Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1986 | 1987 | (Page 1988) | 1989 | 1990 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kutoka kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kulia) kuhusu utendaji kazi wa Kituo hicho. Wengine pichani (kutoka kushoto) ni Msaidizi wa Naibu Waziri, Ngereja Mgejwa, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu na Mwendeshaji wa Mitambo katika Kituo hicho, Benedict Stephano.

  Na Veronica Simba - Dodoma

  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amefanya ziara katika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo eneo la Zuzu mjini Dodoma, leo Oktoba 28, 2017.

  Akiwa amefuatana na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu, Naibu Waziri Mgalu, ametembelea Kituo hicho ili kujionea utendaji kazi wake.

  Akitoa malelezo kwa Naibu Waziri, Kaimu Mkuu wa Kituo hicho, Bosco Mgina amesema kuwa, Kituo hupokea msongo wa umeme wa kilivolti 220 katika njia tatu ambazo ni Mtera, Iringa One na Iringa Two. Aidha, ameongeza kuwa, Kituo kina transfoma mbili za kupoza umeme ambapo kila moja ina uwezo wa kutoa megawati 24 za umeme hivyo kufanya jumla yake kuwa megawati 48.

  Akizungumzia hali ya upatikanaji wa umeme kwa Mkoa wa Dodoma, Meneja Temu ameeleza kuwa kwa sasa huduma ya nishati hiyo muhimu imerejea katika maeneo yote baada ya jitihada za Shirika hilo katika kutatua matatizo yaliyojitokeza hivi karibuni.

  Akihitimisha ziara yake katika Kituo hicho, Naibu Waziri Mgalu amewasisitiza viongozi wa TANESCO kuhakikisha huduma ya umeme wa uhakika inaendelea kutolewa kwa wateja katika maeneo yote.
  Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kushoto), akimwonesha Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), namna umeme unavyopokelewa kituoni hapo na kusambazwa kwa wateja.
  Kaimu Mkuu wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Zuzu mjini Dodoma, Bosco Mgina (kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), wakati Naibu Waziri alipotembelea Kituo hicho kujionea utendaji kazi wake. Kulia ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akikagua ukarabati wa barabara ya Malendi Wilayani Iramba yenye urefu wa kilomita mbili ambapo ameridhishwa na ubora wa kazi hiyo. Dkt Nchimbi amefanya ukaguzi huo kujiridhisha na ubora wa barabara zote kuu za Kuingia na kutoka Singida katika kipindi cha mvua.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akikagua ukarabati daraja lililopo katika barabara ya Malendi Wilayani Iramba ili kujiridhisha na ubora wa barabara zote kuu za Kuingia na kutoka Singida katika kipindi cha mvua.
  Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida Mhandisi Leonard Kapongo (aliyenyoosha mkono) akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi wakatia akikagua matengenezo ya barabara ya Malendi Wilayani Iramba ili kujiridhisha na ubora wa barabara zote kuu za Kuingia na kutoka Singida katika kipindi cha mvua.
  Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa barabara ya Malendi Wilayani Iramba yenye urefu wa kilomita mbili ili iwe na ubora wa juu wa kupitika katika kipindi cha mvua.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amewatoa hofu wana Singida na watanzania wote kuwa kuelekea kipindi cha mvua barabara kuu zote za kuingia na kutoka Mkoani Singida zinapitika vizuri. Dkt Nchimbi ameyasema hayo mara baada ya kukagua ukarabati wa barabara ya Malendi Wilayani Iramba ambapo ameridhishwa na ubora wa kazi hiyo huku akimtaka Mkandarasi wa barabara hiyo kuongea muda wa kazi ili kukamilisha matengenezo makubwa kabla ya mvua kubwa kuanza.

  Amesema barabara kuu za Kuingia na kutoka Singida ni kiunganishi cha mikoa katika kila upande pamoja na kuiunganisha mikoa hiyo na nchi za jirani kama Rwanda, Burundi na Kongo ambazo hutumia barabara hizo. Dkt. Nchimbi amemtaka mkandarasi Medics Technique Group of Company kuichukulia kwa uzito na thamani ya kimataifa barabara ya Malendi kwa kuwa kutokamilika kwa muda kutawaadhiri watanzania wengi na nchi za jirani kushindwa kusafirisha bidhaa zao kwa wakati.

  “Thamani ya barabara hii sio ya ki mkoa, hapa pakiwa na shida watakaoumia sio wana Iramba au Singida pekee, kuna magari yanasafirisha bidhaa kutoka bandarini Dar es Salaam kuelekea nchi za jirani watapata shida pia, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha hapa panapitika kwa usalama”, amesisitiza Dkt Nchimbi.

  Ameongeza kuwa kutokana na matarajio ya Mkoa wa Singida kupata mvua za wastani na juu ya wastani mkandarasi huyo aongeze masaa mawili kila siku ili kazi hiyo iishe mapema na ifikapo mwezi Disemba magari yaweze kupita juu ya hiyo barabara. Dkt Nchimbi amemtaka mkandarasi huyo kutengeza njia ya mchepuo yenye viwango vya juu ili barabara hiyi ipitike wakati wowote na katika hali yoyote ile.

  Aidha amezitaka halmashauri kujiandaa kupokea mvua kwa kukagua mabwawa kama yanaweza kupokea maji ya mvua vizuri pamoja na mifereji inayopitisha maji isafishwe mapema ili mvua hizo zisilete madhara bali zisaidie kuifanya Singida kuwa ya Kijani na yenye maji ya kutosha. Amewaasa wananchi kuandaa mashamba kwa ajili ya kilimo ili wasipishane na kipindi cha kulima, kupanda au palizi bila kusahau kurekebisha makazi yao ili yawe imara kwa kuhimili mvua za aina yoyote.

  Kwa upande wake Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida Mhandisi Leonard Kapongo amesema mradi wa Malendi unahusisha matengenezo ya barabara yenye urefu wa kilomita mbili kwa upande wa Singida na mita 500 kwa upande wa Mkoa wa Tabora huku ukigharimu shilingi bilioni tatu.

  Mhandisi Kapongo amesema Mkandarasi Medics Technique Group of Company anatarajiwa kukamilisha kazi zote mwezi Machi mwakani kwa kujenga madaraja mawili, makaravati mawili na barabara hiyo kwa kiwango cha lami ijapokua hadi kufikia Disemba barabara hiyo itapitika bila ya lami.

  Ameongeza kuwa ana imani kuwa mkandarasi huyo mzawa atakamilisha kazi hiyo kwa uboa unaotakiwa kutokana na ujuzi na vifaa alivyonavyo huku akieleza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutafanya barabara zote kuu kuwa katika kiwango cha lami yenye ubora zaidi.

  Naye Diwani wa Kata ya Mgongo Mkumbo Wilson ameishukuru serikali kwa kufanya marekebisho katika barabara hiyo ya Malendi kwakuwa imekuwa ni eneo lenye matatizo hasa kipindi cha mvua nyingi. Wilson amesema kipindi cha mvua hasa miaka miwili iliyopita maji yalikuwa yanajaa na kufunika barabara hiyo hivyo kuhatarisha maisha ya wasafiri na wakazi wa Malendi.

  Ameongeza kuwa uharibifu wa mazingira katika mashamba yaliyo jirani na barabara hiyo yameongeza tatizo la kujaa maji eneo hilo kwakuwa mvua zikinyesha maji yanashindwa kuzuiwa mashambani na kujaa barabarani hivyo wataongeza bidii katika kuelimisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Chama cha Wasafirishaji Tanzania (TAT), Omar Kiponza akizungumza na vyombo vya habari kuelezea kero mbalimbali zinazowakabili wanachama wake leo katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam.

  CHAMA CHA WASAFIRISHAJI TANZANIA (TAT)
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Ukumbi wa Mikutano wa TAT
  Ofisi ya TAT Bamaga.

  Kwa niaba ya bodi ya chama cha wasafirishaji na kama tulivyokubaliana wiki moja iliyopita, tunapenda kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakijitokeza Katika shughuli za kila siku za wanachama wetu na kumekuwa na malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na kuhusiana na kero hizo.

  Hivyo kama chama cha wasafirishaji tumeonelea ni vyema tukayaweka mambo haya bayana ili vyombo husika viweze kuchukua hatua ili kuwawezesha wanachama wetu kufanya biashara zao bila usumbufu na kupunguza gharama ambazo hazina tija Katika uendeshaji wa biashara hii usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi.
  Malalamiko hayo ni kama ifuatavyo :-

  Tungependa kutoa malalamiko haya kwa TANROADS kuhusiana na maegesho yaliyopo Katika baadhi ya barabara ambazo magari ya wanachama wetu yamekuwa yakipitia kila siku Katika barabara hizo na ukiangalia hakuna sehemu maalum ya maegesho hivyo utaratibu unaotumiwa kuvuta magari bila ridhaa sababu wamekuwa wakivuta magari bila kutaka maelezo hata kama gari linaweza kutembea lenyewe na kosa kubwa wanalosema ni kwamba umepaki kwenye road reserve hata kama dereva amesimama kwa ajili ya dharura ya posho au document wanakuambia gari iondolewa iende misugusugu na fine wanazotoza huwa ni kubwa mno.ikiwa mwanachama wetu atafanya gereji Barabarani au kufunga njia kwa uzembe basi hapo hatuna pingamizi lolote sheria ifuate mkondo wake na hatuwezi kutetea uharibifu wa miundombinu ya nchi yetu.

  Vile vile kuna suala la mzani ambao upo nje ya Bandari kutokana na usumbufu ambao wanachama wetu wanaoupata endapo mzigo umezidi na unatakiwa kupangwa upya hivyo  tunaomba mamlaka husika ambao ni TANROADS watusaidie kwenye hili suala ikiwezekana huu mzani uwekwe ndani ya Bandari.

  Wakati wa kupakia na kushusha mizigo Bandarini na kwenye Bandari kavu pia kumekuwa na usumbufu huu na kumekuwa na sintofahamu kubwa juu ya nani mwenye barabara hizi kwa sababu kuna wakati wanakuja watu wa manispaa wanasema wrong parking na wakati mwingine TANROADS pia wanasema umepaki gari vibaya sasa hatuelewi kukinzana kwa mamlaka mbili Katika suala moja la maegesho inakuaje utaratibu huu.

  Kuna suala la mizani kutofanyiwa calibration hili suala limekuwa likizunguziwa kwa muda mrefu sana na mizani mingi haina uwiano Katika usomaji tunawaomba muliangalie suala hili kwa umakini ili sote tufanye kazi kama marafiki.

  Upande wa mamlaka ya mapato Tanzania yaani TRA pia kumekuwa na kero ambayo wanachama wetu wanapenda kutoa malalamiko hii ni juu ya suala la utozaji wa faini ya shilingi elfu 40,000 endapo gari litakuwa halijavuka mpaka ndani ya siku7 pale tunduma ikifika siku ya 8 TRA Wanaanza kutoza chaji hiyo kwa kosa ambalo si la msafirishaji.

  Vile kuna jambo ambalo limezuka toka SUMATRA ambapo kuna baadhi ya wanachama wetu wananunua trailers au gari ya mtumba tangia mwaka jana 2016 ambayo haijawahi kufanya kazi hapa nchini lakini wakati wa kwenda kuomba leseni ya usafirishaji kumekuwa na hii kero ya kutozwa faini kwa kitu ambacho hakijawahi kutembea kwa kisingizio kuwa faini hiyo ni kwa ajili ya part registration sasa faini ya nini kwa kitu ambacho hakijatumika?

  Vivyo hivyo kuna jambo lingine linalohusisha watu wa maliasili pindi magari yanapopakiwa mkaa na madereva siyo kwa ruhusa ya tajiri lakini wanapokamatwa adhabu yote ya faini analipishwa tajiri wakati huo huo dereva hapewi adhabu yoyote je hii ni sawa kweli,kwa sababu kuna wasafirishaji ambao washapigwa faini kama milioni 24 kwa sababu ya mkaa je mamlaka husika wanafahamu hili au ni sheria watu wanajichukulia mikononi. 

  Mwisho kabisa tungependa kutoa shukrani za dhati kwa Mstahiki Meya wa jiji,Mkurugenzi wa jiji, wakurugenzi wa Manispaa wa wilaya zote,Mratibu wa Maegesho wa jiji kwa kuondoa kero ya madalali waliokuwa wakikamata magari kwa uonevu tunatumai huu ni mwanzo mzuri kwa hatua kama hizi kuchukuliwa na tunahakika serikali yetu ipo makini Katika kuhakikisha wananchi wake wanasikilizwa pale panapokuwa na walakini Katika utendaji na uendeshaji wa shughuli za kila siku.

  KATIBU

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akimsalimiana na viongozi waandamizi na maofisa wa Jeshi hilo alipowasili Ikwiriri Mkoani Pwani kwa lengo la kuzungumza na wazee na wananchi wa Wilaya zote mbili za Ikwiriri na Kibiti.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiteta jambo na Mkuu wa operesheni maalum za Jeshi hilo, DCP Liberatus Sabas alipowasili Ikwiriri mkoani Pwani kwa lengo la kuzungumza na wazee na wananchi wa Wilayay zote mbili za Ikwiriri na Kibiti. Kulia ni Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, DCI Robert Boaz.
  Baadhi ya milipuko 16, Visu 96 na mbolea ya chumvi inayotumika katika kuchanganyia milipuko ikiwa imekamatwa Mkoa wa Mtwara kufuatia operesheni zinazoendelea za jeshi la Polisi. Picha na Jeshi la Polisi

  0 0

  Dkt.Kigwangalla wakikatisha katika maeneo hayo ya Loliondo wakati akikagua maeneo yenye migogoro.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla mapema jana Oktoba 27,2017 ameweza kutembelea eneo la pori tengefu la Loliondo lililopo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha na kujionea mambo mbalimbali juu ya mgogoro wa muda mrefu maarufu Loliondo. 

  Waziri Dk. Kigwangalla ameweza kutembelea katika eneo hilo katika kushuhudia kiini hicho cha mgogoro uliozidi zaidi ya miaka 20, ambapo anatarajia kurejesha majibu kwa Waziri Mkuu pamoja na Rais mara tu baada ya kumaliza ziara yake hiyo pamoja na kukutana na watalaam wake wa Wizara. 

  Waziri Dkt. Kigwangalla ameweza kuoneshwa eneo lenye mgogoro baina ya mwekezaji pamoja na wananchi wa jamii ya wafugaji kwenye eneo hilo sambamba na kufuatilia mipaka baina ya maeneo mbalimbali yanayozunguka mipaka ya pori hilo tengefu pamoja na hifadhi ya Serengeti. 

  Awali Waziri Dk.Kigwangalla akiwa katika mkutano wa wazi kwenye Mji wa Wasso aliweza kusitisha operesheni zilizokuwa zinaendelea katika pori hilo tengefu la Loliondo na huku akiagiza mifugo yote iliyoshikiriwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo haijafikishwa mahakamani kuachiwa huru huku ile mingine iliyofunguliwa kesi kuendelea kushikiriwa mpaka shahuri la msingi litakapotatuliwa. 

  Aidha, Waziri Dkt. Kigwangalla amewataka wananchi hao jamii ya wafugaji katika mgogoro huo kuacha mara moja kuingiza mifugo ndani ya hifadhi licha ya kusitisha Operesheni iliyokuwa ikifanyika na kuwataka wakae meza moja ya majadiriano kupata ufumbuzi. Akiwa ndani ya pori hilo pia alishuhudia kundi kubwa la wanyama mbalimbali kwenye maeneo hayo ambapo imeelezwa awali hawakuwapo kutokana na kukimbia mifugo iliyokuwa imeingizwa na wafugaji hao.
  Waziri wa Maliasili Dkt.Kigwangalla akiwasili eneo la Loliondo kushuhudia kiini cha mgogoro huo
  Dkt. Kigwangalla akifuatilia ramani yenye kuonesha eneo la pori tengefu la Loliondo.
  Baadhi ya wanyama walioonekana wakati Waziri Dkt.Kigwangalla alipotembelea pori hilo ambapo awali wanyama hao walitoweka kutokana na kuingizwa kwamifugo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Taka (kulia) pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Serengeti William Mwakilema wakati wakikagua maeneo hayo yenye mgogoro huo wa Loliondo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akimsikiliza mmoja wa wananchi waliokuwa wakitoa kilio chao kuhusiana na mgogoro huo wa Loliondo.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Godfrey Daniel Chongolo leo amekagua maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu lenye kulenga kutoa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
  Katika ziara hiyo Mhe. Chongolo amesema kwakuwa idadi kubwa ya wananchi wa Wilaya hiyo ni kutoka jamii ya Wafugaji; Kama Wilaya wamejipanga katika kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa vitakavyosaidia kuondokana na changamoto kubwa ya Wahamiaji Haramu; changamoto ambayo ni kubwa kutokana na kupakana na nchi nyingi jirani. Faida nyingine ni  kuwawezesha wananchi wake ambao niwa jamii ya wafugaji kufanya shughuli zao kwa urahisi zaidi hasa wanapokuwa wakihama hama kutafuta malisho ya mifugo.
  “ Katika kuwasajili wananchi moja ya kikwazo kikubwa hapa ni elimu ya kujua kusoma na kuandika na lugha. Lakini kama Serikali tumejipanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma hii kwa kutumia wataalamu tulionao” alisisitiza.
  Wananchi katika Wilaya hiyo ambao asilimia kubwa ni wa jamii ya Maasai; wameeleza kufurahishwa na hatua ya Serikali  kutoa Vitambulisho vya Taifa kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakipata bughudha kubwa toka upande wa Kenya wanapokuwa malishoni kwakuwa wananchi wa Kenya tayari wanatumia Vitambulisho kuwatambua maarufu kama “Kipande”.
  Wilaya ya Longido inakisiwa kuwa na takribani wananchi 120,000 ambao watasajiliwa Vitambulisho vya Taifa, huku idadi ya wananchi wasiojua kusoma na kuandika ikikadiwa kuwa zaidi ya asilimia 65%.
   Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Longido wakipigwa picha na mashine maalumu ya Usajili wakati zoezi hilo likiendelea Wilayani hapo.
   Hawa ni watendaji wa Vijiji vya Namanga na Longido wakichambua fomu za wananchi wao ili kutoa fursa ya kusajiliwa.
   Mhe. Godfrey Daniel Chongolo (Mwenye suti- kushoto) akikagua fomu za wananchi ambao wamesajiliwa kwa ajili ya kupigwa Picha na Saini ya Kielektroniki alipotembelea vituo vya Usajili Kata za Namanga na Karatu. Katikati ni Afisa Usajili Wilaya ya Longido Bw. Emmanuel Tarimo na Kulia ni Bw. Elisha Noel Afisa Usajili Msaidizi.
  Mhe. Chongolo akiangalia namna taarifa za mwananchi zinavyoingizwa kwenye mfumo kwa kutumia mashine maalumu (Mobile Enrollment Unit –MEU).

  0 0


  0 0


  0 0
  0 0


  0 0

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  WAANDISHI wa habari ambao ni wanachama wa kundi la Whatsapp lijulikanalo kama TASNIA HALISI wamezindua kundi hilo Jumamosi jana  Oktoba 28, 2017 kwa sherehe kabambe ya kukata na shoka iliyohanikizwa na nyama choma, vinywaji vya kila aina na muziki.
  Mratibu wa shughuli hiyo Bi. Angela Msangi amesema kundi hilo ni mukusanyiko wa wanataaluma na wadau wa habari na linalenga kuwaleta pamoja wana tasnia kwa nia ya kubadilishana taarifa na kusaidiana kitaaluma na kijamii.
  Katika uzinduzi huo umeshuhudia waandishi kutoka sehemu mbalimbali nchini wakishiriki, ambapo shampeni mbili zilifunguliwa pamoja na kukata keki.

  Sehemu ya wanahabari wanachama wa kundi la Whatsapp la  TASNIA HALISI wakifurahia wakati wa kuzindua kundi hilo Jumamosi jana  Oktoba 28, 2017

  Sehemu ya wanahabari wanachama wa kundi la Whatsapp la  TASNIA HALISI wakifurahia wakati wa kuzindua kundi hilo Jumamosi jana  Oktoba 28, 2017
  Sehemu ya wanahabari wanachama wa kundi la Whatsapp la  TASNIA HALISI wakifurahia wakati wa kuzindua kundi hilo Jumamosi jana  Oktoba 28, 2017
  Mratibu wa wa kundi la Whatsapp la  TASNIA HALISI  Angellah Msangi akiongea na Dennis Msacky wakati wa kuzindua kundi hilo Jumamosi jana  Oktoba 28, 2017
  Mdau mkuu wa  kundi la Whatsapp la  TASNIA HALISI  Tedy Mapunda akifurahia  wakati wa kuzindua kundi hilo Jumamosi jana  Oktoba 28, 2017. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Miss Higher  Learning 2017, Nelly Kazikazi, akipunga mkono kwa furaha akiwa na washindi wenzake baada ya kutangazwa rasmi na kuvishwa Taji katika shindano la Miss Vyuo Vikuu lililofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye Ukumbi wa King Solomon Namanga Dar es Salaam. Kulia ni mshindi wa pili, Queen Elizabeth Makune (kushoto) ni mshindi wa tatu,  Melody Thomas. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
   Shindano hilo pia lilipambwa na burudani kutoka kwa wasanii tofauti kama JK Comedian Jukwaani, Msaga sumu na Barnaba Boy.
   Sehemu ya wageni waliofika kushuhudia shindano hilo wakiwa katika meza za VIP
   Shoo ilianza kama hivi kwa kufungua na shoo ya pamoja
   Miss Higher Learning 2016, Laura Kway, akimvisha Taji Miss Highlearning 2017, Nelly Kazikazi, baada ya kutangazwa mshindi.
  Miss Higher Learning 2017, Nelly Kazikazi, akipunga mkono kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi.
  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Dear Friends of Zuriel,
   Beyond what she does for Girls Education across the globe, speaking at global events and conferences at the UN or similar, and meeting world leaders, Zuriel is still by many accounts, a regular young teenage girl. She plays the Guitar and Piano, hangs out in the mall and on the beach, teaches young women filmmaking, and plays in a Football [soccer] and Basketball league, on the side - mostly on weekends. 
  Here is a rare VIDEO film footage of her on set before a TV shoot in Los Angeles, after a male director said 'he doesn't believe "Zuriel can Ball". Being LA, someone asked her to "show them the money", dug out a basketball, and - well .....

  0 0

  Na Prof Joseph Mbele
  Kampuni ya Ramble Pictures, ambayo inatengeneza filamu, imemaliza kutengeneza filamu inayohusu safari za mwandishi Ernest Hemingway Afrika Mashariki miaka ya 1933-34 na 1953-54. Nilishaandika taarifa za awali kuhusu filamu hiyo katika blogu hii.

  Sehemu kubwa ya filamu hii ni mazungumzo baina ya Mzee Patrick Hemingway na mimi kuhusu safari hizo za Ernest Hemingway, falsafa yake juu ya maisha na sanaa. Patrick Hemingway ni moto pekee wa Ernest Hemingway aliye bado hai. Filamu inaelezea mambo juu ya mwandishi Ernest Hemingway ambayo yalikuwa hayafahamiki vizuri, hasa juu ya namna mwandishi huyu alivyoipenda Afrika.

  Filamu hii inaitangaza Tanzania, kwa kuwa inaonyesha maeneo kadhaa ya nchi na watu wake, pamoja na safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro. Chimbuko muhimu la filamu hii ni kozi niliyotunga na kufundisha iitwayo Hemingway in East Africa.Nilisafiri na wanafunzi 29 wa chuo cha St. Olaf, ninapofundisha, tukawa tunapita katika maeneo kadhaa ya Tanzania ambamo Ernest Hemingway alipita, huku tukisoma na kujadili maandishi yake kuhusu sehemu hizo.
  Wakati filamu hiyo ilipokuwa inatengenezwa, niliweka taarifa mtandaoni, na nilipeleka taarifa sehemu kadhaa katika mfumo wa serikali ya Tanzania, kuelezea kuwa kuhusu filamu hii itakavyoitangaza Tanzania. Nilifarijika kupata ujumbe kutoka Uwakili wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, ukiafiki kuwa hii ni "fursa maridhawa ya kuitangaza Tanzania ulimwenguni" kama nilivyoelezea katika blogu hii.
  Filamu inapatikana katika tovuti ya Ramble Pictures.

  0 0

   Mshindi wa Shindano lasingeli Michano Bagamoyo Dogo Zero, akiwarusha wakazi wa Bagamoyo mara baada ya kutangazwa Bingwa wa Shindano hilo lililofanyika katika viwanja vya Toptop Bagamoyo.
   Watangazaji wa kipindi cha Genge na ma MC wa shindano la Singeli Michano Pido  Samio  Love wakati wa shindano la Singeli Michano Bagamoyo katika programu ya Nje Ndani ya Efm iliyofanyika katika Viwanja vya Toptop Bagamoyo.
   Mmoja wa Washiriki wa Shindano la Singeli Michano kupitia programu ya Nje Ndani ya Efm
   Mashabiki wa Efm Radio wakifatilia shindano la Singeli Michano Bagamoyo kupitia proglamu ya Nje Ndani
   Majaji wa Shindano la Singeli Michano wakiwa na Dj Autorun wakishuhudia washiriki wanavyochuana katika shindano la Singeli Michano
   Mashabiki wakicheza mara baada ya kutangazwa mshindi wa singeli michano

  0 0  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt Anna Peter Makalala ametoa zawadi kwa akina mama na watoto waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Temeke sambamba na kufanya usafi wa mazingira kuzunguka eneo hilo.
  Hatua hiyo imekuja ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jhn Pombe Magufuli la kufanya usafi kila mwisho wa mwezi.
  Kamishna Jenerali Anna alimkabidhi kijarida chenye masuala mbalimbali yanayohusu uhamiaji kwa mganga mkuu wa hospitali ya Temeke na kumtaka kushirikiana nao kwenye kutoa elimu kwa wagonjwa wanaofika hapo pale pindi wapatapo muda.
  Mganga Mkuu wa hospitali ya Temeke Dr Amani Malima  amewashukuru sana kwa kuja kufanya usafi kwenye hospitali hiyo na kutoa zawadi kwa wakina mama na watoto huku akiwahakikishia kuwa watatoa elimu kwa wagonjwa wanaofika hapo kuhusiana na masuala ya uhamiaji.
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akifanya usafi katika Hosptali ya Temeke ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli ya kufanya usafi kila mwisho wa mwezi, usafi huo umefanyika kwa pamoja na wafanyakazi wa Uhamiaji Dar es Salaam Oktoba 28, 2017.  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala pamoja na Mkuu wa Wilaya ya emeke Felix Lyaviva wakifanya usafi katika Hosptali ya Temeke ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli ya kufanya usafi kila mwisho wa mwezi, usafi huo umefanyika kwa pamoja na wafanyakazi wa Uhamiaji Dar es Salaam Oktoba 28, 2017.
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akijadiliana jambo na mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaviva baada ya kuwasili katika Hospitali ya Temeke kwa ajili ya kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli.

  Kamishna Jeenerali akitoa zawadi ya pampers na sabuni kwa wakina mama waliojifungua watoto walio chini ya muda wake (njiti) walipowatembelea kwenye Hospitali ya Temeke walipokwenda kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi.
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akitoa zawadi kwa wakina mama walipowatembelea kwenye Hospitali ya Temeke walipokwenda kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi.
  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na Salum Vuai, MAELEZO
  USHINDI wa kwanza kwa upande wa wanawake na wanaume kwenye mbio za kilomita 10 katika mashindano yaliyoandaliwa na Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), zote zimechukuliwa na wakimbiaji kutoka Tanzania Bara.
  Katika michuano hiyo iliyofanyika leo ikianzia makao makuu ya KMKM Kibweni mnamo saa 1:10 asubuhi,  na kumalizikia viwanja vya Maisara mjini Zanzibar, Dickson Marwa kutoka Musoma aliibuka wa kwanza upande wa wanaume baada ya kukimbia kwa dakika  29:52:02.
  Nafasi ya pili ilikwenda kwa Mkenya Lameck Mwakio aliyetimka kwa dakika 29:52:07, akifuatiwa na Nelson Mbuya aliyepeperusha bendera ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU), ambaye pumzi zake zilimuwezesha kukimbia kwa dakika 29:59:07.
  Kwa matokeo hayo washindi hao walizawadiwa medali za dhahabu, fedha na shaba mtawalia.
  Mwanadada Sarah Ramadhan kutoka Arusha alifanikiwa kunyakua medali ya dhahabu baada ya kuwatupa wafukuza upepo wenzake kwa dakika 37:18:25, huku Sharo Myryuti (Kenya) akishika nafasi ya pili akikimbia kwa dakika 37:38:43 na kuondoka na medali ya fedha.
  Mwanariadha mzoefu wa michuano ya kimataifa Zakia Mohammed Mrisho kutoka Arusha, aliambulia namba tatu akifikisha muda wa dakika 38:43:45 na kutia mikononi medali ya shaba.
   Naibu Mkuu wa KMKM Kapteni Khamis Simba Khamis (suruali nyekundu) akianzisha mbio  za Kilomita 10  (KMKM 10 Km Race) zilizoanzia Makao Makuu ya Kikosi hicho Kibweni na kumalizia viwanja vya Maisra Mjini Zanzibar.
   Washiriki wa mbio  za kilomita 10 zinazoandaliwa na KMKM wakianza kukimbiza kupitia mitaa mbali mbali ya Zanzibar baada ya kuzinduliwa na Naibu Mkuu wa Kikosi hicho Capteni Khamis Simba Khamis.
   Washindanaji wa mbio za kilomita 10 wakipita katika mzunguko wa eneo la Kariakoo Mjini Zanzibar wakielekea viwanja vya Maisara ambapo ndio mwisho wa mbio hizo.
   Mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 10 mwaka 2017 Dickson Marwa kutoka Dar es Salam akimaliza mbio hizo katika viwanja vya Maisara kwa kutumia dakika 29:52.02 akifuatiwa  na Lamek Mwakio kutoka Kenya alietumia dakika 29:52.07. Mshindi wa tatu ni Nelson Prya.
   Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake Sara Ramadhani Makera kutoka Arusha akimaliza mbio hizo kwa kutumia dakika 37:18.25, Mshindi wa pili wanawake alikuwa Sharo Myryuti kutoka Kenya alitumia dakika 37:38.43. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

   Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akimnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, leo. Akizungumza amesema CCM itashinda Udiwani kata zote tatu ambako uchaguzi unarudiwa mkoani Dar es Salaam. Kata zingine ni Saranga na Mbweni.
   Mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Kijichi Eliasa Mtalawanje akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye mkutano huo
   Mtalawanje akitroti  kuelekea jukwaani baada ya kutambulishwa na Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Temeke.
   Mgombea akionyesha ilani baada ya kukabidhiwa
   Mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, akizungumza na kuomba kura baada ya kunadiwa na Kusilawe, leo
older | 1 | .... | 1986 | 1987 | (Page 1988) | 1989 | 1990 | .... | 3285 | newer