Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

BREAKING NYUUUZZZZZ: MAFURU RESIGNS FROM NBC

$
0
0

 I have today 24th December 2012 submitted my formal resignation as Managing Director of NBC to the Chairman of the Board of Directors of NBC to pursue other opportunities outside NBC.


As I had mentioned in my letter to the Chairman, this has not been an easy decision but as career person, there are times in our career life we have to make difficult decisions. The decision to relinquish my position is completely in line with my career objectives. After 4 years of a very progressive career at NBC, first as Country Treasurer since August 2007 and later as Chief Executive Officer since June 2010 to date, I think that it is appropriate to seek other challenges elsewhere and allow others to steer the ship at NBC.


Former NBC boss Lawrence Mafuru
Looking behind 4 years ago – I am very satisfied with the success I have had especially on the transformation agenda of NBC operations. We now have a much cleaner balance sheet, a stronger pool of talented young men and women; our customer experience has improved relative to where we are coming from and even more important we are well positioned for strong and sustainable growth in the next 3 years. On a personal note, I have had the opportunity to grow and develop professionally – I have grown both as business manager and a leader not only in the bank but also at industry level where I was privileged to serve as Chairman of Tanzania Bankers Association, I take pride that I also have been actively involved in shaping the future of banking in Tanzania.


I want to thank the board of NBC, my colleagues in the management team and the entire staff of NBC for the support and dynamism. I have no doubt in my mind that together with new leadership they will consolidate the success we have had in our transformational work and take the bank to the next level of being the ‘Go-To’ bank in Tanzania. All this success would not have been possible if it was not for the continued support from clients, customers and other stakeholders to whom I would like to express my most sincere gratitude.

I will announce my next destination that will certainly take me through the journey of ‘’success to significance’’, once I am through with what my family and I consider a well deserved rest , starting with the festive season, for which I extend my best wishes to all those who touched my life during my time at NBC.


Lawrence Mafuru

24th Dec 2012.


salamu za krismasi toka kwa nathan mpangala

mdau asherehekea kula nondozzz na wazee wasiojiweza

$
0
0
Ni mdau Rehema Mwaituka  ambaye baada ya kula nondozzzz yake  katika fani ya ustawi wa jamii katika Chuo cha Ystawi wa Jamii jijini Dar es salaam aliamua  kusherehekea na wazee wanaoishi katika kijiji cha wasiojiweza cha Msimbazi Centre jijini Dar es salaam
 Rehema akiwakaribisha wazee katika meza ya chakula
 Mdau Rehema akipata mlo na wazee

Mh. Lowassa ashiriki Ibada ya Sikukuu ya Krismas Visiwani Zanzibar leo

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakiungana na Wakristo wengine kwenye ibada ya Sikukuu ya Krismas iliyofanyika leo kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa salaam za Xmas kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar mara baada ya ibada ya Sikukuu hiyo leo.Mh. Lowassa yuko visiwani humo kwa mapumziko ya sikukuu hiyo,ambapo amewataka watanzania kusherehekea sikukuu hizi za krismas na mwaka mpya kwa amani na upendo huku tukilinda umoja na mshikamano uliojengwa na waasisi wetu Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume.

Kusogezwa mbele kwa Fainali ya tuzo za Wazalendo 2012

$
0
0

Kamati ya maandalizi ya Fainali ya tuzo za Mwanasoka Bora wa mwaka (Wazalendo Footballer of the Year), imeamua kusogezwa mbele kwa fainali hizo ambazo zilikuwa zifanyike Desemba 30 mwaka 2012 jijini Dar es Salaam ambapo sasa zitafanyika Januari 31 mwaka 2013.
Licha ya hatua muhimu kukamilika lakini zipo sababu za msingi ambazo kamati imeona ni busara kuzifuatilia ili kufanya tuzo hizo kufanyika kwa ufanisi.
  1. Asilimia 90 (90%) ya Wajumbe wa kamati hiyo ni wanachama wa chama cha makocha wa Tanzania (Tafca) ambao wapo kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu wa chama chao hivyo kushindwa kukamilisha baadhi ya mambo kwa wakati.

  1. Pia wapi baadhi ya wageni muhimu ambao walialikwa asilimia (80%) wameonyesha kutokuwepo kwa tarehe hiyo (Demsemba 30, 2012) kwa sababu watakuwa nje ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya siku kuu za mwisho wa mwaka jambo ambalo kamati imeona pia ni jambo la msingi.
Kwa kuzingatia uzito wa jambo lenyewe kamati imeona ni busara kusogeza mbele kwa siku 30 kwa lengo la kuwapa nafasi wahusika kwa pande zote mbili kuendelea na matayarisho hayo ili kuwa na ufanisi kwenye jambo hili la kitaifa lenye nia ya kusaidia kuinua na kuendeleza vipaji vya soka kwa Watanzania.
Majina yalioingia fainali

Januari Mosi 2013, Kamati ya maandalizi ya tuzo za Wazalendo,  inarajia kutangaza majina ya wanasoka ambao wameingia kwenye fainali mwaka 2012. Hatua hii ni baada ya kukamilisha mchujo wa uliokuwa umefanika hapo awali  wa kupitia majina zaidi ya 93 yaliyopigiwa kura na mashabiki tangu Agosti-Novemba mwaka huu.
Imetolewa na:-

Ahadi Kakore
- Mratibu.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZULU KABURI LA HAYATI IDRIS ABDULWAKIL, MAKUNDUCHI, AMTEMEBELEA MZEE ALI KHAMIS ABDALLAH MWASISI WA AFRO SHIRAZ PARTY

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) akiwa mbele ya Kaburi la Rais wa zamani wa Zanzibar  Hayati Idris Abdulwakil, wakati alipozuru Kijiji cha Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja juzi. Rais  Wakil alifariki dunia mwaka 2001. Dk Bilal alifika  eneo hilo  juzi katika ziara yake ya kuwatembelea  wazee mbali mbali mkoani humo, jana.  
 Makamu akiondoka katika kijiji hicho cha Makunduchi baada ya kuzulu Kaburi la Hayati, Abdulwakil, jana.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee Ali Khamis Abdallah (98) ambaye ni mmoja kati waasisi  10,  waliokaa pamoja na  kuunganisha vyama vya African Association na Shiraz Association na kuwa Chama cha Afro Shiraz Party (ASP), wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea wazee, leo nyumbani kwake Mbweni, mjini Unguja. Kulia ni mke wa Mzee Ali, Asha Ali Ghulam Hussein. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Ali Khamis Abdallah (98) ambaye ni mmoja kati waasisi  10,  waliokaa pamoja na  kuunganisha vyama vya African Association na Shiraz Association na kuwa Chama cha Afro Shiraz Party (ASP), wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea wazee, leo nyumbani kwake Mbweni, mjini Unguja. 
.Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Rais

Dk. Mukangara atembelea vijiji vya kitigiri na Bugalama wilayani Geita

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa kikundi cha Nyakalalo kililopo kijiji cha Kitigiri wilayani Geita, Gideon Msabila (kushoto) ambaye alimuelezea jinsi walivyonufaidika na mkopo wa mfuko wa maendeleo ya vijana fedha ambazo zimewawezesha kufungua duka la rejareja la bidhaa za nyumbani.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) akiangalia nguo zinazoshonwa na kikundi cha ushonaji kilichopo kijiji cha Bugalama wilayani Geita ambacho kimenufaika na mkopo wa shilingi milioni mbili kutoka mfuko wa maendeleo wa halmashauri hiyo. Waziri Dk. Mukangara alitembelea kijiji hicho jana ili kuona fedha za mkopo zimewasaidiaje vijana kujikwamua kimaisha.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Geita, Kata ya Bukondo na kijiji cha Kitigiri mara baada ya kumaliza ziara yake katika kijiji hicho jana ili kuona fedha za mkopo za mfuko wa maendeleo ya vijana zimewasaidiaje vijana kujikwamua kiuchumi.
Vijana wa kikundi cha kusaidiana kulima cha Busaka katika kijiji cha Kitigiri wakifurahia fedha shilingi 50,000/= walizopewa jana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne kulia) kwa ajili ya kununulia soda za sikukuu ya Krismasi . Waziri Dk. Mukangara aliwahimiza vijana hao kujiunga kwenye vikundi vya maendeleo vya kilimo ili weweze kupata mkopo wa kununulia pembejeo na kuweza kuzalisha chakula kwa wingi zaidi.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne kulia) akiongea na vijana wa kikundi cha kusaidiana kulima cha Busaka kilichopo kijiji cha Kitigiri wilayani Geita umuhimu wa kujiunga kwenye vikundi vya maendeleo vya kilimo ili weweze kupata mkopo wa kununulia pembejeo na kuweza kuzalisha chakula kwa wingi zaidi .
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa kikundi cha Bodaboda kilichopo kijiji cha Bugalama wilayani Geita, Enos Komanya wakati alipotembelea kikundi hicho ambacho kilipata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo wa halmashauri. Waziri Dk. Mukangara alitembelea kijiji hicho jana ili kuona fedha za mkopo zilizotolewa na mfuko wa maendeleo ya vijana zimewasaidiaje vijana kujikwamua kimaisha.

MATUKIO YA IBADA YA KRISMASI KATIKA PICHA

$
0
0
Askofu Msaidi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam,  Eusebius Nzigilwa  (katikati) akiongoza ibada ya mkesha wa Sikuu ya Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Paroko wa kanisa hilo, Padri, Joseph Mosha.  (Picha na Habari Mseto Blog)
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Krismasi leo.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akitoa baraka kwa waumini wa Usharika wa Azania Front baada ya ibada ya Krismasi
 Mmiliki wa  Mtandao wa Kijamii wa Kimbunga Net, Dotto Mwaibale akipeana mkono na Askofu Mkuu wa KKKT, Dk. Alex Malasusa baada ya ibada ya Krismasi iliyofanyika leo katika Usharika wa Azania Front. Kulia ni mmiliki wa mtandao wa Mzuka wa Fungo, Omary Fungo.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiwa amembeba mtoto, Prisca John Mkony. Kushoto ni Sia Robinson na Jane Mkony akiwa amembeba mtoto, Patricia.
 Baadhi ya waumini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph wakiwa katika ibada ya Sikukuu ya Krismas.

 Mkurugenzi wa Free Media Ltd, Liliani Mtei (kulia) akiwa na baadhi ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wakisikiliza mahubiri yaliyokuwa yakitolewa na Askofu wa kanisa hilo, Dk Alex Malasusa (hayupo pichani) wakati wa ibada ya Krismasi iliyofanyika.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akipeana mkono na muumini wa kanisa hilo, Sevestine Mtunga baada ya ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika katika kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya akinamama waliojifungua wakati wa mkesha wa Sikukuu ya Krismasi wakiwa na watoto wao katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto  ni Fatuma Shaban mkazi wa Vingunguti, Lucy Dominick mkazi wa Mwananyamala na Moshi Mengi mkazi wa Manzese
  Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akitoa Baraka kwa mtoto, Patricia John Mkony mara baada ya ibada ya Sikukuu ya Krisimasi iliyofanyika katika kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni, Rubani Mkuu mstaafu wa Serikali, Kapteni John Mkony, Jane John na Sia Robinson.
Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia mpya ya Mt. Bonaventure, Kinyerezi wakifuatilia sehemu ya ibada ya Krisamsi iliyokuwa ikiendeshwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, Dar es Salaam leo.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Muadhama Polycarp Kadinali Pengo akipokea michango mbalimbali ya fedha kutoka kwa viongozi wa jumuiya za kikristo katika jimbo la segerea, dar es salaam alipokwenda kuongoza ibada ya Krismasi sambamba na uzinduzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Bonaventure, Kinyerezi, Dar es Salaam leo.

Kibo Sound band ndani ya Four Seasons Safari Lodge, Serengeti

$
0
0
Kibo Sound band wakitumbuiza katika hoteli ya Four Seasons Safari Lodge (zamani Bilila) katika hifadhi ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara.

Vijana wa Kundi la The Voice waakiimba wakati wa Onyesho la Miss East Afrika

hoteli ya serena Serengeti Lodge yaibuka kidedea kwa kunyakua kombe la ujirani mwema kwa kuishinda Four Seasons safari Lodge

$
0
0
: Mabingwa wa Kombe la Ujirani Timu ya hoteli ya Seronera wakifurahia ushindi baada ya kuilaza kwa mabao 5-4 hoteli ya Four Seasons Safari Lodge  katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara leo. Hadi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.  Mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Kikwete.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na timu ya Serena Serengeti Lodge kabla ya mchezo
 Rais Jakaya Kikwete akipozi na timu ya Four Seasons safari Lodge
 Mashabiki wa timu hizo mbili wakicharurana wakati mchezo unaendelea
 Wadau wakishuhudia mpambano huo
Hureeeeeeeee.......!!!! Serena wakishangilia penati ya mwisho iliyowapa ubingwa baada ya kuwashinda Four Seasons safari Lodge kwa matuta.

MERRY MERRY CHRISTMAS (The Sporah Show)

Kumbukumbu

$
0
0
FAMILIA YA BW. DANI & ANNA MAFURU WA DUBAI KWA PAMOJA NA FAMILIA NZIMA YA MAREHEMU MAFURU POPOTE WALIPO, TUNAKUKUMBUKA BABA YETU MPENDWA ULIYE TUTOKA 26.DEC.1997 
NI MIAKA 15 SASA TANGU UTUTOKE KWA 
PAMOJA TUNASEMA UKO PAMOJA NASI KIROHO
UNAKUMBUKWA NA FAMILIA PAMOJA NA UKOO MZIMA

                            AMEN

WAFANYAKAZI WA BENKI YA NBC WATOA ZAWADI ZA X-MAS NA MWAKA MPYA

$
0
0

Meneja Mwandamizi Idara ya Utendaji wa Benki ya NBC, Salim Rupia (kulia) akikabidhi msaada vyakula na vitu vingine vilivyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA, Ally Saidi kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Sikukuu za Christmas na mwaka mpya. Wafanyakazi hao walichanga zaidi ya shs milioni 3 kwa ajili ya vitu hivyo na sehemu ya pesa itatumika kulipia ada za shule kwa baadhi ya watoto mwakani. Wengine ni baadhi ya wafanyakazi hao na watoto wa CHAKUWAMA.
Meneja Huduma kwa Wafanyakazi wa NBC, Suzyo Gwege-Nyirenda (kulia) akikabidhi msaada vyakula na vitu vingine kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha CHAKUWAMA, Sinza jijini Dar es Salaam vilivyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Sikukuu za Christmas na mwaka mpya. Wafanyakazi hao walichanga zaidi ya shs milioni 3 kwa ajili ya vitu hivyo na sehemu ya pesa itatumika kulipia ada za shule kwa baadhi ya watoto mwakani.

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0
Huku Cameroon kulikuwa na gwiji wa muziki barani Africa mtu mzima Manu Dibango ambaye alitamba sana na ngoma yake ya 'Soul Makossa'. Angalia ala zinavyochezewa na kuchezwa...

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

$
0
0

Kundi la Off Side Trick toka Zanziba na Bi Kidude wanatamba hadi leo na kibao chao cha 'Ahmada'

PARTY YA MWISHO YA MWAKA 2012 WASHINGTON DC,JUMAMOSI HII TAR 29..EAST /SOUTH VS WEST AFRICA EXCHANGE..WHO'S THE BEST !!

$
0
0
PARTY YA MWISHO YA MWAKA 2012...JUMAMOSI HII DEC 29 ..NI WEST AFRICA AGAINST EAST/SOUTH AFRICA...BAR IKO WAZI BURE (ALL U CAN DRINK) KUANZIA SAA 4 HADI 5 USIKU..ONLY 16 VIP TABLES LEFT....FUNGA MWAKA KWA STYLE....CLUB BABKUBWA....4 FLOORS TO PARTY....TO GET IN FOR FREE KABLA YA SAA 5 USIKU AU KU RESERVE VIP TABLE...TUMA EMAIL TO RSVP@DMKPROMOTIONS.COM AU MPIGIE "DMK " 301-661-6207

bao

DIAMOND, DIMPOZ WAFANYA KUFURU USIKU WA X-MAS DAR LIVE

$
0
0
...Dimpooo...zzz: Umati ukipiga yowe wakati Ommy Dimpoz akifanya kufuru stejini....Leka dutigite: Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Diamond wakiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa Leka dutigite....Nature ua... Nature ua... Nature ua..: Ndivyo Juma Nature alivyokuwa akienda sambamba kwa staili hiyo na mashabiki.


Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' na Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' usiku wa kuamkia leo wameweka historia kwa kufanya shoo ya aina yake ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. 

Wasanii hao walisindikizwa na mkali Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi, Msanii mkongwe Ally Baucha pamoja na Bendi ya Extra Bongo. Shoo hii imeletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Serengeti Premium Lager na Vodacom - Wajanja wa Kujirusha.

Yaliyojiri kwenye Vodacom Krismass Bonanza’ katika ufukwe wa Coco Beach Dar es Salaam

$
0
0
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la ‘TMK Wanaume Halisi’ Juma Nature, akiburudisha mamia ya mashabiki waliohudhuria kwenye ‘Vodacom Krismass Bonanza’ katika ufukwe wa Coco Beach Dar es Salaam jana, Vodacom Tanzania imedhamini Bonanza hilo katika kipindi hiki cha sikukuu.
Mmoja wa wasanii kutoka kundi la TMK Wanaume Halisi, Rashid Ziada, maarufu ‘KR Mula’ akifanya show mbele ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliohudhuria kwenye ‘Vodacom Krismass Bonanza’ katika ufukwe wa Coco Beach Dar es Salaam jana, Vodacom Tanzania imedhamini Bonanza hilo katika kipindi hiki cha sikukuu.
Watoto ndani ya bwawa la kuogelea ‘Swimming Pool’ wakifurahia moja ya michezo waliyoandaliwa Vodacom Tanzania, katika Vodacom Krismass Bonanza lililofanyika kwenye ufukwe wa Coco Beach Dar es Salaam jana.
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images