Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

Chipukizi 10 kutoka “Swahili Fashion Week Emerging Designer Competition” kuonesha mavazi yao mwezi disemba

$
0
0
Wabunifu 10 chipukizi kutoka sehemu mbalimbali nchini wamaechaguliwa kuingia katika shindano la kumi la kumtafuta mbunifu chipukizi bora lililopewa jina la “SFW Washington Benbella Emerging Designer Competition.”washiriki hao wametoka katika jumla ya washiriki 30 walituma maombi yao, na watapatiwa nafasi ya kuonesha nguo zao katika maonesho ya SWAHILI FASHION WEEK & AWARDS yatakayofanyika tarehe 1, 2, 3 mwezi December jijini Dar es Salam nchini Tanzania.

“Awamu ya kumi ya mashindao ya kumtafuta mbunifu chipukizi wa mwaka yamekuwa ya aina yake, si tu kiushindani bali ni ya kushangaza. Washiriki hawa kumi wamebeba sifa ya kuenzi dhamira ya maonesho ya mwaka huu. Macho na masikio yote ya washabiki wa mitindo yapo wazi kutazama mavazi ya kipekee katika kusherekea maadhimisho ya miaka kumi ya Swahili fashion week. Tunaomba kila mtu aweze kufika kushuhudia dunia mpya ya mitindo kutoka kwa watu wabunifu wapya katika setka ya mitindo.” Alisema Glory Urassa Afisa Mradi wa Swahili Fashion Week.

Kamati ya uchaguzi wa mwaka huu, iliundwa na mbunifu Jamilla Vera Swai, mbunifu Samuel Zebadayo, pamoja na mwanamitindo Rio Paul, walivutiwa na michoro ya kipekee na vitambaa vyenye ubora kutoka kwa vijana wenye hasira ya kutawala sekta ya mitindo.

Kwa miaka kumi iliyopita ,toka kuanzishwa kwa mashindano haya mwaka 2008, yamewza kukusanya Zaidi ya vipaji vichanga elfu moja kutoka sehemu mbalimbali afrika ambao wanaendelea kufanya kazi ya mitindo, kufungua nembo zao na kuonyesha mitindo yao katika majukwaa mbalibali duniani. Wafuatao ni washindi waliopita Shaabaz Sayeed (2016), Kulwa Mkwandule (2015), Medrad Mlowe (2014), Bhoke Chacha (2013), Philista Onyang’o (2012), Subira Wahure (2010), 2jenge Africa Mataley (2009) and Edwin Musiba (2008).

Kamati ya majaji ilikaa na kuchagua awamu ya kwanza ya watu kumi amabo ni Liberatha Alibalio, Charity Nyaimaga, Maryimmaculate Gervace, Emmanuel Kisusi, Agness Sixbeabeatus, Mohammed Juma, Anjali Borkhataria, Edina Ibrahim, Gisela Kaguo, na Jackline Ottaru. Mchakato wa kutaendelea hadi pale atakapopatikama mshindi mmoja tu wa mashindano haya, ambaye atapewa tuzo katika siku tatu na ya mwisho ya maonesho ya Swahili Fashion Week 2017, yatakayofanyika  Makumbusho ya Taifa kuanzia tarehe 1 hadi 3 mwezi disemba mwaka huu.

RAIA 21 WA DRC WATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUINGIA NCHINI BILA KUFUATA UTARATIBU

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT, RS –TABORA

JESHI la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia wahamiaji haramu 21 raia wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa tuhuma za kuingia nchini bila kufuata utaratibu. Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora (RPC) Wilbrod Mutafungwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari Ofisini kwake.

Alisema kuwa watuhumiwa hao wa uhamiaji haramu walikamatwa tarehe 17 mwezi huu wilayani Urambo baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema. Kamanda huyo wa Mkoa alisema kuwa baada ya wasamaria wema kutoa taarifa kwa Polisi ndipo waliweka mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao ni wa familia tano tofauti za kutoka DRC.

Alisema kuwa katika orodha hiyo wapo wanaume wawili, wanawake watano na watoto 14 ambao walikamatiwa Urambo baada ya kushuka katika gari la abiria la Saratoga linalofanya safari zake kutoka Kigoma hadi Tabora. Kamanda Mutafungwa aliongeza kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakitatafuta usafiri wa kwenda Tabora mjini kutoka Urambo na ndipo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata.

Alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na Uhamiaji na vyombo vingine kuwahoji sababu ya kuja nchini bila kufuata taratibu inagwa wao wanadai kuwa walikuja kutafuta Kambi ya Wakimbizi kufuatia machafuko yanayoendelea nchini  mwao. Kamanda Mutafungwa alisema watuhumiwa kutoka familia ya kwanza ni  Dieudonne Buloze (32), Kigwasa Mariya(20), Medianne Buloze(3) na Alber Buloze(1). Wengine ni Byamungu Mateus(38), Mulasi Nabunane(33), Busime Mateusi(13), Faida Mateusi(8), Mbamba Mateusi(6), Hadija Mateusi(3) ,Bereke Mateusi(2) na Lebinde Omary(60).

Aliwataja wengine walikamatwa kuwa ni Betie Kasongo(24) , Yoshuwa Ekombe(3) , Yosia Ekombe(miezi 10), Aline Chekanabo (28), Francoise Heva (9), Jistin Faiba (7) , Amida Faiba (6), Kikombe Sumaili(4) na Gulenne(miezi 10). Mmoja wa wahamiaji haramu hao Dieudonne Buloze alikiri kuwa walikimbia DRC kukimbia mapigano yanayoendelea , wakiwa wanatokea Kivu ambapo wavuka mpaka  kupitia ziwa Tanganyika na kujikuta wako upande wa Tanzania.

Alisema wamekuja Tanzania kutafuta hifadhi ili kuokoa maisha yao kutokana na mapigano yanayoendelea baina ya vikosi vya Serikali na Waaasi. Katika hatua nyingine Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora alisema kuwa watoto wawili wa shule ya Ncheli katika Kata ya Sungwizi wilayani Simbo wamefariki dunia baada ya kutumbukia katika kisima kilikuwa hakina uzito.

Alisema kuwa chanzo cha vifo hivyo ni wakati mtoto wa kwanza Mwashi Yohana alipoteleza na kuanguka kisimani wakati akijaribu kutaka kunywa maji na ndipo wa pili ajulikanaye kama Wande Shija alifariki baada ya kutumbukia katika kisima wakati akijaribu kumwokoa mwezie.

Kufuatia vifo hivyo Kamanda Mutafungwa alitoa wito kwa wakazi wote Mkoani hapa kuweka uzio katika visima vyote walivyovichimba wakati wa kiangazi na kuhakikisha wazazi wanawasindikiza watoto wao wakati wa kwenda na kutoka shule hasa kwa wale wa shule za awali.

SERIKALI KUJENGA MABWAWA 10 YA KUOGELEA, TANZANIA YAANZA KWA VISHINDO

$
0
0
Waogeleaji kutoka nchi mbalimbali pamoja na Tanzania waki-dive katika mashindano ya Cana Kanda ya tatu yaliyoanza jana kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini.

Kocha wa timu ya Tanzania, Michael Livingstone akisimamia mazoezi ya timu ya Tanzania katika mashindano ya Cana Kanda ya tatu yaliyoanza jana kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini.

Na Mwandishi wetu
SERIKALI imeahidi kujenga mabwawa 10 ya kisasa ya kuogelea kwa ajili ya kuendeleza mchezo huo hapa nchini.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hapa nchini, Dk Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa mashindano ya kanda ya tatu ya Afrika yanayoandelea kwenye bwawa la shule ya Kimataifa ya Heaven of Peace (Hopac).

Waziri Mwakyembe alisema kuwa wamefarijika sana na vipaji vya waogeleaji wa Tanzania katika mashindano hayo ambayo yameshirikisha jumla ya nchi sita ikiwemo ya Tanzania. Nchi nyingine ni Kenya, Uganda, Sudani, Afrika Kusini na Zambia.

“Nimesikitika sana kusikia kuwa kuna wawekezaji walikuja hapa kutaka kujenga bwawa la kuogelea kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huu na kukatishwa tamaa na baadhi ya watendaji wa wizara yangu,”

“Nawaahidi kulishughulikia suala hili kabla ya mwisho wa mwezi huu, nitakutana na Waziri wa Tamisemi na kuona ugumu upo wapi hasa kwa shule maarufu ya msingi ya Oysterbay ambayo ilikuwa iwe ya kwanza kujengewa bwawa la kisasa la kuogelea,” alisema Waziri Mwakyembe.

Alisema kuwa malengo yake ni kuona mchezo wa kuogelea unafikia kiwango cha juu kabisa kwani amegundua nchi ina vipaji vingi, lakini wanashindwa kufikia kiwango cha juu kutokana na kukosa miundombinu ya kisasa.

Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka aliipongeza serikali kwa ahadi hiyo ambacho ni kilio chao cha siku nyingi.

“Tumefarijika sana na ahadi za serikali, kama mnavyojua, tumekuwa tukiangaikia suala la kupata bwawa la kisasa la kuogelea miaka mingi, naamini mafanikio ya ahadi hiyo yataleta msisimko mpya kwa waogeleaji na wadau wake,” alisema Namkoveka.

Namkoveka pia aliwapongeza wachezaji wa Tanzania kwa kuanza kwa vishindi mashindano hayo na kutwaa medali 21 ambapo, nane ni za dhahabu. Waogeleaji, Sonia Tumiotto na Natalie Sanford kila mmoja alitwaa medali mbili za dhahabu katika mashindano hayo.

Waogeleaji wengine waliotwaa medali za dhahabu I Elia Imhoff, Emma Imhoff, Behnson Tara, Marin De Villard na timu ya relay kupitia kwa Collins Saliboko, Hilal Hilal, Sonia Tumiotto na Emma Imhoff.

KIVUMBI LIGI KUU KUANZA KURINDIMA KESHO

$
0
0

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea kesho Ijumaa Oktoba 20, 2017 kwa mchezo mmoja utakaokutanisha timu za Mwadui na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mwadui mkoani Shinyanga.

Ligi hiyo itaendelea Jumamosi Oktoba 21 kwa michezo sita itakayofanyika kwenye viwanja tofauti huku mechi nyingi zikipata fursa ya kuonyeshwa kwenye chaneli mbalimbali za Azam Tv kupitia king’amuzi cha Azam.

Michezo ya Jumamosi itakutanisha timu za Mbao na Azam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wakati Lipuli itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa ilihali Ruvu Shooting watakuwa wageni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Jumamosi hiyo hiyo Simba yenye mabadiliko kidogo kwenye benchi la Ufundi, itawaalika Njombe Mji kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam huku Ndanda ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Wakati Jumamosi hiyohiyo tena, Mtibwa Sugar wakicheza na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja tu - ambao ni kati ya Stand United na mabingwa watetezi, Young Africans ya Dar es Salaam - mchezo utakaopigwa Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Multichoice yatimiza miaka 20 kwa Mbwembwe.. Ofa kabambe kwa watakaodhuria maonesho Mlimani City!

$
0
0

Kampuni ya Multichoice Tanzania inatimiza miaka 20 toka kuanza kutoa huduma katika soko la Tanzania. Katika Kusheherekea maadhimisho ya miaka 20, Multichoice imeandaa maonesho ya siku 2 yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City kuanzia siku ya Alhamis tarehe 19/10/2017 na Ijumaa tarehe 20/10/2017 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Katika maonesho haya utapata kushuhudia maendeleo ya Teknolojia yetu ya tangu 1997 mpaka sasa na huduma mbali mbali zitolewazo na Multichoice. Kutakuwa na mabanda kadhaa likiwemo la Supersport, MNET, Maisha Magic Bongo, Fashion, Banda la watoto na mengine mengi.
Kutakua na Ofa kabambe ndani ya siku 2 za Maonesho, ambapo Mteja atajipatia full set ya DStv kwa sh. 59,000 tu hii ikijumlisha kifurushi cha mwezi mmoja BURE kwa king’amuzi cha HD cha Zappa. Kwa King’amuzi cha Explora Mteja atapata Kwa sh. 240,000 pamoja na kifurushi cha Compact cha mwezi mmoja BURE…
Ofa hii ni kwa siku za maonesho tu ambazo ni Alhamisi na Ijumaa hii tu, Hii si ya kukosa!!!

HUJAFA HUJAUMBIKA - HUYU NDUGU HANA MIKONO LAKINI.....

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI TORONTO KWA ZIARA YA KIKAZI NCHINI CANADA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka baada ya  kuwasili Toronto leo Oktoba 19, 2017 kwa ziara ya kikazi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka baada ya kuwasili Toronto Oktoba 19, 2017 kwa ziara ya kikazi. Kulia ni mkewe Mama Mary Majaliwa. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

MANARA: SIMBA HAINA TATIZO LA MISHAHARA


MICHUZI TV: Kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili Lulu yaanza kuunguruma mahakama kuu

SAA 24 BAADA YA KUJIUZULU KWA JACKSON MAYANJA, SIMBA YAMTAMBULISHA KOCHA MPYA MRUNDI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa klabu ya Simba leo mchana umemtambulisha kocha mpya atakayevaa viatu vya aliyekuwa kocha msaidizi Jackson Mayanja pamoja na meneja mpya anayechukua nafasi ya Dr Cosmas Kapinga.
Akitoa utambulisho huo mbele ya  waandishi wa habari,  Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa Kocha Masoud Djuma kutoka Rayon Sports ya nchini Rwanda na kocha bora wa msimu uliopita kupitia klabu hiyo anakuja kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyeachia ngazi kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia nchini Uganda.

Manara amesema kuwa, kabla ya kufikia makubaliano ya kuachana na Mayanja tayari walikuwa wameshaanza mazungumzo na kocha Djuma kuja kusaidiana na kocha Jospeh Omog kuinoa klabu hiyo.
Akizungumza baada ya kutambulishwa Kocha Djuma, amesema kuwa amekuja Simba kusaidiana na kocha Omog kuwezesha kupata mataji mbalimbali na sio kufanya maajabu kama watu watakavyodhani.

“Sijaja kufanya maajabu, nimekuja kuisaidia Simba kwa kidogo nilichonacho ili kuisogeza mbele zaidi ”, alisema Djuma huku akiweka wazi zaidi kuwa amekuja kufanya kazi na falsafa yake ni kocha mwenye pande mbili  mkali na mpole lakini huwa mkali pale ambapo mchezaji anataka kuharibu kazi.
Kocha Masoud Djuma akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulisha na afisa wa habari wa Simba Haji Manara (Kulia) akichukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyejiuzulu jana.
“Mimi ni mtu wa pande mbili kwa ufupi ni kama kiganja cha mkono, kina pande mbili. upande mmoja mpole lakini kwa upande mwingine ni mkali. Nimekuja hapa kufanya kazi ili kuipeleka Simba mbele na mimi nisogee mbele.”amesema Djuma.

Kuelekea mechi ya watani wa jadi Okotoba 28, Djuma ameweka wazi kuwa toka amezaliwa ameanza kusikia  Simba na Yanga kwahiyo anazijua vizuri , “Nimezaliwa nimekuwa nazisikia Simba na Yanga, kila sehemu kuna mechi zenye presha kubwa siwezi kuahidi lolote kuhusu mechi ya Simba na Yanga kwa sababu mpira una matokeo matatu.”
Ili kuliboresha benchi la ufundi, Klabu ya Simba imemtambulisha meneja anayerirhi mikoba ya Cosmas Kapinga, Richard Robert mwenye uzoefu wa masuala ya mpira na utawala ambapo awali aliwahi kuwa meneja wa wanja wa ndege na pia katika kituo cha JKM Park.
Afisa habari wa Simba Haji Manara akimtambukisha kocha mpya Masoud Djuma (Kulia) aliyechukua nafasi ya Jackson Mayanja pamoja na meneja mpya wa Simba Richard Robert leo katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. 

BREAKING: Majadiliano kati ya Tanzania na timu ya wawakilishi wa kampuni ya Barrick Gold yafikia tamati

$
0
0
Majadiliano kati ya Tanzania na timu ya wawakilishi wa kampuni ya Barrick Gold inayomiliki migodi ya madini hapa nchini yamekamilika na makubaliano kati ya pande hizo yametiwa saini leo tarehe 19 Oktoba, 2017 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Timu ya Barrick Gold Corporation ilikuwa imeongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo Prof. John Thornton wakati timu iliyowakilisha Serikali ya Tanzania imeongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.

Miongozi mwa mambo waliyokubaliana ni kutekeleza mwelekeo mpya wa biashara ya madini ambapo kutakuwa na mgawanyo sawa wa faida (yaani Tanzania kupata asilimia 50 na Barrick Gold Corporation kupata asilimia 50 ya faida) na kuundwa kwa kampuni ya ubia wa usimamizi wa migodi ya madini iliyopo Tanzania ambayo itakuwa na makao makuu yake Mwanza na ofisi ndogo Dar es Salaam nchini Tanzania badala ya nchini Uingereza.

Mengine ni kufunga ofisi za uhasibu na fedha zilizopo Johannesburg Afrika Kusini na kuhamishia Tanzania na kutekeleza masharti yote ya mabadiliko ya sheria mpya ya madini na rasilimali za nchi ya mwaka 2017.

Aidha, Barrick Gold Corporation imekubali kuwepo kwa wawakilishi wa Serikali katika bodi za migodi yake yote hapa nchini, kazi mbalimbali za kwenye migodi kufanywa na kampuni za Kitanzania, Migodi kutoa ajira za kudumu kwa wachimbaji, wachimbaji hao kuishi majumbani kwao badala ya kuishi kwenye makambi ya migodi na mashauri yote ya kesi mbalimbali kufanywa hapa nchini.

Kampuni ya Barrick Gold pia imekubali kutoa Dola za Kimarekani Milioni 300 sawa na takribani Shilingi Bilioni 700 kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kupitia biashara ya kampuni hiyo.

Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano hayo Prof. Thornton amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa msimamo wake unaojenga misingi ya biashara ya kuaminiana na uwazi, ambayo ni muhimu na ya namna yake kwa biashara katika karne hii ya 21.

Prof. Thornton amesema Barrick Gold Corporation watazingatia makubaliano haya na wanaamini kuwa yamefungua ukurasa muhimu utakaowezesha kufanya biashara kisasa.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amezipongeza timu zote mbili yaani Tanzania na Barrick Gold Corporation kwa kazi kubwa ziliyofanya kufikia makubaliano hayo na kwa kipekee amempongeza Prof. Thornton kwa nia yake thabiti ya kukubali kufanyika kwa mazungumzo na kukubali mambo yaliyofikiwa.

Mhe. Rais Magufuli amesema makubaliano hayo yataisaidia nchi kuzalishaji ajira zaidi, kupata manufaa mbalimbali yanayostahili ikiwemo fedha za kugharamia huduma za kijamii kwa wananchi na yanajenga msingi imara ambao utaiwezesha Tanzania kunufaika na rasilimali zake za madini.

Mhe. Dkt. Magufuli amemuagiza Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Kabudi kuunda timu zitakazoshughulikia biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi pamoja na migodi mingine ya dhahabu haraka iwezekanavyo ili nchi iweze kunufaika ipasavyo.

“Nataka machimbo yote ya dhahabu mchakato kama huu ufanyike, pia nakuagiza Prof. Kabudi biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi nako ni lazima kufuate utaratibu huu, asiyetaka aondoke” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Pia Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi hizi badala ya baadhi yao kuzibeza kwa kuwa zina manufaa kwa taifa na wananchi wake. 
Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

19 Oktoba, 2017 

 Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Profesa John L. Thornton akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Jumanne jioni tayari kushiriki katika mazungumzo ya mwisho na hatimaye makubaliano baina ya Kamati ya serikali na timu ya wataalamu wa kampuni hiyo kuhusiana na makinikia pamoja na biashara ya madini kwa ujumla. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki  Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp.Profesa John L. Thornton alipokutana nae wakati wa kupokea ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea  na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp.Profesa John L. Thornton alipokutana nae wakati wa kupokea ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp. Profesa John L. Thornton akiwa na Afisa Uendeshaji wa Barrick Gold  Richardc William huku Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Florens Luoga nao pia wakiweka saini ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp. Profesa John L. Thornton akiwa na Afisa Uendeshaji wa Barrick Gold  Richardc William huku Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Florens Luoga nao pia wakiweka saini ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na  timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu bishara ya madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 19, 2017

Naibu Waziri – Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa mgeni rasmi Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya SACCOS

$
0
0
 Mgeni Rasmi, Naibu Waziri – Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa akiangalia sehemu ya bidhaa za chakula zilizosindikwa kutoka katika Vikundi vilivyoanzishwa chini ya  Ushirika wa Akiba na Mikopo wa TANESCO (TANESCO - SACCOS) katika Viwanja vya Chuo cha Mipango wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya SACCOS inayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Dodoma
 Naibu Waziri – Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa akinunua dagaa walioongezwa thamani kutoka kwa kina Mama wa MWACIWOTE SACCOS ya  Jijini Mwanza. SACCOS hiyo imeundwa na kina Mama Waalimu wa Shule za Msingi na Sekondari
 Mgeni Rasmi, Naibu Waziri – Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa akipa maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Ngome SACCOS Brigedia Jenerali Charo Hussein Yateri namna ambavyo inajiendesha kwa mafanikio makubwa ikiwa na Wanachama zaidi ya 12,500 nchini katika Viwanja vya Chuo cha Mipango wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya SACCOS inayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Dodoma
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri – Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa akipa maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa TANESCO SACCOS Bibi Somoe Ismail namna ambavyo inajiendesha kwa mafanikio makubwa ikiwa na Wanachama zaidi ya 5,612 nchini kote katika Viwanja vya Chuo cha Mipango wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya SACCOS inayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Dodoma

DKT. KIGWANGALLA ATOA SIKU SABA KWA MIFUGO, MATREKTA NA VIFAA VINGINE KUTOKA NJE YA NCHI KUONDOLEWA NDANI YA PORI TENGEFU LOLIONDO

Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Kuanza Hivi Karibuni - Waziri wa Oman

$
0
0
Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi akinywa maji toka katika kisima cha maji ya baraka kilichopo katika eneo la ulipojengwa msikiti wa kwanza pwani ya mashariki katika eneo la Kaole wilayani Bagamoyo wakati wa ziara yakutembelea eneo la Bandari ya Bagamoyo iliyopo Mbegani, maeneo ya uwekezaji na historia wilayani Bagamoyo leo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwaonyesha eneo la bahari ujumbe kutoka Serikali ya Oman unaoopngozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi (mwenye miwani mwenyeusi) walipotembelea eneo la Bandari ya Bagamoyo iliyopo Mbegani katika ziara ya kutembelea maeneo ya uwekezaji na historia wilayani Bagamoyo leo. Mwenye vazi la kitenge ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaji Majjid Hemed, Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya wakitoka katika Bandari ya Bagamoyo wakati wa ziara ya Waziri huyo katika maeneo ya uwekezaji kiuchumi (EPZA), maeneo ya kihistoria la Kaole na eneo itakapojengwa bandari mpya.

Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Utalii wa Oman Bi. Maitha Saif Majid Al- Mahrouqi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi, Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. Al Mahruqi na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majjid Hemed wakimsikiliza mhifadhi ya makumbusho ya mali kale ya Kaole walipotembelea eneo hilo leo.
Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania mara baada ya kutembelea eneo itakapojengwa bandari mpya wilayani Bagamoyo leo. Kushoto ni Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. Al Mahruqi, Balozi wa Tanzania nchini Oman Abdallah Kilima, Naibu Waziri wa Utalii wa Oman Bi. Maitha Saif Majid Al- Mahrouqi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo,Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya, Waziri wa Uwekezaji wa Oman Salem Bin Nasser Al Ismaily. 
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO

LIGI DARAJA LA KWANZA (FDL) KUENDELEA WIKIENDI HII

$
0
0
Raundi ya Sita ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL), itaendelea kesho Ijumaa Oktoba 20, 2017 kwa mechi za makundi yote matatu.

Katika Kundi ‘A’, Mvuvumwa FC ya Kigoma, watacheza na Mgambo JKT katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mvuvumwa anatumia Kanuni ya 6 (1) na (2) kuhamishia mechi zake za nyumbani Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kutoka Uwanja wa Tanganyika, Kigoma.
Mechi nyingine kwenye kundi hilo itafanyika Jumapili Oktoba 22, mwaka huu kwa michezo mitatu.
Mechi hizo ni kati ya Kiluvya United na Mshikamano kwenye Uwanja wa Filbert Bayi, ilihali African Lyon itacheza na Ashanti United kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Friends Rangers itapambana na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam, Dar es Salaam.
Katika Kundi ‘B’ siku hiyo ya Ijumaa Oktoba 20, mwaka huu Polisi Dar itacheza na Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Azam wakati michezo mingine katika kundi hilo ikichezwa Jumamosi na Jumapili.

Jumamosi Mbeya Kwanza itacheza na JKT Mlale Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani na Jumapili Polisi Tanzania watawakaribisha KMC kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Ushirika Moshi, huku Mawenzi Market ya Morogoro wakiwaalika Mufindi United kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Katika Kundi ‘C’ kutakuwa na mchezo mmoja siku ya Ijumaa Oktoba 20, 2017 Pamba SC ya Mwanza itacheza na Alliance Schools nayo ya Mwanza kwenye Uwanja wa Nyamagana huko Mwanza na michezo mingine itafanyika Jumamosi na Jumapili.
Michezo ya Jumamosi itazikutanisha Biashara Mara dhidi ya JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Karume Mara,Transit Camp itakuwa mwenyeji wa Dodoma FC kwenye Uwanja wa Kambarage Mjini Shinyanga,wakati mchezo mwingine wa Kundi C, Toto Africans ya Mwanza itacheza na Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

MAONESHO YA VIWANDA VYA TANZANIA DESEMBA 7 HADI 11, 2017 VIWANJA VYA SABASABA

WAZIRI DKT. MWAKYEMBE AZINDUA MASHINDANO YA KUOGELEA YA KANDA YA TATU

$
0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwasili katika shule ya Heaven of Peace kwa ajili ya kufungua mashindano ya kanda ya tatu ya kuogelea yaliyoshirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan pamoja na nchi za kanda ya nne ambazo ni  Afrika ya Kusini na Zambia leo jijini Dar es Salaam.
 Waogeleaji kutoka Tanzania wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu yaliyofunguliwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe leo Jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wa mashindano ya kuogelea kutoka nchi za Afrika Kusini, Sudan, Uganda, Zambia na Tanzania wakiimba wimbo wa taifa wa Tanzania pembeni ya bwawa la kuongelea wakati wa mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu leo Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kanda ya tatu ya kuogelea yaliyoshirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan pamoja na nchi za kanda ya nne ambazo ni South Afrika na Zambia leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan, Afrika Kusini na Zambia wakichupia majini kushindana wakati wa mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu yaliyofunguliwa leo katika shule ya Heaven of Peace jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (watano kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa kuogelea pamoja na waratibu wa mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu baada ya kufungua mashindano hayo leo jijini Dar es Salaam katika shule ya Heaven of Peace na kushirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan pamoja na nchi za kanda ya nne ambazo ni  Afrika ya Kusini na Zambia leo jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM

Ziara ya ​Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland CIARAN CANNON jijini Mwanza

$
0
0
 CIARAN CANNON,WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA MAENDELEO YAKIMATAIFA WA JAMUHURI YA IRELAND,AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MJI WA MISUNGWI KOANI MWANZA WAKATI WA UZINDUZI WA AWAMU YA PILI YA PROGRAM YAKUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA,DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA WALAYANI MISUNGWI.
 WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA MAENDELEO YA KIMATAIFA WA JAMHURI YA IRELAND CIARAN CANNON AKIZINDUA AWAMU YA PILI YA PROGRAM YA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI MISUNGWI.
MHE. CIARAN CANNON,WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA MAENDELEO YAKIMATAIFA WA JAMUHURI YA IRELAND,KATIKATI NI RUAIRI DE BURCA,MKURUGENZI WA SHIRIKA MISAADA LA IRELAND,WA MWISHO PAUL SHERLOCK,BALOZI WANCHI YA  IRENLEND.
 WAZIRI CANNON AKIZUNGUMZA NA MAAFISA WA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO LA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA.

Ziara ya Waziri January Makamba visiwani Zanzibar yaingia siku ya pili

$
0
0
  Imebainika kuwa Bandari ya Zanzibar ni miongoni mwa Vyanzo vya Mapato vinavyopelekea ukuaji wa uchumi baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na fursa zilizopo katika nyanza za biashara. 
Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Captain Abdallah Juma Abdallah katika siku ya pili ya ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ambapo amepata fursa ya kutembelea Bandari ya Zanzibar.
Katika siku ya pili ya ziara yake ya siku saba Visiwani Zanzibar Waziri Makamba amebainisha kuwa lengo la ziara yake ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa masuala waliyokubaliana katika vikao baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar katika vikao vya mashirikiano.
"Niko Zanzibar kwa ziara ya kikazi na nimejikita zaidi katika kushughukikia masuala ya uchumi ikiwa ni pamoja na masuala ya Bandari, Forodha, Kodi na kubaini changamoto zilipo, utekezaji wa maazimio yaliyokubaliwa katika vikao vya majadiliano na kuangalia maeneo mapya yanayohitaji kuingizwa katika mfumo wa utatuzi," Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba amesema kuwa kuwepo kwa bandari ni ufanisi kwa uchumi na ni namna bora ya kuimarisha  Muungano  na ustawi wa Zanzibar na pande zote mbili za Muungano hazina budi kuondoa changamoto zilizopo kwa manufaa ya wote.
Waziri Makamba pia amepata fursa ya kutembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Mapato Zanzibar na kuwafahamisha kuwa lengo la Serikali zote mbili ni kuhakikisha kuwa pande zote mbili za Muungano zinanufaika na fursa za uchumi zilizopo, na kila upande unufaike na fursa zilizopo katika mambo ya Muungano na yale yasiyo ya Muungano.
Katika ziara hiyo Waziri Makamba amewataka  watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania upande wa Zanzibar kuzifanyia kazi changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza kwa haraka, kupunguza urasimu na kuongeza elimu kwa umma ili kujenga uelewa kwa wananchi  juu ya mambo yanayopaswa kuzingatiwa na yale yasiyopasa ili kuondoa vikwazo vinavyojitokeza katika bandari ili kuondoa malalamiko ya wananchi.
Nae Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  kwa upande wa Zanzibar Bw. Mcha Hassan Mcha amesema kuwa ni vema wananchi wazingitae kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ikiwa pamoja na kupata risiti halali kwa kila bidhaa wanazonunua ili kuepuka usumbufu pindi wasafirishapo bidhaa baina ya Tanzania bara na Zanzibar. 
Ziara ya Waziri Makamba visiwani Zanzibar itaendelea kesho kwa kutembelea miradi mbalimbali ya Mazingira.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba (kushoto) akimsikiliza Kapteni Abdallah Juma Abdallah Mkurugenzi Mkuu wa Bandari - Zanzibar alipokuwa akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa kazi za bandari mara baada ya Waziri Makamba kupata fursa ya kuwatembelea.
 Viongozi waandamizi wa Bandari - Zanzibar wakifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba alipotembelea bandari hiyo hii leo kujionea utendaji kazi wao na kuwapa fursa ya kuianisha changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya kukabiliana nazo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba (katikati) akifafanua jambo kwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar  wa (pili kulia). Waziri Makamba amefanya ziara ya kutembelea ofisi zao na kupata fursa ya kufanya majadiliano kwa manufaa na ustawi wa Muungano wetu. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akiwa katika kikao na Menejimenti ya Bodi ya Mapato Zanzibar. Wa pili kushoto ni Kamishna wa Bodi Bw. Amour Hamil Bakari na Bi. Khadija Shamte  Naibu Kamishna. Waziri Makamba yuko ziarani Zanzibar kutembelea Taasisi za Muungano na zile zisizo za Muungano.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango akutana na Wafanyabiashara Jijini Mwanza

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji jana amekutana na wafanyabiashara Jijini Mwanza kwa ajili ya kusikiliza na kutatua baadhi ya kero za kibiashara kutoka kwa wafanyabiashara hao chini ya chama chao cha TCCIA.
Dkt.Kijaji aliwahakikishia wafanyabiashara hao kwamba serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara huku akibainisha kwamba mashine za kutolea stakabadhi EFD's sasa zinatolewa na Mamlaka ya Mapato nchini TRA na hivyo wafanyabiashara hao wataondokana na baadhi ya kero walizokuwa wakikumbana nazo kutoka kwa mawakala wa mashine hizo ikiwemo kuzinunua kwa bei kubwa.
Awali wafanyabiashara hao walilalamikia suala la machinga kupanga bidhaa zao kando ya milango ya maduka yao ambapo Naibu Waziri Kijaji aliwasihi kuwa na subira wakati serikali utaratibu wa kuwasajili na kuwapatia machinga vitambulisho kama ilivyoelezwa kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 na hatimaye kuwaboreshea maeneo yao ya kufanyia biashara. Na Binagi Media Group


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji (aliyesimama), akizungumza na wafanyabiashara Jijini Mwanza jana. Wengine ni Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Ernest Dundee (wa kwanza kushoto), Injinia Boniphace Nyambele aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoa wa Mwanza Elibariki Mmari (kulia).

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoa wa Mwanza Elibariki Mmari, akizungumza kwenye kikao hicho
Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria kikao hicho akiwemo Makamu wa Rais wa TCCIA, Joseph Kahungwa (kushoto)

Baadhi ya wafanyabiashara Jijini Mwanza ambao walihudhuria kikao cha majadiliano baina ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji.
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images