Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

NEC YAAGIZA WALIOPOTEZA VITAMBULISHO KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WADIWANI

$
0
0



NEC-DODOMA

Tume ya Taifa ya uchaguzi imesema kuwa Wapiga kura waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura watapata fursa ya kupiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa Madiwani wa Kata 43 unaotarajiwa kufanyika Novemba 26, mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo (16.10.2017) na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Ramadhani Kailima Mjini Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi na wasimamizi wasiadizi wa uchaguzi yanayoratibiwa na kuendeshwa na NEC.

Bw. Kailima amesema wapiga kura hao wataruhusiwa kutumia vitambulisho vya uraia vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Hati ya kusafiria na Leseni ya udereva.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia kifungu namba 62 (a) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambacho kinasema mpiga kura aliyeandikishwa kwenye daftari atakwenda mwenyewe kwenye Kata aliyojiandikisha na kituo alichopangiwa” Amesema.

Ameeleza kuwa hatua hiyo ni kumridhisha msimamizi wa kituo au msimamizi msaidizi wa uchaguzi kwamba yeye ndiye mpiga kura halali na kuongeza kuwa kifungu hicho kinamtaka Mpiga Kura aonyeshe kadi yake ya kupigia. Aidha, kinaeleza kwamba Tume inaweza ikaelekeza utambulisho mwingine wowote utakao msaidia mpiga kura kuweza kupiga kura iwapo hana kadi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Koplo Faustina Ndunguru kutoka Makao Makuu ya Trafiki kitengo cha Elimu ya Usalama Barabarani katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa ,Manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro, wengine pichani ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira (kushoto) na Kulia ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa Usalama na Mazingira kutoka TANROADS Makao Makuu Bi. Zafarani Madayi wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho yanayotoa elimu ya usalama barabarani katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa ,Manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi Msaidizi Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Joyce Mbunju akimuelezea Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan namna Wizara ilivyojipanga nakuja na mbinu za teknolojia ya kisasa katika kuhakikisha usalama barabarani unakuwepo wakati wote.
Mwanafunzi wa Darasa la 5 kutoka shule ya msingi Muungano Bi. Aisha Ayoub akishiriki kuima nyimbo za kuelimisha masuala ya usalama barabarani akiwa mmoja kati ya wanafunzi waliotoka shule 10 za Manispaa ya Moshi mjini wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambao umefanyika katika viwanja vya Mashujaa ambapo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa ,Manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.


Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

JAMII YAASWA KUENDELEA KUWASAIDIA WATOTO WENYE UHITAJI NA WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU

$
0
0
PICHA NA JOEL MADUKA.

Jamii Mkoani Geita imetakiwa kujitoa kwa moyo wa kupenda kuendelea kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu na wale ambao ni yatima. Rai hiyo ilitolewa na katibu wa umoja wa wanawake wa chama cha mapiduzi wilayani Geita,Bi Mazoea Salum wakati alipokuwa akiwakabidhi vifaa vya shule watoto.

wa kituo cha kulea watoto cha Bright light kwenye kikao cha kwanza cha jumuiya hiyo tangu uchaguzi kufanyika ndani ya chama.

Alisema kuwa ni vyema jamii kwa ujumla kukumbuka kuwasaidia watoto ambao wana uhitaji kwani hata kwenye vitabu vya Mungu vimeendelea kuelekeza kutoa msaada kwa yatima,wajane na wale ambao
hawajiwezi kwani kufanya hivyo ni kumpendaza Mungu.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho ,Methew Daniel ameelezea kuwa pamoja na kuendelea kufanya vizuri kwenye kituo hicho bado wanakabiliwa na matatizo ya jamiii kuendelea kukichukulia kituo hicho kuwa kina wafadhili jambo ambalo ni kinyume na kituo kilivyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi (CCM)Wilayani Geita Bi,Antonia Charles akikabidhi sababuni pamoja na vifaa vya shule kwa Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto cha Bright light na watoto ambao wanaishi kwenye Kituo hicho wakati wa kikao cha kwanza cha Jumuiya hiyo.
Katibu wa umoja wa wanawake wa chama cha mapiduzi wilayani Geita,Bi Mazoea Salum ,Akizungumza na kusisitiza wananchi kujitolea kuwasaidia watoto waishio mazingira magumu.
Wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia zoezi la utoaji wa msaada kwa watoto waishio mazingira magumu.
Uongozi wa Jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa Bright light pamoja na Mkurugenzi wa Kituo hicho.

DKT. NDUNGULILE AFANYA ZIARA KUJIRIDHISHA NA HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA

$
0
0
NA WAMJW-DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile amefanya ziara kwenye baadhi ya vituo vitoavyo huduma za afya kwa ajili ya kujiridhisha na hali ya upatikanaji wa dawa jijini Dar es salaam.

Akizungumza lengo la ziara hiyo Dkt. Ndungulile amesema kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuungana na Mhe. Rais wa wamau ya tano Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kutatua tatizo la dawa katika vituo vinavyotoa huduma za afya mpaka kufikia 2020.

“Mpaka kufikia hivi sasa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imetenga shilingi Bilioni 262 kwa ajili ya kutatua tatizo la uhaba wa dawa nchini kutoka shilingi bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/2016 “ alifafanua Dkt. Ndungulile.

Aidha Dkt. Ndungulile amesema kuwa katika ziara hiyo amegundua kwamba vituo vinavyotoa huduma ya afya vina dawa zote muhimu isipokuwa kuna upungufu wa vifaa tiba ambapo tatizo hilo litafanyiwa kazi mara moja .
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo jinsi ya dawa zinavyoagizwa MSD kutoka kwa Mfamasia wa Hospitali ya Mwananyamala Bw. Marco Sallingu kulia wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa pili kulia akiangalia dawa ziliozopo katika stoo za wa Hospitali ya Mwananyamala wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo jinsi ya dawa zinavyoagizwa MSD kutoka kwa Mfamasia wa Hospitali ya Sinza Palestina Bi. Doris Messanga kulia wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa katikati waliosimama akiongea na wagonjwa wakati wa ziara yake Hospitalini Sinza Palestina alipotembelea vituo vinavyotoa huduma ya afya leo jijini Dar es salaam.

USAJILI MWANZA; WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI KUSAJILIWA

$
0
0
Usajili Vitambulisho vya Taifa katika mkoa wa Mwanza na wilaya zake umepamba moto, ambapo wananchi kutoka Wilaya za Kwimba, Ukerewe, Ilemela, Misungwi na Sengerema wamejitokeza kwa wingi kusajili. Kwa wananchi wa Wilaya Nyamagana, taratibu za kuanza kwa Usajili zinaendelea ambapo wataanza usajili rasmi wiki hii. 

Katika kufanikisha zoezi hilo Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa pamoja na Watendaji wa mitaa/Vijiji wamejizatiti kwa dhati kuhakikisha zoezi hili linafanyika na kukamilika kwa wakati uliopangwa. Aidha; Wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kutokana na manufaa mapana ya zoezi hilo kwa mwananchi mmoja mmoja na kwa Taifa kwa ujumla.
Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Wilayani ya Ukerewe likiendelea, pichani ni baadhi ya wananchi wa kata ya Kakelege wakisubiri zoezi la kupigwa picha na kuchukuliwa alama za Kibaiolojia.
Afisa Usajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ndg. Zabron Rusohoka akiwaelekeza baadhi ya wananchi taratibu wanazopaswa kuzifuata wakati wa ujazaji fomu za maombi ya Wilayani Ukerewe.
Umati wa wananchi wa Kata ya Ukerewe kijiji cha Nakatunguru wakisubiri huduma ya Usajili wakati zoezi la Usajili likiendelea Wilayani humo. 

WAZIRI MKUCHIKA AWAELEKEZA WATUMISHI WA UMMA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KASI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) akiongea na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais –Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) kuongea na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi (hawapo pichani).
Watendaji wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) wakiwa katika kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) leo jijini Dar es salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 16.10.2017

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU


MAKAMU WA RAIS AONDOKA MKOANI KILIMANJARO NA KUREJEA JIJINI DAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemaliza ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama uliofanyika Kitaifa mkoani Kilimanjaro na kurejea Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mara baada ya kufungua maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo Kitaifa yamefanyika mkoani Kilimanjaro.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri wa Mambo Ndani Mh Mwigulu Nchemba katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mara baada ya kufungua maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo Kitaifa yamefanyika mkoani Kilimanjaro.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Waegesha Ndege wa JNIA Wapigwa Msasa

$
0
0
WAEGESHA ndege 10 wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), leo walianza mafunzo ya siku saba ya uegeshaji ndege kutoka kwa wakufunzi wa Kiwanja cha Ndege cha Hague cha Uholanzi yanayofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga (CATS) jijini Dar es Salaam.

Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwani yatazidi kuwajengea uwezo na uzoefu washiriki hao.

Bw. Mayongela amewasisitiza washiriki hao kuzingatia kila wanachofundishwa ili waweze kuwa mahiri na weledi katika uongozaji wa ndege za ndani na nje ya nchi zinazotumia kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

“Waongoza ndege ni moja ya kazi inayohusisha mawasiliano ya moja kwa moja kati ya watoa huduma ndani ya kiwanja cha ndege, hivyo ni lazima tufikie viwango vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria kimataifa,” amesema Bw. Mayongela.

Hata hivyo, amesema TAA inajukumu kubwa la kuwaongezea uwezo watumishi wake kwa kuwapeleka kwenye mafunzo mbalimbali ili kujijengea uwezo na maarifa.Bw. Mayongela amewashukuru waendeshaji wa mafunzo hayo yanayotolewa na mfuko wa Avi Assist wa Uholanzi, ambapo amewahahakikishia kuendeleza ushirikiano waliouanzisha kwa kushirikiana katika utoaji wa mafunzo ya kada mbalimbali.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Waongoza ndege cha JNIA, Bw. Lugano Mwinuka amesema mafunzo haya yamekuja wakati muafaka, kwa kuwa walikuwa yakiyahitaji kwa muda mrefu, na sasa anauhakika wa washiriki wataongeza ujuzi katika utendaji wao wa kazi.

Bw. Mwinuka amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa nadharia na vitendo, ambapo washiriki hao wamegawanywa katika makundi mawili ya watu watano, ambao ni Earisner Waihula, Emmanuel Nyaulingo, Anunciatus Alex, Fadhili Meena na Oscar Kibiki.

Watakaoingia kundi la pili ni pamoja na Denis Kinyaga, Zennobius Mwimba, Raynard Komba, Said Mussa na Meshack Elisante.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (aliyesimama kulia) leo akifungua mafunzo ya wiki moja ya Waegesha ndege yanayofanyika kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (CATS) kilichopo kwenye Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBI).
Wakufunzi Ralf Overduya (kushoto) na Martiyn Ouwendyki kutoka Kiwanja cha Ndege cha Hague cha Uholanzi leo wakianza kufundisha baadhi ya waegesha ndege wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) katika mafunzo yanayofanyika kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki, wakufunzi na waandaaji wa mafunzo ya waegesha ndege yaliyoanza leo kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Avi Assist wa Uholanzi Bw. Tom Kok.

Serikali ya Oman kulikarabati Jumba la Ajabu aka Beit El Ajaib Zanzibar

$
0
0
Na Salum Vuai, MAELEZO
 UJUMBE wa Serikali ya Oman uliokuwepo Zanzibar tangu Oktoba 12, 2017, leo umebariki maandalizi ya matengenezo makubwa ya jengo la kihistoria Beit El Ajaib lilioko Forodhani katika
Mji Mkongwe wa Zanzibar. 
Ujumbe huo ukiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dk. Mohammed Hamad Al Rumhy, umelitembelea jengo hilo ukiambatana na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukagua hali yake halisi. 
 Lengo la ziara hiyo lilikuwa kuweka jiwe la msingi kama ishara ya maandalizi ya matengenezo hayo chini ya ufadhili wa Serikali ya Oman inayoongozwa na Sultan Qaboos bin Said, yanayotarajiwa kuanza wakati wowote kutokea sasa. Jengo la Beit El Ajaib lililojengwa mwaka 1883 wakati wa utawala wa Sultan wa pili wa Zanzibar Barghash bin Said, limeachwa kutumika kwa miaka kadhaa sasa kutokana na kukabiliwa na uchakavu mkubwa ikiwemo kuanguka baadhi ya kuta zake. 
Beit El Ajaib ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii hapa Zanzibar, na kabla kuzuiwa matumizi yake, lilikuwa likiingizia mapato serikali kwa kutembelewa na watalii wengi kutoka nchi mbalimbali duniani. 
Matengenezo hayo yanatarajiwa kulijejeshea haiba jengo hilo ambalo ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii humu visiwani, na kuanza kutumiwa tena wa shughuli za kitalii. OKTOBA 2017

Jumba la Ajabu aka Beit El Ajaib Zanzibar  

Jumba la Ajabu aka Beit El Ajaib linavyoonekana kwa sasa

JUKWAA LA HAKI JINAI LATEMBELEA MAGEREZA NA VITUO VYA POLISI IRINGA,NJOMBE NA RUVUMA

$
0
0
Timu ya wataalamu kutoka Jukwaa la Haki Jinai nchini ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome inatembelea Magereza katika mikoa ya Iringa, Njombe  na Ruvuma ili kujionea changamoto zinazowakabili  wafungwa na mahabusu nchini katika kupata haki zao wakiwa vizuizini au magerezani na kuangalia namna ya kuzitatua. 
Akizungumza katika siku ya kwanza ya ziara hiyo mjini Iringa, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Mchome amesema utekelezaji wa mradi huo pia unalenga kuziongezea  uwezo taasisi zinazoshughulika na utoaji haki na kusimamia haki za binadamu nchini ili ziweze kutoa huduma stahiki kwa watanzania ya utoaji haki na ulinzi wa haki za binadamu. 
Amesema ni matarajio ya Serikali kuwa ziara hiyo itawezesha taasisi zinazosimamia utoaji haki nchini kuchukua hatua katika kuhakikisha wafungwa na mahabusu wanapata haki zao kwa wakati.

Ujumbe huo wa jukwaa  la haki jinai unamshirikisha Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) Biswalo Mganga, Naibu Mkurugenzi Upelelezi Makosa ya Jinai nchini (DDCI) Charles Kenyela, Ofisi ya Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Magereza na Jeshi Polisi.

Ujumbe huo umetembelea Gereza la wilaya ya Iringa,  Selo iliyoko katika kituo cha Polisi Iringa mjini, Gereza la Wilaya Njombe na selo iliyoko katika kituo cha Polisi Njombe na kujionea mazingira yaliyopo na kusikiliza kero zinazowakabili wafungwa na mahabusu walioko katika vituo hivyo vya polisi na magereza hayo katika kupata haki zao.

Wananchi hao waliomba kupata msaada katika maeneo ya kufikishwa mahakamani kwa wakati, uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili kufanywa kwa wakati, kupatiwa nakala za hukumu kwa wakati   ili wawahi muda wa kukata rufaa na mashitaka yao kusikilizwa kwa wakati ikiwa ni pamoja na kusikilizwa kwa rufaa zao. 
Ziara hiyo ni utekelezaji wa mradi wa upatikanaji haki na ulinzi wa haki za binadamu nchini unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa –UNDP.

 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka akiongea na wataalamu wa Jukwaa la haki jinai nchini ambao walioongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome  walipoanza ziara ya kutembelea magereza na vituo vya polisi mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza akiwakaribisha ofisini kwake  wataalamu wa Jukwaa la
haki jinai nchini ambao walioongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome mjini Iringa walipoanza ziara ya kutembelea magereza na vituo vya polisi mkoani humo juzi.

 Wataalamu kutoka taasisi zinazosimamia utoaji haki nhini ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome wa pili kulia waliosimama mbele wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka wapili kushoto waliosimama mbele Wataalamu hao walikwenda kumsalimia Mkuu wa Mkoa  wa Njombe kabla ya na kutembelea gereza la wilaya ya Njombe na kituo cha Polisi cha wilaya hiyo na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko kizuizini katika maeneo yao na kutatua changamoto zinazowakabili.
 Timu ya wataalamu kutoka Jukwaa la Haki Jinai nchini ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. SifuniMchome katika picha ya pamoja na askari magereza nje ya gereza la wilaya ya njombe baada ya kutembelea gereza hilo na kuzaungumza na wafungwa na mahabusu walioko katika gereza hilo mjini Njombe jana
ilikujionea changamoto zinazowakabili  wafungwa na mahabusu nchini katika kupata haki zao wakiwa vizuizini au magerezani na kuangalia namna ya kuzitatua.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza (katikati waliosimama mbele) katika picha ya poamoja na wataalamu wa Jukwaa la haki jinai nchini ambao walioongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome baada ya kutoka kumsalimia Mkuu huyo wa mkoa Ofisini kwake mjini Iringa walipoanza ziara ya kutembelea magereza na vituo vya polisi mkoani humo juzi.

INTRODUCING "BANG" BY Benjamin wa Mambo Jambo

$
0
0
This is to announce you that, Benjamin wa Mambo Jambo has released his new music video from his latest song "BANG' The Video was shot in Dar-es-Salaam, Tanzania by Kokwa Production. Cinematography by Kudra Makunzo (Makunzo Media) and Kokwa Production. Directed by Benjamin Busungu for kokwa Production https://www.instagram.com/kokwaproduction/. Thanks to Kokwa Production team, Revocatus Busungu, Michael Kizo, Kareem Kandoro, Irene Thadeo and Emil Tibihika.

Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman yawasili Dar es salaam kutokea Zanzibar

$
0
0
Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ iliyofika Zanzibar Oktoba 12, 2017, imeng’oa nanga leo mchana kuelekea Dar es Salaam kuendelea na safari yake ya kusambaza ujumbe wa ‘Amani na upendo’ duniani. 
Taarifa kutoka ubalozi mdogo wa Oman zimeeleza kuwa, meli hiyo itakaa Dar es Salaam kwa siku nne kabla kuelekea Mombasa Kenya kwa madhumuni hayo hayo. 
Akizungumza baada ya kuagana na ujumbe wa meli hiyo bandarini Zanzibar, Balozi Mdogo wa Oman Dk. Al Habsi, ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzbar chini ya Rais wake Dk. Ali Mohamed Shein na wananchi wote kwa mapokezi mazuri na ukarimu mkubwa waliouonesha kwa ndugu zao wa Oman. 
Ameomba hali hiyo iendelee, akisema mahaba na ukarimu ndiyo mambo yanayowafungamanisha Wazanzibari na Waomani ambao kihistoria ni ndugu wa miaka mingi.
 Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH ikiingia katika Bandari ya Zanzibar ikitokea Oman ikiwa na Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo,ikiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi  Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumhi wa Serikali ya Oman.
 Meli ya iliyobeba ujumbe kutoka Oman ijulikanayo kwa jina la Fulk Al Salamah ikiwasili katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa na ujumbe wa watu takribani 350 kutoka Oman.

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussen Mwinyi akimlaki Waziri wa Mafuta na Gesi toka Oman Dkt. Mohamed Hamed  Al- Rumhi ambaye ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka kwa mfalme wa Oman uliowasili na meli ya mfalme ya Fulk Al Salamah katika bandari ya Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiteta jambo na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. Al Mahruqi walipokutana katika hafla ya mapokezi ya meli iliyobeba ujumbe kutoka kwa mfalme wa Oman uliowasili katika bandari ya Dar es Salaam leo. Katikati ni Mfanyabiashara wa Tanzania Seif A. Seif.


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussen Mwinyi akiwa na kiongozi wa ujumbe kutoka Oman Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohammed Hamed Al-Rumhi wakitazama ngoma toka kwa moja ya kikundi cha watumbuizaji mara baada ya meli ya Fulk Al Salamah ikiwa na ujumbe wa watu 350 kutoka kwa mfalme wa Oman kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam leo. Picha na: Frank Shija - MAELEZO

DICOTA HEALTH FORUM NOVEMBER 11, 2017


UWANJA WA NDEGE SUMBAWANGA KUANZA KUJENGWA MWEZI DESEMBA MWAKA HUU

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa uwanja wa ndege wa Sumbawanga utaanza kujengwa kwa kiwango cha lami kuanzia mwishoni mwa mwaka huu baada ya taratibu za kumpata mkandarasi kukamilika.

Akizungumza na wananchi wanaozunguka Uwanja huo Prof. Mbarawa amewahakikishia  wananchi wote wanaostahili kulipwa fidia kutokana na kupisha ujenzi huo watalipwa fidia zao katika kipindi kisichozidi miezi miwili kuanzia sasa.

“Jumla ya wananchi 97 ndio wanaostahili kulipwa fidia na kiasi cha shilingi bilioni 3.3  kimetengwa na wataanza kulipwa hivi karibuni kabla ya zoezi la ujenzi wa uwanja huo kuanza” amesema Prof. Mbarawa.

Amewataka wananchi hao kuacha kupita katika uwanja huo kwani ni hatari  kwa usalama wa ndege na usalama wa wananchi wenyewe.

Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Sumbawanga unajengwa kwa kiwango cha lami na kuongezwa urefu kutoka kilomita 1.5 had 1.7 ili kuwezesha ndege kubwa zaidi kutumia uwanja huo na hivyo kuufungua mkoa wa Rukwa na mikoa mingine hali itakayochochea maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa mkoa huo.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mkoa wa  Rukwa, Mussa Mchola amemshukuru Waziri Prof. Mbarawa kwa hatua ya kulipa fidia na kumhakikishia kuwa watamsimamia mkandarasi huyo kikamilifu ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati na kwa ubora unaostahili.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Mbarawa amekagua Ujenzi wa Barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port KM 112 na mizani ya Singiwe na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo ambapo  amemtaka mkandarasi China Railway 15, Bereau  Group Corporation (CR15G)  na Henan Provincial Newcentry Road na Bridge Consultants Limited JV anaejenga kuongeza kasi katika maeneo korofi kabla ya Mvua za masika kuanza. 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mwl. Julieth Binyura amezungumzia umuhimu wa ukamilishaji wa barabara hiyo utakavyonufaisha wilaya hiyo kwa kuwa inaunganisha Wilaya hiyo na bandari ya Kasanga na mpaka wa Kasesha unaounganisha Tanzania na Zambia na hivyo kuchochea uzalishaji na uchukuzi kati ya Tanzania, Kongo na Zambia.

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano iko katika mchakato wa kuunganisha kwa kiwango cha lami barabara zinazoingia katika bandari za mipakani ili kukuza huduma za uchukuzi kati ya Tanzania na nchi jirani kwa njia za magari, ndege na meli.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kushoto), akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mkoa wa  Rukwa, Mussa Mchola (wa pili kulia), wakati alipokagua Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga, Mkoani Rukwa.

 Muonekano wa barabara ya kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga, Mkoani Rukwa. Upanuzi wa Uwanja huo unatarajiwa kuanza mapema mwezi Ujao.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa nne kushoto), akimsikiliza Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mkoa wa Rukwa, Mussa Mchola alipokuwa akimwonyesha mipaka ya uwanja huo Mkoani humo.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akichanganya zege katika Mizani ya Singiwe katika Barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga KM 112, Mkoani Rukwa wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akikagua eneo korofi katika sehemu ya Matai-Kasanga, Mkoani Rukwa wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MADEREVA WA BODABODA ACHENI HARAKA - MAKAMU WA RAIS

$
0
0
Madereva wa Pikipiki (bodaboda) nchini wametakiwa kutii sheria za Usalama Barabarani bila shuruti kwani ajali nyingi zinazotokea barabarani zimekuwa zikisababishwa na uzembe unaofanywa na madereva hao.

Akizungumza leo katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama kitaifa mkoani Kilimanjaro Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa chanzo kikuu cha ajali hizo ni uharaka walionao madereva hao na ukosefu wa mafunzo ya usalama barabarani kwa baadhi ya madereva.

“Madereva wa bodaboda naomba mbadilike, muwe na tabia ya kutii sharia za usalama barabarani bila shuruti kwani ajali nyingi nchini zimekuwa zikisababishwa na nyinyi kutokana na haraka haraka zenu”, amesema Makamu Rais.

Aidha, amefafanua kuwa Tathmini iliyofanywa na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu katika mkoa wa Kilimanjaro imebaini kuwa kuna ajali za Pikipiki 84 zilizojitokeza ambazo kati ya hizo, 61 zimesababisha vifo na zilizobaki majeruhi.

Kuhusu ajali za mabasi ya abiria Mheshimiwa Makamu wa Rais amesema kuwa zimepungua kutokana na uwepo wa mbinu za udhibiti wa mabasi hayo kama vile upigaji picha kwa magari yanayozidisha spidi yakiwa barabarani (Tochi),  na ukaguzi wa mara kwa mara unaofanywa na Jeshi la polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani katika magari ya abiria nchini.

Makamu wa Rais amefurahishwa na mkakati wa Serikali wa uandaaji wa mfumo mpya na wa kisasa wa kuweka kamera zitakazorekodi makosa ya usalama barabarani yanayofanywa na madereva nchini.

Ametoa rai kwa Askari wa Usalama Barabarani kutotumia kigezo cha kupiga Tochi kwa kuwaonea, kuwanyanyasa madereva na kudai rushwa kwani vitendo havikubaliki kisheria na hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo.

“Taswira tunayoitaka ni kuwa wananchi wawaone askari  kama walinzi wa mali zao na maisha yao na si vinginevyo”, amesisitiza Makamu wa Rais.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amelitka Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na wadau wake kuhakikisha wanabadilisha mbinu za namna ya kukabiliana na tatizo la ajali nchini na kuongeza nguvu katika kudhibiti mwendo kasi, ulevi kwa madereva, kutovaa kofia ngumu kwa waendesha bodaboda, kutofunga mkanda kwa baadhi ya abiria na ukosefu wa vifaa vya kuwalinda watoto wadogo wakiwa kwenye gari.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba (Mb), amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa wataboresha na kuunda mbinu mbalimbali ili kudhibiti ajali za barabarani zinazoweza kuepukika.

Amewataka wananchi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika kupunguza ajali za Barabarani na kuwasisitiza madereva kuzingatia sheria za usalama Barabarani kwani hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote anayekiuka sheria hizo.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius Kwandikwa (Mb), amesema kuwa Baraza limekuwa likifanya jitihada mbalimbali ili kudhibiti ajali za barabarani kama utoaji wa elimu kwa umma kupitia vyombo vya Habari kama Televisheni na Redio pamoja na uandaaji wa viperushi na majarida.

Maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa yaliyobeba kauli mbiu “Zuia ajali, Tii Sheria – Okoa maisha”, kwa mwaka huu yameadhimishwa mkoani Kilimanjaro amabapo yameshirikisha wadau mbalimbali wa usalama nchini.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa yaliyofanyika mkoani humo
Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa yaliyofanyika mkoani humo, leo.

 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usalama Barabarani na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joyce Mbunju, akieleza mikakati inayofanywa na Serikali katika kudhibiti ajali za barabarnia kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro
 Mpima magari kutoka mzani wa Himo, mkoani Kilimanjaro kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo Mhandisi Adam Labay, akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipotembelea Banda la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kwenye maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiungana na kikundi cha ngoma za asili cha Msanja, kutoka Mkoani Kilimanjaro kucheza   ngoma hiyo katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa yaliyofanyika mkoani humo, leo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, 
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

MAGAZETI YA JUMANNE LEO OCTOBER 17,2017

TOSAMAGANGA ALUMNI ASSOCIATION WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA ZAIDI YA SH MILION MOJA LAKI SITA KATIKA HOSPITALI YA TOSAMAGANGA

$
0
0

Na Fredy Mgunda,Iringa

Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wametoa msaada wa mashuka sabini na tano na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 1,672,500 katika hospitali ya Tosamaganga iliyopo katika katta ya kalenga mkoani Iringa kwa lengo la kuendelea kuboresha sekta ya afya ikizingatiwa kuwa wengi wao waliwahi kutibiwa hapo wakati wanasoma.

akizungumza wakati wa hafla ya kukadhi msaada huo mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi alisema kuwa walijipanga kuja kutoa msaada huu kwa kuwa wangi wao walikuwa wanatibiwa katika hospital hiyo wakati wakiwa masomoni miaka mingi iliyopita.

“Leo hii tunaafya njema kwa ajili tulitibiwa vizuri kipindi tulivyokuwa tunaumwa na ilitusaidia kufanya vizuri masomo yetu na ndio maana leo hii tupo hapa bila kupata huduma iliyobora nafikiri wengi wetu tusinge kuwa hapa” alisema Mbilinyi

Mbilinyi alisema kuwa wamechangisha kidogo walichopata wameamua kununua vifaa hivyo ambavyo wanafikiri vitakuwa na msaada kwa wagonjwa waliopo hospitalini hapo.

“Hiki kidogo tu lakini tunajua kwa namna moja au nyingine vinaweza kuwasaidia wagonjwa na kuwapunguzia mzigo uongozi wa hospitali yetu pendwa ambayo imekuwa ikitutibu kwa muda mrefu sana kipindi tukiwa masomoni katika sekondari ya Tosamaganga” alisema Mbilinyi.
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwa wanajadili kitu walipokuwa kwenye ziara ya kuitembelea shule waliyosoma
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Tosamaganga mkoani Iringa
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwa katika hospital ya Tosamaganga.



SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI

$
0
0
SERIKALI imewataka wananchi kuunga mkono juhudi za usafi kwa kunawa mikono na sabuni ili kujikinga na maradhi yatokanayo na uchafu ili kujenga Taifa lenye watu wenye afya bora.

Akizungumza katika kilele cha wiki ya unawaji mikono kwa maji na sabuni iliyofanyika Kata ya Kiwalani, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Ubora wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(DAWASA), Dk Sufiani Masasi alisema kama Taifa ni muhimu kuwekeza nguvu katika kuelimisha jamii hasa umuhimu wa kunawa mikono na majisafi na sabuni ili kujenga Taifa lenye afya bora.

Akizungumza na jumuiya ya wananchi, waalimu na wanafunzi wa shule za msingi Umoja, Yombo, Mwale na Bwawani, Dk Masasi alisema DAWASA ni mdau muhimu wa usafi wa mazingira ndio sababu waliamua kuadhimisha wiki hiyo kwa kutoa elimu kwa walimu 44 kutoka katika shule hizo pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya mtaa ili wawe mabalozi
wazuri katika kuwaelimisha wanafunzi juu ya umuhimu wake.

Alisema kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni ‘Mikono safi kwa manufaa ya sasa na baadae’ inaikumbusha jamii kuona umuhimu wa kunawa mikono na sabuni ili kujikinga na maradhi yatokanayo na uchafu.

Hivyo alitaka juhudi za pamoja zichukuliwe kuhakikisha wanafunzi wanaelewa umuhimu wa kunawa mikono kwani wao ndio wazazi wa siku zijazo na kwamba DAWASA itaendelea kuunga mkono kampeni za usafi hasa kwa kuendelea kubuni na kutengeneza miundombinu ya majisafi katika Maeneo mbalimbali ya jiji.

Dk Masasi alisema tayari DAWASA imefanikiwa kufikisha mradi huo wa majisafi kwa shule hizo ambapo utanufaisha wanafunzi 5123 pamoja na zahanati ya eneo hilo na kwamba itaendelea kufadhili miradi ya aina hii ili kuunga mkono juhudi hizo za usafi wa mazingira.

Mkufunzi wa mafunzo kwa walimu wa shule hizo, Juhudi Nyambuka ambaye ni Afisa Afya Manispaa ya Temeke alipongeza juhudi za DAWASA katika kusaidia jamii kupata huduma za majisafi na kueleza zitasaidia kupunguza magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji.

Katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma rasmi za maji ya bomba DAWASA, jumuiya za wananchi pamoja na wadau wa maendeleo wamekuwa wakijenga miradi ya maji kupitia programu ya maji na usafi wa mazingira kwa jamii. 

Miradi hiyo ipo katika maeneo mbalimbali kama vile Ukonga, Yombo, Kitunda, Mbagala, Kijichi, Feri,Kigamboni.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Wanafunzi wa Shule za Msingi zilizopo Kata ya Kiwalani wakishiriki igizo lenye lengo la kuelimisha jamii umuhimu wa kunawa mikono na majisafi na sabuni wakati wa kilele cha wiki ya unawaji mikono kwa maji na sabuni yaliyofanyika Kiwalani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images