Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 18 | 19 | (Page 20) | 21 | 22 | .... | 3286 | newer

  0 0


  Tunawashukuru wadau wote wa Mtandao wa WWW.FULLSHAANGWEBLOG.COM kwa uvumilivu wenu baada ya mtandao wetu kutokuwa hewani kwa siku mbili kutokana na matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wetu.

   Mtandao wa FULLSHANGWEBLOG umerejea hewani usiku wa kuamkia leo mara baada ya timu ya wataalam wetu kukamilisha kazi ya marekebisho na tayari tulishaanza kumuvuzisha matukio usiku huohuo.

  Tunasema asante kwa uvumilivu wenu na kutuelewa kila mlipotupigia simu kuulizia hali ikoje,tunawashukuru pia kwa simu zenu kwani tumejiona ni wenye bahati na kumbe mchango wetu mnautambua vizuri asanteni sana wadau.

  Tunatoa shukurani kwa wadau wetu wawezeshaji Benki ya NBC, Benki ya NMB,NHIF, TTB, SERENGETI BREWERIERS , WILNA INTERNATIONAL ,BAYPORTna R&R kwa uvumulivu wenu tunasema asanteni sana na Mablogger wote ambao walitusemea wakati tulipokuwa na tatizo hili.

  Shukurani za Pekee zimwendee Mustafa Selemani mtaalam wetu na timu yake kwa kuhakikisha wanarekebisha tatizo hilo mpaka tunarejea tena hewani usiku wa kuamkia leo tunakushukuru Mustafa na timu yako ya G5CLICK.

  Mwisho tunasema kazi inaendelea mbele na wadau wote mnakaribishwa kututumia habari na matukio mbalimbali kupitia Email ya johnbukuku@gmail.com na info@fullshangweblog.com nasi tutazimuvuzisha mtandaoni kama kawaida.

  0 0
 • 01/16/13--01:37: Kuni zipo Sokoni
 • Pamoja na kwamba Serikali imekuwa ikipiga vita sana ukataji wa Miti hovyo,lakini imekuwa tofauti kwa aliepanga kuni hizi kwa lengo la kuziuza kama kamera yetu ilivyozikuta katika eneo la Bunju A,jijini Dar.


  0 0

  Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi,Gilles Muroto akiongea na wananchi wa Mtaa wa Sanawari (hawapo pichani) uliopo kata ya Sekei halmashauri ya jiji la Arusha juu ya uanzishaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi
  Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi,Gilles Muroto (wa tatu kulia) akimtambulisha Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii Mkoa wa Arusha,Mrakibu wa Polisi (SP),Mary Lugola pamoja na askari wengine wa kitengo hicho mkoani Arusha. (Picha na mahmoud ahmad).


  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Gilles Muroto amewaambia wakazi wa Mtaa wa Sanawari waliopo Kata ya Sekei iliyopo halmashauri ya jiji la Arusha waunganishe nguvu zao pamoja ili waweze kuushinda uhalifu.

  Hayo aliyasema jana katika mkutano kati jeshi la Polisi na wananchi hao uliofanyika katika uwanja wa wazi uliopo mtaani hapo ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa jeshi hilo juu ya utoaji wa elimu ya polisi jamii kuanzia ngazi ya mtaa na vitongoji vya Mkoa huu wa Arusha.


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee (kulia)akibadilishana mawazo na Muakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi huko Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar.Baraza la Nane la Wawakilishi limeanza rasmi leo ikiwa ni Kikao cha kwanza 16 January 2013,Zanzibar.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee (katikati)akisisitiza jambo katika mazungumzo na Muakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jusa Ladhu nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawaklilishi huko Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar wamwanzo kushoto ni Muakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin. PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

   Mtandao wako uupendao wa www.globalpublishers.info hauko hewani kwa sasa kutokana na matatizo ya kiufundi yaliyojitokeza mapema leo ambayo yanashughulikiwa na wataalamu wetu.

  Ni maratajio yetu kuwa tatizo lililopo litatatuliwa mapema na Mtandao kurudi katika hali yake ya kawaida. Hata hivyo kwa wale wanaosoma magazeti yetu On Line, wataendelea kusoma kama kawaida kwa kwenda moja kwa moja kwenye anauani hii:

  Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote utaojitokeza katika kipindi hiki.

  Asanteni kwa uvumilivu wenu

  Web Master
  Global Publishers Ltd

  0 0

  U.S. Ambassador Alfonso E. Lenhardt, (in black suit at the center), pose in a group photo with awarded grantees after the Ambassador's Special Self-Help Fund grants presentation ceremony held yesterday at the U.S. Embassy in Dar es Salaam. During the presentation ceremony, he awarded Community Grants Program funds to eleven organizations working to improve the lives of Tanzanians and refugees living in Tanzania. The grants, which totaled $97,635 USD (approximately 151 million Tanzanian shillings), support five key sectors: education, economic development, water, solar power, and refugee assistance. The projects supported by the grants promote the United States' goal to partner with Tanzanians who lead efforts to promote development in their communities through their own leadership and ideas.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza kwa wajumbe wa mkutano wa tathmini ya mbio za Mwenge mwaka 2012 kuhusu serikali kufuatiliaji maendeleo ya miradi inayozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge mjini Zanzbar.
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ali Nassoro Lufunga akizungumza na viongozi na waratibu wa mbio za Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013.Mkoa wa shinyanga ulikuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kwa mwaka 2012.

  0 0

   Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Dar es Salaam wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda cha Bia cha TBL Arusha, Ben Mwanri (wa pili kushoto), walipotembelea Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, wakati wa  ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.
  Kiongozi wa ujumbe wa maofisa wa Jeshi kutoka Chuo ChaTaifa cha  Ulinzi (NDC) Mafunzo ya Kijeshi na Usalama, S.M Minja  (kushoto) akimkabidhi zawadi  Meneja wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda cha Bia cha TBL Arusha, Ben Mwanri, walipotembelea kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mgeni wake ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2013.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi wakiongea katika mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2013.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi wakiangalia ngoma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2013.
  Jakaya Mrisho Kikwete akiandika jambo huku akiangaliwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo Januari 16, 2013.PICHA NA IKULU

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akibadilishana mawazo na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
  Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
  Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
  Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Cleopa Msuya akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu mchakato wa Katiba Mpya leo (Jumatano, Januari 16, 2013) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.

  0 0

  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akimsikiliza Gavana wa Lions Ukanda wa Uganda na Tanzania, Joseph Kiwanuka, wakati alipomtembelea leo ofisini kwake akiwa na ujumbe wa watu watano.
  Waziri Simba akiangalia baadhi ya vyerehani viwili viliyotolewa na Lions kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wajane. Vyerehani hivyo ni kati ya 100 vitakavyotolewa na Lions kuwawezesha wanawake kujikimu kimaisha.
  Gavana Kiwanuka akimkabidhi cherehani Waziri Simba kabla ya kumkabidhi mfaidika wa pili wa vyerehani hiyo Bi. Mariam Mohamed.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akfungua rasmi jengo jipya la hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam baada ya kufungua jengo lake jipya leo Januari 16, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na baadhi ya Wafanyakazi wa hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua jengo lake jipya leo Januari 16, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia baadhi ya wafanyakazi na uongozi wa hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam baada ya kufungua jengo lake jipya leo Januari 16, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua jengo lake jipya leo Januari 16, 2013. PICHA NA IKULU

  0 0


  Wadau watatu wa mpira wa miguu wamechukua fomu za kuwania urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kufanya idadi ya waliojitosa katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24 mwaka huu kufikia 30.

  Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.

  Waliochukua leo (Januari 16 mwaka huu) kuwania urais ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne Nyamlani, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), Jamal Emil Malinzi na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kigoma, Omari Mussa Nkwarulo.

  Mwengine aliyechukua leo ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias Mwanjala anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuwakilisha Kanda ya Iringa na Mbeya.

  Orodha kamili ya wadau waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais), Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (umakamu wa rais).

  Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

  Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).

  Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).

  Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti.

  0 0

  Mke wa Rais mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)jioni ya leo,kesho atafunga mkutano wa kimataifa juu afya ya mama katika ukumbi wa mikutano AICC.
  Mke wa Rais mama Salma Kikwete akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Mama Itanisa mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)jioni ya leo,kesho atafunga mkutano wa kimataifa juu afya ya mama katika ukumbi wa mikutano AICC.
  Mke wa Rais mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Arusha,John Mongela mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)jioni ya leo,kesho atafunga mkutano wa kimataifa juu afya ya mama katika ukumbi wa mikutano AICC.
  Mke wa Rais mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)jioni ya leo,kesho atafunga mkutano wa kimataifa juu afya ya mama katika ukumbi wa mikutano AICC.
  Mke wa Rais mama Salma Kikwete akiwapungia mkono waimbaji wa kikundi cha Msanja cha jijini Arusha , mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)jioni ya leo,kesho atafunga mkutano wa kimataifa juu afya ya mama katika ukumbi wa mikutano AICC.
  Mke wa Rais mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi wa Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT) Mkoa wa Arusha, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)jioni ya leo,kesho atafunga mkutano wa kimataifa juu afya ya mama katika ukumbi wa mikutano AICC.Picha zote na Filbert Rweyemamu

  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na ujumbe wa watu wa Misri ulioongozwa na Waziri wa Maji wa nchi hiyo Dk.Mohamed Saad (kushoto) walipofika ofisini kwake kwaajili ya mazungumzo mbalimbali kuhusu sekta ya maji na umwagiliaji hassa suala la maji ya mto Nile ambayo chanzo chake ni ziwa Victoria. Magembe aliwataka kuimarisha Ushirikiano wa nchi hizo kwenye mambo yote wanayokubaliana na kwayale wasiokubaliana kuendelea na majadiliano.
  Waziri wa Maji wa Misri  Mohamed Saad (katikati) akizungumza na watendaji wa Wizara ya Maji nchini kulia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.Jumanne Maghembe kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Bilinith Mahenge.
  Wajumbe wa Serikali ya Tanzania wakinukuu mambo mbalimbali yaliyokuwa yakielezwa na ujumbe wa Wizara ya maji ya nchini Misri jijini Dar es Salaam leo.
  Balozi wa Misri nchini Tanzania,Hossam Moharam (kushoto) akiwa sambamba ujumbe wa nchi yake uliofika nchini kwa majadiliano ya mambo mbalimbali ya sekta ya maji.
  Ujumbe wa Wizara ya Maji ya nchini Misri ukifuatilia majadiliano.

  0 0


  H.E. Jakaya Mrisho Kikwete (right), President of the United Republic of Tanzania today met with H.E. Bon Yayi, President of the Republic of Benin for official talks in the State House, in Dar es Salaam. President Yayi who is also a Chairman for the African Union, is in the country for an official visit to discuss various matters including political situation in Madagascar, the situation in Mali and the progress in Somalia.

  President Kikwete gives his opening remarks during a press conference, highlighting recent SADC Organ Summit he Chaired, which was held on January 10 to 11, 2013 in the State House, in Dar es Salaam.

  During the press conference, President Kikwete talked about political impasse in Madagascar, saying that it was a work in progress. However, he welcomed and commended President Andry Rajoelina of Madagascar for taking a bold, patriotic decision not to contest the upcoming elections for the sake of peace and stability of the Madagascar.

  President Kikwete further noted that, the Southern Africa Development Community (SADC) had made a Declaration last week in respect to political situation in Madagascar. However, he said that the Declaration was placed on hold until President Rajoelina fulfills his commitment of not contesting the upcoming election in that country.

  "Given that President Rajoelina has done so, the SADC now will proceed and release the said Declaration", said President Kikwete.

  President Kikwete also commended former President of Madagascar, Mr. Mark Ravalomanana for taking a stand of not contesting the election. "It is an expression of greater political maturity for putting first the interest of people of Madagascar before himself," said President Kikwete.

  In concluding his remarks, President Kikwete expressed his pleasure of what had transpired in respect to Madagascar, reaffirming SADC's commitment to work with people of Madagascar before and during the elections, until political normalcy returns back in that country.


  Government Delegation from the Republic of Benin included Mr. Nassirou Arifari Bako (left), Minister for Foreign Affairs, Mrs. Mariam Aladji (center), Special Advisor to the President - Diplomatic Affairs and Mr. Aganu Laisi, Interpreter.

  President Kikwete concluding his remarks before members of the press (not in the photo). Listening on is his counterpart H.E. Boni Yayi of the Republic of Benin.

  Hon. Bernard K. Membe (MP), (center), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation listening to President Kikwete(not in the photo) during the press conference. Others are Mr. Nassirou Arifari Bako (right), Minister for Foreign Affairs of Benin and Ambassador Liberata Mulamula (left), Senior Advisor to President Kikwete - Diplomatic Affairs.

  President Boni Yayi of the Republic of Benin gives his remarks during the press conference. In his remarks, President Yayi extended his appreciation to President Kikwete (right) for his hospitality during his two-days official visit.

  President Yayi said he was also pleased to hear the report on the recent SADC Organ Troika Summit that President Kikwete had chaired, in particular, the political situations in Madagascar, Zimbabwe and Eastern Congo DRC.

  During the press conference, President Yayi said in his meeting with his counterpart H.E. Kikwete, the two Presidents discussed other regional areas such as Somalia and Mali.

  He updated the press on the current situation in Mali, saying that currently there are troops being deployed from Nigeria, Benin and Burkina Faso heading to that region. President Yayi welcomed other member States from the African Union to deploy more troops to Mali to secure the country's fallout.

  In concluding his remarks, President Yayi extended his invitation to President Kikwete to visit his country Benin, to the latter that President Kikwete accepted wholeheartedly.


  Hon. Bernard K. Membe (MP) (right), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation exchanges views with Ambassador Liberata Mulamula (left), Senior Advisor to President Kikwete (Diplomatic Affairs).

  H.E. Jakaya Mrisho Kikwete (right), President of the United Republic of Tanzania in a photo with H.E. Boni Yayi (left), President of the Republic of Benin. 
  All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation

  0 0

  APRM Tanzania Executive Secretary, Ms Rehema Twalib

  The African Union (AU) programme for governance assessment-the Peer Review Mechanism (APRM) Tanzania chapter has urged for views of the people to prevail on the future structure of the Union between Tanganyika and Zanzibar which formed the United Republic of Tanzania.

  Submitting the opinion of its stakeholders’ before a section of members of the Constitution Review Commission on Wednesday in Dar es Salaam, the APRM Tanzania Executive Secretary, Ms Rehema Twalib said their researchers have found out that the views of the people on the Union are diverse.

  “While our findings in the APRM report are clear that there are a number of Union queries which should be resolved, the views are so diverse on the future structure of the Union,” said Ms Rehema adding that: “On this basis APRM cannot have its own opinion on the matter but to leave it for the Constitution Review Commission to thoroughly consult the people to come up with a better position.”

  Tanzania joined the APRM since 2004 and is scheduled to present its final report in Addis Ababa, Ethiopia at the end of January, 2013 for consideration before an AU/APRM Forum of Heads of State and Government.

  The programme’s Coordinator for Socio-Economic Development, Dr. Cuthbert Ngalepeka told the Commission that in the APRM review consultations were held all over the country including desk research and perception survey.

  On his part the APRM Tanzania head of Media and Communications, Hassan Abbasi told the Commission that governance stakeholders’ also advised for improve legal and policy framework for press freedom and right to information.

  He urged that for better media related provisions; be it in the Constitution or any other enabling laws to be drafted, the Commission should, among other references expose itself to a model legislation championed by the AU Special Rapporteur on Freedom of Expression and Right to Information.

  31 out of 54 African countries are currently participating in the APRM.  Kenya and Zambia are also expected to submit their reports for consideration in the Addis Ababa Forum. Tanzania will enact its new constitution by 2014.

  0 0

  Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula na ujumbe wa kamati yake ya fedha wametembelea halmashauri ya manispaa ya Ilala kwa maagizo ya Mhe.Waziri Mkuu ili kujionea mbinu za kisasa za kukusanya mapato. Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa amewakaribisha na kuwaeleza jinsi walivyoweza na wanavyoendelea kukusanya mapato. Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilala zinaanzisha Udada.
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa akiendesha kikao hicho
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa kitoa somo
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa katika picha ya pamoja na wageni wake kutoka Mwanza

  0 0


  Photo: THE MIC KING: SADAM OUT, WATATU DANGER ZONE! MSHIRIKI wa Shindano la The Mic King lililoendelea kutimua vumbi kila Jumapili katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem jijini Dar, Sadam Rashid ‘KM 18’ ameliaga shindano hilo huku washiriki wengine watatu wakiingia kwenye eneo la hatari (danger zone). Awali, wasanii wawiliwawili kutoka katika makundi ya Risasi, Championi, Uwazi na Ijumaa waliwasilisha jukwaani kazi walizokuwa wamepewa huku majaji wa shindano hilo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, Ally Baucha na John Dilinga ‘DJ JD’ wakitoa komenti zao. Mwishoni, MC wa shindano hilo alimtangaza Sadam (pichani)kuwa ametolewa kutokana na kupata kura chache kutoka kwa watazamaji huku Hamza ‘KM 11’, Paizo ‘KM 17’ na Salum ‘KM 20’ wakitangazwa kuingia kwenye danger zone. Shindano huoneshwa kila Jumanne saa nne usiku katika Runinga ya DTV na marudio ni Alhamisi saa 10 jioni na Jumamosi kuanzia saa 8 mchana ambapo mashabiki hupata fursa ya kuwapigia kura washiriki wakati wakijinadi runingani.

  MSHIRIKI wa Shindano la The Mic King lililoendelea kutimua vumbi kila Jumapili katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem jijini Dar, Sadam Rashid  ‘KM 18’ ameliaga shindano hilo huku washiriki wengine watatu wakiingia kwenye eneo la hatari (danger zone). Awali, wasanii wawiliwawili kutoka katika makundi ya Risasi, Championi, Uwazi na Ijumaa waliwasilisha jukwaani kazi walizokuwa wamepewa huku majaji wa shindano hilo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, Ally Baucha na John Dilinga ‘DJ JD’ wakitoa komenti zao. Mwishoni, MC wa shindano hilo alimtangaza Sadam kuwa ametolewa kutokana na kupata kura chache kutoka kwa watazamaji huku Hamza ‘KM 11’, Paizo ‘KM 17’ na Salum ‘KM 20’ wakitangazwa kuingia kwenye danger zone. Shindano huoneshwa kila Jumanne saa nne usiku katika Runinga ya DTV na marudio ni Alhamisi saa 10 jioni na Jumamosi kuanzia saa 8 mchana ambapo mashabiki hupata fursa ya kuwapigia kura washiriki wakati  wakijinadi runingani.

  0 0


  Afisa Utekelezaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini katika Kitengo  cha Magari Bandari ya Dar es Salaam, Principal Operation Officer and Head of Motor Vehicle Section Dar es Salaam Port), Bw. Daniel Sira (wapili kusho) akiwaonyesha stika kwenye moja ya gari ambalo limekidhi vigezo vyote vya kuondoka bandarini. 
  Wengine wanaoshuhudia ni Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Bi. Janeth Ruzangi (katikati), kaimu afisa mawasiliano mkuu, Bw. Peter millanzi (kushoto) na afisa mawasiliano Mwandamizi, Bi. Levina Msia (Kulia). Waandishi wa habari walitembelea kitengo hicho cha kujionea shughuli za upakuaji magari.


  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema baada maboresho ya vitendea kazi yaliyofanyika bandari hapo hivi karibuni, kitengo cha magari (Motor Vehicle section) kinauwezo wa kupakua magari 1,000  kwa shifti moja ya masaa nane tofauti na kipindi cha nyuma ilikuwa inapakua chini ya magari 400.
  Afisa Utekelezaji Mkuu ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Magari Bandari ya Dar es Salaam (Principal Operation Officer and Head of Motor Vehicle Section Dar es Salaam Port),Bw. Daniel Sira aliwaambia waandishi wa habari waliotembelea kujionea upakuaji wa magari  bandarini hapo jana kuwa huduma ya upakuaji magari ni nzuri na inafanyika kwa haraka.
  “Tumefanya hivi kwa nia ya kutaka kutoa huduma nzuri na kwa haraka kwa wateja wetu wanaoagiza magari na wenye meli wasiweze kutumia muda mwingi katika bandari yetu,” na kuongeza kusema kuwa vifaa na ari ya kufanya kazi kwa bidii ndiyo imeongeza ufanisi huo.
  Alisema wameboresha upakuaji kwa kuwa na vifaa vya kutosha katika upakuaji ili kuruhusu meli kukaa muda mfupi bandarini sababu meli ikikaa bandari muda mrefu ni ghrama na hii inavutia wenye meli kuzidi kuleta meli zaidi kwenye bandari hii.
  Alifafanua kuwa wamefanya hivyo sababu mwenye meli na wenye magari wote ni wateja wa bandari hivyo wanategemea kazi ifanyike kwa haraka ili waweze kuondoka kwa haraka ndiyo maana wamefanya hivyo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wateja wote hao.
  Bw.Sira alisema utaratibu wa sasa wa kukaguwa magari wakati wa upakuaji kutoka kwenye meli wafanyakazi wanafanya kwa umakini mkubwa na huweka alama ya stika ya njano kwa magari yasiyo na matatizo ya upungufu wa vyifaa,na alama nyekundu kwa magari yaliyo na vifaa pungufu.
  Alisema katika eneo la upakuaji, magari yaliyokamilika vifaa vyote yanaruhusiwa kuondoka katika eneo hilo yakiwa na alama ya stika ya kijani na alama nyekundu kwa yale yenye matatizo kivifaa tangu yakiwa kwenye meli.Shughuli ya ukaguzi huo inafanyika wakati wa upakuaji kutoka kwenye meli ili kuwa na uhakika wa uzima wa magari pindi tu yanapokuwa yanapakuliwa huku wenye meli wakiwa pale kwa ajili ya kukabidhiana.
  “Zamani wakati wa upakuaji kulikuwa na ucheleweshaji sababu kila gari likiwa nzima au linamatatizo yote yaliandikiwa formu ya Vehicle Discharge Inspection and Transfer Tally (VDITT) lakini kwa sasa haifanyiki hivyo.
  Alisema magari mazima kwa sasa hayaandikiwi fomu hizo, bali yanaruhusiwa kuondoka toka eneo la upakuaji kwa kuwekewa alama ya kijani, na zile zenye matatizo kutoka kwenye meli zinaandikiwa fomu hiyo katika eneo la upakuaji wakati wa makabidhiano na wenye meli ili mamlaka isiweze kuingia garama ambayo haikuhusika.
  Alisema pia magari yaliyoshuka ambayo ni mazima lakini yakanyofolewa vifaa bandarini wakati wa makabidhiano na wakala wa mizigo yanaandikiwa fomu ya Vehicle Handover (VHF) ili kuonyesha uharibifu huo umetokea bandarini hapo.
  Alisisitiza magari yakiwa na matatizo tangia kwenye meli, wenye meli anakuwa na jukumu la kulipa gharama ya magari kwa wenye magari sababu amesabisha uharibifu huo, na kuongeza kusema kuwa inapotokea magari yamepakuwaliwa yakiwa yamekamilika kivifaa lakini likatokea tatizo la kunyofolewa vifaa yakiwa bandari basi mamlaka inakuwa na jukumu la kulipa gharama hizo kwa wenye magari.
  Alisema gari likiwa na stika nyekundu kabla ya mteja kukabidhiwa linakaguliwa upywa kati ya karani wa bandari na wakala wa mzigo, wanasainishana kwa kuangalia vifaa vilichopungua baada ya kushushwa kwenye meli.
  “Katika mazingira hayo kama gari limepungua vifaa likiwa kwenye meli mteja anatakiwa kumdai mwenye meli au alikonunua na kama limepungua vifaa likiwa bandarini basi mteja aidai bandari,”.
  Pia alitoa wito kwa waagizaji wa magari wauzaji au mtu mmoja mmoja anayeagiza gari kuwa wanatakiwa kudai fomu ya VDITT na VHF ambazo ni nyaraka zinazosaidia kujiridhisha magari yao kama yako salama au vinginevyo.
  Alisema wenye magari wanatakiwa kudai fomu hizo kutoka kwa wakala wa mizigo (Clearing and Forwarding Agency) ambao wanakuwa na fomu hizo baada ya makabidhiano kati yao na bandari
older | 1 | .... | 18 | 19 | (Page 20) | 21 | 22 | .... | 3286 | newer