Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

MASHINDANO YA WANAFUNZI WA SEKONDARI KWA MASWALA YA KODI YAFANA JIJINI DAR

0
0
Mamlaka ya mapato nchini (TRA) iliendesha na kudhamini shindano la shule za sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani jijini humo. Mashindano hayo yaliyoshirikisha shule mbalimbali za Dar es salaam na Pwani lilipambwa na maigizo ya maswala ya kodi ambapo mgeni Rasmi alikuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere.

Shule ya Sekodari Misitu iliyotia fora katika ufunguzi wa mashindano hayo ulimvutia mgeni rasmi na kudhamiria kushiriki mashindano hayo mwanzo hadi mwisho ambapo alipata fursa ya kujionea na kufurahia vipaji vya wanafunzi waliondaliwa vyema kuwa mabalozi wa maswala ya kodi katika nyanja mbalimbali kwa sasa na siku zijazo. 

Baada ya kufungua mashindano hayo yaliyonogeshwa na wanafunzi wenye vipaji mbalimbali vya kuwasilisha mada hatimaye shule ya sekondari Tumbi iliibuka kidedea na kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo Kombe, Luninga ya Kisasa, Saa ya Ukutani pamoja na cheti. 

Shule ya Sekondari Minaki ilichukuwa nafasi ya pili ikijinyakulia pia Kikombe, Komputa, Printa, Saa ya ukutani na cheti huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Shule ya Sekondari Maarifa ambayo kadhalika ilipata Kikombe, Komputa, Saa ya Ukutani pamoja na cheti.

Hadija Jumanne Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Misitu aliibuka Muwasilishaji mada bora na kujinyakulia Komputa mpakato, Saa ya Ukutani, Kikombe cha chai chenye chapa ya TRA. 

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere baada ya kukunwa na uzuri wa mashindano hayo aliahidi kuyaboresha zaidi mwakani ili kuwapa motisha zaidi wanafunzi na walimu wao kujiandaa vyema na kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kodi ambayo ndio mhimili muhimu wa kuboresha huduma za jamii na kuleta maendeleo kwa nchi. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akiwasili ukumbi wa Chuo cha Kodi (ITA) kuhudhuria mashindano ya Kodi kwa Shule za Sekondari za Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani yaliyoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka (kulia) ni Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akimkabidhi Hadija Jumanne Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Misitu baada ya kuibuka mwanafuzi bora katika uwasilishaji wa mada ihusuyo kodi ya ongezeko la thamani (VAT), wakati wa shindano la maswali ya Kodi lililoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho. Pamoja naye (kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna wa idara ya walipakodi wakubwa, Yeremiah Mbaghi na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs).

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akimkabidhi Mwalimu shule ya Sekodanri Jangwani zawadi ya kikombe baada wakati wa shindano la maswali ya Kodi lililoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho. Pamoja naye (kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna wa idara ya walipakodi wakubwa, Yeremiah Mbaghi, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo (wa tatu kulia) na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati. 
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee wakiwa wamembeba mwalimu wao Boniface Mulambo baada yakukadidhiwa zawadi ya Kikombe na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere kwa kuwaandaa vyema wanafunzi wake walioshiriki mashindano hayo.

Stamico sasa kuleta mapinduzi kwa wachimbaji wadogo

0
0
Mwenyekiti wa Bodi wa Stamico , Elexender Muganda akizungumza na waandishi habari juu shirika la Taifa la Madini (Stamico) kupata mtambo wa kisasa wa uchorongaji kwa kutumia upepo , jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa Stamico, Alex Rutagwelela akitoa ufafanuzi juu ya mtambo wa kisasa wa uchorongaji miamba jijini Dar es Salaam, kushoto ni Meneja Masoko na Uhusiano, Koleta Njelekela.
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji, Alex Rutagwelela akiangalia mtambo wa uchorongaji wa miamba Bandarini , jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

SHIRIKA la Taifa la Madini (Stamico) limepata mtambo wa uchorongaji kwa kutumia upepo (Air Rotary Drill Rig) wenye thamani dola za Kimarekani milioni 1.3 utakaotumika kupata taarifa za kijiolojia na mashapo kwa wachimbaji wadogo .

Kunufaika kwa wachimbaji wadogo kunatokana na stamico kupata mtambo wa kisasa wa uchorongaji miamba. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa Stamico, Elexender Muganda amesema kuwa mtambo umetengenezwa nchini Canada ambapo  mtambo huo utasaidia wachimbaji wadogo kupata taarifa za kjiolojia na mashapo katika maeneo yao kwa gharama nafuu.

Amesema mtambo huo umetolewa na serikali kupitia Wizara ya Madini chiini ya ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa usimamizi endelevu wa rasilimali ya madini Tanzania (SMMRP).
Muganda amesema huo una uwezo wa kuchoronga miamba kwa kutumia upepo na kwa haraka zaidi kati ya kina mita 30 hadi 200 na kwa gharama ambazo mchimbaji mdogo anamudu na kuchana uchimbaji wa kubahatisha pamoja kuwezesha kupata mikopo katika taasisi za fedha.

Aidha amesema kuwa wachimbaji wadogo wanaohitaji huduma za uchorongaji kwa kutumia upepo wafike katika ofisi za Stamico ili kupata taarifa zaidi.

SERIKALI YAANZA KUTOA MATIBABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI BURE

0
0
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia,wazee, na watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu ya Utaratibu wa utoaji wa matibabu ya Saratani bure. kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndungulile akifatilia kwa makini.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu pamoja na Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndungulile wakipokea vifaa hivyo vilivyotolewa kwa lengo la kufanya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti kwa wanawake nchini ambapo vifaa ivyo vitasambazwa katika vituo vya afya mbalimbali vitakavyotoa huduma hizo

Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii - Dar es Salaam

Wanawake wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kupima saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti ili kusaidia kupunguza ongezeko la ugonjwa huo na kutakiwa kuwahi mapema kupima kabla ya tatizo kuwa kubwa kwani saratani inaweza kutibika kwa gharama nafuu kabisa.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia,wazee, na watoto Ummy Mwalimu na kusema kuwa vituo vya afya vihakikishe vinatenga siku maalum kila mwezi kwa lengo la wanawake kupatiwa huduma ya upimaji wa saratani ya matiti pamoja na shingo ya kizazi na huduma hizi zinatolewa bila malipo ili kuhamasisha upimaji kwa wanawake hapa nchini.

"Wanawake wajitokeze kwa wingi katika kupima ili kujua afya zao na hii itasaidia kupunguza saratani ya matiti pamoja na shingo ya kizazi kwa kina mama,kuliko kusubiri tatizo liwe kubwa kwani tatizo likiwa dogo saratani inatibika na kwa gharama ndogo kabisa kuliko kukaa na kusubiri kuwa kubwa ". Amesema 

Amesema katika kuboresha huduma hizo serikali imenunua mashine za kisasa kabisa 100 za tiba mgando,mashine 9 za upasuaji mdogo ambazo zitatumika kwa ajili ya matibabu ya awali ya saratani kwa wanawake pamoja na mitungi 173 ya gesi ya carbon dioxide zitakazowezesha mashine hizo kufanya kazi.

Aidha Waziri ametoa onyo kwa waganga wa kienyeji wanaowarubuni watu kuwa wana uwezo wa kutibu ugonjwa huo kutokana na miti shamba na kuwataka kuachana na hio tabia Mara moja kwani dawa za asili hazitibu saratani ila zinatuliza tu.

" Hakuna dawa ya tiba asili inayotibu saratani waganga wa kienyeji waache tabia ya kuwarubuni wananchi kuwa dawa hizo zinatibu saratani jambo ambalo siyo kweli ila dawa hiyo inapunguza tuu maumivu na kama kuna mtu anaudhibitisho kuwa inatibu alete ifanyiwe uchunguzi ili tubaini kama ni kweli inatibu". Amesema.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndungulile amesema kuwa katika kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje,Serikali ya awamu ya tano imeamua kuboresha huduma za afya hususani upande wa saratani ili kuweza kuhakikisha wagonjwa hao wanatibiwa hapa nchini.

"Ifahamike kuwa takribani wagonjwa wapya elfu 50 kila mwaka wanagundulika kuwa na saratani ,na idadi hii inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2020".Amesema.

UKUTA MKUBWA WA BEIJING (THE GREAT WALL) UNAVYOINEMEESHA NCHI YA CHINA KATIKA SEKTA YA UTALII

0
0
Sehemu ye Ukuta Mkubwa ndani ya Mji wa Beijing nchini China (The Great Wall),kama uonekanavyo pichani mapema leo mchana,ambapo Maelfu ya watu wakiwemo Wenyeji na wageni hufurika kutembelea ukuta huo wenye historia kubwa nchini humo.Kuusoma zaidi BOFYA HAPA,Ukuta huo umekuwa kivutio kikubwa kwa wenyeji na wageni mbalimbali ambao wamekuwa wakifurika kila kukicha na kujionea historia kubwa ya ukuta huo nchini China,inaelezwa kuwa ukuta huo ni mojawapo ya chanzo kikubwa cha mapato katika nchi hiyo hasa kwa upande wa sekta ya Utalii.

Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies wapita maelezo mafupi kutoka kwa wenyeji wao kabla ya kupanda Ukuta wa The Great Wall mapema leo mchana,ikiwa ni sehemu ya kujifunza,kuona na kutazama fursa mbalimbali za Kiutalii mjini humo na namna wenyeji wa mji wa Beijing wanavyofanya shughuli zao kiutalii.
Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies na baadhi ya wenyeji wakielekea kwenye geti kuu la kuingilia Ukuta huo wa The Great wall,mapema leo mchana.
Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies wakiwa na Mwenyeji wao,wa tatu kulia wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya The Great Wall,mjini Beijing nchini China. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies Mohamed Said Kiluwa (mwenye njano),akipata maelezo mafupi kutoka kwa mmoja wa wadau wake aliombatana nao Risasi Mwaulanga,huku baaadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani wakisikiliza kwa makini,kulia ni Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha,Mansoury Kisebebo pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani (pichani kati)Zuberi Mhinana na nyuma yake ni Katibu Tawala Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala pamoja
Sehemu ye Ukuta Mkubwa ndani ya Mji wa Beijing nchini China (The Great Wall),kama uonekanavyo pichani mapema leo mchana,huku ukiwa mesheheni Maelfu ya watu wakiwemo Wenyeji na wageni (watalii) wakipanda ukuta huo ikiwa kama sehemu ya utalii na kujua historia ya ukuta huo uliopo nje kidogo ya mji wa Beijing nchini China.
The Great Wall ndani ya mji wa Beijing kama uonekanavyo mapema leo.

Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo mara baada ya kupanda Ukuta wa kihistoria ndani ya mji wa Beijing,nchini China
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies Mohamed Said Kiluwa akiwa na Wenyeji wake,ambao kwa pamoja wanatarajia kuandaa kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda kwa kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Pwani (ambao tayari wamekwishawasili mjini humu),wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na makampuni mbalimbali,litakalofanyika jijini Beijing,nchini China Oktoba 25,2017 ,litakalojumuisha wafanyashabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China. 

MBUNGE WA ILALA MHE MUSSA AZZAN ZUNGU ALIPOONGELA HATUA ZA KULINDA RASILIMALI ZA NCHI

MWENYEKITI WA UDP MHE JOHN CHEYO AONGELEA HATUA ZINAZOCHUKULIWA KULINDA RASILIMALI ZA NCHI

MWENYEKITI WA CUF PROFESA IBRAHIM LIPUMBA ALIPOONGELA HATUA ZA KULINDA RASILIMALI ZA NCHI

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MHE. WILLIAM LUKUVI AFAFANUA KUHUSU BOMOABOMOA


WAZIRI WA MADINI MHE. ANGELA KAIRUKI AKIONGEA WAKATI WA KUTUNUKU VYETI KWA WAJUMBE WA KAMATI ZA MADINI

Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara kuanza Novemba 26, 2017

0
0
Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Novemba 26, 2017 katika vituo viwili vya Dar es Salaam na Arusha, imefahamika.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (pichani) amesema Kundi A litakuwa Dar es Salaam na timu za Simba Queens ya jijini Dar Es Salaam iliyopanda daraja msimu huu.

Timu nyingine kwenye kundi hilo ni Mburahati Queens, JKT Queens, Evergreen zote za Dar es Salaam pamoja na timu za Fair Play ya Tanga na mabingwa watetezi – Mlandizi Queens.
Kundi B litakuwa na timu za Alliance ya Mwanza ambayo imepanda kutoka kituo cha Dodoma. Timu nyingine ni Marsh Academy pia ya Mwanza; Panama ya Iringa; Kigoma Sisterz ya Kigoma, Baobab ya Dodoma na Majengo Queens ya Singida.
Time hizo zitapambana katika vituo hadi Desemba 9, mwaka huu kabla ya kutoa jumla ya timu nane kwa maana ya nne kutoka kila kundi. Timu hizo nane zitapambana katika hatua ya Nane Bora ya Ligi hiyo kuelekea ubingwa. Ligi inatarajiwa kumalizika Machi 28, mwakani.
Kabla ya kuanza kwa ligi hiyo, TFF imetoa kalenda ya mashindano hayo ambako usajili utakuwa kati ya Oktoba 25 na Novemba 10, mwaka huu.
Novemba 12 hadi 17, mwaka huu ni kipindi cha pingamizi  wakati Novemba 18, mwaka huu kutakuwa na kikao cha  Kamati ya Sheria kabla ya Novemba 20, mwaka huu kutoa leseni za wachezaji.
Novemba 24, mwaka huu kutakuwa na Semina ya Viongozi wa klabu, Waamuzi na Makamishna jijini Dar es Salaam.
Baada ya kumalizika hatua ya makundi Desemba 9, mwaka huu Ligi Kuu hatua ya Nane Bora ‘Super 8’ itaanza Desemba 20, mwaka huu.

new webisode "How to Feed Chickens" by Maburu Maburu.

0
0

Courtesy of  Producer Zulfiqar Manzi

JINSI YA KUANDAA NA KUTAYARISHA LISHE YA SUPU YA ULIMI WA N’GOMBE MAALUMU KWA WATU WALIOKONDA NA KUDHOOFIKA MWILI.

0
0

Tafiti mbalimbali za kitaalamu zinautaja ulimi wa n’gombe kuwa na kiwango kikubwa cha protini inayo tokana na wanyama na ambayo ni muhimu sana katika ukuaji wa sehemu mbalimbali za mwili wa mwanadamu. 

Kama nyumbani kwako, una mtu ambae amekonda na kudhoofu mwili na anataka kurejesha afya ya mwili wake kwa njia ya vyakula vya asili, ni vyema ukajifunza namna ya kuandaa na kutayarisha supu ya ulimi wa n’gombe. 
Kufahamu jinsi supu ya ulimi wa n’gombe inavyo andaliwa na kutayarishwa ili iweze kutumika kwa watu walio konda na kudhoofika mwili na ambao wanahitaji kunenepa, tembelea: 

MGOMBEA UDIWANI CCM SARANGA HAROUN MDOE ACHUKUA FOMU YA TUME KWA AFISA MTENDAJI

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mgombea Udiwani wa kata ya Saranga Wilaya ya Ubungo katika uchaguzi mdogo kupitia chama cha Mapinduzi(CCM) ,Haroun Mdoe amechukua fomu rasmi katika ofisi ya Mtendaji wa kata hiyo leo.
Mdoe amechukua fomu hiyo leo mchana akiwa amesindikizwa na wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ya kata ya Saranga  ambapoiZoezi  hilo la uchukuaji fom lilifanyika katika  ofisi ya afisa mtendaji kata ya saranga  Ndandasi Kijo    ambae ni kaimu Mkurungenzi  wa uchaguzi  katika kata hiyo.
Katika marudio hayo ya uchaguzi vyama mbali mbali  navyo  vimejitokeza kuchuku fomu  hizo ikiwemo   chama cha demokrasia na  maendeleo( chadema),  chama cha wanachi  cuf,  Act wazalendo,  n.k
mara baada ya kuchukua fomu hiyo afisa Mtendaji huyo  Kijo alipiga marufuku  kufanyika kwa kampeni za aina yoyote  kwani  mda wa kampeni bado na hivyo yoyote akibainika  anafanya kampeni shelia kali zitachukuliwa  dhidi ya chama  hicho pamoja na mgombea wake.
 Katibu wa wilaya ya Ubungo, Salum Kali akimkabidhi barua ya uteuzi kwa mgombea Udiwani wa kata ya Saranga kupitia CCM  Mdoe   Katika uchaguzi mdogo unaotaraji kufanyika wilaya ya Ubungo
Mgombea Udiwani wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo wa Kata ya Saranga, Horoun Mdoe akimkabidhi mtendaji wa kata barua ya uteuzi wake kupitia CCM.
 Mgombea Udiwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Saranga  Wilaya ya Ubungo, Haroun Mdoe akisoma kwa umakini barua yake ya uteuzi  kupitia chama chake cha ccm
Baadhi ya viongozi  walio ambatana na mgombea wakati wa kuchukuo fomu wakiwa katika picha ya pamoja
--

MSAMA AUCTION MART YAANZA KUWAKAMATA WATU WOTE WANAOFANYA UHARAMIA WA KAZI ZA SANAA NCHI NZIMA

0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha zoezi la ukamataji wa wezi wa kazi za sanaa kwa kurudufu bila kibali na kuwauzia watu kwenye simu zao za mkononio jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya haki miliki na haki shiriki.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama  akiwa amebeba vifaa  vilivyokamatwa ambavyo vinatumika kurudufu kazi za wasanii

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama  akionyesha watu wanaotakiwa kukamatwa ambao wamekutwa wanafanya kaziya kurudufu kazi za wasanii
 Askari wa jeshi la Polisi wakiwa wamemkamata mmoja wa wezi wa kazi za wasanii wanaorudufu kwa kutumia kompyuta eneo la Kariakoo
 Askari wa jeshi la Polisi wakiwa wamemkamata mmoja wa wezi wa kazi za wasanii wanaorudufu kwa kutumia kompyuta eneo la Kariakoo
 Askari wa jeshi la Polisi wakiwa wamemkamata mmoja wa wezi wa kazi za wasanii wanaorudufu kwa kutumia kompyuta eneo la Kariakoo ambapo Msama SAuction Mart inafanya zoezi la kuwakamata watu wanaorudufu kazi za Wasanii kwa kutumia Kompyuta.
 Vijana wa kazi kutoka Msama Auction Mart wakipakia vyombo vinavyo tumika kurudufu kazi za wasanii kinyume cha Sheria.

Stamico yaleta mapinduzi kwa wachimbaji wadogo, yapata mtambo wa kuchoronga kwa kutumia upepo

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
SHIRIKA la Taifa la Madini (Stamico) limepata mtambo wa uchorongaji kwa kutumia upepo (Air Rotary Drill Rig) wenye thamani dola za Kimarekani milioni 1.3 utakaotumika kupata taarifa za kijiolojia na mashapo kwa wachimbaji wadogo . 
Kunufaika kwa wachimbaji wadogo kutatokana na Stamico kupata mtambo wa kisasa wa uchorongaji miamba. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa Stamico, Balozi Alexender Muganda amesema kuwa mtambo umetengenezwa nchini Canada na  utasaidia wachimbaji wadogo kupata taarifa za kjiolojia na mashapo katika maeneo yao kwa gharama nafuu. 
Amesema mtambo huo umetolewa na serikali kupitia Wizara ya Madini chiini ya ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa usimamizi endelevu wa rasilimali ya madini Tanzania (SMMRP). Balozi Muganda amesema mtambo huo una uwezo wa kuchoronga miamba kwa kutumia upepo na kwa haraka zaidi kati ya kina cha mita 30 hadi 200 na kwa gharama ambazo mchimbaji mdogo atamudu na kuachana na uchimbaji wa kubahatisha pamoja kuwezesha kupata mikopo katika taasisi za fedha. Aidha amesema kuwa wachimbaji wadogo wanaohitaji huduma za uchorongaji kwa kutumia upepo wafike katika ofisi za Stamico ili kupata taarifa zaidi.
 Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji Bw.  Alex Rutagwelela akiangalia mtambo huo wa uchorongaji wa miamba baada ya kuwasili bandari ya  Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa Stamico  Balozi Alexander Muganda akizungumza na waandishi habari juu shirika la Taifa la Madini (Stamico) kupata mtambo wa kisasa wa uchorongaji kwa kutumia upepo , jijini Dar es Salaam.

WANANCHI KILOSA WAONYWA KWA SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZINAZOBOMOA TUTA LA MTO MKONDOA LILOJENGWA KUZUIA MAAFA YA MAFURIKO

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo ya uharibifu wa tuta la mto mkondoa mjini Kilosa kutoka kwa Meja. Yenu Mgugule, kulia kwa Waziri ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. jen. Mbazi Msuya.
 Muonekano wa tuta la mto mkondoa mjini Kilosa ambalo limeanza kupasuka kutokana na shughuli za kibinadamu zinazofanywa kando ya mto huo na baadhi ya wananchi wa mji huo. Tuta hilo lenye urefu wa km 4.36 na kimo cha wastani wa mita 5 lilijengwa na serikali baada ya tuta la awali kuharibika kutokana na mafuriko yaliyotokea mwaka 2010.
 Sehemu ya tuta la mto mkondoa mjini Kilosa ambayo nyasi zinazozunguka tuta hilo kuzuia maji wakati wa mafuriko zimechomwa moto na baadhi ya wananchi wa mjini humo. Nyasi hizo zilipandwa na Jeshi la Wananchi Tanzania waliokuwa na jukumu la urejeshaji wa tuta hilo.
Baadhi ya Wananchi wa mjini Kilosa wakinyoosha mikono kuashiria kuunga mkono magizo juu ya kulilinda tuta la mto mkondoa kwa kutofanya shughuli za kibinadamu zilizokuwa zinaendelea pembenzoni mwa mto na tuta. Maagizo hayo yalitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea na wananchi wa mjini Kilosa (hawapo pichani), ambapo alielekeza Halmashauri hiyo kuw na mpango mkakati wa kulilinda tuta hilo pamoja na kuwaonya wananchi kufanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa tuta hilo.

WANANCHI WILAYANI NANYAMBA MKOA WA RUVUMA WAANZA UJENZI WA ZAHANATI KWA NGUVU ZAO

0
0
Serikali imewahakikishia wakazi wa halmashauri ya mji wa nanyamba mkoani Mtwara kuanza kupata huduma ya upasuaji miezi mitatu ijayo kufuatia kuanza ujenzi wa kituo cha afya katika halmashauri hiyo Wakazi wa halmashauri hiyo kwasasa wanalazimika kusafiri kwenda halmashauri ya jirani ya tandahimba au Mtwara jambo ambalo wamekuwa wakilalamikia kwamba linaongeza gharama za matibabu.

INTRODUCING MKUBWA NA WANAWE'S NEW HIT SINGLE "MAZOEA" BY KANUMBA

MASHINDANO YA WANAFUNZI WA SEKONDARI KWA MASWALA YA KODI YAFANA DAR ES SALAAM

0
0
Na Mwandishi Wetu.
Mamlaka ya mapato nchini (TRA) iliendesha na kudhamini shindano la shule za sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani jijini humo. Mashindano hayo yaliyoshirikisha shule mbalimbali za Dar es salaam na Pwani lilipambwa na maigizo ya maswala ya kodi ambapo mgeni Rasmi alikuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere.


Shule ya Sekodari Misitu iliyotia fora katika ufunguzi wa mashindano hayo ulimvutia mgeni rasmi na kudhamiria kushiriki mashindano hayo mwanzo hadi mwisho ambapo alipata fursa ya kujionea na kufurahia vipaji vya wanafunzi waliondaliwa vyema kuwa mabalozi wa maswala ya kodi katika nyanja mbalimbali kwa sasa na siku zijazo. 


Baada ya kufungua mashindano hayo yaliyonogeshwa na wanafunzi wenye vipaji mbalimbali vya kuwasilisha mada hatimaye shule ya sekondari Tumbi iliibuka kidedea na kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo Kombe, Luninga ya Kisasa, Saa ya Ukutani pamoja na cheti. 


Shule ya Sekondari Minaki ilichukuwa nafasi ya pili ikijinyakulia pia Kikombe, Komputa, Printa, Saa ya ukutani na cheti huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Shule ya Sekondari Maarifa ambayo kadhalika ilipata Kikombe, Komputa, Saa ya Ukutani pamoja na cheti.


Hadija Jumanne Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Misitu aliibuka Muwasilishaji mada bora na kujinyakulia Komputa mpakato, Saa ya Ukutani, Kikombe cha chai chenye chapa ya TRA. 

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere baada ya kukunwa na uzuri wa mashindano hayo aliahidi kuyaboresha zaidi mwakani ili kuwapa motisha zaidi wanafunzi na walimu wao kujiandaa vyema na kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kodi ambayo ndio mhimili muhimu wa kuboresha huduma za jamii na kuleta maendeleo kwa nchi. 

Zifuatazo ni picha mbalimbali za matukio ya mashindano hayo. 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili  kulia) akiwasili ukumbi wa Chuo cha Kodi (ITA) kuhudhuria mashindano ya Kodi kwa Shule za Sekondari za Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani yaliyoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka (kulia) ni    Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho.  
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akimkabidhi Hadija Jumanne Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Misitu baada ya kuibuka mwanafuzi bora katika uwasilishaji wa mada ihusuyo kodi ya ongezeko la thamani (VAT), wakati wa shindano la maswali ya Kodi lililoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho. Pamoja naye (kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna wa idara ya walipakodi wakubwa, Yeremiah Mbaghi na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati. 


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akimkabidhi Mwalimu shule ya Sekodanri Jangwani zawadi ya kikombe baada wakati wa shindano la maswali ya Kodi lililoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho. Pamoja naye (kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna wa idara ya walipakodi wakubwa, Yeremiah Mbaghi, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo (wa tatu kulia) na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati.  

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee wakiwa wamembeba mwalimu wao Boniface Mulambo baada yakukadidhiwa zawadi ya Kikombe na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere kwa kuwaandaa vyema wanafunzi wake walioshiriki mashindano hayo. 
(Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)

RC KAGERA AONGOZA UZINDUZI WA MASHAMBA DARASA WILAYANI MISSENYI

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu  (wa tatu kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi  rasmi wa mashamba darasa ya kilimo bora cha mihogo na migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa (tissue culture), kwa ufadhili  wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB) katika vijiji vya  Bunazi na Kashaba wilayani Missenyi mkoani humo leo. Shamba hilo litasimamiwa na Kikundi cha Ushirika cha Batekaka. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali, Denis Mwila, Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Belington Kyokwete, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Missenyi, Projestus Tegamaisho.

 
 Ofisa Ugani wa Kata ya Kasambya, Hakika Ibrahim, akizungumza kataika uzinduzi huo.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein, akizungumza katika uzinduzi huo.

 Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku akielezea mbegu hiyo mpya ya migomba. 

  Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu (wa tatu kulia),  Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein na Mkuu wa  Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali, Denis Mwila (kulia), pamoja na Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirika cha Batekaka, Belington Kyokwete, wakiwa wameshika mmoja wa mche wa mgomba katika uzinduzi huo. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images