Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1964 | 1965 | (Page 1966) | 1967 | 1968 | .... | 3272 | newer

  0 0

  WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist iliyopo Boko Basihaya katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wameonyesha kufurahishwa na kampeni iliyozinduliwa hivi karibuni ya '3D' yenye maana ya !Nidhamu, Nidhamu, Nidhamu! kuwa imewaongezea morali wa kufanya vizuri darasani. 

  Wakizungumza na waandishi wa habari jana, wanafunzi hao walisema kampeni hiyo imewasaidia sana katika kufanya vizuri katika masomo yao darasani kwa kile walichodai kuwa kuwa bila ya nidhamu katika jambo lolote hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana. 

  Doroth Samson mmoja wa wanafunzi hao wa kidato cha nne shuleni hapo alisema hawana budi kuupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuzindua kampeni hiyo kwani imewasaidia kuwaongezea nidhamu ya hali ya juu ambayo ni chachu ya kufanya vizuri katika masomo yao. 
  Mwanafunzi wa kidato cha nne, Doroth Samson akizungumza na waandishi wa habari
  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya John Baptist, Aspiter Kibona akizungumza na waandishi wa habari. 
  Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiwa wanajisomea darasani.  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Mwanjelwa akipokea zawadi ya boga lenye uzito wa kilogramu 11 kutoka kwa Afisa Kilimo (Kitengo cha Hifadhi na Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo) kutoka Halmashauri ya Bukombe katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yanayofikia kilele leo tarehe 16 Oktoba, 2017 Mkoani Geita

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtaka Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Temeke,(RCO) kufika mahakamani hapo bila kutoa udhuru, kujieleza kwa nini upelelezi dhidi ya kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mritana mfanyabiashara Revocatus Muyela haukamiliki.

  Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba amesema hayo baada ya wakili wa serikali, Patrick Mwita kuieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua za mwisho kukamilika.

  "RCO aje kutueleza mwenyewe hatua ya upelelezi wa kesi hiyo, kwa sababu imekuwa ikiahirishwa kwa mara hakuna excuse" amesema hakimu Simba

  Kufuatia agizo hilo kesi imeahirisha hadi October 30/2017.

  Washitakiwa Miriam na Revocatus Februari 23, mwaka jana waliachiwa huru mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa kisha wakakamatwa tena na baadaye kusomewa mashtaka upya ya mauaji.

  Katika kesi hiyo namba 5/2017 wanadaiwa Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Kwa makusudi walimuua Dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya.

  0 0

   Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Joyce Moshi, (56) akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka aliyonayo.

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
  MHASIBU wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Joyce Moshi, (56), leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka tisa matatu ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo  wizi akiwa mtumishi wa umma, kujipatia fedha kwa njia ya uongo na utakatishaji wa fedha USD 150,000.

  Mwendesha mashtaka wakili wa serikali, Wankyo Simon amedai Octoba 25 mwaka jana, katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania katika jiji la Maputa nchini msumbiji mshtakiwa Joyce kwa lengo la kufanya udanganyifu alighushi barua ya tarehe 25 October 2016 kwa madhumuni ya kuonesha kuwa ubalozi wa Tanzania nchni Msumbiji umeelekeza benki ya Millenium Bim, Maputo kuamisha USD 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Joyce Moshi.

  Imedaiwa kuwa, akaunti zote hizo zipo katika benki ya Millennium Bim-Julius Nyerere Maputo, huku akijua kuwa siyo kweli.
  Aidha mshtakiwa Joyce anayeishi Temeke anadaiwa Februari 10 mwaka huu huko huko Ubalozini nchini msumbiji, alighushi USD 100,000 na pia Aprili 12 mwaka huu alighushi tena USD 40,000.
  Katika shtaka linguine Wankyo alidai kuwa, Oktoba 25, mwaka jana katika benki ya Millenium Bim-tawi la Julius Nyerere lililopo Maputo nchini Msumbiji. 

  Imedaiwa, mshtakiwa akifahamu na kwa njia ya udanganyifu aliwasilisha nyaraka ambayo ni barua ya tarehe Oktoba 25 mwaka jana kwa dhumuni la kuonyesha kuwa,  ubalozi wa Tanzania nchni Msumbiji umeelekeza benki ya Millenium Bim, Maputo kuamisha USD 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Joyce Moshi.
   
  Pia aligushi barua ya Februari 10 mwaka huu ili kuhamisha USD 100,000 na barua ya Aprili 12 mwaka huuu ili kuhamisha USD 40,000.
  Mshtakiwa Joyce anadaiwa pia kuwa, katika siku tofauti tofauti kati ya Oktoba 25 mwaka jana na Aprili mwaka huu, katika ofisi hizo za Ubalozi, akiwa muajiriwa wa utumishi wa umma wa kitengo cha fedha ubalozini hapo, aliiba USD 150,000 mali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

  Pia Joyce anadaiwa kujipatia kiasi hicho cha pesa kwa njia ya udanganyifu kwa kujifanya kuwa ameelekezwa kutoa fedha hizo kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inaymilikiwa na Joyce Moshi huku akaunti zote hizo zimehifadhiwa kwenye benki hiyo ya Millenium.

  katika shtaka la mwisho imedaiwa, katika tarehe tofauti kati ya Octoba 25 mwaka jana na Aprili 12 mwaka huu alijipatia USD 150,000 huku akijua kuwa fedha hizo ni matokeo ya kosa la kughushi.

  Hata hivyo, mshtakiwa amekana shtaka hilo na amerudishwa rumande kwa kuwa kosa la utakaishaji halina dhamana na kesi hiyo imeairishwa hadi Octoba 30 mwaka huu.
  Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

  0 0

  *Asisitiza Uwaziri si fursa ya kujitajirisha          
                             
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri watumie madaraka yao kwa manufaa ya Taifa na kamwe wasiyatumie kama fursa ya kujitajirisha wao binafsi.

  Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 16, 2017) alipozungumza na baadhi ya Mawaziri, Manaibu na Makatibu Wakuu katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

  Amesema Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza kwamba amewateua ili wafanye kazi na kamwe wasitumie madaraka waliyopewa kwa maslahi yao binafsi.

  “Madaraka haya ya Uwaziri si fursa ya kujipatia utajiri, tunatakiwa tufanye kazi kwa weledi, uadilifu, bidii na uaminifu mkubwa ili kuondoa kero za wananchi kwa wakati.”

  Amesema Mawaaziri na Manaibu Waziri wazingatie Katiba ya nchi, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ya Serikali katika utekelezaji wa majikumu yao ya kila siku.Waziri Mkuu amesema Mawaziri hao wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.

  Pia utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 pamoja na ahadi alizozitoa Rais Dkt Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi.Waziri Mkuu amewaagiza Mawaziri wahakikishe wanakwenda kufanya ufuatiliaji wa tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao.

  Pia amewataka Mawaziri hao wakasimamie kikamilifu ukusanyaji wa mapato na kuanzisha vyanzo vipya vya ukusanyaji pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu.Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka Mawaziri hao wakapunguze urasimu katika utekelezaji wa malengo ya Serikali kwa sababu wananchi wanahitaji kuhudumiwa kwa wakati.

  Mawaziri waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Bw. Suileiman Jaffo pamoja na Manaibu wake Bw. Joseph Kandege na Bw. George Kakunda, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile.

  Wengine ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu wake Bw. Jumaa Aweso, Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Charles Mwijabe na Naibu wake Mhandisi Stella Manyanya.

  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Naibu wake Bw. Josephat Hasunga, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Naibu wake Bw. William Ole Nasha, Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw. Abdallah Ulega pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo.


  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania

  Leo siku ya Oktoba 16 dunia inaadhimisha Siku ya Chakula Duniani ambapo Shirika la Chakula Duniani (FAO) kila mwaka huadhimisha kwa shughuli na kauli mbiu mbalimbali. Kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Badili Hali ya Uhamiaji ya Baadaye: Wekeza Katika Usalama wa Chakula na Maendeleo ya Vijijini.’ Kwa mujibu wa FAO, dunia inapitia mabadiliko kadha wa kadha kila kukicha. 

  Watu wengi wamelazimika kuhama makazi yao kutokana na sababu tofauti kama vile kuongezeka kwa migogoro na kutokuwepo usalama wa kisiasa. Lakini njaa, umasikini, na kuongezeka kwa matukio ya hali ya hewa yanayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa ni sababu zingine za muhimu zinazochangia katika kupelekea watu kuhama.
  Miongoni mwa changamoto kubwa inayowakumba watu siku za hivi karibuni ni katika upatikanaji wa chakula, matumizi yake na namna ya kudhibiti ili kutoleta athari katika mwili. Kwa kuwa leo ni maadhimisho ya ‘Siku ya Chakula Duniani,’ Jumia Travel ingependa kukushirikisha aina za vyakula vya kupunguza au kuacha kula kabisa kama unataka kupunguza uzito wa mwili wako.
  Chipsi. Kwa wakazi wengi wa sehemu za mijini kama vile jiji la Dar es Salaam, chipsi ni mojawapo ya chakula kinachotumiwa na idadi kubwa ya watu. Na hii ni kutokana na upatikanaji wake kwa urahisi karibu kwenye kila maeneo wanapoishi. Kwa mujibu wa tafiti, chakula hiki kinaongeza uzito mwilini kutokana na kuwa na kalori nyingi ndani yake na ni rahisi kuzila nyingi zaidi kwa mpigo. Tafiti pia zinaendelea kwa kuelezea kuwa chipsi pengine ndiyo chakula kinachochangia kuongeza uzito kuliko chakula chochote. Hivyo basi, kwa afya yako unashauriwa kuvichemsha kwa maji na kula badala ya kukaanga.
  Vinywaji vyenye sukari nyingi. Vinywaji vinavyotengenezwa na kuongezewa sukari ili kuwa vitamu vinatajwa kuwa ni mojawawapo vyakula hatari zaidi kiafya duniani. Vinahusishwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa uzito na vinaweza kuwa na madhara zaidi mwilini endapo vitatumiwa kwa kiasi kikubwa. Ingawa vyakula hivi huwa na kalori nyingi lakini ubongo wako hauvitambui kama ni vyakula vigumu. Kwa hiyo, kama una nia ya dhati kabisa ya kupungua uzito ni vema ukaachana na vinywaji vya aina hii.

  Chokoleti. Inafahamika watu wengi hupendela chokoleti kutokana na utamu wake lakini ni hatari sana kiafya. Hutengenezwa kwa kuongezewa sukari nyingi zaidi, mafuta na unga uliosafishwa zaidi kiwandani kwa kiasi fulani. Chokoleti zina kalori nyingi huku virutubisho vikiwa ni vichache. Kipande cha kawaida cha chokoleti kina kadiriwa kuwa kalori takribani 200-300, huku vipande vikubwa zaidi vinaweza kuwa nazo nyingi zaidi. Lakini kwa bahati mbaya unaweza kukutana na chokoleti karibu kila mahala tena zikiwa zimewekwa kwa kutamanisha zaidi ili kukushawishi kununua. Inashauriwa kama unataka kula chakula kidogo cha kawaida badala yake kula kipande cha tunda au karanga angalau.
  Juisi za viwandani. Juisi nyingi za matunda unazoziona madukani zinakuwa na virutubisho vidogo sana ukilinganisha na tunda halisi. Nyingi huwa zinatengenezwa viwandani na kuongezewa sukari. Kiukweli, huwa na sukari nyingi na kalori sawa na soda, tena inawezekana vikazidi. Kwa kuongezea juisi za viwandani hazina nyuzinyuzi ambazo unaweza kuzipata kwenye matunda halisi. Hivyo basi unashauriwa ni vema ukala tunda kamili badala ya juisi kwani faida zake haziwezi katu kulingana kama wengi tunavyoamini. 


  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  Baada ya kukaa gerezani kwa siku tano, leo vigogo wawili wa zamani wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) wameachiwa huru baada ya kukamilisha masharti ya dhamana waliyopewa ma Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

  Washtakiwa hao ambao wametimiza masharti ya na kuachiwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ni, Kaimu Mtendaji wa (TIA), Shaha Hanzuruni na Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Onesphor Luhungu wa Hakimu Mkazi Mkuu,


  Katika masharti yao ya dhamana kila mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini bondi ya milioni 250 na pia mdhamini mmoja kati ya wadhamini hao kuwasilisha fedha taslimu mahakamani Sh 250 milioni ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha na kwamba mali hiyo ni lazima iwepo Dar es Salaam.

  Mbali na hayo kila mshtakiwa alitakiwa kusalimisha pasi yake ya kusafiria mahakamani na wasitoke nje ya jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha Mahakama.

  Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 24,2017 ambapo washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali (PH).Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara ya Sh 1, 097,681,107.


  0 0

  Na Veronica Simba – Dodoma.

  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Khamis Mgalu, ameripoti rasmi Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma asubuhi hii, Oktoba 16, 2017.
  Naibu Waziri Mgalu amepokelewa na watumishi wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini waliopo Dodoma, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lusias Mwenda.

  Baada ya kuwasili, Naibu Waziri ametumia muda mfupi kuzungumza na wafanyakazi ambapo amewataka kufanya kazi kwa bidii, weledi na kujituma.

  Akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya wafanyakazi, Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu, Miriam Mbaga, amemwahidi Naibu Waziri kuwa, wafanyakazi wako tayari kumpa ushirikiano yeye na viongozi wengine wa Wizara ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwatumikia wananchi kikamlifu.

  Naibu Waziri Mgalu, ni miongoni mwa Mawaziri wapya walioteuliwa na Rais John Magufuli na kuapishwa Oktoba 9, 2017, wakati alipofanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.
   Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lusias Mwenda (kulia), akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Subira Mgalu, Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani), aliporipoti rasmi Makao Makuu ya Wizara, mjini Dodoma.
   Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu, Miriam Mbaga, akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, wakati wakimpokea Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani).
   Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akizungumza na wafanyakazi aliporipoti rasmi Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
   Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Amon Marco (wa pili kutoka kulia), akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), wakati Naibu Waziri alipowasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto), akisalimiana na watumishi, alipowasili Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.

  0 0

  Na Mwandishi wetu wa Globu ya Jamii.

  KATIKA kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 18 ya kifo  cha hayati Baba  wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Chama Cha Mapinduzi(CCM)  katibu wa chama wilaya ya ubungo,Salum  kali  ameweka jiwe la Msingi kwa ajili ya   ujenzi wa ofisi za chama katika tawi la sinza "A"  

  Akihutubia wanachama walio  jitokeza  katika shughuli  hiyo  kali amesema, Baba wa taifa  alitengeneza  heshima kwa  Mtanzania  aheshimu  kwanza  maadili ya taifa lake ndio aweze  kuheshimiwa na watu wengine.

  aidha kali amesema kuwa ,  Mwalimu Nyerere  aliamini ndani ya  chama  cha Mapinduzi  CCM ndiko  kunapo patikana  viongozi bora  ambao wana uwezo  wa kufanya  kazi  kwa umakini pasipo  malumbano wala fujo  kama tunavyo  ona kwa wenzetu  wa pembeni.

  "Mwalimu Nyerere  aliamini  viongozi wa ccm  pekee ndio wanao weza  kusimamia  amani ya nchi hii na ndio kitu ambacho  mpaka sasa chama cha Mapinduzi  kinaendelea kufanya  kupitia Rais   wa  Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli" amesema Kali.
   Katibu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM)  Salum  Kali akishiriki ujenzi wa ofisi za chama kata ya Sinza A.
   Katibu wa chama akizindua jiwe la msingi la  ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Sinza "A"  Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   Ugawaji wa Vyeti kwa wadau wa Utalii katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Mdau wa Utalii akipokea Cheti cha Ushiriki katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizindua Mradi  wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqqaro akisalimia na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa ili kuzindua mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Mdau wa Utalii akiuliza Swali kwa waendesha Mada katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.
   Ndugu Salehe akiuliza Swali kwa waendesha Mada katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha.


  0 0

  A Tanzanian former president Hon.Ally Hassan Mwinyi leading a thousands of participants who participated in the Rotary Dar Marathon. The Marathon took place in Dar over the weekend was organised by the Rotary Clubs in partnership with bank M with the aim of raising funds for construction of a new clinic at CCBRT. With the white cap is the Minister of Information, Culture,Artists and Sports Dr. Harrison Mwakyembe who also participated in the Marathon.
  A Tanzanian former president Hon.Ally Hassan Mwinyi posing for a photo after awarding the 3rd winner of the Rotary Dar Marathon Alex Nizeyimana. The Marathon took place in Dar over the weekend was organised by the Rotary Clubs in partnership with bank M with the aim of raising funds for construction of a new clinic at CCBRT. Looking on (left) is the Minister of Information, Culture,Artists and Sports Dr. Harrison Mwakyembe.
  A thousand of participants of the rotary Dar Marathon which was organized by the rotary clubs in partnership with bank M.

  0 0

  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam inatarajia kuanza kusikiliza kesi ya mauaji ya bila kukusudia inayomkabili Mwigizaji Elizabeth Michael maarufu kama Lulu October 19, 2017.
  Lulu anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kumuua Msanii mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia, kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu (PC), April 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican.
  Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji ya bila kukusudia iliyotolewa na Mahakama Kuu, kesi ya Lulu itaanza kusikilizwa siku hiyo ya October 19, 2017 mbele ya Jaji Sam Rumanyika.
  February 18, 2014 akisomewa maelezo ya awali (PH) alikiri Mahakamani kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kanumba na pia kuwa kulikuwepo na ugomvi baina yao siku ya tukio la kifo cha Mwigizaji huyo.
  Lulu aliachiwa kwa dhamana January 29, 2013 baada ya kesi hiyo kubadilishwa hati ya mashtaka kutoka kwenye kesi ya mauaji ya bila kukusudia ambapo badiliko hilo lilimpa nafasi ya kupata dhamana.
  Katika kesi ya msingi namba 125 ya mwaka 2012, inadaiwa kuwa April 7, 2012 Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia.

  0 0

  Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akizungumza baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme mkoani Mtawara leo Oktoba 16, 2017 ili kujionea kazi inayofanywa na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) kurekebisha mashine 8 kati ya tisa zilizoharibika. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, na kulia ni Kamu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.

   NA K-VIS BLOG/Mtwara.

  Serikali imewaomba wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kuwa na subira, katika kipind hiki ambapo upatikanaji wa umeme kwenye mikoa hiyo umeathirika baada ya mashine 5 kati ya 9 za kufua umeme (turbines) kuharibika.

  Hata hivyo Mafundui wa TANESCO wamekuwa katika juhudi kubwa za kuzifanyia matengenezo mashine hizo, zilizofungwa miaka 10 iliyopita.

  "tayari tumeagiza vipuri kwa ajili ya kutengeneza mashine hizo ambazo kwa ujumla wake huzalisha Megawati 18 za umeme, ambazo zitawasili ndani ya siku 7 ili kuweza kuondoa tatizo la kuzimika umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara." Alisema Dkt. Kalemani.

  Alisema, baada ya kwasili kwa vipuri hivyo, kazi ya kuzifanyia matengenezo itaendelea na amememuagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, kuleta wataalamu wote wa TANESCO popote walipo nchini, wafika Mtwara na kuungana na wataalamu waliopo ili kazi ya kuzitengeneza mashine hizo iende kwa kasi.
   Fundi wa TANESCO, akitengeneza moja ya mashine zilizoharibika kwenye kituo cha kufua umeme mkoani Mtwara.
   Fundi wa TANESCO, akichukua spana ili kuendelea na kazi.
   Hii ni moja kati ya mashine zizlizoharibika.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Dar es Salaam. Tanzania itawakilishwa na timu mbili za kuogelea katika michezo ya kanda ya tatu ya kuogelaa ya Afrika yaliyopangwa kuanza Alhamis katika bwawa la Hopac la jijini.

  Tanzania imepewa nafasi ya kuwa na timu mbili kutokana na kuwa mwenyeji.Katibu Mkuu wa Chama Cha kuogelea Tanzania (TSA) Ramadhan Namkoveka alisema jana kuwa timu ya kwanza imepewa jina la Tanzanite ambayo itakuwa na jumla ya wachezaji 30 na ya pili inajulikana kwa jina la Platinum ambayo itakuwa na wachezaji 21.

  Namkoveka alisema kuwa timu ya Tanzanite itakuwa na wachezaji 15 wanaume na 15 wanawake na ile ya Platinum itakuwa na wachezaji tisa wanawake na 12 wavulana.Timu hizo zipo kambini hotel ya Giraffe chini ya makocha, Alexander Mwaipasi na Michel Livingstone na zinafanya mazoezi yake kwenye bwawa la Hopac kila siku.

  Wachezaji wanaoumda timu ya Tanzanite ni Rania Karume , Chichi Zengeni, Maia Tumiotto, Smriti Gokarn (Sonia Tumiotto, Anjani Taylor ambao wote wanatoka klabu ya DSC, huku wengine ni Natalie Abwooli Sanford (MIS), Anna Guild, Emma Imhoff (MSC), Sanne Kleinveld ( ISM Moshi), Angelica Spence, Tara Behnsen, Tami Triller,Kayla Gouws na Amani Doggart ambao wanatoka klabu ya Taliss.
  Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Hilal Hemed Hilal akishindana wakati wa mashindano ya Taifa ya kuogelea.
  Mchezaji wa kuogelea wa timu ya Taifa, Collins Saliboko akichuana katika mashindano ya Taifa ya kuogelea.  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kulia) hii leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini  Tanzania Hanne-Marie Kaarstad (katikati) Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuendelea kushirikiana katika sekta ya Hifadhi na Usimamizi endelevu wa mazingira nchini.
   Sehemu ya wajumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na wale wa Ubalozi wa Norway wakifuatilia majadiliano hayo baina ya Balozi wa Norway nchini  Tanzania Hanne-Marie Kaarstad na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri Makamba akiongea na wageni kutoka Ubalozi wa Norway hapa nchini walipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Mathias Canal, Geita

  Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba leo Octoba 16, 2017 amefunga rasmi maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita kuanzia Octoba 10 mpaka Octoba 16, mwaka 2017.

  Akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho hayo waziri Tizeba alisema kuwa Kuanzia msimu huu wa kilimo Wakulima wa korosho watapata bure pembejeo aina ya salfa zilizokuwa zikiuzwa kwa bei ya ruzuku.

  Alisema Hatua hiyo ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha vikwazo vyote vilivyokuwa, vikiwakabili Wakulima wa zao la korosho vinaondolewa ili kuwawezesha kuongeza uzalisha na tija zaidi kutokana na zao hilo.

  Mhe Tizeba alisema Madhumuni ya Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ni kutoa nafasi ya kutafakari, namna Jamii katika ngazi ya Kaya, Kijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa, Taifa na Kimataifa zinavyoweza kuhakikisha ongezeko la uzalishaji na upatikanaji wa chakula cha kutosha na chenye lishe bora kwa watu wote na kwa wakati wote. 

  Alisema kuwa Kila mwaka Shirika la Chakula Duniani (FAO) baada ya kufanya tathmini ya hali ya Chakula hutoa Kaulimbiu ambayo huwa ni dira ya maandalizi na maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani. 
  Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
  Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba alipotembelea banda la Kampuni ya POLYTECH MACHINERY inayojishughulisha na uuzaji wa mashine mbalimbali ikiwemo za kukamua mafuta ya alizeti wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita. Mwingine ni Mhe Dkt Mary Mwanjelwa Naibu waziri wa Kilimo (Kulia).
  Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya siku ya chakula Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
  MKUU wa Wilaya ya ISame Mkoa wa Kilimanjaro, Rosemary Sinyamule ameongoza mazoezi ya wakazi wa Wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya utamaduni waliojiwekea watumishi na wakazi wa eneo hilo kila ifikapo mwisho wa wiki.

  Dc Sinyamule amesesma kuwa mazoezi yamekuwa ni utamaduni hivyo wananchi hao upata fursa ya kujumuika na viongozi wao katika siku ambazo sio za kazi na kuweza kupata nafasi ya kuzungumza mambo ya kawaida yanayohusu maisha yao ya kila siku katika mfumo wa kawaida . 

  " leo wananchi wamepata fursa muhimu ya kusikiliza maelekezo ya afya kutoka na  umuhimu wa mazoezi kutoka Kwa mganga Mkuu wa Wilaya ya Same . Dr. Andrew ambaye aliwataka wakazi wa eneo hilo kutunza afya  kwa kufanya mazoezi mara tatu kwa wiki hili kuweza kujiepusha na magonjwa yasiyokuwa ya lazima" amesema Dc Sinyamule.

  DC Sinyamule ameongeza kuwa  katika kuadhimisha wiki ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayat Mwl Julius Nyerere ni kila mmoja kuona namna anavyomuenzi kwani alikuwa Mazalendo na alipigania Uhuru akiwa katika umri mdogo hivyo  kuwasisitiza Vijana kufanya yale yote yaliyofanywa na Mwalimu katika harakati zake.

  DC Sinyamule alimaliza kwa kuwashukuru wananchi wa Same Kwa kuendelea kujitokeza Kwa wingi. Pia aliwakumbusha kila mmoja kujipangia ratiba ya mazoezi kila siku. na si kungoja siku moja Kwa mwezi.
   Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akiwa katika picha ya pamoja na Wanachi waliojitokeza katika Mazoezi Wilaya ya Same.
  Wakazi wa Wilaya ya Same wakiwa katika Mazoezi ya Pamoja yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Rosemary Sinyamule.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeelezwa kuwa, upelelezi dhidi ya kesi ya kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii  wa Face book kuhusu mazungumzo kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia, inayomkabili Mkazi wa Chato Geita, Obadia Kiko bado haujakamilika.

  Wakili wa Serikali, Adolf Mkini amesema hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

  Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 14 mwaka huu.

  Katika kesi hiyo, inadaiwa Agosti 3, mwaka huu huko Chato Geita mshtakiwa obadia anadaiwa kusambaza maneno kuwa " Taarifa kutoka kikao cha mazungumzo kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia kuwa wanasheria wa upande wetu wanashindwa kutafsiri baadhi ya vifungu vya sheria hadi kufikia kuomba msaada kwa wanasheria wa Acacia sasa huoni hivi ni vituko mwizi anakusaidia sheria haahaa haha."

  Inadaiwa aliendelea kusambaza maneno kuwa "Mazungumzo bado yanaendelea lakini wanasheria wetu wamebanwa sana ukizingatia wale jamaa wana vielelezo vyote vya mikataba kiukweli tumuombe mungu maana Serikali ikitaka kuvunja mkataba na Acacia gharama kubwa zitatuusu."

  "Lakini pia kuendeleza uvyama utatugharimu saana,  baada ya mh. Rais Magufuli angewashirikisha Mawakili wasomi waliokwishaiva wakili Lissu, wakili Kibatara na Fatma Karume kwenye mambo ya umuhimu kama haya yeye kaleta uchama sasa itatugharimu .// Dicteta Magufuli mist go" . Maneno hayo yanadaiwa kusambazwa na mshtakiwa huyo kupitia mtandao huo wa kijamii wa Facebook.

  Ilidaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo la kupotosha umma

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
  MKUU wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule  amewataka Vijana kuwa wazalendo hili kuweza kuyaenzi yale yote yaliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kipindi cha uhai wake .

  hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule alipokuwa akitoa mada  kwa vijana iliyohusu  "Kijana na Uzalendo"  kwa Vijana wa Ukwata zaidi ya 1000 wa Wilaya ya  Same na uzinduzi wa Kitabu kilichohusu Maisha ya Mwalimu Nyerere.

  "Mwl. Nyerere alivyokuwa mzalendo na mpaka sasa ndiye Mtanzania wa kwanza aliyeonyesha Uzalendo wa kiwango cha juu kabisa akifuatiwa na Rais wetu wa sasa Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli hivyo nyie Vijana Mnapaswa kuenenda kama viongozi wetu hawa wanavyotutaka hili tuwe na Taifa la Wachapakazi na Wazalendo" amesema Sinyamule. 


  katika Uzinduzi wa kitabu kilichoandikwa na Kijana kwa ajili ya kuelimusha vijana wa kike kujitambua na kuchukua hatua muhimu kwa ajili ya mustakabali wao wa baadaye  kinachokwenda kwa jina la  " A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".


  Mara baada ya kuzindua kitabu hicho mkuu wa Wilaya hiyo aliweza kununua vitabu 51 na kuagizwa visambazwe kwenye shule zote 51 za Sekondari Wilaya ya Same, viwekwe maktaba ili wanafunzi waweze kuvisoma 

  Aidha Dc Sinyamule alimpongeza  mwandishi wa kitabu hicho Elihuruma kwa uandishi huo na kumtaka aendelee kuandika vitabu vingi zaidi kwa faida ya Vijana na watanzania kwa ujumla.
   Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akizungumza wakati akitoa mada kwa Vijana wa Ukwata Wilaya hiyo na kabla ya kuzindua kitabu cha A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".
   Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akizungumza wakati akitoa mada kwa Vijana wa Ukwata Wilaya hiyo na kabla ya kuzindua kitabu cha A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".
  Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akizindua kitabu cha A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".
  Wanafunzi wa UKWATA wamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Same juu ya mada ya Uzalendo

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiwa na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt.Mohammed Bin  Hamed Al Ruhmi katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja wakati  hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Ujumbe wa Serikali ya Oman uliotembelea Zanzibar kwa ziara ya siku tatu Nchini iliyofanyika jana.
    Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi na Ujumbe wa Serikali ya Oman wakiwa katika hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja
   Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi wakiwa katika hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kwa Ujumbe wa Serikali ya Oman uliotembelea Zanzibar kwa ziara ya siku tatu ambayo iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja
   Kikundi cha Taifa cha Sanaa ya Muziki wa Taarab kilipokuwa kikitumbiza jana wakati  hafla ya Chakula cha jioni kilichoandalia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kwa Ujumbe wa Serikali ya Oman uliotembelea Zanzibar kwa ziara ya siku tatu Nchini, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Zamani wa baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1964 | 1965 | (Page 1966) | 1967 | 1968 | .... | 3272 | newer