Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109609 articles
Browse latest View live

Mawakala wa benki ya CRDB watakiwa kuendeleza uadilifu

0
0


Mawakala kutoka wila ya za Nyamagana, Ilemela, Magu, Misungwi, Kwimba, Sengerema pamoja na Ukerewe walihudhuria kwenye semina hiyo iliyofanyika alhamisi iliyopita Oktoba 12,2017 Jijini Mwanza.
Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa CRDB tawi la Nyanza Jijini Mwanza, Wambura Calystus aliwasihi mawakala hao kuwa waaminifu katika kuwahudumia wateja ikiwemo kutunza siri za mihamara ya pesa za wateja wao huku wakitoa huduma bora kama ilivyo ada ya benki ya CRDB wanayoiwakilisha katika maeneo yao.
Mawakala hao walieleza kwamba semina hiyo itawasaidia kuboresha huduma zao kwa wateja na hivyo kuwahimiza wateja wa benki ya CRDB kuendelea kutumia huduma za benki hiyo kwani zinapatikana kwa urahisi katika maeneo yote nchini.
Na Binagi Media Group
Mawakala wa benki ya CRDB kupitia huduma ya Fahari Huduma kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza, wakiwa kwenye semina iliyoyandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya kuwajengea weledi na uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja.

Mkurugenzi wa CRDB tawi la Nyanza Jijini Mwanza, Wambura Calystus, akifungua semina hiyo
Meneja wa CRDB tawi la Nyanza Jijini Mwanza, Mafwimbo Mulungu akizungumza kwenye semina hiyo
Afisa wa CRDB, Danford Muyango akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
Mmoja wa maofisa wa benki ya CRDB, akizungumza kwenye semina hiyo.Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

JARIDA LA NISHATI NA MADINI TOLEO LA 194

TANZANIA NA OMAN KUANZISHA UTALII WA PAMOJA WA KIHISTORIA NA UTAMADUNI

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla amesema  Tanzania na Nchi ya Oman zimefanya mazungumzo katika kuimalisha sekta ya Utalii hasa kwenye Utalii wa kukuza Utamaduni na ule wa Kihistoria uliokuwepo miaka mingi kwa Mataifa hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Kigwangalla amebainisha hayo jioni ya jana Oktoba 18,2017, wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho ya nyimbo na ngoma za Taifa la Oman yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam ambapo pia tukio lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri na viongozi wa Taifa hilo la Oman ambao wapo Nchini kwa ziara ya kusambaza Ujumbe wa Amani na Upendo kupitia meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohamed Hamad Al Rumhy alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akiongea  na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, wakati akishuhudia tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam
 Bendi ya Jeshi la Taifa la Oman wakipiga nyimbo za Taifa hilo zinazofanyika wakati wa vita na ukombozi
 Baadhi ya wananchi wakiwa na bendera za Taifa la Oman na Tanzania wakishuhudia tukio hilo
 Baadhi ya Askari wa kikosi Maji cha Oman wakiwa katika tukio hilo.

SOMA ICT GREEN BIRD COLLEGE

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 19.10.2017

MKUTANO WA TEHAMA KUFUNGUA FURSA KWA WANANCHI

MAGAZETI YA LEO IJUMAA OCTOBER 20,2017

RC GAMBO AFUNGUA KIKAO MKAKATI CHA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) ARUSHA

0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza na wanachama wa baraza la wafanyakazi wa shirika la Bima la taifa leo jijini Arusha mara alipoalikwa kama mgeni ramsi kufungua kikao cha baraza hilo kilichofanyika katika ukumbi wa veta jijini Arusha jana 
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akiwa pamoja na baadhi ya wajumbe na viongozi wa baraza la wafanyakazi wa shirika la Bima la Taifa leo katika ukumbi wa Veta jijini hapa mara bada ya kufungua mkutano wa baraza hilo. 
Baadhi ya wanachama wa baraza la wafanyazi wa shirika la Bima la Taifa wakiwa katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika leo ndani ya chuo cha Veta jijini Arusha, 
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akinyanyua mikono na viongozi wa baraza la wafanyakazi wa Bima la Taifa leo katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika katika chuo cha Veta jijini Arusha,kushoto kwake ni mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Bima la Taifa,Laston Msongole. 
Mwenyekiti wa bodi ya shirika la Bima la Taifa,Laston Msongole aliyeshika kipaza sauti akizungumza katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo jana katika ukumbi wa veta jijini hapa,pembeni yake ni mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo 



MAKAMU WA RAIS,SAMIA SULUHU AMKABIDHI CHETI CHA PONGEZI AFANDE IBRAHIM SAMWIX

0
0
 Makamu wa Rais, Samia Hassan Suhuhu akimpa Mkono, Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Mabasi cha Ubungo, Ibrahim Samwix  katika wiki usalama barabarani iliyofanyika mkoani Kilimanjaro.Ikiwa ni pongezi kwa kusimamia vizuri sheria za usalama barabarani.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Lameck Nchemba akimpa mkono Mkuu wa Ukaguzi wa Kituo cha Mabasi cha Ubungo, Ibrahim  Samwix  katika  Wiki Usalama Barabarani  iliyofanyika mkoani Kilimanjaro, Mkuu kituo cha mabasi ubungo alitunukiwa cheti cha  usimamizi wa sheria za usalama barabarani .

BENKI YA EXIM YATOA MAGODORO NA VITANDA 40 YENYE THAMANI YA MILIONI 20 KWA HOSPITALI YA MKOA, MTWARA.

0
0



Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Exim Tanzania, Dinesh Arora akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Hon Halima Dendego vitanda na magodoro 40 venye thamani ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya hospital ya rufaa ya Ligula mjini humo kama sehemu ya kampeni yake yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii, Mganga Mkuu wa Mkoa Dr.Wedson Sichalwe.

Wafanyakazi wa benki ya Exim wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya Ligula mjini.

BENKI ya Exim Tanzania imekabidhi vitanda na magodoro 40 yenye thamani ya TZS 20M / - kwa Hospitali ya mkoa iliyoko Mtwara, kama sehemu ya kampeni yake yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii.

Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka huu,kwakuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujalijamii”ambao Benki hiyo itawekeza shilingi milioni 200 katika sekta ya afya Tanzania.

Mradi huu unalenga kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali nchini - hivyo benki ya Exim itatoa magodoro na vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini.

Hospitaliyamkoa, Mtwara, nihospitaliyatatukupokeamchangohuu, baadayaHospitaliyaMnaziMmoja, Unguja, Zanzibar mweziuliopita. TukiolilifanyikakwenyehospitalihiyonamgenirasmialikwaMkuuwamkoa Halima Dendego.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim, Stanley Kafualisema, “ Mwaka huu benki ya Exim imefikia hatua muhimu sana. 
Tunasheherekea miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwajamii. Kwa miaka mingi benki ya Exim imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya, mazingira na elimu nchini.
Tunatambua juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya hivyo basi tumejitolea mwaka huu mzima kuwekeza katika hospitali za serikali katika maeneo mbalimbali nchini.” 

Hospitali na kliniki nyingi nchini zinatatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa. Takwimu za Shirika la afya duniani ‘WHO’ zinaonyesha kuwa Tanzania ina uwiano wa vitanda saba kwa kila watu elfu kumi. Hivi sasa hali ya kuona wakina mamawajawazito wawili wa kitumia kitanda kimoja au wengine  kulala sakafuni ni jambo la kawaida katika hospitali hizi. 

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego alipongeza Exim Bank Tanzania kwa ahadi yake ya kukabiliana na upungufu wa  vitanda kwenye hospitali ambao unakabiliwa na taifa na kuleta juhudi zake kwa hospitali ya  Mkoa wa Mtwara.

Afisa wa matibabu wa Hospitali ya mkoa,Mtwara alisema“Upungufu wa vitanda katika hospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wahivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii.”

TADB NA CDA YA CHINA WAJADILIANA NA MFUKO WA MAENDELEO YA AFRIKA NA CHINA

0
0
 PICHA YA PAMOJA ya baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Ushiriani wa Biashara na Uwekezaji kati ya China na Tanzania likilofanyika Guangzhou China tarehe 16 Oktoba 2017.
Katikati ni Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof.  Adolf Mkenda aliyekuwa Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo, kulia kwake ni Adam Kimbisa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki; Katibu Mkuu wa Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar Bw. Juma Alli Juma; Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki, na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Akaro. Kulia kabisa aliyesimama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania (TADB) Bw. Francis Assenga.
 Ujumbe wa Tanzania wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Makamu Rais wa Mfuko wa Maendeleo ya Africa wa China 'CADFUND". Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bwn. Francis Assenga, Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji ,Adolf Nkenda, Makamu Rais na Naibu Mtendaki Mkuu wa CadADFUND, Wang Yong na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja.
 
 Kutoka kushoto ni Michael Kitulizo (Mtendaji Mkuu wa Mema Holdings), Mhe. Mbelwa Kairuki (Balozi wa Tanzania Nchini China  ) Prof. F. Lekule (Mtendaji Mkuu wa International Tanfeeds Ltd), Francis Assenga (Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kilimo -TADB) wakati wa Kongamano la Biashara Viwanda na Uwekezaji kati ya China na Tanzania, mjini Guangzhou China juzi.

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanya mazungumzo na Taasisi mbili muhimu za kifedha na kiuchumi nchini china kwa ajili ya upatokanaji wa fedha za uwekezaji mkubwa kwenye miundo mbinu na viwanda nchini Tanzania husuan kwenye Sekta ya Kilimo.

Majadiliano hayo yalifanywa kati ya Ujumbe wa TADB ulioongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Francis Assenga alipokutana na Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya China (China Development Bank) Bwn. Chris kwenye Mkutano uliofanyika Shangrila Hotel, Guangzhou China wakati wa Kongamano la Pamoja la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na China.

Pande zote mbili zilikubaliana kuendelea na kuimarisha ushirikiano  utakaowezesha kupatikana kwa fedha kwenye uwekezaji wa miundo mbinu ya kilimo na viwanda vidogo vidogo vya uongezaji thamani kwenye mazao ya kilimo kwa wakulima nchini.

Aidha, TADB pia ilikuwa na majadiliano ya kina na Mfuko wa Maendeleo ya Africa wa Vhina (China African Development Fund) ambao hufanya uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo na ya kibiashara (Equity investmenta) kwenye nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.
Kusoma zaidi bofya hapa.

SHEIKH SHARIFF MAJINI KUFANYA KONGAMANO KUBWA IRINGA JUMAMOSI NA JUMAPILI HII

0
0
Sheikh Shariff Majini kutoka katika kituo cha Dua na Maombi Mabibo Mwisho jijini Dar es salaam, mwishoni mwa Mwezi Oktoba Jumamosi tarehe 28 na Jumapili tarehe 29 anataraji kufanya Kongamano kubwa pamoja na Dua katika Mkoa wa Iringa.
Kongamano linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa OLUFEA uliopo KITANZINI Manispaa ya Iringa Mjini. Kongamano litafanyika kuanzia saa saba mchana mpaka saa kumi naa mbili jioni.
Sheikh amelazimika kufanya kongamano Iringa kufuatia kila siku kupigiwa simu na waumini wa Iringa ili afike kwa ajili ya kuwasikiliza shida zao mbalimbali.

DAKTARI WA KANUMBA AMEIEEZA MAHAKAMA KUWA KANUMBA ALIFIA NYUMBANI

0
0
 Msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael akiwa na wazazi wake katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam akisubiri kusomewa mastahaka yanaymkabili jijini Dar es Salaam leo.
 Msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael akiongea jambo na wakili wake, Peter Kibatala wakizungumza jambo kabla ya kuanza kusomwa kesi yake ya kuua bila kukusudia jijini Dar es Salaam leo.
Msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael akitoka katika mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam mara baada ya kesi yake kumaliza kusomewa na kuhairishwa mpaka Jumatatu Oktoba, 23, 2017.
Msanii wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael akiwa nje ya mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa kesi ya kuua bila kukusudia ya msanii mwenzake Steven Kanumba.

Karama Kenyunko na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
DAKTARI wa familia ya msanii maarufu wa filamu nchini, marehemu Steven Kanumba, Dkt, Paplas Kagaia, ameileza mahakama Kuu ya Tanzania kanda Dar es Salaam Kanumba alifariki toka nyumbani baada ya kumpima na kukuta mapigo yake ya moyo hayakuwepo.

Dk, Paplas amedai hayo leo Oktoba 20, 2017 huu wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Sam Rumanyika.

Amedai kuwa, baada ya mdogo wa marehemu kumfuata hospitali kwake na kumwambia kuwa Kanumba amefariki, alichukua kipino cha sukari na shindikizo la Damu(pressure) na kwenda moja moja nyumbani kwake Sinza ambako baada ya kufika nyumbani kwake alimpima sukari na kukuta io kawaida lakini alipompima pressure haikuwepo kabisa. 

Daktari Huyo mwenye elimu ya stashada ya juu (Advance diploma) aliyejipatia Elimu yake chuo cha uuguzi cha jeshi cha Lugalo amedai kuwa, alikuwa daktari wa familia ya Kanumba kwa zaidi ya miaka mitano na anamiliki Hospitali yake binafsi ya St. Anna iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam alikuwa akimtibu Kanumba magonjwa ya kawaida na hakuwahi kugundua tatizo lake lolote. 

Mahojiano kati ya Dr Paplas na Wakili wa serikali Batlida Mushi yalikuwa kama ifuatavyo;

Wakili: Ulipata wapi taarifa kama ya kuugua kwa Kanumba?
Shahidi: Nikiwa naudumia wagonjwa kama kawaida nilipigiwa simu na Seth akiniomba niende kumuona Kanumba amedondoka, nikamwambia muda ule ulikuwa ni usiku sana aende kumchukua.

Wakili: kwani nini Seth akupigie wewe simu?
Shahidi: Nilikiwa daktari wa familia yao kwa miaka kama mitano hadi sita.

Wakili: Baada ya kukupigia simu, ulifanya nini?
Shahidi: Nilichukua vifaa vya mashine ya sukari na BP, niliingia chumbani kwake nikifuatana na Seth nilipofika nilikuta Kanumba amelala chini chali, nikampima sukari ilikuwa normal nikampima pressure mapigo ya moyo hayakuwepo kabisa.

Wakili:Baada ya kujua mapigo ya moyo hayapo ulifanya ulichukua hatua gani?
Shahidi: Nilimwambia Sethi Fanya umvalishe nguo wafanye utaratibu wa kumpeleka hospitali kubwa ya Muhimbili akafanyiwe Vipimo.
 
Wakili: Baada ya hapo ulifanya nini?
Shahidi: Baada ya kumvalisha nguo kwa kisaidiana na kijana mmoja wa jirani na mama mwenye nyumba tulimpeleka Muhimbili kitengo cha emergency.

Wakili: Mlipofika Muhimbili kitengo cha Emergency ulifanya nini?
Shahidi: Nilimuomba Dk tuliyemkuta pale ampime Kanumba na alipompima alisema kuwa ameshafariki.

DC SINYAMULE APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KUTOKA TAWI LA NMB SAME

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii .
MKUU wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule   amepokea Msaada wa  vifaa vyenye thamani ya Tshs. 10M  kutoka Benki ya NMB kwa  kwa ajili ya ujenzi wa Choo cha Wanafunzi wa Kike katika shule ya sekondari Kazita iliyopo kata ya Mhezi Same.

akizungumza wakati wa kupokea Msaada huo DC  Sinyamule  aliwashukuru NMB kwa vifaa hivyo vilivyojumuisha mabati, cement, mchanga, tofari, mawe, rangi na masink ya choo ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza tatioz la uhaba wa vyo vya watoto wa kike shuleni hapo. 

Dc Sinyamule aliwataka viongozi kuanzia bodi ya shule hadi Halmashauri kusimamia ujenzi wa vyoo hivyo na vikamilike kwa siku 45. Ili mwezi Novemba mwishoni tufanye uzinduzi wa vyoo hivyo. 

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya Aliwakumbusha fursa zilizopo Same kuwa ni pamoja na kufungua matawi mengine ya benki maeneo ya Ndungu na Mamba myamba kwani Wilaya inaendelea na uwekezaji mkubwa katika maeneo hayo. 

Naye meneja wa Benki hiyo Ndugu Mpimbi alieleza Benki hiyo ilivyoboresha huduma na kuwa ni benki inayoongoza kwa kurudisha faida kwa wateja katika mahadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja . 

alimaliza  kwa  kusema kuwa Kukamilika kwa vyoo hivyo kutafanya shule hiyo kutokuwa na upungufu tena wa vyoo jambo ambalo litasaidia sana watoto wa kike. 
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akipokea  Vifaa vya ujenzi na Saruji kutoka kwa Meneja wa NMB Wilaya ya Same.
Sehemu ya Vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na Benk ya NMB W ilaya ya Same
akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Benki ya NMB Wilaya ya Same.

DC KIGAMBONI AZINDUA MPANGO WA DARMAERT NA VIFAA VYA MAWASILIANO WAKATI WA DHARULA NA MAAFA

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa  akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa Mpango wa DarMaert na Vifaa vya Mawasiliano wakati wa Dharura na Maafa
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akikata utepe  kuashiria uzinduzi wa chumba cha Mawasiliano DarMaert na Vifaa vya Mawasiliano wakati wa Dharura na Maafa.
Sehemu ya Askari wa Jeshi la Zima Moto waliohudhuria uzinduzi wa mpango wa Dar Maert na Vifaa vya Mawasiliano wakati wa Dharura na Maafa.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

PROF. KABUDI ATOA UFAFANUZI KUHUSU MAKUBALIANO KATI YA TANZANIA NA KAMPUNI YA MADINI YA BARRICK

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ambaye ni Kiongozi wa Timu ya Tanzania katika majadiliano kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick kuhusu biashara ya madini ya Dhahabu nchini, atoa ufafanuzi zaidi kuhusu yale yaliyofikiwa baada ya kuwepo sintofahamu kwa baadhi ya watu kuhusu muafaka wa ripoti iliyotolewa jana tarehe 19 Oct 2017, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

WATANO WAFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA HIACE NA LORI

0
0
 Watu watano wamefariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Hiace kugongana na lori kisha kuwaka moto.
Ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Kyamyorwa wilayani Muleba mkoani Kagera. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Oktoba 20, saa 12:00 asubuhi.
 Amesema mwendo kasi wa dereva wa gari dogo la abiria ni chanzo cha ajali hiyo.
Ingawa Kamanda Olomi hakuwataja waliokufa, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango amesema miongoni mwao ni dereva wa gari dogo, kondakta na abiria watatu.
Amesema watu hao walishindwa kujiokoa kutokana na mlango wa gari kubanwa hivyo kushindwa kufunguka. (Picha kwa Hisani ya BukobaWadau Blog)

VETA CHANG'OMBE YAPATA MSAADA WA MAGARI TISA YA KUFUNDISHIA

0
0
Sehemu ya magari tisa yaliyotolewa na shirika la EGPAF.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
CHUO cha Ufundi Cha VETA Chang'ombe  kimepata msaada wa magari tisa kutoka katika shirika la Elizabeth Glasser Padiriatic  Foundation (EGPAF) yatakayotumika kwa ajili kujifunzia wanafunzi katika chuo hicho.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam, Habib Bukko amesema kuwa msaada wa magari ni mkubwa kutokana na changamoto walikuwa wanakabiliana nayo.

Bukko amesema kuwa chuo cha ufundi  kimekuwa hakina magari ya kutosha kwa ajili ya kujifunzia na taratibu za serikali zinataka magari yanunuliwe mapya lakini msaada huo ni hatua moja nzuri ya kusaidia chuo hicho.

Amesema kuwa watu wengine wenye mashirika wanaweza kuwasaidia magari yao ambayo wanataka kuyauza kwani kwao ni msaada mkubwa kutokana na mahitaji yaliyopo katika zaidi vyuo 700 vya ufundi.

Aidha ameesma kuwa zaidi vijana milioni 25 wanahitaji kupata mafunzo hivyo kuna umhimu wa kuwa rasilimali ya vifaa katika kuweza kuendana na idadi hiyo.

 Nae Mkurugenzi wa Uendeshaji wa  EGPAF, Jacquesdol Massawe amesema kuwa wanatambua umhimu magari hayo kwa ajili ya kuwafundishia vijana wakitanzania na kuweza kupata ujunzi na kuja kutumika katika uzaslishaji.

Amesema uchumi wa viwanda unahitaji kuwa rasilimali watu wenye ujuzi kuweza kutumika katika uzalishaji wa viwanda hivyo.
 Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam wa VETA, Habib Bukko akizungumza na waandishi habari juu ya msaada wa magari tisa yalitolewa na Shirika la EGPAF leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa EGPAF, Jaccquesdol Massawe akizungumza juu ya msaada  magari tisa jinsi yatavyotumika katika kufundishia vijana vyuo vya VETA, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha VETA Changombe,  Douglas Kipokola akizungumza namna ya kuyatumia magari hayo katika chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam wa VETA, Habib Bukko akipokea nyaraka za magari hayo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa EGPAF, Jaccquesdol hatika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI, SUBIRA MGALU ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI WA VITUO VYA UMEME KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (wapili kulia), akifurahia jambo na wahandisi na mafundi wa TANESCO alipotembela  mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kigamboni jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2017.
 Naibu Waziri, Mhe. Subira Mgalu(katikati), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANSECO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, (anayeshughulikia usafirishaji umeme), Mhandisi Kahitwa Bishaija, (kushoto), wakiwasili kwenye eneo la mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kigamboni jijini Dar es Salaam Oktoba 20, 2017.
 Wahandisi wa TANESCO wakimalizia kazi ya kufunga mitambo kwenye kituo cha Kigamboni.


NA  K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu ameendelea na ziara yake ya kujifunza kwa kukagua miradi mingine miwili mmoja wa ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme Kimbiji na kingine cha kupoza umeme cha Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2017.
Alhamisi Oktoba 19, 2017, Mhe. Mgalu alifanya ziara kama hiyo kwa kutembelea vituo viwili vya kupoza umeme vya Mbagala na Kurasini wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Akiwa Kigamboni, Naibu waziri ambaye alifuatana na Katibu Tawala wa Wilaya mpya ya Kigamboni, Bi. Rachel Mhando na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na viongozi wengine wa juu wa Shirika hilo, alianza kwa kukagua kituo cha Kigamboni ambapo aliwakuta mafundi wa TANESCO wakimalizia kufunga mitambo kwenye kituo hicho.
Aidha Naibu waziri alimalizia ziara yake kwa kutembelea eneo la ujenzi wa kituo kipya cha Kimbiji ambapo kazi ya kusafisha eneo la ujenzi nayo imekamilika na kinachosubiriwa ni kuwasili kwa vifaa ili ujenzi uanze.
Mheshimiwa Mgalu alisema kutokana na ongezeko kubwa la watumiaji wa umeme, vituo hivyo vitasaidia sana kuboresha huduma ya upatikanaji umeme hususan katika kipindi hiki ambacho serikali ya awamu ya tano imejielekeza kujenga uchumi wa viwanda na hitajio kubwa katika utekelezaji wa mpango huo ni upatikanaji wa umeme wa uhakika.
“Niwashukuru tu kwa ksuema, ziara yangu hii ni ya kwanza kwenye eneo hiki tangu niteuliwe na nimeona nije ili nijionee jitihada hizi za kuboresha hali ya umeme wilayani Kigamboni ambapo kuna uhitaji mkubwa wa umeme ,kutokana na ongezeko kubwa la watu.” Alisema.
Akieleza zaidi Mheshimiwa Mgalu alihimiza Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ambalo kwa niaba ya serikali ndilo linatekeleza mradi huo kuongeza kasi ya ujenzi ili hatimaye wananchi wapate huduma ya umeme katika hali bora zaidi.
Aidha Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Bi. Rachel Mhando, Aliishukuru serikali kwa kuleta mradi huo katika wilaya hiyo na kusema serikali wilayani Kigamboni itatoa kila aina ya msada ili kuhakikisha mradi huo mkubwa unakamilika.
“Hii ni wilaya mpya ni jambo la kushukuru kuwa katika kipindi kifupi wilaya inaletewa mradi mpya wa kuboresha umeme kwa kweli wananchi wana matarajio makubwa na mradi huu na sisi tumefarijika sana.” Alisema Katibu Tawala wa wilaya ya Kigamboni.




 Naibu waziri akipatiwa maelezo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usafirishaji umeme, Mhandisi Kahitwa Bishaija, (wapili kushoto). Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWATAKA WAFANYAKAZI MIZANI KUACHA RUSHWA.

0
0
Wafanyakazi wa mizani nchini wametakiwa kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kuachana na vitendo vya rushwa ili kuleta tija na ufanisi wa kazi zao 
katika usimamiaji na ulinzi wa barabara ambazo Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa katika ujenzi wake.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa, leo mkoani Shinyanga, alipokuwa akikagua  mzani wa Tinde (Shinyanga), na Mwendakulima (Kahama),  ambapo amesisitiza ushirikiano kati ya wafanyakazi hao na madereva ili kutatua changamoto zinazojitokeza katika  vituo vya mizani.

"Watumishi na madereva shirikianeni kutokomeza vitendo vya rushwa, kamwe msijihusishe kutoa wala kupokea rushwa ili kupata huduma za haraka, tukikubaini tutakuchukulia hatua kali za kisheria", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.
Aidha, ametoa wito kwa madereva wa magari ya mizigo wanaotakiwa kuwa na stika maalum za usafirishaji wa mizigo yao kufuata utaratibu wa kuchukua stika hizo mahali husika ili kuepusha usumbufu na msongamano wa magari katika vituo vya mizani.
Akiwa katika eneo la sehemu ya maegesho na kulaza magari mjini Kahama Naibu Waziri Kwandikwa, ametoa wito kwa viongozi wa Halmashauri hiyo kuchukua hatua kali kwa madereva wanaopaki nje ya eneo hilo, ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaoweza kufanywa na baadhi ya madereva hao.
Ameshauri kwa uongozi wa Halmashauri hiyo kuona namna ya kujenga maegesho mengine kama hayo ili kupata chanzo cha mapato na kusaidia kuujenga mji kuwa na Taswira nzuri.
Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani Shinyanga, Mhandisi Mibala Ndilindi, amethibitisha kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwa baadhi ya wafanyakazi wa mizani nchini ambapo amefafanua katika kupambana na suala hilo kwa watumishi wa mkoa wake tayari mwezi uliopita amewachukulia hatua za kinidhamu watumishi watatu wa mzani wa Mwendakulima.
Naye, Msimamizi wa shughuli za mzani wa Mwendakulima kutoka TANROADS Shinyanga, Bi Herieth Monjesa, amesema kuwa changamoto za msongamano wa magari katika mizani zinasabaishwa na baadhi ya madereva wa magari ya mizigo wanaotakiwa kuwa na stika maalum za usafirishaji wa mizigo yao kushindwa kufuata utaratibu, hivyo kupelekea usumbufu kwa wahudumu na watumiaji wengine wa mizani.  

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kwandikwa, amekagua barabara ya Uyovu-  Bwanga (KM 45), ambapo ujenzi wake kwa sasa umefika asilimia 98 na mkandarasi amebakisha kazi za ujenzi wa mifereji na uwekaji wa alama za barabarani.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mwenye suti), akiangalia namna shughuli za upimaji wa magari zinavyoendeshwa katika mzani wa Tinde, mkoani Shinyanga. Kushoto kwake ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), wa mkoa huo, Mhandisi Mibala Ndilindi.
 Msimamizi wa shughuli za mzani wa Tinde kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani Shinyanga, Bw. Lugembe Vicent (kushoto), akitoa taarifa ya kiutendaji ya mzani huo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa. Mzani huo unapima magari 300 kwa siku.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa, akiangalia namna watumishi wa mzani wa Tinde, mkoani Shinyanga wanavyopima na kurekodi taarifa za magari yanaoingia kupima uzito kwenye mzani huo.
 Magari yakiwa katika foleni kusubiri huduma za upimaji uzito ili kuendelea na safari kwenye mzani wa Tinde, mkoani Shinyanga. 
Muonekano wa barabara ya Uyovu- Bwanga (KM 45) kwa kiwango cha lami iliyopo mkoani Geita, ikiwa imekamilika kwa asilimia 98.
Viewing all 109609 articles
Browse latest View live




Latest Images