wapambe wao, wakiwa na furaha baada ya kufunga ndoa katika Kanisa la Bungo KKKT, Morogoro tarehe Novemba 4, 2017 
Mdau Muganyizi Bisheko na mkewe Bi. Brenda Ngowo wakiwa ni wenye furaha baada ya kufunga ndoa Novemba 4, 2017 katika Kanisa la Bungo KKKT, Morogoro.

MICHUZI TV: WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WACHANGIA MILIONI 15 UJENZI WA OFISI ZA WALIMU JIJINI DAR

TAKUKURU yatangaza zawadi nono kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa mhasibu wake

$
0
0
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bregedia John Mbung’o akizungumza na waandishi wa habari kuhusu atakayewezesha kupatikana  kwa aliyekuwa mhasibu wa taasisi hiyo, Godffrey Gugai anayedaiwa kujilimbikizia mali.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bregedia John Mbung’o akionesha picha ya aliyekuwa mhasibu wa taasisi hiyo, Godffrey Gugai  kwa waandishi wa habari leo JIjini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko
Taasisi ya kuzuia na kupamabana na rushwa nchini (TAKUKURU) imetengaza zawadi nono ya shilingi milioni kumi kwa mtu atayewezesha kupatikana kwa aliyekuwa mhasibu wa taasisi hiyo, Godffrey Gugai anayedai kuwa na ukwasi mkubwa wa fedha na mali isiyolingana na kipato chake halali akiwa kama mtumishi wa umma.
 Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bregedia John Mbung’o amesema, baada ya kuchunguza na kutoa taarifa ya awali walimuita Gugai na kumuhoji ambapo alionyesha ushirikiano wa kujibu hoja hizo zinazomkabili na kuwa na mali nyingi kuliko kipato chake
Amesema, kwa mujibu wa kifungu cha 27 cha sheria ya Kuzuia na kupaambana na Rushwa ni kosa la jinai kwa afisa wa serikali au mtumishi wa umma kuwa na mali nyingi au maisha ambayo yanazidi kipato chake bila ya kuwa na maelezo yoyote anayoelezea mali zile amezipata wapi au kwa namna gani.
“Bwana Gugai aliweza kujikusanyia mali nyingi ambazo awali tulijaribu kumuuliza na alielekea kuonyesha ushirikiano lakini baadae alipoona kwamba hana maelezo ya namna gani amezipata zile mali akapotea. tumeendelea kumtafuta na taarifa ambazo tumekuwa tukizipata amekuwa ni mtoro amekimbilia nje ya nchi kupitia njia ambazo siyo rasmi” amesema Bregedia Jenerali Mbung’o.
Mhasibu huyo anamiliki maghorofa saba, nyumba za kawaida tisa, magari matano na pikipiki pamoja na viwanja 37.
 Amesema ni kosa kubwa kwa mtumishi wa umma kutumia ofisi yake kujipatia mali  nje ya kipato akipatacho ni kosa, aliwahi kuchukuliwa maelezo, alipogundua hana maelezo sahihi akaamua kukimbia.
Maghorofa, nyumba za kawaida na viwanja vya mhasibu huyo viko kwa mtawanyiko katika maeneo mbalimbali nchini yakiwamo ya ghali karibu na bahari, Kigamboni na Mbweni jijini Dar es Salaam na pia Bagamoyo mkoani Pwani. Kwingineko kuliko na mali hizo ni Kinondoni (Dar), Musoma, Nyegezi, Kiseke jijini Mwanza, Arusha na Tanga
Hata hivyo, mali za Gugai zimewekewa zuio la mahakama na mawakala wake na watu wengine wote wanaomwakilisha wamezuiwa kuuza au kuhamisha umiliki au kuweka dhamana mali zote zilizowekewa zuio.

 Pia Msajili Msaidizi wa magari ameagizwa asiruhusu uhamishaji wa umiliki wa vyombo vya moto vilivyowekewa zuio mpaka mahakama itakapoelekeza vinginevyo.
mwisho

VODACOM YATANGAZA KUFANYA VIZURI NUSU YA KWANZA YA MWAKA

$
0
0
Vodacom Tanzania PLC (“Vodacom”) leo imetangaza matokeo ya uendeshaji ya  hesabu zake kwa nusu ya mwaka ulioishia Septemba 30, 2017. Kampuni hiyo imetangaza kuimarika kwa matokeo ya biashara ukijumwisha Matokeo ya biashara yalikuwa mazuri ikiwemo ukuaji wa mapato ya huduma, ambayo kwa pamoja yalisababishwa na ukuwaji wa huduma za fedha za M-Pesa na data. Mapato ya huduma nayo yalikua Mtiririko wa fedha huru umekuwa kwa asilimia  kwa asilimia 73.2 hadi shilingi bilioni kufikia  58.3 katika billion kwenye kipindi hicho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom’s, Bw. Ian Ferrao alisema mwaka , “2017 umekuwa ni mwaka muhimu kwa Vodacom Tanzania. Kwa miezi ya hivi karibunindani ya miezi, zoezi la uuzaji wa tumekamilisha mauzo ya toleo la awali la za awalihisa (IPO), ambalo lilikuwailiyokuwa ni kubwa zaidi katika historia ya soko la hisa la Dar es salaam (DSE) nchini; ku tume  fanya mkutano wetu mkuu wa kwanzawa mwaka, tukiwa kama kampuni ya umma.Na tumetangaza gawio la kwanza kama kampuni iliyoorodheshwa na soko la hisa la Dar es Salaam kutokana na mikakati tuliyojiwekea tumepata matokeo chanya yaliyochagizwa na kasi ya kibiashara,ukuaji thabiti wa mapato yatokanayo na data,M-pesa,na huduma kwa taasisi mbalimbali.Vilevile, biashara yetu imeleta matokeo chanya kutokana na uwezo wa kibiashara na ukuaji wa mapato kwa upande wa data, M-Pesa na huduma nyingine”.

Mkurugenzi huyo alifafanua zaidi kuhusiana na matokeo chanya ya kibiashara nakusema kwamba,“Matokeo haya ya muda mfupi yanatia moyo kwani yanaonyesha kuwa kwamba huduma yetu bora ya mtandao wa hali ya juu kama vile M-Pesa na huduma nyingne zinazozingatia matakwa ya wateja,vilisaidia kukuza biashara ndani katika hali ya ushindani mkubwa wa soko. 
Pamoja na changamoto za kibiashara nchini Tanzania, kuimarisha ukuaji wa tumeweza kudumisha mapato nakukuza  kukuza idadi ya wateja, kuendelea kushikilia nafasi yetu kama kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za simu za mkononi na za kifedha. Hali mafanikio haya hiyo ni matokeo ya kuendelea kwa uwekezaji pale uliinapohitajika tulioufanya katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.  Uwekezaji huo umewezeshaumesaidia ongezeko la kuongeza wigo wa huduma zetu, na kutuweka kwenye nafasi ya mbele kwa upande wa huduma za kifedha na data.
Katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka huu wa fedha, Vodacom imewekeza kiasi cha shilingi bilioni TZS 102.4 bn katikakupanua wigo wa  kuongeza mtandao. “Uwekezaji  huuwa mtandao wetu ulilenga zaidi kuongeza wa mtandaouwezo. Tuliongeza uwezo wa huduma ya data ya 3G kwenye minara yetu iliyopo kwenye miji mikubwa kwa zaidi ya asilimiakw 25 katika miji mikubwa, wakati huo huo tukizindua huduma ya 4G kwenye majiji matatu, na kuboresha huduma hiyo kwenye jiji la Dar es Salaam. 

Kwa kushirikiana na wabia wetu za gharama nafuuKampeni yetu ya simu rahisi za mkononi za kisasa “Smartphone” ilifanikiwa sana, kwani ushahidi umeonyesha kwamba ilikua Ukuaji wa idadi ya wateja hadi kufikia asilimia 27 ya soko la simu . Wakati tumeingiaTunapoingia katika  nusu ya pili ya mwaka wetu wa fedha, tutaendelea kukuza huduma na matumizi ya data ikiwemo kwa simu zisizo ambazo sio Smartphones na walekwa wateja  wanaotumia kiwango kidogo cha data.

 Kwa kupitia lengo letu la kuongeza wigo wa huduma, tutaendelea kuwa kwenye nafasi ya kwanza dhidi ya washindani wetu katika kiwangoKwa kutilia mkazo ubora wa mtandao na huduma kwa wateja,tutadumisha nafasi yetu kama kinara wa huduma bora iliyokubalika zaidi na wateja na kuendelea kushirikilia usukani dhidi ya washindani wetu cha juu,” alisema Ferrao.

AZAM FC KUSHUSHA VIFAA VIWILI, KUSAJILI KUZIBA PENGO LA YAHYA MOHAMED

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa klabu ya Azam umepanga kufanya usajili wa mchezaji mmoja wa kigeni kutoka katika nchi za  Ghana na Zambia ambapo wanatarajia kushusha wawili ili kupata straika mmoja kati yai atakayemrithi Yahaya Mohamed.

Mapema mwezi huu, uongozi wa timu hiyo ulivunja mkataba na mshambuliaji wake Yahaya Mohammed ukiwa unakaribia mwaka mmoja tangu alipojiunga na timu hiyo kwa kile kinachodaiwa ni kushindwa kuonyesha kiwango kizuri tangu ajiunge na timu hiyo.

Azam FC imefikia makubaliano ya pamoja na mchezaji huyo raia wa Ghana na tayari wamemkabidhi barua ya kumruhusu kuondoka klabuni hapo.


Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba, wiki ijayo uongozi wa Azam utamwagiza wakala wao wa kufuatilia wachezaji wa nje ya nchini kwa ajili kwenda Ghana na Zambia kufuatiliwa wachezaji hao na iwapo ataridhishwa na mmoja kati yao basi atarudi naye kwa ajili ya kujiunga nao.

“Baada ya kuachana na straika wetu Yahya Mohamed, kocha amependekeza kati ya wachezaji wawili kutoka Ghana na Zambia ili aweze kumpata mmoja wao kwa ajili ya kuziba nafasi ya huyo aliyeondoka,”alisema.

Wakati huo huo, Jafari alisema, kikosi cha Azam kinatarajiwa kuondoka kesho kwenda Njombe kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Njombe Mji, mchezo wa raundi ya 10 wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Jumamosi hii kwenye uwanja wa Sabasaba.

Alisema, kikosi cha wachezaji 22 akiwemo na Stephane Kingue ambaye alikuwa majeruhi, kinatarajiwa kuondoka kikiwa pamoja na viongozi wa benchi za ufundi kwa ajili ya kwenda mjini humo.

“Timu inaondoka mapema kwa ajili ya kwenda kuzoea mazingira ya baridi na Njombe ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuwavaa wenyeji Njombe Mji kwenye mchezo huo,” alisema Jaffar.

TAIFA STARS YAREJEA DAR, KUSUBIRI MAANDALIZI YA CHALLENJI

$
0
0
Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imereja alfajiri ya leo salama kutoka nchini Benin walipokuwa wameenda kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin.

Stars iliyokuwa ugenini iliweza kutoka sare kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wenyeji Benin uliofanyika Uwanja wa La Amitie jijini Continou na kutoka sare ya 1-1.

Mara baada ya kurejea, kambi ya Stars ilivunjwa kwa wachezaji kusafirishwa kwenda kwenye timu zao kadiri ya makubaliano kuanza maandalizi ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom, Tanzania Bara inayoendelea mwishoni mwa wiki.

Safari hii Stars imecheza mechi yake bila nyota wake wanne wakiwamo Erasto Nyoni na Muzamiru Yassin ambao walikuwa wanatumikia kadi nyekundu huku Nahodha wa timu, Mbwana Samatta na Kiungo mahiri, Farid Mussa ambao ni majeruhi.

Taarifa kutoka Genk ya Ubelgiji, zinasema kwamba Mbwana Samatta amefanyiwa upasuaji mdogo katika goti la kulia na mpaka kupona, itamchukua hadi wiki nane ili kurejea uwanjani.

Wachezaji waliorejea ni Aishi Manula, Peter Manyika, Gadiel Michael, Boniphas Maganga, Kelvin Yondani, Nurdin Chona, Himid Mao, Hamis Abdallah, Raphael Daudi, Mohamed Issa, Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Faridi Mussa, Ibrahim Ajib, Mbaraka Yusuph na Elias Maguli.

Wakati huo huo, kambi ya timu ya Taifa ya Vijana Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 23 ‘Kilimanjaro Warriors’ inatarajiwa kufikia ukomo Alhamis Novemba 16, mwaka huu.

Timu hiyo yenye wachezaji 34 kutoka timu mbalimbali za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzana Bara, ipo kambini kwa ajili ya mchujo wa kupata wachezaji wasiozidi 25 watakaunda kikosi kamili cha vijana wenye umri wa chini ya miaka 23.

Kadhalika, Serengeti Boys – Timu ya Taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, wanatarajia kuingia mwishoni mwa mwezi huu kujiandaa na michuano ya kuwania Kombe la Chalenji kwa vijana itakayofanyika Burundi kuanzia Desemba 12 hadi 22, mwaka huu.

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA PAMOJA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA HUAWEI TANZANIA.

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne – Marie Kaarstad (katikati) pamoja na Msaidizi wake katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne – Marie Kaarstad (kulia) alipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Technologies Tanzania, Ndg. Gao Mengdong (katikati) na Msaidizi wa Mkurugenzi, Ndg. Kyle Ma (kulia) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Technologies Tanzania, Ndg. Gao Mengdong pale alipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja  na ugeni kutoka ubalozi wa Norway ulioongozwa na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne – Marie Kaarstad (wa pili kulia) walipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WATANZANIA WATAKIWA KUPATA VIPIMO VYA KITAALAM KABLA YA KUTUMIA DAWA.

$
0
0
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
WATANZANIA wanatakiwa kwenda vituo vya kutolea huduma za afya kupata vipimo kutoka kwa wataalam kabla ya kutumia dawa kwa mazoea ili kuepuka usugu wa vimelea vya wagonjwa kwenye miili yao na kusababisha vifo vya mara kwa mara.

Hayo yamezungumzwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mradi wa kupambana na usugu wa vimelea kutoka Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) Dkt. Raphael Sallu wakati wa semina na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

“Tatizo la kutumia vijiuasumu(Antibiotics) bila ya kupata vipimo na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya limekua kubwa ambalo linasababisha madhara ya kiuchumi na uhai kutokana na kuzidiwa na vimelea vya ugonjwa ambavyo vinakua sugu kutokana na matumizi mabaya ya dawa hapa nchini” alisema Dkt. Sallu.

Aidha, Dkt. Sallu amesema kuwa elimu ya kutumia dawa bila ya kupata ushauri na vipimo kutoka kwa wataalamu wa afya ianze kutolewa kuanzia ngazi za shule ya msingi na ngazi ya jamii kwa ujumla.

Mbali na hayo Dkt. Sallu amesisitiza kuwa wanahabari wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kuelimisha umma umuhimu wa kutumia dawa kwa kufuata ushauri kutoka kwa wataalam kuhusu ugonjwa unaomsumbua pamoja na matibabu yake.
Mwakilishi Mkuu wa mradi wa kupambana na usugu wa vimelea (FAO) Dkt. Raphael Sallu akiwasilisha mchango wake wakati wa semina na Waandishi wa habari kuhusu matumizi bora ya Antibiotic, ilofanyika katika ofisi za FAO jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Taifa wa mradi wa kupambana na usugu wa vimelea katika Shirika la chakula na kilimo duniani (FAO) Dkt. Bachana Rubegwa (aliesimama) akieleza maudhui ya semina hiyo niliyofanyika mapema leo katika ofisi za FAO jijini Dar es Salaam.

 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa kupambana na usugu wa vimelea vya ugonjwa Bi Rose Shija akiwasilisha mchango mbele ya wadau wa habari, pembeni yake ni Afisa Habari wa Wizara ya Afya Catherine Sungura.
 Mmoja ya wadau wa Habari ambae pia ni mmiliki wa Blog ya Full Shangwe akitoa mchango mbele ya wadau wenzie wa habari na wawakilishi wa Mashirika ya kimataifa katika Semina ya kuhamasisha matumizi bora ya antibiotic.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436

$
0
0
Dares Salaam, Novemba 14, 2017: Sweden imeipatia Tanzania Msaada wa jumla ya Fedha ya Sweden SEK. Bilioni 1.64 ambayo ni sawa na takribani Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu. 

Makubaliano ya msaada huo yamesainiwa Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting.

Bw. James alisema kuwa imesainiwa Mikataba mitatu ya msaada huo ambayo ni; mkataba kwa ajili kusaidia Bajeti ya Serikali wa kiasi cha SEK milioni 600 ambazo ni sawa na Sh. bilioni 159.59 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2019/2020, ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 watatoa takribani Sh. bilioni 53.20.

Alisema fedha hizo zitaelekezwa katika kuboresha uhalisia wa Bajeti ili kuweza kutimiza majukumu ya kisera, kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ya kikodi na yasiyo ya kodi na pia kusaidia Serikali kutoa huduma nzuri kwa wananchi kupitia taratibu za manunuzi. 

Mkataba mwingine ni kwa ajili ya kusaidia Mpango wa Elimu kwa Matokeo (EPforR) wa kiasi cha Fedha ya Sweden SEK milioni 885 ambayo ni sawa na Sh. bilioni 235.40 kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2020/2021.

“Lengo la msaada huu ni kusaidia Mpango wa Elimu kwa Matokeo ambapo tunapimwa namna ambavyo tumeweza kutimiza wajibu wetu tuliojiwekea katika bajeti. Baada ya ya Serikali kutimiza wajibu wake wa kupeleka fedha katika Sekta ya Elimu kwa wakati, wameamua kutupatia fedha hizo ambazo Serikali tunazipangia kazi kulingana na vipaumbele”, alieleza Bw. James.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (wa pili kushoto) wakisaini Makubaliano ya Msaada wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia)na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (kushoto) wakisaini Makubaliano ya Msaada wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (kushoto) wakiwa wameinua juu Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Maafisa waandamizi kutoka Ubalozi wa Sweden Nchini Tanzania wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

TANESCO YATOA MILIONI 10 KUSAIDIA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO WALIOLAZWA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, (JKCI)

$
0
0

 Meneja Mwandamizi  wa Shirika la umeme nchini, TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (wapili kushoto), na wafanyakazi wenzake, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, akikabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 10, kwa Mkurugenzi Myendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Profesa Muhammed Janabi, (mwenye miwani), katika hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 14, 2017. Msaada huo w afedha utawezesha matibabu ya moyo kwa watoto watano waliolazwa kwenye taasisi hiyo.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limetoa msada wa Shilingi milioni 10 kusaidia matibabu ya watoto wanaougua maradhi ya moyo kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam leo Novemba 14, 2017.

Akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya alisema, baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Taasisi hiyo inahitaji msaada ili iweze kuwafanyia upasuaji watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia matibabu hayo, uongozi wa TANESCO ulisikia maombi hayo.

Kwa kawaida upasuaji kwa motto hugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 2.
“Tumekuwa na uhusiano mzuri na Taasisi yako, kwa hivyo japo hatuna uwezo mkubwa lakini Mkurugenzi Mtendaji aliona ni vema tutoe msaada wa kuwezesha upasuaji wa watoto watano, na leo tutakabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10.” Alisema Mhandisi Mgaya katika hafla ya kukabidhi hundi hiuyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa JKCI, Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Aidha Mhandisi Mgaya alisema mbali na msada huo wa fedha, TANESCO pia imeondoa tatizo la upatikanaji wa umeme wa kutosha kwenye taasisi nhuyo kwa kuwawekea huduma maalum ili kuhakikisha umeme unapatikana bila ya shida yoyote.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakayab Kikwete, Profesa Mohammed Janabi, alisema ili kuenzi msada huo wa TANESCO, mmoja wa watoto watakaofaidika na msada huo atapewa jina la TANESCO.

“Tutawaalika katika hatua ya mwamzo kabla ya upasuaji ili muone hali halisi ya mgonjwa na baada ya upasuaji na tutamuita TANESCO motto huyo.” Alisema Profesa Janabi wakati akitoa shukrani zake.

Naye Daktari bingwa wa moyo kwa watoto, Dkt. Naiz Majani alisema kwa mwaka Taasisi hupokea wagojwa wanaohitaji upasuaji kiasi cha 200,000, kwa hivyo msada huo na minbgine kutoka kwa wasamaria husaidia pakubwa katika kuokoa maisha ya watoto wa Kitanzania.

“Tunawashukuru sana kwa msada wenu na tunaomba muendelee kusaidia jamii katika kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapatriwa matibabu ya moyo hata kama uwezo wao ni mdogo.” Alisema Dkt. Majani.Katika hatua nyingine wafanyakazi wa TANESCO wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto waliolazwa kwenye taasisi hiyo wanaosubiri kufanyiowa upasuaji.


 Mhandisi Mgaya na Profesa Janabi, wakimsikilzia Mwenyekiti wa TUICO, Tanesco, Bw.Hassan J.M Athumani, wakati akitoa shukrani.
 Profesa Janabi (kulia), akimkabidhi jarida la taasisi hiyo, Mhandisi Mgaya

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

PROF KAMBI AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA WADAU WA SEKTA YA AFYA NCHINI

$
0
0
--
 Mganga Mkuu wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof  Mohamed Kambi  akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la  nne la Wadau wa Sekta ya Afya nchini lililofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, ambalo lilipata fursa ya kujadili jinsi ya kuboresha utoaji wa huduma katika sekta ya Afya Tanzania.
 Rais wa Kongamano laNne la Wadau wa Sekta ya Afya nchini, DK Omari Chilo akizungumza kabla ya kumaribisha mgeni rasmi wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la nne la wadau wa sekta hiyo lililofanyika Jijini Dar es Salaam leo.
Kiongozi Mkuu wa  HDIF, David McGinty akizungumza katika Mdahalo wa mabadiliko ya Sayansi Ubunifu na Sera katika kuboresha utoaji wa huduma za Afya wakati waKongamano la nne la wadau wa Sekta ya Afya nchini

Mratibu wa wa Kongamano la 4 la Sekta ya Afya nchini Dr Peter Maduke akizungumza wakati wa kongamno hilo likiwa linaendelea katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


KAMPUNI YA BIMAA YA UAP YATOA FIDIA KWA WAATHIRIWA NA JANGA LA MOTO SOKO LA SIDO MKOANI MBEYA

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala (kushoto) akimkabidhi mteja wa bima ya Kampuni ya UAP Ndugu Godi Sanga kama fidia kutokana kukumbwa na janga la moto la kuungua kwa Soko la Sido Agosti 15 ,2017
Mteja wa Kampuni ya UAP akikabidhiwa mfano wa hundi ya malipo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala ,ambapo kampuni hiyo ya bima imekamirisha kulipa fidia hizo kwa wateja wake ambapo zaidi ya shilingi milioni 250 zimelipwa huku kiwango cha chini kulipwa katika fidia hiyo ni shilingi milioni Saba huku mteja wa juu kulipwa ni shilingi milioni 180.
Mkurugenzi Mtendaji wa UAP Mick Itunga akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi wateja wa kampuni ya bima ya UAP jana Nov 14 katika viwanja vya soko la Sido jijini mbeya ambapo amesema kuwa UAP ni kampuni kongwe katika sekta ya Bima duniani kwa miaka zaidi ya 170 ambapo amesema kampuni hiyo ndiyo yenye mtaji mkubwa wa Bima Tanzania ikiwa na zaidi ya shilingi Bilioni 20. Aidha Mkurugenzi huyo pia ametumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara wa mbeya kuendelea kuiamini UAP kama bima bora nchini nakwamba itakuwa mstari wa mbele mara wanapokutwa na majanga ya moto kama yaliyotokea katika soko hilo la Sido jijini Mbeya.
Mfanyabiashara wa Soko la Sido jijini Mbeya Ndugu Godi Sanga ambaye ni mteja wa Bima ya Kampuni ya UAP akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya malipo kutoka kwa kampuni hiyo ya Bima ambapo ametumia fursa hiyo kuishukuru kampuni hiyo kwa kumlipa fidia yake sanjali na kuwataka wafanyabiashara wenzake kuhakkisha wanajinunga na makampuni ya bima ili kujiwekea usalama wa biasahra zao.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika Picha ya pamoja na wadau wa bima.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa

$
0
0
aziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa alieambatana na wawekezaji wa Kichina walioonesha nia ya kuwekeza katika mkoa wa Iringa.

katika Ziara hiyo, Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe Bi. Amina Masenza ameelezea mikakati iliyopo katika mkoa wake ya kuhakikisha anapokea wawekezaji na kuwapatia maeneo ya kujenga Viwanda ili kuhahakisha wananchi wanaajiriwa kukuza kipato chao.

Mhe. Waziri amesifu jitihada zinazofanywa na Viongozi wa Mkoa wa Iringa katika kuhakikisha wanahimiza ujenzi wa Viwanda na kushirikiana na wawekezaji.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (Mb) akimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Bi, Anna Masenza.
Wawekezaji walioonesha nia ya ya kuwekeza katika Mkoa wa Iringa, wakisikiliza kwa makini majadiliano yakiendelea katika ofisi ya Mhe. Waziri wa Viwanda.
Wajume kutoka Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakati wakujadili masuala mbalimbali ya uwekezaji katika mkoa wa Iringa.

Bunge lapitisha Muswaada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano ya Simu Tanzania ya Mwaka 2017

$
0
0
Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswaada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano ya Simu Tanzania ya Mwaka 2017 (The Tanzania Telecomunications Corporation Bill, 2017) mapema leo mjini Dodoma ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na Serikali kuimrisha sekta ya Mawasiliano.

Akizungumza wakati akijibu hoja za Wabunge waliochangia muswada huo Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa kuanzishwa kwa Shirika hilo kutawanufaisha wananchi walio wengi hasa wanaoishi maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma ya mawasiliano ya simu hali itakayochochea kukua kwa uchumi nchini.

“Kuanzishwa kwa Shirika la Mawasiliano ya Simu Tanzania kutawanufaisha Watanzania wote kutokana na fursa zitakazojitokeza katika maeneo yote ya nchi yetu zikiwemo ajira kwa kuwa Shirika hili halitabagua Watanzania katika swala la ajira ilimradi mhusika ana sifa stahiki ” Alisisitiza Prof. Mbarawa

Akifafanua amesema kuwa kuwepo kwa Shirika hilo kutasaidia kuimarisha ushindani katika sekta ya Mawasiliano hapa nchini kwa kuwa Muundo wa shirika hilo utabadilika na hata utendaji wake utajikita katika kuongeza tija na kulinda maslahi ya Taifa.

Aliongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kuona kuwa shirika hilo linafanya kazi kwa tija na kuzalisha faida hali itakayopelekea Serikali kupata gawio kutokana na faida iliyozalishwa.Aidha Prof. Mbarawa amesema kuwa Serikali imepokea maoni ya wabunge kuhusu kuongeza mtaji wa Shirika hilo ili liweze kuongeza tija katika kutoa huduma kwa wananchi.

Bunge limepitisha Muswaada wa Sheria ya Kuanzishiwa kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2017 ambapo Shirika hilo pamoja na mambo mengine litakuwa na jukumu la kuimarisha mawasiliano nchini, kulinda Usalama, kukuza uchumi na masuala ya Kijamii.

sababu zilizomfanya lau masha aamue kuvua gwanda

RC GEITA ATOA ONYO KALI KWA VIONGOZI WA VIJIJI, KATA NA TARAFA WANAOTUMIA MICHANGO YA WANANCHI KWA MASLAHI BINAFSI

$
0
0
Viongozi wa vijiji, kata na tarafa Wilayani Bukombe wametakiwa kutumia michango inayotolewa na wananchi kwa shughuli zilizokusudiwa ili kuwaletea wananchi maendeleo katika maeneo yao.

Akizungumza katika kijiji cha Kazibizyo kata ya Ng'anzo Wilaya ya Bukombe Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita amesema katika  vijiji, kata na tarafa wananchi wamekuwa wakihimizwa kujitolea kuchanga michango ya hiari ili kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo lakini baada ya michango hiyo kukusanywa inatumika kwa maslahi binafsi ya Viongozi.

Amesema kuwa Viongozi hao wasio na maadili  wanapanga matumzi ya fedha za wananchi bila kujali vipaumbele vya vijiji kwa maslahi yao binafsi vitendo hivyo vinawavunja moyo wananchi wa kutoendelea kutoa michango ya maendeleo. "Kuna vidudu vinavyoleta magonjwa watu wanasubili maendeleo hayatokei inabidi tuvitoe tuvipige sindano kubwa vife humu humu viongozi wa namna hiyo wasio na maadili wamekuwa wakihamishwa wakati hawajatoa taarifa za mapato na matumizi alah! kama yupo Geita arudi arejeshe fedha za wananchi popote alipo".

Amesema kama kuna mtu au mtendaji anayeona hatoshi apishe akae pembeni ili wanaoweza kufanya kazi wafanye ili kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi. Hata hivyo, ametoa wito kwa wananchi kutumia rasilimali zinazowazunguka kujiletea maendeleo badala ya kukaa na kulalamika maisha magumu wakati kuna rasilimali nyingi katika maeneo wanayoishi.  Aidha, amezitaka Halmashauri Mkoani Geita kusajili na kuvitumia vikundi vya mafundi vinavyojitolea kujenga madarasa na Zahanati bila malipo katika miradi ya fedha katika maeneo mbalimbali ili vijana hao wanufaike badala ya kutoa kazi zote kwa wakandarasi.

Awali  Josephat Maganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa Wilaya ya Bukombe ina vijiji 52 na Vitongoji 372 lakini kuna Zahanati sita (6) tu za Serikali.  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akiwa Wilayani humo amezindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati katika vijiji vya Kazibizyo na Bulama kwa kushiriki katika ujenzi na harambee iliyoleta michango ya mifuko 93 ya simenti, fedha tasilimu  shilingi 340000/=, tofali 500,mbao 50 na misumari kilo3.

 Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita (Aliyevaa kofia usalama) akishiriki kubeba mawe  na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa msingi katika Zahanati ya kijiji cha Kazibizyo Wilayani Bukombe.Wananchi wa kijiji hicho wanatembea umbali wa Kilometa 20 kwenda Ushirombo kupata huduma za afya.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akishirikiana na mafundi wa ujenzi kujenga msingi wa Zahanati ya kijiji cha Kazibizyo alipotembelea kijiji hicho kuzindua kampeni ya ujenzi wa Zahanati na Vyumba vya madarasa.
 Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kazibizyo Wilaya ya Bukombe baada ya uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa Madarasa na Zahanati Wilayi Bukombe.

 Mhandisi Robert Gabriel akishirikiana na wananchi pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Bukombe kuchanganya mchanga na sementi kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi kijiji cha Bulama. 
Josephat Maganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bulama wakazi wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kijijini hapo ili kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati. Habari na picha: Magesa Jumapili - Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live




Latest Images