Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

KUCHELEWA KUTOA FEDHA ZA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANANCHI KWASABABISHA MWEKAHAZINA WA KALIUA KUKALIA KUTI KAVU

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT

KUCHELEWA kupelekwa fedha ambazo zilitakiwa kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za wananchi ili waweze kukamilisha Mradi wao wa Ujenzi wa jengo la Mashine ya Usindikaji wa Mafuta katika Kijiji cha Kombe umesababisha Mwekahazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kupewa wiki mbili kuhakikisha fedha hizo zinafika haraka la sivyo atakuwa amejiundoa kazini mwenyewe.

Msimamo huo umetolewa jana wilayani Kaliua na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Mashine ya kukamulia mafuata ya alizeti ambao umekwama kumalizika kwa zaidi ya miezi mitatu baada ya Halmashauri kuchelewa kupeleka fedha ambazo ilitakiwa itoe.

Alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wananchi wamejituma kujenga jengo kwa ajili ya kuweka mashine ya kusindika mafuta ya alizeti lakini  Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua hadi hivi sasa hajitoa milioni 4 zilizotakiwa kuunga mkono nguvu za wananchi hao.

 Aidha Mwanri aliongeza kuwa pia kiasi kingine ni zile milioni 17 zilizotolewa na Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Miombo kwa ajili shughuli mbalimbali kama vile ufugaji kuku, kilimo cha uyoga, ufugaji nyuki zimekwama kupelekwa kwa walengwa kwa sababu ya Ofisi ya Uhasibu ya Halmashauri hiyo kuchelewesha wakati Wilaya nyingine zimeshapeleka kwa walengwa na kuanza kufanyakazi. Alisema kuwa hawezi kumvumilia mtumishi wa sampuni hiyo ambaye ameshindwa wa kutumia fedha miradi kwa wakati ambazo zimetengwa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi katika kuwainua kiuchumi na kuwaletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla kwa sababu ya urasimu usio na maana kwani kufanya hivyo ni kuwakatisha tamaa.

Mwanri alisema kuwa ndani ya wiki mbili mbili anataka kupata majibu ya hatua ambazo zimefikiwa katika kuhakikisha kuwa fedha hizo za mradi endelevu wa miombo zimeshapelekwa eneo husika na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua imeshawakabidhi wananchi hao milioni 4 ili wamalizie  jengo la mashine yao.

Mwanri alisema kuwa kinyume cha hapo wahusika wote watakuwa wamesbabisha mradi huo kutofanikiwa waanze kuondoka kwa hiari yao. Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alitoa siku mbili kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kuhakikisha wanapeleka taarifa ya miradi yote inayotekelezwa na gharama zake na muda wa kukamilisha mradi. Alisema kuwa hatua hiyo inataka kufanya Ofisi yake kuwa na uhakika wa thamani halisi ya fedha na ubora wa mradi ili kuona kama kweli utawanufaisha wananchi.

 Naye Mratibu wa Mradi wa Miombo Wilayani Kaliua Bennett  Kamara alisema kuwa taratibu zote za kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa na miombo zinatolewa na Mkurugenzi Mtendaji ili ziunge mkono juhudi za wananchi zilishakamilika muda mrefu  lakini kwa muda mrefu fedha hizo bado ziko ofisi ya Uhasibu.

 Kwa upande wa Katibu Tawala Msaidizi Dkt. Philip Ntiba alitoa wito kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kutoa haraka fedha mapema ili kuwakatisha tamaa wananchi waliojitolea nguvu zao kuanzisha mradi huo.

ZANTEL YATOA MSAADA WA MIAMVULI 60 KWA CHUO CHA USTAWI WA JAMII JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Jensen Msechu (kushoto) akisimika moja ya miamvuli iliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa Chuo cha Ustawi wa Jamii hivi karibuni jijini Dar es salaam.Jumla ya Miamvuli 60 ilitolewa kwa chuo hicho kwa lengo la kuwakinga jua wanafunzi wakati wa kujisomea wawapo chuoni hapo. Katikati ni Afisa Rasilimali watu Mwandamizi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Remidius Leonard na kulia ni Rais wa Wanafunzi, John Filimon.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii kilichopo eneo la Bamaga jijini Dar es salaam wakijisomea kwenye moja ya kizimba kilichosimikwa moja ya miamvuli iliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel hivi karibuni jijini Dar es salaam. Jumla ya miamvuli 60 ilitolewa kwa ajili ya kuwakinga jua Wanafunzi wa chuo hicho wakati wa kujisomea wawapo chuoni hapo.

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWAPONGEZA TANROADS KUDHIBITI VITENDO VYA RUSHWA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), amewapongeza Wakala wa barabara nchini (TANROADS), kwa mikakati wanayotumia kudhibiti vitendo vya rushwa katika vituo vya mizani hapa nchini.

Akifungua Mkutano wa tisa wa baraza la wafanyakazi la TANROADS mjini Kigoma, Naibu Waziri Kwandikwa, amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha watendaji wake wote wanakuwa waadilifu ili rasilimali chache zitumike kwa manufaa ya wote.

“Hakikisheni kila mtakaye mkamata kwa vitedo vya rushwa hatua za kisheria anachukuliwa ikiwemo na kufukuzwa kazi ili kuonyesha kuwa jambo la rushwa tunalichukia na hatulipendi katika Serikali”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), akizungumza na wajumbe katika mkutano wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), lililofanyika mkoani Kigoma.
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa baraza la tisa la wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (hayupo pichani) katika ufunguzi wa baraza hilo, mkoani Kigoma.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi akitoa taarifa ya utendaji kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (kulia), mkoani Kigoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Tunakoelekea msichana hatoolewa bila ya “leaving Certificate” - Naibu Waziri TAMISEMI

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda amewatahadharisha Viongozi wa dini nchini kujihadhari na kuwaozesha wasichana ambao hawajamaliza elimu ya kidato cha nne ili kuwakamata wazazi wote wanaoshiriki kuwaozesha watoto wao kwasababu ya kupewa mimba wakiwa masomoni.

Amesema kuwa watoto wa kike wanashindwa kumaliza masomo kwasababu ya mimba ama kuozeshwa jambo ambalo limeendelea kuisumbua serikali katika juhudi zake za kuokoa maisha ya watoto wa kike ili waendelee na masomo na kuongeza kuwa Wilaya ya Nkasi kuna tatizo sugu la mimba kwa kuwa na mimba 152 kati ya 325 kwa Mkoa mzima.

Amefafanua kuwa serikali ya awamu ya tano inathamini sana maisha ya watoto wa kike na inaendelea kuweka mikakati ya kila namna ili kuhakikisha kuwa wasichana hao wanapata elimu stahiki, kwa kuanza na elimu bure na kuendelea na mikakati ya marekebisho ya sheria kadhaa ili watoto wa kike waendelee na masomo.

“Haiwezekani mtu anatakatisha fedha hapati dhamana, halafu mtu anampa mimba mwanafunzi na kisha anapata dhamana, tunakoelekea ili uolewe lazima uwe na “leaving Certificate” ama tujue kuwa hukusoma kabisa ili tuwahoji wazazi, mwananfunzi ambae ataolewa kwa kukatishwa masomo kamata wote na funga miaka 30, wazazi wa pande mbili, aliyeoa, aliyeolewa, wanaoshangilia, aliyefungisha ndoa wote miaka 30 jela,” alifafanua.

Aidha, amewashauri wanaharakati kuungana pamoja katika kuwaelimisha watoto wa kike na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha mimba zinapungua na kuwa vitendo hivyo haviendelei, ili kuwainua watoto wa kike kielimu.

Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya katika majumuisho ya ziara yake ya siku moja katika Mkoa wa Rukwa kwa kutembeleavituo vya afya, Shule zinazoendelea kujengwa pamoja na miradi ya maji.

Sambamba na hilo Mh. Kakunda pia ameagiza kutosajili vijiji, vitongoji wala kupeleka umeme kwenye hifadhi na kuwaondoa wale wote waliopo kwenye hifadhi na kusisitiza kuwa wananchi wasidanganyike na viongozi wa vyama vya siasa kwa kuwambia kuwa watawalindwa ili kuendelea kuharibu hifadhi, jambo hilo halipo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Milundikwa Pius Msongoli wakati alipotembelea shule hiyo inayoendelea kujengwa huku serikali ikichangia shilingi milioni 250 za ujenzi wa shule hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda (Kaunda suti Nyeusi) akitoa maagizo ya kuwaondoa wale wote waliopo ndani ya hifadhi ya msitu wa mfili, kwa kuwa wanachangia kuharibu chanzo cha maji na bwawa la Mfili.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya ujenzi wa maabara inayoendelea kujengwa katika shule ya sekondari Milundikwa mbele ya Mkuu wa Shule hiyo Pius Msongole, Katibu tawala wa Wilaya ya Nkasi Festo Chonya pamoja na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Emanuel Mtika.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda (aliyeshika chepe) akisaidia ujenzi wa wodi za kituo cha afya Nkomolo, Wilayani Nkasi.

SIMBA HAOO.....KUELEKEA MBEYA KUZIFUATA POINTI 6

$
0
0

KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kuondoka kesho kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya michezo miwili ya  ligi kuu Vodacom dhidi ya Mbeya City na Prison huku  kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog akiweka wazi kuwa anataka kuvunja rekodi ambayo ni kuibuka na pointi sita kwenye michezo miwili mbele ya wapinzani wao, Mbeya City na Prisons.


Omog na jeshi lake la Simba litakuwa na kibarua kigumu cha kucheza kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo mara kwa mara wamekuwa na matokeo mabaya, ambapo Jumapili watawavaa Mbeya City kwenye uwanja huo kisha kumaliza na Prisons, Novemba 18, mwaka huu.

Mcameroon huyo amesema pamoja na rekodi mbaya kila wanapocheza uwanjani hapo lakini safari hii hawataruhusu hilo litokee kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa wa pointi tatu za kila mchezo.

“Tunajua kuwa mara kwa mara tunasumbuka kupata matokeo hapa Sokoine, lakini safari hii sitakubali kuona hilo linatokea tayari tumeshaweka mikakati kabambe ya kupata pointi sita kutoka kwa wenyeji wetu".

“Tunataka tushinde kwa ajili ya kujiongezea wigo wa pointi dhidi ya mahasimu wetu ambao tunalingana nao kwenye msimamo, na hatuwezi kuwakimbia bila ya kupata matokeo mazuri hasa kwenye mechi kama hizi za ugenini.

“Niseme wazi kwamba lile suala eti la kuwa na rekodi ya kupoteza mechi kila tunapokuwa hapa Mbeya kwa sasa ndiyo limefika mwisho,” alisema kocha huyo.


Mratibu wa timu hiyo, Abbas Ally alisema taratibu zote za kukamirisha safari hiyo zimekamilika.“Timu inatarajiwa kuondoka jijini Dar kesho saa tatu kamili asubuhi na ndege tukielekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wetu wa Jumapili dhidi ya Mbeya City na Prison.


NAIBU WAZIRI WA KILIMO ATEMBELEA KIWANDA CHA MBOLEA MINJINGU-MANYARA

$
0
0

Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky) mara baada ya kuzuru katika kiwanda hicho kilichopo katika eneo na Kata ya Minjingu Mkoani Manyara. (Picha Zote Na Mathias Canal).
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).

HOTUBA YA RAIS DKT. MAGUFULI WAKATI ALIPOFUNGUA KIWANDA CHA POLYBAGS MWANZA TAREHE 31 OKTOBA 2017

NEC YATOA DARASA KWA WAGOMBEA NA WAPIGAKURA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI


TAFITI ZA KISAYANSI ZIKITUMIKA ZITAPUNGUZA MAGONJWA KWA ASILIMIA 40

$
0
0
Katibu wa Tanzania Health Summit, Rebecca John akizungumza juu ya usajili wa ushiriki wa mkutano wa sekta ya afya utakaofanyika Novema 14 hadi 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam. wengine ni Rais wa Tanzania Healt Summit, Dk. Omary Chillo pamoja na Mwakilishi wa APHFTA, Joseph Mhagama.

Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii

TAFITI  za kisayansi zikitumika kwa ufasaha  zitasaidia kupunguza magonjwa kwa binadamu kwa asilimia 40. Tafiti hizo ni pamoja na wananchi kupata taarifa za masuala ya afya pamoja na kufuata ushauri wa wataalam juu ya kujiepusha na magonjwa mbalimbali.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na  Rais wa Tanzania Health Summit, Dk. Omary Chillo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya Mkutano wa  Kitaifa  wa Sekta ya Afya nchini utakaofanyika Novema 14 hadi 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Chillo amesema kuwa mkutano huo utajadili changamoto za sekta za afya  nchini pamoja na kuboresha sekta hiyo ili iweze kuhudumia jamii kwa upatikanaji wa huduma bora za afya. Amesema mkutano huo utatoa mapendekezo yanayoonesha suluhisho la mjadala watakayojadili na litaandikwa kwenye kitabu na kusambazwa kwa taasisi za afya na kufuatilia utekelezaji wake.

Mada zitazokuwemo katika mkutano huo ni maendeleo ya huduma za afya, mijadala ya watoa mada  wazoefu wa sekta ya  Afya, kuwasilisha matokeo ya uchaguzi, majadiliano katika vikundi pamoja na kuwa na maonesho ya huduma za bidhaa kutoka kwa wasambazaji wa huduma za afya na mashirika ya umma binafsi,”amesema.

Aidha a amesema kuwa  wanatarajia kupata wadau wa Afya takribani 500 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wataalamu wa Afya, watunga sera, watafiti wa magonjwa, wachumi, wazambazaji wa vifaa tiba na dawa, wawekezaji katika sekta ya Afya pamoja na wadau wote wa sekta ya Afya.

Amesema watafiti mbalimbali watajadili na kutoa majibu ya tafiti zao kama walizofanya kwa panya kugundua magonjwa ambapo tafiti hizo zikitumika vizuri mtu anauwezo wa  kujikinga na magonjwa kwa asilimia 40.

Nae  Katibu wa Taasisi hiyo, Dk Rebecca John ametoa wito kwa wadau wa afya kutoka Serikalini, mashirika binafsi, hospitali, Asasi zisizo za kiserikali,taasisi za kitaalamu, watengenezaji wa bidhaa za afya, wazambazaji, wawekezaji na washiriki wa maendeleo kushiriki katika mkutano huu.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘Ni jinsi gani tunaweza kufikia malengo ya kuimarisha upatikanaji wa afya bora kwa kuunganisha tafiti za kisayansi, ubunifu na sera za afya huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mganga Mkuu wa Seriakali, Profesa Hashim Kambi.

MASHINDANO KOMBE LA AZAM ASFC YAANZA KURINDIMA KWA MICHEZO YA AWALI

$
0
0
Wakati Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam Sports Federation Cup (ASFC), ikianza leo  Novemba 02, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), tayari limezilipa timu zote sita zinazoanza kuchuana hatua ya awali.


Mchezo kati ya Kisarawe United ya Pwani na Silabu ya Mtwara umeahirishwa hadi hapo baadaye utakapotangazwa tena kwa sababu ya majeruhi ya wachezaji. Baadhi ya wachezaji wa Silabu – mabingwa wa Mkoa wa Mtwara wameumia kutokana na ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Mchinga mkoani Lindi wakiwa safarini kwenda Pwani.



Mechi zinazochezwa  ni kati ya Buseresere ya Geita itayocheza na Isako ya Songwe; ilihali Usamala ya Simiyu itacheza na Sahale All Stars ya Tanga katika mechi hizo za awali kuwania taji la ASFC.



Baada ya mechi hizo, itakuja Raundi ya Kwanza ya ASFC ambayo itachezwa kati ya Novemba 7, 8 au 9 ambako TFF imepanga kesho Novemba 2, mwaka huu kutuma fedha zote za maandalizi ya timu husika ili kusiwe na kisingizio chochote cha kujiandaa.



Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred ameagiza Idara ya Fedha na Utawala ya TFF kulipa fedha hizo haraka, lakini kwa masharti ya taratibu za malipo kwamba lazima yapitie benki, badala ya akaunti ya mwakilishi ye yote au kiongozi.



Kidao ameagiza kwamba kwa timu ambayo haijafungua akaunti watakuta fedha hizo kwenye Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa (FA), lakini TFF ingependa kusisitiza kwa wadau hao kufufua akaunti au kufungua akaunti haraka.



Katika raundi hiyo ya kwanza Mashujaa ya Kigoma itacheza na Mshindi kati ya Buseresere ya Geita na Isako ya Songwe; wakati mechi nyingine zitakuwa Msange ya Tabora itacheza na Milambo pia ya Tabora ilihali Bulyanhulu ya Shinyanga itacheza na Area C ya Dodoma.



Kwa mujibu wa droo, Mji Mkuu FC ya Dodoma imeangukia kwa Nyundo ya Kigoma wakati Baruti FC ya Mara itacheza na Ambassodor ya Kahama, Shinyanga huku Eleven Stars ya Kagera ikipangwa kucheza na Ndovu ya Mwanza.



Changanyikeni ya Dar es Salaam itacheza na Reha FC pia ya Dar es Salaam wakati Mshindi kati ya Kisarawe United na Silabu ya Mtwara atacheza na Kariakoo ya Lindi huku Cosmopolitan ikicheza na Ajabalo wakati Makumba FC itapambana na Green Warriors ya Kinondoni wakati Namungo FC ya Lindi itachuana na Villa Squad ya Dar es Salaam huku Dar City ikicheza na Majimaji Rangers ua Nachingwea.



Michezo mingine ya hatua ya kwanza itakutanisha timu za Shupavu FC ya Morogoro na Sabasaba pia ya mjini humo wakati Motochini FC ya Katavi dhidi ya Ihefu FC ya Mbeya wakati The Mighty Elephant ya itacheza na Makanyagio ya Rukwa.



Timu ya Burkina FC ya Morogoro itacheza na Mbinga United ya Ruvuma wakati Makambako Heroes ya Njombe itacheza na Mkamba Rangers ya Morogoro wakati Real Moja Moja itapambana na African Wonderers – zote za Iringa. Boma FC ya Mbeya itacheza na African Sports ya Tanga.



Mechi nyingine za hatua hiyo itakuwa ni kati ya Pepsi ya Arusha ambayo itacheza na Kilimanjaro Heroes ya Kilimanjaro; huku Stand Misuna ya Singida itacheza na Madini FC ya Arusha ilihali AFC ya Arusha itacheza na Nyanza ya Manyara wakati New Generation itacheza na Mshindi kati ya Usamala FC na Sahale ya Tanga. Bodaboda FC itacheza na Kitayose ya Kilimanjaro.



Michuano hiyo ambayo Bingwa Mtetezi ni Simba SC ya Dar es Salaam, inashirikisha timu 91 msimu huu kwa mchanganuo wa timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL); 24 za Ligi Daraja la Pili (SDL) na 27 za Ligi ya Mabingwa wa Mkoa (RCL).

Balozi Mbarouk akabidhi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran

$
0
0
Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mbarouk Nassor Mbarouk, mwenye Makazi yake Umoja wa nchi wa Falme za Kiarabu (U.A.E) akikabidhi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Hassan Rouhani. katika hafla ya Makabidhiano hayo iliyofanyika katika Ikulu ya Rais, Mjini Tehran tarehe 28 Oktoba, 2017.
Rais Hassan Rouhani akisoma hati za utambulisho alizokabidhiwa na Balozi Mbarouk, ambapo alitumia fursa hiyo kumkaribisha Mhe. Mbarouk na kuahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.
Rais Hassan Rouhani akizungumza na Balozi Mbarouk baada ya kukabidhi hati. Katika mazungumzo yao wameahidi kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano kwa lengo la kukuza uchumi wa mataifa yao. 

AMREF YAZINDUA MRADI WA HAMASA KATIKA UZAZI WA MPANGO KWA MIKOA 24

$
0
0
 Mfamasia wa kitengo cha afya ya uzazi na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Wanawake, Jinsia na Watoto, Machumu Mayeye akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa Hamasa na Tiba kwa Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango, uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi mkazi wa Amref Health Africa, Dk. Florence Temu akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mradi wa Hamasa na tiba kwa ajili ya Uzazi wa Mpango kwa mikoa 24 nchi nzima ili kuweza kusaidia sekta ya Afya kwa msaada wa Serikali ya Uholanzi.
 Mfamasia wa kitengo cha afya ya uzazi na Mtoto kutoka kutoka Wizara ya Afya Wanawake jinsia na Watoto, Machumu Mayeye akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa masuala ya afya ya uzazi na mtoto.
 Meneja mradi wa Masuala wa hamasa na Tiba kwa afya ya Uzazi na Mtoto kutoka Amref Africa, Dk. Sarafina Mkuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wadau walioshiriki katika Uzinduzi wa mradi  wa Hamasa na tiba kwa ajili ya Uzazi wa Mpango kutoka kwa Amref Afrika kwa msaada wa Serikali ya Uholanzi.
Baadhi ya Wadau walioshiriki wakati wa Uzinduzi wa mradi  wa Hamasa na tiba kwa ajili ya Uzazi wa Mpango kutoka kwa Amref Afrika kwa  msaada wa Serikali ya Uholanzi.wakiwa katika picha ya pamoja.

Ubalozi wa Norway nchini Tanzania wachangia Milioni 300 Sauti za Busara 2018

$
0
0
Balozi wa Norway nchini Tanzania kupitia kwa Balozi wake Balozi Bi. Hanne-Marie Kaarstad leo wameweza kutiliana saini mkataba wa udhamini wa donge nono la kiasi cha Dola 128200(USD) ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania Milioni 300, ambazo zitaenda kusaidia Shirika lisilo la Kiserikali la Busara Promotion kwa ajili ya tamasha la Sauti za Busara 2018. Halfa hiyo ya kutiliana saini imefanyika mapema leo Novemba 2,2017 katika Ubalozi wa Taifa hilo la Norway, Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari. 

Awali Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud alishukuru Ubalozi wa Norway nchini Tanzania kwa kutoa udhamini huo ambao utasaidia uhai wa tamasha hilo ambalo limejizolea sifa kwa muda mrefu. “Sauti za Busara imepata msaada, shukrani kwa ubalozi wa Norway nchini Tanzania. Norway inaonyesha mfano mzuri wa kuigwa Duniani kwa kuchangia katika maendeleio ya kudumu na mazingira rafiki. Kama ilivyo katika malengo yake nchini Tanzania. 
Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad akizungumza katika tukio hilo mara baada ya kutiliana saini. Anayemfuatia ni Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na kulia ni Ofisa wa Busara Promotions.

Ubalozi wa Norway tangu mwaka 2009 unatoa mchango mkubwa wa kifedha kwa shirika la Busara Promotions, ili kuliwezesha kutimiza mpango mkakati wake hii ni pamoja na kusaidia shughuli za kiutendaaji wa tamasha kwa kila mwaka na tunafurahia kwani tunaamini utaendelea pia kwa mwakani” alieleza Mkurugenzi huyo Yusuf Mahmoud. Pia akifafanua umuhimu wa tamasha la Sauti za Busara, Mkurugenzi huyo Yusuf Mahmoud alibainisha kuwa, tamasha hilo limekuwa likiunganisha watu wa rika na asili tofauti huku pia likiheshimu uhuru wa kujieleza sambamba na kuleta umoja, Amani na kuimalisha jamii. 

“Tamasha la Sauti za Busara linatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sekta ya muziki kukutana na kujifunza. Linaimarisha utaalamu katika sekta ya Sanaa nchini hivyo yote haya lengo kuu la tamasha ili ni kuhakikisha kutangaza amani, mshikamano na kuheshimu tamaduni tofauti” alimalizia Yusuf Mahmoud. 

Kwa upand wake, Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad ameahidi kuendeleza ushirikiano na Busara Promotions katika kusaidia Sanaa na Utamaduni ambapo lengo kuu ni kukuza mashirikiano na maingiliano ya kitamaduni kupitia sanaa hasa muziki katika jamii kwa njia ya tamasha hilo la kila mwaka la Sauti za Busara. “Najisikia furaha sana katika siku ya leo katiliana saini udhamini huu mnono. 

Tumekuwa na Busara Promotion kwa muda mrefu kuanzia 2008 mpaka sasa tukiendelea kukuwa zaidi na kuleta mageuzi kwa jamii hasa kuleta mageuzi makunwa sana kwa jamii ya Wazanzibar, Tanzania Bara na Ukanda wa Afrika kwa ujumla. Tunaamini Sauti za Busara wamejijengea mizizi imara Visiwani Zanzibar na Tanzania Bara kwa ujumla kupitia tamasha lao ambalo linainua na kulinda utamaduni wa Mzanzibar huku pia likilinda hutu na utamaduni wake ndani ya visiwa hivyo vya Zanzibar.” Alieleza Balozi Bi. Anne-Marie Kaarstad. 


Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakitiliana saini udhamini huo mapema leo Novemba 2, 2017. Wengine wanaoshuhudia ni maafisa kutoka Ubalozi wa Norway na Busara Promotions.

Balozi huyo aliongeza kuwa, tamasha hilo pia limekuwa na nguvu kubwa ikiwemo kukusanya watu wengi zaidi kutoka pande mbalimbali za Dunia na kukutana mahala pamoja kufurahia. Aidha, Mkurugenzi wa Busara Promotions, Yusuf Mahmoud amebainisha kuwa, msimu wa Sauti za Busara kwa 2018, tayari wametangaza listi ya wasanii na vikundi ambapo jumla ya vikundi 20 kutoka Tanzania Bara, pia vipo kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, DRC, Nigeria, Morocco, Algeria, Kenya, Rwanda, Burundi, Malawi, Misri Sudan, Gambia. 

Pia vipo vikundi kutoka nchi za Reunion, Norway, Denmark na Switzerland. Katika vikundi hivyo vinatarajia kuwa na Wasanii 400, ambapo wataonyesha uwezo wao kwenye majukwaa matatu tofauti, shoo 46 zote zikiwa asilimia 100 ‘live’ kwa siku nne mfululizo. Pia kutakuwa na mambo mbalimbali ikiwemo warsha na semina kwa wanamuziki wa ndani na nje ambao watapata kubadirishana ujuzi na mbinu za kukuza sanaa na masoko ya muziki wao. 
Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakibadilishana hati walizotiliana saini udhamini huo mapema leo Novemba 2, 2017. (PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE).

CECAFA SASA YARUDISHA MICHUANO YA CHALENJI, KUANZA NOVEMBA 25-9DEC

$
0
0
Baada ya kupita miaka miwili bila kuchezwa kwa mashindano ya kuwania Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki, michuano hiyo imerejea tena msimu huu na Tanzania imethibitisha kushiriki.

Nchi wanachama Tanzania Bara, Zanzibar, Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Eritrea na Ethiopia.

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amethibitisha kikosi cha kwanza cha ‘Taifa Stars’ kushiriki na matarajio ya kufanya vema michuano hiyo itakayofanyika kuanzia Novemba 25, 2017 hadi Desemba 9, mwaka huu.

Kidao amesema kwamba uteuzi wa timu za kwanza kwa kila nchi mwanachama wa Baraza la Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki ni makubaliano ya viongozi wa CECAFA waliokutana kwa pamoja huko Sudan, Septemba, mwaka huu.

Kutokana na makubaliano hayo ya kuita timu za kwanza, michuano hiyo itaathiri kidogot ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwa kuwa wachezaji wengi wanaounda kikosi hicho, wanatoka timu za VPL.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura amesema: “Tutakaa kama kamati na kuangalia siku ya Jumatano na Alhamisi baada ya michuano hiyo na kupanga ratiba ya mechi ambazo zitapanguliwa wakati wa michuano ya Chalenji.”

Mbali ya michuano hiyo, Tanzania imethibitisha kushiriki michuano ya Chalenji ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 itakayofanyika Bujumbura nchini Burundi kuanzia Desemba 12, 2017 hadi Desemba 22, mwaka huu.

Kadhalika, Tanzania imethibitisha kushiriki michuano ya Chalenji kwa wanawake ikienda kutetea taji katika michuano itakayofanyika Rwanda mwezi Desemba, mwaka huu. Tarehe rasmi itatajwa baadaye.

CECAFA imeamua kurejesha hadhi yake kwani mara baada ya michuano ya Chalenji ya vijana huko Burundi, mwakani itakuwa ni zamu ya Tanzania ambako michuano hiyo inatarajiwa kuanza Agosti 11, 2018 hadi Agosti 25, mwakani.

Wakati huo huo Kidao amethibitisha Tanzania kuwa wenyeji wa mashindano ya Vijana ya Chalenji ya CECAFA/CAF kwa vijana chini ya miaka 17 mwakani na mashindano hayo yatatumika kama sehemu ya kufanya maandalizi Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (AFCON – U17).

Michuano ya mwakani ina baraka za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa sababu shirikisho hilo linataka kutumia michuano hiyo ya vijana ya Kanda mbalimbali za Afrika kupata timu saba katika michuano AFCON – U17 ya mwaka 2019.

Kanda hizo ni CECAFA (Afrika Mashariki), COSAFA (Nchi za Kusini mwa Afrika), WAFU – UFOA (Afrika Magharibi); UNAF (Afrika Kaskazini) na UNIFFAC (Afrika ya Kati).

SPIKA NDUGAI AFUNGUA SEMINA YA WANACHAMA WA CHAMA CHA MTANDAO WA WABUNGE WANAOPAMBANA NA RUSHWA.

$
0
0

Mgeni rasmi, Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akifungua semina kuhusu maadili na mapambano dhidi ya rushwa kwa Wanachama wa Chama cha Mtandao wa Wabunge wanaopambana na Rushwa Tanzania (APNAC) iliyofanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akifuatilia semina kuhusu maadili na mapambano dhidi ya rushwa kwa Wanachama wa Chama cha Mtandao wa Wabunge wanaopambana na Rushwa Tanzania (APNAC) iliyofanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma. wa pili kulia ni katibu wa Bunge, Mheshimiwa Stephen kagaigai, wa pili kushoto ni katibu wa Chama hicho, Mheshimiwa Daniel Mtuka na kushoto ni kaimu Mwenyekiti wa Chama hicho, Mheshimiwa Cecilia Pareso.

Wanachama wa Chama cha Mtandao wa Wabunge wanaopambana na Rushwa Tanzania (APNAC) wakifuatilia semina kuhusu maadili na Mapambano dhidi ya rushwa iliyofanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge Mheshimiwa, Job Ndugai (kulia) akipokelewa na Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Mtandao wa Wabunge wanaopambana na Rushwa Tanzania (APNAC), Mheshimiwa Cecilia Pareso (kushoto) kwenda kufungua semina kuhusu maadili na Mapambano dhidi ya rushwa iliyofanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

CCM MKOA WA RUVUMA YATAMBA KUCHUKUA KATA ZOTE KATIKA UCHAGUZI

$
0
0
Chama cha mapinduzi ccm mkoa wa rRuvuma kimepanga kushinda kata zote zinazoshiriki uchaguzi mwaka huu kwa zile zilizokumbwa na matatizo kama vifo na nk hayo yamebainishwa na katibu wa ccm mkoa wa ruvuma B.Amina imbo wakati akimweleza mkuu wa mkoa wa ruvuma b mndeme alipotembelea ofisini kwake.

HAYA NDIYO MAJIBU YA NEC KUHUSU SAKATA LA NYALANDU

YANGA YAWAFUATA SINGIDA, NI VITA YA LWANDAMINA NA PLUIJM

$
0
0
KIKOSI cha Yanga kimeondoka leo kuelekea Singida kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Singida United Jumamosi Uwanja wa Namfua.

Yanga imeondoka bila kuwa na Lwachezaji wake wanne tegemeo ambao ni beki Juma Abdul, kiungo Thabani Kamusoko, washambuliaji Mzimbabwe mwenzake, Donald Ngoma na Mrundi, Amissi Tambwe.Kikosi hicho kinachonolewa na Mzambia George Lwandamina kitavaana na Singida wanaonolewa na aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo Hans Van De Pluijm.

Yanga inakwenda kwenye mchezo huo, ikitoka kutoa sare na wapinzani wa jadi, Simba kwa kufungana 1-1 Jumamosi iliyopita Uwanja wa Uhuru.Sare hiyo imefanya timu hizo ziendelee kufungana kwa pointi 16 kileleni mwa Ligi Kuu, 16 kila moja sawa na Azam FC na Mtibwa Sugar. 

Mbali na Juma Abdul anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Ngoma, Tambwe na Kamosoku wao wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi.Ligi Kuu itaendelea Ijumaa, Maji Maji FC wakiikaribisha Stand United Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, wakati Jumamosi Singida watakuwa wenyeji wa Yanga Uwanja wa Namfua, Singida na Ndanda FC wataikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara. 

Mechi nyingine za Jumamosi, Kagera Sugar wataikaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Njombe Mji FC wataikaribisha Mbao FC Uwanja wa Saba Saba na Azam FC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. 

Jumapili kutakuwa na mechi mbili, mbali na Mbeya City kuwa wenyeji wa Simba, Lipuli FC nao wataikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Samora mjini Iringa.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI

RC DODOMA - NAKUKABIDHI MKOA WA RUVUMA UKIWA SALAMA

$
0
0
Aliekuwa mkuu wa mkoa wa RUVUMA ambaye ameamishiwa kanda ya kati DODOMA DKT BILINITH MAHENGE amekabidhi ofisi yake rasmi kwa mkuu wa mkoa wa RUVUMA BI.CHRISTINE MNDEME ili aweze kuwatumikia wananchi wa mkoa wa RUVUMA huku akimtaka kushirikaina vyema na wafanya kazi wa ngazi wote ili mkujenga nchi ya viwanda
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images