Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1970 | 1971 | (Page 1972) | 1973 | 1974 | .... | 3286 | newer

  0 0

   Kwa idhini waliyopewa na Ubalozi wa Marekani  watauza kwa mnada wa hadhara  Funicha za nyumbani na ofisini,Vifaa vya tehama, Gari, Generator na Digital Voltage Stablizer  tarehe 21 October, 2017 Jumamosi saa 4:00 asubuhi. Mnada utafanyika Golden Resort Sinza,  Lion Street.

  Fenicha nyumbani na ofisini pamoja pamoja na vifaa vya tehama zitaanza kuuzwa kuanzia saa 4:00 asubuhi: Sofa set, Recliner, Wing chairs, Chest drawer, Dressers,  China base, Hutch, Credenza, Entertainment Centre, Coffee table, Meza za chakula /Viti, Meza za ofisi/Viti, Book case, Garden table/ Chairs,  Carpet, Vitanda ,Magodoro, Fridge, Freezer, Washer, Dryer, Majiko ya umeme, A/c split units, Maturubahi, Computer set, Pressure washer,  Air compressor na vingine vingi.

  Generator, Gari na AVR vitaanza kuuzwa kuanzia saa 6:00 mchana: 

  MASHARTI YA MNADA:
  Mnunuzi  wa Fanicha na Voltage Stabilizer atatakiwa kulipa malipo yote kwa keshia (cashier). Na mnunuzi wa Gari na Generator  atatakiwa kulipa 25% pale pale na salio lilipwe ndani ya siku 4 za kazi  mwisho wa kulipa tarehe 26 October 2017, saa 10:00 jioni Ubalozi wa Marekani. ukishindwa kulipa kwa muda huo Gari/ Generator litauzwa  kwa mshindi mwingine aliyefata  na dhamana haitarudishwa.

  Mali zote zitauzwa kama zilivyo bila dhamana. Malipo ni pesa taslimu (hundi na miamala haipokelewi). Mnunuzi atawajibika kulipa ushuru na kodi zingine zote.(TRA watakuwepo mnadani). Mali yote iliyouzwa itatakiwa kuondolewa baada ya kulipa malipo yote pamoja na kidi

  Kila mtu atatakiwa kuwa na bid namba itakayo patikana getini.

  Kwa maelezo zaidi waone:
  UNIVERSAL AUCTION CENTRE 
  PLOT NO: 5 “E” LION STREET SINZA                       DAR ES SALAAM
  CELL NO:  0754 284 926, 0757 284 926              E-mail: universalauction@hotmail.com  0 0  0 0
  0 0

  Timu ya wataalamu kutoka Jukwaa la Haki Jinai iliyoko mkoani RUVUMA imetembelea magereza ya KITAI na MBINGA pamoja na Kituo cha Polisi Wilaya ya MBINGA. 

  Timu hiyo ya wataalamu inayoongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome imekutana na kuzungumza na mahabusu na wafungwa walioko katika magereza hayo kuhusiana na changamoto wanazokabiliana nazo wakiwa ndani ili kuweza kupata haki zao kwa wakati.

  Timu hiyo imetumia nafasi hiyo kutoa huduma na ushauri kwa wafungwa na mahabusu hao huku ikiwataka kuishi vyema wakiwa katika magereza. Timu hiyo pia imewataka wafungwa na mahabusu hao kuhakikisha wanaishi kwa kutii sheria bila ya shuruti na hivyo kuwa raia wema.

  Timu hiyo ilipotoka katika magereza hayo ilitembelea Mahakama ya Wilaya ya Mbinga na kuwasilisha changamoto zinazowakabili wafungwa na mahabusu walioko katika magereza ya Mbinga na Kitai ili kuweza kuhakikisha mahakama hiyo inayafanyia kazi malalamiko ya watuhumiwa hao.

  Ziara hiyo ni miongoni mwa ziara ambazo zimeshafanyika katika mikoa ya Iringa na Njombe zilizolenga kutatua changamoto zinazowakabili wananchi walioko jela na vizuizini katika harakati za kupata haki zao kwa wakati.

  Ujumbe huo ambao unajulikana kama jukwaa la haki jinai unamshirikisha Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) Biswalo Mganga, Naibu Mkurugenzi Upelelezi Makosa ya Jinai nchini (DDCI) Charles Kenyela, Ofisi ya Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Magereza na Jeshi Polisi.


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba ameanza ziara ya kikazi ya siku saba visiwani Zanzibar. Katika siku ya kwanza Mhe. Makamba amepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kubaini fursa na changamoto zinazowakabili na kuona namna bora ya kupata ufumbuzi.

  Miongoni mwa changamoto zilizojadiliwa na kuwekewa mikakati ya utekelezaji ni pamoja na masuala ya kodi, namna ya kunufaika kutoka na fursa zilizopo baina ya pande zote mbili za Muungano na kuondoa vikwazo vinavyotokana na changamoto hizo ili kuleta ufanisi.

  Mhe. Makamba amewahakikishia wana juimuiya hao kuwa Ofisi yake itaratibu vikao kati ya Ofisi yake na wafanyabiashara hao ili kupata fursa ya kutoa mrejesho wa utekelezaji wa mambo waliyokubaliana.

  Mbali ya kukutana na wafanyabiashara hao Waziri Makamba pia amepata fursa ya kutembelea Vyombo mbalimbali vya Habari hapa Unguja kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Muungano. Vyombo vilivyotembelewa ni pamoja na Zenji FM na Zenji Tv, Bahari FM na Cocunut FM.

  Ziara ya Waziri Makamba katika siku pili atatembelea Miradi mikubwa ya Mazingira na kuwa na Vikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRB).
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akizungumza na wanajumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar (hawapo pichani). Kikao hicho kimefanyika hii leo eneo la Kinazini Zanzibar. Wengine katika picha ni viongozi wa Jumuiya hiyo.
  Sehemu ya wafanyabiashara wa Zanzibar wanaounda Jumuiya ya Wafanya Biashara wa Zanzibar wakiwa katika kikao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba aliyewaalika kujumuika kubadilishana uzoefu na kuwaomba waainishe changamoto zinazowakabili na kuona namna bora ya kuzipatia ufumbuzi.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akisalimiana na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano katika Serikali ya awamu ya nne Mhe. Mohammed Seif Khatibu ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Zanzibar Media Coorporation, Waziri Makamba alipata pia wasaa wa kufanya mahojiano katika chombo cha Habari cha Zenji FM na Zenji TV.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akifanya mahojiano maalumu katika Kituo cha Redio cha Cocunut FM.

  0 0

  Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akimsikiliza Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Engie, Johan Kerrebroeck (wa pili kushoto) katika Ofisi ya Waziri jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Kamishna Msaidizi wa Nishati-Maendeleo ya Nishati, James Andilile (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Haji Janabi (wa pili kulia) na Mhandisi Msafiri Baraza kutoka Wizara ya Nishati.
  Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akiwa na Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Engie, Johan Kerrebroeck katika Ofisi ya Waziri jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Engie, Johan Kerrebroeck (wa kwanza kulia) akisalimiana na Mhandisi Nishati Mkuu, Salum Inegeja katika Ofisi ya Waziri wa Nishati jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishna Msaidizi wa Nishati-Maendeleo ya Nishati, James Andilile.

  Na Teresia Mhagama, DSM
  Waziri wa Nishati,  Dkt Medard Kalemani ameeleza kuwa jumla ya kaya 3000 zitasambaziwa nishati ya Gesi katika Jiji la Dar es Salaam ndani ya miaka miwili au zaidi mara baada ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo mwezi Aprili mwaka 2018.

  Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa  kampuni ya Engie ya Ufaransa, Johan Kerrebroeck ambaye alifika wizarani ili kueleza nia ya kampuni yake katika kuwekeza kwenye mradi huo pamoja na miradi mingine ya uzalishaji Umeme kwa kutumia Gesi Asilia ukiwemo wa Somanga Fungu wa megawati 240.

  Dkt Kalemani alisema kuwa mradi huo wa usambazaji Gesi  utaelekezwa  pia katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo kaya zaidi ya 1500 zinatarajiwa kufaidika na mradi husika.
    
  “ Hatutaishia katika mikoa hiyo tu bali baada ya hapo tutasambaza katika mikoa mingine nchini kama Morogoro, Dodoma na Pwani  na katika magari,” alisema Dkt. Kalemani.

  Dkt. Kalemani alisema kuwa, usambazaji wa Gesi majumbani utasaidia kutunza mazingira kwani utapunguza matumizi ya Mkaa ambayo ni zaidi ya asilimia 90 nchini.

  Waziri wa Nishati, aliikaribisha kampuni ya Engie  kuwekeza katika mradi huo wa usambazaji Gesi kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

  Kuhusu suala la kuwekeza katika mradi wa uzalishaji Umeme wa megawati 240 kwa kutumia Gesi Asilia wa  Somanga Fungu, Dkt Kalemani alisema kuwa upembuzi yakinifu wa mradi huo utakamilika mwezi Aprili mwaka 2018 hivyo baada ya hapo ndipo hatua nyingine za uendelezaji mradi zitakapoanza kufanyika kwa kukaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

  Kwa upande wake, Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa  kampuni ya Engie, Johan Kerrebroeck alitumia fursa hiyo kumpongeza Dkt. Kalemani kwa kuteuliwa kuwa Waziri mwenye dhamana ya Nishati nchini.

  Aidha alisema kuwa kampuni yake ina uzoefu wa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya Nishati katika nchi mbalimbali duniani  ikiwemo Peru na Mexico. Nchini Tanzania, kampuni hiyo imewekeza katika mradi mdogo wa Umeme Jua wa Kilowati 16 katika Kijiji cha Ketumbeine mkoani Arusha.

  Kampuni ya kimataifa ya Engie imejikita katika uendelezaji wa miradi ya  Umeme, Gesi Asilia na huduma nyingine za Nishati  ambapo inafanya shughuli zake katika nchi  70 duniani.

  0 0

  Muigizaji wa Filamu nchini, Elizabeth Michael "Lulu" akiwa katika Mahakama kuu Dar es salaam akisubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi inayomkabili ya mauaji ya bila kukusudia. Lulu anakabilia na kesi ya kifo cha aliyekuwa muigizaji mwenzake wa filamu za Kibongo, Marehemu Steven Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012 jijini Dar es salaam. Kulia ni Mama wa Muigizaji huyo.

  HABARI KAMILI ITAKUJIA BAADAYE KIDOGO

  0 0

  Waziri wa kazi, ajira, sera, bunge, vijana na wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amelipongeza Shirika la NSSF kwa kuwa mfano wa kuigwa katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Waziri mkuu aliyasema hayo katika mkutano wa wadau wa NSSF unaoendelea katika Kituo cha kimataifa cha mikutano AICC, Arusha

  Waziri wa kazi pia alipongeza NSSF kwa kuandaa mkutano wa wadau unaofanyika hapa jijini Arusha, alisema mkutano huo siyo muhimu kwa NSSF na wadau tu bali pia kwa maendeleo na ustawi wa Taifa letu. Pia alifurahi kupata  nafasi ya kufuatilia utendaji wa NSSF pamoja na kuona moja kwa moja kutoka kwa wadau wa NSSF.
  Pia aliwapongeza  wadau wa NSSF kwa kuitikia wito wake wa kuja kushiriki ili kupata taarifa za utekelezaji wa maazimio waliyokubaliana mwaka jana, taarifa za utendaji na kuchangia mawazo yatakayoleta tija ya kulijenga Shirika. Aidha, aliwapongeza Wageni mbalimbali katika mkutano huo ambao ni pamoja na Mhe. Anthony Mavunde, Katibu Mkuu Ndg. Eric Shitindi, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA na Wakurugenzi wa Mifuko mingine ya Pensheni.

  Vile vile Waziri wa kazi alitoa pongezi kubwa kwa namna ambavyo NSSF  ilivyojitolea katika kutekeleza jukumu la kukuza Uchumi wa Viwanda  kwani alisema Ujenzi wa Taifa si jukumu la Serikali Kuu peke yake bali ni la kila Mtanzania mmoja mmoja, taasisi na makampuni, na ndio maana NSSF pamoja na kuwa na jukumu la hifadhi ya jamii kwa mujibu ya sheria yake husika, imeona haja ya kupanua wigo wa uwekezaji wake na kuelekea katika viwanda jambo ambalo litaongeza ajira, kuongeza uzalishaji, na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla. 
   Waziri Mhagama alitoa  mfano katika uwekezaji wa NSSF  katika kukuza viwanda tumeshuhudia uwezekano wa kuzalisha ajira za moja kwa moja kwa Watanzania kutoka na uwekezaji ilioufanya katika viwanda mbali mbali. Nichukue fursa hii kuipongeza NSSF kwa kutoa mkopo wa shilingi bilioni 3.1 kwa lengo la kuongeza uzalishaji katika kiwanda cha madawa kilichopo Kibaha chini ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). Katika kiwanda hiki ambapo ajira 100 zimezalishwa. Uzalishaji wa viuadudu ulianza Mwezi Desemba 2016 na mpaka sasa kiwanda kimezalisha jumla ya lita 327,400 ambazo ziliuzwa katika masoko ya ndani na nje.

  Shirika lilitoa Mkopo kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanda cha Chaki kilicho chini ya Usimamizi wa Halmashauri ya Maswa, Mkoani Simiyu mnamo mwezi June, 2017. Mkopo huu kwa ujumla utaongeza uzalishaji wa chaki kutokea vipande 432,000 vya chaki nyeupe (sawa na  Katoni 180) kwa siku hadi vipande milioni 4.8 vya chaki nyeupe na za rangi (sawa na Katoni 2,000) kwa siku. Ongezeko la uzalishaji huu wa chaki utasaidia kuendeleza Sera ya Serikali ya “Elimu Bila Malipo” kwani itasaidia kupunguza mahitaji makubwa ya chaki katika shule za awali na msingi. Jumla ya Ajira 100 za moja kwa moja zinatarajiwa kutokana na uwekezaji huu.
   Pia aliwapongeza NSSF kwa kushirikiana na PPF, na Jeshi la Magereza kupitia Kampuni ya Mkulazi, wamewekeza katika Mradi mkubwa wa shamba la miwa na Kiwanda cha Sukari kilichopo Mbigiri ambapo tayari hatua za upandaji miwa zimeanza nami nikiwa miongoni mwa j waliopata fursa ya kupanda miwa yamwanzo kabisa. 

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  Meneja Uhusiano wa Multi Choice Tanzania Johnson Mshana akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusiana na shamra shamra mbalimbali katika siku hiyo ya Kampuni ya Multichoice Tanzania kutimiza miaka 20 toka kuanza kutoa huduma katika soko la Tanzania.
  Meneja Uendeshaji Baraka Shelukindo akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu Kampuni ya Multichoice Tanzania kutimiza miaka 20 toka kuanza kutoa huduma katika soko la Tanzania. Baraka amesema kuwa katika Kusheherekea maadhimisho ya miaka 20, Multichoice imeandaa maonesho ya siku 2 yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City kuanzia siku ya leo Alhamis tarehe 19/10/2017 na kesho Ijumaa tarehe 20/10/2017 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. "Katika maonesho haya utapata kushuhudia maendeleo ya Teknolojia yetu ya tangu 1997 mpaka sasa na huduma mbali mbali zitolewazo na Multichoice",amesema Baraka.
  Mkuu wa Channel ya Africa Bongo Magic Barbara Kambogi akifafanua zaidi kuhusiana na hafla hiyo,alisema kuwa Kutakuwa na mabanda kadhaa likiwemo la Supersport, MNET, Maisha Magic Bongo, Fashion, Banda la watoto na mengine mengi,na kwamba kutakuwepo na Ofa kabambe ndani ya siku 2 za Maonesho, ambapo Mteja atajipatia full set ya DStv kwa sh. 59,000 tu hii ikijumlisha kifurushi cha mwezi mmoja BURE kwa king’amuzi cha HD cha Zappa. Kwa King’amuzi cha Explora Mteja atapata Kwa sh. 240,000 pamoja na kifurushi cha Compact cha mwezi mmoja BURE.
  Wanahabari wakisikiliza kwa makini

  0 0

  Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Profesa John L. Thornton akiwasili Dar kwa ndege maalum Jumanne jioni kuhudhuria mazungumzo ya biashara ya madini ya dhahabu, maarufu kama MAKINIKIA baada ya majadiliano ya kina, baina ya wataalamu wa Tanzania na wa Kampuni hiyo ambayo yamekuwa yakiendelea kwa karibu miezi mitatu sasa. Hii ni mara ya pili Prof Thornton kuja Tanzania kwa shughuli hiyo.


  Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Profesa John L. Thornton akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa JNIA,jiji Dar kwa ndege maalum Jumanne jioni kuhudhuria mazungumzo ya biashara ya madini ya dhahabu, maarufu kama MAKINIKIA baada ya majadiliano ya kina, baina ya wataalamu wa Tanzania na wa Kampuni hiyo ambayo yamekuwa yakiendelea kwa karibu miezi mitatu sasa. Hii ni mara ya pili Prof Thornton kuja Tanzania kwa shughuli hiyo.
  o  0 0

   Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako (centre), is convoyed by Barclays Bank Tanzania Board Chairman, Simon Mponji (left), University of Dar es Salaam (UDSM) Deputy Vice Chancellor Research, Prof. Cuthbert Kimambo (right), some Barclays senior officials and invited dignitaries before the launching ceremony of  Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday.
   Barclays Bank Head of Marketing and Corporate Relations Aron Luhanga (third left), and University of Dar es Salaam (UDSM) Deputy Vice Chancellor Research, Prof. Cuthbert Kimambo, sign contract documents to officiate the launching  of Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday. Looking on from left are Barclays Bank Tanzania Board Chairman, Simon Mponji, Barclays Head of Human Resources, Patrick Foya, UDSM  Deputy Corporate Counsel, Dr. Saudin Mwakaje and Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako. 
   Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako (centre), addresses participants during the official launching of Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday.
   Minister for Education, Science and Technology, Prof. Joyce Ndalichako (centre), Barclays Bank Tanzania Board Chairman, Simon Mponji (left) and University of Dar es Salaam (UDSM) Deputy Vice Chancellor Research, Prof. Cuthbert Kimambo (right) in a souvenir photo pose with some Barclays senior officials and other invited dignitaries after the official launching of   Barclays internship scholarships programmes in Dar es Salaam yesterday.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Faustine Kamuzora  (kulia) mara baada ya mazungumzo ambapo  Mhe. Kangi Lugola alijitambulisha  kwa mara ya kwanza kama Naibu wa Wizara hiyo kwa Makamu wa Rais. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola (katikati)akitembea kwa miguu akielekea ofisini kwake barabara ya Luthuli mara baada ya kumaliza mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Faustine Kamuzora. (picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam, Sadi Kusilawe amewataka viongozi wa chama hicho kuvunja Makundi na kuacha kabisa swala la maneno ili kufanikisha ushindi wa kishindo katika marudio ya uchaguzi wa Udiwani kata ya Saranga.

  Kusilawe amesema hayo alipokuwa anaongea na wajumbe wa halmashauli kuu ya wilaya ya ubungo katika mkutano ulio wakutanisha viongozi hao na kutumia muda huo kuwaasa viongozi hao kuchagua kiongozi bora na atakaye kubalika kwa wananchi ili chama kiweze kupata ushindi wa kishindo kwenye marudio hayo ya uchaguzi.

  "uchaguzi ni kama biashara, leo tuko saranga, mmepiga kura za maoni jana, kura zile zitakuja kuwaambia kuwa saranga tunakwenda na kuku au bata , tutakapo kwenda watatuambia , nikimaanisha tunapaswa kumchagua mgombea ambaye anafaa na anauzika kwa kwa jamii , kwani ukiwa umepita na kuku watu watakuuliza hiyo ni biashara ???? Lakini ukibeba bata hakuna atakae kuuliza kwakuwa wanajua unaenda kufuga hivyo hawaulizi bei na sisi tufanye uchaguzi ambao utatupa kiongozi anaye pendwa na kukubalika na jamii na majibu tutapata kesho kutwa" amesema Kusilawe.

  Aidha aliwaasa viongozi kuwa na moyo wa kutunza vitu na kulinda sana mdomo kwani wote tunajua mdomo ni jumba la maneno kuna wakati unaweza kuongea kitu ambacho kinajenga au kubomoa, huku akisisitiza kuwa na weledi wa kuchambua mambo punde unapo letewa taarifa yoyote , alizidi kueleza kuwa kiongozi bora hupaswi kuwa na maneno mengi, kiongozi akipenda kuongea sana huyo sio kiongozi bali ni kiwanda cha kuzalisha maneno.

  Sambamba na hayo aliwaonya makatibu wa matawi kusimamia vyema vitega uchumi vyote vya chama kwa umakini kwani kuna baadhi ya makatibu wamejibinafsishia vitega uchumi hivyo na kuvimiliki kama vyao kitu ambacho chama hakito kubali wala kufumbia macho vitendo hivyo vya wizi wa mali za chama.

  Pia ndg sadi alitumia nafasi hiyo kutoa onyo kali kwa viongozi ambao hawapendi kuvaa sare za chama cha mapinduzi na kuwataka waache mara moja tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo watajikuta kwenye matatizo ya kuitwa kunguru ikiwa na maana ya mamluki wa chama ambao wanavujisha siri za chama na hivyo kujikuta kwenye kashfa zisizo na maana yoyote, alihoji kuwa RAIS na MWENYEKITI wa CCM Taifa mheshimiwa JOHN MAGUFULI anafanya kazi nzuri hivyo hakuna aja ya kukificha chama chako hivyo ni muhimu kwa wajumbe kuvaa sale za chama .

  Alimalizia kwa kuwaasa wanachama wa chama hicho kuacha kuvaa nguo zinazo wabana , vimini na nguo ambazo zinaonesha maumbile ya mtu jinsi yalivyo au kuvaa nguo chini ya makalio kwani kufanya hivyo ni kukosa maadili. pia kikao hicho kiliudhuliwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya ubungo , katibu wa chama wilaya ya ubungo , wajumbe wa halmashauli kuu wiaya ya ubungo , madiwani n.k.
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Sadi Kusirawe akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu wa Wilaya ya Ubungo.
  Baadhi ya madiwani wa chama cha mapinduzi wakimsikiliza katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam.
  Kamati ya Watendaji ya CCM wilaya ya Ubungo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi

  0 0

  Askari wa kikosi cha Usalama Barabarani CPL Juma Selemani, akitoa elimu katika Shule ya Msingi Custom iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Barabarani.
  Askari wa kikosi cha Usalama Barabarani PC Ndugunamiti, akiwa na Juma Abdallah mwanafunzi wa Shule ya msingi Majengo wilayani Same Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akichangia mada iliyokuwa ikitolea shuleni hapo katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Barabarani.
  Mkaguzi wa kikosi cha Usalama Barabarani wilayani Moshi Mshangama Nyangasa, akitoa elimu katika shule ya msingi Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Barabarani.

  0 0

  Aliyekuwa kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba Ametangaza kuachana na Chama hicho leo na kuamua kijunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) .

  Mwigamba amewaeleza Waandishi wa Habari kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo bila kulazimishwa na mtu  yoyote, hivyo yeye na baadhi ya wanachama wa ACT wametangaza rasmi kujivua uanachama wa ACT-Wazalendo na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  “nimefikia uamuzi huo baada ya viongozi wa ACT-Wazalendo kuwa na maamuzi ambayo ni tofauti na lengo la kuanzishwa kwa chama akitolea mfano kuipinga serikali hata katika shughuli za maendeleo hivyo Uongozi wa sasa wa chama hiki unachepuka kwa kasi kubwa mno nje ya misingi ya chama na sasa chama kimebaki kuwa jahazi ambalo tanga lake limechanika”amesema Mwigamba.


  ameongeza kuwa baada ya kutangaza kujivua uongozi baadhi ya viongozi wa ndani ya chama waligeuka vichaa wakinitukana kila aina ya matusi na cha ajabu hata wale wanaofahamu na kuitetea misingi ya chama walitukanwa na viongozi wakiwepo na wamekaa kimya.
  0 0

  Na Mwandishi wetu
  KAMPUNI ya Huawei, yenye makao yake makuu mjini Shenzhen nchini China, inatarajia kuutambulisha mpango wake wa utoaji elimu kwa njia ya Tehama, unaojulikana kwa jina la E-education.

  Hayo yalibainishwa mapema wiki hii na maofisa kuytoka kampuni hiyo wakati wa ziara ya waandishi wa habari nchini China waliotembelea kujionea namna mradi ‘Smart education’ wanaoutekeleza katika shule ya msingi Baogang nchini China na kuwa wa mafanikio.

  Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo, Schloss glenn James, alisema kuwa kuanzishwa kwa mradi kama huo wa elimu kwa njia ya teknolojia ya Tehama kwa shule za msingi na sekondari itasaidia kuinua kiwango cha elimu nchini kama ilivyothibitika katika mradi ulioanzishwa katika shule ya msingi Baogang.

  James alisema Huawei kwa sasa wamejikita zaidi katika miradi ya mifumo ya elimu kwa mtandao ambapo kupitia mradi huu, matarajio ni kuboresha kiwango cha elimu kwa kiwango cha juu kupitia teknolojia ya Tehama kwa ajili ya kufundishia na kusoma.

  Kwa mazingira hayo, Huawei wamekuwa wakihamisha ujuzi wao kwenda kwa watumishi mbalimbali nchini kwa kuwatumia wataalamu waliobebea ndani ya Huawei.

  Meneja huyo alisema katika kutekeleza jukumu hilo, Huawei ikiwa na watumishi 120, wamekuwa wakitoa mafunzo na elimu kwa vitendo kwa wanafuzni wa fani ya Tehama.

  Sambamba na hayo, mkakati wa kampuni hiyo ya Huawei, ni kupanua wigo wao katika uboreshaji wa miundombinu ya ICT kwa lengo la kuiunganisha nchi ya Tanzania.

  Alifafanua kwamba ajenda ya kampuni hiyo ni kuhakikisha wanaendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wa kiwango cha kimataifa katika kuyafikia mageuzi ya kweli katika nyanja mbalimbali kupitia utaalamu wa teknolojia ya tehama.

  Kwa mwaka huu, Huawei wamekuwa katika mkakati kamambe wa kutafuta njia mbadala na bora zaidi za kuisaidia Serikali katika malengo yake yake ya kiuchumi ifikapo mwaka 2020/2025.

  Huawei wamekuwa wakifanya hivyo kwa maslahi ya nchi katika kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha vyanzo na njia mpya za kuharakisha maendeleo zinapatikana.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Naibu Mkuu wa Kikosi Maalum cha kuzuiya Magendo KMKM, Kapteni Khamis Simba Khamis katika hafla iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo.
  Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Naibu Mkuu wa Kikosi Maalum cha kuzuiya Magendo KMKM Kapteni Khamis Simba Khamis,iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
  Baadhi ya Makamanda wa Kikosi cha KMKM waliofika katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar wakati wa kuapishwa kwa Naibu Mkuu wa Kikosi Maalum cha kuzuiya Magendo KMKM Kapteni Khamis Simba Khamis (hayupo pichani) hafla iliyofanyika leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi baada ya kumuapisha Naibu Mkuu wa Kikosi Maalum cha kuzuiya Magendo KMKM Kapteni Khamis Simba Khamis (wa pili kulia) katika hafla iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.Picha na Ikulu Zanzibar.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Susan Kolimba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maadhimisho ya 72 ya Umoja wa Mataifa ambayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 24 Oktoba katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez.
  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maadhimisho ya 72 ya Umoja wa Mataifa ambayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 24 Oktoba katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Susan Kolimba na kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa toka Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Selestine Mushi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Susan Kolimba (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maadhimisho ya 72 ya Umoja wa Mataifa ambayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 24 Oktoba katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa toka Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Selestine Mushi. Picha na Eliphace Marwa - Maelezo.

  0 0

  Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico) wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi John Nayopa leo jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico), Mhandisi John Nayopa akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.
   Picha mbalimbali za wafanyakazi katika baraza la wafanyakazi.

  KAMISHNA Msaidizi wa Madini kutoka Wizara ya Madini Bw. Julius Sarota amewataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kukuza ubunifu katika kutekeleza majumu yao ili kuleta ustawi endelevu wa Shirika hilo na tija kwa Taifa.

  Bw. Sarota ametoa rai hiyo leo, wakati akizungumza katika mkutano wa tatu wa Baraza la Wafanyazi wa STAMICO, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini; uliofanyika katika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam.
  Bw. Sarota amesema Baraza la Wafanyakazi mahala pa kazi ni chombo muhimu cha kukuza ustawi wa taasisi husika; hivyo ni wajibu wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la STAMICO kuongeza ubunifu na kutekeleza miradi ya utafiti na uchimbaji madini; itakayoleta faida kwa STAMICO na kukuza uchumi wa Tanzania.

  “ Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza azma ya Taifa ya kujenga Tanzania ya Viwanda, ambavyo vitahitaji madini kutumika kama mali ghafi. Nichukue fursa hii kusisitiza STAMICO mtekeleze miradi ya uchimbaji madini itakayosaidia kutoa mali ghafi kwa viwanda vinavyotarajiwa kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini.” Alisisitiza Bw. Sarota.

  Amesema STAMICO inabidi iongeze mwendo katika utekelezaji wa miradi yake ya vipaumbele, ili kwenda sambamba na kasi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi na ya viwanda; hatimaye kumudu soko la mali ghafi za madini nchini kama vile phosphate na graphite, hatua ambayo itasaidia kuwazuia wenye viwanda kuhangaika kuagiza mali ghafi hizo kutoka nchi za nje.

  Kusoma zaidi bofya hapa.

  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam,Wakiwa wamebeba kompyuta 10 zilizotolewa msaada na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo kwa watoto hao kituoni hapo.

   Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam,Wakiwa wameshikilia kompyuta 10 walizokabidhiwa msaada na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo yao kituoni hapo.

    Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Jacquiline Materu(wapili kulia)na Meneja biashara kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Grace Lyon(kulia)wakiwapigia makofi ya kuwapongeza baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam baada ya kuwakabidhi msaada wa kompyuta 10 uliotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo yao kituoni hapo.
  Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam,Khalid Ismail akipokea moja ya kompyuta kati ya 10 kwa niaba ya wenzake toka kwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Jacquiline Materu(kulia)Msaada huo uliotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya mafunzo ya watoto hao kituoni hapo.

   Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakicheza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in The Sun cha Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam,Walipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kukabidhi msaada wa kompyuta 10 zilizotolewa na Vodacom Tanzania Foundation  kwa ajili ya mafunzo kwa watoto hao kituoni hapo.

older | 1 | .... | 1970 | 1971 | (Page 1972) | 1973 | 1974 | .... | 3286 | newer