Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

HITILAFU YA MFUMO WA KUPOKELEA GESI KINYEREZI I, TATHIMINI YAONYESHA MATENGENEZO MAKUBWA YANAHITAJIKA, MAFUNDI WAKO KAZINI: TANESCO

0
0
Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, TANESCO


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
TATHMINI iliyofanywa na Wahandisi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kufuatia mfumo wa kupokea gesi asili kwenye mitambo ya kufua umeme, Kinyerezi I jijini Dar es Salaam kupata hitilafu, imebaini matengeenzo makubwa yanahitajika kufanyika ili kuhakikisha mfumo unarudi katika ubora wake..
Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, iliyosambazwa kwa vyombo vya habari leo Novemba 1, 2017, imesema kufuatia mfumo huo kupatwa na hitilafu majira ya mchana Oktoba 32, 2017, hatua ya kwanza iliyochukuliwa na wataalamu wa TANESCO ni kuzima mitambo ili kuruhusu kazi ya usafishaji kuondoa gesi hiyo kufanyika.
”Baada ya usafishaji wa Mitambo kukamilika, matengenezo yalianza usiku wa kuamkia leo Novemba 1, 2017, kwa kutumia wataalamu wa ndani wa Shirika pamoja na Mkandarasi wa kampuni ya JACOBSEN ELEKTRO AS.” Taarifa hiyo ya TANESCO ilisema.
Taarifa hiyo iliendelea kusema, “Kutokana na ukubwa wa matengeenzo na uangalifu wa hali ya juu unaotakiwa katika kazi hii hususan suala la usalama wa mitambo pamoja na watumishi wa Shirika waliopo katika eneo la mitambo, hatua za tahadhari zimechukuliwa.” Taarifa hiyo ilisema.
Aidha taarifa imefafanua kuwa kutokana na Mitambo hiyo kuzimwa ili kuruhusu kazi ya marekebusho ya hitilafu hiyo kukamilika kwa wakati, kutakuwa na upungufu wa umeme katika maeeno mbalimbali ya nchi.
“Uongozi wa Shirika unawaomba radhi wateja wake na wananchi kwa ujumla kwa maeneo ambayo bado yanakosa huduma ya umeme katika kipindi hiki cha matengenezo hayo na tutaendelea kuwaarifu wananchi jinsi kazi ya matengenezo inavyoendelea hadi kukamilika kwake.” Taarifa hiyo ilisema

MBUNGE LIVINGSTONE LUSINDE AMVAA LAZARO NYARANDU

NAIBU WAZIRI WA AFYA ATEMBELEA MFUKO WA TAIFA YA BIMA YA AFYA LEO

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Naibu  Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile amewataka Mfuko wa taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) kuhakikisha watanzania wote wanapaya huduma ya bima ili kuweza kupata matibabu kwa urahisi na wakati sahihi.

Hayo yamesemwa leo alipotembelea makao makuu ya mfuko huo na kujionea namna wanavyofaya kazi zao ikiwemo kuhifadhi nyaraka za madai kutoka katika vituo tofauti vya afya.

Dr Ndungulile amesema, NHIF wanatakiwa kujitanua zaidi ikiwemo kujitangaza na amewasifu kwa huduma nzuri wanazozitoa kwa wananchi pamoja na kutoa vifaa tiba kwa wateja wao.

"napenda niwapongeze NHIF kwa hatua kubwa mliyofikia ya kutoa huduma kwa watanzania na nimesikia kutoka kwa mkurugenzi kuwa mpaka sasa mna asilimia 31  ya watanzania wote lakini mikakati yenu ni kufika asilimia 50  kwa mwaka 2020,"amesema Dr Ndungulile.

Ameongezea katika kuhakikisha wateja wanapata huduma nzuri basi yale malalamiko yanayotolewa na baadhi ya vituo vya afya kucheleweshewa malipo yao asingependa ayasikie tena, wanatakiwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa wakati na kuwalipa kile wanachostahili.

 Naye  Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga amesema kuwa wao kama mfuko wa bima kwa sasa wanatoa huduma katika vituo vingi vya afya na pia wameweza kupata idadi kubwa ya wateja wapya.

Konga amesema kuwa, kwa sasa NHIF wanatoa huduma za matibabu ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kutoa vifaa tiba, kusafishwa kwa figo, upasuaji na mengineyo.
Naibu  Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile akipata maelezo ya namna Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanavyohifadhi nyaraka zao katika makabati maalumu na yanaweza kudumu kwa zaidi ya miaka saba, Kulia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga 
 Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga akimuelezea Naibu  Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile mikakati yao ilikoanzia na mpaka walipo sasa kwenye utoaji wa huduma za kiafya, pia katika kuendeleza kutoa huduma bora kwa wateja wao ikiwemo kuongezeka kwa wateja wa huduma ya bima kufikia aailimia 50 ya watanzania kwa mwaka 2020.

 Naibu  Waziri wa Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile akielezewa jinsi wanavyoweza kushughulikia simu zote za wateja wanazopiga kwa ajili ya kupata huduma, na wanapata takribani simu 200 kwa siku  kutoka kwa wateja tofauti kushoto ni  Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MPANGO WA UENDESHAJI WA KIJINSIA KWA AJILI YA MWITIKIO WA UKIMWI TANZANIA BARA WATAMBULISHWA RASMI KWA MKOA WA SINGIDA

0
0
Serikali kupitia Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imeandaa Mpango wa uendeshaji wa Kijinsia kwa ajili ya mwitikio wa Masuala ya Ukimwi ambao umetambulishwa rasmi kwa timu ya Kuthibiti Ukimwi Mkoani Singida.

Mratibu wa Jinsia Kutoka TACAIDS Jacob Kayombo ameongoza mafunzo hayo kwa timu ya kuthibiti Ukimwi Mkoa wa Singida ambapo amewaeleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuratibu na kutoa dira katika utekelezaji wa program mbalimbali za Ukimwi kwa ngazi ya Mkoa.

Kayombo amesema Mafunzo hayo yamelenga kuutambulisha mpango huo pamoja na fomu zitakazotumika katika ukusanyaji wa taarifa zihusuzo jinsia na Ukimwi.“Mafunzo haya tunayotoa yamejikita katika kuufafanua mpango huu utakavyotumika pamoja na namna ambavyo fomu hizi zitatumika kukusanya taarifa za jinsia na Ukimwi kwa Mkoa wa Singida na jinsi ambavyo taarifa hizo zitasaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu masuala ya Ukimwi”, amesema Kayombo.

Ameongeza kuwa matarajio yanayotegemewa baada ya mafunzo hayo kutolewa ni kuona masuala yote ya kijinsia yanapewa kipaumbele katika program mbalimbali za Ukimwi.Kayombo amesisitiza kuwa mpango huu utakuwa ni mwongozo wa wadau wa masuala ya Ukimwi ili waweze kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia usawa wa kijinsia hasa katika kuweka mikakati ya kuthibiti Ukimwi yenye uelekeo wa Usawa wa kijinsia.
ratibu wa Jinsia kutoka TACAIDS Jacob Kayombo na Afisa Jinsia kutoka TACAIDS Judith Luande wakijadili baadhi ya maoni, maswali na mapendekezo ya wajumbe ambao ni timu ya kudhibiti Ukimwi ya Mkoa wa Singida wakati wa Mafunzo juu ya mpango wa uendeshaji wa kijinsia.
Mjumbe wa mafunzo juu ya mpango wa uendeshaji wa kijinsia Afisa wa Serikali za Mitaa Hussein Mwatawala akipitia fomu zitakazotumika katika kukusanya taarifa za masuala ya Kijinsia mkoani Singida.



DC WILAYA YA NYANG'WALE ASEMA BILA YA KUWEPO USALAMA WA CHAKULA NCHINI HAKUNA KITAKACHOWEZA KUFANYIKA

0
0
Na Dotto Mwaibale, Nyang'wale, Geita

MKUU wa Wilaya ya Nyang'wale Mkoa wa Geita Hamim Buzohera Gwiyama amesema bila ya kuwepo kwa usalama wa chakula nchini bado kutaendelea kuwepo na changamoto nyingi za maendeleo na kuwa pasipo chakula hakuna kitakachoweza kufanyika.

Hayo yalisema na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Fabian Sospeter  kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo, Hamim Gwiyana wilayani humo jana wakati akipokea mbegu bora za mahindi aina ya Wema na mhogo aina ya Mkombozi kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kwa ajili ya kuanzisha mashamba darasa ya mbegu katika vijiji vya Kakora, Nyang'wale, Kanegele na Nyugwa.

"Bila ya kuwepo kwa chakula cha kutosha hakuna kitu kitakachoweza kufanyika kwani shughuli zote zitasimama hivyo ni muhimu kuhimizana katika kilimo chenye tija kama tunavyo himizwa na wataalamu wetu kutoka COSTECH, Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ukiriguru Mwanza na Maruku mkoani Kagera" alisema Gwiyama.

Alisema usalama wa kujilinda na adui hauna shida kwani mtu anaweza kuandaa jeshi lake la kukabiliana na adui huku akiwa na silaha nzito lakini sio usalama wa chakula ambao unahitaji maandalizi ya kutosha na watu kujituma na kufanya kazi kwa bidii hasa za kilimo chenye tija.
 Mtaalamu wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula, akiwaelekeza wananchi wa Kata ya Nyugwa jinsi ya upandaji wa mbegu ya mhogo aina ya Mkombozi kwenye shamba darasa.
 Mkulima Pendo Sangoma akishiriki kupanda mbegu ya Wema katika shamba darasa katika Kijiji cha Kakora wilaya humo. Kushoto ni Ofisa Ugani, David Makabila kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.
 Ofisa Ugani wa Kijiji cha Nyang'wale, akitoa maelekezo kwa watafiti wa kilimo kuhusu masuala ya kilimo.

Mshauri wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia katika Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange, akizungumza na viongozi wa Kijiji cha Kanegele, maofisa ugani na watafiti kabla ya kupanda mbegu ya mhogo katika shamba darasa kwenye kijiji hicho. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji hicho, Makoye Malikwisha.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


JE WAJUA KUTELEKEZA ARDHI NI PAMOJA NA HAYA.

0
0
Na  Bashir  Yakub. 

Kuna  mambo ambayo  yafaa  tujihadhari  nayo  sana  hasa  kipindi  hiki. Wengi wamefutiwa  umiliki wa  ardhi. Takwimu  za kufutiwa ni kubwa sana kipindi hiki kama ulikuwa hujui. Kwa  watu  wanaonunua  ardhi  na  kwenda  kuishi  nje  ya  nchi  hili  lawahusu  sana kabla hamjapoteza ardhi zenu.  

Najua  unachojua kuhusu  kutelekeza ardhi  ni pengine  kutokujenga,  au  kutoitumia  kama ilivyopangiwa matumizi, nk. Ni kweli lakini  hiyo ni maana  finyu  ya kutelekeza ardhi. Maana  ni  zaidi ya hiyo,  na  hapa tutaona  ili  ujihadhari na  uwezekano wa  kupoteza  ardhi  yako.

1.MAMBO  AMBAYO  UKIFANYA  UTAHESABIKA  KUTELEKEZA  ARDHI.

Mambo  haya  yameelezwa   na  Sheria  Namba  4  ya  ardhi  ya  1999 kifungu  cha  51(1).

( a ) Kutokulipa  kodi, tozo  au  ushuru  wowote  ambao  upo  kisheria  kwa  ajili  ya  ardhi  ni  kutelekeza  ardhi  kwa  mujibu  wa  sheria hiyo.  Mnazijua  kodi  za  majengo,  kodi  za  ardhi  nk.  Hizi  ni  muhimu  sana  na  kimsingi  ndizo  zinazoeleza  uhai  wa  ardhi  yako.

Ikiwa hulipi  hizi  hata  kama  eneo  hilo  umejenga  kiwanda  kinachofanya  kazi  saa  24  siku  7  za  wiki  bado  mbele  ya  macho  ya  sheria  unahesabika  kutelekeza  ardhi.  Dawa  ya  kuepuka  hili  ni  ndogo.  Lipa  hizo  kodi  na  tozo  kwa  mujibu  wa  sheria. Yamkini  hizi  huwa si  pesa  nyingi  sana ya  kumshinda  mmiliki  kulipa.

( b ) Jengo  ndani  ya  ardhi  kuwa  gofu  ni  kutelekeza  ardhi  kwa  mujibu  wa  sheria.  Lakini  pia   katika eneo  hilo  sheria  imetumia  neno “disrepair”.  Maana   yake  kutokufanya  ukarabati.  Kwa  tafsiri  hii  ni  kuwa  kumbe  hata  kutokufanyia  majengo  yetu ukarabati  nako ni  kutelekeza  ardhi. 

Utaona  katikati  ya  miji  yetu  majengo ya  zamani machafu,  yaliyopauka. Japo  ndani  mwake  watu  wanaishi  na  maofisi  yamo  bado kwa tafsiri  ya  neno  “disrepair”  ni  kuwa  jengo  hilo  limetelekezwa.  Na  sheria  imeeleza  zaidi  kuwa itakuwa  mbaya  zaidi  ikiwa  jengo  hilo  linahatarisha  afya  au maisha  ya  watumiaji  wake , majirani  au  hata  wapita  njia. 




                   KUSOMA  ZAIDI   

RC MNDEME AWATAKA VIONGOZI WA MKOA NA WILAYA KUSHIRIKIANA KULETA MAENDELEO KWA WANANCHI.

0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma B.Christina Mndeme amewataka viongozi wa mkoa wa Ruvuma na wilaya kuhakikisha wanashirikana katika kuuletea maendeleo mkoa,uki kiwataka kumpa ushirikiano zaidi

MAGAZEETI YA ALHAMIS LEO NOVEMBA 2,2017

SERIKALI YATAIFISHA NG’OMBE 6648 MISENYI KAGERA

0
0

NA MWANDISHI MAALUM MISENYI

Akiwa katika muendelezo wa ziara zake za oparation kamata mifugo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina Ameagiza kukamilisha taratibu za Uhamiaji na Mahakama kupitia mwanasheria mkuu wa Serikali wa Wilaya ya Misenyi Pamoja na Uhamiaji, ili kuweza kupigwa mnada kwa idadi ya ng’ombe 6648 walioingia nchini kinyemela toka nchi jirani ya Uganda na kukamatwa.

Waziri mpina alisema uvamizi wa kundi kubwa kama hilo la wanyama linaweza kusabisha madhara makubwa katika mazingira kama vile mmomonyoko wa ardhi, kuharibifu wa vyanzo vya maji, kumaliza malisho ya mifugo iliyoko nchini, kusababisha migogogoro ya mara kwa mara kwa wakulima na wafugaji na hata kuleta maambukizi ya magonjwa ya wanyama. 

“Sisi kama Serikali hatuwezi kuruhusu hali hii iendelee na mimi kama Waziri Mwenye dhamana nina jukumu la kuhakikisha tunalinda lasimali hii ya malisho” Alisema Mpina.

Mpina alisema suala hili haliingiliani na Ushirika wa Afrika Mashariki kwani Ushirika huo upo kisheria hivyo wavamizi wanaoingiza mifugo kinyemela nchini toka nchi jirani ni wahalifu kama wahalifu wengine. “Kwa hiyo naangiza ng’ombe hawa 6648 waliokamatwa hatua ziendelee na ambao hawajakamatwa wakamatwe na wataifishwe na Serikali.”Alisisitiza Waziri Mpina.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiiongea na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Misenyi mara baada ya zoezi la kutaifisha ng'ombe.
Katika Picha ni sehemu ya ng'ombe 6638 waliotaifishwa na serikali baada ya kuingia nchini kinyemela kutoka nchi jirani ya uganda ng'ombe hao wanasubiri maamuzi ya Mhakama kwa ajili ya Kupigwa mnada.
 
Aliyeshika Samakai aina ya Sato ni Waziri Mpina alipotembelea Mradi wa Mabwawa ya Samaki wa Luhanga Wilayani Muleba.
Waziri Mpina katika Picha akivua samaki aina ya kambale alipotembelea Mradi wa mabwawa ya samaki wa Luhanga Wilayani Muleba.


MAJABA ALIVYOPOKELEWA KWENYE NYUMBA YAKE BUNJU B JIJINI DAR

0
0
Msafara wa magari ukiongozwa na pikipiki zaidi ya tano ulitokea makao makuu ya Global Group Sinza Mori Dar, huku Mshindi wa Shindano la Nyumba Awamu ya Pili, George Majaba akiwa kwenye gari la wazi aina ya BMW huku mke wake akiwa kwenye gari lingine na watoto wao . 

Msafara ulipita Barabara ya Shekilango, ukaingia Barabara ya Ali Hassani Mwinyi kisha ukaingia New Bagamoyo, njiani kwa kuwa kulikuwa na gari la matangazo, watu walikuwa wamejipanga kumshuhudi Majaba aliyejawa na tabasamu akipita akiwa kwenye gari hilo la wazi. 

 Msafara ulipofika Tegeta umati ulikuwa mkubwa na wengi waliokuwa wakimuona Majaba walikuwa hawaamini macho yao kwani yeye mshindi alikuwa akiwapungua mkono na msafara ukawa unaenda kwa mwendo wa polepole, hali iliyofanya baadhi ya wananchi kumkaribia mshindi na walisikika wakisema ‘Hongera, Hongera!” Lakini abiria waliokuwa kwenye mabasi ya daladala nao walionekana wakitoa vichwa vyao madirishani na kumpongeza Majaba ambaye mara zote alikuwa na tabasamu usoni. 
 Nyumba iliyopo Bunju B ilivyokuwa kabla ya makabidhiano jana. Mkurugenzi wa Mkuu wa Global Group, Eric Shigongo (wa kwanza kulia) na George Majaba (wa pili kulia) pamoja na Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho wakijadiliana jambo. ... Shigongo akizungumza machache mbela ya nyumba hiyo kabla ya kumkabidhi George Majaba jana.

WADAIWA SUGU WA MAJI WILAYA YA KIBONDO KUUNDIWA KIKOZI KAZI

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MKUU wa Wilaya ya Kibondo Luis Bura ameahidi kuunda kikosi kazi, kitakacho pita na kukusanya kiasi cha shilingi milioni 50 kwa Wadaiwa sugu wa Mamlaka ya maji safi Wilayani kibondo na kuhakikisha zinalipwa na kukabidhiwa kwa bodi mpya ya maji pamoja na kusitishia huduma ya maji kwa wale wote watakao shindwa kulipia madeni yao ya Nyuma.

Aidha Bura aliwaagiza wale wote wanao lima karibu na vyanzo vya maji kuacha kulima na kuondoa mazao yao kabla ya kuanza kutolewa kwa nguvu na kuharibiwa,vyanzo hivyo kujaa michanga wakati wa masika kutokana na baadhi ya wananchi kukosa uwelewa na kulima kwenye vyanzo na kupelekea upungufu wa maji katika wilaya hiyo.

Akizungumza jana Wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya maji Wilayani humo Mkuu huyo alisema, Serikali hadi sasa imeingia gharama ya kulipia deni la umeme ili kuhakikisha Wananchi wanaendelea kupata maji , wakati kuna baadhi ya Taasisi zikiwemo za Serikali na Wananchi wanadaiwa kiasi cha zaidi ya milioni 50.

Alisema Mamlaka hiyo imekuwa ikijiendesha kwa hasara hali iliyo walazimu kuanzisha mfumo mpya wa usambazaji wa maji kwa kutumia Sola ilikupunguza gharama za matumizi ya umeme ambayo hayaendani na Makusanyo ya mamlaka ya maji na kuagiza fedha hizo zitakazo kusanywa kuanzia kesho zipelekwe kwenye marekebisho ya sola na wananchi waweze kuepukana na kero ya ukosekanaji wa maji.

"Nimepitia orodha ya wadaiwa Mimi pia ni miongoni mwa wadaiwa nimekuta na mimi kuda deni kubwa halijalipwa, taasisi zote na Wananchi muhakikishe mnalipa deni hilo wananchi wamekuwa wakikosa maji kwakuwa uwezo wa mamlaka kulipia bili ya umeme haiwezi kutokana na madeni hayo kila mtu ataubeba msalaba wake nitahakikisha fedha hizo zinakusanywa ukishindwa kulipa utasitishiwa huduma", alisema Mkuu huyo.
 MKUU wa Wilaya ya Kibondo Luis Bura alipokuwa akizungumza wakati wa kuzindua bodi mpya ya maji wilayani humo mkoani Kigoma
 Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakiwemo na watumishi wa bodi hiyo mpya ya maji wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

ASKARI MAGEREZA KUTUKA WILAYA YA TEMEKE ASHINDA DAU KUBWA LA MILIONI 11O ZA TATU MZUKA

0
0

Afisa Magereza Bwana Neuro Mbwilo amejishindia dau kubwa kuwahi kutolewa na Tatu Mzuka la shilingi milioni 110 kupitia Mzuka jackpot iliyoonyeshwa kupitia vituo mbalimbali vya runinga nchi nzima siku ya Jumapili ya Tarehe 29 Nov 2017.

Kama ma milioni ya wachezaji wengine nchini Tanzania, Mbwilo alidhani ilikuwa ni fursa nzuri kutumia Shilingi 500 kubadilisha maisha yake pamoja na familia milele.

Bwana Mbwilo, ambaye ni Askari gereza wilayani Temeke alielezea mshtuko wake juu ya bahati iyo iliyomtembelea. "Ni hisia ambayo haielezeki kabisa. Nina furaha kubwa sana, nimejawa na shukrani nyingi,na kwangu hii ni ajabu kabisa ", alielezea mbele ya vyombo vya habari.

Katika kutoa hundi ya ushindi huo wa milioni 110 Bwana Sebastian Maganga, Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka alielezea zaidi juu ya ushindi huo mkubwa lakini aliwakumbusha Watanzania kwamba kuna njia nyingi za kushinda kupitia Tatu Mzuka. Alifafanua kuwa katika wiki 13 tu Tatu Mzuka imetengeneza zaidi ya washindi milioni 2 na kutoa billion 4 kwa washindi.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva ( Kushoto)  akimkabidhi Mfano wa hundi ya sh Milioni 110 Ofisa ya Jeshi la Magereza Neuro Mbwilo, ambaye ni mshindi wa bahati nasibu ya Mzuka jackpot, Dar es Salaam.
 Mshindi wa millioni 110 Bwn. Mbwilo akiwa na washkaji zake wawili Juma Athuman na Joseph Haule Walio zawadia  milioni moja moja na Tatu Mzuka kwenye promotion ya "Cheza na Washkaji na Shinda na Washkaji".
  Bwana Mbwilo akisherekea ushindi wake na Mke wake Nyumbani kwao Keko.

RC MAKONDA AZINDUA UJEZI WA OFISI 402 ZA WALIMU JANA JIJINI DAR

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ,amezindua zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu mkoa hapo na kuongeza kuwa ujenzi wa Ofisi utafanka kwa haraka, chini ya Vijana wenye morali ya kazi kutoka JKT, Magereza na Jeshi la Polisi.

Ramani ya ofisi hizo inaonyesha kuwa na Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu Mkuu Msaidizi, Ofisi ya Walimu wa kawaida, Mhasibu, Karani, Chumba cha kuhifadhi Mitihani, Vyoo vya kisasa, Stoo, Jiko, Chumba cha Mikutano na sehemu kuweka Mafaili ambapo ndani ya ofisi zitafungwa AC, Feni, Samani, Taa za kisasa na Umeme.

Akizungumza Katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na upandaji wa Miti RC Makonda amesema kuwa lengo la ujenzi huo ni kuwezesha Walimu kufanyakazi katika Mazingira mazuri yatakayowapa morali na hamasa ya kufundisha Wanafunzi.

Sanjali na hayo Makonda amewapongeza Walimu wa shule za msingi kwakuwezesha Mkoa wa Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa Darasa la saba ukilinganisha na nafasi ya nne waliyo pata mwaka jana na amewaomba kutoichia nafasi hiyo , pia walimu wa shule za sekondari nao wajitahidi ili waongoze katika matokeo ya mtihani kitafa.

"Rais ,ameshatuonyesha dira kwa kutoa elimu bure na sisi wasaidizi wake ni lazima tuendeleze maono yake, mimi sio kiongozi wa kusubiri kuagizwa ndio nifanye kazi kama ilivyo kwa Remote hadi ibonyezwe ndio ifanye kazi, mimi ni kiongozi wa kujiongeza, sijachaguliwa kuwa mzigo kwa serikali bali kuleta matumaini kwa wananchi"alisema.
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiashiria kuzinduliwa kwa zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu mkoa hapo
Mku wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikabidhiwa riasala iliyosomwa na mkuu wa shule ya msingiMajohe Grace Ndaro wakati wa uzinduzi wa zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu mkoa hapo
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akizungumza na wananchi wa kata ya Majohe wakati wa uzinduzi wa zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu mkoa hapo
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa kazini kuashiria uzinduzi wa ujenzi za ofisi hizo ukiwa tayari umepamba moto.
Wananchi waliojitokeza.

MFAHAMU HADIJA JABIRY, KIJANA ALIYEJIKITA KWENYE KILIMO


SERIKALI YADHAMIRIA KUKABILIANA NA TATIZO LA KUGHUSHI VYETI VYA ELIMU NA TAALUMA KWA WATUMISHI WA UMMA NCHINI

0
0

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jasson S. Rweikiza (Mb) akichangia hoja mara baada ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro kuwasilisha Taarifa ya uhakiki wa watumishi na vyeti vya kufaulu mtihani wa kidato cha nne, cha sita na ualimu kwenye Kamati hiyo.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akisikiliza hoja mbalimbali toka kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, mara baada ya kuwasilisha Taarifa ya uhakiki wa watumishi na vyeti vya kufaulu mtihani wa kidato cha nne, cha sita na ualimu kwenye Kamati hiyo.

WATANZANIA WAISHIO CHINA WATAKIWA KUCHANGIA JUHUDI ZA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA LA TANZANIA

0
0
Na Happiness Shayo- China.

Balozi wa Tanzania  nchini China  Mhe Mbelwa Kairuki amewataka Watanzania wanaosoma katika Taifa hilo  kutumia fursa hiyo kuunga mkono juhudi za Tanzania kuelekea Uchumi wa kati ifikapo  mwaka 2025.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa shirikisho la Jumuiya za Watanzania wanaosoma katika  Taifa la China(TASAFIC) uliofanyika hivi karibuni katika mji wa Wuhan, Jimbo la Hubei.

Balozi Kairuki alisema kuwa yapo maeneo kadhaa ambayo Watanzania hao wanaweza  kutoa michango yao katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwenye ujenzi wa Viwanda  ili sekta hiyo isaidie na kuleta tija katika ukuaji wa Uchumi. 

Akizungumzia kuhusu sekta ya Utalii, Balozi Kairuki  aliitaja China kama soko jipya wanalopatikana watalii na kwamba kwa mwaka 2016 ni Wachina Millioni 120 waliokwenda nje ya nchi kutalii sawa na idadi ya watu wote wa  nchi za Tanzania,Kenya,Uganda,Burundi  na Rwanda,  idadi inayoonekana ni kubwa sana,ambapo kwa mwaka huo huo ni watalii 30,000 walipokelewa Tanzania kutoka China.

“Zipo hatua kadhaa ambazo sasa zimechukuliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini China, hivi sasa tunazungumza  na kampuni kubwa inayomiliki mitandao ya kijamii hapa ya  China ya TENCENT ili tuweze kutumia mtandao wao wa QQ kurusha vivutio vyetu vya utalii hapa China mubashara, lakini pia mwezi huu tulikuwa na Mazungumzo na Serikali ya China kuwajulisha nia ya shirika letu la ndege la Air Tanzania kuanza safari za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Guangzhou. 
 Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akihutubia katika mkutano wa Shirikisho la Jumuiya ya Watanzania wanaosoma katika  Taifa la China(TASAFIC) uliofanyika mjini Wuhan, jimbo la Hubei hivi karibuni. 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Watanzania wanaosoma nchini China (TASAFIC) Bw. Remidius Emmanuel akizungumza katika mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika mjini Wuhan, jimbo la Hubei hivi karibuni.
 Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China (Mwambata wa Elimu) Bw. Lusekelo Gwassa Akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa TASAFIC kwa Mwaka 2017.
 Baadhi ya Watanzania wanaosoma nchini China waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya ya Watanzania wanaosoma katika  Taifa la China(TASAFIC) uliofanyika mjini Wuhan, jimbo la Hubei hivi karibuni. 


Baadhi ya Watanzania waliohudhuria  Mkutano Mkuu wakiwa katika Picha ya pamoja na Balozi Mbelwa Kairuki.


TFDA YAZIDI KUNGARA KATIKA UDHIBITI DAWA NA VIFAA TIBA KATIKA NCHI ZA AFRIKA –WAZIRI UMMY MWALIMU

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekuwa ni Taasisi bora kwa Bara la Afrikakatika kudhibiti dawa na chakula ili watanzania wapate huduma bora.

Ummy ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Maabara Hamishika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa katika kulinda afya za  wananchi ni kupata dawa zinazostahili ambazo zimedhibitiwa na TFDA.Amesema kuwa matumizi ya dawa zisizo sahihi zinarudisha kasi ya uchumi ambayo inatokana na watu kuingia  gharama za kununua dawa hizo mara kwa mara na tatizo kubaki pale pale.

Ummy amesema kuwa licha ya kudhibiti dawa lakini TFDA isiwe kikwazo cha uwekezaji katika sekta ya viwanda ambapo wawekezaji wanatakiwa kufuata taratibu za nchi zilizowekwa.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maabara hamishika hizo, wakwanza kushoto ni mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthius Kamwa, watatu kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya TFDA Bi. Zainabu na wa mwisho ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Hiiti B. Sillo.
Mh. Ummy Mwalimu akipata maelekezo kuhusu Maabara hamishika hiyo wakati wa uzinduzi wa maabara hamishika mapema leo katika ofisi za Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthius Kamwa.
 Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa maabara hamishika mapema katika ofisi za Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DPP aomba siku 14 kukamilisha utaratibu wa kupeleka taarifa za kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya USD 527,540, Mahakama kuu inayowakabili vigogo wa RAHCO

0
0
Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya jinai (DPP) ameomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwapa siku 14 ili kukamilisha utaratibu wa kupeleka taarifa za kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya USD 527,540, Mahakama kuu.

 Kesi hiyo inawakabili vigogo wa Kampuni Hodhi ya Mali za Reli (Rahco), Benhardard Tito aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji,  Mwanasheria wa Rahco, Emmanuel Massawe na mfanyabiashara ambaye pia ni mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma.

Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maghela Ndimbo amewasilisha ombi hilo leo Novemba 2, 2017 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa

Kufuatia maelezo hayo, Hakimu Simba ametoa ahirisho la mwisho na kuwaeleza upande wa mashtaka kuwa ataifuta kesi hiyo kwa kiwango ambacho washtakiwa hao hawatakamatwa tena.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 16, mwaka huu.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka nane ya uhujumu uchumi likiwamo la matumizi mabaya ya madaraka, kula njama na kusababisha hasara ya USD  527,540.

Washtakiwa hao wadaiwa kuwa kati ya Septemba Mosi, 2014 na Septemba 30, 2015 kwa nia ya kutenda kosa walikula njama kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Tito, anadaiwa kuwa  Februari 27, 2015 katika ofisi za Rahaco zilizopo Ilala alitumia madaraka yake vibaya kwa kuiajiri Kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Ltd kama mshauri wa mradi wa uimarishaji reli ya kati bila idhini ya Bodi ya Zabuni ya Rahaco.

Tito na Massawe wanadaiwa kuwa Machi 12, 2015 wakiwa katika nyadhifa zao, walisaini barua ya kuihalalisha kampuni hiyo ya Afrika Kusini kuwa mshauri wa mradi wa uimarishaji reli ya kati na kutoa huduma za ushauri wa kifedha kuhusu mradi huo.

Aidha washtakiwa hao wanadaiwa  kuwasilisha mkataba wa huduma ya ushauri kati ya kampuni hiyo ya Afrika Kusini na Rahaco.

Pia wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya kwa kusaini mkataba wa kutoa huduma za ushauri na kampuni ya Afrika Kusini bila ridhaa ya Bodi ya Zabuni ya Rahaco na kushindwa kuwasilisha mkataba walioingia na kampuni ya Afrika Kusini kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Aidha wanaodaiwa kati ya Machi mosi na Septemba 30, 2015 katika ofisi za Rahaco, waliipa kazi kampuni hiyo ya ushauri na kuilipa kwa kutoa huduma za ushauri, malipo ambayo yaliisababishia Rahaco kupata hasara ya dola za Marekani 527,540.

Tito anadaiwa kuwa, Agosti 18, 2015 katika ofisi za Rahaco Ilala, ambapo kwa kutumia madaraka yake vibaya aliipa Kampuni ya Ujenzi wa Reli ya China kazi ya kujenga kilomita mbili za reli maeneo ya Soga iliyogharimu dola za Marekani 2,312,229.39 bila idhini ya Bodi ya Zabuni ya Rahaco.

HALMASHAURI ZA MKOA WA DODOMA ZAPEANA SOMO, SHUGHULI YAANZIA MANISPAA YA DODOMA

0
0
HALMASHAURI zote nane za Mkoa wa Dodoma zimekubaliana kuwa na utaratibu wa ziara za kubadilishana uzoefu hususan katika uendeshaji wa vikao na mikutano ikiwemo Baraza la Madiwani.

Hayo yalisemwa jana na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe wakati akiwatambulisha baadhi ya Wenyeviti na Wataalam wa Halmashauri za Wilaya za Mkoani humo waliohudhuria mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Dodoma ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa ushirikiano huo.

Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Dodoma, ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mheshimiwa White Zuberi Mwanzalila ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mheshimiwa Danford Chisomi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mheshimiwa Samweli Kaweya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Rachel Chuwa. 

Halmashauri zinazounda Mkoa wa Dodoma ni Manispaa ya Dodoma, Bahi, Chamwino, Kongwa, Mpwapwa, Kondoa Mji, Kondoa Vijijini, na Chemba.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa White Zuberi Mwanzalilaakijitambulisha kwa wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma jana. Picha Zote-Ramadhai Juma-Ofisi Ya Mkurugenzi Manispaa Ya Dodoma
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifuatilia mkutano wa Baraza jana katika ukumbi wa Manispaa.
Baadhi ya Wageni Waalikwa wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Robert Mwinje, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma White Zuberi (wa pili kushoto), na Mwneyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Danford Chisomi (wa pili kulia). Kushoto ni Meya wa Jiji la Mbeya Mstahiki David Mwasilindi.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images