Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 199 | 200 | (Page 201) | 202 | 203 | .... | 3270 | newer

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana alikutana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF)Profesa Ibrahim Lipumba na kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam.Mazungumzo hayo yalihusu masuala mbalimbali ya siasa na uchumi nchini.Pichani Rais Kikwete akiwa na Professa Lipumba katika nyakati tofauti  ikulu jijini Dar es Salaam
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF)Profesa Ibrahim Lipumba 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF)Profesa Ibrahim Lipumba baada ya mazungumzo yao

  0 0

  HABARI ZIMETUFIKIA PUNDE TU ZINASEMA MFANYABIASHARA MMOJA MAARUFU NCHINI SAID MOHAMED AMEMWAGIWA  KITU KINACHODHANIWA NI TINDIKALI NA WATU WASIOJULIKANA MAENEO YA MSASANI JIRANI NA KITUO CHA POLISI CHA OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM.

  MFANYABIASHARA HUYO ANAEMILIKI MADUKA YA HOME SHOPPING CENTRE INASEMEKANA AMEPATWA NA SHAMBULIO HILO MARA BAADA YA MUDA WA KUFUTURU.

  AIDHA, WANAHABARI WETU WAMESHUHUDIA MAGARI KADHAA YA POLISI YAKIWA KWENYE MAEGESHO YA DUKA MOJA KUBWA  LILILOPO MAENEO KARIBU NA OYSTERBAY POLICE, AMBAKO HAKUNA ALIYETAKA KUSEMA CHOCHOTE, JAPO HABARI ZINASEMA HAPO NDIPO TUKIO LILIPOTOKEA.

  JUHUDI ZA KUMSAKA KAMANDA WA POLISI MKOA WA KINONDONI AMA KAMANDA WA KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM AFANDE SULEIMAN KOVA ZINAENDELEA. NASI TUTAWAJULISHA KILA TUTAPOPATA HABARI ZAIDI.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Watu wa China, Bw. Liu Jiayi alipofika Wizarani na Ujumbe wake kwa mazungumzo kuhusu Serikali hizi mbili kushirikiana kwa kubadilishana uzoefu katika masuala ya ukaguzi wa hesabu za serikali.
  Bw. Liu Jiayi (wa kwanza kulia) na ujumbe wake akiwemo Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lv Youqing (wa tatu kutoka kulia) wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo nae.
  Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Ludovick Utoh na ujumbe wake wakimsikiliza Bw. Lui Jiayi (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo na Mhe. Membe.
  Mhe. Membe na wajumbe kutoka Tanzania na China kwa pamoja wakimsikiliza Bw. Liu Jiayi.

  Mhe. Membe na Bw. Utoh wakimsikiliza Bw. Liu Jiayi alipokuwa akifafanua jambo katika moja ya taarifa za ukaguzi za nchini kwake alizomkabidhi Mhe. Membe.
  Mhe. Membe akiagana na Bw. Liu Jiayi.

  0 0

  WAKAZI wawili wa Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  kwa ajili  ya hapo baadae kuja kuunganishwa katika kesi ya wizi wa Paspoti 26 inayomkabili Msainii wa Muziki wa asili, Chingwele Che Mundugwao (pichani) na wenzake wanne.
  Wakili wa serikali  Aidah Kisumo mbele Hakimu Mkazi Sundi Fimbo aliwataja washitakiwa hao walifikishwa jana kwa mara ya kwanza mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa yanayofanana ambayo yanamkabili Chemundugwao na wenzake ni  Rajab Momba na Haji Mshamu.

  Akiwasomea mashitaka Momba na Mshamu, Wakili Kisumo alidai kuwa tarehe isiyofahamika washitakiwa walikula njama ya kutenda kosa. Aidha tarehe tofauti Dar es Salaam, Momba aliiba hati ya kusafiria yenye namba AB 651926 mali ya serikali.
  Alidai Momba, Mshamu na Iqbal wanadaiwa tarehe isiyofahamika Dar es Salaam, walighushi hati ya kusafiria yenye namba hiyo, kuonesha ni halali na imetolewa na Idara ya Uhamiaji ya Tanzania jambo ambalo si kweli.

  Mbali na Che mundugwao washitakiwa hao wataunganishwa na Raia wa Uingereza Ahsan Iqbal au Ali Patel, Ofisa  Ugavi wa  Idara ya Uhamiaji Shemweta Kiluwasha, Injinia Keneth Pius wa Kikosi  cha Zimamoto na Uokoaji na mfanyabiashara Ally Jabir.

  Hata hivyo washitakiwa  hao walikana mashitaka na kurudishwa rumande kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),Dk.Eliezer Feleshi aliwasilisha hati ya kuwafungia dhamana washitakiwa hao wawili kama alivyofanya kwa kina Chemunduwao na wenzake na kwamba  upelelezi bado haujakamilika na kesi itatajwa tena Julai 22, mwaka huu, ili waunganishwe na Chemundugwao ambapo kesi yao nayo imepangwa kuja kutajwa Julai 22 mwaka huu.
  Juni 3 mwaka huu, Chemundugwao na wenzake walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa mbalimbali yakiwemo kosa la wizi wa paspoti 26, ambapo hata hivyo DPP aliwasilisha hati ya kuwafungia dhamana ambapo hadi sasa wapo gerezani.

  0 0

  Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani umemfanyia hafla fupi ya kumtambulisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwa kwa Whe. Mabalozi wa nchi jirani na nchi marafiki wa Tanzania wakiwemo viongozi wa jumuiya mbalimbali za Watanzania DMV. Kwenye picha Kaimu Balozi na Mkuu wa Utawala na Fedha Mama Lily Munanka (kati) akimkaribisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula mara tu alipowasili Ubalozini hapo akiambatana na familia yake, kulia ni Charles Gray ambaye ni Balozi wa hiari anayeitangaza Tanzania nchini Marekani na anayeishi Pennsylvania kwenye mji uitwao Bala Cynwyd.
  Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Charles Gray.
  Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa.
  Mhe. Liberata Mulamula akiongea jambo na Mhe. Edward Lowassa.
   Kaimu Balozi na Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka akiongea machache yakiwemo kuwakaribisha Whe. Mabalozi na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania DMV kwenye Hafla hiyo fupi na baadae kumkaribisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuongea nao.
   Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea machache yakiwemo kuwashukuru Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi kwa kuandaa Hafla hiyo fupi ya kumtambulisha kwa Whe. Mabalozi wa nchi jirani na nchi marafiki wa Tanzania na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania DMV wakiwemo wanahabari wa DMV pia alielezea kwamba leo Alhamisi July 18, 2013 alipeleka hati yake ya utambulisho kwa Rais Barack Obama na anafuraha kukutana nao hapo Ubalozini na hii isiwe mwisho wanakaribishwa muda wote wajisikie wapo nyumbani.
  Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Afisa Mindi Kasiga ili aongoze kuimba wimbo wa Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote. Mindi Kasiga ndiye aliyekua mshereheshaji wa Hafla hiyo.
  Mhe. Balozi Liberata Mulamula akitambulisha familia yake kutoka kushoto ni mwanaeTanya, Alvin na Mumewe Bwn. George Mulamula.
  Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifanya tosi.
  Whe. Mabalozi, Viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania DMV, wageni waalikwa wakitosi pamoja na Mhe. Balozi.

  0 0

  Na Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma

  Picha mbalimbali za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime akitembelea wilaya ya Mpwapwa na vijiji vyake kwa ajili ya kuhamasisha mkakati wa Polisi Jamii na uanzishaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi katika vijiji na kata za wilaya ya mpwapwa hivi karibuni.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime akiachana na gari lake na kuungana na kikundi cha ulinzi shirikishi kilichofahamika kwa jina la Mwananzele kilichopo katika kijiji cha Mbori kata ya Matomondo wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, waliokwenda kumpokea akiwa njiani kabla ya kufika kijijini hapo kwa ajili ya kuongea na wanakijiji hao masuala mbalimbali yahusuyo ulinzi na usalama wa watu na mali zao.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime, akifanya Ukaguzi kwa askari wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha Mwananzele cha kijiji cha Mbori kata ya Matomondo wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, kuangalia na kujua ukakamavu wao uko imara kiasi gani.
  Wazee wa Kimila wa Kijiji cha Mbori katika kata ya Matomondo wilayani Mpwapwa, wakimvika vazi rasmi na kumkabidhi mkuki Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime Kama ishara ya kumtambua rasmi kuwa kamanda na mlezi wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha mwananzele katika kata hiyo.
  Wanakijiji wa Mbori katika Kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa wakimsikiliza kwa makini Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime, ambaye alikuwa akiwahutubia wanakijiji hao kuhusu miradi mbalimbali Iliyopo katika mpango wa Polisi jamii na Ulinzi shirikishi juu ya umuhimu na faida zake kwa jamii hiyo.

  0 0

  Na Anna Nkinda – Maelezo

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wanawake wa dini zote nchini kutokubaguana kutokana na itikadi zao za vyama vya siasa bali wawe mstari wa mbele kuhubiri amani na upendo.

  Mama Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwafutarisha wanawake wa dini mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Mama Kikwete alisema kuwa ukosefu wa amani ukitokea katika nchi wanawake na watoto ndiyo wahanga wakubwa hivyo basi wasikubali watu kuwadanganya bali wawe na msimamo na umoja ili waweze kuilinda amani ambayo ndiyo silaha pekee ya kuwaletea ukombozi iliyoasisiwa na wazee wa nchi yao.

  “Ninawashukuru kwa kuacha shughuli zenu na kuitikia wito wangu wa kuja na kufuturu pamoja nami, nawatakia mfungo mwema nini nyote mnaofunga ili Mwenyezi Mungu awakubalie heri zenu nanyi msiofunga Mwenyezi Munguawabariki katika maisha yenu ya kila siku”, alisema Mama Kikwete.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania Taifa (BAKWATA) Shamim Khan alimshukuru Mama Kikwete kwa upendo wake wa kuwaalika wanawake hao kupata futari ya pamoja.

  Mama Khan alisema kuwa kukutana kwao kumewafanya wajifunze kuwa wakitaka amani ni lazima washirikiane bila ya kujali rangi, dini na kabila kwani wanawake wote wanamatatizo yanayofanana ambayo wanaweza kuyatatua kwa pamoja bila ya kuangalia kuwa huyu ni mkristo au muislamu na wakikaa pamoja amani inapatikana.

  Naye Olive Lwema ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wakristo Tanzania alisema kuwa aliposikia wamepata mwaliko huo alifurahi sana kwasababu wanapokutana wanawake ambao ni wazazi wa watoto wa taifa, wake wa waume wanaoongoza nchi hakuna jambo litakaloharibika na ameshuhudia kwa kuona nyuso za ushirikiano na upendo baina yao.

  Mama Lwema aliwaomba wanawake wanaofunga kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wajitoe kufunga kwao kwa ajili ya maombi maalum ya kuombea amani na watoto kwani hivi sasa vijana wengi wanaomaliza vyuo hawana ajira, shule haziendi sawa na wanaopata machungu ya haya yote ni wanawake.

  0 0

  Ticket prices for international fans attending the football World Cup in Brazil will start at $90 (£59, 69 euros) for initial group matches.

  Football's governing body Fifa announced that the cheapest ticket for overseas fans for the final on 13 July was $440 (£288) and the most expensive $990 (£650).

  The tournament starts on 12 June next year, with the first game being played in Sao Paulo.
  Tickets will go on sale from 20 August.

  Fans have until 10 October to apply and a ballot will be held to decide which of these applications are successful.

  Only later will tickets be sold on a first come, first served basis. In total about three million tickets will be available for fans.

  'No surprises'

  For Brazilian nationals the cheapest tickets start at $15. These are only available for students, those aged over 60 and people on social welfare programmes. For other Brazilians tickets start at $30.

  The lowest price paid for a ticket in the 2010 World Cup in South Africa was $20, also for group stage matches in the special category set aside exclusively for residents.

  The governing body had previously said that tickets in Brazil would be the "cheapest ever".

  The Fifa ticket website will include a map of the ground that shows the location of different categories of tickets.

  This meant there would be "no surprises" over where fans would end up sitting, said Fifa marketing director Thierry Weil, who is in charge of ticketing strategy.

  Supporters can request a maximum of four seats per match, and for a maximum of seven matches.

  He said there would be a reselling system run by Fifa, if people were unable to attend games for which they had bought tickets.

  At least 400,000 tickets will be reserved exclusively for residents of Brazil, with about 50,000 for construction workers who were involved in building and upgrading the grounds for the tournament.

  SOURCE: BBC

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,alijumuika na Waislamu na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika Swala ya Magharibi kabla ya kufutari nao pamoja kwa futari aliyowaandalia wananchi hao jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Wananchi na waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba waiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi,baada ya Swala ya Magharibi,na kuendelea na Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Ikulu ya Wete.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto)alipojumuika na Viongozi na wananchi wa na Waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika futari aliyowaandalia jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba.
  Wananchi wa Mkoa wa Kasakazini Pemba walipojumuika kwa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika futari aliyowaandalia jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba.
  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,(katikati) akiwa na Viongozi wakat wa futari aliyowaandalia akinamama wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Pemba jana.
  Akina Mama wa Mkoa wa Kaskazini Pemba walihudhuria katika futari walioyoalikwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama mwanamwema Shein,jana katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Pemba, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0


  0 0


  0 0

  Mdau Donald Wilson Ndesanjo (shoto) aliyekula Nondozzz ya BA International Business Chuo Kikuu cha Middlesex University nchini Uingereza.akiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wake,Baba Wilson Ndesanjo na Mama Florence Ndesanjo pamoja na Dada yake Leonora Ndesanjo wakati wa mahali yao yaliyofanyika hivi karibuni.
  Mdau Donald Ndesanjo akiwa na Marafiki zake Daniel kutoka Jamaica na Mohamed kutoka Dubai wakifurahi baada ya kulamba Nondozz zao.
  Mdau Donald na wanafunzi wenzake wa pili Ania na Alexandra kutoka Poland.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto) wakisalimiana na Madwani wa Songea Vijijini baada ya kuwasli kwenye kijiji cha Mkenda kuweka jiwe la Msingi la Soko wakiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 19,2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara , Joyce Mapunjo wakiweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko katika kijiji cha Mkenda wialyani Songea Vijijini Julai 19, 2013. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipima katika mzani gunia la mahindi kuashiria uzinduzi wa msimu wa ununuzi wa mahindi katika kijiji cha Mpitimbi akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 19, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza katika Mkutano wa Teknolojia ya Kupambana na Uhalifu uliofanyika katika Jiji la Lyon nchini Ufaransa hivi karibuni. Waziri Nchimbi alishiriki mkutano huo pamoja na washiriki wengine kutoka nchi mbalimbali duniani.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (katikati) akimsikiliza kwa makini Rais wa Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol), Mireille Ballestrazzi (kushoto) baada ya Mkutano wa Kimataifa wa Teknolojia ya Kupambana na Uhalifu uliofanyika katika Jiji la Lyon nchini Ufaransa hivi karibuni. Kulia ni Meya wa jiji hilo, Gerald Collomb.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol) Mireille Ballestrazzi (kushoto) na Kulia ni Meya wa Jiji la Lyon, Gerald Collomb. Waziri Nchimbi alishiriki mkutano huo wa Kimataifa hivi karibuni. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


   Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Simba wa kujadili maendeleo ya klabu hiyo ulioanza saa nne kamili na kumalizika saa tano kamili katika Bwalo la Maofisa wa Polisi jijini Dar es Salaam leo, ambapo wanachama zaidi ya 700 walihudhuria mkutano huo.
  Mwanachama wa Simba kutoka Iringa akiuliza swali katika mkutano huo.
   Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali (kushoto) akifuatilia mkutano huo.
   Baadhi ya wanachama wa Simba wakiwa katika mkutano huo.


  0 0


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha utambulisho wa Ukufunzi wa Kozi maalum ya Kwanza ya Mafunzo, katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Prof. Ibrahim Lipumba, wakati wa sherehe za kufunga Kozi hiyo zilizofanyika katika Chuo hicho, Kunduchi jijini Dar es Salaam, leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha utambulisho wa Ukufunzi wa Kozi maalum ya Kwanza ya Mafunzo, katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Gen Mstaafu wa Jeshi, George M. Waitara (Rtd) wakati wa sherehe za kufunga Kozi hiyo zilizofanyika katika Chuo hicho, Kunduchi jijini Dar es Salaam, leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha utambulisho wa Ukufunzi wa Kozi maalum ya Kwanza ya Mafunzo, katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Dkt. Regnald Abraham Mengi, wakati wa sherehe za kufunga Kozi hiyo zilizofanyika katika Chuo hicho, Kunduchi jijini Dar es Salaam, leo.


  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kocha wa zamani wa Taifa Stars, Bert Trautmann (89) kilichotokea jana (Julai 19 mwaka huu) nchini Hispania.

  Kabla ya kuwa kocha, Trautmann aliyezaliwa 1923 mjini Bremen, Ujerumani alikuwa kipa wa timu ya Manchester City ya Uingereza ambapo anakumbukwa kwa kucheza mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Birmingham City akiwa amevunjika shingo.

  Manchester City ilishinda fainali hiyo iliyochezwa mwaka 1956 mabao 3-1. Trautmann ambaye aligongana na mshambuliaji wa Birmingham, Peter Murphy zikiwa zimesalia dakika 17 mechi hiyo kumalizika aligundua kuwa amevunjika shingo siku tatu baadaye.

  Mbali ya kuwa kocha wa Taifa Stars mwanzoni mwa miaka ya 60, Trautmann pia alikuwa mkufunzi wa makocha ambapo hapa nchini aliendesha kozi mbalimbali zilizotoa makocha waliokuja kutamba baadaye.

  TFF itamkumbuka Trautmann kwa mchango wake aliotoa katika maendeleo ya mpira wa miguu nchini ikiwemo wazo lake la kuanzishwa kwa Ligi Kuu (Daraja la Kwanza) ambalo alilitekeleza katikati ya miaka ya 60.

  Msiba huo ni pigo kwa familia ya Trautmann, TFF na familia ya mpira wa miguu kwa ujumla nchini kutokana na mchango alioutoa kwa Tanzania hasa wakati akiwa kocha na mkufunzi wa makocha.

  TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Trautmann, Chama cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DFB), Chama cha Mpira wa Miguu cha Uingereza (FA) na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito.

  Mungu aiweke roho ya marehemu Bert Trautmann mahali pema peponi. Amina

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

  Sehemu ya Masanduku yenye miili ya askari wa saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki dunia hivi karibuni huki Darfur nchini Sudani wakati wakilinda amani,yakishushwa kwenye Ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,Jijini Dar es Salaam leo alasiri.
  Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki duni Darfur wakati wakilinda amani, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo alasiri.
  Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipakia  moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki dunia huko Darfur nchini Sudan wakati wakilinda amani, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo alasiri.

  Miili ya Askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki Dunia wakati wakiwa katika kazi ya kulinda amani kwenye Mji wa Darfur nchini Sudan,imewasili nchini leo majira ya alasili kwa kutumia ndege maalumu ya Umoja wa Mataifa.

  Askari hao waliuwawa kwa shambulio la kushtukiza na kundi la waasi wakati wakiwa kwenye kazi yao ya kulinda amani nchini Sudan.

  Jeshi la JWTZ lilitoa taarifa likisema kuwa tukio hilo ni pigo kubwa kwa nchi ya Tanzania ikiwa ni la kwanza kutokea tangu Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 2007. 

  0 0older | 1 | .... | 199 | 200 | (Page 201) | 202 | 203 | .... | 3270 | newer