Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1985 | 1986 | (Page 1987) | 1988 | 1989 | .... | 3270 | newer

  0 0


  0 0
  0 0


  0 0

  Shirika la Amref Health Africa Tanzania kwa kushirikiana na Bank M, linawakaribisha wananchi wote kwenye Matembezi ya Hisani 2017 yanayolenga kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, kwa kuwasomesha wauguzi wakunga ili kupata ujuzi wa kutoa huduma bora wakati wa kujifungua.
  Matembezi hayo yatafanyika Novemba 04, 2017 katika Viwanja vya Green Grounds Oysterbay Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa kumi na mbili na nusu mpaka saa nne asubuhi (12:30 – 4:00 asubuhi).
  Mgeni Rasmi katika matembezi hayo anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ambapo yanaambatana na kauli isemayo “Wauguzi  Wakunga Zaidi, kwa Uzazi Salama”.
  Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wanahimizwa kuungana na Amref katika juhudi za kuongeza idadi ya wauguzi wakunga wenye ujuzi kwa kununua tiketi kwa shilingi 25,000 ambapo tiketi hiyo itaambatanishwa na tisheti matembezi hayo.
  Tayari tiketi zinapatikana katika ofisi za Amref zilizopo Upanga karibu na ubalozi wa Japani Jijini Dar es salaam lakini pia waweza kupiga simu nambari 0767 30 30 14 ama 0658 00 67 07 kwa ufafanuzi zaidi.
  Aidha malipo kwa ajili ya kupata tiketi yanafanyika kupitia nambari ya M-PESA 0762  223  348 ama kupitia Bank Account nambari 02 50 02 73 31 BANK M
  Tembelea ukurasa wa Facebook wa Amfref  //www.facebook.com/AMREFHealthAfricaTZ/# ama tovuti www.amref.org kwa taarifa zaidi.
  0 0

  Waziri wa Mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa mkoani Kigoma zenye thamani ya shilingi Milioni thelalini na moja kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi hilo katika serikali hii ya awamu ya tano.
  Akiongea mara baada ya kuteketeza nyavu hizo hizo mapema leo, Mpina alionyesha kushangazwa na suala la uvuvi haramu kuwa sugu “kwa nini vita hii haina mwisho? Lazima yawezekana mbinu zinazotumika ni dhaifu ama silaha zinazotumika ni duni, ifike mahala suala hili  liwe historia”. Alisema Mpina.
  Akitoa Maelekezo kwa viongozi wa Mikoa ambayo shughuli hizi zinafanyika, Mpina aliwataka viongozi hao wawe na jukumu la kulinda rasilimali za taifa ikiwa ni mapoja na Bahari, Maziwa na mito.
  “kama nitashindwa kushughulia suala zima la uvuvi haramu, niitaaachia dhamana hii niliyopewa na Mheshimiwa Rais, na mpaka kufikia hatua hiyo lazima wengi watakuwa wamejuruhiwa.” Alisisitiza Mpina.
  Akiwa katika ziara ya Oparesheni Maalum ya Ondoa Mifugo kutoka katika mikoa ya mipakani na nchi jirani akiwemo Mkoani kigoma, Mpina Pia alitembea mwalo mpya wa Kibirizi Mjini Kigoma na kumtaka Afisa Mifugo na Uvuvi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma kushughulikia changamoto za mitambo wa kugandisha barafu inayokikabili kikundi shirikishi cha rasilimali za uvuvi mwaloni hapo pamoja na suala la kuwauzia dagaa wafanya biashara wanaozisafirisha nje ya nchi. Waziri Mpina Pia alitembelea chuo uvuvi mjini Kigoma.
  Zoezi la opareshini ondoa mifugo na kukomesha rasmi uvuvi haramu limeanza rasmi kwa viongozi wa Wizara husika wakiongozwa na mawaziri Luhaga Mpina na Abdalah Ulega kuingia kazini katika mikoa inayokabiliwa na changamoto hizo. 
   Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akimimina mafuta ya taa kabla ya zoezi la kuteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu mjini Kigoma leo. Nyuma yake ni baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Kigoma watumishi wa umma na wanahabari wakishuhudia tukio hilo.
   Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiwasha moto kuteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu Mjini Kigoma leo.
  Nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zenye dhamani ya shilingi milioni 31 zikiteketea kwa moto kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi la kupambana na uvuvi haramu nchini. 

  0 0

  Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa pongezi kwa Umoja wa Mataifa (UN) kwa kuendelea kushirikiana na kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeleo pamoja na kusaidia changamoto mbali mbali zinazoikabili jamii katika karne hii ya 21 hapa nchini. 
   Dk. Shein aliyasema hayo katika hafla ya kuadhimisha mika 72 tangu ulipoanzishwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN), hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Mjini Zanzibar ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Umoja huo pamoja na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Katika hotuba yake, Dk. Shein alisema kuwa Umoja wa Mataifa (UN) kupitia Mashirika yake ya Maendeleo hapa nchini umeweza kutoa ushirikiano wake mkubwa katika kupambana na umasikini, maradhi, majanga na kusaidia sekta mbali mbali za maendeleo. 
   Alisema kuwa Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na taasisi zake umekuwa ukishirikiana vyema na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kutoa mchango wake mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wa mipango mbali mbali ya maendeleo katika sekta zote za kiuchumi na kijamii. 
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi na Mwakilishi wa UNAIDS katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Leopold Zekeng,wakati alipowasili katika Hoteli ya Serena Zanzibar katika sherehe za Umoja wa Mataifa UN kutimiza miaka 72 tokea kuasisiwa kwake (katikati) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa  Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo UNDP Nchini  Tanzania Bw.Alvaro Rodriguez
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi na Mwakilishi wa UNAIDS katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Leopold Zekeng,wakati alipowasili katika Hoteli ya Serena Zanzibar jana katika sherehe za Umoja wa Mataifa UN kutimiza miaka 72 tokea kuasisiwa kwake (katikati) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa  Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo UNDP Nchini  Tanzania Bw.Alvaro Rodriguez.
   Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na wageni mbali m,bali na waalikwa wakiwa  katika sherehe za Umoja wa Mataifa UN kutimiza miaka 72 tokea kuasisiwa kwake zilizofanyika jana katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
   Mratibu Mkaazi wa Umoja wa  Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo UNDP Nchini  Tanzania Bw.Alvaro Rodriguez wakati akitoa hutuba yake katika sherehe za kutimiza miaka 72  ya Umoja wa Mataifa UN, tokea kuasisiwa kwake zilizofanyika  katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za kutimiza miaka 72  ya Umoja wa Mataifa UN, tokea kuasisiwa kwake zilizofanyika katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazaa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mratibu Mkaazi wa Umoja wa  Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo UNDP Nchini  Tanzania Bw.Alvaro Rodriguez (kulia) wakati wa sherehe za kutimiza miaka 72  ya Umoja wa Mataifa UN, tokea kuasisiwa kwake zilizofanyika katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar. Picha na IKULU.

  0 0

  Na  Greyson Mwase, Geita
  Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amesema Serikali inatarajia kuwasilisha majina ya wananchi 1062 waliofanyiwa  tathmini katika eneo la Kiseme wilayani Geita ili kulipwa fidia  kwa ajili ya kupisha shughuli za uchimbaji madini za Mgodi wa Dhahabu wa Buckreef katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kufanyiwa uhakiki na kubaini uhalali wa umiliki wake kabla ya kuanza kwa taratibu za malipo.
  Waziri Kairuki aliyeambatana na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameyasema hayo mapema leo  katika Mgodi wa Dhahabu wa Buckreef uliopo wilayani Geita mkoani Geita  mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku moja katika mgodi huo ili kujionea maendeleo  ya mgodi huo na kutatua changamoto zake. 
  Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara zake pamoja na Naibu  Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo katika migodi ya serikali, binafsi na wachimbaji wadogo katika mikoa ya  Kagera na Geita ili kufahamu kwa undani  mafanikio na namna ya kutatua changamoto zilizopo katika sekta  ya madini.
  Alisema kuwa, kabla ya kuanza kwa ulipaji wa fidia, ni lazima Wizara ya Madini ihakikishe majina ya wanaodai fidia yanafikishwa katika  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki na wataalam wa wizara hiyo  ili kuepuka udanganyifu kwenye umiliki wa ardhi.
  Aliendelea kusema kuwa katika sekta ya madini kumekuwepo na migogoro mingi hususan katika  madai ya fidia kutokana na wamiliki wengi  wasiokuwa halali kujitokeza na kudai  fidia  hali inayochangia  wawekezaji kushindwa kulipa kutokana na gharama kuwa kubwa.
  Katika hatua nyingine, Kairuki alitaka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lenye umiliki wa asilimia 45 katika mgodi  huo kwa niaba ya  Serikali kuhakikisha linafanya tathmini ya vifaa vyote vinavyotumika katika uchimbaji na uchenjuaji madini pamoja na mikataba  kati yake na mbia wake ambaye ni kampuni ya Tanzam 2000 mwenye asilimia 55.
  “Mkumbuke kuwa mmepewa dhamana  na Serikali ya kusimamia mgodi huu, hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha kuwa maslahi ya Taifa yanaangaliwa huku mkifanya kazi kwa ubunifu wa hali ya juu  ili uchimbaji ulete tija,” alisema Kairuki.
  Wakati huo huo Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza  katika kikao na  uongozi na wafanyakazi wa mgodi wa  dhahabu wa Busolwa Mining Limited, alisema kuwa Serikali ipo tayari kuwasaidia wachimbaji wadogo ili uzalishaji wao  ulete manufaa kwenye uchumi wa nchi.
  Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga katika kuhakikisha kuwa wachimbaji wa madini hususan wazawa wanafanya  shughuli zao katika mazingira rafiki na kupata faida kubwa na kutoka kwenye lindi la umaskini
  Alisisitiza wachimbaji wa madini kufuata kanuni na sheria katika shughuli zao na kuongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini itaendelea kutoa elimu kuhusu kanuni na sheria za madini.
   Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buckreef, Peter Zizhou (kulia) akielezea teknolojia ya zamani ya  uchenjuaji wa dhahabu kwa  Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati) mara alipofanya ziara kwenye mgodi huo uliopo mkoani Geita kwa ajili ya kujionea maendeleo ya shughuli zake tarehe 27 Oktoba, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
   Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akimshukuru  Kaimu Afisa Mtendaji kutoka Kampuni ya  Tanzanian Royalty Exploration, Jeffrey Duval (katikati) mara baada ya kampuni  hiyo kupitia Mgodi wa Buckreef ulioko mkoani Geita kutoa mchango wa madawati 105 yenye thamani ya shilingi milioni saba kwa ajili ya shule ya sekondari moja na shule za msingi nne zilizopo katika kata ya  Busanda wilayani Geita mkoani Geita. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Busanda,  Justa Mabala.
  Mmiliki wa Mgodi wa Busolwa Mining Limited, Christopher Kadeo (wa pili kulia mbele) akielezea shughuli zinazofanywa na mgodi huo kwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati) na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ( kushoto mbele) mara walipofanya ziara katika mgodi huo.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amewataka viongozi wa Serikali na wale wenye upande wa mgogoro wa pori tengefu la Loliondo kukaa chini ili kupata ufumbuzi wa suala hilo lililochukua karibu miaka zaidi ya 20 sasa huku akitoa tamko la kusitisha operesheni zote zilizokuwa zikiendelea katika suala hilo.
  Waziri Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo kwenye mkutano wa wazi Oktoba 26,2017 wakati akizungumza mamia ya wananchi wa Loliondo wakiwemo wale wenye mgogoro na pori hilo.
  “Kuanzia leo, mimi kama Waziri wa Maliasili na Utalii, nina waahidi kufanya uhifadhi endelevu, kukaa na wananchi kuhifadhi. Hivyo nawaomba viongozi wa Serikali na wananchi kwenye mgogoro huu sasa kufikia mwisho na kukaa meza moja.
  Mgogoro utatatuliwa kwa kukaa mezani. Kwa pande zote mbili sasa kuja na jibu moja juu ya kusitisha mgogoro huu. Hatutaki tumuone Mkuu wa Wilaya mbaya ama Mkurugenzi wake ama wahifadhi wabaya au Waziri wa Maliasili  bali, sote tuwe kitu kimoja katika meza ya majadiliano na kufikia mwisho” alieleza Dk.Kigwangalla.
  Ameongeza kuwa:
  “Tutasimamia kushirikiana na nyie. Lakini hatutokubalana na watu miongoni mwetu wa watu ambao wataivunja sheria kwa makusudi. Kwa msingi huo, napenda kutamka kuwa, nasitisha operesheni iliyokuwa ikiendelea Loliondo ile ya kukamata wafugaji na kuwatesa ama vitendo vingine vibaya. 
  Pili naagiza watalaam wa maji, wakae na watalaam wa hifadhi washirikiane na serikali ya kijiji wawaruhusu wafugaji kunywesha mifugo yao.
  Pia naagiza kwa Wahifadhi na Kamati ya Ulinzi na Usalama, mifugo yote ambayo imekamatwa na mamlaka ambayo ipo chini ya Wizara ambayo nasimamia mimi ile yote ambayo haijahukumiwa na mamlaka za kisheria iachiwe huru kwa wenyewe  kwa  mifugo ambayo itabaki chini ya idara iliyopo kwenye wizara yangu ni ile yenye migogoro ya usuluhishi tu” alieleza Dkt.Kigwangalla.
  Waziri Dkt.Kigwangalla yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya siku sita ambapo awali alianza kutembelea Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)mjini Arusha, na baadae Mamlaa ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo pia aliweza kukutana na jamii ya wafugaji wanaoishi kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa namna ya kitatua migogoro kati yao na wahifadhi wa Ngorongoro.

   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubua  kwenye mkutano wa wazi wakati akizungumza mamia ya wananchi wa Loliondo. Pamoja naye jukwaani ni mkalimani
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubua  kwenye mkutano wa wazi wakati akizungumza mamia ya wananchi wa Loliondo. Pamoja naye jukwaani ni mkalimani
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubua  kwenye mkutano wa wazi wakati akizungumza mamia ya wananchi wa Loliondo. Pamoja naye jukwaani ni mkalimani
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubua  kwenye mkutano wa wazi wakati akizungumza mamia ya wananchi wa Loliondo. Pamoja naye jukwaani ni mkalimani

  0 0

  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
  Jeshi la Polisi mkoani Arusha limeunga mkono juhudi za Umoja wa Boda Boda Jiji la Arusha (UBOJA) za kutaka kuanza kusajili wanachama wake pamoja na vituo vyote kwa njia ya kisasa katika mfumo wa kompyuta kama hatua ya kuweka kumbukumbu itakayosaidia watambulike haraka kwa sura, majina yao, vyombo vyao vya usafiri na maeneo yao wanayoishi kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya.
  Akizungumzia nia ya kufanya hivyo na namna itakavyotekelezwa jana katika ukumbi wa bwalo la Polisi ulilopo jijini hapa, Mwenyekiti wa UBOJA Bw. Maulid Makongoro alisema kwamba wameamua kufanya hivyo ikiwa ni mkakati wa kuliunga Jeshi la Polisi katika kutokomeza uhalifu.
  Bw. Makongoro alieleza ili kufanikisha suala hilo la usajili, kila kituo kitatakiwa kwanza kilipe ada ya mwaka mzima lakini pia kitatakiwa kulipia gharama ya Shilingi 20,000 ambapo wanachama wake bila kujali idadi waliyonayo wote watapigwa picha na taarifa zao zitapelekwa kwa viongozi wa wilaya likiwemo Jeshi la Polisi lakini pia kila mmoja atakuwa na kitambulisho.
  “Usajili wa awali ulikuwa wa kibubu bubu kwa mfano baaadhi ya vituo vilikuwa vinamsajili mwanachama bila kumpiga picha lakini kumbukumbu zilikuwa hazifiki ngazi ya juu lakini wa sasa utakuwa wa Kidijitali kwa kuwa ofisi ya UBOJA itakuwa na kumbukumbu hizo kwenye vitabu na kwenye mfumo wa kumbukumbu wa Kompyuta”. Alifafanua Bw. Makongoro.
  Alisema wameamua kufanya hivyo ili kuwadhibiti watu wanaofanya uhalifu kwa mgongo wa waendesha boda boda jambo ambalo linaweza kuwaletea taswira ambayo si nzuri machoni mwa watu.
  Naye mgeni rasmi wa mkutano huo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba, Jeshi la Polisi linaunga mkono moja kwa moja wazo hilo la UBOJA kwani hatua hiyo itasaidia kudhibiti uhalifu.
  Alisema hatua hii inaonyesha nia njema walionao UBOJA kwa Jeshi la Polisi katika kushirikiana na kudhibiti vitendo vya uhalifu katika jiji la Arusha lakini pia mbali ya kuonyesha taswira nzuri kwa jamii itawasaidia kwa usalama wao.

  Kamanda Mkumbo alisema kwa hivi sasa ushirikishwaji wa jamii katika kudhibiti uhalifu ni muhimu sana na kuwataka waendelee kuliunga mkono Jeshi hilo kwa kutoa taarifa mbalimbali za uhalifu hasa unaotokea maeneo yao ya kazi.
  “Kwa hivi sasa wezi wengi wanapenda kuwatumia kwa kuwakodi waendesha pikipiki; kukagua eneo la kufanya uhalifu lakini pia baada ya kufanya uhalifu wanatoroka kwa pikipiki hivyo ukimgundua mtu wa namna hiyo toa taarifa haraka kwa askari yeyote unayemuamini au kwa viongozi ili tumkamate”. Alisisitiza Kamanda Mkumbo.
  Aliwaasa katika utendaji wao wa kazi kutoweka mbele sana pesa bali waangalie uhai wao kwanza hasa wanapoona baadhi ya abiria wanawakodisha kwa pesa nyingi na kuwapeleka maeneo tete hasa usiku kwani wengine hawana nia nzuri.
  Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Joseph Charles Bukombe, aliwataka wananchi wote wa mkoa huu wafuate sheria za usalama barabarani kwani kwa kufanya hivyo hakuna mtu atakayewakamata.
  Mkuu huyo wa Usalama Barabarani alisisitiza suala la kuvaa kofia ngumu “Helmet” kwa dereva na abiria na kusema hatakuwa na msamaha kwa mtu yeyote atakayekaidi hilo awe mtumishi wa serikali au mwendesha pikipiki za abiria na kuongeza kwamba endapo vyombo vya usafiri vitaendeshwa salama basi vitabaki salama na watu watakuwa salama na kutaja kauli mbiu ya mwaka huu ya wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani inayosema “ENDESHA SALAMA HATUTAKI AJALI TII SHERIA TUNATAKA KUISHI”.
    Mwenyekiti wa UBOJA wilaya ya Arusha Bw. Maulid Makongoro akielezea faida ya kusajili wanachama kwa mfumo wa kompyuta na kuonyesha kitabu cha sasa ambacho kina orodha ya waendesha pikipiki wa jiji la Arusha (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
   Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mrakibu wa Polisi (SP) Joseph Charles Bukombe akiwasisitiza waendesha boda boda waliohudhuria mkutano huo kufuata sheria za usalama babarabani ikiwemo kutokuacha kuvaa kofia ngumu "Helmet".(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
   Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akiongea na waendesha bodabdoa wapatao 220 wakati wa kikao cha mkakati wa uhalifu kilichofanyika jana mchana katika ukumbi wa bwalo la Polisi uliopo jijini Arusha. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
  Baadhi ya waendesha pikipiki za abiria maarufu kama boda boda wapatao 220 wa jiji la Arusha waliohudhuria kikao kilichokuwa kinajadili juu ya kuweka kumbukumbu za wanachama wake kwa mfumo wa kompyuta ambacho kilifanyika katika ukumbi wa bwalo la Polisi jijini hapa.
   (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).

  0 0


  0 0

  Na Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma              
  Serikali imejenga kuta na kupanda mikoko katika fukwe mbalimbali hapa nchini ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yalikuwa yakisababisha uhalibifu mkubwa katika fukwe hizo.
  Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Januari Makamba wakati wa mahojiano katika kipindi cha  "TUNATEKELEZA" kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC1) kuhusu mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu Tano.
  “Tumeamua kutafuta fedha ili kupanda mikoko na kujenga kuta ili kudhibiti fukwe kuliwa na bahari,” alisema Makamba.
  Aidha, amesema kuwa, mabadiliko ya tabia ya nchi katika fukwe za bahari yamesababisha  kupotea kwa maeneo ya kilimo kutokana na maji ya bahari kuingia katika mashamba na kuharibu mashamba hayo ambayo mengi ni ya mpunga.
  Makamba amesema kuwa ujenzi wa kuta na upandaji wa mikoko utasaidia kulinda mashamba hayo kutoingiliwa na maji ya bahari pamoja na kuzilinda fukwe za bahari ambazo ni moja ya vivutio vya utalii wa nchini.
  “Bila kuhifadhi mazingira hakuna utalii, uzuri na ubora wa fukwe unategemea fukwe hizo kutoliwa na maji ya bahari” alifafanua Makamba.
  Kwa upande wa Muungano, Makamba amesema Wizara yake imefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili wakazi wa bara na visiwani likiwemo suala la usafirishaji wa magari kwa pande zote mbili.
  “Kulikuwa na malalamiko mengi juu ya kutotambulika kwa magari yanayotoka upande wa Bara kutotambulika upande wa Visiwani, hivyo  hivyo kwa magari yanayosajiliwa upande wa Visiwani  kutotambulika upande wa Bara. Tumelisimamia na kutaka kulimaliza katika sheria mpya za usalama barabarani” alifafanua Makamba.
  Makamba amesema, makubaliano ya sheria hiyo mpya yameshafanyika na kamati za pamoja zaTanzania Bara na Visiwani zimepitisha sheria hiyo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa katika moja ya ziara zake alizozifanya hivi karibuni Mjini Zanzibar

  0 0

  Na Mathias Canal, Singida
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu amezindua msimu wa kilimo 2017/18 ikiwa ni Sehemu ya kuwasihi wananchi kuanza kujiandaa kwani tayari wakati wa kuanza kilimo umekaribia.
  Katika uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji na kata ya Ihanja wilayani Ikungi Mhe Mtaturu pamoja na  mambo mengine lakini amewasihi kutumia vizuri mvua za mwanzo kupandia.
  Katika mkutano huo wa uzinduzi  Mhe Mtaturu pia ameanzisha utaratibu huo wa kuzindua msimu wa kilimo kila mwaka ili kuwaandaa wakulima kuingia msimu mpya mapema ikiwemo kuyakumbusha makampuni ya mbegu kuwafikishia wakulima mbegu kabla mvua kuanza kunyesha.
  Sambamba na utaratibu huo wa kuzindua msimu wa kilimo kila mwaka  pia kutakuwa na zoezi la kufanya maonesho ya zana na teknolojia mbalimbali za kilimo ili wakulima wapate muda wa kujifunza mbinu mpya za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
  Mhe Mtaturu aliwaagiza maafisa ugani kuwa na mashaba darasa na madaftari ya wakulima sambamba na  kuwaunganisha wakulima hao na makampuni ya mbegu ili waweze kupanda mbegu bora zikiwemo zile zinazokomaa kwa muda mfupi.
  Aliwakumbusha wakulima wote kulima mazao ya chakula ili kuwa na usalama wa chakula ambapo aliyataja mazao hayo ambayo yanastahili hali ya ukame kuwa ni pamoja na Mtama, uwele, Mpunga, viazi lishe,viazi vitamu na mihogo.
  Pia aliwataka wakulima kulima mazao ya biashara ili kuwa na uchumi imara huku akitikisa msisitizo  zaidi katika mazao ya kipaumbele katika wilaya hiyo ambayo ni Korosho, Pamba na Alizeti.
  Mhe Mtaturu aliwahakikishia wananchi kupanda mbegu mapema za korosho na dawa za kupulizia ili kuua vijijidudu vinavyoshambulia.
  Alisma kuwa tayari Wilaya ya Ikungi imepokea Mbegu Tani 20 za Pamba ambazo zitaanza kusambazwa wiki ijayo kwa wakulima waliojiandikisha.
  Akisoma taarifa ya idara ya kilimo kwa Mkuu wa Wilaya, Kaimu afisa kilimo Wilaya  ya Ikungi Ndg Teendwa Senkoro alieleza lengo la wilaya hiyo ku ni kulima hekta 124,038 za mazao mbalimbali katika msimu wa mwaka 2017/18 na kuvuna tani 208,700 za mazao mbalimbali.
  Mhe Mtaturu ametimiza ahadi yake ya kuanzisha msimu wa kilimo aliyoahidi hivi karibuni wakati alipofanya kikao kazi na wakuu wa Idara na Vitengo
  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe Ally Mwanga alimpongeza Mhe Mtaturu kwa juhudi zake mbalimbali za kimaendeleo anazozifanya katika Wilaya hiyo tangu ateuliwe kuhudumu katika nafasi hiyo. 
  Alisema kuwa waheshimiwa Madiwani na Halmashauri wataendelea kumuunga mkono katika jitihada hozo ili kuwasaidia wananchi kujiletea maendeleo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu akiwa katika hatua mbalimbali za uzinduzi wa msimu wa kilimo 2017/18  katika kijiji na kata ya Ihanja wilayani Ikungi
   

  0 0

  Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole Gabriel amewaaga watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo mjini Dodoma.
  Prof. Elisante awali ndiye alikuwa anaiongoza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla ya mabadiliko ya safu ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Alhamisi Oktoba 26, 2017.
  Prof. Elisante amewashukuru watumishi hao kwa ushirikiano waliompatia tangu alipoingia Wizarani hapo Aprili 01, 2012 akiwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, Naibu Katibu Mkuu na baadae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Idara ya Maendeleo ya Vijana kwa sasa ipo Ofisi ya Waziri Mkuu.
  “Tunapimwa kwa utendaji kazi, endelezeni utamaduni wa kuchapa kazi kwa kujituma, kushirikiana, kupendana na kuwajali watumishi wote hasa wa ngazi za chini” alisisitiza Prof. Elisante.
  Aidha, amewataka watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa wabunifu ili utendaji kazi wao uwe wenye tija kwa wananchi wote watakao kuja kupata huduma wizarani hapo.
  Kwa upande wa watumishi wa Wizara hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Maedeleo ya Utamaduni Bi. Lilly Beleko amemhakikishia Prof. Elisante kuwa wataendelea kutumia fursa zilizopo kwa maedeleo ya Wizara na taifa kwa ujumla kwa kutumia ujuzi walionao kulingana na taaluma zao. 
  Naye Mkurugenzi wa Sera na Mipango Petro Lyatuu amesema watamkumbuka Prof. Elisante kwa utendaji wake wa kazi kwa kujali muda, kila mara na alikuwa akiwasisitiza kutumia simu kimkakati kwa kupokea na kujibu simu ambapo kila mara alikuwa akisisitiza “Simu zenu mziweke kimkakati wakati wote”.
  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo sasa inaongozwa na viongozi wapya ambapo Katibu Mkuu wake ni Bi. Suzan Paul Mlawi na Naibu Katibu Mkuu akiwa Nicholaus B. William.
   Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyevaa kaunda) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo mjini Dodoma ambapo awali ndiye alikuwa anaiongoza kabla ya mabadiliko ya safu ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Alhamisi tarehe 26 Oktoba, 2017.
   Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyevaa kaunda) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo mjini Dodoma. 
  Picha na Eleuteri Mangi-WHUSM, Dodoma

  0 0

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Seleman Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa nchini kuhakikisha kuwa kila mmoja anajenga viwanda vipya 100 kuanzia Desemba 2017 hadi Desemba 2018.
  Akizungumza na Wakuu wa mikoa wapya walioapishwa jana Ikulu, na kufanya nao mazungumzo katika Ofisi ya TAMISEMI Jijini Dar es Salaam, Waziri Jafo alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo Desemba 2018, mikoa yote 26 ya Tanzania Bara inakuwa na viwanda vipya 2600. 
  Waziri Jafo alisema Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kufikia nchi ya uchumi wa kipato cha kati kupitia ujenzi wa viwanda, hivyo aliwataka wakuu wa Mikoa yote nchini kuhakikisha kuwa wanaibua viwanda vidogo na vya kati kwa kuhamasisha ushiriki wa Viongozi ndani ya mikoa na wananchi wote katika maeneo yao ya utawala.
  Aliongeza kuwa katika kusimamia utekelezaji wa agizo hilo, Ofisi yake itaweka utaratibu maalum wa kupima utendaji kazi wa Kila Kiongozi wa Mkoa katika kuangalia ushiriki wake wa kuwajengea hamasa Viongozi wa chini wakiwemo Wakuu wa Wilaya na wananchi.
  “Serikali itatoa vyeti kwa Mikoa yote itakayofanya vizuri katika ujenzi wa viwanda, hatua hii inalenga kutoa motisha kwa mikoa iliyobaki kuweza kujifunza na kubaini mbinu mbadala katika kuibua viwanda ili kuweza kuwakomboa kiuchumi wananchi” alisema Jafo.
  Kwa mujibu wa Waziri Jafo alisema katika kufanikisha dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini Serikali inaendelea kuweka mkazo na kipaumbele katika upatikanaji wa malighafi za kilimo, na hivyo kuwataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kuwa Maafisa Ugani wanatekeleza vyema majukumu yao ya kazi.   
  Aidha Jafo aliwataka Wakuu wa Mikoa nchini kusimamia vyema makusanyo ya fedha za ndani zinazokusanywa katika Halmashauri zote nchini na kutumia vyema fedha  za asilimia 5 zilizotengwa katika halmashauri kuwawezesha na kuhamasisha wananchi kupata mikopo ili kuwawezesha kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
  Waziri Jafo pia aliwataka Wakuu wa Mikoa kuwaelekeza  Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kuweza kuhamasisha wananchi kujiunga katika vikundi vya ushirika ili weweze kupatiwa mikopo kupitia mifuko ya fedha inayotolewa na Serikali na hivyo kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi.
  Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima alisema ili kufanikisha dhana ya uchumi wa viwanda, Serikali haina budi kuwapa msukumo na ushirikiano wa karibu  Wanasayansi ili kuwawezesha kuibua viwanda vingi zaidi pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa malighafi za kilimo nchini.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Selemani Jafo katikati akizungumza na Wakuu wa mikoa wapya 6 walioapishwa na Rais Dkt. Dkt. John Pombe Magufuli jana Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI), Tixon Nzunda na kushoto ni Naibu Waziri (TAMISEMI), Josephat Kandege.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Selemani Jafo katikati akizungumza na Wakuu wa mikoa wapya 6 walioapishwa na Rais Dkt. Dkt. John Pombe Magufuli jana Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akizungumza wakati wa mkutano baina ya Wakuu wa Mikoa wapya 6 walioapishwa w na Rais Dkt. Dkt. John Pombe Magufuli jana Ikulu Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa wapya 6 walioapishwa na Rais Dkt. Dkt. John Pombe Magufuli jana Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Selemani Jafo (kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima mara baada ya kumalizika kwa kikao baina yao kilichofanyika katika Ofisi za TAMISEMI jana Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa.


  0 0

  STARTIMES Tanzania kupitia chaneli yake ya Star Swahili hatimaye imemaliza shindano la kusaka vipaji vya sauti katika fainali iliyofanyika Ijumaa hii jijini la Dar es Salaam.
  Shindano hili lilifanyika katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam pamoja na Zanzibar na kupatikana washindi takribani 25 waliofuzu kuingia fainali. Washindi kumi wamepatikana ambao watakwenda kufanya kazi ya kuigiza sauti makao makuu ya Kampuni ya Startimes nchini China.

  Akizungumza wakati wa Fainali hiyo Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif  alisema Washindi wa mwaka jana wamepata nafasi ya kuhudhuria makongamano makubwa ya kuonyeshatamaduni mmablimbali likiwemo lile la One Belt One Road na kufanya onyesho la Kiswahili.Pia Shindano hili ni nafasi ya kukabiliana na tatizo la ajira kwani washindi wanaopatikana, moja kwa moja hupata nafasi ya Ajira makao makuu ya Kampuni ya Startimes nchini China.
  Msanii maarufu nchini Tanzania Kutoka kundi la Orijino Komedi maarufu kama Mpoki a k a Muarabu wa Dubai(wa kwanza kulia) kizungumza jambo mara baada ya kutaja washindi 25 waliofuzu kuingia fainali ya shindano la Vipaji vya Sauti katika tamthiliya za kigeni kwa awamu ya pili ya mwaka 2017.
  Majajji wa shindano la vipaji vya sauti la awamu ya pili  lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kishoto ni Msanii wa filamu nchini Jacob Stephen maarufu kama JB, kulia  Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto pamoja na aliyekuwa mshindi wa shindano la vipaji vya sauti mwaka 2016/17.
  Washindi 10 wa shindano la vipaji vya sauti walioshinda kwenda nchini China kufanya kazi makao makuu ya Kampuni ya Startimes  kwenye fainali hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
   Mmoja wa washindi walioingia kumi bora akipokea zawadi ya simu ya Startimes kutoka kwa Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif mara baada ya kumalizika kwa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi(kulia) akimkabidhi zawadi ya Television ya Startimes mshindi wa kwanza wa shindano la vipaji vya sauti msimu wa pili, Coletha Raymond mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo.  0 0

  Wanafunzi wakifurahia msaada waliopewa kwa kunyosha juu vifaa vya kujifunzia 

  Na MWandishi Wetu
  Shirika lisilo la kiserikali la Rise charity limezindua kampeni iitwayo Mtoto kwanza Elimu ni Msingi Ambapo kampeni hiyo yenye dhumuni la kusaidia watoto wa shule za msingi kwa kuwachangia vifaa mbalimbali vitakavyo wawezesha katika Masomo . 
  Kampeni hiyo imezinduliwa kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Morogoro wilaya ya kilosa kijiji cha Ngoisani ndani ya shule ya Mabwegere ikiwa ni kampeni inayotarajiwa kuzunguka katika mikoa mbalimbali Tanzania. 

  Aidha wakati wa uzinduzi huo ulioambatana na kutoa msaada wa vifaa vya kujifunzia Katibu wa kampeni hiyo Atley Timothy Kayuni amewaasa watoto kwa kusema
  "Msaada huu umetolewa na watanzania na wapenda maendeleo hivyo muutumie vizuri na kwamanufaa ya upataji elimu bora ambayo itawasaidia mbeleni katika maisha hivyo mkazane ili kutimiza ndoto zenu" amesema Kayuni.

  Naye Mmoja wa walimu katika shule hiyo Mwl. Mbapila amelishukuru shirika hilo kwa kuwakumbuka na kwenda kuwaona na kusema ni watu wachache sana wenyemoyo wa kujitolea hivyo wasichoke kutoa kwani shule ni nyingi na nyingi zinahari mbaya hususani vijijini.
   Katibu wa kampeni ya "mtoto kwanza elimu ni msingi" Atley T Kayuni akitoa somo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mabwegere iliyopo Kilosa Mkoani Morogoro kabla yakutoa msaada kwa wanafunzi hao.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Rise Media, Innocent Horomo akitoa msaada wa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi, ikiwa ni kampeni inayoendeshwa na Rise Charity iliyofanyika katika shule ya shule ya Mabwegere wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
   Afisa habari wa Rise Media ambae pia ni mwakilishi wa Rise Charity akiteta jambo na wanafunzi wa shule ya msingi mabwegere wakati wa zoezi la uzinduzi wa kampeni ya Mtoto kwanza elimu ni msingi
   Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mabwegele wakiwa darasani wakati wa zoezi la kampeni ya Mtoto kwanza elimu ni msingi.

  0 0
 • 10/28/17--04:10: Article 1

 • 0 0

  Na Mathias Canal, Arusha 
   Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) leo Octoba 28, 2017 amekipongeza Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) kwa kuendelea kufungua matawi mengi nchini ya kuuza pembejeo bora za kilimo. 
   Mhe Mwanjelwa ametoa pongezi hizo wakati akihutubia kwenye Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Tanganyika Farmers’ association (TFA) uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha. 
   Alisema kuwa hiyo ni ishara njema ya kuunga mkono Ilani ya Chama cha Mapinduzi na juhudi za Serikali katika kuendeleza Sekta za kiuchumi ambazo ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi. 
  Alisema kuwa wwa wajibu huo, Wizara ya kilimo imeona juhudi kubwa na za makusudi za Kampuni ya TFA jinsi ilivyojipanga katika kuwahudumia Wananchi na Wakulima nchini. 
   Kupitia Mkutano huo Aliwaomba Wananchi wote kuendelea kuiunga mkono Kampuni ya TFA ili waweze kupata maendeleo ya haraka kwa kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo ili kuondokana na kilimo cha mazoea na kuingia katika kilimo cha kisasa.
   Mgeni Rasmi- Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.Picha zote Na Mathias Canal
   Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akishiriki sala ya kumuombea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
   Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Katibu wa Kampuni ya TFA na Ofisi ya kisheria Bi Pendo Jacob mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA), Mwingine ni Bi Cathy Elizabeth S. Long'lway. leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.

   Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza maelezo kuhusu Kazi za TFA banda la TFA mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA), Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TFA Ndg Peter Ezrah Sirikikwa, na kushoto kwake ni Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro. leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha. 
  0 0

   
  Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelacius Byakanwa akikata utepe kuzindua rasmi maabara yenye nyenzo za elimu ya kidigitali ya Tigo eSchools kwa shule ya sekondari wasichana Machame jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo.
  Mkuu wa wilaya ya Hai, Gelacius Byakanwa (aliyekaa kulia)akipata maelezo ya matumizi ya kujisomea vitabu kwa njia ya mtandao kupitia Tigo eSchools toka kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari wasichana Machame, Delynes Laurian mara baada ya kampuni ya Tigo kukabidhi huduma hiyo shuleni hapo jana.
  Mtaalam wa tovuti toka Shule Direct, Emmanuel George akielezea jambo kwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Gelacius Byakanwa wakati wa uzinduzi wa Tigo eSchools shule ya wasichana Machame leo. Wengine nyuma kushoto Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda kaskazini, Henry Kinabo, mwalimu mkuu wa shule ya Machame, Asteria Massawe.
  Umati wa wanafunzi wa shule ya wasichana Machame Machame wakiwa wanashuhudia uzinduzi wa Tigo eSchoolsl mapema jana.

  0 0

  ZIKIWA zimebaki siku chache tu kufanyika kwa mbio za Rock City Marathon,  kampuni ya Ujenzi ya CRJE leo imekabidhi hundi yenye thamani Tsh milioni 10 kwa waandaaji wa mbio hizo ikiwa ni udhamini wa kampuni hiyo. 

  Mbio zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  Akikabidhi hundi hiyo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi, Ofisa Mahusiano na Utawala wa kampuni ya CRJE Bw Henry Kasapira alisema udhamini huo unalenga kuunga mkono juhudi za serikali kuhamasisha michezo na utalii wa ndani hapa nchini.

  “Michezo huleta uimara wa afya na uimara wa afya ndio nguzo muhimu katika sekta ya ujenzi na ndio maana pamoja na kuinua utalii tunaunga mkono pia mpango huu unaolenga kuhamasisha uimara wa afya za wananchi.’’ Alisema.

  Aliahidi kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na waandaaji wa mbio hizo katika kuboresha zaidi mbio hizo kwa miaka ijayo huku akitoa wito kwa vijana wengi zaidi kutoka mikoa mbalimbali kujiandaa kwa ajili ya mbio hizo.

  Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo, Ngowi alisema ushiriki wa kampuni hiyo ya kimataifa katika kufanisha Rock City Marathon utaongeza viwango vya ubora wa mbio hizo sambamba na kuwavutia zaidi washiri wa kamataifa ambao wamekuwa wakiiamini kampuni kutokana na utendaji wake wenye ufanisi.
  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ujenzi ya CRJE (East Africa Ltd), Bw Xie Zhixiang (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (kulia) ikiwa ni udhamini wa mbio hizo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Mahusiano na Utawala wa kampuni ya CRJE Bw Henry Kasapira (wa pili kushoto) na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Steven Otieno 


older | 1 | .... | 1985 | 1986 | (Page 1987) | 1988 | 1989 | .... | 3270 | newer