Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1992 | 1993 | (Page 1994) | 1995 | 1996 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Watalaam wa Masuala ya Nishati wakifuatilia taarifa kuhusu masuala ya umeme wakati wa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Asteria Muhozya, Arusha

  Wataalam wa Masuala ya Nishati wanaoshiriki Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaondelea jijini Arusha wameibua masuala kadhaa katika mkutano huo ambayo yanalenga kuharakisha utekelezaji wa miradi ya Nishati iliyokubaliwa na Jumuiya hiyo. Hayo yalibainika katika siku ya Pili ya mkutano wa Timu ya Wataalam kutoka Jumuiya hiyo ulioanza tarehe 30 Oktoba, 2017. Mkutano wa Wataalam umefanyika kabla ya kikao cha Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 2 Oktoba, 2017 na kitafuatiwa na kikao cha Mawaziri wa Nishati kinachotarajiwa kuhitimisha mkutano huo tarehe 3 Oktoba,2017.

  Baadhi ya miradi ya umeme iliyojadiliwa ni pamoja na ile ya ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha Umeme inayounganisha nchi na nchi ambayo imeelezwa kuwa na kasi ndogo katika utekelezaji wake. Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na mradi wa Miundombinu ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 wa Singida- Arusha- Namanga, mradi wa kV 220 wa Rusumo- Nyakanazi na mradi wa kV 400 wa Iringa- Mbeya - Tunduma. Pia, Wataalam hao wamejadili masuala ya kodi kwa vifaa vya umeme jua, miradi ya umeme ya mipakani ikiwemo miradi ya Murongo/Kigagati na Nsogezi pamoja na Sera ya Usalama wa Nishati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Baadhi ya Wataalam kutoka Tanzania wakijadiliana jambo wakati wa mkutano huo.

  Aidha, katika siku mbili za majadiliano, Watalaam kutoka Jumuiya hiyo pia wamejadili masuala kadhaa yakiwemo yanayohusu nishati jadidifu, gesi asilia na mafuta. Kikao cha Makatibu Wakuu, kitakachofanyika tarehe 2 Oktoba, kitatanguliwa na kikao cha Kamati ya Nishati cha Baraza hilo kinachofanyika leo tarehe 1 Oktoba, 2017 ambapo hoja mbalimbali zilizoibuliwa na Wataalam hao zitajadiliwa katika kikao hicho.

  Awali, akifungua mkutano wa Baraza hilo kwa upande wa Wataalam tarehe 30 Oktoba, 2017 Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki upande wa Sekta za Kijamii na Uzalishaji, Christophe Bazivamo alieleza umuhimu wa nchi husika kuongeza kasi ya upatikanaji wa Nishati miongoni mwa nchi wananchama ili kuwezesha mapinduzi ya Viwanda na kusisitiza kuwa, miongoni mwa maeneo ya kipaumbele ya Jumuiya hiyo ni Nishati.
  Wataalam kutoka nchi mbalimbali wakijadiliana kuhusu masuala ya mafuta na gesi asilia wakati wa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Bazivamo aliongeza kuwa, ili nchi hizo ziendeleee kiviwanda zinahitaji nishati kwa kuwa ndiyo kichocheo kikuu cha maendeleo na kwamba, bado idadi kubwa ya wananchi wa jumuiya hiyo haijaunganishwa na nishati ya umeme. Pia, aliongeza kuwa, ukosefu wa nishati hiyo siyo tu unadidimiza maendeleo ya watu pia unaathiri sekta ya elimu kwa kuwa, kukosekana na nishati kunasababisha wanafunzi hususani waishio vijijini kutumia muda mwingi kutafuta nishati ya kuni kwa ajili ya kupikia badala ya kujikita na masomo.

  Nchi zinazoshiriki mkutano huo ni pamoja na Tanzania, Uganda, Rwanda, Uganda na Kenya. Aidha, Tanzania inawakilishwa na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji, Mazingira na Nishati ya Zanzibar, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wakala wa Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta , Zanzibar (ZURA). Mwenyekiti wa Mkutano wa 12 wa Baraza hilo ni nchi ya Uganda na Katibu ni nchi ya Rwanda.
  Baadhi ya Wataalam kutoka nchini Kenya wakijadiliana jambo.

  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ametoa muda wa siku 21 kwa Mkandarasi Nyanza Road Works kuongeza vifaa vya kazi na wafanyakazi ili kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami.

  Mhe. Kwandikwa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma leo, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa ujenzi huo unatakiwa kukamilika haraka ili kuweza kufungua mkoa huo na kurahisha shughuli za usafirishaji.

  “Hakikisheni ndani ya wiki tatu vifaa vya ujenzi vinakuwepo eneo la kazi na ajira zinatolewa kwa wananchi ili mradi ukamilike mapema iwezekanavyo”, amesisitiza Mhe. Kwandikwa.Kuhusu suala la malipo, Mhe. Kwandikwa amefafanua kuwa hivi sasa hakuna tatizo lolote la malipo kwani mkandarasi ameshalipwa na kilichobaki sasa ni mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili ujenzi ukamilike.

  “Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi anazozifanya kwani hivi sasa hali ya fedha ni nzuri, mapato yanaongezeka hivyo tutegemee kupata matunda ya maendeleo ya miundombinu bora hapa nchini”, amesema Naibu Waziri Mhe. Kwandikwa.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), akikagua kalvati katika barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (aliyevaa suti) akikagua matofali katika kambi ya mkandarasi ya Nyanza Road Works alipokuwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.
  Meneja wa mradi kutoka Kampuni ya Nyanza Road Works Massimo Cartura, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inaojengwa kwa kiwango cha lami. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.


  Meneja wa mradi kutoka Kampuni ya Nyanza Road Works Massimo Cartura (kulia), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), aina ya kokoto zinazotumika katika ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.


  0 0

  KADRI siku zinavyokwenda mbele, wadau wanaoguswa na sanaa hapa nchini wanasaka namna ya kusaidia tasnia hiyo ambayo ni eneo adhimu kwa jamii duniani. Mara nyingi wasanii wamekuwa wakilalamika kwamba wanafanywa kama yatima ambao wanakosa msaada wa kuwasogeza katika njia ya maendeleo baada ya kufanya kazi zao kwa ufanisi. Wasanii hulalamika katika matukio mbalimbali ya kazi zao, hali ambayo husababisha kuonekana kwamba tasnia hiyo sio eneo la kukimbilia kwa sababu ya malalamiko kutoka kwa baadhi ya wasanii.

  Wasomi wa Sanaa hapa nchini wanaguswa kwa kiasi kikubwa na sanaa za Tanzania ambao wanatekeleza kwa vitendo kazi hizo, Asasi ya East Africa Art Biennale (EASTAFAB) inaguswa na malalamiko, vilio vinavyotolewa na baadhi ya wasanii katika matukio yanayoandaliwa na baadhi ya wadau  wanaoguswa na mdororo wa maendeleo ya kazi za sanaa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa EASTAFAB, Dr. Kiagho Kilonzo anasema mguso huo umejikita kwenye kupromoti sanaa za Ufundi  ambazo zina idadi kubwa ya wasanii ambao wakiwemo Wachongaji, Wachoraji, Wasusi, Wafinyanzi na wengineo ambao wanaingia kwenye Sanaa za Ufundi.       

  Dr. Kilonzo anasema promosheni hiyo hufanyika kupitia Maonesho ya Sanaa ambayo yalianza tangu mwaka 2003 ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili. Anasema mara zote 7, maonesho hayo ya Afrika Mashariki yamekua yakifanyika jijini Dar es Salaam ambayo pia hushirikisha wasanii wengine kutoka nje ya Afrika Mashariki na kushirikisha wasanii wa Afrika, Ulaya na Amerika lakini mwaka huu limepanua wigo kwa kufanyika katika majiji ya Afrika Mashariki.

  Anasema pamoja na kufanyika katika majiji ya Afrika Mashariki pia kutakuwa na semina ya wasanii na matukio mengi yanayoendana na mwenendo wa hali ya sanaa pamoja na masoko ya sanaa.Dr. Kilonzo anasema katika semina hiyo itakayofanyika Novemba 3, kutakuwa na wawasilishaji mada wa nchi za Tanzania (kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania), Revocatus Kundy, Kenya (kutoka Taasisi ya Elimu Kenya), Dr. Jennifer Wambugu na Uganda (kutoka Kituo cha Maendeleo ya Mitaala), Christopher Muganga.


  Katika semina hiyo mbali ya watoa mada  kuchanganua mipangilio mbalimbali ya sanaa pia wasanii watajadili hoja mbalimbali zitakazowasilishwa mezani na watoa mada. Dr. Kilonzo anasema pamoja nao katika semina hiyo kutakuwa na wahusika wa masoko ya sanaa hapa nchini ambao ni pamoja na Origenes Uiso (Karibu Art Gallery), Abel Shuma (Alliance Francaise), Tim Amstrong kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Franciscar Shirima-Frankoo Design.


  Anasema semina hiyo itafanyika nyumbani kwa Balozi wa Uswiss,  Arthur Mattli Masaki mtaa wa Kenyata Drive jijini Dar es Salaam ambaye pia atazindua maonesho hayo Novemba 4 katika kituo cha Nafasi Art Mikocheni jijini Dar es Salaam huku ufunguzi wa kwanza utafanyika Novemba 2 ambao utafanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Olle Gabriel.

  Dk. Kilonzo anasema mgeni rasmi Novemba 3 atakuwa Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu, Habib Fent.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  NA ESTOM SANGA-TASAF

  Vikao Kazi vya Serikali na Wadau wa Maendeleo vinaendelea kufanyika mjini Dar es salaam kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

  Mapitio hayo ni utaratibu wa kawaida wa kupima mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unaohudumia kaya za walengwa zipatazo MILIONI MOJA NA LAKI MOJA nchini kote.

  Washiriki wa vikao kazi hivyo vinavyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za makao makuu ya TASAF mjini Dar es salaam, ni pamoja na baadhi ya maafisa wa serikali kutoka Wizara ya Fedha, serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Ofisi ya Rais,Benki ya Dunia,UNICEF,Shirika la Misaada la Ireland,na Shirika la Misaada la Uingereza DFID.

  Wengine ni kutoka UNDP,USAID ,ILO,Fundacion Capital,Brac Tanzania, SVPO Zanzibar,PO- RALG Dodoma, VPO-DOE,MOHCDGEC ,Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Ujenzi,na Wizara ya Kilimo. TASAF imekuwa ikishirikiana na Wizara na wadau hao wa Maendeleo katika kutekelezaji jitihada za serikali za kupunguza adha ya umaskini kwa wananchi wanaoishi katika umasikini uliokithiri.

  Vikao kazi hivyo ambavyo vinafanyika baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya utekelezaji wa Mpango pia vinajadili muundo wa Awamu ya pili ya Mpango wa kunusuru kaya masikini na vitahitimishwa hapo kesho na kisha siku inayofuata andiko la pamoja la mapendekezo ya kuboresha utekelezaji wa Mpango litafikiwa na kisha kuwasilishwa serikalini kupata idhini.
  Moja ya kundi la watendaji wa serikali, wadau wa maendeleo na TASAF wakiendelea na mjadala.
  Pichani, baadhi ya maafisa wa TASAF na wadau wa maendeleo wakiendelea na majadiliano juu ya masuala ya uboireshaji wa shughuli za mpango.
  Pichani ya juu na chini ni wajumbe wa kikao kazi cha maafisa wa TASAF na wadauy wa maendeleo wakiwa kwenye moja ya kumbi kujadili mafanikio na changamoto wa Mpango wa kunusuru kaya masikini.
  Pichani baadhi ya washiriki wa vikao kazi kati ya wadau wa maendeleo, TASAF na serikali wakiendelea na mjadala.

  0 0
 • 11/01/17--03:47: RC Adam Malima Huru
 • Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Novemba 1/2017 imeifuta kesi ya shambulio inayomkabili  aliyekuwa Naibu Waziri wa  Fedha ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Kigoma Malima  na dereva wake Ramadhani Mohammed Kigwande baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP), kuwasilisha Nolle Prosequi. 
  Uamuzi wa kufutwa na kuachiwa kwa washtakiwa hao umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kuomba ifutwe chini ya kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa Mashauri ya Jinai kufuatia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.

  Mhe. Adama Malima na familia yake.
  Picha na Mashughuli Blog
  Baada ya wakili Kishenyi kuwasilisha ombi hilo mahakama hapo Hakimu Mwijage alimuhoji kama anasababu na kwamba kama hana haifuti.

  Kishenyi alisoma kifungu hicho ambacho kinampa mamlaka DPP kuiondoa kesi mahakama ni wakati wowote pale anapoona inafaa na pia kinamruhusu kuirudisha mahakama pia.

  Baada ya Kishenyi kukisoma kifungu hicho, Hakimu Mwijage alikubali na kuwaachia huru washtakiwa wote.

  Kesi hiyo leo ilikujwa kwa ajili ya shahidi wa pili wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wake.
  Hata hivyo, washtakiwa hao walikwishasomewa melezo ya awali (PH),ambapo wote wawili walikubali maelezo yao binafsi, siku ya tukio walikuwepo Masaki, walikamatwa na kushtakiwa na wakayakana mashtaka yote yanayowakabili.
  Katika kesi hiyo, Malima anadaiwa kuwa Mei 15,2017 katika eneo la Masaki kwa makusudi alimzuia ofisa wa polisi H.7818 PC ABDU kufanya kazi yake kwa kumzuia afisa huyo kufanya kazi yake ya kumkamata Ramadhani Kigwande kwa kosa la kumshambulia Mwita Joseph.
  Mshtakiwa Ramadhani Kigwande naye anadaiwa, kumshambulia Mwita Joseph kufanya kazi yake, Mwita ni afisa oparesheni wa kampuni ya Priscane Business Enterprises  wakati alipokuwa akimkamata kwa kupaki vibaya gari namba T 587 DDL alimshambulia na kumsababishia maumivu.

  0 0

  Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati wamempokea rasmi Katibu Mkuu mpya, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua, Makao Makuu ya Wizara, mjini Dodoma. Mapokezi hayo yalifanyika Oktoba 31, 2017 na kuongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lusias Mwenda. Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali wakati wa mapokezi hayo.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu mpya wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto), mara baada ya Katibu Mkuu kuwasili rasmi Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
  Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lusias Mwenda (kushoto), mara baada ya kuwasili rasmi Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
  Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto), akisalimiana na wafanyakazi mbalimbali wa Wizara (kulia), alipowasili rasmi Makao Makuu ya Wizara, mjini Dodoma.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea hati ya ukamatwaji iliyojazwa katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwa muigizaji maarufu wa filamu nchini, Wema Sepetu  kama kielelezo kwa upande wa mashtaka na kutupilia mbali hoja za upande wa utetezi zilizowasilishwa mahakamani hapo na wakili Peter Kibatala.

  Uamuzi huo umetolewa leo, Novemba 1, 2017 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na kusema kuwa upekuzi huo ulifanywa nyumbani kwa Wema na siyo Maungoni mwake kwani kama upekuzi ungefanyika maungoni mwake basi ni lazima angepekuliwa na askari wa kike.

  Awali upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula uliiomba mahakama ipokee hati ya ukamataji Mali uliofanyika nyumbani kwa Wema kama kielelezo huku upande wa utetezi ukipinga.

  Kesi hiyo sasa itaendelea Novemba 16, mwaka huu. Huku Hakimu Simba akiagiza mashahidi wote wa upande wa mashtaka wafike siku hiyo.

  Katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwa Wema panadaiwa kuwa palikutwa na  misokoto inayodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya bangi.

  Katika ushahidi uliotolewa na Inspekta Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Wille (43) kutoka ofisi ya Mkuu wa Upelelezi  wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya  Dar es Salaam yeye alidai katika upekuzi huo walifanikiwa kukuta misokoto inayodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya bangi.

  Wema anashtakiwa pamoja na wafanyakazi wake wawili, Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas. Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

  0 0  0 0

  Aliekuwa mkuu wa mkoa wa RUVUMA Dkt BILINITH SATANO MAHENGE ambaye sasa amekuwa mkuu wa mkoa wa DODOMA amemwagiza mkuu wa mkoa wa ruvuma CHRISTINA MNDEME kuhakikisha kuwa wakala wa barabara mkoa wa RUVUMA TANROAD wasiendeshe bomoa bomoa katika maeneo ya manispaa ya SONGEA kwa sababu wameshindwa kuendeleza barabara hizo na kama watafanya hivyo basi wahakikishe wanalipa pesa kwanza ndivyo wafanye zoezi hilo taarifa kamili hii hapa video yake.

  0 0

  KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi (SACP) Fortunatus Musilim,  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati akimtangaza rasmi mdhamini mkuu wa Wiki ya Nenda kwa usalama mkoa wa Dar es Salaam, inayotarajia kuanza Nov 18 hadi 25 kwenye Viwanja vya Biafra jijini. Kushoto kwake ni Mkuu wa Matawi na Mitandao wa Benki ya StanBic, ambao ni wadhamini, Mussa Kitoi (kulia) ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Teddy Mapunda. Picha na Muhidin Sufiani

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waishio Canada wadumishe mshikamano wao na wawe na uzalendo kwa Taifa lao.

  Ametoa wito huo jana (Jumanne, Oktoba 31, 2017) wakati akizungumza na Watanzania waishio Toronto, Canada.

  Waziri Mkuu ambaye yuko Canada kwa ziara ya kikazi, alisema kila Mtanzania anapaswa ahubiri utaifa wake. “Tembea huku ukiringia nchi yako, wakati wote ringia nchi yako, unapotakiwa kuisemea nchi yako, isemee vizuri kama ambavyo wengine wanasemea vizuri nchi zao licha ya matatizo waliyonayo.”

  Aliwataka wakumbuke kuweka akiba na wanapopata fursa watume fedha zao nyumbani ili zisaidie kuleta maendeleo. “Ukipata kitu kidogo, rusha nyumbani; ukipata mtu anayeweza kuleta tija, mlete nyumbani, nasi tutawapokea wewe na yeye,” alisisitiza. 

  “Tunawasisitiza muitangaze nchi yetu kwa mataifa mengine ili nao waone Tanzania ni mahali pa fursa, na akitaka kuwekeza ajue kuwa anawekeza mahali ambapo ni salama,” alisema.

  Alisema Serikali inasisitiza wananchi waishio nje ya nchi, wawe wazalendo na washirikiane kuhakikisha wanazitumia vizuri fursa za kimaendeleo kwa manufaa ya nchi yao.

  Awali, Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Nzoka, alitumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania waishio nchini humo wazingatie sheria za nchi hiyo.“Wote sisi tunawatambua kama mabalozi katika nafasi zenu hapa Canada. Tunawashauri muwe raia wema, na muishi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi hii na msisahau mlipotoka, kwani hakuna mahali pazuri kama nyumbani,” alisisitiza.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  JUMATANO, NOVEMBA MOSI, 2017.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watanzania waishio nchini Canada, kwenye hoteli ya The Ritz-Carlton Toronto Oktoba 31, 2017
  Watanzania waishio nchini Canada,wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipo kutana nao kwenye hoteli ya The Ritz-Carlton Toronto Oktoba 31, 2017.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

  Baraza la Sanaa la Taifa nchini, leo Novemba 1, limezindua nembo ya miaka 10 ya wiki ya maonyesho ya mitindo ya ‘Swahili fashion week and Awards’, yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 1 hadi 3 mwaka huu, jijini Dar es Salaam. 

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa wa Basata, Vivian Shalua amesema maonyesho hayo yanalenga kuinua uchumi wa nchi, kukuza lugha ya Kiswahili na kupanua fursa ya masoko Tanzania na Afrika Mashariki.Aidha, Shalua amesema, maonyesho hayo ya mitindo ni moja ya maonyesho yanayozalisha ajira za kudumu na hata za muda na pia kuzalisha pato na kuongeza fedha za kigeni kwa kuuza nguo nje ya nchi.

  “Nawapongeza sana waandaji wa maonyesho ya mitindo ‘Swahili Fashion week and Awards’ kwani ni mashindano pekee ambayo hayajawahi kusimama hata mara moja tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008” amesema Shalua. Aidha amewaasa wanamitindo wote ambao wanafanya kazi zao kinyemela bila ya kupitia Basata kwa minajili ya kukwepa kulipa kodi mwisho wao umefika, waache mara moja kwani serikali hii ya awamu ya tano haitawaacha bure. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Swahili Fashion Week na mbunifu mbunifu mkongwe, Mustapha Hassanali amesema maonyesho haya ya Swahili fashion week yatasaidia kutekeleza pia juhudi za Rais Pombe Magufuli katika sera ya kuwa na Tanzania ya uchumi wa viwanda kupitia bidhaa za nguo zinazotengenezwa nchini.

  Amesema, hatua hii kubwa ya kusherehekea miaka kumi itaendelea kuwa kivutio katika maonyesho yote ya mitindo nchini Tanzania huku wabinifu wa ndani na wale wakimataifa wakipata hisia za dhati kwani Swahili fashion week ni jukwaa la kwanza lenya ubunifu kwa wabunifu wa mitindo Africa nzima kwa kuonyesha mavazi yao ulimwenguni kote.

  Amesema, maonyesho ya Swahili week mwaka huu yatafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kuanzia tarehe 1-3 Desemba na pia yatakuwa na wabunifu zaidi ya 50 kutoka nchi mbali zikiwemo, Nigeria, Malawi, Kenya, Uganda, Kenya na nyinginezo ambapo wajasiliamali watapata fursa ya kuonyesha kazi zao za mikono.

  “Tunaomba wadau wajitokeze kwa wingi kusherehekea nasi siku hii muhimu kwa kuwaunga mkono wabunifu wetu wa mitindo vile vile watashuhuhudia mitindo ya kipekee katika maonyesho haya”, amesema Hassanali.Kwa upande wake, Meneja mradi wa Swahili Fashion Week, Glory Urrasa amesema katika sherehe hizo, wanakazania kuboresha sekta ya ukuaji wa mitindo kwa Africa Mashariki wananchi wakishuhudia ukuaji mzuri wa wabunifu wa mitindo,

  “Tofauti na miaka iliyopita, maonyesha haya ya kumi yanajumuisha na utoaji wa tuzo katika siku zote tatu za maonyesho huku tukisisitiza jamii kuwa mitindo ni pato linalozalisha tasnia ya ubunifu na kukuza dhana ya bidhaa za Africa. amesema Urrasa.
   Mkurugenzi wa Swahili Fashion Week, Mustapha Hassanali akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa nembo ya miaka 10 ya wiki ya maonyesho ya mitindo ya ‘Swahili fashion week and Awards’, yatakayofanyika kuanzia Desemba 1 hadi 3 mwaka huu, jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa wa Basata, Vivian Shalua akizungumza na waandisishi wa habari na kuzindua wiki ya maonyesho ya mitindo ya ‘Swahili fashion week and Awards’ yatakayofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Swahili Fashion Week, Mustapha Hassanali na kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vipindi wa Azam TV, Charles Hillary.
   Baadhi ya wanamitindo wakifuatilia jambo kwenye mkutano wa uzinduzi wa nembo ya miaka 10 ya wiki ya maonyesho ya mitindo ya ‘Swahili fashion week and Awards’ yatakayofanyika jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa wa Basata, Vivian Shalua akizindua nembo ya miaka 10 ya wiki ya maonyesho ya mitindo ya ‘Swahili fashion week and Awards’ leo jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa wa Basata, Vivian Shalua akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Swahili Fashion Week, Mustapha Hassanali  pamoja na baadhi ya wanamitindo wa hapa nchini.

  0 0

   Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakifuatilia kikao cha pamoja cha kamati hiyo walipotembelewa na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai kwa lengo la kuangalia jinsi kamati hiyo inavyotekeleza majukumu yake. katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma, uliopo Mjini Dodoma.

   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma, uliopo Mjini Dodoma. kushoto ni katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai na kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mheshimiwa, Sebastian Kapufi.
  Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa lengo la kuangalia jinsi kamati hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma, uliopo Mjini Dodoma. wa tatu kulia ni Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mheshimiwa, Sebastian Kapufi.

   Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, wakifuatilia kikao cha kamati hiyo walipotembelewa na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai na katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai kwa lengo la kuangalia jinsi kamati hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika kilichofanyika leo ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma, uliopo Mjini Dodoma. kushoto ni Mheshimiwa Mary Chatanda, katikati ni Mheshimiwa Atupele Mwakibete na kulia ni Mheshimiwa Neema Mgaya.

   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akiwasili na kupokelewa na  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Ndg. Sebastian Kapufi (kulia) kabla ya kuanza kikao na kamati hiyo kilichofanyika leo ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma, uliopo Mjini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya NchI Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja.
   Baadhi ya Makamanda wa Idara mbali mbali za SMZ wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), alipozungumza na Uongozi wa Wizara  ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
   Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Radhia Rashid Haroub (kulia) alipokuwa akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 katika kikao cha siku moja    kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
   Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Mhe.Haji Omar Kheir (katikati) alipowasilisha Muhtasari wa  Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017, wakati wa kikao cha siku moja cha  Uongozi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)wengine ni  Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya  Mzee (kulia) na Naibu Waziri wa Wizara  hiyo Mhe.Shamata Shaame Khamis.
  Kamishna wa Vyuo vya Mafunzo Zanzibar, Ali Abdalla Ali akitoa maelezo kuhusi Taasisi yake wakati wa kikao cha Uongozi wa Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwepo na Mkuu wa JKU Kanali Ali Mtumwenio Ali. (Picha na Ikulu)

  0 0

  WILAYA ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, imeelezea siri ya kuwa ya kwanza kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, huku ikiipongeza shule ya Hazina ambayo imekuwa ya kwanza kwa Mkoa wa Dar es salaam.

  Ofisa Elimu Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni, alisema jana kuwa matokeo hayo ni matunda ya ushirikiano mzuri baina ya viongozi wa Wilaya hiyo, wamiliki wa shule, walimu na wanafunzi.Alisema hii ni mara ya kwanza kwa Wilaya yake kuwa ya kwanza kitaifa na kwamba hata kiwango cha ufaulu walichofikia hawakuwahi kukifikia hivyo ni mafanikio ya kujivunia.

  “Haya ni matunda ya ushirikiano wetu, tunafanyakazi kama timu moja kuanzia wazazi, uongozi wa Wilaya, kata, uongozi wa shule hivyo tunaahidi kuendelea na ushirikiano huu na mimi kama kiongozi wa elimu wa Wilaya nitahakikisha tunazidi kuwa juu,” alisema.

  Aliipongeza shule ya Hazina kwa kushika nafasi ya kwanza kwa Wilaya ya Kinondoni, wa kwanza Mkoa wa Dar es salaam kwa kundi la shule zenye zaidi ya wanafunzi 40 na vile vile kushika nafasi ya saba kitaifa.Alisema shule za umma nazo zimefanya vizuri sana kwenye matokeo hayo ingawa zilikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi huku akisifu mpango wa elimu bure kuwa chachu ya mafanikio hayo.

  Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Patrick Cheche, alisema kwa miaka zaidi ya 10 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo wamekuwa wakipata mafanikio makubwa mwaka hadi mwaka kwenye matokeo ya kitaifa.Alitoa mfano kuwa shule imekuwa ikipata matokeo mazuri kitaaluma kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na hadi Taifa na kumekuwa na mabadiliko channya kila mwaka ambapo mwaka huu imefanikiwa kuongoza wilaya ya Ilala, nafasi ya kwanza mkoa na nafasi ya saba kitaifa.

  Alisema wamefanikiwa kufungua shule nyingine maeneo ya Bunju ijulikanayo kama New hazina ikiwa ni mipango yao ya kuboresha elimu kuendana na malengo ya millennia.

  Cheche alisema malengo yao ni kuendelea kufundisha kwa bidii sana ili kuendelea kushika nafasi za juu katika mitihani ya kitaifa na kusaidia watoto wengi wa Tanzania kupata elimu bora.
  Ofisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni, Kiduma Mageni akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Hazina, Emma James kwenye mahafali ya shule hiyo. Anayefuata ni Mkuu wa shule hiyo, Patrick Cheche.
   Wanafunzi wa Shule ya Msingi Hazina wakionyesha moja ya michezo yao kwenye mahafali ya shule hiyo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Ofisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Kiduma Mageni.

   Wanafunzi wa Shule ya Msingi Hazina iliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam , wakiwa kwenye shindano ya kujibu maswali ya papo kwa papo wakati wa mahafali ya shule hiyo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Ofisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Kiduma Mageni.

  0 0

  Na Genofeva Matemu, WHUSM, Dodoma.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameitaka Bodi ya Filamu pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa kuendelea kusimamia kazi za sanaa na filamu ili ziweze kukidhi soko la ndani na la kimataifa.

  Waziri Mwakyembe amesema hayo leo Mjini Dodoma wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu.

  “Bodi ya Filamu na BASATA wamekua wakifanya kazi nzuri ya kukinua vipaji katika tasnia ya filamu na muziki nchini. Ni wajibu wenu sasa kuendelea kusimamia tasnia hizo ili ziweze kukidhi matakwa ya nchi yetu pamoja na kuitangaza nchi kimataifa” amesema Mhe. Mwakyembe
  Kwa upande wake Mhe. Grace Tendega amezitaka taasisi hizo kuweka mikakati thabiti ya kusimamia tasnia ya filamu na muziki hatua itakayowasaidia wanatasnia hizo kuboresha maudhui ya maadili katika kazi filamu na muziki.

  Naye Mhe. Kasuku Bilago ameitaka Serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya filamu nchini kwani sekta hiyo inayofasi kuhimu katika kuinua uchumi wa nchi kwa kasi zaidi kama ilivyo katika nchi za wenzetu
  Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Selukamba amewataka wajumbe wa kamati hiyo kuwa na ushirikiano na Serikali katika kubadili mtazamo wa kukuza sekta ya filamu na muziki nchini.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii Mhe. Peter Selukamba (kushoto) akifungua kikao cha wizara na kamati hiyo kujadili  maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Bi. Pamela Palangio
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Suzan Mlawi.
    Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akiwasilisha taarifa ya Bodi ya Filamu wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili  maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma. 
   Mhe. Grace Tendega (kulia) akichangia mada wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma. Kushoto ni Mhe. Sikudhani Chikambo
    Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akiwasilisha taarifa ya Basata wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Suzan Mlawi (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicholaus Willium (kushoto) wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma.  
  Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM

  0 0


  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na maofisa wa forodha wa Sirari wilayani Tarime, kuongeza juhudi katika kulinda rasirimali ili kuunga mkono kasi ya Rais Dk John Mafuguli ya kulinda rasirimali hizo.

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka maofisa wa forodha wa Sirari wilayani Tarime kuongeza juhudi katika kulinda rasirimali ili kuunga mkono kasi ya Rais Dk John Mafuguli ya kulinda rasirimali hizo.

  Ulega ameeleza hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa forodha hiyo katika kikao kati yake na watendaji baada ya kufanya ziara katika eneo hilo.
  Alitoa kauli hiyo, baada ya kuelezwa kwamba wilaya hiyo haina tatizo la mifugo kutoka nje ya nchi na kuingia nchini lakini kumekuwa na tabia kwa baadhi ya madalali kutorosha mifugo na kuuza nchi jirani ya Kenya.

  “Hili halikubaliki kabisa… kwa sababu kama Serikali tunakosa mapato yanayotokana na mifugo hii, na endapo ingekuwa inafuata utaratibu wa kupita katika forodha ya hii, tungepata mapato lakini  badala yake inapitishwa kwa njia za panya hadi Kenya”. Alisema Ulega.

  Aliwaataka watendaji hao kutobabaika badala yake wasimamie sheria na kufanya kazi kwa uadilifu ikiwamo kushirikiana ili kudhibiti hali hiyo ambayo inarudisha nyuma jitihada za Serikali za kuleta maendeleo.

  Pia Ulega alitumia nafasi hiyo kuwaeleza watumishi hao kwamba wizara itahakikisha kituo cha ukaguzi wa mifugo cha Kirumi wilayani Butiama kinafanya kazi kwa ufanisi kwa kuweka miundombinu ya maji na umeme ili mnada uliopo uanze kufanya kazi.

  Kabla ya kwenda katika forodha hiyo, Ulega alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na walipeana mikakati mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha sekta ya mifugo na uvuvi inasonga mbele.

  Katika mazungumzo yao viongozi hao walikubaliana suala la kudhibiti uvuvi haramu hasa unaofanyika katika ziwa Victoria ambapo Malima alimuahidi Ulega kwamba atahakikisha anatumia vyombo vya dola ili kukabiliana na hali hiyo.

  Wakati Malima akieleza hayo, Ulega naye alimuhakikishia kwamba wizara hiyo itakuwa bega kwa bega kushirikiana na mkoa huo katika kuhakikisha sekta hizo zinapiga hatua na kusonga mbele.

  Mbali na hilo, viongozi hao walikubaliana kuanza kwa mchakato wa kufufua viwanda vya kusindika samaki na nyama vilivyopo ili kuunga mkono jitihada za Dk Magufuli za Tanzania ya viwanda
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima alipo wasili juu ya mikakati mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha sekta ya mifugo na uvuvi inasonga mbele.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na watendaji wa wilaya ya Rorya wakati alipofanya ziara kutembelea na kupata taarifa ya hali ya mifugo na uvuvi katika wilaya hiyo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Mara.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa forodha ya Sirari wilayani Tarime.


  0 0

  Ikiwa ni msimu mpya wa ufunguzi wa vyuo mbalimbali nchini, Benki ya CRDB imewapa ahueni kubwa wanafunzi wa elimu ya juu katika vyuo mbalimbali nchini kwa kusogeza huduma za kibenki katika maeneo yanayotumika kufanya usajili wa wanafunzi. Kupitia matawi yake yanayotembea na wakala wa benki (FahariHuduma), Benki ya CRDB imeweza kupeleka huduma za kuweka na kutoa fedha ili kurahisisha malipo mbalimbali yanayofanywa na wanafunzi wakati wanajisajili chuoni ikiwemo kulipia ada na gharama nyingine za chuo.

  Ukiondoa huduma za kuweka na kutoa fedha, zoezi la ufunguzi wa akaunti maalum ya wanafunzi ya Scholar limekua likifanyika ili kuwawezesha wanafunzi hususani wale wanaopokea mikopo ya elimu ya juu kuweza kutunza fedha zao kwa usalama. Katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambacho kina jumla ya vitivo saba ndani yake, Benki ya CRDB imeweza kusogeza huduma za kifedha katika vitivo vyote saba pamoja na kuwa na tawi na mashine za kutolea fedha katika vitivo vyote.

  Akizungumza na mwandishi wetu mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Dodoma Ikupa Mwambene amesema, “tunaishukuru sana Benki ya CRDB kwa kuweza kutusogezea huduma hadi katika vitivo vyetu kwani imeweza kuturahisishia zoezi kufanya usajili na kuokoa muda mwingi”. Nae Afisa Uhusiano wa chuo hiko Bi. Beatrice Baltazar amesema kuwa uwepo wa huduma za benki zinatozolewa na Benki ya CRDB umeweza kuwapa unafuu mkubwa wanafunzi kwa kuwa ilikua ikiwalazimu kwenda nje ya chuo kufata huduma za kibenki kasha kurudi chuoni ili kufanya usajili jambo lililokua linachukua muda mwingi sana.
   Baadhi ya wanafunzi wapya wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wakipatiwa huduma za kuweka na kutoa fedha kutoka Benki ya CRDB kupitia matawi yake yanayotembea na wakala wa benki (FahariHuduma), ili kurahisisha malipo mbalimbali yanayofanywa na wanafunzi wakati wanajisajili chuoni ikiwemo kulipia ada na gharama nyingine za chuo.
   Wakala wa FahariHuduma wa Benki ya CRDB akichukua taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) leo wakatika walipowasogezea huduma za kuweka na kutoa fedha ili kurahisisha malipo mbalimbali yanayofanywa na wanafunzi wakati wanajisajili chuoni ikiwemo kulipia ada na gharama nyingine za chuo.
   Baadhi ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma wakiendelea kupatiwa huduma kutoka kwa Maafisa wa Benki ya CRDB wa tawi lake linalotembea na wakala wa benki (FahariHuduma),


older | 1 | .... | 1992 | 1993 | (Page 1994) | 1995 | 1996 | .... | 3270 | newer