Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

MWENYEKITI TPLB ATEUA KAMATI MPYA YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA LIGI

0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Clement Sanga ameteua Kamati mpya ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi.

Wajumbe wanaounda Kamati hiyo ambayo ataiongoza yeye mwenyewe ni Shani Mligo (Makamu Mwenyekiti), Boniface Wambura (Katibu), Issa Batenga, Leslie Liunda na Wakili Saleh Njaa.

Wengine ni Dr Ellyson Maeja, George Malawa, Isaac Chanji, Baruan Muhuza, Mbakileki Mutahaba na Ally Mayay.

Kamati hiyo ya TPLB ndiyo inayoshughulikia uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na Ligi Daraja la Pili (SDL).

Pia Mwenyekiti ameteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB. Wajumbe hao ni Kanali Charles Mbuge ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Ruvu Shooting, na Abuu Changawa (Majeki).

Kwa mujibu wa Ibara ya 28(vi) ya Kanuni za Uendeshaji (Governing Regulations) za TPLB, Mwenyekiti ana nafasi ya kuteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi.

Boniface Wambura
Ofisa Mtendaji Mkuu
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)

WANANCHI MANISPAA YA DODOMA WAITWA KUHUDHURIA MIKUTANO YA BARAZA LA HALMASHAURI

0
0
WAKAZI wa Manispaa ya Dodoma wameshauriwa kuhudhuria Mkutano wa Baraza la Madiwani ili kupata taarifa za miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Manispaa yao na kujua kazi inayofanywa na Madiwani waliowachagua.

Wito huo umetolewa na Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede kuelekea Mkutano wa Baraza hilo wa kisheria kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18  utakaopokea taarifa mbalimbali za Manispaa hiyo kitakachonyika Oktoba 31 mwaka huu katika ukumbi wa Manispaa. Naibu Meya Ngede alitoa wito huo wakati alipoongoza Mkutano wa awali wa Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo lililopokea taarifa za utekelezaji wa miradi kutoka katika Kata zote 41 za Manispaa ya Dodoma Oktoba 25 mwaka huu.

Aliiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuongeza matangazo kwa wananchi kuhusu tarehe ya Mkutano huo ili waweze kuhudhuria kutokana na umuhimu wa mkutano huo ambao ni wa wazi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) akizungumza wakati wa Mkutano wa awali wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo Oktoba 25 mwaka huu. Katika ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Jumanne Ngede na kulia ni Afisa wa Serikali za Mitaa Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Emmanuel Kuboja.

SERIKALI HAINA NIA YA KUCHUKUA MIFUGO YENU -NAIBU WAZIRI ULEGA

0
0
 Serikali imewatoa  hofu wafugaji  nchini kuhusu  mchakato  wa  upigaji  chapa wa  mifugo  na kusema kuwa mpango huo haulengi kuchukua mifugo bali Serikali inataka kubaini  mifugo iliyopo.

Naibu Waziri  wa  Mifugo  na  Uvuvi, Abdallah  Ulega  ametoa hofu jana wakati akizungumza  na wakulima na wafugaji wa kijiji  cha  Perani  wilayani  Mkinga mkoa wa Tanga.

 Kauli hiyo ya Ulega imekuja baada  wafugaji wa Perani kumweleza kwamba hawana elimu ya kutosha kuhusu mchakato huo na kwamba wanahisi kama mifugo yao inachukuliwa na Serikali .

Ulega  amesema Serikali ya Awamu ya Tano, ni sikivu na imedhamilia kuwatumikia vyema Watanzania na siyo kuwanyonya wananchi wa Taifa.
"Rais wetu ni mtu wa wanyonge, hakuna mtu yoyote atakayechukuliwa ngo'mbe zake.Bali tunataka  kujua mifugo yote iliyopo ili kuzuia mwingiliano na ile inayotoka nchi za jirani,"amesema  Ulega. 

Naibu waziri huyo, ametumia nafasi hiyo kuwasihi wafugaji na wakulima wa  eneo hilo kuacha mapigano baina yao kwani siyo jambo zuli na halileti taswira nzuri

"Naomba muishi kwa amani na utulivu kuanzia leo tatizo lenu nitalifikisha ngazi ya juu kuanzia kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela  ili atume wataalamu waje kuangalia namna ya kusimamamia  vyema mpango kazi,"amesema Ulega.

Awali mwenyekiti wa kijiji hicho, Letinga Oyaya alimweleza naibu waziri huyo kwamba wanaomba kuelimishwa namna ambayo mchakato wa upigaji chapa utakavyotekelezwa na madhumuni yake.

Miss Universe kufanyika Jumamosi Oktoba 29, warembo watembelea Tatedo

0
0
Mashindano ya kumsaka mrembo wa Kiss Universe Tanzania yamepangwa kufanyika leo (Jumamos) kwenye ukumbi wa  Makumbusho ya Taifa jijini. Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 10 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa mujibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Tsehai Sarungi.

Maria amewataja mabondia hao kuwa ni Lilian Maraule , Glory Gideon, Melody Tryphone, Anitha Mlay, Silvia Mkomwa, Rogathe Ally, Prisca Dastan ambao wote wanatoka Dar es Salaam. Warembo wengine ni Maureen Foster na Mary Peter wanaotoka Mwanza wakati anayetoka mkoa wa Mbeya Zahra Abdul. Warembo hao walipata mafunzo mbalimbali katika kambi ikiwa pamoja na mafundisho ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO) chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Jensen Shuma.

Warembo hao walipata ujuzi wa jinsi ya kutengeneza majiko ya kisasa ya kupikia kwa kutumia udongo na bati, jinsi ya kutengeneza majiko ya kuoka keki yenye gharama nafuu, jinsi ya kutengeneza mkaa kwa kutumia pumba mbalimbali na ujuzi mwingine. Maria alisema kuwa walipata mafunzo hayo kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais upande wa Mazingira  ili kuwawezesha warembo kupata ufahamu na kuhamasika kujiajiri ili kujipatia kipato.

 “Maandalizi ya mashindano  hayo yamekamilika na wapenzi wa masuala ya urembo watapata burudani safi kutoka kwa  DDI Dance, poetry group (Romantic), A beautiful song kutoka kwa Jeff  Mduma,” alisema Maria.

Alifafanua kuwa wamedhamilia kumpata mrembo bora ambaye atarejesha heshima ya mashindano hayo kama ilivyokuwa kwa Flaviana Matata ambaye alimaliza katika nafasi tano bora nchini Mexico mwaka 2007.

“Tumefanya uchaguzi wa warembo vizuri na wengi ni bora, kwa sasa tunawafundisha masuala mbalimbali ya urembo, lengo ni kuwafanya wawe bora, wote ni washindi, lakini tunahitaji mshindi mmoja ambaye ataliwakilisha Taifa katika mashindano ya Kimataifa,” alisema.

Alisema kuwa mashindano hayo pia yatamtoa mshindi wa taji la Miss Earth Tanzania na mshindi wa taji la Miss Tourism Queen International wa Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Lisilo la Kiserikali na shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO)Jensen Shuma akielezea warembo wa Miss Universe Tanzania jinsi ya kutengeneza mkaa kwa kutumia pumba na mabaki mbalimbali. Anayefuatilia maelezo hayo ni Mtaalam wa Nishati Endelevu na mabadiko ya Tabia nchi Shima Sango.
Mmoja wa wataalum wa Shirika Lisilo la Kiserikali la TaTedo Eva John aliwaelezea washiriki wa mashindano ya Miss Universe Tanzania jinsi ya kutumia jiko la kisasa la kuoka keki.
Mmoja wa warembo wa Miss Universe Tanzania akitengeneza jiko la kisasa la udongo na bati mara baada ya kupata maelekezo na mmoja wa wataalam wa Taasisi ya Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO).
Warembo wanaowania taji la Miss Universe Tanzania 2017, wakiwa katika picha ya pamoja Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi ((kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Lisilo la Kiserikali la (TaTedo) Jensen Shuma na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Martha Ngolowela mara baada ya kutembelea ofisi hizo na kujifunzo ujuzi mbalimbali wa kujiajiriamali.

SETH ASIPTIBIWA HARAKA ANAWEZA KUFARIKI...... PUTO LIMEISHA MUDA WAKE

0
0
MSHTAKIWA wa makosa ya uhujumu Uchumi, Harbinder Singh Sethi ambaye ni mmiliki wa IPTL, ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa 'Puto-Balloon' alilowekewa tumbon limeisha muda wake (expire) na asipobadilishwa litamsababishia kifo.

Wakili wa Seth, Alex Balomi mbele ameileza hayo leo Octoba 27 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Takukuru, Leornad Swai kueleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba kesi iahirishwe.

Katika kesi hiyo Sethi anashtakiwa  pamoja na mmiliki mwenza, James Rugemarila ambapo wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Akielezea kuhusu matibabu ya Sethi, wakili Balomi amedai, pamoja na kutekelezwa kwa amri ya mahakama ya kuamuru mshtakiwa akatibiwe Muhimbili, ambapo alipelekwa na kufanyiwa vipimo lakini mpaka leo hajapatiwa majibu ya vipimo wala matibabu.

Amedai kuwa Puto lililowekwa tumboni kwa mshytakiwa limeisha muda wake, na  linatakiwa kubadilishwa mwishoni mwa mwezi huu wa Octoba

"Kama hilo balloon halitabadilishwa linaweza kugeuka sumu na kuondoa uhai wake, hivyo daktari aliyechukua vipimo anapaswa kumpatia majibu,". Alidai

Kufuatia hali hiyo ya mteja wake, ameomba upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwani  watuhumiwa wanateseka jela bila sababu huku

Akijibu hoja hizo, Wakili Swai amedai mshtakiwa Seth alipelekwa hospital Octoba 13 mwaka huu na kufanyiwa vipimo na daktari, lakini majibu yake ni siri ya Daktari na mshtakiwa na sio vya kuongelea mahakamani.

Alidai kuwa kuhusu upelelezi wanaendelea kufanyia kazi.

Baada ya hayo yote, Hakimu Shaidi amesema mahakama ilitoa amri kwamba Seth apelekwe hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu na amepelekwa, hivyo daktari amekamilisha kazi yake,  mawakili wanaweza kwenda kuulizia kuhusu vipimo vyake huko Hospitali

Aidha ameuagiza upande wa mashtaka kuhakikisha upelelezi unakamilika mapema. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 10 mwaka huu.

MELI YA UTAFITI WA MAFUTA NA GESI YAZINDULIWA ZANZIBAR

0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Baloz Seif Ali Idi katikati akiwa na viongozi wengine akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Meli ya Utafiti wa Mfuta na Gesi BGP EXPLORER kutoka China uzinduzi uliofanyika katika Bandari ya Zanzibar.
Meli ya BGP EXPLORER kutoka China itayoshughulika na Utafiti wa Mafuta na Gesi ambayo imezinduliwa na Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi ikiwa imetia nanga katika Bandari ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Baloz Seif Ali Idi akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Meli ya Utafiti wa Mfuta na Gesi BGP EXPLORER kutoka China uzinduzi uliofanyika katika Bandari ya Zanzibar.kulia ni Waziri wa Ardhi,Maji Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib na kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya RAKGAS Dk,Osama.

STAGE IS SET FOR THE TOP 100 MID SIZED COMPANIES AWARDS TODAY

0
0
Permanent Secretary to the Ministry of Industry and trade Prof. Adolf Mkenda speaking to the stakeholders of the Top 100 Mid sized companies survey during the conference held in Dsm yesterday. The conference was towards the Top 100 Mid sized companies awards to be held today in Dsm today which is organised by KPMG and Mwananchi Communications Ltd in partnership with Bank M. With him, Research Solution Africa MD Jassper Grosskurth (left) and Mustafa Hassanali from Tanzania’s Oil & Gas Suppliers Conference.

Research Solution Africa MD Jassper Grosskurth briefing the stakeholders in regard to the Top 100 mid sized companies survey findings during the stakeholders conference yesterday. The Top 100 mid sized companies awards will take place today evening at Mlimani City Hall.

MICHUZI TV: AMSHA KIPAJI CHAKO NA MISS MBEYA 2017/18


NAIBU WAZIRI ATIMUA WANANCHI WALIOVAMIA HIFADHI YA KATAVI, AAGIZA WATUMISHI WALIOPIMA VIWANJA NDANI YA ENEO LA HIFADHI WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA

0
0

Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (kushoto) akipokea taarifa ya Serikali ya Mkoa wa Katavi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo Mej. Jen. Mst. Rafael Muhuga baada ya kusomwa mbele yake jana alipotembelea mkoa huo kwa ajili ya kutatua migogoro ya hifadhi na wananchi.

NA HAMZA TEMBA -WMU-KATAVI
..............................................................
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga, amewataka  wananchi wa Kitongoji cha Situbwike ambao wamevamia Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kuanzisha shughuli za kibinadamu kinyume cha sheria waondoke kwa hiari ndani ya wiki mbili zijazo kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Naibu Waziri Hasunga amesema hayo jana katika Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi baada ya kutembelea kitongoji hicho chenye kaya zaidi ya 82 ndani ya hifadhi hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutatua migogoro kwenye maeneo ya hifadhi nchini.

"Naagiza, mamlaka husika muhakikishe wananchi hawa wanahama ndani ya wiki mbili zijazo, lazima sheria ziheshimiwe, ifikapo tarehe 10 Novemba, hatutaki tukute mtu hapa, atakayekaidi kitakachompata asitulaumu" aliagiza Naibu Waziri Hasunga.

Kwa upande wa wananchi wa kitongoji hicho ambao wamevamia hifadhi hiyo na kuanzisha shughuli za kilimo, makazi na ufugaji walikiri kuwa wapo ndani ya hifadhi na kwamba walipewa eneo hilo bila ya wao kujua na uongozi wa kijiji cha Stalike ambao kwa sasa haupo madarakani.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga alisema Serikali ya Wilaya hiyo ilitoa notisi ya siku 30 kwa wananchi hao waondoke jambo ambalo halijatekelezwa huku taarifa zikieleza kuwa baadhi yao wamekaidi kuondoka kwa madai kuwa mpaka waone polisi ndio watakusanya virago vyao.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Hasunga ameuagiza uongozi wa TANAPA kuendelea na zoezi la uwekaji wa vigingi vya mpaka katika eneo hilo la hifadhi lenye mgogoro ikiwa ni pamoja na kupima umbali wa mita 500 kutoka kwenye mpaka huo na kuweka mabango yanayoonyesha kuwa eneo hilo haliruhusiwi kwa shughuli za kibinadamu kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mwailwa Pangani kuwatafuta maafisa ardhi waliohusika kuwapimia wananchi wa kitongoji cha Mgolokani eneo la makazi ndani ya hifadhi ya msitu wa Msanginya kinyume cha sheria.

"Nakuagiza Mkurugenzi wa halmashauri, wale wote waliopima eneo hili ndani ya hifadhi hii watafutwe wahojiwe, labda walikuwa na sababu, wakikutwa na makosa wachukuliwe hatua stahiki za kisheria, hawa wanapaswa kuwajibika" alisema Naibu Waziri Hasunga.

Aidha, alimuagiza mkurugenzi huyo kutafuta maeneo kwa ajili ya kuwagawia wananchi waliondolewa katika hifadhi hiyo ya msitu pamoja na wale walioondolewa hifadhi ya taifa ya Katavi waweze kuanzisha makazi mapya, kilimo na ufugaji.

Mwisho alitoa wito kwa watumishi wa Serikali, taasisi na mamlaka zote za Serikali kufanya kazi kwa ushirikiano kuepuka migogoro isiyo ya lazima inayosababishwa na mkanganyiko wa maamuzji baina ya viongozi wa Serikali.
Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mej. Jen. Mst. Rafael Muhuga (kulia) alipotembelea mkoa huo jana kwa ajili ya kutatua migogoro ya hifadhi.
Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga akizungumza katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Katavi alipotembelea mkoa huo jana kwa ajili ya kutatua migogoro ya hifadhi.

SMILE BRINGS THE LOWEST DATA PRICES AT THE FASTEST INTERNET SPEEDS TO TANZANIANS

0
0
From far left Smile Tanzania Country Manager Mr Walingo Chiruyi, Smile Group's Executive Director Mr Ahmad Farroukh, Manager of Usage and Retention Mr Eric Mchaki and Smile Tanzania's Chief Commercial Officer Mr Arindam Chakrabarty together cutting the cake to indicate the launching of the best value internet bundles offered by Smile Tanzania.

Today 27 October 2017, Smile Communications Tanzania (“Smile Tanzania”) brings a new range of data bundles at the lowest data prices with the highest internet data speeds to Tanzanians with ‘Bei ya Ndizi’.

With Bei ya Ndizi all Tanzanians have access to the lowest data prices with SmileAnytime bundles (daily, weekly and monthly validity), setting a new trend for the best value internet at SuperFast speed over 4G LTE, starting from only Tsh 2,000.

Smile Chief Commercial Officer, Arindam Chakrabarty says, “It is our endeavour that everyone in Tanzania is able to fully benefit from the internet world and we now bring our customers’ a wider range of data bundles that is more affordable and still offers the fastest internet in Tanzania”.

He further said that Bei ya Ndizi will see Smile customers being rewarded with BONUS data plus FREE data for Social Media, each time they recharge with SmileAnytime bundles. The FREE data for Social Media gives customers FREE access to Facebook, Instagram, WhatsApp and Twitter.

Smile, known for championing InternetFreedom in Tanzania, is also introducing new bundles for daily, weekly and monthly use, giving customers more freedom of choice and affordability.

“Smile’s SuperFast affordable internet service is available in Dar es Salaam, Mwanza, Moshi, Dodoma, Morogoro, Arusha and Mbeya. We’ve reduced our prices that everyone can have the opportunity to experience Smile’s TRUE 4G LTE service and to stay productive and entertained at the fastest data speeds; daily, weekly or monthly.” concluded Mr Chakrabarty.

Customers in Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Mwanza, Dodoma, Mbeya and Morogoro can now experience the fastest, most reliable internet in Tanzania at the best data rates in town and can look forward to further 4G LTE innovations form Smile.

VIONGOZI WA WALEMAVU AFRIKA WAJADILI SERA YA PAMOJA KWA WALEMAVU

0
0
VIOGOZI wa vyama vya walemavu barani Afrika wakutana jijini Dar es Salaam kwaajili ya kujadili maswala mbalimbali ya walemavu pamoja na kuwa na sera ya pamoja ya walemavu barani Afrika.

Maswala na sera wanazozijadili ni pamoja na maswala ya
kisiasa, kiuchumi, kimiundombinu, kijamii, kiafya, ajira na kielimu ambapo yatawapa fursa walemavu kujikwamua  kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Shirikiso la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Ummy Ndeliananga wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa bara la Afrika unaoendelea kufanyika leo na kesho jijini Dar es Salaam.

Tunatakiwa kuwa na sauti ya pamoja watu wenye ulemavu barani Afrika ambapo tutakuwa na hatua tofautitofauti pia ametoa wito kwa serikali kujenga miundombinu ambayo inafikika kwa walemavu wote katika bara la Afrika.
  Mkurugenzi wa mipango  na ushirikiano wa kimataifa wa Africa Disability alliance), Mpho Ndebele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Muungano wa watu wenye ulemavu wa nchi za bara la Afrika ili kuwa na sera ya pamoja katika kila nchi ili kuwapa nafasi wa lemavu katika nyanja mbalimbali kama kisiasa, kiuchumi, kimiundombinu, kijamii, kiafya, ajira na kielimu ili kupata sauti ya pamoja katika nchi za bara nzima bila kuangalia ni nani anaongoza.
Mwenyekiti wa Shirikiso la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania(SHIVYAWATA), Ummy Ndeliananga akizungumza katika mkutano wa siku mbili ambapo watazungumza masuala mbalimbali ya walemavu katika nyanja mbalimbali kama kisiasa, kiuchumi, kimiundombinu, kijamii, kiafya, ajira na kielimu ili kupata sauti ya pamoja katika nchi za bara nzima bila kuangalia ni nani anaongoza katika nchi zote za afrika.
 Watafsiri wa Lugha za Alama kutoka Kenya na Uganda wakitafsiri mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea ya kuunda sera ya pamoja ya walemavu wa bara Afrika.
 Mtafsiri wa lugha za Alama kulia azingumza na watu wenye ulemavua ambao ni viziwi ili kwenda pamoja katika mkutano utakao fanyika kwa siku mbili ambapo walemavu watajadiliana masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi, kimiundombinu, kijamii, kiafya, ajira na kielimu ili kupata sauti ya pamoja katika nchi za bara nzima bila kuangalia ni nani anaongoza.
 Mkurugenzi mtendaji wa Muungano wa walemavu Afrika kutoka nchini Afrika Kusini (Africa Disability alliance), Dagnachew Wakene akizungumza wa viongozi mbalimbali wavyama vya walemavu barani Afrika wakizungumza maswala mbalimbali ya walemavu na kuunda  sera ya pamoja kwa bara la Afrika.
 Mratibu wa Mkutano wa viongozi wa watu wenye ulemavu, Oktaviani Simba akizungumza katika mkutano unaoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu barani afrika wakiwa katika mkutano unaofanyika jijini Dar es Salaam.

UPANDE WAUTETEZI WA KESI YA MALINZI WAIOMBA MAHAKAMA KUMWITA DPP

0
0
 UPANDE wa utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Jamal Malinzi na wenzake wawili wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imuite Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP) aje kueleza kwanini jalada la kesi hiyo limekaa  ofisini kwake kwa siku 37.

Maombi hayo yamewasilishwa na Wakili Richard Rweyongeza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Takukuru, Leonard  Swai kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada kusikia hayo, wakili Rweyongeza amedai upande wa Mashtaka awali uliomba wiki mbili ili walete taarifa kamili kuhusu jalada hilo kutoka kwa DPP.ambapo Swai alidai hawajapata taarifa ya DPP kuhusu jalada hilo na kwamba bado wanafuatilia.

Amedai kuwa wanawasiwasi mkubwa kuwa, huenda ofisi ya DPP imeamua kuwapeleka washtakiwa gerezani na kuwaegesha kama magari kwa sababu kesi yao haina dhamana ili ikiwapendeza ndio wawachukulie hatua.
“Tunasita kusema ni matumizi mabaya ya sheria ama ni matumizi mabaya ya mamlaka ya DPP lakini hakuna lugha nzuri zaidi inabidi tuseme hivyo”, alisema Rweyongeza.

Wakili Rweyongeza aliomba mahakama imuite DPP mahakamani hapo ili afike kueleza ni nini kinasababisha upepelezi kuchelewa na ili haki ionekane inatendeka kwa muda muafaka anajukumu la kisheria la kuzingatia Haki na kutenda kazi yake kwa kuzingatia Haki. 

Wakili wa utetezi, Abrahamu Senguji alidai naye alishawahi kufuatilia jalada hilo kwa DPP bila mafanikio hivyo ni bora DPP mwenyewe aitwe mahakama kueleza ni kwanini jalada hilo limekaa ofisini kwake kwa muda mrefu au ikiwezekana upande wa mashtaka wawabadilishie washtakiwa mashtaka wapate dhamana wao waendelee na upelelezi.

Swai alisema, jalada hilo lilipelekwa kwa ajili ya kupitiwa ili atoe kibali liendelee ama upelelezi zaidi ufanyike ama hakuna ushahidi wa kutosha ifutwe.

Kufuatia mabishano marefu, Hakimu Mashauri amesema atatoa uamuzi wa hoja hizo Novemba 10,mwaka huu.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 28, yakiwamo ya utakatishaji fedha wa Dola za Marekani, 375,418.

Waziri Jaffo afagilia mchango wa shule binafsi.

0
0



Wanachama wa Chama cha Wawekezaji Binafsi kwenye Elimu TAPIE , wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo, alipokuwa akifungua mkutano wao Mkuu Maalum mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo, akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Wawekezaji Binafsi kwenye Elimu TAPIE uliofanyika mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo,akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa chama cha Wawekezaji Binafsi kwenye Elimu TAPIE , mara baada ya kufungua mkutano wao maalum uliofanyika mkoani Mwanza.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza.
WAZIRI Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo, amesifu mchango wa shule binafsi kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuiinua sekta ya elimu hapa nchini.

Jaffo alitoa sifa hizo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu Maalumu wa siku moja wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Elimu (TAPIE), uliofanyika Jijini Mwanza.

Alisema mchango wa shule hizo umesaidia kuifanya Tanzania ionekane kuwa iko katika hali nzuri kielimu kwa kutoa vijana waliofuzu kimasomo na kuwa na uwezo kuiwakilisha katika mikutano mbalimbali ya nchi za nje.

Mkutano huo wa siku moja ulikuwa na lengo la kujadili namna ya kuboresha sekta ya elimu kwa kuwaleta pamoja wawekezaji na wamiliki wa shule binafsi kuwa na jukwaa la mijadala na midahalo kuhusu uendeshaji wa shule na maslahi ya jamii nzima.

“Kiukweli Shule binafsi zimekuwa zikisaidia kwa kiwango kikubwa katika kuinua elimu ya nchi yetu kwa kutoa vijana waliofuzu vizuri kimasomo na kuipatia sifa Tanzania, ingwa mnafanya vizuri niwaombe muwe waminifu katika kipindi hiki cha mitihani ya kidato cha nne inayotarajia kuanza hivi karibuni, ,”Jaffo.

Naye Rais wa (TAPIE) Ester Mahawe ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), alisema Serikali na wananchi kwa ujumla watambue taasisi hiyo ni chombo kinachowapatia fursaa wamiliki kuwa sehemu ya uandaaji wa sera, miongozo na sheria, za kuendeshea, kuwa kiungo muhimu na mshiriki wa kuisaidia serikali katika kuongeza fursa ya elimu kwa vijana wa Kitanzania na uboleshaji wa utoaji wa elimu hapa nchini.

“TAPIE inahakikisha maslahi ya wamiliki wa shule binafsi hapa nchi yanalindwa na kutetewa katika ngazi na idara zote za serikali na ikumbukwe changamoto za uwekezaji katika sekta ya elimu ni nyingi sana,kuanzia umiliki wa ardhi,kodi na tozo mbalimbali,” alisema na kuongeza

“Sheriia na miongozo isiyo rafiki kwa wamiliki, gharma za wafanyakazi, mikopo yenye riba kubwa nk, hivyo kwa sasa tunahitaji chombo chenye maono na dhamira ya dhati ili kuona mitaji yetu na nguvu zetu zinazotumika zinakuwa na tija na zinalindwa kimfumo,”alisema Mahewa.

Vita ya zamani ya Simba na Yanga imerudi tena, mashabiki wazungumzia kipute Uwanja wa Uhuru Jumamosi

KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA ARDHI APOKELEWA KWA SHANGWE

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika (Kushoto) akipokelewa na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Ardhi mara baada ya kuapishwa na kuwasili katika ofisi zilizopo kanda ya Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika (Kulia) akipokelewa na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Ardhi mara baada ya kuapishwa na kuwasili katika ofisi zilizopo kanda ya Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimpokea kwa shangwe Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara ya Ardhi zilizopo kanda ya Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Dorothy Mwanyika wakati akiongea nao baada ya kuapishwa na kuwasili katika ofisi za Wizara ya Ardhi zilizopo kanda ya Dar es salaam.

Waziri Mwakyembe na Naibu Waziri Shonza washiriki Jukwaa la Sanaa

0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wadau wa tasnia ya muziki (hawapo pichani) wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika leo katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akifafanua jambo wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika leo katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Bibi. Shani Kitogo akijibu hoja wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika leo katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wasanii wakifuatilia mada zilizokua zikiendelea wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika leo katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.

DKT. MWANJELWA AWASILI JIJINI ARUSHA, TAYARI KWA KUFUNGUA MKUTANO WA TFA KESHO

0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro mara baada ya kuwasilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mwingine ni Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza kwa makini maelezo ya hali ya Upatikanaji wa Chakula kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro mara baada ya kuwasilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akijadili jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro wakati akiondoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mwingine ni Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Rasilimali watu (Utawala) wa Mkoa wa Arusha.

Na Mathias Canal, Arusha

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) leo Octoba 27, 2017 aewasili Mkoani Arusha Kwa Ziara ya kikazi ambapo kesho Octoba 28, 2017 atafungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA).

Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha utahudhuriwa na viongozi mbalimbali huku ukitaraji kuhudhuriwa na Wanachama wa Tanganyika Farmers’ Association (TFA).

Pamoja na mambo mengine mkutano huo utabainisha vyema kazi na Huduma zinazotolewa na TFA ambazo ni kuuza Zana bora za kilimo, Pembejeo za kilimo kama Mbolea, Mbegu bora, Viuwatilifu mbalimbali pamoja na kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa Wakulima, kama juhudi ya kumpunguzia mkulima karaha ya upataji wa huduma hizo,

TFA ni mojawapo ya Taasisi kongwe na muhimu kwenye maendeleo ya Sekta ya Kilimo nchini Tanzania na imekuwa ikihudumia Sekta hiyo kwa miaka zaidi ya 80 sasa, tangu ilipoanzishwa mnamo mwaka 1935.

Aidha, Kampuni ya TFA imekuwa ikifanya kazi na Serikali kwa njia ya kutoa huduma kubwa kwa Wakulima wote nchini pale ambapo TFA ina matawi ambayo husambaza na kuwafikishia Wakulima, pembejeo za kilimo zenye ubora wa hali ya juu, kwa wakati na kwa bei nafuu.

WAZAZI NA WALEZI WASIENDEKEZE KUCHANGIA SHEREHE ZAIDI KULIKO ELIMU - NSEKELA

0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Globu ya Jamii - Bagamoyo

WAZAZI wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani wametakiwa kuamka kwa kuona umuhimu wa kuchangia elimu pasipo kuendekeza kuchangia sherehe mbalimbali, ili kuwajengea msingi bora watoto wao katika sekta hiyo.

Meneja wa benki ya CRDB wilayani humo, Nitike Nsekela aliyasema hayo kwenye mahafali ya 6 ya kidato cha nne shule ya sekondari ya wasichana ya Mandera, Chalinze wilayani humo .

Alisema umefika wakati kwa wazazi na walezi kugeukia elimu kama ilivyokuwa katika sherehe na kuacha kuona elimu ni jukumu la serikali pekee .

Aidha Nsekela alikerwa kuwepo kwa tabia za baadhi ya wazazi na walezi kuwakatishwa masomo watoto wao wakike hali ambayo ni kumnyanyasa na kumnyima haki mtoto huyo .

Alieleza ,mwanafunzi wa kike kumkatisha masomo kisha kumuozesha kabla muda wake ni kuyeyusha ndoto yake.

Nae mwalimu Rose Umila akisoma taarifa ya shule alisema wanaotarajia kufanya mtihani wa kuingia kidato cha tano mwishoni mwa mwezi huu ni 98.

Alielezea kwamba ,wanakabiliwa na changamoto ikiwezo ukosefu wa bwalo la chakula, maabara, maktaba, ukumbi wa mikutano sanjali na uchakavu wa majengo yanayohitaji ukarabati.

"Katika ufaulu tumejitahidi kupandisha ufaulu kutoka wanafunzi 12 wa mwaka 2015 kufikia 27 mwaka 2016,"
"Shule hii ina wanafunzi 390, walimu 33 kati ya hao wa sayansi 7, sanaa 25, na biashara mmoja, wafanyakazi wasio walimu 7 ambao ni vibarua kati yao walinzi watatu, wapishi watatu na mlinzi mmoja," alieleza mwalimu huyo.

Shule hiyo ilianzishwa mwaka 2009, huku ikiwa na malengo ya kuhakikisha watoto wa kike wanapatiwa fursa ya kielimu.

RAIS DKT MAGUFULI AAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe.Bi. Christine Solomon Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kabla ya kumbadilisha na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, kubadilishana na Dkt. Bilinith Mahenge anayehamia Dodoma Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Thomas Didimu Kashililah kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya KilimoIkulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017 .

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 27/10/2017

Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images