Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1979 | 1980 | (Page 1981) | 1982 | 1983 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Moja wa maafisa wa Benki ya Dunia,ambaye pia huratibu shughuli za TASAF (TTL) katika benki hiyo , bw. Muderis Mohamed (aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo na serikali mjini Dar es salaam.
   Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano wa TASAF ,Bi. Zuhura Mdungi (aliyesimama) akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- PSSN- kwenye mkutano wa wadau na serikali kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF ,mjini Dar es salaam.

   Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa maendeleo, serikali na watumishi wa TASAF –wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo kupata maelezo ya hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini kabla ya kuanza ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali nchini kukutana na walengwa na viongozi.


  Na Estom Sanga-TASAF
  Baadhi ya watendaji wa Serikali na Wadau wa Maendeleo wanaanza ziara katika maeneo mbalimbali ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- kukutana na walengwa wa Mpango huo na kuona mafanikio na changamoto za utekelezaji wake.

  Akitoa maelezo kabla ya kuanza kwa ziara hizo zitakazofanyika katika mikoa ya Ruvuma, Njombe, Kigoma, Tabora, Singida, Kilimanjaro ,Morogoro na Zanzibar ,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga ameishukuru serikali na wadau wa maendeleo kwa mchango mkubwa wa kufanikisha shughuli za Mpango huo unaohudumia zaidi ya kaya masikini MILIONI MOJA na Laki MOJA nchini kote.

  Hata hivyo Bwana Mwamanga amesema licha ya kuweko kwa mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Mpango, bado kuna asilimia 30 ya vijiji nchini ambavyo havijafikiwa na huduma za Mpango jambo linaloendelea kulalamikiwa na wananchi ambao hawajafikiwa na Mpango huo na hivyo amesema serikali kupitia TASAF inalifanyia kazi kwa karibu suala hilo.

  Aidha katika maelezo ya utekelezaji wa Mpango huo yaliyowasilishwa na Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano wa TASAF,Bi. Zuhura Mdungi imeonyeshwa kumekuwa na mafanikio katika kubadili fikra na za kaya za walengwa katika kupambana na umasikini kwa kutumia huduma za Mpango huo mkubwa kupata kutekelezwa nchini .

  Shughuli za ziara na majadiliano kati ya serikali,wadau wa maendeleo na maafisa wa TASAF hufanyika kila baada ya miezi sita kuona namna utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unavyoendelea kwa kukutana na walengwa ,viongozi,wataalam na kuwasikiliza namna huduma za Mpango huo zinavyosaidia jitihada za serikali za kupunguza adha ya umaskini kwa wananchi.

  0 0

  Msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu (aliyeshika kichwa) akiwa katika Mahakama kuu anakosomewa kesi yake ya kuua bila kukusudia.

   Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeamuru askari Polisi aliyechukua maelezo ya mke wa Dk. Wilbroad  Slaa, Josephine Mushumbus ambaye alipaswa kuwa shahidi wa pili wa upande wa  utetezi katika kesi ya mauaji bila kukusudia inayomkabili msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu kufika mahakamani hapo kesho kwa ajili ya utetezi.

  Jaji Sam Rumanyika amesema hayo mapema leo October 24, wakati kesi hiyo ya mauji ya 'Lulu' dhidi ya msanii mwenzake, marehemu Steven Kanumba ilipokuja kwa ajili ya kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi.

   Jaji Rumanyika ametoa uamuzi huo, baada ya Wakili wa utetezi, Peter Kibatala kudai kuwa jitihada za kumpata Josephine Mshumbusi (mke wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema), zimeshindikana kwa kuwa yupo nje ya nchi na kuomba kusoma na kuyatoa maelezo hayo ili mahakama iyatumie kama kielelezo cha upande wa utetezi.

  Wakili wa Serikali, Faraja George alipinga vikali maelezo hayo kusomwa na kutolewa na Kibatala akieleza kwamba Kibatala anazifahamu sheria hivyo alitegemea kwa kuwa aliyetoa maelezo polisi hapatikani, basi angeletwa askari aliyeandika maelezo hayo ili aweze kutoa taarifa hiyo.

  Amedai kuwa Kibatala hana mamlaka ya kutoa taarifa hiyo wala kusoma kwani hawezi kuvaa kofia mbili kwa wakati mmoja, badala yake atabaki kumuwakilisha mteja wake hivyo afuate taratibu zilizowekwa.
  Akitoa uamuzi huo, Jaji Rumanyika amesema swali la msingi ni nani atakayeitoa taarifa hiyo mahakamani kati ya wakili na aliyeandika maelezo.

  "Kupatikana kwa shahidi imekuwa ngumu lakini anayepaswa kutoa maelezo hayo ni yule ambaye imeshindikana kufika mahakamani hapo na mwengine anayetakiwa kutoa maelezo hayo ni askari Polisi namba E 103 Nyangea. Hivyo, askari huyu anatakiwa kuja kesho kutoa maelezo na hati ya wito apatiwe," alisema Jaji Rumanyika.

  Katika kesi ya msingi namba 125 ya mwaka 2012, inadaiwa kuwa Aprili 7,  2012 Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, Lulu alimuua Msanii wa filamu, Steven Kanumba bila kukusudia.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. HAB Mkwizu (kulia) akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) alipofanya ziara katika Kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji TSN Dkt. Jim Yonazi
   Mhariri wa gazeti la Daily News Bw. Leonard Mwakalebela (kushoto) akimwelezea Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) namna habari zinavopitiwa na kupangwa katika gazeti hilo alipofanya ziara katika kampuni ya TSN jana Jijini Dar es Salaam
   Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (watano kushoto) katika picha ya pamoja na menejimenti ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) alipofanya ziara katika kampuni hiyo na kuangali shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam
   Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akimsikiliza mkuu wa TBC International Bw. Deogratius Salufu (kulia) alipotembela studio za redio hiyo jana wakati wa ziara yake katika Shirika la Utangazani la Taifa (TBC) Jijini Dar es Salaam
   Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akiwa katika meza ya kusomea taarifa ya habari ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) jana wakati wa ziara yake katika TBC Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba
  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (watatu kushoto) katika picha ya pamoja na menejimenti ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) jana wakati wa ziara yake TBC Jijini Dar es   Salaam. Watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu TBC Dkt. Ayoub Rioba. Picha na:Genofeva Matemu - WHUSM. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

   Afisa forodha msaidizi wa TRA, akitoka katika mahaka ya hakimu mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabiri ya kimiliki mali nyingi kuliko kipato chake.
  Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii.

  Afisa Forodha msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi leo October 24, 2017 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kukutwa akimiliki mali isiyolingana na kipato chake halali ambapo ni magari 19 ya aina tofauti.

  Mshtakiwa huyo ameshtakiwa chini ya kifungu cha 27, (1) (a) na (b) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007. Jennifer amesomewa hati ya mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter  mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shaidi wa mahakama hiyo.

  Wakili Peter akisoma hati ya mashtaka amedai, kati ya Machi 21 na Juni 30 mwaka jana, jijini Dar es Salaam mshtakiwa Jennifer akiwa  ameajiriwa na TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akimili magari 19 ya aina mbali mbali

  Magari hayo yalitajwa kuwa ni, Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck, Toyota Viz, Suzuki Carry, Toyota Ipsum, Toyota Wish, Toyota Mark II, Toyota RAV4, Toyota Wish na  Toyota Mark X.

  Mengine ni Toyota Regiusage, Toyota Estimated, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown,  Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Passo na Suzuki Carry ambapo yote yanathamani ya Sh 197, 601, 207/- Mali ambayo hailingani na kipato chake halali.

  Katika shtaka la pili imedaiwa, kati ya Machi  21 ,2012 na  Machi 30, mwaka jana jijini Dar es Salaam, Jennifer alikutwa akiishi maisha ya kifahari  yenye thamani ya Sh 333,255,556.24/- fedha ambayo hailingani na Kipato chake halali.

  Mshtakiwa amekana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na mdhamini mmoja atakayeweka bondi ya milioni 20.

  Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo umekamilika. Imeahirishwa hadi Novemba 7 kwa ajili ya kusikilizwa maelezo ya awali.

  0 0


  0 0


  Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 24 ambao watacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Benini mapema mwezi ujao.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 24 ambao watacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa mapema mwezi ujao.

  Baada ya kucheza nyumbani mfululizo mechi za kirafiki za kimataifa, Taifa Stars sasa itatoka mwezi ujao kwenda Benin kucheza na wenyeji Novemba 11, mwaka huu.

  Mayanga ameita kikosi cha wachezaji 24 ambacho kitaingia kambini Novemba 5 mjini Dar es Salaam kabla ya kusafiri Novemba 9 kwenda Benin tayari kwa mchezo huo na amewarejesha kikosini kiungo Farid Mussa na mshambuliaji, Elias Maguri kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki .

  Katika kikosi hicho amewaorodhesha Maguri aliyekuwa anacheza Oman na Farid Mussa anayecheza Tenerife B ya Hispania, ambao wote hakuwaita kwenye mchezo uliopita dhidi ya Malawi, uliomalizika kwa sare ya 1-1 Oktoba 7, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

  Kikosi kamili cha Taifa Stars kilichotajwa leo kinaundwa na makipaAishi Manula (Simba SC), Peter Manyika (Singida United) na Ramadhani Kabwili, mabeki Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afruka Kusini), Gardiel Michael (Yanga), Kevin Yondan (Yanga), Nurdin Chona (Prisons), Erasto Nyoni (Simba) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).

  Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba), Raphael Daudi (Yanga), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba), Ibrahim Hajib (Yanga), Mohammed Issa (Mtibwa), Farid Mussa (Tenerife/Hispania) na Abdul Mohammed (Tusker/Kenya) na washambuliaji Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Mbaraka Yussuf (Azam FC), Elias Maguri (Huru) na Yohanna Nkomola (Huru).

  0 0

   Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti  akizungumza na Waandishi wa habari mara baada Puma Energy Tanzania yatiliana sahihi mkataba wa hiari pamoja na chama cha wafanyakazi TUICO
    Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti  Akitiliana Saini na Kiongozi wa TUICO, Jonathan Peres huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuuu, Sera, Bunge, kazi, Vijana, ajira na Walemavu, Jenister Mhagama akishuhudia.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuuu, Sera, Bunge, kazi, Vijana, ajira na Walemavu, Jenister Mhagama akizungumza wa wakati wa kushuhudia zoezi la utiaji saini Mkataba wa hiari kati ya Puma Energy Tanzania na Chama cha Wafanyakazi (TUICO).
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


  0 0

   Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI Mhe.Tixon Nzunda  akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa unaofanyika  katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa unaofanyika  katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma.
   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongela wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa na Taasisi ya Uongozi Institute wanaoendesha  warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inayofanyika katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma.
   Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI Dk Zainabu  Chaula(kushoto mwenye miwani) pamoja na washiriki wengine wa warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(hayupo pichani) leo mkoani Dodoma.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Ndugu Alvaro Rodriguez mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Karimjee kwenye sherehe za kutimiza miaka 72 ya Umoja wa Mataifa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride maalum katika sherehe ya Siku ya Umoja wa Mataifa ambapo Umoja huo umetimiza miaka 72 tangu kuanzishwa kwake na sherehe hizo zilifanyika kwenye viwanja vya Karimjee kwenye sherehe za kutimiza miaka 72 ya Umoja wa Mataifa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye sherehe ya siku ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

  0 0

  Na  Mwandishi wetu.
  Mashindano ya kumsaka mrembo wa Kiss Universe Tanzania  yamepangwa kufanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa  Makumbusho ya Taifa jijini.
  Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 10 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa mujibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Tsehai Sarungi.

  Maria amewataja mabondia hao kuwa ni Lilian Maraule , Glory Gideon, Melody Tryphone, Anitha Mlay, Silvia Mkomwa, Rogathe Ally, Prisca Dastan ambao wote wanatoka Dar es Salaam.

  Warembo wengine ni Maureen Foster na Mary Peter wanaotoka Mwanza wakati anayetoka mkoa wa Mbeya Zahra Abdul.

  Alisema kuwa warembo hao watakuwa chini ya Miss Universe namba mbili wa mwaka jana, Lilian Loth katika kambi ya mashindano hayo yaliyodhaminiwa na SeaCliff Court Residence, Diana Magese, MnM, Kasakana na Bonuzi.

  “Maandalizi ya mashindano  hayo yamekamilika na wapenzi wa masuala ya urembo watapata burudani safi kutoka kwa  DDI Dance, poetry group (Romantic), A beautiful song kutoka kwa Jeff  Mduma,” alisema Maria.
  Alifafanua kuwa wamedhamilia kumpata mrembo bora ambaye atarejesha heshima ya mashindano hayo kama ilivyokuwa kwa Flaviana Matata ambaye alimaliza katika nafasi tano bora nchini Mexico mwaka 2007.

  “Tumefanya uchaguzi wa warembo vizuri na wengi ni bora, kwa sasa tunawafundisha masuala mbalimbali ya urembo, lengo ni kuwafanya wawe bora, wote ni washindi, lakini tunahitaji mshindi mmoja ambaye ataliwakilisha Taifa katika mashindano ya Kimataifa,” alisema.

  Alisema kuwa mashindano hayo pia yatamtoa mshindi wa taji la Miss Earth Tanzania na mshindi wa taji la Miss Tourism Queen International wa Tanzania.

  Miss Universe wakijipodoa katika kambi yao ya SeaCliff Residence iliyopo Masaki jijini.

  0 0


  0 0

  Na Frank Mvungi-MAELEZO, Dodoma.

  Serikali imetoa takribani Shilingi Bilioni 21 kwa ajili ya kuboresha shule 85 za Kata hapa nchini ili ziwe na Kidato cha Tano na Sita hali itakayoongeza ubora wa kiwango cha elimu na kuimarishwa kwa miundombinu.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Selemani Jafo wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) siku za Jumatatu na Alhamisi.

  Akifafanua Waziri Jafo amesema kuwa dhamira ya Serikalini katika kuboresha sekta ya elimu ambapo kila mwezi imekuwa ikitoa takribani Bilioni 23 zinazotumika kugharimia elimu bure hali inayochochea kuongezeka kwa wanafunzi wanaojiunga katika shule za msingi na Sekondari .

  “Tumejenga madarasa mengi na vyoo vingi ili kuendana na kasi ya udahili wa wanafunzi na pia tutahakikisha kuwa kuna kuwa na uwiano katika mgawanyo wa walimu katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Aliongeza kuwa Serikali katika kuboresha huduma za Afya imeshapeleka fedha katika vituo 172 kote nchini ili kuboresha huduma zinazotolewa na pia watumishi katika sekta hiyo wataajiriwa kwa kuzingatia mahitaji kutokana na nafasi zilizoachwa wazi baada ya zoezi la ukaguzi wa vyeti feki.

  Aidha Waziri Jafo aliwataka Viongozi wote katika Mikoa na Halmashauri kusimamia vizuri miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao ili thamani halisi ya fedha zilizowekezwa ionekane. “Nawasihi watanzania walipe kodi kwa kuwa fedha zinazotokana na kodi ndizo zinazotumika kutekeleza miradi ya maendeleo na ni matumaini yangu kuwa maelekezo niliyotoa kwa wakurugenzi kuhusu ukusanyaji wa mapato yatazingatiwa na watasimamia kazi hiyo vyema na kubuni vyanzo vipya vya mapato”Alisisitiza Jafo.

  Aidha Waziri Jafo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kuwa hadi sasa watumishi zaidi ya 300 wameshachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu kwa kushindwa kutimiza wajibu wao.

  Kwa upande wa sekta ya Viwanda amebainisha kuwa wamejipanga vyema kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kutenga maeneo maalum ya uwekezaji katika Halamashauri na Mikoa.

  0 0

  Baadhi ya waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari zikiwemo Televisheni na Magazeti Jana walitembelea vituo vya Usajili mkoa wa Arusha kuona hatua za usajili na mwitikio wa wananchi katika kupata haki yao msingi ya kikatiba ya kusajiliwa.

  Wananchi wa Mkoa wa Arusha wameendelea kujitokeza kwa wingi kujisajili Vitambulisho vya Taifa; huku idadi ya Kata za Usajili zikiongezeka. Moja ya Kata iliyoanza Usajili jana kwa upande wa Wilaya ya Arusha mjini inaendelea kuwasajili wananchi katika Kata ya Themi, Sekei, Sombetini na wameongeza Kata nyingine ya Sinoni.

  Wilaya ya Monduli inakamilisha usajili kwenye Kata za Monduli Mjini, Monduli Juu na Engutoto; ikijipanga kuendelea na Kata za Lashaine, Sepeko, Meserani na Mfereji. Kwa Upande wa Arumeru Kata zinazofanya Usajili ni Musa, Ambureni, Leburuki, Imbasenyi na Ngabobo, Longido ni Kata za Olubomba, Namanga na Kimokoa na wanajiandaa na Kata za Kamwanga, Tingatinga, Olumorodi na Sinya. Karatu wanaendelea na Usajili kwenye Kata ya Karatu na Rhotia kabla ya kuhamia Ganako. Wilaya ya Ngorongoro wameanza na Tarafa ya Ngorongoro kabla ya kuanza Mitijo.

  Uongozi wa Mkoa umejizatiti kuhakikisha wananchi wote wanasajiliwa kwa wakati na kupata Vitambulisho vya Taifa vitakavyowawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali pamoja na upatikanaji kirahisi wa huduma za kijamii.
  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (NIDA) Bi. Rose Joseph (mwenye miwani) akizungumza na baadhi ya waandishi wa Vyombo vya Habari vya Televisheni na Magazeti walipotembelea kituo cha usajili cha Sombetini, Arusha mjini kuangalia shughuli za kuwasajili wananchi zinazoendelea kituoni hapo.
  Wananchi wakiendelea kupata huduma za usajili kabla ya kupigwa picha kama wanavyoonekana pichani. Wananchi hao ambao ni kutoka Kata ya Sombetini wamekuwa wakijaziwa fomu na kugongewa mihuri na wenyeviti kwenye mitaa wanayoishi kabla ya kusajiliwa kwenye mfumo wa NIDA.
  Mwenyekiti wa mojawapo ya mitaa ya Kata ya Sombetini (mwenye kofia) akigonga mhuri kwenye fomu ya mwananchi kuthibitisha kumtabua, na mkazi wa eneo lake.
  Akina mama pamoja na jukumu la malezi wamejitokeza kusajiliwa kama anavyoonekana pichani mmoja wa akinamama wa Kata ya Sinoni akiwa amembeba mtoto wake mkono mmoja na mkono mwingine akiwa anaendelea na hatua za usajiliwa.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki (tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo uliomtembelea ofisini kwake mapema leo .Picha na Ahmad Michuzi-China.
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies  ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Mohamed Kiluwa (pichani kulia) pamoja na viongozi Waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani wakiongozwa na Katibu Tawala mkoa wa Pwani Zuberi Semataba, mapema leo kwenye Ofisi za Ubalozi huo,Ujumbe huo umewasili mjini Beijing,nchini China kushiriki Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda linalotarajiwa kufanyika mjini humo kesho Oktoba 25,2017 .

  Kongamano hilo kubwa lenye uhamasishaji mkubwa wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies na litawashirikisha wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao zaidi ya 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.

  Balozi Kairuki amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies  Mohamed Kiluwa kwa kuonesha juhudi kubwa za kuwahamasisha na kutafuta washirika mbalimbali katika suala zima la uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania.

  Balozi Kairuki amesema kuwa,Kampuni ya Kiluwa kwa kufanya hivyo  wanaibeba dhana ya Tanzania ya Viwanda kwa utekelezaji kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Viwanda,na kuongeza kuwa yuko tayari kutoa kutoa ushirikiano wa kutoka katika suala zima la kuwahamasisha wawekezaji kutoka nchini China na kwenda kuwekeza nchini tanzania katika suala zima la Viwanda.
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies, Mohamed Said Kiluwa (pichani kulia) pamoja na Muwakilishi wa baadhi ya viongozi waandamizi wa mkoa wa Pwani,Katibu Tawala mkoa wa Pwani Zuberi Semataba waliofika mjini Beijing,nchini China kushiriki Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda linalotarajiwa kufanyika mjini humo kesho Oktoba 25,2017, Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,litajumuisha wafanyashabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao zaidi ya 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.
  Katibu Tawala mkoa wa Pwani Zuberi Semataba akifafanua jambo mbele ya Balozi wa Tanzania nchini China,Mh. Mbelwa Kairuki mapema leo walipokwenda kumtembelea Ofisini kwake,pamoja na kupanga maandalizi ya Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda linalotarajia kufanyika mjini Beijing hapo kesho Oktoba 25,2017. Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies na kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Pwani,wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na makampuni mbalimbali.

  Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Naima Kiluwa akiandika kilichokuwa kikijiri kwenye mazungumzo hayo mafupi na Balozi Mh.Mbelwa Kairuki mara baada ya kuukaribisha ujumbe huo Ubalozini kwake na kuzungumza mambo mbalimbali yaliyohusu masuala ya uwekezaji kwa Tanzania,na baadae kupata chakula cha pamoja.
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi mmoja wa watakaoshiriki Kongamano la Viwanda linalotarajia kufanyika kesho mjini Beijing,likatalojumuisha Wamiliki wa Viwanda,Wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali wapatao zaidi ya 200,anaeshuhudia kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Semataba
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa 
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Naima Kiluwa 
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akiwatambulisha baadhi ya washirika wake mbele ya Balozi Kairuki (hayupo pichani),mapema leo mjini Beijing nchini China,wakiwa tayari kwa maandalizi ya Kongamano la Uwekezaji wa Viwanda linalotarajia kufanyika hapo kesho Octoba 25,2017 mjini humo.
  Rais wa wanafunzi wasomao nchini China,Hussein Mtoro akiukaribisha Ujumbe kutoka Serikali ya Mkoa wa Pwani ikiongozwa na Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Semataba pamoja na uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies ukiongozwa na Mohamed Said Kiluwa (njano),walipofika Ofisini kwa Balozi wa Tanzania nchini China,Mh Mbelwa Kairuki,mapema leo mchana .Picha na Ahmad Michuzi-China.

  0 0

   Askofu Mkuu wa  Jimbo Kuu  Katoliki  la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akiaga  mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa mara baada ya Misa iliyofanyika katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam.
    Askofu Mkuu wa  Jimbo Kuu  Katoliki Tabora, Paul Ruzoka akiaga  mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa mara baada ya Misa iliyofanyika katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.
    Katibu wa Rais, Ngusa Samike akiaga mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa mara baada ya Misa iliyofanyika katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Mapadri nao wakipita mbele kuaga mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na  Masasi Castor Paul Msemwa mara baada ya Misa katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0


  0 0

   Wafanyakazi wa Benki ya NBC Tawi la Samora wakipozi kwa picha ya pamoja wakiwa katika umbo la moyo ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na ukarimu kwa wateja wao kipindi hii benki yao ikiendelea kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja.
   Mteja wa Benki ya NBC, Neema Xibona (kulia) akionyesha furaha mbele ya wafanyakazi wa benki hiyo Tawi la Samora,  Dar es salaam ambapo sasa NBC inaendelea kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Wafanyakazi hao wanatumia muda wao kuwa karibu na wateja kusikiliza maoni yao kuhusu huduma na changamoto wazipatazo na kuzitafutia ufumbuzi.
   Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbagala, Sady Mwang’onda (kulia), akizungumza na mmoja wa wateja, Elias Kaaya alipofika katika tawi lake kupata huduma.
  Meneja wa NBC Tawi la Samora, Faustina Maeda, akimkaribisha Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi (kulia) alipotembelea katika tawi hilo kuangalia ubora wa huduma zinazotolewa kwa wateja na pia alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wateja. 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Frank Shija -MAELEZO
  Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ametoa wito kwa Kampuni na Taasisi mbalimbali nchini kujitokeza kusaidia tasnia ya sanaa ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.
  Wito huo ameutoa leo jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya utiaji saini makubailiano ya mradi wa utambuzi wa sanaa za ufundi na uchoraji (TACIP),mkataba uliosainiwa baina ya Kampuni ya Data Vision International na Shirikisho la sanaa za ufundi na uchoraji (Tafca).
  Naibu Waziri Shonza amesema kuwa mradi huo wa TACIP utasaidia kuwaletea maendeleo wasanii husika kwa kuwa watakuwa wanatambulika kisheria hivyo itakuwa rahisi kwao kupata fursa mbalimbali ndani na nje ya nchi.
  “Mradi huu utawezesha upatikanaji wa masoko ya uhakika ya kazi za sanaa kwani utawaleta wasanii wote pamoja, ambapo wataweza kujadiliana na kutatuaa kero zao kwa pamoja” alisema Mhe. Shonza.
  Aidha Mhe. Shonza alitumia fursa hiyo kuwaponge wabia wote wa mradi huo kwa ubunifu mkubwa waliouonyesha nakuwataka wasanii wa fani zingine waige mfano huo.
  Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi na Uchoraji Tanzania (Tafca) Adrian Nyangamale amesema kuwa mradi huu wa utambuzi wa sanaa za ufundi na uchiraji umekuja wakati muafaka jambo litakalosaidia kulete maendeleo katika tasnia hiyo.
  Amesema kuwa lengo kubwa la kubuni mradi huo ni kuhakikisha kuna kuwa na kanzi data ya wasanii wote wa sanaa za ufundi na uchoraji nchini ili waweze kutambuliwa na mamlaka husika.
  Naye Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Data Vision International William Kihula amesema kuwa kutokana na ukweli kuwa Kampuni yao inajihusisha na masula la ya ukusanyaji wa takwimu,utoaji wa vitambulisho wameona watoe mchango wao kwa tasnii ya sanaa kama jitihada zao za kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano iliyoahidi kupitia Ilani ya uchaguzi kuinua wasainii.
  Aliongeza kuwa Data Vision watahakikisha mradi huu wa Jitambue,Tambulika, Inalipa unafanikiwa kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau ambao ni wasanii wa sanaa za ufundi na uchoraji.
  Data Vision ni Kampuni inayijishugulisha na masuala ya ICT, UTAFITI, Vitanmmbulisho ambapo limekuwa likifanya kazi kwa karibu zaidi na Serikali kwa takribani miaka 20 sasa limeamua kugeukia sekta zisizo rasmi ili kuweza kutoa mchango wake.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza (aliyesimama katikati) akishuhudia Utiaji Saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Shirikisho la Sanaa za Ufundi (TAFCA) na Kampuni ya Data Vision International 24 Oktoba, 2017 Jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiongea na wadau wa Sanaa na Ufundi wakati wa Hafla ya Utiaji Saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Shirikisho la Sanaa za Ufundi (TAFCA) na Kampuni ya Data Vision International 24 Oktoba, 2017 Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sanaa za ufundi pamoja watendaji wa Kampuni ya Data Vision International mara baada ya kukamilisha Hafla ya Utiaji Saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Shirikisho la Sanaa za Ufundi (TAFCA) na Kampuni ya Data Vision International 24 Oktoba, 2017 Jijini Dar es Salaam. 
  PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM
  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1979 | 1980 | (Page 1981) | 1982 | 1983 | .... | 3353 | newer