Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110010 articles
Browse latest View live

KUKATIKA KWA UMEME NCHI NZIMA: DKT. KALEMANI AWAOMBA RADHI WANANCHI

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (pichani juu), amewaomba radhi wananchi kufuatia kukatika kwa umeme nchi nzima Oktoba 25 na 26, 2017 kulikosababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa.
Dkt. Kalemani amabye alikuwa mjini Dodoma akishiriki vikao vya kamati za bunge, alilazimika kusafiri mapema leo asubuhi Oktoba 26, 2017 kuja jijini Dar es Salaam ili kufuatilia juhudi za kurekebisha tatizo hilo.

"Ndugu wananchi hali ilivyotokea sisi kama Shirika la TANESCO na Serikali tunawataka radhi wananchi kwa matatizo yaliyotokea lakini niseme tu kwamba kuna hatua madhubuti zinazochukuliwa hivi sasa kurekebisha hali hiyo ili wananchi muendelee kupata umeme wa uhakika." Alisema Dkt. Kalemani katika taarifa yake kwa wananchi aliyoitoa makao makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam baada ya ziara yake ya kutembelea kituo cha udhibiti cha Gridi ya Taifa, (GCC), kilichoko Ubungo na kituo cha kufua umeme wa gesi cha Kinyerezi1 jijini  Dar es Salaam.

Taarifa za awali zilieleza kuwa kukatika kwa umeme kulisababishwa na "Gridi kuchomoka" Oktoba 25, 2017 majira ya saa 10;08 alfajiri na kurejea saa 12:09 asubuhi ambapo umeme ulirejea mikoa yote isipokuwa Zanzibar, ingawa juhudi za mafundi wa TANESCO ziliwezesha umeme kurejea Zanzibar majira ya saa 1 asubuhi.

Hata hivyo tatizo hilo lilirejea tena majira ya saa 12:30 jioni siku hiyo hiyo ya Oktoba 25, 2017, ambapo takriban mikoa yote iliathirika. Umeme ulirejea tena majira ya saa 3 usiku lakiji ilipofika Oktoba 26, 2017 majira ya saa 12:03 tatizo hilo likajirudia tena na kuathiri takriban mikoa yote ikwiemo Zanzibvar.

"Nimekuja kutoka Dodoma ili kuona nini kimetokea, nini kimesababisha na hatua gani za haraka zichukuliwe ili kuondoa tatizo hilo hii ndio hasa dhamira ya safari yangu." Alisema Dkt. Kalemani baada ya kufika kwenye kituo cha udhibiti Gridi ya Taifa, Ubunmgo.

Lakini niwapongeze TANESCO kwa kutoa taarifa mapema kwa wananchi kuwajulisha kuhusu tatizo hilo, alisema. Akifafanua zaidi Dkt. Kalemani alisema, chanzo cha tatizo ni pamoja na mfumo wenyewe (GCC) na bado unafanywiwa marekebisho na taratibu zinaendelea, na kule Kinyerezi kuna mashine moja haifanyi kazi nayo inafanyiwa marekebishiom ikiwa ni pamoja na valvu moja iliyoharibika nayo pia inafabnyiwa kazi.


"Gridi ya taifa imerejea tangu jana usiku (Oktoba 25), na umeme unapatikana nchi nzima lakini hata hivyo yapo maeneo machache ambayo hayapati umeme wa kutosha kwa sababu mtambo mmoja wa Ubungo namba mbili wenye jumla ya megawati 129 haujaanza kufanya kazi na nimeelekeza wataalamu wafanye kazi usiku na mchana na wamenihakikishia kufikia saa 5 asubuhi kesho  (Oktoka 27), mtambo huo utaanza kufanya kazi na umeme utarejea katika hali yake ya kawaida." Alibainisha.



Dkt. Kalemani akiwa kwenye kituo cha udhibiti wa Gridi ya Taifa (GCC), Ubungo jijini Dar es Salaam.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji (Generation), Mhandisi Abdallah Ikwasa, (kushoto), akimpatia maelezo Waziri Dkt. Kalemani alipotembelea mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi 1 jijini Oktoba 26, 2017. Wakzanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Nishati, Dkt. Juliana Palagyo.

Meneja Mwandamizi wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji, Mhandisi Costa Rubagumya akifafanua jambo.

Meneja wa udhibiti ifumo ya Gridi ya Taifa (Protection), Mhandisi Izahaki Mosha, akimfafanulia Waziri Dkt. Kalemani (kushoto).

Dkt. Kalemani (kushoto), akiwa kwenye chumba cha udhibiti cha Kinyerezi 1 akifafanua jambo.

HAFLA FUPI MARA BAADA YA MKUTANO WA UWEKEZAJI WA VIWANDA MJINI BEIJING KUISHA

MARUDIO YA UCHAGUZI WA RAIS NCHINI KENYA LEO

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YARIDHIA MUSWADA WA SHERIA YA TTCL

$
0
0
Serikali imeandaa Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kuwa inamilikiwa kwa asilimia moja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na iweze kujiendesha kibiashara na hatimaye kutoa gawio kwa Serikali.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa (Mb) wakati akijibu hoja za Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ambao umewasilisha mbele ya Kamati hiyo ambapo wajumbe waliupitia Muswada huo, kutoa maoni, ushauri na mapendekezo ya kuuboresha Muswada. Mawasilisho hayo ya Serikali na majadiliano na wajumbe wa Kamati hiyo yamefanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni mjini Dodoma. 
Mhe. Kwandikwa ameongeza kuwa lengo la Serikali kuandaa Muswada huo, ni kuiwezesha TTCL kujiendesha kibiashara, kutoa gawio kwa Serikali, kuendana na ushindani wa hali ya soko la mawasiliano nchini na kwa maslahi mapana ya taifa kwa kuzingatia kuwa TTCL inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100. Muswada huu utakapokamilika na kuwa Sheria itaiondoa TTCL kwenye Sheria ya makampuni na kuwa chini ya Sheria ya mashirika ya umma na hivyo kuifanya TTCL kuwa Shirika na sio Kampuni tena. 
Katika kikao hicho, Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imepokea hoja kutoka kwa Kamati hiyo za kuboreha Muswada huo. Hoja zilizopokelewa ni hoja 26 zenye makosa ya kiuandishi zinazohusu Muswada huo ambapo zitafanyiwa marekebisho na hoja mahususi nne zilizojikita kwenye kifungu cha 7(5) na 7(7) kinachozungumzia wajumbe wa Bodi, kifungu cha 9(1) kinachohusu mamlaka na maelekezo ya Waziri mwenye dhamana kwa Bodi na kifungu cha 15(3)(b)kinachohusu kigezo cha uzoefu wa uongozi wa mtendaji mkuu wa shirika wa angalau miaka 8 ya atakayeteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu ambazo zimetolewa ufafanuzi na Mhe. Kwandikwa kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.  
Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeridhia Muswada huo ikiwa ni pamoja na majibu ya Serikali ya hoja 26 za Kamati zenye makosa ya kiundishi, hoja moja ya kifungu cha 7(5) kati ya hoja nne mahususi. Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Prof. Norman Sigalla King ameieleza Serikali kuwa msimamo wa Kamati yake ni kuitaka Serikali ipunguze muda wa uzoefu wa uongozi wa mtendaji mkuu wa shirika kutoka kigezo cha muda wa angalau miaka minane na kuwa miaka mitatu kama ilivyo kwenye kifungu cha 15(3)(b). 

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias John Kwandikwa (kushoto) akifafanua hoja kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni, Dodoma. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Norman Sigalla King.
 Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete (aliyekaa katikati) akifuatilia majadiliano ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Emmanuel Mwakasaka (anayeongea) akichangia hoja kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania uliowasilishwa kwenye Kamati hiyo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (hayupo pichani) kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni, Dodoma.

Waziri Mahiga afungua Mkutano wa Mawaziri wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (TRIPARTITE)

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifungua Mkutano wa kwanza wa Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Miundombinu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (TRIPARTITE) uliofanyika katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Oktober 2017.
Viongozi na wajumbe kutoka Nchi Wanachama wakifuatilia Mkutano, wa tatu kutoka kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbalawa na wa nne kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima.

Sehemu nyingine ya Wajumbe kutoka nchi Wanachama wakifuatilia Mkutano.
Mkutano ukiendelea.

Picha ya pamoja.
Kwa taarifa zaidi BOFYA HAPA

Dkt. Kigwangalla atua Loliondo, afanya kikao kizito na Kamati ya Ulinzi na Usalama Ngorongoro

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amewasili Makao makuu ya Wilaya ya Ngorongoro na kisha kufanya mkutano maalum na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo ambapo kisha atazungukia kwenye maeneo yenye migogoro. 
Waziri Dkt.Kigwangalla ametua uwanja mdogo wa Wasso uliopo eneo la Loliondo na kisha kukutana na viongozi hao wa Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Rashid Mfaume Taka.Dk Kigwangalla baada ya kumaliza kikao hicho maalum na wakuu hao, anatarajia kutembelea maeneo yenye migogoro ili kubaini kiini cha mgogoro wa eneo hilo la pori tengefu la Loliondo. 
Aidha, pia anatarajia kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo pamoja na kufanya mkutano wa wazi ikiwemo kusikiliza kero kutoka kwa wananchi hao.Waziri Dkt.Kigwangalla yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya sita ambapo awali alianza kutembelea Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)mjini Arusha, na baadae Mamlaa ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo pia aliweza kukutana na jamii ya wafugaji wanaoishi kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa namna ya kitatua migogoro kati yao na wahifadhi wa Ngorongoro.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye ndege wakati akiwasili Loliondo kufuatilia kwa kina mgogoro unaoendelea Loliondo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiongozana na na viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro kwenye uwanja wa ndege wakati akiwasili Loliondo kufuatilia kwa kina mgogoro unaoendelea wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Rashid Mfaume Taka akimwakilisha Waziri Dk.Kigwangalla katika mkutano huo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA HABARI,UTALII,UTAMADUNI NA MICHEZO

$
0
0
 Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe.Rashid Ali Juma  (katikati) alipokuwa akisoma taarifa yake katika   kikao cha siku moja cha  Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 cha  Uongozi wa Wizara  hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
 Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali zilizo chini ya Wizara ya  Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo  wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),alipozungumza na Uongozi wa Wizara hiyo leo katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja
Katibu Mkuu wa  Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Nd,Omar Hassan Omar (king)(kushoto) alipokuwa akifanya uchambuzi wa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 cha Wizara ya hiyo,wakati wa kikao cha siku moja   kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein

Mkurugenzi Mkazi Andy Karas Azuru Progamu za USAID Mkoani Morogoro

$
0
0
Toka tarehe  17 hadi 20 Oktoba, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Andy Karas alifanya ziara mkoani Morogoro ili kujionea matokeo ya programu mbalimbali zinazoendeshwa na USAID mkoani humo pamoja na kufanya mazungumzo na wabia na walengwa wa programu hizo. 
Ziara hii inaakisi wigo mpana wa miradi inayofadhiliwa na Marekani nchini Tanzania, ikijumuisha sekta za kilimo, lishe, elimu, afya, wanawake na vijana na utawala bora. 
Kwa muda mrefu, mkoa wa Morogoro umekuwa mlengwa wa msaada wa maendeleo wa Serikali ya Marekani kutokana na fursa yake kubwa ya kilimo, taasisi za kielimu na kuwa katika eneo zuri la kimkakati lililo karibu na miundombinu ya usafirishaji. 
Mkoani humo ndipo ilipo mojawapo ya programu za kwanza kabisa kufadhiliwa na USAID nchini Tanzania – ambayo ni uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.  
Akiwa chuoni hapo, Mkurugenzi Mkazi Karas alitembelea maabara mpya ya TEHAMA iliyofadhiliwa na USAID  na kukutana na wanafunzi wa Shahada ya Uzamili walionufaika kutokana na mradi wa utafiti wa kilimo ujulikanao kama Innovative Agricultural Research Initiative -iAGRI, uliokuwa ukifadhiliwa na USAID. 
Ziara hiyo iliangazia msaada unaotolewa na USAID kwa shule, vituo vya afya, mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Dakawa na ushirika wa wakulima 950 wanaonufaika nao. Hali kadhalika, ziara ilihusisha miradi ya kijamii ya lishe na ile ya kuboresha utoaji huduma katika sekta ya umma na mamlaka za serikali za mitaa.  
Aidha, Mkurugenzi Mkazi Karas alikutana na viongozi wa serikali mkoani humo pamoja na washiriki wa programu nyingine zinazofadhiliwa na Serikali ya Marekani ikiwa ni pamoja na Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps na wahitimu wa mpango wa kuwaendeleza vijana wa Kiafrika katika uongozi uitwao Young African Leaders Initiative (YALI).
Mkurugenzi Mkazi Andy Karas alijiunga na USAID/Tanzania mwezi Agosti 2017. Amewahi kufanyakazi na USAID katika nchi za Rwanda, Afghanistan, Djibouti, Ghana na Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki jijini Nairobi.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Andy Karas akiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Dumila wakati alipofanya ziara mkoani Morogoro ili kujionea matokeo ya programu mbalimbali zinazoendeshwa na USAID mkoani humo hivi karibuni.

MICHUZI TV BREAKING: KUKATIKA KWA UMEME NCHI NZIMA, WAZIRI WA NISHATI DKT. KALEMANI AWAJIA JUU TANESCO

MICHUZI TV NEWS ALERT: MVUA YALETA MAAFA DAR, MTU MMOJA AFARIKI DUNIA ILALA

BREAKING NYUZZZZ: RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR LEO

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Oktoba 26, 2017 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali  wakiwemo Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara, Mabalozi pamoja na Wakuu wa Mikoa. 
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akisoma majina ya  walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani  Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam leo Oktoba 26, 2017

Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu wao

Ofisi ya Rais Ikulu - Katibu Mkuu Alifayo Kidata

Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na utawala Bora - Katibu Mkuu Dr. Lawrian Ndumbaro
 Naibu Katibu Mkuu - Bi. Dorothy Mwaluko

Ofisi ya Rais TAMISEMI - Katibu Mkuu Eng. Mussa Iyombe
 Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI Afya) - Zainabu Chaula
Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI Elimu) - Dickson Nzunda

Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira - Katibu Mkuu Eng. Joseph Kizito Manongo (alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo hiyo)
 Naibu Katibu Mkuu - Bi. Butamo Kasuka Philipo

Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi na Ajira - Katibu Mkuu Erick Shitindi
Bunge na Waziri Mkuu - Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi
Sera - Katibu Mkuu Faustine Kamuzora (amehamishwa kutoka ofisi ya makamu wa rais)

Wizara ya Kilimo - Katibu Mkuu Eng. Mathew Mtigumwe
Naibu Katibu MKuu - Dr. Tomas Didim Kashilila

Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Mifugo - Katibu Mkuu Dr. Maria Mashingo
Uvuvi - Katibu Mkuu Dr. Yohana Budeba

Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano
Uchukuzi - Katibu Mkuu Dr. Leonard Chamuriho
Ujenzi - Katibu Mkuu Eng. Joseph Nyamuhanga
Mawasiliano - Katibu Mkuu Dr. Maria Msasabo
Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano - Eng. Adelina Madete

Wizara ya Fedha na Mipango - Katibu Mkuu Dotto James Mgosha
 Naibu Katibu Mkuu Utawala - Bi. Suzan Mkapa
 Naibu Katibu Mkuu Fedha za Nje - Bi. Amina Shaaban
 Naibu Katibu Mkuu Sera - Dr. Hakingu M. Kazungu

Wizara ya Nishati - Katibu Mkuu Dr. Hamis Mwinyimvua (Anatoka ofisi ya Waziri Mkuu)

Wizara ya Madini - Katibu Mkuu Prof. Saimon S. Msanjila (alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu)

Wizara ya Katiba na Sheria - Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome > Naibu Katibu Mkuu - Bwana Amon Mbanju

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Katibu Mkuu Prof. Adolph Mkenda (ambaye ni Mchumi, anatoka Wizara ya Biashara na Uwekezaji).

 Naibu Katibu Mkuu - Balozi Ramadhan Muomba Mwinyi
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Katibu Mkuu Dr. Florence Nduruka

 Naibu Katibu Mkuu - Bi. Emmaculate Peter Ngwale

Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa
Mkoa wa Manyara - Mkuu wa Mkoa ni Alexandar Pastor Mnyeti (Alikuwa DC wa Arumeru)
Mkoa wa Rukwa - Mkuu wa Mkoa ni Joachim Leonard Wangabo (alikuwa DC wa Nanyumbu)
Mkoa wa Geita - Mkuu wa Mkoa ni Bwana Robert Gabriel Lughumbi (alikuwa DC wa Korogwe)
Mkoa wa Mara - Mkuu wa Mkoa ni Adam Kigoba Ally Malima (aliwahi kuwa kwenye baraza la mawaziri awamu ya nne)
Mkoa wa Dodoma - Mkuu wa mkoa ni Bi. Christine Solomoni Mndeme (alikuwa DC wa Dodoma Mjini)
Mkuu wa Mtwara - Gelasius Gasper Byakanwa (alikuwa DC wa Hai)

Uteuzi wa Mabalozi
Dr. Aziz P. Mlima - Ameteuliwa kuwa Balozi (alikuwa Katibu Mkuu wizara mambo ya nje)
IGP Mtaafu Ernest Mangu - Ameteuliwa kuwa Balozi

Hawa Vituo vyao vya kazi vitatangazwa.
Wote wanatarajiwa kuapishwa kesho saa nane mchana.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMIS 26.10.2017

Benki za TPB na Mwalimu Commercial Bank zasaini makubaliano

$
0
0
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi (wa pili kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank (MCB),Ronald Manongi, wakibadilishana hati za makubaliano jijini Dar es Salaam leo ambapo wateja wa benki ya upande mmoja wataweza kupata huduma za kibenki katika matawi ya  benki ya upande mwingine. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi ( kushoto waliokaa) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank (MCB),Ronald Manongi, wakisaini hati za makubaliano jijini Dar es Salaam leo ambapo wateja wa benki ya upande mmoja wataweza kupata huduma za kibenki katika matawi ya  benki ya upande mwingine. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TPB na Mwalimu Commercial Bank (MCB), ambapo wateja wa benki ya upande mmoja wataweza kupata huduma za kibenki katika matawi ya  benki ya upande mwingine. Kushoto kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Mwalimu,  Ronald Manongi .
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank (MCB),  Ronald Manongi (kulia),  akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya MCB na Benki ya TBP ambapo wateja wa benki ya upande mmoja wataweza kupata huduma za kibenki katika matawi ya  benki ya upande mwingine. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi (wa tano kushoto) akishikana mikono na  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank (MCB),Ronald Manongi mara baada ya kumalizika kwa tukio la utiaji saini makubaliano hayo. Pamoja nao ni baadhi ya maofisa wa benki za TPB na MCB. 

IDHAA YA KISWAHILI YA DW YAANDAA MDAHALO MKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM IJUMAA HII

MAGAZETI YA IJUMAA LEO OKTOBA 27,2017


WANAFUNZI 11,481 WAPATA MIKOPO AWAMU YA PILI 2017-2018

$
0
0
Kiasi cha shilingi bilioni 72.2 mpaka sasa kimetolewa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 21,677 kati ya wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza waliopangwa kupatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 108.8 kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul-Razaq Badru imesema kuwa idadi ya wanafunzi waliobaki wapatao 8,323 watapangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 36.6 katika awamu inayofuata ili kukamilisha idadi iliyopangwa.

Idadi ya wanafunzi 21,677 waliokwishapangiwa mikopo na ambao wamedahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu vinavyotambulika; ni asilimia 72.2 ya wanafunzi 30,000 wanaotarajiwa kunufaika na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Orodha ya majina ya wanafunzi hao 21,677 inapatikana kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz  na itatumwa kwenye vyuo husika kwa ajili ya hatua zaidi za kukamilisha malipo ya mikopo.

Wakati huo huo, Bodi imeendelea kutoa mikopo kwa ajili ya wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo na ambao wamefaulu masomo yao ya mwaka wa masomo 2016/2017.

Jumla wanafunzi 54,936 wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu wamepatiwa mikopo mpaka sasa na taarifa zao kuwasilishwa kwenye vyuo husika.

Bodi inatarajia kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi 123,295 kwa mwaka wa masomo 2017/2018 wakiwemo wa mwaka wa kwanza 30,000 na wanaoendelea na masomo wapatao 93,295.

Bodi ya Mikopo inawasisitizia waombaji wa mikopo kuendelea kuwa na subira wakati ikikamilisha orodha inayofuata ya wanafunzi waliopata mikopo na itaendelea kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na tovuti ya Bodi mara kwa mara.

Takukuru kuhakiki matumizi STAMIGOLD – Kairuki

$
0
0
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati) akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja Uchenjuaji kutoka Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo, Joseph Kamishina (kulia mbele) katika ziara hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

Na Greyson Mwase, Geita

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ameitaka Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwasilisha taarifa zote za gharama za uendeshaji wa Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo ili kujiridhisha pamoja na kuchukua hatua za kisheria iwapo kama kuna taratibu za manunuzi zimekiukwa.

Kairuki ameyasema hayo leo tarehe 27 Oktoba, 2017 alipofanya ziara katika mgodi huo uliopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera lengo likiwa ni kufahamu shughuli za migodi ya serikali, binafsi na wachimbaji wadogo.

Alisema kuwa gharama za uendeshaji wa shughuli za mgodi huo zimekuwa ni kubwa mno pamoja na madeni hali inayopelekea shirika hilo kujiendesha kwa hasara badala ya kujiendesha kwa faida.
Kaimu Meneja Uchenjuaji kutoka Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo, Joseph Kamishina (katikati mbele) akimwongoza Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ( wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kulia) kuelekea kwenye eneo la uchenjuaji katika mgodi huo.

Aliendelea kusema kuwa STAMIGOLD imekuwa ikitumia gharama kubwa sana katika uendeshaji wa shughuli zake kwa kutumia mashine za kukodi na kutaka watendaji wa mgodi huo kuwa wabunifu kwa kuibua mikakati mipya kupunguza matumizi na kuzalisha faida kubwa ili hatimaye waweze kutumia vifaa vyake badala ya kukodi.

“ Ukiangalia gharama inayotumika kukodi mashine za uchorongaji na uchimbaji madini na nyinginezo utabaini kubwa sana ambapo kama STAMIGOLD ingejipanga ingekuwa na uwezo kabisa wa kununa mashine na mitambo yake yenyewe na kuepuka gharama kubwa za kukodi.
Kaimu Meneja Uchenjuaji kutoka Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo, Joseph Kamishina(katikati) akielezea shughuli za uchenjuaji madini zinavyofanyika kwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) katika ziara hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

Aidha, Waziri Kairuki alielekeza Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kushirikiana na menejimenti ya Mgodi wa STAMIGOLD kuwasilisha mpango wa kibiashara wenye kuainisha gharama za uzalishaji, mapato na faida.

“ Tunataka kuanzia sasa STAMIGOLD uwe ni mgodi wa mfano wenye kuzalisha kwa faida Tanzania, badala ya kufanya kazi kwa mazoea,” alisema Kairuki. Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki aliutaka Mgodi wa STAMIGOLD kutumia Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kwenye tafiti zake za madini kwa kuwa wakala huo una wataalam na maabara za kutosha.

Alieleza kuwa kutokana na wakala huo kuwa na uzoefu katika utafiti wa madini ni muhimu kwa Mgodi wa STAMIGOLD kushirikiana nao kwenye utafiti wa madini kama njia mojawapo ya kuboresha tafiti zake.
Kutoka kushoto mbele ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Balozi Alexander Muganda, Waziri wa Madini, Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde wakiendelea na ziara katika eneo la Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo.

Naye Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo aliitaka STAMIGOLD kuwa wabunifu kwa kufanya utafiti na kubaini maeneo yenye mashapo ya madini ya dhahabu ili kuwa na miradi endelevu ya uchimbaji madini Alisema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa sekta ya madini inakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi, hivyo inaanza na usimamizi wa karibu kwa migodi yote inayosimamiwa na serikali, binafsi na wachimbaji wadogo na kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazojitokeza.

WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE

$
0
0
Watafiti, Dk.Beatrice Lyimo (wa tano kushoto) na Bestina Daniel (wa pili kulia), kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),wakiwakabidhi mbegu bora ya mihogo Wanakikundi cha Chapakazi katika Kijiji cha Kalebezo wilayani Biharamulo mkoani Kagera jana, kwa ajili ya kuanzisha shamba darasa wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani humo. 

Na Dotto Mwaibale, Biharamulo Kagera.

WAKULIMA wilayani Biharamulo mkoani Kagera wameipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kwa kuwapelekea mbegu bora ya migomba,mihogo na viazi lishe ambayo itapandwa katika mashamba darasa na kusambazwa kwa wakulima wengine katika wilaya hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala wakati wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu ya mhogo kwenye shamba darasa katika Kijiji Kalebezo wilayani humo.
Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala (kulia), akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu ya mhogo kwenye shamba darasa katika Kijiji Kalebezo wilayani humo.

"Kwa niaba ya Ofisa Kilimo wa wilaya napenda kuishukuru COSTECH kwa kutuletea mbegu hizo katika wilaya yetu hasa baada ya kuona changamoto tuliyokuwa tukikabiliana nayo ya magonjwa ya mihogo kama batobato" alisema Ngawagala.

Ngawagala alisema msaada huo hautapotea bure kwani watahakikisha wanayahudumia vizuri mashamba darasa hayo likiwemo la mihogo lililopo katika Kijiji Kalebezo na lile la viazi lishe lililopo Kijiji cha Msenyi ambayo yamezinduliwa na kuhudhuriwa na wakulima kutoka vikundi vya Chapakazi katika Kijiji cha Kalebezo na Chapajembe cha Kijiji cha Msenyi vyote vya wilaya hiyo.

Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Chapakazi, Thadeo Kibuka alisema mbegu hiyo waliyoletewa itakuwa mkombozi wao kwani kwa muda mrefu walikuwa na changamoto ya kupata mazao yenye magonjwa kutokana na kukosa mbegu bora na ukame.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapakazi, Thadeo Kibuka akizungumza katika uzinduzi huo.

"Tutahakikisha shamba ili tunalo lizindua leo hii kwa msaada wa COSTECH na OFAB linakuwa la mfano wa kuzalisha mbegu bora katika wilaya hii" alisema Kibuka.

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Mtafiti Dk. Beatrice Lyimo alisema COSTECH kwa kushirikiana na OFAB wanaendesha mradi huo ili kuhakikisha kuhakikisha matokeo mazuri ya kazi za tafiti yanawafikia wakulima na kupata chakula cha kutosha.

Alisema COSTECH ndio mshauri mkubwa wa serikali katika masuala ya kilimo cha kitafiti hivyo wanakila sababu ya kuhakikisha tafiti zinazofanyika nchini zikiwafikia walengwa ili waweze kufanya vizuri katika kilimo.
Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel, akizungumza.

Dk. Lyimo aliwataka wakulima hao kwa kushirikiana na maofisa ugani kuyatunza mashamba darasa hayo ili kupata mbegu nyingi za mazao hayo na kuzisambaza kwa wakulima wengine.

BASHE AGAWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU KWA WAZEE JIMBONI KWAKE

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini ​Mhe. Hussein Mohammed Bashe​ amekabidhi Vitambulisho vya Matibabu ya Bure kwa wazee ndani ya Jimbo la Nzega Mjini.

Katika awamu hii ya kwanza zaidi ya wazee 1,080 watapata  Vitambulisho huku wazee 540 ndio wamekabidhiwa leo hii na wengine wataendelea kupokea kutoka katika Ofisi ya Mbunge kwa muda wa wiki nzima huku matarajio yakiwa ni kuwafikia wazee 3,284 katika jimbo zima.

Aidha, sherehe hizo zimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega ​Mhe. Godfrey Ngupula​ ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi.

​Mhe. Ngupula​ amepongeza jitihada za ​Mheshimiwa Bashe​ katika shughuli za maendeleo na kuwatumikia wananchi na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Mhe. Bashe alipohojiwa alisema ya kuwa ..."wazee hawa wameitumikia nchi hii kwa muda mrefu ni jukumu letu sasa kama vijana na taifa kuhakikisha nasi tunawalipa sehemu ya nguvu kubwa walizotumia kuifikisha Tanzania hapa ilipo leo kwa kuwapatia Matibabu bora na kuwaondolea gharama za Matibabu ili kuleta unafuu wa maisha"
"Nilichokifanya ni kugharamia fedha zote za Vitambulisho ili kuhakikisha kila mzee ndani ya Jimbo la Nzega Mjini anapata kitambulisho cha matibabu ya Bure".... Hussein Bashe.

Jimbo la Nzega Mjini ni jimbo pekee ndani ya Halmashauri ya Mji wa Nzega hivyo tukio hili linaifanya Halmashauri hii kuwa moja kati ya Halmashauri chache kitaifa kutekeleza kwa vitendo Sera ya Taifa Matibabu ya Bure kwa wazee.

RC MAKONDA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA SHOWROOM ZA MAGARI KIGAMBONI

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni , Hashim Mgandilwa, vinongonzi mbalimbali  wakiangaria ramani ya eneo maalumu lililotengwa Kigamboni kwa ajili ya Showroom zote za Magari jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda jana alitembelea na kukagua Maendeleo ya ujenzi wa miundombinu  kwaajili ya Showroom zote za Magari kwenye eneo Maalumu lililotengwa Kigamboni.

RC Makonda ameongozana na viongozi wa Taasisi mbalimbali ikiwemo TRA, SUMATRA, NSSF, Bank ya watu wa Zanzibar pamoja na Jeshi la Polis na Jeshi la Zimamoto na uokoaji ambao wameenda kuonyeshwa maeneo yaliyotengwa kwaajili ya Ujenzi wa Ofisi.


Makonda amesema kuwa lengo kuhamishia Showroom Kigamboni ni kufanya Kigamboni kuwa soko la Magari Africa, kuwapa Wananchi fursa ya kuchagua gari analotaka kwenye  eneo moja, kuiwezesha Serikali kupata mapato na kupunguza wizi wa magari.


Akiwa kwenye eneo hilo ameshuhudia ujenzi wa miundombinu ya Barabara, Madaraja, Umeme na Maji ikienda kwa kasi kubwa.

Tayari baadhi ya Taasisi na wenye Showroom waliokabidhiwa maeneo wameanza kujenga ili kuhakikisha ifikapo January Mosi wanakuwa wamehamisha Showroom zao.

Ndani ya eneo hilo kutakuwa na ofisi za Taasisi zote zinazohusiana na biashara ya Magari ikiwemo TRA, TPA, SUMATRA, Bank, NSSF,Bima, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na uokoaji, Garage, Sheli na Wauzaji wa Vipuri vya Magari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda  pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa,viongonzi mbalimbali  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu  katika eneo maalumu lililotengwa  kwaajili ya Showroom zote za Magari.(Picha na Emmanuel Massaka,Glob ya jamii)
Viewing all 110010 articles
Browse latest View live




Latest Images