Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1973 | 1974 | (Page 1975) | 1976 | 1977 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mratibu wa kampeni ya kuwezesha wanawake kutoka Oxfam Bi. Magdalena Thomas akielezea kwa ufupi hali ilivyo katika suala zima la kuwawezesha wanawake linavyohitaji nguvu zaidi huku akitolea mfano namna Mama Shujaa wa Chakula ilivyofanikiwa kuleta mtazamo chanya na kufumbua macho washiriki pamoja na jamii inayowazunguka.
  Sambamba na hilo aligusia safari iliyowahusisha washindi wawili wa Mama Shujaa wa Chakula Bi. Elinuru Pallangyo mshindi wa mwaka 2014 pamoja na Bi.Maria Mbuya mshindi wa mwaka 2016 ambao walizuru nchi za Uholanzi pamoja na Italia na kukutana na wabunge nchini humo.
  Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 Bi. Elinuru Pallangyo akielezea namna safari hii ilivyompa fursa ya kupaza sauti Kimataifa kueleza uhalisia uliopo katika jamii ya Tanzania hasa katika sekta nzima ya kilimo na namna wakulima wadogo hususan wanawake wanavyohitaji kushikwa mkono ili kuboresha uzalishaji pamoja na kukuza kipato.
  "Miongoni mwa mambo niliyopazia sauti ni kuwahamasisha wenzetu walioendelea kupitia mashirika pamoja na serikali kuja kuwekeza zaidi wakitulenga wakulima wadogo wanawake kwani mchango wetu ni mkubwa lakini mazingira siyo rafiki sana kuweza kutimiza malengo" alisema Bi.Elinuru.
  Akizungumza katika mkutano huo Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula mwaka 2016 alisema yeye alijikita katika kuelezea changamoto zinazowakabili wanawake katika uendeshaji wa kilimo nchini huku akianisha kuwa suala la umiliki wa ardhi, wataalamu wa kilimo, miundombinu pamoja na mabadiliko ya tabia nchi vimekuwa vikwazo vikubwa kwani wengi wakulima wadogo hasa wanawake ni wenye mitaji midogo.
  Naye Mratibu wa Kampeni ya chakula na mabadiliko ya tabia nchi kutoka Oxfam Bi. Nuria Mshare amesema Oxfam ni shirika la kimataifa linalofanya kazi katika nchi 90,ikiwemo Tanzania,ambapo lengo moja wapo ni kufanikisha mabadiliko endelevu kwa kuwainua wakulima wanawake wadogo kwa kuwasaidia katika sekta ya kilimo.

  Sambamba na hilo aliongeza kuwa miongoni mwa juhudi zinazofanywa na Oxfam ni kushawishi serikali kuongeza bajeti katika wizara ya kilimo na pia kuezidi kushawishi wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika sekta ya kilimo na hasa kwa wakulima wadogo.
  Na Dickson Mulashani

  0 0

  Benny Mwaipaja, Shinyanga
  Serikali inatarajia kuajiri wafanyakazi 400 wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi kifupi kijacho ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa watumishi katika Mamlaka hayo, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi na makusanyo ya kodi.

  Ahadi hiyo imetolewa Mjini Shinyanga na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utendaji wa Mamlaka hayo mkoani humo.

  Dkt. Kijaji amesema kuwa taratibu zote zimekamilika na wakati wowote nafasi za ajira zitatangazwa na kwamba nafasi hizo zimelenga kuiwezesha TRA kuwafikia watu wengi zaidi na kuongeza wigo wa makusanyo ya kodi.

  “Tunatambua changamoto ya uchache wa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ndio maana tumeamua kuajiri wafanyakazi hao 400 ambao ni wengi kuliko kada nyingine ili tuweze kuimarisha utendajikazi wa Mamlaka na hivyo kuongeza makusanyo ya kodi zinazotakiwa kwa shughuli za maendeleo nchini” alisema Dkt. Kijaji

  Alisema kuwa pamoja na uhaba wa watumishi, anaamini kuwa lengo la mwaka huu la kukusanya shilingi trilioni 17 ambazo Mamlaka hayo imepangiwa yatafikiwa na ikiwezekana kuzidi kwa kutumia wafanyakazi waliopo.

  Dkt. Kijaji alitoa rai kwa wafanyakazi wa TRA kuwa waadilifu na kwamba atakayebainika kukiuka maadili yake ya kazi atachukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria.

  Awali Meneja wa Mamlaka ya Mapato mkoa wa Shinyanga Bw. Jumbe Samson, alieleza kuwa mkoa wake umepangiwa lengo la kukusanya Shilingi bilioni 18 na kwamba wanauhakika wa kufikia lengo hilo kutokana na mikakati mbalimbali waliyojipangia ikiwemo kusimamia ukusanyaji kodi kikamilifu katika sekta ya madini.

  Kwa upande wake, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA Bw. Beatus Nchota alisema kuwa Mamlaka yake imejiwekea mipango ya kufungua ofisi zake kila wilaya hapa nchini ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali ili lengo walilopewa la kukusanya shilingi trilioni 17 liweze kufikiwa.

  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Josephine Matiro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, alisema kuwa Serikali mkoani humo itahakikisha kuwa TRA inatimiza malengo yake ya kukusanya kodi na kumhakikishia Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji kwamba watasimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwasisitiza watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga kuhakikisha wanafanyakazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya kukusanya Shilingi trilioni 17.
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (aliyesimama) akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga kuhusu nia ya Serikali katika kuhakikisha kodi ya majengo na mabango inakusanywa kikamilifu kwa manufaa ya wananchi na Taifa, alipofanya ziara ya kikazi katika mkoa huo.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wengine wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga, alipofanya ziara ya kikazi kukagua namna Mamlaka hayo inavyokusanya kodi.
  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)​

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Na Mwandishi Wetu- Dodoma
  Halmashauri za Temeke na Mbeya zimeonesha mafanikio makubwa katika utekelezaji wa Mpango wa Kijamii wa  Marekebisho ya Tabia kwa Watoto waliokinzana na Sheria ambapo kwa miaka mitano kuanzia 2012 mpaka 2017 jumla ya watoto 1000 wamefikiwa na kupewa msaada wa kisheria na wengine kufutiwa mashtaka.

  Takwimu hizi zimetolewa mjini Dodoma na Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi alipokuwa akifungua kikao cha mwaka cha Tathmini ya Mwaka ya Mpango wa Kijamii wa Marekebisho ya Tabia kwa watoto waliokinzana na Sheria.

  Bw. Rabikira Mushi ameongeza kuwa katika watoto 1000 waliofikiwa, watoto 416 walipelekwa katika vituo vya marekebisho ambapo wengine wamerudi shule, kuhitimu mafunzo ya VETA na kurejeshwa katika hali ya heshima na staha.

  “Niseme Serikali itakuwa inaendelea kutekeleza Mpango huu kwa ubia baina ya Asasi za Kirai na Halmashauri husika” alisema Bw. Mushi. 

  Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Jiji la Mbeya Bi. Bupe Joel amesema kuwa kwa mkoa wa Mbeya mpango huu ulianza kutekelezwa kuanzia Novemba, 2014 hadi Oktoba, 2017 kama mpango wa majaribio na umefanikiwa katika utekelezaji wake kwa kusaidia watoto 185.

  “Mpango huu umesaidia sana kupunguza idadi ya kesi za jinai watoto katika Mahakama kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya” alisema Bi Bupe.

  Aidha Naye Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Temeke Bi. Neema Mambosho amesema kuwa Halmashauri ya Temeke kwa kushirikiana na vituo vya utekelezaji wa mpango imekuwa ikiangalia njia mbali mbali za kuwasaidia watoto mara tu wamalizapo muda wao wa kuwa katika mpango wa marekebisho ya tabia (after care plan). 

  Ameongeza kuwa Katika kufanya hivyo Halmashauri imeweza kuwapatia nafasi ya mafunzo VETA watoto 14 pamoja na kuwasaidia watoto 53 ambao walishaacha shule kurudi shuleni. 

  Madhumuni makubwa ya Mpango wa Marekebisho ya Tabia kwa Watoto waliokinzana na Sheria ni kuwachepusha watoto kuingia katika mfumo wa mahakama na kwenda magerezani kutoka na makosa mbalimbali.
   Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi Magreth Mussai akifafanua jambo wakati kikao cha Tathmini ya mwaka ya Mpango wa Kijamii wa Marekebisho ya Tabia kwa watoto waliokinzana na Sheria kilichojumuisha Maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii, TAMISEMI, na wadau wa Watoto kilichofanyika katika ukumbi wa NHIF Mjini Dodoma.
   Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi (katikati) akizungumza na wadau wa utekelezaji wa Mpango wa Kijamii wa Marekebisho ya Tabia kwa Watoto waliokinzana na Sheria alipokuwa akifungua kikao cha mwaka cha Tathmini ya Mpango huo katika ukumbi wa NHIF Mjini Dodoma.
   Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na Watoto Bw. Darius Damas akielezea jambo kwa washiriki wa kikao cha mwaka cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango wa Kijamii wa Marekebisho ya Tabia kwa watoto waliokinzana na Sheria kilichofanyika katika ukumbi wa NHIF Mjini Dodoma.
   Afisa Ustawi wa Jamii wa Jiji la Mbeya Bi. Bupe Joel akielezea mafanikio ya utekelezaji wa Mpango wa Kijamii wa Marekebisho ya Tabia kwa watoto waliokinzana na Sheria katika Jiji la Mbeya wakati wa kikao cha mwaka cha tathmini ya mwaka ya Mpango huo kilichofanyika katika ukumbi wa NHIF Mjini Dodoma.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe ametembelea Mradi wa Maji Longido, mkoani Arusha kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wake, kwa lengo la kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa Longido.

  Mhandisi Kamwelwe ametembelea mradi huo na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa hadi sasa, ambao Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliweka jiwe la msingi mnamo Oktoba 21, 2017 na kuagiza ukamilike kwa wakati na kuanza kuhudumia wakazi wa Mji wa Longido na Kijiji cha Engikaret.

  ‘‘Serikali imedhamiria kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa majisafi na salama Wilayani Longido kwa kutekeleza mradi huu mkubwa wa maji kutoka katika chanzo cha maji cha Mto Simba kilichopo Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro umbali wa kilomita 64 mpaka Longido.’’

  ‘‘Nimeridhishwa na hatua ya utekelezaji wa mradi huu unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mji wa Arusha (AUWSA) na utaigharimu Serikali kiasi cha Sh. bilioni 15.8 ambazo ni fedha za ndani’’, alisema Waziri Kamwelwe.

  Mradi huo unategemea kuzalisha lita 2,160,000 kwa siku wakati mahitaji halisi kwa sasa ni lita 1,462,000, na unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 100 (sawa na wakazi 26,145 kwa sasa) wa Mji wa Longido kufikia 2024 na Kijiji cha Engikaret chenye wakazi wapatao 1,294.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akikagua chanzo cha maji cha Mto Simba, wilayani Siha.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akiangalia kazi ya uunganishaji wa mabomba yanayolazwa kwa ajili ya mradi wa Longido, Siha, mkoani Kilimanjaro.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (AUWSA), Mhandisi Ruth Koya Kilimanjaro, wakiwa mbele ya tenki la maji Longido.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Engikaret, ambao ni miongoni mwa watakaonufaika na mradi wa maji wa Longido, mkoani Arusha.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha kawaida cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2017. PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Tercisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu wa Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi Mhashamu Castory Msemwa, kilichotokea jana tarehe 19 Oktoba, 2017 nchini Oman.

  Mhashamu Askofu Castory Msemwa amefariki dunia Mjini Muscat akiwa safarini kuelekea nchini India kwa Matibabu.
  "Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Baba Askofu Msemwa, kilichotokea huko Oman, Baba Askofu Msemwa ametoa mchango mkubwa sio tu katika kutimiza majukumu yake ya huduma za kiroho bali pia katika kuisaidia jamii kupata huduma mbalimbali anazostahili binadamu na amekuwa akitoa ushirikiano mkubwa kwa taasisi nyingine zikiwemo za Serikali katika kudumisha amani, upendo, umoja na kuwahudumia wananchi, mchango wake utakumbukwa daima" Amesema Mhe. Rais Magufuli.
  Mhe. Rais Magufuli amemuomba Rais wa TEC Mhashamu Tercisius Ngalalekumtwa kumfikishia pole nyingi kwa Maaskofu wote wa TEC, Mapadre, Makatekista na waumini wote wa Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi kwa msiba huu mkubwa uliotokea na amesema anaungana nao katika kipindi cha majonzi na maombi kwa Marehemu.
  "Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie, Marehemu Askofu Castory Msemwa apumzike kwa amani, Amina" Amemalizia Mhe. Rais Magufuli.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  20 Oktoba, 2017

  0 0

  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeadhimisha siku ya Viwango Dunia kwa kutoa zawadi na vyeti kwa wanafunzi walioshinda shindano la uandishi wa Insha kama sehemu sehemu ya maadhimisho hayo na pia kuwajengea uwezo na uelewa wanafunzi juu ya umuhimu wa viwango.  Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Prof.Egid Mubofu alisema shirika lake linaipa siku ya viwango duniani kwa kuwajengea uwezo vijana kwa kuwashindanisha kwenye uandishi wa insha. 
  “Lengo kubwa la maadhimisho haya ni kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa viwango katika kuboresha maisha ya wananchi katika ubora wa vitu vyao, afya , usalama na biashara,” alisema Prof.Mubofu Prof. Mubofu alisema kila mwaka Shirika la Viwango Duniani huwa na Kauli mbinu yake ambayo kwa mwaka huu ni “Viwango huifanya Miji kuwa ya Kisasa zaidi” ambapo kauli mbiu hii inaweka msisitizo kupitia viwango uboreshaji wa maisha ya wakazi wa mijini kuwa ya kisasa zaidi. 
   “Shirika huandaa mashindano ya Insha katika shule za sekondari kupitia kauli mbinu ya mwaka ya viwango lengo ikiwa kupima uwezo wa wananfunzi katika ufahamu wao kuhusu viwango,” alisema Prof.Mubofu Alisema hii inatoa nafasi ya kupima kwa namna gani wananchi wanaelewa juu ya umuhimu wa viwango na kipi kifanyike katika kuwajengea uwezo hasa wanafunzi katika kuelewa juu ya majukumu na umuhimu wa viwango katika maisha yao. 
   Prof.Mubofu alisema TBS imetoa zawadi pamoja na vyeti kwa washindi wa insha ikiwa ni motisha ilikuchochea ushiriki wa wanafunzi wengine katika mashindano mbalimbali yanayotolewa na shirika kuhusu umuhimu wa viwanda. Aliongeza kuwa kutoka na ushiriki wa wanafunzi katika shindano hilo kuwa mkjubwa, TBS imejipanga kuboresha vigezo vya ushiriki ili kutoa nafasi kwa wanafunzi wa ngazi zote kushiriki kikamilifu. 
   “ TBS imejipanga kuboresha maisha ya watanzania kwa kusimamia viwango vya ubora katika maeneo yote hasa uzalishaji na ujenzi na afya,” alisema Prof.Mubofu na kuongeza kuwa azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda itatekelezeka kwa kuwa na usimamizi madhubuti wa viwango. 
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa uandaaji viwango TBS, Bi. Edna Ndumbaro alisema matumaini ya TBS kupitia mashindano ya insha katika maadhimisho ya siku ya viwango duniani ni kuwapatia uelewa na elimu kuhusu maswala ya viwango kwa manufaa ya sasa na jamii ijayo. 
   “Wanafunzi 10 kutoka Shule za sekondari za Kibaha,Feza, Elboru na Loyola walipatiwa zawadi ikiwa ni ishara ya kuifanya elimu ya viwango kuwa endelevu,” alisema Bi.Ndumbaro Mshindi wa kwanza wa shindano la Insha alikuwa mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Kibaha,Bw. Barnabas Michael ambaye alisema kushiriki kwenye mashindano kunamfanya mwanafunzi kujijengea uwezo wa kujieleza na pia kuwa na ufahamu wa mambo kwa mapana yake.
  “Wito wangu kwa wanafunzi wenzangu ni kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mashindano mbalimbali kwani yanasaidia kuongeza maarifa na uwezo wa kupambanua mambo mbalimbali,” alisema Bwana Michael Siku ya Viwango Duniani uazimishwa kwa lengo la kuelimisha juu ya uelewa miongoni mwa mamlaka za udhibiti, viwanda na walaji kuhusiana na umuhimu wa viwango kwa uchumi wa dunia ikiwepo Tanzania.
   Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS) Prof.Egid Mubofu akitoa mada kwenye hafla ya maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani yaliyofanyika katika ofisi za shirika hilo Ubungo jijini Dar salaam. Katika maadhimisho hayo yaliambatana na utoa wa vyeti na zawadi kwa wanafunzi walioshinda katika shindano la uandishi wa insha uliendana na kauli mbiu ya maadhimisho ambayo ni “VIWANGO HUIFANYA MIJI KUWA YA KISASA ZAIDI”
  Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS) Prof.Egid Mubofu akikabidhi zawadi ya Laptop, cheti na Kiasi cha shilingi laki tatu na nusu kwa mshindi wa Kwanza wa uandishi wa Insha mwanafunzi Shule ya Sekondari Kibaha Bw. Barnabas Michael katika shindano maalum la kuadhimisha siku ya viwango Duniani ikiwa na kauli mbiu “VIWANGO HUIFANYA MIJI KUWA YA KISASA ZAIDI” . shindano hilo limelenga wanafunzi kwa lengo la kuandaa kizazi chenye uwelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa viwango katika ubora, Afya, Usalama na Biashara.

  0 0

  Ofisi ya Msajili wa NGOs inapenda kuujulisha umma kuwa imesimamisha shughuli za Shirika la COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY (CHESA) kuanzia tarehe 20 Oktoba, 2017 ili kupisha uchunguzi unaofanywa dhidi ya tuhuma za shirika tajwa kujihusisha na uhamasishaji wa vitendo vya ndoa za jinsia moja katika maeneo mbalimbali nchini. 

  Shirika tajwa pamoja na tuhuma mbalimbali zilizopo, linatuhumiwa kuratibu warsha kuhusu masuala ya ndoa za jinsia moja tarehe 17 Oktoba, 2017 katika hoteli ya Peacock, Ilala – Dar es Salaam.

   Kwa taarifa hii uongozi wa Shirika unaagizwa kusimamisha shughuli zake zote ikiwa ni pamoja na kufunga ofisi zote za Shirika hadi uchunguzi utakapokamilika. Ikumbukwe kuwa ndoa za jinsia moja hazikubaliki nchini kwani ni kinyume na mila, desturi na sheria za nchi.

  M.S. Katemba
  MSAJILI WA NGOs

  0 0


  0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa East Point hotel ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro akitoa maelezo kwa watembeleaji wa banda la Zara Tours kwenye maonesho ya kimataifa ya Utalii (International Tourism and Travel Showjijini Montreal, Canada, leo ambako makampuni ya utalii na usafirishaji watalii kutoka nchi zaidi ya 100 yanashiriki kwenye maonesho hayo ya siku tatu
   Afisa Mtendaji Mkuu wa East Point hotel ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro akiwa tayari kuhudumia watembeleaji wa banda la Zara Tours kwenye maonesho ya kimataifa ya Utalii (International Tourism and Travel Show ) jijini Montreal, Canada, leo ambako makampuni ya utalii na usafirishaji watalii kutoka nchi zaidi ya 100 yanashiriki kwenye maonesho hayo ya siku tatu
   Afisa Mtendaji Mkuu wa East Point hotel ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro akiwa tayari kuhudumia watembeleaji wa banda la Zara Tours kwenye maonesho ya kimataifa ya Utalii (International Tourism and Travel Show ) jijini Montreal, Canada, leo. 

  0 0
  0 0  0 0

  Mwenyekiti wa ALAT Taifa ambaye pia ni Mshtahiki Meya wa Shinyanga, Gulam Hafeez Mukadam wa pili kulia akipokea mifuko ya saruji 500 kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Saruji ya Simba Cement Benedict Lema katikati ni Katibu Tawala Msaidizi Rasilimali watu na Utawala Mkoa wa Tanga, Radhiya Msuya ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano ya Nje wa Simba Cement, Noor Mtanga.
  Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Saruji ya Simba Cement Benedict Lema wa pili kushoto akimkabidhi mifuko ya saruji 500 Mwenyekiti wa ALAT Taifa ambaye pia ni Mshtahiki Meya wa Shinyanga, Gulam Hafeez Mukadam wa pili kutoka kulia kwa ajili ya ujenzi miundombinu katika sekta ya elimu katikati ni Katibu Tawala Msaidizi Rasilimali watu na Utawala Mkoa wa Tanga, Radhiya Msuya ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano ya Nje wa Simba Cement, Noor Mtanga.
  Sehemu ya Saruji iliyokabidhiwa leo.

  NA MWANDISHI WETU, TANGA. 

  IMEELEZWA kuwa sekta ya viwanda inahitaji wahandisi ambao watashiriki katika shughuli mbalimbali baada ya wale waliopo hivi sasa kustaafu kwa kuwekewa mazingira mazuri wanaochipukia katika uimarishaji wa miundombinu shuleni.

  Hayo yalisemwa leo na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Tanga Cement),Benedict Lema wakati akikabidhi mifuko 500 ya Saruji kwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam kwa ajili ya shule zao katika kuboresha maendeleo na ujenzi wa vyoo vya wanafunzi na maeneo mengine ya elimu na afya.

  Mifuko hiyo ina zaidi ya thamani ya milioni 6 iliyotolewa Halmashauri ya Shinyanga kwa ajili ya kuweza kukabiliana na uhaba wa miundombinnu ya shule ikiwemo vyoo. Lema alisema ili kuweza kusaidia harakati za kuelekea Tanzania ya Viwanda ndio sababu kubwa wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali kuwezesha kupunguza baadhi ya changamoto zilizopo ili kuhakikisha zinakwisha.

  Aidha alisema wanafunzi wanapaswa kuongeza bidii ili kuweza kufanikiwa katika masomo yao jambo ambalo litawezesha kupatikana kwa wahandisi wengi ambao watasaidia sekta ya viwanda.

  Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Rasilimali watu na Utawala Mkoa wa Tanga, Radhiya Msuya aliishukuru kampuni ya Tanga Cement kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa katika kusaidia sekta ya elimu ya vijana wetu ambao watakuwa wataalamu kwenye maeneo mbalimbali.

  Alisema mchango wao huyo ni mkubwa kwa sababu unasaidia katika harakati za kuelekea Tanzania ya Viwanda kwa kuona mbali kwa kuwekeza kwenye sekta ya elimu ambayo ndio nguzo muhimu kufikia malengo hayo.

  Naye kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT ) Taifa ambaye pia ni Mshtahiki Meya wa Shinyanga, Gulam Hafeez Mukadam aliishukuru kampuni hiyo kwa kuthamini harakati za kuinua elimu hapa nchini kwa kusaidia mifuko hiyo ya saruji ambayo itakuwa ni chachu kubwa kufikia malengo yao kielimu.

  Alisema anawashukuru sana kwa kuunga mkono agizo la Rais kuelekeza nguvu kwenye sekta ya elimu katika kutatua changamoto za madawati na vyoo ili kusaidia harakati za elimu ambazo zinafaida. Hata hivyo alisema wataendelea kuwahimiza vijana kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili kuweza kupatikana wahandisi wengi ambao watakuwa ni chachu kubwa baada ya waliopo kustaafu.

  0 0

  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mbele kushoto) pamoja na Watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Puma Energy wakiendelea na ziara katika sehemu ya kampuni hiyo Kurasini, jijini Dar es Salaam tarehe 19 Oktoba, 2017.

  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameziagiza kampuni za Puma Energy na Tiper Tanzania kuwa kuanzia mwisho wa mwezi huu ziwasilishe mara moja taarifa ya shughuli zake za kila baada ya miezi mitatu Serikalini, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya kampuni hizo.

  Pamoja na hayo Waziri Kalemani amesema kuanzia sasa ni marufuku mafuta kupotea kwenye vituo vya kupokelea mafuta na kubainisha kuwa anatarajia kuchukua hatua kwa kushirikiana Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ili kudhibiti tatizo hilo.

  Dkt. Kalemani aliyasema hayo Dar es Salaam tarehe 19 Oktoba, 2017 alipofanya ziara katika kampuni hizo na kutembelea Bohari za kuhifadhia mafuta, pamoja na kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha kupokelea mafuta ya dizeli kilichopo Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

  Alisema Serikali kama mbia mwenye asilimia 50 kwenye hisa za kampuni hizo inatakiwa kushiriki ipasavyo ikiwa ni pamoja na kupata taarifa za kila baada ya miezi mitatu kuhusu utendaji, faida, hasara pamoja na changamoto zinazokabili kampuni

  “Nataka mtambue kuwa ninyi kama kampuni ni sehemu ya serikali na kuanzia sasa jicho la serikali litakuwa linawaangazia kila mnachokifanya, huu sio wakati wa kufanya kazi kwa mazoea,” alisema Dkt. Kalemani.

  Akiwa katika kampuni ya Puma Energy yenye vituo 49 nchi nzima, Dk. Kalemani aliagiza kampuni hiyo kupanua shughuli zake kwa kufungua vituo zaidi kwenye mikoa kwa kuwa hadi sasa mikoa sita nchini bado haijafikiwa na vituo vya Puma Energy.

  Aidha aliitaka kampuni hiyo yenye matanki manne ya kuhifadhia mafuta huku moja likiwa ni bovu kuhakikisha matengenezo yanafanyika mara moja ndani ya wiki moja ili kuhakikisha kuwa mafuta ya kutosha yanapatikana. Akiwa katika kampuni ya Tiper, Dkt. Kalemani aliagiza kampuni hiyo kuanza kuwasilisha taarifa ya utendaji kazi wake kuanzia mwisho mwa mwezi huu pamoja na taarifa ya matumizi ya shilingi bilioni nane ambazo zilitolewa na serikali kwa ajili ya ukarabati wa tanki moja la kampuni hiyo lililokuwa limeharibika.

  Aidha, aliitaka kampuni hiyo kuyafufufua matanki manne ya kuhifadhia mafuta ambayo hayafanyi kazi kwa sasa ndani ya kipindi cha miezi minne kuanzia sasa ili kuongeza kiwango cha kuhifadhi mafuta.

  Katika hatua nyingine Dkt. Kalemani alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha kupima mafuta aina ya dizeli kutoka kwenye meli kilichopo chini ya Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) kilichopo Kigamboni na kukagua mashine mbili za flow meters zilizofungwa kituoni hapo. Waziri Kalemani aliagiza ukarabati wa mashine hizo kufanyika kwa haraka ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha hakuna upotevu wa mafuta kabisa.
  Meneja Bohari kutoka Kampuni ya Puma Energy, Auni Yateri (kulia) akielezea shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo kwa Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani(katikati).
  Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani (kulia) akizungumza na vyombo vya habari katika Kituo cha Puma Energy, Kurasini jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea kituo hicho.
  Sehemu ya Kituo cha Puma Energy, Kurasini jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani (kulia) akitoa maelekezo katika kituo cha kupima mafuta aina ya dizeli kutoka kwenye meli kilichopo chini ya Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akifungua moja kati ya vitanda 14 vya kujifungulia vilivyotolewa na Rais Magufuli mapema leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.

  Halmashauri saba za Mkoa wa Singida zimeagizwa kununua vitanda kumi kwa ajili ya akina mama kujifungulia ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli za kuboresha afya ya mama na mtoto. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa agizo hilo mapema leo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupokea vitanda vya kujifungulia 14, magodoro 20 na mashuka 50 vyenye thamani ya zaidi ya milioni 121 kutoka kwa Rais Magufuli.

  Dkt Nchimbi amesema halmashauri zinatakiwa kuiga mfano wa Rais Magufuli anayojali afya kwa ajili ya wananchi hivyo wanapaswa kutenga kiasi cha shilingi milioni kumi na tatu kwa ajili ya kununua vitanda hivyo kwa mwaka huu wa fedha.

  “Tumezoea kupokea tu na tumepokea sana vifaa tiba kutoka kwa rais wetu mpendwa Magufuli, hebu tujifunze upendo wake kwa wananchi, hivyo naagiza kila halmashauri inunue vitanda kumi vya kujifungulia nadani ya mwaka huu wa fedha”, amesisitiza Dkt Nchimbi.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisaidiana na wataalamu wa afya pamoja na Mbunge wa Viti maalumu Aisharose Mattembe kufunga moja kati ya vitanda 14 vya kujifungulia vilivyotolewa na Rais Magufuli mapema leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.

  Amengeza kuwa akina mama wajawazito wanatakiwa kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya kwakuwa kuna huduma bora zaidi huku akiwataka wakunga wa jadi wawasaidie wajawazito kufika katika vituo hivyo. Aidha Dkt Nchimbi amemshukuru Mbunge wa Viti Maalumu Singida Aisharose Mattembe aliaminiwa na Rais Magufuli na kumtuma kufikisha vitanda hivyo Mkoani Singida huku akimtaka kuanzisha tunzo ya wakunga watakaosaidia kufikisha akina mama wajawazito katika vituo vya kutolea huduma za afya.

  “Natoa shukrani zangu za dhati kwa niaba ya wananchi wa Singida kwa Rais Magufuli kwa kuendelea kutujali wana Singida, pia nakushukuru kwa uaminifu wako mbuge wetu Mattembe kwa kufikisha vifaa hivi salama ila naomba uanzisishe tunzo ya wakunga wa jadi watakaowashauri vizuri na kuwafikisha katika vituo vya kutolea huduma za afya akina mama wajawazito”, amesema Dkt Nchimbi.
  Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Aisharose Mattembe akizungumza na wauguzi, madaktari na Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) mkoa wa Singida kabla hajakabidhi vitanda 14 alivyopewa na Rais Magufuli ili avifikishe kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

  Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Emmanuel Kimario amemshukuru Rais Magufuli kwa vitanda hivyo vitakavyosaidia kupunguza uhaba wa vitanda, hasa kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambapo wajawazito wengi wanapenda kujifungulia kwakuwa na imani napo kutokana huduma bora zinazotolewa. Dkt Kimario amesema mpaka sasa bado kuna akina mama wanajifungulia nyumbani na kwa wakunga wa jadi jambo linalohatarisha afya ya mama na motto hivyo wafuate ushauri wa kufika katika vituo hivyo mara tu wanapo hisi kuwa na ujauzito.

  ‘Takwimu za kuanzia kipindi cha mwezi wa saba mpaka wa tisa mwaka huu zinaonyesha kuwa akina mama waliojifungulia ni 12,431 ambapo kati yao 190 wamejifunguliwa nyumbani, akina mama 78 wamejifunguliwa kwa wakunga  na wengine 258 wamejifungulia njiani”, amesema Dkt Kimario.
  Kaimu Mganga Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Emmanuel Kimario akimshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia vitanda vya kujifungulia ili kupunguza uhaba wa vitanda kwa Mkoa was Singida.

  Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Maulidi Kiaratu amewapongeza wauguzi na madaktari wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa huduma nzuri wanazotoa hadi kusababisha wagonjwa wengi kukimbilia hapo.

  Amesema, “unakuta mgonjwa anaacha aspirini pale kituo cha afya Sokoine na kuja hapa Hospitali ya Mkoa akiwa na imani kubwa hata akipewa dawa ile ile hapa atapata nafuu, hivyo nawapongeza sana na muendelee na moyo huo wa kuwahudumia vizuri wagonjwa hata kama tunapata changamoto akati wa kuwalaza wanapokuwa wengi”, amesisitiza Kiaratu. Ameongeza kuwa Mbunge wa Viti maalumu Singida Aisharose Mattembe amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia afya ya mama na mtoto inaboreka Mkoani Singida huku akijitolea vifaa mbalimbali kama vitanda na mashuka,  jambo ambalo ni faraja kwa akina mama na wananchi wote.

  Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida wakifurahia mara baada ya kukabidhiwa vitanda vya kujifungulia vilivyotolewa na Rais Magufuli.

  0 0

  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza (kulia) akimsikiliza Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza alipofanya ziara katika Taasisi hiyo, Oktoba 20, 2017 Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akimsikiliza Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (wapili kushoto) alipofanya ziara katika Taasisi hiyo na kukagua ukumbi wa maonyesho ya sanaa Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akizungumza na watendaji wa BASATA (hawapo pichani) alipofanya ziara katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi.
  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akiangalia moja ya batiki zinazotengenezwa na wajasiriamali wa fani za sanaa alipofanya ziara katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza.
  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na watendaji wa BASATA alipofanya ziara katika Taasisi hiyo. Kulia waliokaa ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza. Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM.

  0 0

  Waogeleaji wa Tanzania, Sonia Tumitto, Collins Saliboko, Hilal Hilal na Emma Imhoff (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na waogeleaji kutoka Zambia na Kenya mara baada ya kutwaa medali ya dhahabu kwa upande wa Relay.

  Waogeleaji wa Tanzania wameendelea kung’ara katika mashindano ya Cana ya Kanda ya tatu ya Afrika baada ya kuendelea kukusanya medali mbalimbali kwa siku ya pili mfululizo. Kutokana na kutawala mashindano hayo, matumaini ya timu hiyo ya Taifa kulitetea kombe hilo yameongezeka na wanatarajia kuweka historia ya pili kwa kutwaa ubingwa wa jumla wa mashindano hayo.

  Siku ya kwanza, Tanzania ilitwaa medali zaidi ya 21, huku ikishinda medal tisa za dhahabu, tano za shaba na saba za fedha katika mashindano hayo yanayoshirikisha jumla ya nchi sita ambazo ni Kenya, Uganda, Zambia, Afrika Kusini, Sudan na wenyeji Tanzania.

  Muogeleaji wa kwanza wa Tanzania kutwaa medali ya  dhahabu ni Natalie Sanford ambaye alishinda mita 800 kwa staili ya freestyle kwa waogeaji waliochini ya miaka 14 na baadaye muogeleaji nyota wa Tanzania wa kike, Sonia Tumiotto akishinda kwa waogeleaji wa kike wenye umri zaidi ya miaka 15.

   Waogeleaji wengine waliotamba na kutwaa medali za dhahabu ni, Elia Imhoff, Natalie, Emma Imhoff, Tara Behnsen, Marin De Villard na kwenye ‘relay’ kupitia kwa Sonia Tumitto, Collins Saliboko, Hilal Hilal na Emma Imhoff.
  Kocha wa timu hiyo, Michael Livingstone alisema kuwa wana matumaini makubwa ya kutetea ubingwa huo pamoja na upinzani mkali kutoka kwa nchi shiriki hasa Zambia.

  “Mashindano ni magumu sana, ushindani ni mkubwa, tuna uhakika asilimia 100 kuwa tutashinda, waogeleaji wetu wamefanya vyema katika mashindano ya awali na tunaongoza kwa kutwaa medali,” alisema Michael. Alisema kuwa wamefuraishwa sana na jinsi waogeleaji wao wanavyojituma kwa kutambua kuwa wapo nyumbani nna kukataa kata kata kushindwa.

  Mashindano hayo yaliyoanza Alhamis, yatafungwa kesho Jumamosi saa 11.00 jioni na ambapo zawadi mbalimbali za washindi zitatolewa.
  Waogeleaji wakijiandaa ‘kuchumpa’ katika mashindano ya kuogelea ya Cana Kanda ya Tatu Afrika.
  Muogeleaji wa Kike wa Tanzania Kayla Temba akipigania medali katika mashindano ya Cana Kanda ya tatu.

  0 0

  Katika jitihada za kukabiliana na kuhimili athari za mabadiliko ya Tabianchi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kutafuta fedha kwa wafadhili na wadau wa maendeleo ili kupambana na changamoto hii inayoikabili dunia kwasasa.

  Waziri January Makamba ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa ukuta wa kuhimili wingi wa maji na upandaji wa mikoko katika eneo la Kilimani na Kisakasaka Unguja.

  Athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri kwa sasa, sisi kama serikali tunachukua hatua za dhati ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha sehemu mbalimbali duniani ili kuendelea kutekeza miradi mingi zaidi kama hii ya kupanda mikoko na kujenga kuta zitakazosaidia kupunguza kasi ya maji kufika kwenye makazi ya watu, Makamba alisisitiza.

  Waziri Makamba ameainisha kuwa lengo la Serikali ni kulinda na kuokoa uchumi wa wananchi wa kuweka miundombinu wezeshi kwa ustawi wa maendeleo endelevu. "ingawa masuala ya mazingira si jambo la muungano lakini hatuna budi kusaidiana na kushirikiana" alisema Waziri Makamba.

  Nae msimamizi wa mradi huo Mhandisi Khamis Nassoro kutoka Kampuni ya Dezo Civili Contractors amesema kuwa changamoto kubwa ni uelewa mdogo wa wananchi juu ya hifadhi ya mazingira na kuwata wananchi wote kufahamu kuwa suala la kutunza na kuhifadhi mazingira sijukumu la serikali bali ni wajibu wa kila mmoja wetu.

  Mradi huo unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi minne na utagharimu dola za kimarekani 74,166.02
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akikagua eneo lililopandwa miti aina ya mikoko katika eneo la Kisakasaka Unguja. Azma ya Serikalini kuhakikisha maendeleo endelelevu kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mazingira Bw. Sheha Mjaja.
  Pichani ni miti aina ya mikoko iliyopandwa katika eneo la Kilimani - Unguja ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Fedha za kupanda mikoko hiyo ziko chini ya mradi wa Kuhimili mabadiliko ya tabianchi unasimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

  0 0

  Mtaalamu wa masuala ya Masoko kutoka Ufilipino, Dk.Wenfredo Muni akikabidhiwa zawadi ya maua na Meneja Uhusiano wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Neema Fredrick wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jioni hii. Aliyevaa fulana ya njano ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange na Mdau Haji Mohamed. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
  Waziri wa zamani wa Afya, Dk. Rashid Seif akisalimiana na Dk. Muni
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mkikita, Dk. Kissui S Kissui akisalimiana na Dk. Muni wakati wa kumlaki mgeni huyo kutoka ufilipino.

  Na Richard Mwaikenda

  UONGOZI wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Dk. Kisusui S Kissui na Mkurugenzi Mtendaji, Adam Ngamange kumlaki Mtaalamu wa Masoko kutoka Ufilipino, Dk.Wenifredo Muni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

  Mtalaamu huyo ambaye atakuwa nchini kwa miezi mitatu kwa mualiko wa Mkikita atafanya semina mbalimbali pamoja na kutembelea mashamba yanayosimamiwa na matandao huo yakiwemo pia ya watu binafsi blia kusahau mifugo.
   
  Akizungmza wakati wa mapokezi, Mkurugenzi wa Mkikita, Adam Ngamange amesema kuwa ujio wa mtalaamu huyo utawanufaisha wakulima na wafugaji wa mtandao huo kwa kupanua uwanja mpana wa masoko ya mazao na mifugo nje ya nchi.

  Aliwaasa wanachama kutoiacha fursa hiyo pekee ambayo haijawahi tokea na kuwataka kuhudhuria semina zilizoandaliwa ili wapate matokeo chanya ya fursa za masoko duniani.

  Katika mapokezi hayo Mkikita iliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Dk. Kissui S Kissui, Wajumbe wa Bodi, Catherina Edward, Neema Fredrick na Elizabeth na baadhi ya wanachama wa mtandao huo.

  Wadau wengine waliojitokeza kumpokea ni aliyekuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Rashid Seif., Haji Mohamed, Suchekk Bangragh na Mbaga Edward.

older | 1 | .... | 1973 | 1974 | (Page 1975) | 1976 | 1977 | .... | 3272 | newer