Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV VPL: SIMBA SC 1 - 1 MTIBWA SUGAR


NGUVU YA PAMOJA INATAKIWA KUKABILIANA NA VITENDO VYA MIMBA KWA WANAFUNZI

$
0
0
Na Tiganya Vincent, RS-Tabora

SERIKALI ya Wilaya ya Tabora imesema kuwa kunahitajika nguvu ya pamoja kwa wanajamii wote katika kukabilana na vitendo vya baadhi ya watu wazima kuwapa mimba watoto na hasa wanafunzi katika shule mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Queen Mlozi wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha watendaji mbalimbali wa Mkoa wa Tabora.

Alisema kuwa jitihada hizo zinatakiwa kuwa ni pamoja na kutoa elimu ya uzazi kwa wananfunzi juu ya kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kuwasababisha kupata ujauzito na hivyo kukatisha ndoto ya kupata elimu kwa ajili kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye na kuwa viongozi wajao.

“Jambo ambalo tunaloweza kufanya ni kutoa elimu kwa watoto wetu wa kike , wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari…wazazi tupo, viongozi tupo, walezi tupo na walimu tupo tunafanya nini kuwakinga watoto hao wasipate mimba…inabidi tufanye kazi kwa pamoja katika kukomesha vitendo hivyo” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Alisema kuwa kwa upande wake ataendelea kutumia mikutano yake atakayokuwa akifanya kuhakikisha kuwa anawaelimisha wanafunzi na wazazi juu ya kupambana na tatizo hilo linarudisha nyuma maendeleo ya watoto wa kike.

Queen alitoa wito kwa wazazi kuwaelimisha watoto wao wa kike kuhusu mabadiliko ya miili yao na athari za kutojikinga.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa itakapobainika kuwa mtoto ana ujauzito atamkamata mzazi na mtoto ili wamumtaje mhusika.

KARIA AMPONGEZA SANGA AKIAHIDI USHIRIKIANO TPLB

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amempongeza Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ligi Kuu, Clement Andrew Sanga wa Young Africans kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa TPLB baada ya kupata kura 10 kati ya 16. Katika  katika uchaguzi uliofanyika leo Oktoba 15, 2017 kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mpinzani wa Sanga, Hamad Yahya Juma wa Mtibwa Sugar alipata kura sita kati ya 16 za Klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Wakati Sanga akichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Shani Christoms Mligo wa Azam FC alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa TPLB. Shani aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo alipata kura 15 kati ya 16 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Nafasi tatu za kuwakilisha klabu za Ligi Kuu kwenye Kamati ya Uongozi zilivutia wagombea wawili; Hamisi Mshuda Madaki (Kagera Sugar) na Ramadhani Marco Mahano (Lipuli) ambao wote wameshinda. Madaki alipata kura 12 na Mahano 13.

Almasi Jumapili Kasongo kutoka Ashanti United FC ni mgombea pekee aliyejitokeza kuwania nafasi ya uwakilishi wa klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 35 kati ya 40 zilizopigwa. Edgar William Chibura kutoka Abajalo FC alishinda nafasi ya Ujumbe kutoka Klabu za Ligi Daraja la Pili ambako zina nafasi moja kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB. Chibura alipata kura 35 kati ya 40.

“Natuma salamu zangu za pongezi kwa wote walioshinda. Nina imani nao kwamba tutashirikiana vema, kufanya kazi katika sekta ya mpira wa miguu, najua wanajua changamoto za ligi yetu hivyo naamini wataweza,” amesema Rais Karia mara baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocatus Kuuli kutangaza matokeo.

Mapema kabisa leo asubuhi, Rais Karia aliahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Kamati mpya ya Uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) waliochaguliwa leo Oktoba 15, 2017. Rais Karia aliyeambatana na Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred alitoa ahadi hiyo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Baraza la TPLB uliofanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

“Tupo kwenye kikao hiki ambacho pia kitachagua viongozi wakaoongoza miaka minne ijayo, viongozi watakaochaguliwa leo kwa nia njema wataongoza Bodi kwa miaka minne… “Bahati nzuri nilikuwa mmoja wa viongozi wa kwanza wa Bodi ya Ligi. Kwa hiyo najua changamoto tangu uundwaji wake. Hivyo nakifahamu chombo hiki vema, najua kwa undani malengo ya chombo hiki, lazima tuyafikie.

“…Lakini niwahakikishie tu kwamba hatutafika kama tutaendesha shughuli zetu bila uwazi, uadilifu na uwajibikaji,” amesema Rais Karia.

“Naahidi kuona kamba chombo hiki kipo huru. TFF itakuwa ikifanya monitoring. Tukiona mambo hayaendi sawa, hatutasita kukaa nanyi watu wa Bodi ili tushirikiane kuweka mambo sawa,  mvumiliane huku mkifuata taratibu,” amesema.

Rais Karia amesema kwamba uadilifu, uwazi na uwajibikaji upo zaidi kwa lengo la mpira wa miguu kuchezwa kwa weledi ili tupate mabingwa wa kweli  katika mashindano yanayosimamiwa na kuendeshwa na TFF. Rais Karia aliasa viongozi wa klabu kubadilika na hasa kutoa ushirikiano kwa viongozi wa TPLB, “Nami nitatoa ushirikiano kwenu.”

Awali kabisa Mwenyekiti wa TPLB, Hamad Yahya akimkaribisha Rais Karia, aliwakaribisha viongozi wote waliohudhuria huku akiwapa pole kwa safari ndefu hadi kuja kwenye mkutano. Baada ya matokeo, Yahya alirudi tena kuzungumza na Wajumbe ambako aliwashukuru kwa ushirikiano waliompa wakati akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa TPLB na kuahidi, “Nipo bado kwenye mpira tutaendelea kushirikiana. Uchaguzi umekwisha, hakuna makundi.”

Kwa upande wake, Sanga alimshukuru Mungu na wajumbe wote kwa uchaguzi wa amani na utulivu, ishara inayompa nguvu kutekeleza vema majukumu yake mapya.

PROF. MBARAWA AMCHARUKIA MKANDARASI WA SIA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, (kushoto) , akikagua ujenzi wa jengo la abiria linalojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), Waziri huyo alifanya ziara ya ukaguzi na kuangalia maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi huo hadi sasa. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa mkandarasi GM Construction anayejenga jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), kukamilisha ujenzi huo.

Amesema Serikali hairidhishwi na kasi ya ujenzi wa jengo hilo ambalo limetumia miaka minne badala ya miwili iliyokubalika katika mkataba wa awali hivyo kumtaka mkandarasi huyo kuhakikisha analikabidhi jengo hilo ifikapo Januari 30 mwakani.

“Kushindwa kukamilisha jengo hili ifikapo mwezi Januari mwakani itakuwa ndio tiketi yako ya mwisho ya kutopewa kazi kwasababu Serikali hii inafanya kazi kwa kuzingatia ubora na muda”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa kusimamia kikamilifu ujenzi huo ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa.

“Ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege kwa sasa unasimamiwa na TANROADS na uendeshaji wake unasimamiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuongeza kasi ya ujenzi wa viwanja vya ndege na ubora wa huduma zinazotolewa katika viwanja hivyo”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa, amekagua upanuzi wa barabara katika mji wa Tunduma unaolenga kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo na kuwahakikishia wananchi kuwa ujenzi wake utakamilika mwishoni mwa mwezi ujao.
Amewataka wakazi wa Tunduma kuilinda miundominu ya barabara hizo kwa kuzingatia matumizi sahihi ili kuleta usalama kwa wananchi.

Naye Meneja wa TANROADS, mkoa wa Songwe Eng. Yohane Kasaini, amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kwamba barabara za michepuko zitaongezwa katika eneo la Tunduma ili kurahisisha shughuli za kibiashara na uzalishaji katika mji huo.

Prof. Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua miundombinu katika mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa.
Mhandisi Mshauri anayesimamia ujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), Eng. Nyamhanga Wanda, akitoa maelezo ya mradi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, mkoani Mbeya.
Mkandarasi anayejenga jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), Kannan Thiyagamoorthy, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, mkoani Mbeya.
Muonekano wa Jengo la abiria linalojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA). Jengo hilo limetakiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwezi Januari, 2018.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza na wananchi wa Tunduma wakati akikagua upanuzi wa njia nne ya barabara ya Tunduma-Sumbawanga KM 1.45, mkoani Mbeya.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Songwe Eng. Yohane Kasaini (katikati), akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), wakati wa ukaguzi wa upanuzi wa njia nne ya barabara ya Tunduma-Sumbawanga KM 1.45, mkoani Mbeya.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Tunduma-Sumbawanga KM 1.45 inayojengwa kwa njia nne, mkoani Mbeya ili kupunguza msongamano wa magari jijini hapo.

TOSAMAGANGA ALUMNI ASSOCIATION WATUMIA ZAIDI YA MILLION 30 KUJENGA CHOO BORA KATIKA SHULE SEKONDARI YA TOSAMAGANGA WALIOSOMA.

$
0
0


Na Fredy Mgunda.



Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefanikiwa kuijengea shule choo bora chenye thamani ya  zaidi ya shilingi milioni thelethini (30,000,000) kwa lengo la kurudisha  fadhila walizozipata wakiwa wanasoma hapo kwa kuwa ndio umekuwa msingi bora wa mafanikio ya wanafunzi wengi waliosoma katika shule hiyo.

akizungumza wakati wa hafla ya kukadhi choo hiyo mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi alisema kuwa lengo ni kukikisha kila wakati wanatafuta pesa za kusaidia kukarabati shule hiyo kutokana na miundombinu ya sasa si rafiki kwa wanafunzi.

"Maendeleo niliyopata mimi ni kutokana na kupata elimu katika shule ya Tosamaganga hivyo lazima tuikumbuke kwa kuendelea kuipatia msaada kadili tunavyoweza maana ukituangalia hapa unatuona wote tunavipato vizuri hivyo ni budi kukumbuka wapi tumetoka na tulikotoka kupoje tujia hivyo tutaithimini hii shule kila wakati kama tulivyofanya hivi sasa" alisema Mbilinyi

Mbilinyi aliwakata wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule kongwe kurudisha upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio chanzo cha mafanikio yao ya leo.

“Leo nimerudi katika shule hii ya Tosamaganga kuja kusaidia kutatua changamoto ambazo zipo katika shule hii ukizingatia kuwa shule hii inauchakavu wa majengo na miundombinu hivyo sisi  tumeanza kwa kujenga choo lakini changamoto bado zipo nyingi" alisema Mbilinyi
Mkuu wa shule ya sekondari Tosamaganga Iringa Damas Mgimwa akiwa na mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi wakati wa kukata utepe wa kufngua choo hicho
Mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi akiwa na mgeni rasmi wa hafla hiyo Robert Masunya ambaye ndio mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakikagua ubora wa vyumba vya vyoo hivyo
Hili ndio jengo jipya la choo kipya kilichojengwa na Tosamaganga Alumni Association kwa gharama ya shilingi millioni 30
Hawa ni baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefanikiwa kuijengea shule choo bora chenye thamani ya  zaidi ya shilingi milioni thelethini (30,000,000) kwa lengo la kurudisha  fadhila walizozipata wakiwa wanasoma hapo.

TIMU YA WAANDISHI WA HABARI ZA VIJIJINI WAFANYA ZIARA WILAYANI KILWA

$
0
0

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Zabron Bugingo,akielezea mradi mkubwa wa uoteshaji wa miche ya korosho kwa waandishi wa habari waliohitimu mafunzo ya uwandishi wa habari vijijini Mkoani Morogoro pindi walifanya ziara katika halmashauri hiyo jana.(Picha na Pamela Mollel).

Picha ikionesha miche ya korosho ikiwa katika hatua ya awali ya uoteshwaji.
Picha ikionesha jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohitimu mafunzo ya uwandishi wa habari za vijijini wakiwa katika boti kuelekea katika ziara ya kuona na kujifunza magofu ya kale kisiwani kilwa.

WANACHAMA 113 WAJITOKEZA KUWANIA UENYEKITI UVCCM

$
0
0
Wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.

Kwa sasa nafasi hiyo inashikiliwa na Mbunge wa Donge Visiwani Zanzibar, Sadifa Juma Khamis ambaye alichaguliwa katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2012.

Akizungumza leo Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamidu amesemma wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM linafanya usahili wagombea waliomba nafasi mbalimbali za uongozi.

Amesema usahili huo unafanyika kwa waliomba kugombea wa nafasi za mwenyekiti, makamu, wajumbe watano wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC), wajumbe watano wa baraza kuu la umoja huo Taifa na wajumbe wa kuwakilisha jumuiya hiyo katika jumuiya nyingine za chama.

Amesema zoezi hilo ambalo limeanza tangu Aprili limefanikisha kupatikana kwa viongozi mbalimbali wa ngazi za shina hadi wilaya na kwamba kinachofanyika hivi sasa ni mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi za kitaifa.“Vijana 113 wamejitokeza kuomba nafasi ya uenyekiti. Huu utakuwa ni uchaguzi wa kihistoria kati ya chaguzi zote zilizowahi kufanyika tangu mwaka 1978 ilipoanzishwa jumuiya hii mwaka huu. Kwa maneno mengine tumevunja rikodi,”amesema.

Amesema kwa upande wa nafasi ya umakamu mwenyekiti waliomba kugombea ni 23 wakati ujumbe wa Nec 118 wanachuana kugombea nafasi tano zilizopo kikatiba.Shaka amesema jumla ya wagombea ambao wanawafanyiwa usahili katika kikao cha Kamati ya Utekelezaji wa baraza la Kuu la UVCCM ni 375 huku nafasi ya uenyekiti Taifa ikiongoza kwa waombaji wengi katika zoezi hilo.
Viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

DKT MWANJELWA AISHAURI (IITA) KUONGEZA SPIDI UTOAJI ELIMU KWA WANANCHI KUKABILIANA NA SUMU KUVU

$
0
0
Na Mathias Canal, Geita

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.

Alisema kuwa elimu hiyo inatakiwa kutolewa katika maeneo mbalimbali nchini ili wananchi waweze kutambua namna bora katika uandaaji wa mashamba wakati wa msimu wa kilimo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mashamba hayashambuliwi na magugu wala wadudu waharibifu.

Naibu Waziri ametoa ushauri huo wakati akizungumza na Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi Eveline Massam mara baada ya kutembelea Banda hilo wakati wa Maonesho ya 36 ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita kuanzi Octoba 10 mpaka Octoba 16.

Dkt Mwanjelwa alisema kuwa wakulima wengi nchini wanalima pasina kufahamu taratibu za kilimo cha kisasa jambo ambalo linapelekea mazao yao kuathiriwa na wadudu husani Sumu Kuvu na kupelekea uduni wa mavuno.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kuhusu namna ya kuikabili Sumu Kuvu kutoka kwa Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi Eveline Massam wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akipokea zawadi ya Boga kutoka kwa Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mara baada ya kutembelea Banda la Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Afisa habari na Uelimishaji Jamii kutoka Mamkaka ya Chakula na Dawa Bi Robert Feruzi (Kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa jinsi Mamlaka hiyo inavyofanya kazi wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI KUWATOA SADAKA WATENDAJI WATAKAOZEMBEA UVAMIZI WA MIFUGO TOKA NCHI JIRANI YA KENYA - MPINA NA MWANDISHI MAALUM – KILIMANJARO

$
0
0
Serikali haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.

Hayo yamebainishwa wilayani Mwanga na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina alipozindua rasmi oparesheni maalum ya uvamizi na utambuzi wa mifugo hiyo tokea angani.

Mpina alisema kuwa uvamizi wa mifugo hiyo tokea nchi jirani ya Kenya unaleta changamoto kubwa ya malisho ya mifugo ya ndani ya nchi unaopelekea migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji na husababisha mmomonyoko wa udongo na uharibifu wa mazingira.

Baada ya kupokea taarifa ya timu ya wataalam iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Mifugo na Uvuvi Dkt Maria Mashingo, iliyofanya oparesheni hiyo maalum kwa kutumia ndege ya shirika la taifa la hifadhi ya wanyamapori, (TANAPA) taarifa iliyobaini kuwepo kwa makundi makubwa ya ng’ombe waliokuwa wakihama kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuwepo kwa idadi kubwa ya Maboma, Waziri Mpina alisema ,

“ Haiwezekani ng’ombe wanaingia kwa makundi makubwa hivi nchini na watendaji wa serikali wapo, lazima kutakuwa na shida katika utendaji, Oparesheni hii itakuwa ni ya mwisho, kwa ng’ombe watakaoingia tena watendaji watatolewa sadaka.” Alibainisha Mpina.

“Yawezekana ng’ombe wote 4000 ambao inasemekana walitoroshwa hapo awali wapo, hivyo Oparesheni ianze rasmi tuwakamate ng’ombe wote, tuheshimu sana sheria, na nchi jirani tushirikiane katika mambo tuliyokubaliana kisheria na lolote litakalotokea katika suala hili la uvamizi wa mifugo sheria itachukua mkondo wake na tusilaumiane” Alisisitiza Mpina.

Awali wataalam waliyokuwepo katika oparesheni hiyo maalum waliezeza kuwa mifugo mingi iliyoonekana kutokea angani ilikuwa zaidi katika maeneo ya malisho na maji ya vijiji vya kiti cha Mungu,njiapanda,kirya na kitongoi cha Mangulai.

Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilya ya Mwanga imeingia kazini tayari kwa kuanza oparesheni hiyo maalum. 
 Katika picha kikosi kazi maalum cha oparesheni ya angani ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika Wilaya ya Mwanga inayotokea katika nchi jirani ya Kenya , mbele ni rubani wa ndege hiyo maalum ya TANAPA Bw. Mark Athumani akiongoza ujumbe huo kupanda ndege katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kilimanjaro (KIA).

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiongea na kikosi kazi maalum kikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Maria Mashingo na Rubani wa ndege hiyo  maalum ya TANAPA Bw. Mark Athumani walipokuwa wakijiandaa kwenda kwenye oparesheni maalum ya angani ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika wilaya ya Mwanga wanaotokea katika Nchi jirani ya Kenya.
Waziri Mpina akimpungia mkono Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvivi Dkt Maria Mashingo akiwa na baadhi ya wajumbe wakiingia  kupanda ndege maalum kuanza oparesheni ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika Wilaya ya Mwanga wakitokea Kenya.

INTRODUCING HONGERA DKT MAGUFULI SONG

MAGAZETI YA JUMATATU LEO OCTOBER 16,2017

MELI YA KIFAHARI YA FLK AL SALAMAH YAONDOKA

$
0
0
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mh,Rashid Ali Juma kushoto akiwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wapili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed wapili kushoto na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt,Mohammed Bin Hamad Al Rumh watatu kushoto wakiangalia Ngoma za Utamaduni kabla ya kuondoka Zanzibar na kuelekea Dare es Salaam kwa Meli ya Kifahari ya Sultani Qabous wa Oman FULK AL SALAMAH.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mh,Rashid Ali Jumaakipeana mikono na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt,Mohammed Bin Hamad Al Rumh ikiwa ni ishara ya kuagana na kuondoka Zanzibar kuelekea Dare es Salaam kwa Meli ya Kifahari ya Sultani Qabous wa Oman FULK AL SALAMAH.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wapili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed akipeana mikono na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt,Mohammed Bin Hamad Al Rumh ikiwa ni ishara ya kuagana na kuondoka Zanzibar kuelekea Dare es Salaam kwa Meli ya Kifahari ya Sultani Qabous wa Oman FULK AL SALAMAH.
-Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wapili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Ziara ya Siku Nne alioifanya Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt,Mohammed Bin Hamad Al Rumh pamoja na ujumbe wake kabla ya kuondoka na kuelekea Dare es Salaam kwa Meli ya Kifahari ya Sultani Qabous wa Oman FULK AL SALAMAH.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mh,Rashid Ali Juma akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Ziara ya Siku Nne alioifanya Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt,Mohammed Bin Hamad Al Rumh pamoja na ujumbe wake kabla ya kuondoka na kuelekea Dare es Salaam kwa Meli ya Kifahari ya Sultani Qabous wa Oman FULK AL SALAMAH.
Balozi mdogo wa Oman katika jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaefanyia kazi zake Zanzibar Dkt, Mohammed Bin Hamad Al Rumh akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Ziara ya Siku Nne alioifanya Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt,Mohammed Bin Hamad Al Rumh pamoja na ujumbe wake kabla ya kuondoka na kuelekea Dare es Salaam kwa Meli ya Kifahari ya Sultani Qabous wa Oman FULK AL SALAMAH.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR

Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC yashika kasi

$
0
0
 Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Upendo Njogolo  (kushoto), akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo katika soko la Zakhem  Dar es Salaam, kuhusu kampeni inayoendelea ya akaunti za Malengo ya benki hiyo. Kampeni hiyo ya miezi mitatu itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ huku wengine 24 wakishinda pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.
 Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Evansia Kassuma (katikati), akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo katika soko la Zakhem, Mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana, kuhusu kampeni inayoendelea ya akaunti za Malengo ya benki hiyo. Kampeni hiyo ya miezi mitatu itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ huku wengine 24 wakishinda pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.
 Waendesha bodaboda wa eneo la Kimara, Dar es Salaam wakimsikiliza Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Upendo Njogolo  (kushoto), wakati akizungumza nao kuhusu kampeni inayoendelea ya akaunti za Malengo ya benki hiyo. Kampeni hiyo ya miezi mitatu itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ huku wengine 24 wakishinda pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja. 
Wachuuzi wa mboga mboga nao wakisikiliza kwa makini jinsi wanavyoweza kubadisha maisha yao kiuchumi mara watakapojiunga na akaunti aya Malengo ya NBC. Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC inafanyika nchini kote ambapo washindi sita wakijishindia kila mmoja gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ huku wengine 24 wakishinda pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.


DKT TIZEBA AFUKUZA KAZI WATATU, ATOA ONYO KWA WATATU

$
0
0
Na Mathias Canal, Geita

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kuwafukuza kazi maafisa watatu wa idara ya Maendeleo ya Mazao katika sehemu ya pembejeo ambao wamebainika kuhusika moja kwa moja na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa.

Akizungumza na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Lenny Mjini Geita Mhe Tizeba alisema kuwa kufukuzwa kazi kunajili kutokana na ukosefu wa umakini na usimamizi mzuri wa sheria ya ununuzi wa Umma ikiwemo kusababisha kuchapishwa kwa vocha za pembejeo zenye thamani ya Tshs 78,054,970,000 ambazo ni zaidi ya bajeti halisi iliyotengwa kwa ajili ya ruzuku ya pembejeo kwa kiasi cha Tshs 42,587,419,200

Watumishi waliofukuzwa kazi ni Bw Shenal S. Nyoni aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha pembejeo, Aliyekuwa Afisa kilimo Daraja la I Bw Michael G. Mayabu na Bw Franks F. Kamhabwa.

Waziri Tizeba ametumia mamlaka hayo mara baada ya kupitia taarifa ya waraka wa mkakati wa utekelezaji na Usimamizi wa utoaji wa Ruzuku za pembejeo za kilimo kwa wakulima kwa kutumia vocha wa mwaka 2015/2016 ambapo pamoja na mambo mengine uliainisha utaratibu wa usimamizi wa zoezi la utopaji wa ruzuku ambao ulilenga kuleta ufanisi katika utekelezaji wake.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (katikati) akisisitiza jambo Wakati wa Mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Lenny Mjini Geita, Mwingine ni Naibu Waziri wa wizara ya kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo Wakati wa Mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Lenny Mjini Geita
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (katikati) akisisitiza jambo Wakati wa Mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Lenny Mjini Geita, Mwingine ni Naibu Waziri wa wizara ya kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe.

PROF. MBARAWA AMCHARUKIA MKANDARASI WA SIA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa mkandarasi GM Construction anayejenga jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), kukamilisha ujenzi huo.

Amesema Serikali hairidhishwi na kasi ya ujenzi wa jengo hilo ambalo limetumia miaka minne badala ya miwili iliyokubalika katika mkataba wa awali hivyo kumtaka mkandarasi huyo kuhakikisha analikabidhi jengo hilo ifikapo Januari 30 mwakani.

“Kushindwa kukamilisha jengo hili ifikapo mwezi Januari mwakani itakuwa ndio tiketi yako ya mwisho ya kutopewa kazi kwasababu Serikali hii inafanya kazi kwa kuzingatia ubora na muda”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa kusimamia kikamilifu ujenzi huo ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa
Mhandisi Mshauri anayesimamia ujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), Eng. Nyamhanga Wanda, akitoa maelezo ya mradi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, (kushoto) , akikagua ujenzi wa jengo la abiria linalojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), Waziri huyo alifanya ziara ya ukaguzi na kuangalia maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi huo hadi sasa. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa.
Muonekano wa Jengo la abiria linalojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA). Jengo hilo limetakiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwezi Januari, 2018
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza na wananchi wa Tunduma wakati akikagua upanuzi wa njia nne ya barabara ya Tunduma-Sumbawanga KM 1.45, mkoani Mbeya.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Tunduma-Sumbawanga KM 1.45 inayojengwa kwa njia nne, mkoani Mbeya ili kupunguza msongamano wa magari jijini hapo.


DK.SHEIN AONANA NA BALOZI WA SAUDI ARABIA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Balozi wa Saudi Arabia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mohammed Mansour Al Malik,alipofika Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 16/10/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mohammed Mansour Al Malik, alipofika Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 16/10/2017.

WAZIRI MWIJAGE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA INDIA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb.) akizungumza na Balozi wa India nchini, Mhe. Sandeep Arya kuhusu kuimarisha ushirikiano kwenye masuala ya biashara, viwanda na uwekezaji kati ya Tanzania na India. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Oktoba, 2017. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.), Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Magabilo Murobi (hawapo pichani). 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.) (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima (wa pili kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Magabilo Murobi (wa kwanza kulia) wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Mwijage na Balozi wa India nchini (hawapo pichani). 
Mhe. Dkt. Kolimba akichangia jambo wakati wa mazungumzo kati ya Waziri Mwijage na Balozi Arya. 
Mazungumzo yakiendelea 

SHULE YA SEKONDARI BUYUNI CHANIKA YAONDOKANA NA UHABA WA MAJI

$
0
0
Na Agness Francis,Blog ya Jamii

Naibu mstahiki meya wa Manispaa ya Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto amezindua kisima cha maji katika mahafali ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Buyuni iliyopo Chanika katika Manispaa hiyo.

Katika mahafali hayo yaliofanyika katika Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam Naibu mstahiki meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amesema kuwa ametoa shukrani kwa Taasisi ya Time for Help ya Uturuki kwa ushirikiano wao wa kutoa msaada wa kisima cha maji ili kusaidia wanafunzi hao ambao kwa sasa wameondokana na tatizo la maji.

Nae Katibu wa Taasisi ya Time for Help ya Uturuki Ibrahimu Ibrahim ametoa shukrani za dhati kwa kupata ushirikiano na walimu katika kukamilisha zoezi hilo na pia amewataka wanafunzi hao kutunza vema kisima hicho ambacho kitawasaidia kutunza mazingira na kutatua matatizo mengine madogomadogo.

Vilevile pia Mwalimu mkuu Shule ya Sekondari Buyuni ,Bonifasi Mwalwego ametoa shukrani zake kwa Taasisi ya Time for Help ya Uturuki kwa ufadhili wa kuwaletea mkombozi wa kisima cha maji ambacho kwa sasa kimeanza kuwasaidia kwa matumizi mbalimbali.

Aidha Mwalimu Mwalwego amesema kuwa ikiwa toka shule hiyo ipate usajiri wake mwaka 2006 sasa ni mahafali nane kufanyika shuleni hapo na ametoa wito kwa wanafunzi kuzingatia elimu hasa kwa wasichana wanaohitimu wale wasikivu pamoja na kuwa na nidhamu pindi wanapokuwa majumbani na kutumia vema elimu waliyoipata.
Naibu mstahiki meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizindua kisima cha maji kilichofadhiliwa na Taasisi ya Time for Help ya Uturuki wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam.
Naibu mstahiki meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na wageni waalikwa na wafadhili Taasisi ya Time for Help ya Uturuki waliojitokeza kutoa msaada wa kisima cha maji wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam 
Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Buyuni, Bonifasi Mwalwego akizunguza na wageni waalikwa wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Taasisi ya Time for Help ya Uturuki, Ibrahimu Ibrahim akizungumza na wageni waalikwa akishukuru walimu kwa ushirikiano wao mapaka kukamilisha zoezi hilo la kisima wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam
Wanafunzi wa vidato mbalimbali wa shule hiyo wakitoa burudani ya kucheza nyimbo tofauti tofauti kwa wageni waalikwa kwaya wakati wa mahafali ya Shule ya Sekondari Buyuni kata ya Chanika Jijini Dar es Salaam.

Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha, Mussa Juma (wa pili kulia) akikabidhi kombe la ushindi wa kwanza kwa nahodha wa Taswa FC, Wilbert Molandi mara baada ya kutwaa ubingwa kwa mara ya 12 mfululizo. anayeshuhudia ni mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary.
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha, Mussa Juma (wa pili kulia) akikabidhi kombe la ushindi wa kwanza kwa nahodha wa Taswa Queens, Zuhura Abdinoor mara baada ya kutwaa ubingwa kwa mara ya tano mfululizo. Wanaoshuhudia ni mratibu wa Taswa Queens, Sia Mafuwe, na Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Taswa SC wakiwa katika picha ya pamoja.

Arusha. Timu ya mpira wa miguu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) nay a mpira wa pete (Taswa Queens) zimetwaa ubingwa wa tamasha la 13 la vyombo vya habari la Arusha (Arusha Media Bonaza) lililofanyika kwenye viwanja vya General Tyre.

Wakati Taswa FC ikitwaa nafasi ya kwanza kwa mpira wa miguu baada ya kujikusanyia pointi saba, Taswa Queens ilitwaa nafasi ya kwanza kwa upande wa netiboli baada ya kuifunga Taswa Arusha kwa mabao 19-7 katika mchezo wa kusisimua ulioshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa  Arusha, Mrisho Gambo.

Mbali ya kutwaa vikombe vya mpira wa miguu, timu hizo ambazo zinadhaminiwa na kampuni ya MultiChoice Tanzania (DSTV), benki ya TPB na Property International Limited, pia ilihakikisha vyombo vya ha ari vya Arusha vinaondoka  mikono mitupu baada ya kutwaa nafasi ya kwanza katika mbio za kufukuza kuku. Magret Elia ambaye ashinda kuku wawili na Veronica Deus aliyeshinda mara moja.

Taswa FC ilianza kampeni yake kutetea ubingwa wake kwa kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Radio Sun Rise. Timu hiyo ilisawazisha kupitia kwa Zahoro Mlanzi  baada ya gonga safi za  Wilbert Molandi, Ali Salum na Saidi Seif.
Taswa FC ilibadili upepo wa mashindano hayo baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Taswa Arusha baada ya Ibrahim “Maestro” Masoud kufunga kwa penati na Nicholas Ndifwa kufunga la pili baada ya ushirikiano mzuri wa Martin Shilla, Edward Mbaga, Kulwa Ndege na Muhidin Sufiani.

Mchezo wa kuamua nani bingwa ulikuwa kati ya Taswa SC dhidi ya Radio 5 ambapo Saidi Seif alifunga bao la ushindi kufuatia pasi ya Mohamed Akida aliyecheza vizuri na Majuto Omary.
Timu ya netiboli, Taswa Queens ilishinda mchezo wa fainali kwa mabao 19-7, mchezo ambao ulihudhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Taswa Arusha iliongoza dakika za mwanzoni mwa mchezo kabla ya Taswa Queens kubadili kibao na kuongoza kwa 10-5 mpaka mapumziko. Sharifa Mustafa, Veronica Deus na  Imani Makongoro walifunga kwa  Taswa Queens ambapo Zuhura Abduknoor, Magreth, Elia, Elizabeth Mbassa,  Amina Abdallah, Rukia Juma, Dosca Munthali alihakikisha Taswa Arusha ambayo ilikuwa chini ya  Rehema Mussa haifurukuti.

Kwa matokeo hayo, Taswa  SC zilitwaa kombe na fedha taslimu Sh 300,000. Mwenyekiti wa timu hiyo, Majuto Omary aliwapongeza wachezaji wake na wadhamini, Benki ya TPB, DSTV na Property International Limited kwa kufanikisha safari hiyo.

Katibu Mkuu wa Taswa Arusha, Mussa Juma alizipongeza timu zote kwa kushiriki katika bonanza hilo ambalo lilidhaminiwa na  Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mifuko ya hifadhi ya Jamii ya LAPF na PSPF, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,  Coca Cola, kampuni ya ya vinywaji baridi ya SBC (T) Limited na Palace Hoteli.

IBADA YA MISA YA KUMWOMBEA MPENDWA WETU JOSEPH NDYAMUKAMA BALTIMORE, MARYLAND

$
0
0
Zulia lililonakshiwa na picha ya marehemu Joseph Ndyamukama aliyefariki Sept 25, 2017 na siku ya Jumapili Oktoba 15, 2017 kufanyika Ibada ya misa ya kumwombea marehemu katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani. Picha na Vijimambo Blogna Kwanza Production.
Picha na kisanduku kilichowekwa majivu ya mpendwa wetu Joseph Ndyamukama kwenye ibada ya misa ya kumwombea marehemu iliyofanyika siku ya Jumapili Oktoba 15, 2017 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani.

 Padri Honest Munishi akiongoza ibada ya misa ya kumwombea marehemu Joseph Ndyamukama iliyofanyika siku ya Jumapili Oktoba 15, 2017 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani.
Orgence Matungwa ndugu ya marehemu akiwa na mkewe wakiwasha mishumaa muda mfupi kabla ya kuanza kwa ibada ya misa ya kumwombea marehemu Joseph Ndyamukama iliyofanyika siku ya Jumapili Oktoba 15, 2017 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani.
Padri Honest Munishi akiongoza ibada ya misa ya kumwombea marehemu Joseph Ndyamukama iliyofanyika siku ya Jumapili Oktoba 15, 2017 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images