Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

UCHAGUZI WA TFF KUFANYIKA SEPTEMBA 29,KAMATI YA MAJAJI YAPANGWA KUONGOZA MCHAKATO MZIMA

0
0
 
Wakati uchaguzi mkuu wa Shirikisho  la Soka Tanzania (TFF), ukiwa umepangwa kufanyika Septemba 29, Majaji na wanasheria wametangazwa kuongoza kamati mbali mbali za shirikisho hilo.

Kikao cha kamati ya utendaji kilichoketi jana kilifanya mabadiliko kwenye kamati zake mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutekeleza  agizo la FIFA lilitolewa Aprili mwaka huu baada ya kusimamisha mchakato  wa uchaguzi wa TFF, na kuagiza kwanza yafanyike marekebisho ya Katiba ili kuingiza Kamati ya Maadili, na Kamati ya Rufani ya Maadili ambavyo ndivyo watashughulikia matatizo ya kimaadili kwa familia ya mpira wa miguu nchini.

Mbali ya kamati hizo, mabadiliko hayo pia yametengeneza ngazi mbili za kushughulikia masuala ya kinidhamu ambazo ni; Kamati ya Nidhamu na Kamati ya Rufani ya Nidhamu.Jana Rais wa TFF, Leodegar Tenga alitangaza kamati Maadili itaongozwa na Wakili  Jesse Mguto akisaidiwa na Francis Kambwe (Msajili Mahakama Kuu), Kamanda Mohamed Mpinga, Profesa Madundo Mtambo, na wakili Evod Mmanda.

Kamati ya Maadili ya rufaa itaongozwa na Jaji mstaafu Steven Hema akisaidiwa na Mwanasheria Victoria Makani huku wajumbe ni Mohamed Misanga (Mbunge), Murtaza Mangungu (Mbunge) na Henry Tandau (mshauri wa Fifa).

Pia Kamati ya uchaguzi ambayo ilikuwa inaongozwa na Deo Lyato  sasa itaongozwa na Mwanasheria mzoefu Hamidu Mbwezeleni kwa vile kwa mujibu wa katiba ya sasa ya TFF mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi lazima awe mwanasheria hivyo Hamidu Mbwezeleni ataongoza kamati hiyo akisaidiwa na Moses Kalua (mwanasheria) na wajumbe ni Mustapha Siami (Mwanasheria),Chabanga Ndyamwale (Mwanasheria) na Kitwana Manara.

Kamati ya rufaa iliyokuwa chini ya Idd Mtiginjola sasa itaongozwa na Jaji Benard Rwanda akisaidiwa na  Francis Kiwanga (Wakili), Annesteve Msemo (Mwanasheria), Yohane Masala (Mwanasheria) na Allen Kasamala (Mwanasheria).

Akifafanua kuhusu kufanya mabadiliko kwenye kamati ya rufaa ya uchaguzi Tenga alisema "Tuliitaji kuwa na jaji mzoefu kwenye kamati ya rufaa, mkutano ndio ulivyoamua hivyo, na pia  mwenyekiti aliyekuwepo (Mtiginjola), alishaandika barua ya kujiuzulu na kutaka asifikiriwe kwenye hili. 

Hata hivyo alisema kamati ya nidhamu itabaki kuongozwa na Kamanda Mstaafu Alfred Tibaigana, akisaidiwa na Kambona, Musa Hazan 'Zungu', Yusuf Nzowa (Usalama wa Taifa) na Mohamed Msomali na pia Kamati ya Mgongo Fimbo itabaki kama ilivyo ambapo atasaidiwa na Idd Kipingu, Kibuta, Mshindo Msola na Kamanda Mstaafu Jamali Rwambo.

Pia Tenga alisema Kamati ya marefa wamefanya mabadiliko kwa kuingiza mwenyekiti na Katibu wa Chama cha Marefa ambapo kwa sasa kamati hiyo itaundwa na Kapteni Lugenge, Said Nassoro, Mohamed Mnyaa na Charles Ndagala, wakati ile ya madaktari itaongozwa na Paul Marealle baaada ya dokta Faya kuomba kupumzika wakati wajumbe ni Mwanandi Mwankemwa, Antony Ngome, Helen Msemo, Joachimu Mshanga na Frank Muhonda.

DC HANDENI AAGIZA WAFANYABIASHARA KUTOA STAKABADHI KWA KUTUMIA MASHINE ZA TRA

0
0
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi.

Serikali wilayani Handeni mkoani Tanga, imewataka Wafanyabiasha wilayani humo, kuhakikisha kuwa wananunua na kutumia mashine za TRA za kielektroniki (EFD) katika kutoa risiti wakati wanapouza bidhaa zao kwani kutotoa stakabadhi ni kosa la jinai.

Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu, wakati alipokuwa akifanya uzinduzi wa matuminzi sahihi ya mashine hizo za kielektroniki (EFD) wilayani humo na kusema kuwa itakapobainika kwa mfanyabiashara anauza bidhaa bila ya kutoa stakabadhi atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Bw. Rweyemamu amesema 
kuwa mashine hizo ambazo pia zinahifadhi kumbukumbu za mauzo kwa wafanyabiashara, na hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani zimetengenezwa kwa ubora unaostahili na makampuni yanayoaminika kimataifa.

Amesema kuwa mbali ya kuwa kwa kutumia mashine hiyo Serikali haitakosa mapato yatokanayo na mauzo ya bidhaa za madukani, lakini pia itakuwa ni faida kwa watumiaji kwa vile inahifadhi kumbukumbu za mauzo yao.

Awali Meneja wa TRA wilayani Handeni Bw. Charles Kamuhanda, alimwambia Mkuu huyo wa wilaya kuwa, wafanyabiashara wwengi hawataki kutoa risti wanapouza bidhaa katika maduka yao kwa lengo la kukwepa ushuru.

Hivyo amewataka kujenga tabia ya kutoa risiti kwa kila mmteja atakayenunua bidhaa katika duka husika na kwa kutokufanya hivyo ni sawa na kukwepa ushuru wa Serikali.

Bw. Kamuhanda alisema kuwa mnunuzi yeyote anatakiwa kudai na kupewa risiti kama sehemu ya uwajibikaji kwa taifa na kwamba ni haki kwa kila mteja kudai na kupewa risiti kwani hata  wafanyabiashara wanapokwenda kufungasha wanatakiwa kudai na kupewa risiti pia.

Aidha Bw. Kamuhanda ameitaja faida nyingine za mashine hizo kuwa mbali ya kutunza kumbukumbu za mauzo kwa muda wa miaka mitano, lakini pia mfanyabiashara anaweza kudhibiti wizi endapo anamuachia muuzaji mwingine ambaye sie mwaminifu.       

Waziri Mkuu akiwa Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma

0
0
Waziri Mkuu, Mizenfo pinfa akiwapungia wananchi wa kijiji cha Kiagara wilayani nyassa akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 182013. Kulia ni mkewe Mama Tunu Pinda.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (wapili kushoto)akitazama kazi za mikono alizozawadiwa na wanawake wa Lituhi wilayani Nyassa akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 17,2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI WA UCHUKUZI, DKT. HARRISON MWAKYEMBE AKUTANA NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA ALHAYAT INVETMENT NA NEMBRAS INVESTMENT YA NCHINI OMAN

0
0
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia), akifafanua jambo kwa Mweyekiti wa Kampuni  ya Alhayat Investment na Nembras Investment ya nchini Oman, Shekhe Salim Al-Harthy, wakati walipomtebelea ofisini kwake leo mchana. Kampuni ya Alhayat investment ni kampuni ambayo imeonyesha nia ya kuwekeza kwenye Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
 Mwenyekiti wa Kampuni ya Alhayat investment na Nembras Investment ya nchini Oman, Shekhe Salim Al-Harthy akifafanua jambo kwa Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia),wakati mwenyekti huyo alipomtembelea ofisni kwake leo mchana.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Alhayat investment na Nembras Investment ya nchini Muscat Shekhe Salim Al-Harthy akifafanua jambo kwa Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia),wakati mwenyekti huyo alipomtembelea Waziiri wa Uchukuzi ofisini kwake leo mchana. Kampunji ya alhayat imeonesha nia ya kuwekeza katika Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL).(Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

TPA WAONGEA NA WAANDISHI KUELEZEA MAFANIKIO NA MIKAKATI YA KUBORESHA HUDUMA

0
0
Viongozi wakuu wa idara mbalimbali za TPA wakiongea na waandishi wa Habari leo ukumbi wa Maelezo, kuhusu mafanikio yaliyopatikana na mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma kwa wateja, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa ICT TPA Mr. Magesa, Mkugurenzi Msaidizi wa Maelezo Ms.Kawawa, Meneja Mawasiliano TPA Mrs. Ruzangi, Meneja wa Bandari ya Dar Mr.Masawe, Mkurugenzi wa Mipango TPA Mr.Urioh.

ZIARA YA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI , ABDULAZIZ ABOOD AKIKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO YA WANANCHI IKIWEMO UJENZI WA BARABARA ZA KIWANGO CHA LAMI.

0
0
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood ( kati kati) pamoja na Meya wa Manispaa ya Morogoro , Amiri Nondo, ( mwenye kuvaa koti) Julai 18, 2013, wakibadirishana mawazo  wakati wakikagua ujenzi wa barabara ya Seng’ondo iliyopo eneo la Kata ya Boma, ambayo Meya huyo ni Diwani wa Kata , barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami  na Kampuni ya Uhandisi  ya CGI  na kutaraajiwa  kukamilika  Augosti mwaka huu.( Picha na John Nditi).
 Mbunge Abdulaziz Abood ( kushoto) akiwa na Mwalimu wake ,Madelina Lungu aliyemfundisha wa Shule ya Msingi ya Bungo, mwaka 1967 darasa la nne na tano
 Mbunge Abood akibadilishana mawazo na Mwalimu wake wa zamani wa shule ya msingi, Rehema Ngedere.
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood ( wanne kutoka kulia) akipata maelezo ya uenjezi wa Barabara la kiwango cha lami.
 Moja kati ya baarabara za Manispaa ya Morogoro zinazojengwa kwa kiwango cha lami katika Kata ya Mji Mpya.
Wananchi wa Kata ya Mji Mpya , Manispaa ya Morogoro wakijumuika na Mbunge wao Abdulaziz Abood ( haonekani pichani) kukagua maendeleo ya mwisho ya ukamilishaji wa Zahanat

NEEMA YA MAJI KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUPITIA USHIRIKIANO BAYANA YA TANZANIA NA UJERUMANI

0
0
Dar es Salaam ni moja ya majiji ambayo yanakua kwa kasi kiuchumi. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu, uwekezaji, Viwanda nk. Haya yote yamekuwa yanachangia kwa sehemu kubwa ongezeko la uhitaji wa maji na inakadiriwa kuwa kwa miaka 15 ijayo uhitaji utaongezeka mara mbili zaidi.

Inakadiriwa kuwa zadi ya asilimia 50 ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam hawajafikiwa na huduma ya maji ya bomba. Matumizi ya maji ya kisima kwa jijini Dar es Salaam ni tatizo kutokana na uchafuzi wa mazingira utokanao na Viwanda, maji taka na taka za wakazi wa jiji hilo.

Hii sasa yawezekana ikawa neema kwa wakazi wa jiji hilo kwa ushirikiano huu uliongiwa baina ya Wizara ya Maji na Idara ya Maji ya hapa Hamburg, Ujerumani iitwayo Hamburg Wasser . Ushirikiano huu utalenga kusaidia tatizo la maji katika jiji hili la Dar es Salaam
Kutoka kushoto ni : Eng. Christopher Sayi ( Katibu mkuu Wizara ya Maji ), Godfrey Matola, Mh. Prof. Jumanne Maghembe ( Waziri wa Maji ) , Reinhard Paulsen , Ully Mbuluko, Moses Haule, Eng. Christian Gunner ( Kutoka Hamburg Wasser ) , Mh. Christopher Mvula ( Kaimu Balozi wa Tanzania Ujerumani ) na Godwin Msigwa . Wakipiga picha ya pamoja baada ya Hotuba kutolewa na Waziri wa maji Tanzania na pia kutoka upande wa wenyeji Hamburg Wasser.
Prof. Jumanne Maghembe ( Waziri wa maji ) akisisitiza jambo kwa Petra Hammelman ( Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Tanzania – Hamburg ) baada ya kutoa Hotuba ndani ya jengo la Seneti Hamburg .

Jinsi Halisi ya Kupumua, Kuimba na Kumudu Sauti - JOETT


Darsa za Ramadhani: Diet na Mazoezi wakati wa Mfungo

TAASISI YA MISA NA UBALOZI WA CANADA WAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI NCHINI

0
0
MWENYEKITI wa Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika kanda ya Tanzania (MISATAN), Mohammed Tibanyendera akizungumza muda mfupi kabla mkaribisha Balozi wa Cananda Nchini Tanzania, Alexandre Leveque kufungua mafunzo ya Waandishi wa Habari wa Tanzania kutoka vyombo mbali mbali yaliyoandaliwa na MISATAN kwa kushirikiana na Ubalozi wa Canada Nchini ,mafunzo hayo yalifanyika katika kituo cha British Council Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Leveque akifungua mafunzo ya siku moja kwa Waandishi wa Habari wa Tanzania kutoka vyombo mbali mbali yaliyoandaliwa na Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika kanda ya Tanzania (MISATAN) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Canada Nchini ,mafunzo hayo yalifanyika katika kituo cha British Council Jijini Dar es Salaam .Kulia Mwenyekiti wa MISATAN, Mohammed Tibanyendera.
WAANDISHI mbali mbali wakimsikiliza Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Alexandre Leveque (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali yaliyoandaliwa na MISATAN kwa kushirikiana na Ubalozi wa Canada Nchini , mafunzo hayo yalifanyika katika kituo cha British Council Jijini Dar es Salaam.Picha na Haroub Hussein.

KWIECO WAFANYA MKUTANO MKUU MKOANI KILIMANJARO

0
0
Wajumbe wa mkutano mkuu wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na maswala ya jinsia na wanawake mkoani Kilimanjaro, (KWIECO) wakifanya sala kabla ya kuanza kwa mkutano mku wa shirika hilo.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na maswala ya jinsia na wanawake mkoani Kilimanjaro, (KWIECO) Clement Kwayu akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa shirika hilo.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na maswala ya jinsia na wanawake mkoani Kilimanjaro, (KWIECO) Elizabeth Minde akizungumza wakati wa mkutano huo.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa KWIECO.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi

JUMLA ya wateja 1,660, wamepatiwa ushauri nasaha wa kisheriauliotolewa na shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na maswala yajinsia na wanawake mkoani Kilimanjaro, (KWIECO), katika mwaka 2012.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bi Elizabeth Minde, wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika makao mapya ya shirika hilo yaliyopo eneo la Shanty town mjini Moshi.

Amesema katika kipindi hicho kambi nne za msaada wa kisheria ziliwekwa na ushauri wa kisheria ulitolewa na kuwashirikisha jumla ya watu 1,020 huku kesi muhimu 62 kati ya 50 zilizopendekezwa zikifunguliwa mahakamani katika kuongeza upatikanaji wa haki za wanawake na watoto.

“Katika kuongeza uelewa na ushiriki wa jamii katika kulinda haki za Binadamu na jinsia, kamati za haki za Binadamu ziliundwa katika ngazi za vijiji katika kata saba za Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo mafunzo ya uongozi yalitolewa kwa viongozi wa serikali za mitaa wapatao 318 hivyo kuwajengea ujasiri katika kushughulikia masuala ya kijinsia na haki za watoto”, alisema. Minde

Aidha Minde aliendelea kusema kuwa katika kuongeza uelewa, kulinda na kutetea haki za watoto, mafunzo ya haki za watoto yalitolewa kwa wajumbe 65, wanafunzi 960 na walimu 150, ambapo kamati saba za haki za watoto na klabu 42 za watoto ziliundwa mashuleni.

Aliendelea kusema kuwa katika kuwajengea uwezo wa kiuchumi, jumla ya wanawake 63 walioko maeneo ya pembezoni, walipewa misaada ya kujiajiri wenyewe na 43 walipewa misaada kwenye ajira zisizo rasmi.

Minde alisema katika kipindi hicho cha mwaka jana, kiwango cha umasikini miongoni mwa walengwa wa shirika hilo kilikuwa bado ni changamoto kubwa, sambamba na ile ya watoto kutokuwa na uwezo wa kuchangia mawazo yao mbele ya wazazi jambo ambalo alisema husababishwa na tamaduni na imani potofu za kimila.

SAMSUNG YAJA NA MBINU MPYA YA KUEPUKA BIDHAA FEKI YA PROGRAMU YA E-WARRANT

0
0
  Meneja mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Samsung,Sylvester Manyara (wa pili kulia) akimpigia simu mshindi wa TV ya Samsung nchi 32 wakati wa kucheza droo kwa wateja wa kila mwezi wa bidhaa za kampuni hiyo,ambapo  mkazi wa Dar es Saalaam, Goodluck Mumvuri alijishindia.Kutoka kulia ni Kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi la Samsung Quality Center, Jafari Adam,Mwakilishi wa Bahati na sibu ya Taifa,Mrisho Milao na Mkaguzi wa bidhaa za Samsung,Sadic Abbas.
  Meneja mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Samsung,Sylvester Manyara (katikati)  na Mkaguzi wa bidhaa za Samsung,Sadic Abbas wakionyesha simu mpya za Galaxy Star ambazo ziligawiwa kwa wanahabari kwa njia ya kuchezesha droo ya bahati na sibu.Kushoto ni Mwakilishi wa Bahati na sibu ya Taifa,Mrisho Milao.
  Meneja mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Samsung,Sylvester Manyara (kushoto)  akimkabidhi simu,Mwandishi wa Gazeti la Habari Leo,Theopister Nzanzugwanko mara baada ya kushinda kwenye droo ya wanahabari kwa simu mpya ya Galaxy Star.Katikati ni Mkaguzi wa bidhaa za Samsung,Sadic Abbas.
Meneja mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Samsung,Sylvester Manyara (kushoto)  akimkabidhi simu,Mwandishi wa Gazeti la Majira,Charles Lucas mara baada ya kushinda kwenye droo ya wanahabari kwa simu mpya ya Galaxy Star.Katikati ni Mkaguzi wa bidhaa za Samsung,Sadic Abbas.

WENGI WAJITOKEZA MAZISHI YA MAREHEMU DAVID MAJEBELLE

0
0
 Mwili wa marehemu David majebelle ukiwasili nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam.
 Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu David Majebelle likiwa nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam wakati wa ibada.
 Ibada ya kumuimbea marehemu David Majebelle ikiendelea kanisani.
 Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
 Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu David Majebelle ukishushwa kaburini.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula (kushoto), akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu David Michael Majebele, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinodoni jijini Dar es Salaam jana. Marehemu Majebele ambaye ni mwanahabari mkongwe alifariki Jumapili iliyopita. 
Familia ya marehemu David Michael Majebele, wakiweka mashada ya mauakatika kaburi, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinodnoni jijini Dar es Salaam jana. Marehemu Majebele ambaye ni mwanahabari mkongwe alifariki Jumapili iliyopita. 

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Umoja wa Watanzania Ujerumani (U.T.U ) Kushiriki katika Festival ya "Brüderschaft der völker " mjini Aschaffenburg " Ujerumani

0
0
Watayarishaji wa Festival ya "Brüderschaft der völker " mjini Aschaffenburg, nchini Ujeruamani,wameuhalika Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushiriki katika maonyesho hayo utamaduni wa nchi mbali mbali yatakayo anza 19 hadi 21 Julai 2013.

Watayarishaji wa maonyesho hayo wamevutiwa sana sana na shughuli za Umoja wa Watanzania ujerumani (UTU) kwa juhudi zake za kuitangaza Tanzania,wandaaji wa onyesho hilo wametoa nafasi kwa umoja wa watanzania kushiriki na kuitangaza Tanzania kwa kasi zaidi.

Mwenyekiti wa UTU Bw.Mfundo Peter Mfundo ameupokea mwaliko huo kwa mikono miwili na amewaomba Watanzania wote wanaoishi ujerumani kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo na kuitumia nafasi waliyopewa kwa maslahi ya Tanzania na watanzania, Umoja wa Watanzania (UTU) utakuwa na banda lake katika maonyesho hayo.

Mnakaribishwa wote na kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com pia unaweza kutembelea link ya maonyesho at http://www.bruederschaft-der-voelker.de/2013/05/29/union-of-tanzanians-in-germany/

MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA ATETA NA SWAHILI TV JIJINI WASHINGTON DC


TAASSISI ZA UMMA ZITUMIE FURSA KULETA KASI YAMAENDELEO - KOMBANI

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (MB) akifungua mkutano kuhusu Mchango wa Utumishi wa Umma katika Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano Uliofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

MWENYEKITI WA KIJIJI KILINDI JELA KWA RUSHWA YA KUUZA ARDHI KINYEMELA

0
0
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kwemakumbi katika kijiji cha Kireguru wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Hamza Rajabu Ngaramilo(56), leo amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa ili kugawa ardhi kwa wahamiaji wageni kijijini hapo.

Akisoma hukumu katika kesi nambari 113/12 iliyosomwa kwa mara ya kwanza Mei 7, mwaka jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Handeni mkoani humo Patrick Maligana, amesema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Serikali na hivyo anamtia hatiani mtuhumiwa huyo kama alivyoshtakiwa katika kosa hilo.

Awali Mwendesha Mashtaka wa (TAKUKURU) wilayani Handeni Bw. George Magoti, alidai kuwa Septemba mwaka 2012 siku na wakati usiofahamika, mtuhumiwa akiwa ni mtumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilindi kwa nafasi ya Mwenyekiti wa kitongoji cha Kwemakumbi katika Kijiji cha Kireguru, aliomba na kupokea rushwa ya shilingi 300,000.

Mtuhumiwa huyo wakati huo akiwa na umri wa miaka 55, alipokea fedha hizo kutoka kwa Gwandu Gaheri Langida na Kesi Safari Tlatlab ambao wote ni wahamiaji wageni kutoka katika kijiji cha Mang’ola Barazani wilaya ya Karatu mkoani Arusha ili awapatie ardhi kwa ajili ya kilimo.

Mwendesha Mashitaka huyo alisema, mtuhumiwa huyo aligawa ardhi hiyo yenye ukubwa wa ekari 40 jambo ambalo alisema ni kinyume cha sheria za ugawaji wa ardhi vijijini.

Bw.Magoti ameifafanulia mahakama hiyo kuwa, kwa mujibu wa taratibu za ugawaji wa ardhi vijijini, Mwenyekiti wa kitongoji ama kijiji anao uwezo wa kugawa ardhi isiyozidi ekari kumi kwa malipo ya shilingi 5,000 kwa mwanakijiji mkazi na shilingi 10,000 kwa mwanakijiji mhamiaji tofauti na alivyofanya mtuhumiwa kwa wahamiaji hao wageni.

Mwendesha Mashtaka huyo wa TAKUKURU ameiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa Wenyeviti wengine wanaokiuka utaratibu wa ugawaji wa ardhi vijijini na kuwafanya wananchi kutoa fedha nyingi kinyume na utaratibu kama ilivyo kwa mtuhumiwa huyo kitendo kinachotafsiriwa kuwa ni rushwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Maligana alisema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na kwa kuzingatia umri mkubwa wa mtuhumiwa huyo, anamhukumu kulipa faini ya shilingi 150,000 ama kwenda jela miaka minne kama atashindwa kulipa faini hiyo.

Lakini ili kujua kwamba maisha ni magumu hasa huko vijijini waliopo Wanzania wengi, Mtumiwa huyo alipelekwa Gerezani kuanza kifungo cha miaka minne jela baada ya kushindwa kulipa faini hiyo ya shilingi 150,000 na hivyo kuanza maisha mapya ya kifungwa Gerezani.

Hata hivyo pamoja na Mshitakiwa huyo kubadilishwa jina na kuitwa mfungwa, lakini Hakimu amesema anaweza kutoka Gerezani wakati wowote endapo atatokea ndugu ama rafiki wa kumlipia faini hiyo na stakabadhi ya malipo ya serikali ikapelekwa kwa Mkuu wa Gereza la Handeni. Ardhi husika itaendelea kubaki mikononi mwa walalamikaji.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA JAJI MSTAAFU, BUXTON CHIPETA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya Msiba wa Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, aliyefariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini Dar es Salaam. Makamu alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini leo Julai 19, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013. Marehemu Chipeta, alifariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini Dar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa ndugu wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo, nyumbani kwa marehemu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013. Marehemu Chipeta, alifariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Majaji waliohudhuria msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai, 19, 2013 baada ya kuhani msiba huo wa Jaji mstaafu Buxton Chipeta.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya waombolezaji katika msiba wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013 kwa ajili ya kuhani na kuaga msiba huo.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu katika msiba huo leo.Picha na OMR

Dkt. John Pombe magufuli amwondolea uvivu mkandarasi wa barabara ya Ndundu-Somanga

0
0
Waziri wa ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amekagua ujenzi wa barabara ya Ndundu Somanga yenye kilomita 65 itakayogharimu Shilingi bilioni 58.8 na kuagiza ifikapo Desember 30 mwaka huu mkandarasi wa barabara hiyo asipomaliza kazi afukuzwe na Asipewe kazi nyingine yeyote hapa nchini hata ikiwa ya kufagia.

SSRA, MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NA NIDA katika mikakati ya matumizi ya vitambulisho vya taifa

0
0
SSRA, MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NA NIDA imekutana ili kujadili jinsi vitambulisho vya Taifa vinavyoweza kutumika ili kuongeza wigo wa Wanachama katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii na hivyo kupunguza umaskini Nchini .

Pichani  kushoto mwakilishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Irene Isaka, Mkuu wa Tehama  SSRA Dr. Carina Wangwe na Wakurugenzi, Mameneja na maofisa wa Tehama wa mifuko ya hifadhi ya Jamii jinsi vitambulisho  vya taifa vinavyoweza kusaidia katika kupanua wigo wa hifadhi ya Jamii kwa kila Mtanzania.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images