Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1961 | 1962 | (Page 1963) | 1964 | 1965 | .... | 3348 | newer

  0 0  0 0

   Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati) akitoa maelekezo kwa Meneja mradi (TANROADS) Anold Maeda (wa tatu kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mradi wa barabara ya juu katika makutano ya barabara ya TAZARA jana jijini Dar es Salaam. 

   Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (Katikati) akitoa maelekezo kwa Meneja mradi (TANROADS) Anold Maeda (wa tatu kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya juu unaondelea katika makutano ya barabara ya TAZARA jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhandisi Mkazi kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Kiyokazu Tsuji. 
   Baadhi ya mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa mradi wa barabara ya juu (Fly Over) jana jijini Dar es Salaam.

  Meneja mradi (TANROADS) Anold Maeda (kulia) akitoa maelezo kwa  Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati) kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Fly Over) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mradi huo jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhandisi Mkazi kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Kiyokazu Tsuji.  


   Picha Na Eliphace Marwa - Maelezo


  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Isack Kamwelwe amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Kisarawe, mkoa wa Pwani kufuatilia maendeleo ya Sekta ya Maji katika wilaya hiyo.

  Dhumuni la ziara hiyo ilikua ni kukagua utekelezaji ya miradi ya maji inayotekelezwa na serikali katika wilaya hiyo, yenye changamoto kubwa ya huduma ya maji licha ya kuwa ni moja ya miji ya muda mrefu na historia kubwa nchini.

  “Nimetembelea wilaya kadhaa za mkoa Pwani zikiwemo Rufiji, Mkuranga na Kibiti, lakini hapa Kisarawe kuna changamoto kubwa. Inabidi tufanye kazi ya ziada ili kuinua kiwango cha huduma ya maji ambacho ni asilimia 46, naagiza viongozi wa wilaya mje ofisini kwangu Dodoma tuweke mikakati ya kuinua hali ya maji Kisarawe”, alisema Inj. Kamwelwe.

  Inj. Kamwelwe alisema kuwa anamshukuru Mhe. Rais kwa kuagiza DAWASA waje Kisarawe, kwa kuwa watasaidia kuinua kiwango cha huduma ya maji kwa wakazi wa Kisarawe. DAWASA watatoa maji Ruvu Juu na baada ya miezi 15 maji yatakuwa yamefika Kisarawe. 

  Aidha, Waziri wa Maji na Umwagiliaji alitembelea miradi ya maji ya Mengwa, Kikwete na bwawa la maji la Chole Semvula lilioanza utekelezaji wake mwaka 2013 ambalo utekelezaji wake ulikuwa umesimama kwa changamoto mbalimbali, na kusema kuwa ni bwawa zuri, lililo katika mazingira mazuri na lina maji na kuagiza kuanza utekelezaji wake mara moja. 
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Inj. Romanus Mwag’ingo akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji inayotegemewa kutekelezwa na DAWASA katika Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Isack Kamwelwe akitoa maagizo kwa viongozi na watendaji wa Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji. 
  1. Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Isack Kamwelwe akiwa mbele ya Bwawa la Maji la Chole Semvula alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji katika Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Isack Kamwelwe akiwa kwenye mradi wa maji wa Mengwa pamoja na viongozi na watendaji wa Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji.

  0 0

  Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu baada ya matembezi ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere yaliyoanzia Ikulu mpaka katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo ikiwa pia ni siku ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu wakimsikiliza Katibu Mkuu Alphayo Kidata baada ya matembezi ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere yaliyoanzia Ikulu mpaka katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo ikiwa pia ni siku ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru.
  Mazoezi ya viungo yakiendelea.

  0 0

  Kiongozi wa Ujumbe wa Madaktari bingwa kutoka Jumuiya ya Kiislamu Duniani (WAMY) Dk,Sultan akizungumza machache kuhusiana na matibabu watakayoyaendesha wakati walipokutana nakufanya mazungumzo katika Hoteli ya Mizingani Forodhani mjini Unguja.madaktari hao watakuwepo kisiwani Pemba kutoa matibabu mbalimbali ikiwemo matatizo ya akina mama na mifupa kwa siku 10.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Jumuiya ya Kiislamu Duniani(WAMY)kuhusiana na matibabu watakayoyaendeshaKisiwani Pemba mazungumzo yaliofanyika katika Hoteli ya Mizingani Forodhani mjini Unguja.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akipokea Zawadi ya Sahani baada ya kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Jumuiya ya Kiislamu Duniani(WAMY) kuhusiana na matibabu watakayoyaendesha Kisiwani Pemba mazungumzo yaliofanyika katika Hoteli ya Mizingani Forodhani mjini Unguja.

  PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANIZBAR.

  0 0

  Mapema leo Ijumaa Oktoba 13,washiriki hao wa shindano hilo la mrembo wa mkoa wa Shinyanga linalotarajiwa kufanyika Oktoba 15 mwaka huu,walimwagilia maji miti mbalimbali iliyopandwa mjini Shinyanga.

  Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Mwandaaji wa shindano la Miss Shinyanga mwaka 2017,Grace Shija alisema pamoja na kufanya maandalizi ya shindano hilo pia wanashiriki katika shughuli za kijamii. 

  “Sisi kama sehemu ya jamii tumeamua kushiriki katika kampeni ya upandaji miti kwa kumwagilia maji miti iliyopandwa katika maeneo mbalimbali mjini Shinyanga kwa kujaza maji kwenye chupa zilizowekwa kutiririsha matone ya maji kwenye miti hiyo”,alieleza Shija. 

  Akizungumzia kuhusu shindano la Miss Shinyanga mwaka huu alisema jumla ya warembo 12 kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga watachuana siku ya Jumapili Oktoba 15,2017 katika ukumbi wa NSSF ya Zamani mjini Shinyanga kuanzia saa mbili usiku ili kupata mrembo wa mkoa mwaka huu. 


  Washiriki wa shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga “Miss Shinyanga 2017”,wameunga mkono kampeni ya upandaji miti iliyoanzishwa katika wilaya ya Shinyanga na Mkuu wa wilaya hiyo Josephine Matiro hivi karibuni ili kupambana na hali ya ukame/jangwa mkoani humo. 

  Washiriki wa shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga “Miss Shinyanga 2017” wakiwa wamebeba madumu ya maji kwa ajili ya kuweka kwenye miti ambayo inamwagiliwa maji kwa njia ya makopo ya maji yaliyotobolewa kwa ajili ya kutoa matone kidogo kidogo 
  Zoezi la kumwagilia maji miti likiendelea 
  Warembo wakielekea katika eneo jingine kwa ajili ya kumwagili maji miti iliyopandwa hivi karibuni 

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva (wa katikati) akiwa sambamba na watumishi wa serikali wa manispaa hiyo na vikundi vya mazoezi ya Jogging katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Hayati Mwalim Julius Nyerere leo uwanja wa Taifa  Jijini  Dar es salaam.

  Katika kuadhimisha siku ya kumbumbuku ya hayati Baba wa Taifa Mwl; Julius Kambarage Nyerere, Wilaya ya Temeke yafanya michezo mbalimbali ambayo ilijumuisha watumishi wote wa Wilaya hiyo na vilabu vyote vya michezo vya Mkoa wa Dar.

  Mgeni rasmi wa tamasha hilo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva alifurahishwa na kazi nzuri ya maandalizi ya Tamasha hilo, jinsi watumishi na vilabu vya michezo walivyojitokeza kwa wingi katika kuadhimisha siku hiyo ya kifo cha baba wa taifa.

  Lyaniva alisisitiza kuyaishi maisha ya Mwl Nyerere  kwa kuwa wazalendo wa taifa letu na kuikataa rushwa ambayo ni adui wa maendeleo na adui wa haki. 

  Alisema "Mwalimu Nyerere alikua mpenzi wa michezo ndio maana leo tunamuenzi". Mwl Nyerere ndiye alikua muanzilishi wa michezo mbalimbali. 

  Alisisitiza katika vilabu vyote vya michezo kuwa na shughuli mbalimbali za kijasiliamali ili kujikwamua kiuchumi.

  Alisema hayo alipowakumbusha wanamichezo kuwa pamoja na kwamba michezo ni afya lakini pia ikitumiwa vizuri itakuinua kiuchumi.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva na watumishi wa serikali wa manispaa hiyo pamoja na vikundi vya mazoezi wakifanya mazoezi ya pamoja.
  Wakishiriki michezo mbalimbali ikiwemo kukimbia ndani ya magunia.
  Watumishi wa manispaa ya Temeke wakifurahi kwa pamoja.

  0 0

  Aliyesimama ni mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Paul Chaote akifunga mafunzo kwa wandishi wa habari mwishoni mwa wiki Mkoa wa kigoma (hawapo Pichani) juu ya kuelimisha wananchi umuhimu wa huduma endelevu ya Afya ya mama na mtoto kigoma kwa lengo la kupunguza Vifo vitokanavyo na uzazi ambapo kwa mwaka 2016 wanawake wajawazito 96 Kati ya vizazi 
  Katibu wa Chama Cha Wandishi wa Habari Kigoma Fadhili Abdallah leo kigoma Ujiji Akitoa shukrani kwa wadau wa Afya ( Bloomberg Philanthropies,Thamini uhai na Ingender Health) kwa kuwajengea awesome Wandishi wa humo juu ya uandishi wa habari za afya .Picha na Magnets Magosso Kigoma Ujiji.

  0 0

   Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile aliyesimama akiongea na watumishi wa Taasisi ya Taifa ya Uchunguzi wa Dawa (NIMR) hawapo pichani wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam.

   Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC)  Dkt. Joyceline Kaganda kulia wakati alipotembelea ofisi hizo leo jijini Dar es salaam.

   Watumishi wa Taasisi  ya Taifa ya Uchunguzi wa Dawa (NIMR) waliokaa wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile aliyesimama mbele wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam.

   Baadhi ya watendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile hayupo pichani wakati alipotembelea ofisi hizo leo jijini Dar es salaam.

  Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Taasisi  ya Taifa ya Uchunguzi wa Dawa (NIMR) wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam,  , wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NIMR Dkt. Yunus Mgaya.  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba Watanzania waendelee kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kuiga maisha yake na utendaji wake.

  Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Oktoba 14, 2017) aliposhiriki ibada maalumu ya kumuombea Mwl. Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Minara Miwili Zanzibar.

  Ibada hiyo ya kumbukumbu ya miaka 18 ya kifo cha Mwl. Nyerere ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru uliozimwa leo katika mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar.

  Katika Idaba hiyo Waziri Mkuu amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanamuenzi Mwl. Nyerere kwa kuendeleza mambo mema yote aliyoyafanya enzi za uhai wake.Awali, Katibu wa Jimbo Katoliki Zanzibar Padri Cosmas Shayo ambaye aliongoza ibada hiyo aliwaomba waamini wamuenzi Mwl. Nyerere kwa kudumisha umoja na mshikamano wa Taifa.

  “Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere aliwapenda watu wote bila kujali Imani zao wala itikadi zao. Alikuwa mzalendo na alitaka Watanzania waishi maisha bora.”

  Padri Shayo aliongeza kuwa tunu za amani na umoja zilikuwa miongoni mwa falsafa kuu ya Mwl. Nyerere, ambapo matokeo yake ni umoja na mshikamano wa Taifa uliopo.

  Ibada hiyo ilihudhuriwa na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Idd, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi Jenista Mhagama, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa.

  Wengine ni Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Bi. Mauldine Castico, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira Bw. Anthony Mavunde, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Walemavu Bi. Stella Alex Ikupa na mwakilishi wa familia ya Mwl. Bw. Makongoro Nyerere.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  JUMAMOSI, OKTOBA 14, 2017.         

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye ibada maalum ya kumuombea Mwalimu Julius Nyerere, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Minara Miwili Zanzibar (katikati) ni Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) ni Mke wa Waziri Mkuu mama Marry Majaliwa. Oktoba 14, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waumini waliyo hudhuria kwenye ibada maalum ya kumuombea Mwalimu Julius Nyerere, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Minara Miwili Zanzibar, Oktoba 14, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)     

  0 0
 • 10/14/17--07:40: BAMIZA TOP 20 ZA MAGIC FM • 0 0
 • 10/14/17--07:45: Article 5


 • 0 0


  Na Woinde Shizza,Arusha

  Tamasha la waandishi wa habari, kanda ya kaskazini, linatarajiwa kufanyika jumapili, octobar 15 katika uwanja wa General Tyre ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

  Katika tamasha hilo, ambalo litashirikisha wanahabari zaidi ya 500, kutoka mikoa ya Arusha, Tanga, Manyara na Kilimanjaro,limedhaminiwa na shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) Mifuko ya hifadhi ya Jamii ya LAPF na PSPF, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, kampuni ya vinywaji baridi ya Coca cola na kampuni ya ya vinywaji baridi ya SBC (T) Limited na Palace Hoteli.

  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma, alisema tamasha hilo, limeandaliwa na TASWA kwa kushirikiana na kampuni ya Arusha media na maandalizi yote yamekamilika.

  Juma alisema katika tamasha hilo, bingwa atazawadiwa kikombe na fedha taslimu jumla ya shilingi 500,000, mshindi wa pili fedha taslimu 100,000 na kwa upande wea mpira wa pete mshindi ni kikombe na fedha taslimu jumlaya sh 300,000 na mshindi wa pili sh 50,000.

  Alisema pia kutakuwa na michezo ya mbio za magunia, kuvuta kamba, mbio za vijiko, riadha na masumbwi ambapo tayari waambuzi wanaotambuliwa na mashirika mbali mbali ya michezo watakuwepo.

  Hata hivyo, alisema wadhamini wengine wa tamasha hilo wanatarajiwa kutangazwa, ili kuhakikisha wanahabari wanaburudika ambapo pia kuwa kuwa na benki maalum ambayo itatumnbuiza siku za tamasha.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa TASWA Arusha, Jamila Omar alitoa wito kwa wanahabari wote na familia zao kujitokeza katika tamasha hili ambalo hufanyika kila mwaka mkoani Arusha.

  Alisema kauli mbio ya tamasha hilo, ambalo linaendama na maadhimisho ya kumbukumbu ya mwalimu nyerere ni michezo ni ajira, michezo ni kazi tufanye kazi kwa bidii kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda.

  Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole alizitaja timu ambazo zitashiriki kuwa ni TASWA Dar es Salaam, Triple A,RadioSunrise , chuo cha uandishi habari cha Arusha(AJTC)timu ya Arusha One Fm, TASWA Arusha,Radio ORS ya Manyara ,NSSF na timu ya Wazee Klabu.
  wakwanza kulia ni Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma katikati ni Mwenyekiti wa TASWA Arusha, Jamila Omar akiongea na waandishi wa habari


  0 0

  Na: Thobias Robert.

  Katika kutimiza ndoto ya Tanzania ya uchumi wa kati unaotegemea uzalishaji viwandani, wadau mbalimbali wa maendeleo wamezidi kujitokeza na kutoa mawazo yatakayosaidia kukuza sekta za kiuchumi ili kutimiza ndoto hiyo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

  Akizungumza katika Dkt. Samson Kibona, kutoka Antipa Herbal Clinic amesema kuwa uchumi wa viwanda utaokoa kilimo cha Tanzania na kupandishwa thamani ya mazao yalimwayo hapa nchini na kuongeza kipato kwa wakulima wadogo, wa kati na wakubwa.

  Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa lengo la kuelezea mbinu za kilimo cha kisasa, kutoa ombi kwa serikali juu ya kusimamia kilimo hicho chenye tija na kitakachopunguza uagizwaji wa bidhaa zitokanazo na kilimo kutoka nje ya nchi.

  “Tanzania ya viwanda itaokoa sekta ya kilimo, kupandisha thamani ya mazao na kufanya mazao yanayolimwa nchini kutosafirishwa nje badala yake bidhaa zitokanazo na mazao hayo kama vile mafuta ya kupikia, vyakula vya kawaida, kama biskuti, nafaka halisi ya unga ndizo zitasafirishwa au kuuzwa nje na kuongeza fedha za kigeni,” alieleza Dkt. Kibona.
  Mtaalam wa Kilimo cha Kisasa na Tabibu wa Dawa za Asili Dkt. Samson Kibano akizungumza na Waandsishi wa Habari kuhusu mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo wilaya ya Momba mkoani Songwe katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa aliyeko katika mafunzo kwa vitendo toka Idara ya Habari (MAELEZO).
  Mtaalam wa Kilimo cha Kisasa na Tabibu wa Dawa za Asili Dkt. Samson Kibano akizungumza na Waandsishi wa Habari kuhusu mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo wilaya ya Momba mkoani Songwe katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa aliyeko katika mafunzo kwa vitendo toka Idara ya Habari (MAELEZO) Thobias Robert.   0 0

  NEC –DODOMA

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhan amewaasa wadau wa uchaguzi kuhakikisha kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyika katika Kata 43, Novemba 26 unafanyika kwa amani na utulivu.

  Bw. Kailima ameyasema hayo leo (Jumamosi) mjini Dodoma wakati wa maandalizi ya mafunzo kwa Wasimamizi na Wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi yanayotarajiwa kuanza kesho (Jumapili) mjini hapa.

  “Mlango wa kuchukua fomu kwa ajili ya uteuzi utafunguliwa kuanzia tarehe 20 saa moja na nusu asuhuhi mpaka 25 mwenzi huu, na fomu zinatakiwa kurejeshwa na uteuzi utafanyika tarehe 26 mwenzi Oktoba saa kumi kamili jioni. Nawasihi wadau wote wa uchaguzi tufanye uchaguzi wetu uwe wa amani na utulivu, natumaini kama ambavyo nchi yetu ni kisiwa cha amani na kwa jinsi tulivyojipanga (Tume) uchaguzi utakua wa amani na utulivu,” amesema.

  Bw. Kailima amesema kuwa katika mchakato wa kuendea siku hiyo ya uchaguzi NEC hairuhusu mikutano ya vyama vya siasa bali inaruhusu mikutano ya kampeni.

  “Tume ya Taifa ya Uchaguzi hairuhusu mikutano ya vyama vya siasa, Tume inaruhusu mikutano ya kampeni kwa muda wa siku 30 kuanzia tarehe 27 Oktoba mpaka tarehe 25 Novemba 2017, siku moja kabla ya uchaguzi. Kampeni lazima ziendeshwe kwa utaratibu uliopangwa,” amesema Bw. Kailima.

  Akizungumzia kuhusu maadili ya Uchaguzi, amesema kwa mujibu wa Kifungu Namba 124A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume, Serikali na vyama vya siasa vyote vinapaswa kukubaliana na maadili ya uchaguzi ambayo yalisainiwa na wadau wote tarehe Julai 27, 2015.


  0 0

   Daktari wa Mifugo na Kilimo, Dk.  Aloyce Kessy akitoa mafunzo ya jinsi ya kuandaa vitalu vya miche ya papai katika kikao cha mpango kazi kwa watalaamu wa kilimo wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) watakaokuwa wanasimamia mashamba makubwa yaliyoanzishwa na mtandao huo maeneo ya Ruaha mkoani Iringa, Kibaha na Vikindu mkoani Pwani. Kikao hicho kimefanyika leo eneo la Goba, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Dk. Kessy akifafanua jambo wakati wa kikao hicho. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao huo, Dk. Kissui S Kissui na  Mkurugenzi wa Miradi na Maendeleo ya Biashara wa Mkikita, Edwin Mkwanga
   Washiriki wakisikiliza kwa makini wakati Dk. Kessy akitoa mafunzo hayo
   Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akiwaelea watalaaamu hao kuhusu majukumu yao.


  0 0

  Na: Fatma Salum (MAELEZO)

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa hana mpango wa kufuta mbio za mwenge wa uhuru kutokana na madai ya baadhi ya watu wanaosema kwamba hauna faida.

  Rais Magufuli ameyasema hayo leo Mjini Zanzibar alipokuwa akihutubia kwenye sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

  “Mwenge wa Uhuru hatutaufuta kwa sababu unachochea maendeleo, katika kipindi cha uongozi wangu na Dkt. Shein Mwenge utaendelea kukimbizwa nchini kote,” alisisitiza Rais Magufuli.Alisema kuwa baadhi ya watu wanaodai kwamba mwenge huo unaleta hasara kutokana na gharama zinazotumika, wazingatie kuwa bajeti ya kukimbiza mwenge ni ndogo ukilinganisha na faida kubwa inayopatikana kupitia miradi inayotekelezwa kutokana na hamasa ya mbio za mwenge kwenye maeneo mbalimbali kote nchini.

  Aidha alibainisha kuwa mwenge wa uhuru ni moja ya tunu za nchi ya Tanzania na alama ya uhuru na utaifa wetu hivyo kuufuta ni sawa na kufuta alama kubwa inayotambulisha nchi yetu.“Mwenge huu unatuunganisha watanzania na kuimarisha muungano wetu na yeyote atakayejaribu kuharibu amani au kuvuruga muungano tutapambana naye,” alisema Rais Magufuli.

  0 0

  Na TIGANYA VINCENT-RS-TABORA

  SERIKALI mkoani Tabora imesitisha likizo kwa muda kwa Maafisa Ugani na Watumishi wote wanaowatakiwa kuwasaidia wakulima ili waweze kulima kilimo kinachozingatia utalaamu kwa ajili ya kuwawezesha kuzalisha mazao mengi na kwa tija.

  Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha Wakuu wa Wilaya , Wakurugenzi Watendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo na Seketarieti ya Mkoa huo.

  Alisema kuwa wakati msimu wa mvua unakaribia kuanza sio vema watumishi wa kada hiyo wakaanza likizo kwani wanapaswa kutumia kipindi hicho kuwafanya kazi ya kuwasaidia na kuwaelimisha wakulima ili wafanye vizuri katika shughuli zao na kuleta maendeleo kwa mkoa na Taifa kupitia mavuno mazuri watakayopata.

  Mwanri alisema kuwa pamoja na kuwa likizo ni haki ya mtumishi inabidi wazingatie kuwa likizo zao haziathiri wakulima katika kipindi hiki muhimu kwa ajili ya kilimo.Alisema kuwa baada ya shughuli za kilimo kukaa vizuri Maafisa hao wanaweza kuendelea na likizo zao ikiwa watakuwa wamehakikisha kuwa kwenda kwao likizo hakutakuwa na athari kwa wakulima.

  Aidha Mkuu wa Mkoa wa Tabora amewaagiza Maafisa Ugani wote kuondoka maofisini na kwenda kwa wakulima katika kipindi hiki ili kuhakikisha kila mkulima anazingatia kanuni bora za kilimo kulingana na mazao anayolima.Alisema kuwa lengo ni kutaka Mkoa wa Tabora uwe mfano wa kuigwa katika ulimaji wa kilimo cha kisasa na chenye tija.


  0 0


  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, Mtwara.

  WAHANDISI na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wanapambana usiku na mchana kuzifanyia matengenezo mashine za kufua umeme, ili kuondoa tatizo la kukosekana kwa umeme kwa vipindi virefu kila siku kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi.

   Akizungumza mjini hapa leo Oktoba 14, 2017, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia Uzalishaji, Mhandisi Kaitwa Bashaija, (pichani juu), amesema kwa sasa Wahandisi na mafundi wa shirika hilo wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana ili kutengeneza mitambo hiyo na hivyo kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi kwa haraka.

  K-VIS BLOG ilishuhudia mafundi hao wakifanyakazi ya kurekebisha mitambo hiyo katika kituo cha kuzalisha umeme wa kutumia gesi asilia mkoani Mtwara leo Oktoba 14, 2017.

  “Mitambo hii ina kiasi cha mika 10 tangu ifungwe, na kadiri miaka inavyokweda ndivyo ongezeko la uhitaji wa umeme hususan mkoani Mtwara linazidi kuongezeka kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi,” Alisema Mhandisi Bashaija.

  Alisema, miaka michache iliyopita baadhi ya mitambo iliweza kuzimwa na bado hali ya umeme ilikuwa imara.Wiki iliyopita Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani aliagiza TANESCO kufanya juhudi za ziada kuhakikisha tatizo la umeme mkoani Mtwara na Lindi linapatiwa ufumbuzi wa haraka.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
   Mhandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akifanyia matengenezo moja ya mashine za kufua umeme kwenye kituo cha kufua umeme Mtwara, leo Oktoba 14, 2017
   Wahandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akifanyia matengenezo moja ya mashine za kufua umeme kwenye kituo cha kufua umeme Mtwara, leo Oktoba 14, 2017
   Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa kutumia gesi asilia cha Mtwara, Mhandisi Mkulungwa Chinumba, akizungumzia hatua zinazoendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi wa haraka. Kulia ni Mhandisi Bashaija.

  0 0


   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.Jordan Rugimbana akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa maafisa wa Kijeshi 32 kutoka Majeshi ya nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambao wapo hapa nchini kuhudhuria mafunzo ya Ukamanda na Unadhimu kwenye chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kilichopo Duluti mkoani Arusha 
  Baadhi ya Ujumbe wa maafisa wa Kijeshi 32 kutoka Majeshi ya nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambao wapo hapa nchini kuhudhuria mafunzo ya Ukamanda na Unadhimu kwenye chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kilichopo Duluti mkoani Arusha .
  Mmoja wa baadhi ya maafisa wa Kijeshi 32 kutoka Majeshi ya nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambao wapo hapa nchini kuhudhuria mafunzo ya Ukamanda na Unadhimu kwenye chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kilichopo Duluti mkoani Arusha,akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa Mh.Rugimbana alipokutana nao na kufanya mazungumzo nao mapema leo.
   
  Baadhi ya maafisa wa Kijeshi 32 kutoka Majeshi ya nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambao wapo hapa nchini kuhudhuria mafunzo ya Ukamanda na Unadhimu kwenye chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kilichopo Duluti mkoani Arusha  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.Jordan Rugimbana alipokutana nao mapema leo.


older | 1 | .... | 1961 | 1962 | (Page 1963) | 1964 | 1965 | .... | 3348 | newer