Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110087 articles
Browse latest View live

MASHINDANO YA PIKIPIKI JIJINI MBEYA...


NAIBU WAZIRI KAKUNDA AFANYA ZIARA KILWA

$
0
0
Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda amewataka viongozi wa serikali wilayani Kilwa Mkoani Lindi kuhakikisha wanasimamia vyema upandaji wa miche mipya yazao la korosho hali ambayo itaongeza uzalishaji wa zao hilo kwa wananchi na kuinua uchumi wa Taifa

Hayo aliyasema jana wilayani Kilwa wakati wa ziara yake baada ya kuelezwa kuwa mkakati wa wilaya uliopo ni kuhakikisha wanazalisha na kupanda miche milioni moja kila mwaka hali ambayo itaongeza mashina ya zao hilo kutoka laki sita yaliyopo na zaidi kutokana na mpango huo kuwa wakudumu 

Kufuatia hali hiyo Kakunda alisema ili miche hiyo iote vizuri na kustawi lazima uwepo usimamizi mkubwa kwa viongozi wote wa serikali wilayani humo kuliko kuacha usimamizi kwa wakulima peke yao ambao wanaweza kusababisha kukauka na kushindwa kufikia malengo 

Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo alisema tayari hatua za awali za kuotesha miche milioni moja kila mwaka zinaendelea ambazo miche hizo itagawiwa bure kwa wakulima hali ambayo itainua uchumi wao 

Bugingo alisema mpango huo ni wakudumu ambapo kila mwaka wilaya itazalisha miche hiyo milioni moja na kuigawa kwa wakulima bure hali ambayo itakuwa zaidi ya mara mbili ya uzalishaji wa miche iliyopo ambayo kwa sasa ni laki sita tu iliyowaingizia shilingi Bilioni 13 na halmashauri kujipatia zaidi ya shilingi milioni220

Aliongeza kuwa mbali na kujipatia fedha kwa wakulima pia halmashauri itajiongezea mapato ya ushuru baada ya serikali kufuta baadhai ya vyanzo ikiwemo ya mabango iliyorudishwa serikali kuu hivyo zao hilo la korosho linaweza kuingizia halmashauri zaidi ya shilingi bilioni 40 kutokana na mpango huo kuwa zaidi ya mara mbili zaidi

Mbali na hali hiyo Waziri Kakunda ameupongeza mpango huo wa upandaji wa miche hiyo milioni moja kila mwaka kutokana na kuvuka malengo ya serikali ya kupanda miche elfu 50 kwa kila wilaya inayolima zao la korosho ingawa Afisa kilimo na ushirika wa halmashauri hiyo ya Kilwa John 

Mkinga amesema changamoto iliyopo ni ucheleweshwaji wa mbegu hali inayosababisha zoezi la uoteshaji miche hiyo kwenda taratibu ingawa Kakunda amesema atawasiliana na wizara ya kilimo kumaliza tatizo hilo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo kulia akitoamaelezo ya mradi mkubwa wa uoteshaji wa miche ya korosho kwa Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai 
Afisa kilimo na ushirika wilaya ya Kilwa John Mkinga kushoto akitoa taarifa ya mradi wa uoteshaji wa miche ya korosho mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo
Picha ikionyesha viriba vya kuoteshea miche ya korosho
Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda akiingia katika eneo la uoteshaji wa miche ya korosho,kushoto ni Wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai Pamela Mollel,Kilwa

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AMWAGIZA CHICO KUJENGA KIWANJA CHA NDEGE SHINYANGA.

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Elius Kwandikwa, amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya kichina ya CHICO aliyepewa zabuni ya ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Shinyanga kufika eneo la mradi na kuanza ujenzi wa kiwanja hicho haraka iwezekanavyo.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya kiwanja hicho katika eneo la Ibadakuli leo, mkoani Shinyanga, Naibu Waziri Kwandikwa, amesema kuwa haoni sababu ya mkandarasi huyo kuchelewa kuleta vifaa vyake katika eneo la mradi hadi sasa wakati tayari mkataba wa kuanza kazi hiyo umeshasainiwa.

"Mkandarasi hana sababu ya kuchelewa kuanza kazi wakati fedha zipo na zimeshatengwa kwa ajili ya mradi huu na mkataba umeshasainiwa,  sasa namwagiza mkandarasi huyu kuleta vifaa vyake na kuanza kazi mara moja", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius Kwandikwa akizungumza na wananchi wa Mwigumbi mkoani Shinyanga, alipofanya ziara ya kukagua barabara ya Mwigumbi – Maswa (KM 50.3), inayounganisha mkoa wa Shinyanga na Simiyu.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius Kwandikwa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya kichina ya CHICO alipokuwa akikagua barabara ya Mwigumbi – Maswa (KM 50.3) inayounganisha mkoa wa Shinyanga na Simiyu.

Muonekano wa Barabara ya Mwigumbi – Maswa (KM 50.3), inayojengwa kwa kiwango cha lami  na mkandarasi CHICO kutoka nchini China. Barabara hii inaunganisha mkoa wa Shinyanga na Simiyu.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAKULIMA WA MIWA KAGERA WAASWA KUCHANGAMKIA SOKO LA MIWA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA

$
0
0
Benny Mwaipaja, Karagwe.

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amewataka wakulima wa miwa wanaozunguka Kiwanda cha Sukari cha Kagera (Kagera Sugar) kuchangamkia soko la uhakika la zao hilo kwa  kuongeza uzalishaji wa miwa kutokana na uhitaji mkubwa wa miwa kwa ajili ya uzalishaji wa miwa katika kiwanda hicho

Dkt. Kijaji alitoa wito huo baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuelezwa kuwa katika msimu wa kilimo cha miwa uliopita wakulima wa miwa wanaozunguka kiwanda hicho walilipwa Shilingi bilioni 4 baada ya kukiuzia kiwanda hicho zaidi ya tani 56,000 za miwa.

Alisema kuwa bado mahitaji ya miwa kwa ajili ya kuzalisha sukari kiwandani hapo ni makubwa na kuwataka wakulima hao kupitia umoja wao wa wakulima wadogo wa miwa kuhamasishana kuongeza uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa masuala ya Kielektroniki wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bw. Obed Kiswaga (kushoto) kuhusu utendaji kazi wa kiwanda hicho baada ya kutembelewa na Naibu Waziri huyo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa ameshika mfuko wa sukari wenye ujazo wa kilo moja inayozalishwa katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera, alipokuwa akipata maelezo kuhusu ubora wa sukari inayozalishwa kiwandani hapo kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akiangalia mitambo ya kutengeneza Sukari inavyofanyakazi, alipotembelea katika kiwanda cha Sukari cha Kagera.
 Mtaalam Mwandamizi wa masuala ya Kilimo katika kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bw. Nassoro Abubakari, (wa pili kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) kuhusu mbegu tano za miwa ambazo zinatumika katika shamba la miwa la kiwanda hicho.

KATIBU WA BUNGE NDG.KIGAIGAI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA OFISI YA BUNGE KATIKA KIKAO CHA MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA BUNGE LEO MJINI DODOMA.

$
0
0
 Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kigaigai akizungumza na Menejimenti ya Utumishi wa Bunge katika kikao cha kufahamiana kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Spika Mjini Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakimsikiliza Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kigaigai (katikati) akizungumza wakati wa kikao cha kufahamiana na Menejimenti ya Utumishi wa Bunge kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Spika Mjini Dodoma.
 (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

ALIYEKUWA KOCHA WA SIMBA JACKSON MAYANJA AJIUZULU MWENYEWE

$
0
0
Aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba  raia wa Uganda Jackson Mayanja ni kwamba ameamua kuachia ngazi kutokana na matatizo yake binafsi.

Mayanja ambaye bado yuko jijini Dar es Salaam, ameamua kuachana na Simba akidai ana matatizo binafsi na kutapelekea kushindw akutimiza majukumu yake kama kocha msaidizi wa timu hiyo.

Ametanabaisha kuwa matatizo hayo ni ya kifamilia na hataweza kukuyaweja wazi, “Ni matatizo ya kifamilia lakini suala hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa,” alisema.

Lakini habari kutoka Simba zimeeleza kuwa sasa wako katika hatua za mwisho kuvunja mkataba wake huku kukiwa na sintofahamu kwa siku za hivi karibuni ndani ya klabu ya Simba ikielezwa kwamba kuna matatizo ya kifedha na ucheleweshwaji wa malipo ya mishahara kwa benchi la ufundi na wachezaji kiujumla.

Taarifa hizo ambazo hazijathibitishwa na uongozi wa Simba haujathibisha taarifa hizo zinazosambazwa kwa sasa kuwa hawajawalipa wachezaji wao mishahara ya miezi mitatu.

x

Afisa elimu mkoa wa Dar es salaam ahaidi kuzitatua kero zinazowakabili wamiliki wa shule binafsi

$
0
0
Na Michael Utouh

AFISA Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Hamis Lissu ameahidi kutatua kero zote zinazowakabili baadhi ya wamiliki wa Shule Binafsiinafsi wa mkoa huo ikiwemo ya tozo kubwa za biashara zinazotozwa shule hizo .

Pia amewaomba wamiliki wa shule hizo kipindi cha likizo wajitolee kuwafundisha masomo ya sayansi wanafunzi wanaotoka shule za serikali kwa kuwa wana walimu wengi wa masomo hayo.

Ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua Mkutano Maalumu uliowakutanisha wadau mbalimbali na wamiliki wa shule zilizopo mkoani humo.Amesema wamiliki wa shule hizo pamoja na shule zao wanapaswa watambaue huduma wanazopewa ni stahiki hivyo ni sawa wanazopatiwa shule za Serikali.

“Natamani kuziona shule zote binafsi zikiwa zinazoongoza kutokuwa na changamaoto zozote kwani tunatambua mchango wa uwekezaji hapa nchini,” amesema.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi nchini (TAMONGSCO), Charles Totela ameishukuru Serikali ya mkoa huo kwani imekuwa ikiwapa ushirikiano wa kutosha.

Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali ya mkoa huo kuwaundia dawati la pamoja litakalowakutanisha viongozi wote wa shule binafsi, za serikali na watendaji wao ili waweze kukaa pamoja na kujadiliana baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa hazifanyiwi kazi.

Naye Mkurugenzi wa Shule za Al-Muntazir, Mahmood Ladack amewashukuru wamiliki wa shule hizo kwa kuhitisha mkuatano huo ambao anataraji utakuwa na manufaa makubwa kwao na taasisi wanazosimamia katika kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Afisa elimu wa mkoa wa Dar es salaam akizungumza na washiriki wa mkutano uliowakutanisha wamiliki wa shule binafsi mkoa wa Dar es Salaam
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa shule binafsi (TAMONGSCO), Charles Totela Akizungumza 
Miongoni mwa wamiliki wa shule binafsi pamoja na wawakilishi waliofika kwenye mkutano huo .

SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA)

$
0
0
Benny Mwaipaja, Kagera.

NAIBU waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameziagiza Mamlaka na Taasisi zote za Umma kufanya ununuzi wa vifaa na mafuta kupitia Wakala wa Serikali wa ununuzi na ugavi (GPSA) kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge na kuwaonya wahusika wote watakaoendelea kukaidi maagizo hayo kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.

Dkt. Kijaji ametoa maagizo hayo mkoani Kagera baada ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na Wakala wa Ununuzi na Ugavi GPSA mkoani humo na kubaini kuwa taasii na idara nyingi za umma zinafanya manunuzi nje ya mfumo wa GPSA jambo ambalo amesema ni ukiukwaji mkubwa wa sheria.

Alisema kuwa lengo la Serikali la kuanzishwa kwa wakala huo pamoja na mambo mengine ilikuwa kudhibiti matumizi ya Serikali na kuonya kuwa Serikali haitakubali kuona sheria zinakiukwa kwa makusudi na kwa malengo yanayoonesha kuna nia isiyo njema katika matumizi ya fedha za umma.

“Hili si ombi ni maelekezo na ni agizo, taasisi zote zipate huduma kutoka kwa wakala wetu (GPSA) kwani Serikali ilikuwa na dhamira ya uwepo wa matumizi sahihi ya fedha za matumizi wanazopelekewa na ndiyo maana ukaanzishwa Wakala huu” Alisema Dkt. Kijaji
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akitoa maagizo kwa Kaimu Meneja  wa Wakala Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera, Bi. Dorothea Bugenyi, kuhusu kuwahudumia Taasisi zote za Serikali kwa kuwa ndio wajibu wa Wakala huo, alipofanya Ziara katika Ofisi hizo za Mkoani Kagera.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akielezea namna atakavyoshirikiana na Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini katika Mkoa huo ili kuhakikisha kunakuwa na matumizi adili ya fedha za Serikali, Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea Ofisi za Wakala huo Mkoani Kagera.
 Kaimu Meneja wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera, Bi. Dorothea Bugenyi (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) namna tetemeko la ardhi lilivyo haribu miundombinu ya Ofisi hizo, alipotembelewa na Naibu Waziri huyo katika Ofisi za GPSA Mkoani humo.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba  Bw. Deodatus Kinawiro (kulia) akizungumza jambo wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) alipotembelea Ghala la Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoani Kagera.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA IRELAND

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi katika Idara ya Mambo ya Nje na Biashara mwenye Jukumu Maalum kwa ajli ya Diaspora na Maendeleo ya Kimataifa wa Ireland Mhe. Ciaran Cannon aliyeambatana na Balozi wa Ireland nchini Tanzania.

Katika mazungumzo yao walitilia mkazo katika masuala ya Biashara na uwekezaji hasa ikizingatiwa kwamba nchi zote mbili mazingira yake yanaruhusu .

Makamu wa Rais alimuambia Waziri huyo Tanzania ni nchi nzuri na rafiki kwa kuwekeza hivyo wanakaribishwa kuwekeza hasa katika viwanda na teknolojia, Waziri huyo alieleza kuridhishwa kwake  na jitihada za Tanzania katika kusimamia uchumi wake kwa ujumla.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alielezea vifo vya wakina mama kabla na wakati wa kujifungua na watoto wachanga na kuiomba Serikali ya Ireland kupitia Waziri huyo kuisaidia Tanzania kukabiliana na tatizo hilo, ambapo waziri huyo alioneshwa kuguswa sana hasa pale Makamu wa Rais alipoelezea uzoefu wake mwenyewe aliowahi kukutana nao wakati anajifungua mtoto wake wa tatu.

Makamu wa Rais na Waziri huyo kutoka Ireland kwa pamoja walikubaliana katika suala zima la kuboresha elimu, mafunzo  na kubadilishana ujuzi hasa katika masuala ya Afya, Teknolojia na Anga.Mwisho Makamu wa Rais alisema Ushirikiano wa nchi mbili hizi ni wakudumu na kuiomba Serikali ya Ireland kuendelea kushirikiana na kusaidia Tanzania.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Nchi katika Idara ya Mambo ya Nje na Biashara mwenye Jukumu Maalum kwa ajili ya Diaspora na Maendeleo Kimataifa wa Ireland Mhe. Ciaran Cannon aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam akiongozana na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Paul Sherlock pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Misaada la Irish Ndugu Ruairi De Burca's. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi katika Idara ya Mambo ya Nje na Biashara mwenye Jukumu Maalum kwa ajili ya Diaspora na Maendeleo Kimataifa wa Ireland Mhe. Ciaran Cannon mara baada ya kumaliza mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

DKT. KALEMANI NA WAZIRI WA MAFUTA NA GESI OMAN WAJADILI VIPAUMBELE VYA USHIRIKIANO NISHATI.

$
0
0
Na Teresia Mhagama, DSM.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed Al Rumhi wamekutana  jijini Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano lengo likiwa ni kuendeleza Sekta ya Nishati nchini.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam ambapo Waziri huyo kutoka Oman aliambatana na Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Oman, Naibu Waziri wa Utalii na Balozi wa Oman nchini Tanzania.
Kwa upande wa Tanzania, viongozi mbalimbali walishiriki katika majadiliano hayo akiwemo Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Naibu Katibu Mkuu, Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo na watendaji wengine kutoka Idara ya Nishati na Sheria.

Kwa upande wake Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Rumhi, alisema kuwa lengo la Ujumbe huo kufika wizarani ni kujadiliana na watendaji wa Wizara ya Nishati kuhusu maeneo ambayo ingependa ishirikiane na nchi hiyo ya Oman na kwamba nchi hiyo ipo tayari kushirikiana  na Tanzania.

“ Hapo zamani, Sisi Oman hatukutumia Gesi yetu vizuri kwa kuwa tulifanya haraka kuiuza nje ya nchi lakini ninyi mnayo fursa sasa ya kuitumia gesi yenu ndani ya nchi ili kutengeneza ajira pamoja na kuiendeleza kwa matumizi mbalimbali, na ikiwa ziko fursa za ushirikiano ili kuendeleza nishati hii, sisi tupo tayari,” alisema Dkt. Rumhi.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tano kulia),  Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed Al Rumhi (wa Nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Oman, Dkt. Salim Al Ismaily (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Maitha Al Mahrouqi, (wa pili kushoto), Balozi Mteule wa Oman hapa nchini, Ali Al Mahruqi (wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa nne kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa Tatu kulia), Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kulia) na Balozi wa Tanzania nchini  Oman, Abdallah Kilima, (wa pili kulia).
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa nne kushoto),  Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed Al Rumhi (wa Nne kulia) wakiwa katika Ofisi ya  Waziri wa Nishati jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Oman, Dkt. Salim Al Ismaily (wa tatu kulia), Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Maitha Al Mahrouqi, (wa pili kulia), Balozi Mteule wa Oman hapa nchini, Ali Al Mahruqi (wa kwanza kulia). Wengine ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa tatu kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa pili kushoto), na Balozi wa Tanzania nchini  Oman, Abdallah Kilima, (wa kwanza kushoto).
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tano kulia),  Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed Al Rumhi (wa Tatu kushoto)  wakiagana mara baada ya kikao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Oman, Dkt. Salim Al Ismaily (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Maitha Al Mahrouqi, (wa kwanza kushoto),  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa nne kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa Tatu kulia), Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kulia) na Balozi wa Tanzania nchini  Oman, Abdallah Kilima, (wa pili kulia).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WIKI YA USALAMA BARABARANI: NI ZAMU YETU ABIRIA KUPAZA SAUTI

$
0
0
 Mabasi ya abiria yanayofanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda mikoani  yakiyapita  magari yaliyombele  kwenye   kona na mteremko mkali   barabara kuu ya  Dar es Salaam- Morogoro  eneo zilizopo  Ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania ( TAFORI)  karibu Kingolwira  mjini Morogoro   asubuhi ya Oktoba 17, mwaka huu ( 2017) ikiwa ni  siku mbili  tu baada ya Makamu wa Rais , Samia Suluhu Hassan , kuzindua wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa mkoani Kilimanjaro yenye kauli mbiu ‘ Zuia ajali , Tii Sheria , Okoa Maisha’ . ( Picha na John Nditi).


WAZIRI MKUCHIKA: TOFAUTI KUBWA YA MISHAHARA SERIKALINI KUKOMA

$
0
0
Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma imeagizwa kufanya utafiti wa kina utakaowezesha kuwa na uwiano sawa wa malipo ya mishahara na masilahi ya watumishi wote serikalini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amesema hayo leo wakati wa ziara ya kikazi katika Ofisi za Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mkuchika amesema kuna baadhi ya taasisi/Idara za Serikali zinalipa watumishi wake mishahara mikubwa tofauti na taasisi nyingine jambo ambalo limekuwa likisababisha watumishi kutotulia sehemu moja na kutafuta masilahi bora zaidi sehemu nyingine.

“Hii haiwezekani, mmesoma darasa moja, fani moja na mko cheo kimoja, lakini mnalipwa mishahara tofauti wakati serikali ni moja, ni lazima mlifanyie utafiti wa kina suala hili. Masilahi ya watumishi wa umma lazima yawe sawa” Waziri
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipata maelezo kuhusu mifumo ya TEHAMA inavyofanya kazi wakati wa mikutano ya kieletroniki (Video Conference) katika ofisi za TaGLA wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya mapema leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea taarifa (nakala ngumu na laini) zenye shughuli zinazofanywa na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bw. Charles Senkondo baada ya kumaliza ziara ya kikazi katika wakala hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald Ndagula akitoa neno la shukurani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) mara baada ya Waziri kumaliza kuzungumza na watumishi wa bodi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea nyaraka mbalimbali zinazohusu utunzaji wa kumbukumbu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Charles Magaya katika ofisi za Idara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.

LATIFA KANYANGA ASHEREHEKEA MAHAFALI YAKE YA KIDATO CHA NNE GREEN ACRES SEKONDARI

$
0
0
Afisa elimu Wilaya Ubungo, akizungumza wakati wa Mahafali ya 18 ya shule ya Sekondari ya Green Acres yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi Latifa Kanyanga akipokea cheti kutoka kwa mgeni Rasmi katika mahafali ya 18 ya kidato cha 4 katika Shule ya Sekondari ya Green Acres
Mwanafunzi Latifa Kanyanga akisoma Risala wakati wa Mahafali ya 18 ya Shule ya Sekondari ya Green Acres.

MKURUGENZI WA ILEJE ATEMBELEA KILWA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai kulia akisalimiana na mkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe, Haji Mnasi ,mara baada ya Mkurugenzi huyo kufika ofisini kwake jana kwaajili ya kumsalimu kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Zabron Bugingo(Picha na Pamela Mollel Kilwa)
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai kulia akisalimiana na mkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Zablon Bugingo katikatimkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe  

TAARIFA YA KUONGEZA MUDA WA UTOAJI WA LESENI ZA MACHAPISHO MBALIMBALI NCHINI


ZIMAMOTO WAKONGA NYOYO ZA WANANCHI MAONESHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

$
0
0
 Sajini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji toka Makao Makuu, Damian Muheya (Kulia), akiwaelimisha wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro jinsi vizimia moto vya awali (Fire Extinguisher) vinavyotumika pindi moto unapotokea, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani humo katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
 Wananchi wa Mjini Kilimanjaro wakiwa katika banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakipata elimu juu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwenye vyombo vya Usafiri na Usafirishaji, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani humo katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”.
 Wananchi wa Mjini Kilimanjaro wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kitengo cha Maokozi Saidi Seng’endo (Kushoto) walipotembelea banda hilo, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani humo katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”. 
 Picha ni sehemu ya mabanda ya washiriki mbalimbali wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani Kilimanjaro katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”.
 Picha watoto wakimsikiliza Konstebo Saidi Seng’endo juu ya matumizi ya kifaa kinachohifadhi hewa safi (Breathing Apparatus) kwa ajili ya kumsaidizi Askari wa Zimamoto kwenye matukio mbalimbali.
Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kitengo cha Maokozi toka Makao Makuu, Saidi Seng’endo (Kushoto), akiwa na Konstebo wa Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Simba Mikidadi (Kulia), wakiwaonesha wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro jinsi baadhi ya vifaa vya gari maalum la maokozi  (Fire Rescue Tender) vinavyotumika pindi ajali inapotokea barabarani, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani humo katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu, tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

WANAHABARI WA TANZANIA WATEMBELEA KAMPUNI YA HUWAWEI NCHINI CHINA

$
0
0



 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, wakiwa ndani ya Kiwanda cha Kampuni ya  Huwawei walipotembelea Kiwanda hicho kuijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.

 Wanahabari wakiwa katika kiwanda hicho.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja  Shenzhen nchini China, walipokwenda kutembelea kampuni ya Huwawei na kuijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ikwemo utekelezaji wa mradi wa elimu wa Smart Education na e-Education unaotekelezwa katika shule ya msingi Baogang iliyopo nchini humona hivyo kukabiliana na tatizo la uhaba walimu.mpango huo pia wanatarajia kuuleta hapa nchini ili kuweza kuboresha sekta ya elimu.(Na mpiga picha Wetu).

JARIDA LA WIZARA YA HABARI UTAMDUNI, SANAA NA MICHEZO

KUMBUKUMBU

$
0
0
TWAHA SALUM MATOLA
19/10/1987 – 19/10/2017
Ni miaka 30 imepita tangu ulipotuacha, kwetu tunaona ni kama jana. Tunakukumbuka sana kwa upendo wako mkubwa uliokuwa nao kwetu sisi wote, ulitusaidia wote kwa hali na mali bila kubagua. Hakika hatuwezi kusahau upendo mkubwa uliokuwa nao wa kuwajali ndugu na jamaa zako wakati wa shida na raha. Tunaendelea kukumbuka kwa upendo, ukarimu, ucheshi na malezi uliyotupa.
Unakumbukwa sana na watoto wako, ndugu na jamaa zako wote. Tunamuomba Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema, Aiweke roho yako mahala pema peponi, Akupe pepo ya firdaus.
Inna lillahi wa inna ilaihi raji’un

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 18.10.2017

Viewing all 110087 articles
Browse latest View live




Latest Images