Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1962 | 1963 | (Page 1964) | 1965 | 1966 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Oktoba 14 ametembelea Maonyesho ya Wiki ya Vijana yaliyoambatana na Uzimaji wa Mwenge, yaliyofanyika katika viwanja vya Aman, Zanzibar. 

  Katika kutembelea maonyesho hayo, Makamu wa Rais aliweza  kutembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na kujionea wananchi wa Zanzibar namna walivyojitokeza kwa wingi kupata Elimu kuhusiana na Bima ya Afya na kupatiwa huduma ya vipimo vya magonjwa yasiyo ambukizwa kama Shinikizo la Damu (BP), Uwiano wa Uzito na Urefu (BMI), Sukari sambamba na ushauri wa daktari. 

  Akizungumza alipokuwa katika banda hilo, Makamu wa Rais aliipongeza NHIF kwa kazi nzuri waliyoifanya, na kusisitiza zoezi kama hili la upimaji na utoaji Elimu lifanyike mara kwa mara haswa vijijini au sehemu zilizo pembezoni mwa nchi Bara na Visiwani kwani bado watu hawana uelewa juu ya Umuhimu wa kuwa na Kadi ya Bima ya Afya, na pia kua na desturi ya kucheki afya zao mara kwa mara.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Anjela Mziray amemueleza Makamu wa Rais, kuwa NHIF imejipanga kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na Bima ya Afya na sasa kuna Fao la Toto Afya Kadi ambapo kila mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18 atachangia 50,400 tu kwa muda wa mwaka mmoja na kwa mtototo mmoja. 

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zilizoshiriki Maonesho ya Wiki ya Vijana na Uzimaji wa Mwenge yaliyofanyika Kitaifa Zanzibar. Maonesho hayo yalianza rasmi tarehe 8/ 10 na hadi kufikia kilele tarehe 14/10/2017.

  NHIF imeshiriki Maonesho kwa kutoa Elimu, kufanya upimaji wa magonjwa yasiyoambukizwa na kusikiliza maoni ushauri au kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wadau wa Mfuko huo. Tangu kuanzia ufunguzi wa Maonesho hayo hadi kufikia kilele zaidi ya Wananchi 850 walitembelea banda la NHIF kwa ajili ya kupata Elimu na pia kucheki afya zao. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anjela Mziray alipokuwa akimuelezea juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na NHIF.
  mmoja wa madaktari walioshiriki maonesho hayo akimpima sukari mwananchi kwenye banda la NHIF.
  wananchi wa Zanzibar wakiwa wamejitokeza kwa wingi kupima afya zao siku ya kilele cha wiki ya vijana na uzimaji wa mwenge zilizofanyika katika viwanja vya amaan, Zanzibar.

  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa Shirika la Ugavi la Umeme (TANESCO), TANESCO Saccos Ltd, Somoe Nguhwe akiwasilisha ripoti ya mwaka ya saccos hiyo, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka, uliofanyika katika Ukumbi wa LAPF Kisenga jijini Dar es Salaam jana. PICHA ZOTE/JOHN BADI/DAILY MITIKASI BLOG 
  Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James akifungua mkutano huo.
  Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James akikabidhi Tuzo ya Mwanachama Bora wa Mwaka 2017 kwa Mwanachama Sabina Daati. 
  Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James akikabidhi Tuzo ya Mwanachama Bora wa Mwaka 2017kwa Mwanachama Renatus Mfilinge. 


  0 0

  Benny Mwaipaja, Dodoma

  MAKAMU wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, anayeshughulikia masuala ya nishati Bw. Amadou Hott amesema kuwa Tanzania iko katika njia sahihi kutaka iwe na asilimia 16 ya hisa kwenye miradi inayowekezwa katika sekta ya madini na mafuta ili rasilimali hizo ziweze kuwanufaisha wananchi na wawekezaji.

  Makamu huyo wa Rais ametoa kauli hiyo mjini Dodoma alipofanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kuhusu namna benki hiyo inavyoweza kusaidia kulikwamua Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) kutoka katika mzigo wa madeni unaolikabili ili liweze kujiendesha kibiashara bila kutegemea ruzuku kutoka Serikalini.

  Alisema kuwa nchi kadhaa duniani, zenyewe ama kwa kutumia kampuni ilizoziteua zina hisa ya kati ya asilimia 14 hadi 16 za hisa za bure katika miradi ya rasilimali za madini ili pande zote zinazohusika katika mikataba hiyo ziweze kunufaika na rasilimali za nchi.

  Alitolea mfano wa baadhi ya nchi ikiwemo Senegal ambazo zinatekeleza sera kama hizo na hakuna matatizo yoyote kati ya nchi hizo na wawekezaji na kwamba anaona nia njema ya Tanzania katika kulinda rasilimali zake.

  “Jambo la msingi linalotakiwa ni kuhakikisha kuwa makubaliano ya suala hili kati ya Serikali na Sekta binafsi yawe ya wazi, usawa na haki na ni muhimu wawekezaji wakakubaliana na utaratibu huo” aliongeza Bw. Hott.
  Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu kushoto) wakiwa katika mkutano na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo Bw. Amadou Hott, (wa tatu kulia), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati, Bw. Amadou Hott (kushoto) akisikiliza kwa makini wakati wa mkutano na Waziri wa fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) mkoani Dodoma, kulia ni Mkurugenzi wa benki hiyo anayeshughulika masuala ya maendeleo ya mifumo ya umeme, Bw. Henry Baldeh.
  Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakiwa katika mkutano na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) akichukua kumbukumbu wakati wa mkutano na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) (hawapo pichani) kulia ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bw. John Rubuga, mjini Dodoma.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dorothy Mwanyika (kulia), akichukua kumbukumbu wakati wa mkutano na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) (hawapo pichani) kushoto ni Kamishna wa Bajeti wa Wizara hiyo Bi. Marry Maganga akisikiliza kwa makini wakati mkutano ukiendelea katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt. Charles Tizeba amewataka wamiliki wa viwanda vya kuchambua pamba(ginners) kupeleka pamba mbegu kwenye kiwanda cha kuchakata(kutoa manyoya) mbegu za pamba cha Quton na akasema watakaogoma kupeleka hawatanunua pamba msimu ujao.

  Waziri Tizeba ameyasema hayo jana alipotembelea kiwanda hicho katika Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kwa lengo la kujionea hali ya uzalishaji wa mbegu ya pamba inavyoendelea.

  Amesema suala la wenye viwanda vya kuchambua pamba(ginners) kupeleka pamba mbegu katika kiwanda cha kuchakata mbegu za pamba(kuondoa manyoya) siyo la hiari na walishapewa maelekezo, hivyo wanapaswa kupeleka pamba mbegu katika kiwanda cha Quton ili zitolewe manyoya na baadaye zipelekwe kwa wananchi.

  “ Nimeambiwa watu wa Quton wanashindwa kufanya kazi kwa shift tatu kwa siku kwa sababu walio na mbegu kwenye viwanda vyao vya kuchambua pamba hawataki kuleta pamba hapa, wakati wanayo maelekezo na hii siyo hiari mbegu ikishatengwa na Bodi ya Pamba si yao” alisema Tizeba.

  “Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nakuagiza wapelekee ujumbe huu kwamba ginner atakayegoma kuleta pamba mbegu hapa Quton hanunui pamba mwaka kesho, wanapaswa walete mbegu zitolewe manyoya ziende kwa wananchi ili wapate mbegu bora, katika hili sitabembelezana na mtu” alisisitiza Tizeba.
  Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt.Charles Tizeba (wa tatu kushoto) akisikiliza maelezo kutoka wa Meneja Uzalishaji wa Mbegu,Pheneas Chikaura(kulia) katika Kiwanda cha Kuzalisha mbegu za pamba cha Quton wakati wa ziara yake kiwandani hapo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
  Waziri wa Kilimo, Mhe.Charles Tizeba akikaribishwa na Mkurugenzi wa Quton Tanzania Limited Ndg.Pradyumansinh Chauhan, alipotembea Kiwanda cha kuzalisha Mbegu za Pamba cha Quton kilichopo kata ya kasoli Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
  Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance Ginnery, Ndg. Boazi Ogola(wa pili kushoto) akimuongoza Waziri wa Kilimo, Dkt.Charles Tizeba (aliyeweka mkono kifuani) na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Bariadi na Mkoa wa Simiyu kuelekea kuona kiwanda hicho wakati wa ziara ya Waziri huyo Mkoani Simiyu.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Quton Tanzania Limited, Ndg.Pradyumansinh Chauhan akitoa taarifa ya uzalishaji wa mbegu za pamba zilizotolewa manyoya katika kiwanda cha kampuni hiyo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt.Charles Tizeba alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.


  0 0
  0 0

  Waziri wa Viwanda na Uwekezaji  Charles Mwijage akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wateja waliojitokeza katika uzinduzi wa duka la Danube Home jana  Mlimani City na kuwataka wamiliki wa duka hilo kutumia malighafi zinazopatikana nchini kwani zina ubora wa hali ya juu, Kulia ni Mkurugenzi wa GSM Ghari Said Mohamed na kushoto ni Mkurugenzi wa Danube Home Adel Sajan.
  Muonekano wa nje wa duka la Danube Home lililozinduliwa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Danube Home, Zarina Hassan akizungumza baada ya uzinduzi wa duka la Danube Home na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kwenye duka la lao kwa ajili ya kujipatia bidhaa zenye ubora na thamani nafuu.
   Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage akipata  maelekezo wakati alipotembelea maeneo mbalimbali ndani ya duka la Danube HomeMlimani City jijini Dar es Salaam.
   Baadhi wa wateja waliojitokeza katika ufunguzi wa duka la Danube Home wakiwa wanaangalia baadhi ya bidhaa zinazopatikana kwenye duka hilo jana Jijini Dar es salaam.

   WAZIRI wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage amewataka kampuni ya Danube Home na GSM kuendelea kuwekeza nchini kwani wanaposema uchumi wa viwanja ni pamoja na biashara za samani kama wanazojishughulisha nazo.

  Mwijage ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa duka la Danube Home uliofanyika jana Mlimani City pamoja na kutambulishwa kwa balozi wa Danube nchini Tanzania Zarina Hassan.

  Akizungumza baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya duka hilo, Mwijage amesema kuwa anatarajia kuona Danube wanatumia malighafi zinazopatikana nchini kwa ajili ya kutengenezea samani mbalimbali za ndani ikiwemo masofa, vitanda na zinginezo kwani zinapatikana kwa urahisi.

  "Natarajia kuona mnatumia samani zinazopatikana nchini, pia nimesikia hapa mkisema katika maandalizi ya kufungua duka hili mmewatumia zaidi watanzania na hicho ni kitu kizuri na ninaamini mtaendelea kuwaamini watanzania",amesema Mwijage.

  Mkurugenzi wa Danube Home Adel Sajan amewashukuru watanzania kwa ukarimu mkubwa waliokuwa nao na zaidi Tanzania ni eneo salama kwa ajili ya kufanya biashara kwani kwa kushirikiana na kampuni ya GSM wameweza kufungua duka la tatu.

  Kampuni ya GSM na Danube Home zimeweza kutoa ajira zaidi ya 1000 kwa nchini huku aslimia 99 wakiwa ni watanzania.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk. Joel Bendera akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mkutano wa 10 wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) wa Mkoa huo, katika ufungizi wake uliofanyika mjini Babati wenye kauli mbiu ya uhakika wa mbegu kwa uhakika wa chakula
   Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk. Joel Bendera akizungumzia wakati akifungua mkutano wa 10 wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) wa Mkoa huo, uliofanyika mjini Babati wenye kauli mbiu ya uhakika wa mbegu kwa uhakika wa chakula
  Baadhi ya Washiriki wa mkutano wa 10 wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) wa Mkoa wa Manyara wakimsikiliza Mgeni rasmi.
    Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk. Joel Bendera akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano wa 10 wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) wa Mkoa huo.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola akiongea na washiriki wa mradi wa Uchumi wa Kijani ndani ya Hifadhi ya Hai (GEBR) wakati akifungua mkutano wa majadiliano wa kufunga mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya Ushirikiano wa Kimataifa (KOICA) chini ya Programu ya UNESCO iliyofanyika mjini Tanga. Lengo la mradi huo ilikuwa ni kupunguza umaskini, kuhifadhi bionuwai na maendeleo endelevu katika nchi za kushini mwa Jangwa la Sahara - Usambara ya Mashariki, Tanzania. Picha zote na KAJUNASON/MMG-TANGA.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi ambaye alimwakilisha mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella akifungua rasmi na kumkaribisha mkutano wa majadiliano wa kufunga mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya Ushirikiano wa Kimataifa (KOICA) chini ya Programu ya UNESCO.
  Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe akizungumza wakati akifungua mkutano wa majadiliano wa kufunga mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya Ushirikiano wa Kimataifa (KOICA) chini ya Programu ya UNESCO iliyofanyika mjini Tanga. Meza kuu...


  0 0

   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa pili kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Bidhaa na Wateja Rejareja wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo alipokwenda kuzindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana ambayo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini ambapo ilizindua akaunti maalumu ya kikundi iitwayo ‘NBC Kikundi Account’ ili kuwawezesha watanzania kiuchumi. Akaunti inafunguliwa na  watu kuanzia watano na kuendelea. Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC), Beng`i Mazana Issa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Japhet Justine, Mkurugenzi wa Mifuko ya Uwezeshaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC), Edwin Christant na Mkurugenzi wa Uwezeshaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC), Anna Dominick. 
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia), akimsikiliza Meneja Bidhaa za Uwekezaji wa NBC, Dorothea Mabonye (wa pili kushoto), huku wenzake wakiangalia wakati akitembelea banda la NBC katika maadhimisho hayo.
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia), akisalimiana na Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Witness Leverian alipokwenda kuzindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana. NBC ilikuwa ni kati ya wadhamini wa maadhimisho hayo ambapo imezindua akaunti maalumu ya kikundi iitwayo ‘NBC Kikundi Account’ ili kuwawezesha watanzania kiuchumi katika kikundi cha watu kuanzia watano na kuendelea.  
   Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Witness Leverian (kulia), akitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo kwa baadhi ya washiriki wa maonyesho ya maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.
   Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Rosina Simbila (kushoto), akitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo kwa baadhi ya washiriki wa maonyesho ya maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.
  Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Stephen Ngereza (kulia), akitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo kwa baadhi ya washiriki wa maonyesho ya maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana. 

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakitembea kwenye mitaa ya Stone Town mjini Zanzibar wakielekea katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili kwa ajili ya ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakipokewa na Askofu Augustine Shayo walipowasili  katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili kwa ajili ya ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili kwa wakishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili kwa wakishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Augustine Shayo katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili ambako alishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017.
   Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Janeth Magufuli akiombewa na Askofu Augustine Shayo katika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili ambako alishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na Askofu Augustine Shayo na watawa vkatika kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Minara Miwili ambako alishiriki ibada ya Jumapili leo Oktoba 15, 2017.


  0 0

  NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka wakulima na wafugaji wa vijiji vinne alivyotembelea vya wilaya ya Mkuranga kuondokana na tofauti zao na badala yake wapendane.

  Hayo aliyasema katika ziara yake kwa wananchi wa jimbo lake la Mkuranga-Pwani ambapo aliweza kuelezwa kero mbalimbali na kuahidi kuzishughulikia.

  Katika ziara hiyo pia aliweza kuchangia jumla ya fedha kiasi cha shilingi Mil.6 pamoja na mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati zilizomo katika vijiji hivyo.

  Aidha pia amewaomba wananchi kuunda vikundi mbalimbali vya ujasiriamali hususani ufugaji wa kuku samaki na mifungo mbalimbali ili kuwawezesha kuondokana na umaskini.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega ambaye ni Mbunge wa Mkuranga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyanduturu akiwa ni ziara yake ya kwanza tokea kuteuliwa kwake kuwa Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia ujenzi wa jengo la zahanati ya kijiji cha Nyanduturu kata ya Nyamato ambayo pia amechangia Millioni moja na nusu pamoja na saruji 50 ili kufanikisha ujenzi huo unaoendelea.
  Mwenyekiti wa kijiji cha Mvuleni,Mohammed Mpunjika akimkabidhi risala yao Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega alipofanya ziara yake ya kwanza tokea kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
  Mmoja wa akina mama kutoka katika kijiji cha Tipo kata ya Nyamato akiuliza swali kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wakati alipofanya ziara yake .
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga,Ally Mohammed akizungumza jambo.
  Muonekano wa jengo hilo.  0 0

  Na Jumia Travel 

  TAKRIBANI wadau 150 wa sekta ya utalii wa ndani na nje ya Tanzania wameshiriki kwenye Maonyesho ya tatu ya Kimataifa ya Utalii (SITE – Swahili International Tourism Expo) yaliyofanyika kuanzia Oktoba 13 mpaka 15 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Maonyesho hayo ambayo yameandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) yamefanyika kwa mara ya tatu tangu kuanzishwa kwake kwa mara ya kwanza mwaka 2014 ambapo idadi ya washiriki imeonekana kuongezeka kwa kiasi kikubwa na kuvutia mataifa zaidi ya 13 kama vile Tanzania Bara, Zanzibar, Kenya, Uganda, Rwanda, Malawi, Mauritius na Shelisheli.

  Maonyesho hayo yalifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa akiwemo waziri mpya kwenye sekta ya utalii na maliasili nchini, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangala.
  Katika hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho hayo Makamu wa Rais alibainisha kwamba sekta ya utalii nchini imekuwa na mchango mkubwa kwenye pato la taifa kwani inachangia jumla ya asilimia 17 na hivyo kuifanya mojawapo ya sekta muhimu katika kukuza uchumi wa nchi. Mbali na hapo sekta hiyo inatarajia kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka milioni 1.2 mpaka kufikia milioni 2 kufikia mwaka 2020.

  Akitoa ushuhuda wake baada ya kutembelea Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro siku chache zilizopita, ambapo kihistoria sehemu hiyo ndimo yanapatikana mabaki ya binadamu wa kwanza kuwahi kuishi duniani, alisema kuwa Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vya kitalii vya kila aina ambavyo ni nadra kupatikana sehemu zingine duniani. Kuwepo kwa vivutio vingi kumepelekea kutajwa na taasisi, mitandao na majarida mbalimbali duniani ikiwemo mtandao wa SafariBookings ambao umeitaja Tanzania kuwa ni kinara kwa kutembelewa zaidi na watalii barani Afrika.
  Kwa upande wake akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala alibainisha kuwa ili sekta hiyo iendelee kukuwa na kufikia malengo iliyojiwekea ni lazima kufanyiwa marekebisho, yakiwemo kufungiwa mfumo wa kieletroniki utakaofanikisha uongezaji kasi ya mapato huku akiwatoa hofu watalii juu ya upatikanaji wa vibali vya viza ambapo amesema vitakuwa vikitolewa kwa muda wa nusu saa.

  “Kuna changamoto kidogo ya upatikanaji wa viza kwa watalii wanaowasili hususani muda wanaochukua pale wanapofika uwanja wa ndege kusubiria mpaka kuipata. Na hili ni eneo ambalo tunakusudia kuwekeza zaidi na kupitia huu mfumo jumuishi wa mtandao wa mawasiliano wa serikali tutaweza kupunguza muda wa kusubiria kupata viza mara watalii wanapowasili uwanja wa ndege,” alisema na kuhitimisha Waziri huyo mpya wa Maliasili na Utalii, “Na ni eneo ambalo kwa kweli ili kufanikiwa tunakusudia kushirikiana na wenzetu wa Wizara ya Mambo ya Ndani kufanya maboresho.”
  Jumia Travel ni miongoni mwa wadau wa sekta ya utalii walioshiriki kwenye maonyesho hayo ya kimataifa ya utalii kwa mara ya kwanza ambayo kwa kiasi kikubwa huwakutanisha washiriki wa ndani na kimataifa pamoja.


  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwakaribisha vijana sita waliokimbiza Mwenge wa Uhuru kupata naye chakula cha mchana Ikulu Zanzibar leo Oktoba 15, 2017. Pamoja nao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenister Mhagama
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwakaribisha vijana sita waliokimbiza Mwenge wa Uhuru kupata naye chakula cha mchana Ikulu Zanzibar leo Oktoba 15, 2017. Pamoja nao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenister Mhagama
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwakaribisha vijana sita waliokimbiza Mwenge wa Uhuru kupata naye chakula cha mchana Ikulu Zanzibar leo Oktoba 15, 2017. Pamoja nao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenister Mhagama.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipakua chakula na mmoja wa vijana sita waliokimbiza Mwenge wa Uhuru aliowaalika kupata naye chakula cha mchana Ikulu Zanzibar leo Oktoba 15, 2017.
   Picha ya pamoja.

  PICHA NA IKULU


  0 0

  Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Kiroboto, maarufu Juma Nature, akisababisha jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere
  Mwanamuziki wa muziki Isha Mashauzi akipagawisha mashabiki, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kweneye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere
  Mwanamuziki wa muziki wa Singeli Dula Makabila akiwa jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
  Vijana wa kundi la Mkubwa na Wanawe wakishambulia jukwani.
  Wananchi waliohudhuria tamasha hilo la 'Gusa maisha yao' wakifurahi kuonyesha kuguswa na tamasha hilo ambalo lilikuwa mahsusi kumueenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere. 


  0 0

  Rais Dkt John Pombe Magufuli akiagana na viongozi wa Mkoa wa Mjini Magharibi mapema leo kabla ya kurejea jijini Dar

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma DKT BILINITH MAHENGE amelishukuru shirika la COPE lililochini ya wataliano linalo toa elimu ya mifugo na kilimo katika chuo cha mahinya katika wilaya ya namtumbo mkoani Ruvuma,

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Kilimanjaro na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira pamoja na Viongozi wengine wa Chama na Serikali.

  Makamu wa Rais anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Kilimanjaro kesho Oktoba 16, 2017.

  Kauli mbiu ya mwaka huu ni ” Zuia Ajali-Tii Sheria Okoa Maisha”

  Ufunguzi huo utafanyika katika Uwanja wa Mashujaa uliopo katika Manispaa ya mji wa Moshi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA ambapo anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA ambapo anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

  0 0


  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (R) Semistocles Kaijage amewataka wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa madiwani kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi ili kuepuka kuisababishia serikali hasara.

  Jaji Kaijage ameyasema hayo leo (Tarehe 15.10.2017) mjini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi.“…Tusipozingatia na kufuata taratibu za uchaguzi tunaweza kusababisha kesi nyingi za uchaguzi na kuitumbukiza nchi katika gharama ambazo zingeweza kutumika katika huduma za jamii,” ameonya Jaji Kaijage.

  Mhe. Kaijage amesema kuwa hamasa katika siasa za Tanzania imeongezeka sana na kwamba kumekua na ongezeko la hali ya kutokuaminiana haswa katika mchakato wa uchaguzi na kwamba endapo wasimamizi hawatafanya kazi yao kwa ufasaha wataitumbukiza nchi kwenye matatizo makubwa.

  “Mmeaminiwa na kuteuliwa kwa sababu mna uwezo wa kufanya kazi hii, kitu cha muhimu ni kujiamini na kujitambua. Pia kuhakikisha mnayajua vyema maeneo yenu mnayofanyia kazi, kuhakikisha mnawatumia vizuri wasaidizi mlio nao kwa matokeo bora,” alisema.


  0 0


  -Kaimu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga Leo  amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya ligi kwa kupata kura 10 huku mpinzani wake Hamad Yahaya akipata Kura 6.

   Hamadi ndio alikuwa mwenyekiti wa bodi ya ligi kwa kipindi cha miaka 4.

  Wapiga kura ni klabu 16 zinazoshiriki  ligi kuu Tanzania Bara.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza katika hafla ya Waongoza watalii bora kwa mwaka 2017 iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wengine ni waandaji wa tuzo hiyo. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki ( wa nane kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waongoza watalii bora kwa mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wengine ni waandaji wa tuzo hiyo. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
  Mkurugenzi wa Masoko wa Hifadhi ya Taifa ya Tanzania,Ibrahim Musa akikamkabidhi cheti mmoja wa washindi katika katika hafla ya utoaji tuzo kwa waongoza watalii iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa tano kushoto) akiwa Wakurugenzi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii katika hafla ya Waongoza watalii bora kwa mwaka 2017 iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)

older | 1 | .... | 1962 | 1963 | (Page 1964) | 1965 | 1966 | .... | 3272 | newer