Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live

Waziri Mwakyembe akutana na Viongozi wa Chama cha Mashua Tanzania (TSAA)

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo kwa baadhi ya viongozi wa Chama cha Mashua Tanzania (TSAA) wakati alipokutana na viongozi hao kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.
 Mwanyekiti wa Chama cha Mashua Tanzania (TSAA) Bw. Philemon Nasari (kushoto) akimueleza  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mashua Tanzania (TSAA) Bw. Philemon Nasari (kulia) akimkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe DVD yenye matukio mbalimbali ya chama hicho wakati alipokutana na viongozi hao kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (mwwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Mashua Tanzania (TSAA) na maafisa wa Idara ya Michezo wakati alipokutana na viongozi hao kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo. Picha na Eliphace Marwa – Maelezo


VIINGILIO MECHI YA YANGA NA SIMBA JUMAMOSI UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Young Africans na Simba utafanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam siku ya Jumamosi Oktoba 28, 2017 kama ilivyotangazwa awali. Hakuna mabadiliko.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) jioni hii, viingilio katika mchezo huo kwamba watazamaji watakaohitaji kukaa katika Jukwaa Kuu watalipia Sh 20,000 na Mzunguko ni Sh 10,000.

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA AfYA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja
 Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali katika   Wizara ya Afya   wakiwa katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
 Baadhi ya Maafisa  wa Idara mbali mbali katika ya Wizara ya Afya wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akifungua  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dk.Jamala Adam Taib (wa pili kulia) alipokuwa akisisitiza jambo wakati wa kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. Picha na IKULU

WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI ZANZIBAR WAPEWA TAALUMA JUU YA UTAFUTAJI MAFUTA NA GESI ASILIA

$
0
0
 Naibu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dr. Juma Mohammed Salum akiwakaribisha wahariri wa vyombo vya habari katika warsha ya siku mbili ya utafutaji Mafuta na Gesi Asilia inayofanyika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maji Nishati na Mazingira Mhe. Ali Khalil Mirza akifufungua warsha ya wahariri wa vyombo vya habari inayohusu utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar (kulia) Prof. Martin Mhando na kushoto Naibu Mkurugenzi Muendeshaji Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar Ali Said Bakar.


 Mshauri wa usalama na afya  kwenye mafuta na gesi asilia  Respicious Kundama akiwasilisha mada ya mahusiano ya jamii juu ya athari za mazingira wakati shughuli hizo zikiendelea.
  Mtaalamu wa utafutaji mafuta na gesi asilia kutoka kampuni ya Rakgas ya Rasil Khema Shari Hassan akielezea namna ya shughuli za utafutaji wa mafuta na gesiasilia utakavyofanyika kwa kutumia meli maalumu itakayowasili ijumaa ijayo.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo  Khatibu Suleiman akiuliza suala katika warsha hiyo inayofanyika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.

Wanawake jitokezeni kupima saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti - Waziri Ummy Mwalimu

$
0
0
Na Globu ya Jamii, Dar es Salaam

Wanawake wametakiwa  kujitokeza kwa wingi katika kupima saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti  ili kusaidia kupunguza ongezeko la ugonjwa huo na kutakiwa kuwahi mapema kupima kabla ya tatizo kuwa kubwa kwani saratani inaweza kutibika kwa gharama nafuu kabisa.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia,wazee, na watoto Ummy Mwalimu na kusema kuwa vituo vya afya vihakikishe vinatenga siku maalum kila mwezi kwa lengo la wanawake kupatiwa huduma ya upimaji wa saratani ya matiti pamoja na shingo ya kizazi na huduma hizi zinatolewa bila malipo ili kuhamasisha upimaji kwa wanawake hapa nchini.
"Wanawake wajitokeze kwa wingi katika kupima ili kujua afya zao na hii itasaidia kupunguza saratani ya matiti  pamoja na shingo ya kizazi kwa kina mama,kuliko kusubiri tatizo liwe kubwa kwani tatizo likiwa dogo saratani inatibika na kwa gharama ndogo kabisa kuliko kukaa na kusubiri kuwa kubwa ". Amesema 
Amesema katika kuboresha huduma hizo serikali imenunua mashine za kisasa kabisa 100 za tiba mgando,mashine 9 za upasuaji mdogo ambazo zitatumika kwa ajili ya matibabu ya awali ya saratani kwa wanawake pamoja na mitungi 173 ya gesi ya carbon dioxide zitakazowezesha mashine hizo kufanya kazi.
Aidha Waziri  ametoa onyo kwa waganga wa kienyeji wanaowarubuni watu  kuwa wana uwezo wa kutibu ugonjwa huo kutokana na miti shamba  na kuwataka kuachana na hio tabia Mara moja kwani dawa za asili hazitibu saratani ila zinatuliza tu.
" Hakuna dawa ya tiba asili inayotibu saratani waganga wa kienyeji waache tabia ya  kuwarubuni wananchi kuwa dawa hizo zinatibu saratani jambo ambalo siyo kweli ila dawa hiyo inapunguza tuu maumivu na kama kuna mtu anaudhibitisho kuwa inatibu alete ifanyiwe uchunguzi ili tubaini kama ni kweli inatibu". Amesema.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndungulile amesema kuwa katika kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje,Serikali ya awamu ya tano imeamua kuboresha huduma za afya hususani upande wa saratani ili kuweza kuhakikisha wagonjwa hao wanatibiwa hapa nchini.
"Ifahamike kuwa takribani wagonjwa wapya elfu 50 kila mwaka wanagundulika kuwa na saratani ,na idadi hii inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2020".Amesema.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia,wazee, na watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu ya Utaratibu wa utoaji wa matibabu ya Saratani bure kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine  Ndungulile  akifatilia kwa makini

Waziri  wa Afya Ummy  Mwalimu  pamoja na Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndungulile wakipokea vifaa ivyo vilivyotolewa kwa lengo la kufanya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti kwa wanawake nchini ambapo vifaa ivyo vitasambazwa katika vituo vya afya mbalimbali  vitakavyotoa huduma hizo

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 23.10.2017

MAGAZETI YA JUMANNE LEO OKTOBA 24,2017

MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 24, 2017


RWANDA CULTURAL NIGHT IN TANZANIA

TIME TO RE-THINK TEACHER EDUCATION

$
0
0
KAMPALA, OCTOBER 23RD 2017 The Aga Khan University (AKU), Institute for Educational Development in East Africa (IED, EA) has today began its second annual Education Conference under the theme: “Re-thinking Teacher Education”. The conference was officially opened by the State Minister for Higher Education in the Ugandan Cabinet, Hon. John Chrysestom Muyingo and will be running from today 23rd- 25th October 2017 at the Hotel Africana in Kampala.

Hon. John Muyingo applauded AKU’s commitment to the formation of strong and strategic leadership in the education and health sectors in Uganda. The State Minister said that it is important to make teacher education more attractive. “According to Uganda Vision 2014, presently guiding national policy document, Uganda has made tremendous progress in improving literacy levels of the citizenry. Literacy rate for persons aged ten years and above in the country is quoted to have increased from 69% in 2006 to 73% in 2010 and I would like to congratulate the government, development partners and all education stakeholders in Uganda for this great achievement”, he said.
From Left to Right: Mr. Amin Mawji- Country Representatitve for AKDN, State Minister for Higher Education in the Ugandan Cabinet John Chrysestom Muyingo, Vice Provost AKU- Kweku Bentil, Dr. Jane Egau Okou is the Commissioner for Teacher Instructor Education and Training in the Ministry of Education and Sports Uganda,Professor Joe Lugalla- Director IED-EA, Dr Marriote Ngwaru- Head of Research AKU-IED, Akim Okuni- Country Director Aga Khan Foundation, Bernard- Orimbo- Orimbo Project Director, SESEA Project Coordination Unit-AKF EA.

Hon. John Muyingo further said that “while Uganda has made some progress in terms of enrolment in the last two decades, these achievements have been overshadowed by a persistent decline in educational standards, particularly in public schools at both primary and post primary levels”. Independent studies notably by Uwezo (2010, 2012 and 2015) have consistently recognized the declining quality of education in Uganda. 

“I am very aware that government efforts alone are not enough to improve, innovate and change on teacher education in our country. The efforts on non-government actors are highly appreciated and recommended. I would like to take this opportunity to urge you to increase your efforts in working with the government to improve our education system”, he said.

Professor Joe Lugalla who is the Director IED, EA also said that as an Institution that is driven to produce impactful and quality interventions in education, IED, EA and ultimately AKU would immensely benefit from collaborative partnerships in matters relating to governance, security, religion and education.
State Minister for Higher Education in the Ugandan Cabinet discsusses the need to make the profession of teaching more attractive.

 “Delivering education is a universal principle requiring universal involvement and collaborations, and I strongly believe that we need to work together not only in formulating ideas on how to re-think teacher education in Uganda and East Africa as a whole, but in implementing them as well”, said Professor Lugalla.

The conference has been inspired by the need to interrogate the systems, policies, structures and reforms to drive sustainable teacher education for development of the East African community.

IED, EA’s work is embedded in informed inquiry to demonstrate effectiveness of pedagogies and professional practices in the delivery and promotion of educational services in East Africa. Working closely with education ministries of Tanzania, Kenya and Uganda, IED, EA aligns its activities with the respective national governments’ visions and development plans.
Dr. Jane Egau Okou is the Commissioner for Teacher Instructor Education and Training in the Ministry of Education and Sports Uganda discusses the State of Teacher Education in Uganda.

IED, EA seeks to improve the quality of education in East Africa by enhancing the efficiency and effectiveness of educational institutions; it does this through human resource development, institutional capacity building, outreach activities, research and dissemination, as well as policy analysis and advocacy. The provision of quality education in Uganda is crucial for the country to achieve the socio-economic development goals stipulated in Vision 2025 and achieve the 2030 Sustainable Development Goals (SDG).

In 2005, IED, EA began by offering Professional Development Courses. In 2007 IED EA began offering a Master of Education degree. The aim of IED-EA is to improve the quality of education in East African Countries. Since its establishment, IED, EA has so far trained 372 East African teachers through its Master of Education Degree Program of which 87 are from Uganda, 168 from Kenya, 100 from Tanzania, 12 from Zanzibar and 5 are from Brazil, Rwanda and Burundi.
IED-EA Teacher Education Conference 2017, “Re-thinking Teacher Educaiton” in Kampala Uganda.

These teachers have been trained in a variety of specialist pathways namely: Teacher Education, Educational Leadership and Management, Science in Education; Mathematics in Education; Language and Literacy, Early Childhood Education and Assessment, Measurement and Evaluation.

These graduates are currently working in different parts of East Africa and Africa at large as Education Directors, School principals, Primary and Secondary School Head Teachers/Masters and Deputy Head Teachers/Masters, Early years trainers, Principals of Teacher Training Colleges, Tutors and Education officers.

KUMBUKUMBU

$
0
0
Marehemu Dafrosa Sabinus Kweka 
1970 - 1999  

Ni miaka kumi na nane (18) sasa toka umerudi kwa baba. Ninapokosa maneno yako ya busara na hekima, ucheshi na ujasiri. Ninakukumbuka sana na kukuombea mimi mtoto wako wa pekee Jesca, pia unakumbukwa sana na mume wako mpendwa, Ibrahim Msengi, kaka zako Festo na Thade, dada zako Jane, Eugenia, Elizabeth na Cesilia pamoja na Mjukuu wako Dafrosa Michael Chenza. “Msijisumbue kwa neno lolote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, haja zenu zijulikane na Mungu.” Fil: 4:6

BODA BODA TABORA KUKABILIANA NA WACHAFUZI WA MAZINGIRA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT, RS-TABORA

VIJANA wanaondesha shughuli za usafirishaji wa  abiria kwa njia ya Pikipiki (Boda boda) mkoani Tabora wamepewa jukumu la kuhakikisha wanasimamia usafi kwa kuwakamata watu wenye tabia za kutupa takataka  ovyo katika maeneo mbalimbali  miji na hivyo kuhatarisha afya za watu wengine.

Jukumu hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kwenye  mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kanyenye wakati akiwahamasisha wananchi awamu ya pili zoezi la upandaji miti mingine na usafi wa mazingira. Alisema kuwa kuanzia sasa Boda boda watakuwa wanajukumu la kukamata watu watakaotupa taka taka za aina yoyote katika mitaa na kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi na kuwafikisha katika Halmashauri husika.

Mwanri alisema kila mtu atakayekamatwa kwa kutumia Sheria ndogo ndogo za eneo husika atalazimika kulipa silingi elfu 50 ambapo kati ya hizo mkamataji atalipwa shilingi elfu 25 zilizobaki zitakuwa mali ya Halmashauri husika.

“Ndugu zangu boda boda leo nawapa mpango mzuri wa kupata pesa ambao ni huu …ukimwano mtu katupa karatasi ya vocha kamata…ukimwona katupa gunzi kamata…chupa ya maji kamata na mpeleke Halmashauri kisha atalipa elfu 50 wewe watakupa elfu 25 mnaonaje mpango huo? Aliuza Mwanri .

Alisema kuwa haiwezekani Tabora ikaendelea kubaki nyuma katika suala la usafi na viongozi na wananchi wapo ni lazima watu wabadilike na waanze kuzingatia suala la usafi kwa ajili ya kulinda afya zao na jamii inayowazunguka. Alisema kuwa lengo la mpango huo ni kutaka kuhakikisha Mkoa mzima wa Tabora unaondokana na aibu ya kuwa na takataka zilizotupwa ovyo na hatime uwe Mkoa wa kwanza hapa nchini kwa kuzingatia usafi.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewaagiza viongozi wa Halmashauri zote kuhakikisha kuwa maduka yote yanayotoa huduma za kuuza vinywaji , vibanda vya vyakula na baa  ambazo hazina vyoo zinafungwa mara moja. Alisema kuwa hakikuta sehemu mtu anayeendesha biashara hiyo huku hana choo atalazimika kuwachukulia hatua viongozi husika ikiwemo kuwasimamisha kazi kwa kushindwa kusimamia majukumu yao ikiwemo kulinda afya za wananchi. Mwanri alisema kuwa inapotea tatizo la mlipuko wa magonjwa Serikali inaingia gharama kubwa kuhakikisha inaokoa maisha ya wananchi kwa hiyo ni vema kuchukua tahadhari mapema.

Alisema kuwa hawezi kuvumilia kuona watu wanaendelea kutoa huduma katika mazingira ambayo sio salama kwa kuwa analojukumu na dhamana ya kuhakikisha wakazi wote wa Tabora wanakuwa salama na afya bora. Mmoja wa Madreva wa Boda boda Bonos Binamungu apongeza hatua ya Mkuu wa Mkoa kuwakabidhi jukumu la kusimamia usafi na kuahidi kutekeleza jukumu hilo kwa misingi ya Sheria na taratibu bila kumwonea mtu.

Alisema kuwa kuondoa mikwaruzano ni vema wananchi wa Tabora wakaanza kutii sheria ikiwa ni pamoja na kutupa takataka katika maeneo husika ili kuepuka kupata hasara ya kulipa fedha ambazo hakutarajia.

Introducing Lameck Ditto's new hit "Nabembea"

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) latoa elimu ya shughuli zake kwa wadau wa biashara

$
0
0
 Mwakilishi wa kampuni ya Tansafrica Water System Bi. Imelder Kimambo akitoa maoni yake katika  semina ya wadau wa biashara katika ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) jijini Dar es Salaam jana.Lengo la semina hiyo ni kubadilishana mawazo na kuelekezana namna taratibu za viwango zinavyofanyika.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Profesa Egid Mubofu akisisitiza jambo kwenye semina ya wadau  wa biashara iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo  jijini Dar es Salaam jana ikiwa na lengo la kutoa elimu na taratibu mbalimbali kuhusiana  na bidhaa zinazozalishwa ndani na kuingizwa kutoka nje ya nchi.

TTCL yazindua huduma ya 4G mkoani Shinyanga

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainab Telack amezindua rasmi huduma ya TTCL 4G mkoani Shinyanga, na kuitaka kampuni kutoa huduma bora za uhakika na zenye gharama nafuu ambazo Wananchi wa kawaida watamudu.

Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika jana katika ofisi za TTCL, mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba, viongozi wa vyombo vya usalama, viongozi wa Mkoa na Wafanyakazi wa TTCL.

Akizungumza katika hafla hiyo, Telack ameitaka TTCL kuongeza ubunifu na juhudi katika kutoa huduma ili iweze kupambana na ushindani uliopo kwenye soko la mawasiliano. “Soko la huduma za Mawasiliano limepanuka sana hapa Nchini, Watoa huduma wapo wengi, ushindani mkali ambapo kila Kampuni inabuni mbinu za kujitanga ili kuvutia Wateja kwa ofa na zawadi mbalimbali.

"Tunataka TTCL yetu nayo ifanye hivyo, ishindane sokoni, iongoze kwa kuwajali Wateja na kutoa huduma bora za uhakika, zenye gharama nafuu ambazo Wananchi wa kawaida watamudu. Tunahitaji kuona sababu ya msingi ya kutoka huku tulipo na kurejea nyumbani TTCL” amesema Mkuu wa Mkoa Shinyanga.

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba amesema kuwa TTCL imekuja Shinyanga kuwapa suluhisho bora la Mawasiliano, huduma bora, gharama nafuu na za uhakika. 

“Tumewafuata Wafanyabiashara wa Madini na Vito vya thamani, tumewafuata Wafugaji wa mifugo aina zote, Wakulima wa Mazao yote ya chakula na biashara, Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa ngazi zote” amesema Bw. Waziri Waziri Kindamba.

Ameongeza kuwa TTCL imeleta huduma ya mawasiliano katika Mkoa wa Shinyanga ili kuongeza ufanisi washughuli za Viwanda, Elimu, Ulinzi na Usalama wa Wananchi kwa ujumla. “Tunataka tuyafikie Makundi yote haya na kuyawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi ili waweze kufikia ndoto na malengo yao pamoja na kuchangia Maendeleo ya Nchi yetu kupitia shughuli zao za kila siku hasa katika kupata taarifa za Masoko na Bei nzuri ya mazao yao. Amesema Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akitoa hotuba katika uzinduzi wa huduma ya TTCL 4G Mkoani humo katika hafla iliyofanyika Oktoba 23, 2017 katika ofisi za TTCL.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba pamoja na Meneja wa Mkoa wa Shinyanga-TTCL, Abdalah Lugage wakishika bango kuashiria uzinduzi wa huduma ya TTCL 4G Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TTCL katika uzinduzi wa huduma ya 4G Mkoani humo.


HOTUBA KAMILI YA RAIS MAGUFULI BAADA YA KUKABIDHI VYETI KWA WAJUMBE WA KAMATI ZA UCHUNGUZI WA MADINI

Balozi wa Tanzania nchini China Mh.Mbelwa Kairuki azunumza na viongozi na watendaji wa mkoa wa pwani jijini Beijing leo

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA ARDHI, MAJI, NISHATI NA MAZINGIRA ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe.Salama Aboud Twalib (katikati) akitoa maelezo katika kikao cha siku moja cha Uongozi wa Wizara hiyo katika Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wengine Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee (kulia) na Naibu Waziri Mhe.Juma Makungu Juma.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira wakiwa katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Nd,Ali Halil Mirza akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),akiwepo na Mshauri wa Rais masuala ya Ardhi na Ujenzi Mhe.Burhani Saadat Haji (kulia).

Ofisi ya Msajili wa NGOs Yasimamisha shughuli za Shirika la KBH Sisters

WAZIRI MPINA AWAAGA WATUMISHI WA NEMC

$
0
0
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akitia saini katika kitabu cha wageni kwenye Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC  alipokwenda kuagana nao na kutoa neno baada ya kufanya nao kazi kama Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara Mpya ya Mifugo na Uvuvi.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akizungumza wakati wa kuagana na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, kulia ni mkaguzi wa Mazingirakanda ya Mashariki Bw. Jafari Chimgege na kushoto ni Dkt. Ruth Rugisha Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Baraza.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na baadhi  ya viongozi katika Management ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC.
Waziri Mpina akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi wa watumishi wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC.
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live




Latest Images