Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1959 | 1960 | (Page 1961) | 1962 | 1963 | .... | 3284 | newer

  0 0

  MKE wa Rais wa awamu ya nne mama Salma Kikwete  alikabidhiwa  tuzo ya heshima kutokana na kutambua jitihada zake za kumlinda na kumtetea mtoto wa kike  iliyotolewa na  Taasisi isiyo ya Kiserikali inayifahamika kwa jina la Room to Read.

  Mama Kikwete alikabidhiwa tuzo hiyo  Mkurugenzi wa Room To Read  Peter Mwakabwale kwenye hafla iliyofanyika viwanja vya Bwawani Kihaba Maili Moja Mkoani Pwani.

  Akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka katika shule mbalimbali za mkoa  wa Pwani mama  Kikwete amezitaka Hamlashari kutenga bajeti ya kujenga mabweni katika shule kwa ajili  ya wanafunzi wakike  sanjari  na kujenga  maabara  na vyumba  vya madarasa  ili kuweza  kuwarahisishia  wanafunzi  hususani wasichana  ili waweze kujifunza  bila  kikwazo chochote na kufaulu vema masomo yao.
  Mama Salma Kikwete amesema kuwa  Mkoa wa Pwani unashika nafasi ya kumi  kitaifa kwa mimba  huku sababu mojawapo ni  ukosefu wa mabweni ya wasichana hali inayopelekea wasome shule za kutwa na kukutana na vishawishi wawapo njiani kuelekea ama kurudi shule.
  Maadhimisho hayo yamefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Room to Read linaloendesha mradi wa Elimu kwa Wasichana  katika mkoa wa Pwani  na  kuzihusisha  Wilaya za Bagamoyo, Chalinze na Kibaha ambapo wamekuwa wakitoa elimu ya stadi za maisha kwa wasichana lakini pia kuwasaidia gharama za mahitaji ya shule pamoja na karo kwa familia zisizo na uwezo wa kifedha 
   Siku ya kumuenzi mtoto wa kike  huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 11 kufuatia  maazimio  ya malengo endelevu  ya Umoja wa mataifa , viongozi  wa nchi mbalimbali  duniani  walikubaliana  na kuyapitisha   huku miongoni mwa malengo  matano   mojawapo  kuhakikisha  tunafikia usawa  wa kijinsia  na uwezeshaji  wa wasichana  na wanawake  wote  duniani ifikapo mwaka 2030.

  Wahamasishaji wa Mradi wa Elimu kwa wasichana Room to Read wakionesha kazi wanazozifanya katika maadhimisho ya mtoto wa Kike duniani October 11 mkoani Pwani -kibaha

  0 0


  0 0

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana. Mkurugenzi huyo alisema katika maadhimisho hayo NBC imezidi kuboresha ubora wa huduma na bidhaa mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya wateja wao wa kada zote. Kulia ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi wakikata utepe ili kurusha ‘puto’ kuashiria uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana.
   Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha NBC, Ngwitika Mwakahesya akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC jijini Dar es Salaam jana.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), akizungumza waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo  katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana.


  0 0  UONGZI wa Shamba la Kahawa la Aviv, lililoko kijiji cha Lipokela, kilomita 45 kutoka Songea mjini, umesema Mradi wa umeme wa Makambako-Songea utaleta nafuu kubwa ya kupunguza gharama za kuendesha majenereta ya kufua umeme kwenye shamba hilo kwa asilimia 70, Meneja wa shamba Bw.Hamza Kassim amesema.

  Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea shamba hilo ili kupata maoni ya wamiliki kuhusiana na mradi mkubwa wa umeme wa 220kV, Makambako- Songea Oktoba 12, 2017, Bw. Kassim alisemamahitaji ya umeme kwenye shamba hilo ni Megawati 2.25 hadi 2.5 na zote hizo zinazalishwa na umeme wa kutumia mafuta (Jenereta). 

  shamba hilo linalo ilikiwa na kampuni ya Olam Tanzania Limited yenye makao yake makuu nchini Songapo, lina ukubwa wa Hekta 1,012 kati ya hizo, Hekta 1,000,000 zimepandwa mazao.“Mimea ya Kahawa ambayo imefikia hatua ya kupevuka (matured), ni Hekta 800, huku Hekta 200 bado ni Kahawa changa, tunatumia nishati ya umeme kwa shughuli za umwagiliaji na ubanguaji wa Kahawa ambapo kwa siku tunatumia lita 4,000 za dizeli kuendesha jenereta hizo.” Alifafanua Bw. Kassim.

  Ujio wa mradi huu ni faraja kubwa kwetu na tunashukuru mradi huu utakapokamilika utatupunguzia gharama za uendeshaji kwa asilimia 70 na hivyo kutupa fursa ya kufanya upanuzi zaidi wa kilimo cha kahawa, Alibainisha Meneja huyo.
  Meneja wa Shamba la Kahawa, Aviv, linalomilikiwa na kampuni ya Olam Tanzania Limited lililoko kijiji cha Lipokela, kilomita 45 kutoka Songea mjini Bw.Hamza Kassim, (katikati), akizungumzia mradi wa umeme wa Makambako-Songea ambao utaunganishwa kwenye kiwanda chake, mbele ya wahariri wa vyombo vya habari waliofika kiwandani hapo ili kujionea manufaa yatokanayo na mradi huo katika uwekezaji mkubwa, Oktoba 12, 2017.
  Meneja wa Mradi wa umeme wa 220kV, Makambako-Songea Mhandisi Didas Lyamuya, akifafanua baadhi ya mambo kwenye eneo la ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme cha Songea ambacho kiko katika hatua ya ujenzi wa msingi wa kufungia mitambo. Chini ya mradi huo jumla ya vituo vipya viwili vya kupoza umeme vinajengwa huko Madaba na kimoja kinafanyiwa upanuzi huko Makambako
  Taswira ya ujenzi wa msingi wa kufungia mitambo kituo kipya cha kupoza umeme cha Songea.


  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akifafanua jambo wakati akiongoza kikao cha Secretariet ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kwa  maandalizi ya vikao vya kikanuni vya Umoja wa Vijana wa CCM vitakavyofanyika Dodoma
  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiongoza kikao cha Secretariet ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kwa  maandalizi ya vikao vya kikanuni vya Umoja wa Vijana wa CCM vitakavyofanyika Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine vitajadili waombaji wa nafasi mbali mbali za uongozi kwa nafasi za Mkoa na Taifa kupitia Umoja wa Vijana wa CCM kabla kuwasilisha katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi kwa uteuzi wa mwisho.(picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )

  0 0

   Waziri wa  Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi , Prof Makame Mbarawa , akizungumza na Wahandisi majengo wakati wa ufunguzi wa semina yao ya siku mbili katika ukumbi  wa Mlimani City Jijini  Dar es Salaam
   Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi , Prof Makame Mbarawa , akikabidhi zawadi kwa Mwalimu wa shule ya Sekondari Royola , Venancy Robert mara baada ya kuibuka mshindi wa jumla kwa sekondari zote nchini
   Waziri wa  Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi , Prof Makame Mbarawa ,  kwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Royola,Ashraf Raphael mara baada ya kuibuka bingwa wa kitaifa katika uandishi wa Insha
   Washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi,Prof Makame Mbarawa.
  Waziri wa  Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi , Prof Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa Insha za uandishi wa majengo
  PICHA ZOTE NA HUMPHREY SHAO

  0 0

   Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kawe, wakishiriki maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani kwa kushiriki semina iliyoandaliwa kwa pamoja na taasisi ya Her Initiative na TAHMEF kwa ajili ya kutoa elimu hya kujitambua, ushauri wa kitaalamu na kupima afya za mabinti, semina iliyofanyika shuleni hapo, jana.  0 0

  SABABU kubwa za wanafunzi wa shule za msingi  kutokufanya vizuri darasani imeelezwa inatokana  na uoni hafifi kwa baadhi yao na sio kwamba hawana akili .

  Lakini pia imebainishwa pia kati ya watu 100 kati ya 15 wana kabi liwa na tatizo la macho ambalo limekuwa likiwaathiri kwa asilimia na kushindwa kufikia malengo yao.

  Hayo yalibainishwa juzi na Mratibu wa Huduma za Macho Mkoani Tanga Dkt Frida Kassiane wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo yalienda sambamba na upimaji wa macho uliokuwa ukiendeshwa na kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga.

  Alisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi kuumwa macho huku wakiwa hawajitambui kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu za utoaji wa huduma za upimaji machi kwao hususani mashuleni.

  “Ukiangalia leo hii baadhi ya wanafunzi utakuwa walikuwa wakifanya vizuri katika mitihani yao lakini ghafla wanaanza kushuka kiwango na hili unaweza kukuta linasababishwea na tatizo la macho kama lilivyogundulika kwa wanafunzi wachache kwenye shule tulizopita “Alisema.

  Alisema suala hilo linasababishwa pia na lishe dunia kwa asilimia kubwa ya watoto wengi ikiwemo kukosa kupata vyakula vilivyokuwa na virutubisho vinavyoweza kuongeza nguvu na kinga ya macho.

  Alisema zoezi hilo ambalo limeanza siku nne zilizopita limewafikia zaidi ya wanafunzi 1500 katika shule za Msingi,Kwanjeka,Mabokweni na Nguvumali ambapo baadhi yao walibainika kuna matatizo hayo na kusaidia matitabu zaidi na kampuni hiyo.
   Mwalimu wa shule ya Msingi Nguvumali Jijini Tanga akichukua maelezo ya wanafunzi kabla ya kuanza zoezi la upimaji wa huduma ya macho wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo siku hiyo iliendana na sambamba na upimaji macho ulioendeshwa na Duka la Miwani la Noor Optics kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji hilo kwa wanafunzi wa shule za msingi za mabokweni,kwanjeka na nguvumali,
   Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Tanga,Dkt Frida Kassiane akiwapima macho mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Nguvumali Jijini Tanga wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo siku hiyo iliendana na sambamba na upimaji macho ulioendeshwa na Duka la Miwani la Noor Optics kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji hilo kwa wanafunzi wa shule za msingi za mabokweni,kwanjeka na nguvumali,

   Amina Nasoro ambaye Mratibu wa Huduma ya Afya ya Macho katika kampuni ya kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga akichukua maeleza ya wanafunzi kabla ya kuwapima.
   Amina Nasoro ambaye Mratibu wa Huduma ya Afya ya Macho katika kampuni ya kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga akichukua maeleza ya wanafunzi kabla ya kuwapima.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akiongoza askari kuhamisha udongo "Kifusi" toka kwenye msingi wa ujenzi wa nyumba za Polisi na kupeleka kwenye mtaro.

  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  Ujenzi wa kituo kidogo cha Polisi cha Morombo kilichopo kata ya Murieti halmashauri ya Jiji la Arusha  huenda ukawa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo ambalo linakuwa kwa kasi kibiashara na ongezeko la  idadi ya watu.

   Uwepo wa kituo hicho utawezesha kusogeza huduma ya kiusalama kwa wakazi hao kwa ukaribu zaidi lakini pia kesi zao zitaripotiwa hapo hapo badala ya Kituo kidogo cha Sombetini au kituo Kikuu ambavyo vipo umbali mrefu toka eneo hilo.

  Akizungumza katika eneo la kituo hicho, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba ufunguzi wa kituo hicho ambacho kipo kwenye hatua za umaliziaji unatarajia kwenda sambamba na wa nyumba za askari watakaofanya kazi kituoni hapo na hiyo itasaidia askari kutoa huduma kwa haraka na ukaribu kwa kuwa watakuwa wanaishi eneo hilo.

  Kamanda Mkumbo alisema kwamba, yeye pamoja na askari wapatao 200 wa vikosi mbalimbali jana waliamua kushiriki katika kuchimba msingi na kubeba udongo “Vifusi” kutoka eneo la ujenzi na kwenda kuumwaga kwenye mtaro.

  Alisema pamoja na majukumu walionayo ya kuhakikisha jiji la Arusha pamoja na wilaya nyingine za mkoa huu zinakuwa salama lakini pia wameamua kufanya hivyo kwa nia ya kupunguza gharama na watakuwa tayari kushiriki katika kusogeza matofali kwa mafundi na hata kukoroga zege pindi nguvu kazi itakapohitajika. 

  “Pamoja na sisi kujitoa kufanya kazi hizi lakini pia wananchi wanaozunguka eneo hilo wanapaswa kujitolea kubeba vifusi kwa kuwa kituo hicho ni cha kwao”. Alitoa wito huo Kamanda Mkumbo.

  Kwa upande wake mkazi wa eneo hilo aliyejulikana kwa jina la mzee Isihaka Kivuyo alisema kwamba, kituo hicho  kitasaidia kuiweka jamii karibu na jeshi hilo jambo ambalo litasaidia kupunguza uhalifu. 

  Alisema kwamba wananchi wanatakiwa wafurahie ujenzi wa kituo hicho hivyo na kuwataka wajitolee katika shughuli ndogondogo za ujenzi wa nyumba hizo za askari badala ya kazi hizo kufanywa na askari Polisi pekee ambao wana majukumu mengine ikiwemo kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao unakuwepo.

  Ujenzi wa kituo hicho chenye hadhi ya daraja B ambao umefadhiliwa na Kampuni ya Lodhia Group ulianza toka mwaka 2016 mwezi Mei, lakini pia ujenzi wa nyumba saba za askari kwa sasa upo kwenye hatua za uchimbaji wa msingi na unatarajiwa kwenda kwa kasi ili uende sambamba na ufunguzi wa kituo.
  Baadhi ya askari wakichimba na kubeba udongo toka eneo la ujenzi wa nyumba saba za askari kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya ujenzi.
  Kituo kipya cha Polisi Mrombo kilichopo kata ya Murieti halmashauri ya jiji la Arusha ambacho kina hadhi ya daraja "B" kipo katika hatua za mwisho za umaliziaji.

  0 0

  Na Agness Francis, Blogu ya jamii.

  Baraza la Sanaa Taifa(BASATA) limemfungia rasmi mmiliki wa Click Media Entertainment, Edward Majura kujihusisha  kuendesha  matukio  yeyote ya sanaa hasa la utendaji wa mashindano ya urembo  hapa nchini kwa muda usiojulikana.

   Akizungumza hayo katibu mtendaji (BASATA) Godfrey Mngereza katika ofisi za (BASATA) jijini Dar es Salaam amesema kuwa Edward Majura ambaye ni mtendaji wa mashindano ya urembo miss Mbeya amekiuka sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa  mashindano hayo hapa nchini .

  Vilevile katibu Mngereza amewataka wadau na waandaaji wote wa matukio ya sanaa kuhakikisha wanafuata taratibu zote zilizowekwa  ikiwa ni pamoja na kupata vibali  na kufanya kazi kwa karibu na ofisi za utamaduni katika ngazi za wilaya na kimkoa pindi wanapohitaji kufanya tukio lolote la sanaa na hapa nchini.

  Aidha Katibu mtendaji huyo ametanabaisha kuwa muandaaji yoyote atakae tumia wakala walioko nchini katika tukio lake la sanaa atawajibika kuhakikisha wako chini yake na wanafata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa tukio husika, ambapo kinyume na makubaliano hayo ( BASATA) haitasita kumchukulia hatua yoyote ya kisheria.

  Hata hivyo Mngereza ametoa tamko kuwa  wadau wote nchini watakaoendesha  matukio yoyote ya sanaa ikiwemo  mashindano ya urembo wanatakiwa  kuwasilisha zawadi zao sehemu husika ambayo ni  (BASATA) katika ofisi za utamaduni siku 14 kabla ya kilele cha mashindano hayo.

  Katibu mtendaji (BASATA) Godfrey Mngereza akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa sanaa nchini kuhusu kufata kanuni na taratibu za kufanya matukio ya sanaa hasa na mashindano ya urembo katika ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam.

  0 0

   


  0 0

  Na Agness Francis ,Blogu ya jamii
  Waziri wa habari,utamaduni, sanaa na michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amehudhudhuria  mkutano   wa  wasanii wa shirikisho la sanaa za ufundi  hapa nchini kusikiliza maendeleo na changamoto zinazowakabili wasanii hao na kuwataka kuchangamkia fursa kazi za mikono yao.

  Katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Shirikisho hilo la sanaa za ufundi  hapa nchini ambalo lilianza rasmi mwaka 2009 na kupata usajili wake mwaka 2010 ambapo wasanii hao walimepata mafanikio  kwa kushirikiana na (BASATA)pamoja na ubalozi wa China katika mradi ambao ulijulikana kwa jina la Tingatinga Art Biennale na walipatikana washindi wawili ambao walizawadiwa tiketi ya kwenda nchini China.

  Vile vile shirikisho limeeleza changamoto zinazowakabili wasanii hao kuwa Elimu ya sanaa za ufundi haifundishwi  mashuleni, hakuna kituo maalumu  cha Taifa cha kuonesha kazi za wasanii na masoko ya sanaa kuwa hafifu kutokana na ugumu wa usafirishaji wa vinyago kwenda  nje ya nchi kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

  Aidha Waziri Mwakyembe amekanusha dhana potofu isemwayo  kuwa wasanii wa sanaa za ufundi wengi wao  hawajaenda shule na amesema kuwa wizara yake itaunga mkono na kushirikiana bega kwa bega  na juhudi za  sanaa hiyo ili kuepukana na wanyonyaji wa  kazi ya wasanii hao.

  Nae naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Juliana Shonza amemalizia kwa kutoa wito kwa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) kuendelea kuinua vipaji  kwa kuweza kuwafikia hasa  wasanii wa mikoani  na wilayani ambao wamesahaulika kwa muda mrefu katika kuiendeleza tasni hiyo.
   Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wasanii wa shirikisho la sanaa za ufundi Tanzania pamoja kuwapongeza kwa kazi za mikoni wanazozifanya wasanii hao leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
   Naibu waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo Juliana Shonza, akizungumza na wandishi wa habari pamoja na wasanii wa shirikisho la sanaa za ufundi Tanzania na kuwataka( BASATA) kuendelea kuinua vipaji vya wasanii hapa nchini hasa kwa wale walioko wa mikoani.
  Wageni waalikwa waliojitokeza kwa wingi katika kuhudhuria mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
  Wasanii wa maigizo ya maonyesho ya  jukwaani wakifanya igizo linalohusu kampeni ya kuzuia rushwa  leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas akizungumza na waandishi vyombo mbalimbali vya habari nchini, wakati akitolea ufafanuzi madai ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) juu ya tuhuma dhidi Rais na Serikali yake. Mkutano huo umefanyika mchana huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Habari na Picha wa Idara ya Habari MAELEZO, Rodney Thadeus.


  0 0

   Mr Fredrick Kanga, Head of Human Resources at Exim Bank Tanzania addressing guests, customers and media during the official launch of Exim Bank Dodoma Branch located inside the University of Dodoma, at Chiwaga area yesterday. Others are Mr Stanley Kafu, Head of Marketing at Exim Bank Tanzania (left) and the guest of honour District Commissioner Christina Mndeme.
   Dodoma District Commissioner Christina Mndeme, addressing the guests, customers and media during the official launch of Exim Dodoma Branch located inside the University of Dodoma, at Chiwaga area yesterday. Others are Mr Fredrick Kanga, Head of Human Resources at Exim Bank Tanzania (left) and Mr Stanely Kafu, Head of Marketing at Exim Bank Tanzania (left).
   Dodoma District Commissioner Christina Mndeme on behalf of the Regional Commissioner Jordan Rugimbana, officially launches Exim Bank Dodoma Branch earlier yesterday during the official ceremony. The branch which is located inside the University of Dar es Salaam Dodoma will serve the captive clients of the University of Dodoma, which consists of over 25,000 students, 2000 employees and over 8 Government Ministries who have moved there. It will also serve the Dodoma City clients, as the branch is only 5 to 7 minutes drive from the city centre. To her right is Mr Fredrick Kanga, head of Human Resources at Exim Bank Tanzania.
   Exim Bank Dodoma Branch staff interacting with the guest of honour Dodoma District Commissioner, Christina Mndeme during the official launch of the branch located inside the Universty University of Dodoma, at Chiwaga area yesterday.


  BENKI ya Exim Tanzania imethibitisha  kujitolea  kuimarisha ushirikishwaji wa wa nanchi kwenye mfumo rasmi wa kifedha nchini kwa kuzindua tawi jipya katika mkoa wa Dodoma,Tanzania. UtanuzihuuutaongezauwepowaBenkiya Exim kuwanajumlayamatawi 33nchinikote.
  Akizungumza katika uzinduzi rasmi Fredrick Kanga, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu katika Benki ya Exim Tanzania, alisema, "Utanuzi wa benki ni sehemu ya mkakati wetu wakukuza huduma zetu katika maeneo ambayo yanatuleta karibu na wateja wetu. Tawi litatoa huduma kamili za kibenki kama vile kuhifadhi pesa, huduma za uwekezaji, na suluhisho za malipo ya kampuni."
  Tawi la Dodoma, lililopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma, litawahudumia wateja wa Chuo Kikuu hiko, ambacho kina wanafunzi zaidi ya 25,000, wafanyakazi2000 na Wizara za Serikali zaidi ya 8 ambazo zimehamia huko. 
  Tawi litawatumikia wateja wa Jiji la Dodoma, kwa kuwa tawili na umbali wadakika 5 hadi 7 kwa mwendo wa gari kutoka katikati ya jiji.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alipongeza Benki ya Exim Tanzania kwa kujitolea kwake "Tunafurahi kuwa na uwepo wa Benki ya Exim katika mji mkuuwa Tanzania, ili kuimarisha ushirikishwaji wa wananchi kwenye mfumo rasmi wa kifedha  unao wawezesha kupata huduma, bidhaa za kifedha,na mitaji kwa jamii na watu binafsi wa Dodoma. "
  Benkiya Exim  imeongezeka kwa ujasiri ilikukuza msingi wa mali na kufanikiwa kutanua uwezo  kwa wateja Shughuli za Benki zinapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Iringa, Mbeya na Mtwara ndani ya Tanzania na kampuni tanzu nje ya nchi katika Visiwa vya Anjouan, MohelinaMoroni vya Union of Comoros ,kwenye Jamhuri ya Djibouti na Uganda – uwepo wa benki ya Exim.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la UNAIDS na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.Michel Sidibe alipofika Ikulu Mjini Zanzibar na Ujumbe wake.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la UNAIDS na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.Michel Sidibe alipofika Ikulu Mjini Zanzibar na Ujumbe wake.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la UNAIDS na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.Michel Sidibe alipofika Ikulu Mjini Zanzibar na Ujumbe wake(hawapo pichani)
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la UNAIDS na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.Michel Sidibe (wa pili kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar na Ujumbe wake (Picha na Ikulu) 

  0 0

   Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali  hawapo pichani wa Wizara ya afya kuhusiana na kuimarisha huduma bora za afya nchini  leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Naibu wa wizara hiyo Dkt. Faustine Ndungulile na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya. Wakati wa kikao chake na wakuu hao.


  NA WAMJW-DAR ES SALAAM
  WIZARA ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imejidhatiti kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto mpaka kufikia 2020 ili kutokomeza vifo vya wajawazito na watoto wachanga .

  Hayo yamesemwa na Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipokutana na Wakuu wa Idara na vitengo Mbalimbali kwa ajili ya utambulisho wa Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndungulile  katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.

  “Vifo vya wajawazito vimekua tishio nchini hivyo ni lazima tuimarishe huduma za afya ya mama na mtoto ili tufikie malengo ya kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi mpaka kufikia 2020 ili kujenga taifa lenye watu wenye afya bora” alisema Waziri ummy.

  Aidha Waziri Ummy amesema kuwa katika kuboresha hilo amewaagiza wakuu wa idara wizara ya afya kushirikiana na mfuko wa bima ya afya nchini(NHIF) kuona kama kuna uwezekano wa kuanzisha bima ya afya kwa wajawazito kwa bei nafuu hadi kufikia Julai mosi 2018.

  Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa wanamipangilio ya kutokomeza kabisa tatizo la dawa nchini kwa kuweka mpango mkakati kati ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na vituo  vitoavyo huduma za afya  ili kuepuka tatizo hilo lisijirudie mara kwa mara .

  Kwa upande wake Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndungulile amesema kuwa ameshukuru kwa kupewa dhamana hiyo na atashirikiana vyema na Waziri pamoja na watendaji wa Wizara hiyo ili kuleta ufanisi na Huduma bora za afya nchini.

  “Nitashirikiana na Waziri wangu pamoja na nyinyi watendaji wenzangu katika kusimamia na kutekeleza sera ya afya ili kuweza kutoa huduma bora za afya kwa watanzania wote bila ya kujali rika,jinsia wala umri” alisema Dkt. Ndungulile.


  Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa wamepokea maagizo hayo amabayo baadhi  wameanza kuyatekeleza na mengine  atawahimiza watendaji wake kuendana na kasi ya awamu ya tano ya HAPA KAZI TU ili kuifikisha nchi katika afya bora.
   Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto Dkt.  Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akiongea na wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya hawapo pichani kuhusiana na kuimarisha huduma bora za afya nchini  leo jijini Dar es salaam, katikati ni Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu na kulia ni Katibu Mkuu Wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya. Alipokutana na wakuu hao.
   Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Waziri mwenye dhamani hiyo  Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile hawapo pichani wakati wa kikao na wakuu wa idara hizo leo jijini Dar es salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 10/13/17--08:14: Article 8
 •  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kufungua Maonyesho ya Tatu ya Kimataifa ya Utalii yanayojulikana kwa jina la Swahili linalofanyika kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya ya Tatu ya Kimataifa ya Utalii ya Swahili uliofanyika kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi kinyago maalum Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANAPA Jenerali Mstaafu George Waitara kama ishara ya shukrani kwa kuwa mmoja wa wadhamini wa Maonyesho ya Tatu ya Utalii ya Kimataifa ya Utalii ya Swahili.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Bw. Allan Kijazi mara baada ya kupokea kinyago maalum ikiwa ni shukrani kwa kuwa mmoja wa wadhamini wa Maonyesho ya Tatu ya Utalii ya Kimataifa ya Utalii ya Swahili. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya mkutano wa biashara uliondaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake pamoja na wadau wengine wa sekta ya fedha. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha benki hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akizungumza  na baadhi ya wateja wa benki hiyo jana jijini Dar es Salaam baada ya mkutano wa biashara uliondaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake pamoja na wadau wengine wa sekta ya fedha.

  Ecobank imeeleza  mikakati  yao kutoa huduma bora kwa wateja wake na wafanyabiashara nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla huku ikitoa wito kwa wateja wote kuendelea kufurahia huduma bora  za kibenki zinazotoa ufumbuzi kwa mahitaji mbalimbali yakiwemo yale yanayohusu malipo kwa kuwa huduma zao zinauwezo wa kuvuka mipaka ya nchi kwa kuwa mtandao wao umeendea na unauwezo wa kuhudumia  Afrika na duniani kote

  Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee wakati wa mkutano wa kibiashara ambao uliandaliwa na benki hiyo na kuhusisha wateja pamoja na wadau wengine wa benki hiyo.

  Alisema Ecobank inatoa ufumbuzi wa kipekee wa biashara ya intra-Afrika, na kuwezesha wateja wake kukabiliana na biashara zao za kimataifa kwa ufanisi na kupunguza upotevu wa malipo pamoja na kufanya kazi kwa ukaribu na wateja katika maeneo muhimu kama vile kushughulikia Malipo, Usindikaji, mambo yanayohusu Makazi, mambo ya kifedha, kupunguza upotevu wa fedha pamoja na kuimarisha mikopo.

  Kuhusu suluhisho la biashara ya kifedha alisema, "Wateja wanafaidika kutokana huduma za  mikopo barani kote ambako benki hiyo ina matawi kwenye nchi 33."

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo, wateja wanapata muda muafaka kwa uharaka na urahisi wakati wa kupata huduma kama kuagiza LCs, makusanyo ya kutoka nje ya nchi, dhamana kwa bidhaa za wateja, Export LCs (kushauri na kujadili), makusanyo ya kutoka nje ya nchi, kuwekewa dhamana, dhamana ya utendaji, huduma za kibiashara barani Afrika, makusanyo ya kikanda pamoja na Malipo ya Kimataifa.

  "Lengo la Ecobank ni kutoa huduma za kipekee kwa wateja watu huku pia tukiimarisha ushirikiano wa kifedha barani Afrika na kutoa ufumbuzi wa kuwezesha wafanya biashara katika maeneo mbalimbali. Huduma za kibiashara za Ecobank huwawezesha  wafanya biashara nje ya nchi kupata dhamana ya malipo bila haja ya Barua ya Mikopo na gharama zake zinazohusiana na muingizaji, "alisema Bi Mzee.

  Alisema Ecobank ikiwa kwenye pande zote mbili za kibiashara, wateja wanafaidika kutokana na suluhisho la mwisho la kukamilika na kuongeza kwa ukusanyaji wa fedha kikanda  na pia huwapa fursa wafanyabiashara kupata papo kwa uhamisho chini ya dola 10 000 huduma ambayo inaruhusu fedha kuhamishiwa kote barani Afrika na kupata pesa ya papo hapo.

  "Ikiwa inapatikana kwenye nchi 33 za Afrika - zaidi ya benki yoyote duniani - Washirika wa Ecobank wanaweza kuthibitisha na kujadili Barua ya Mikopo kwa wateja katika nchi hizo, na pia kusimamia malipo yanayohusiana na biashara kutoka kwa mabenki nje ya Afrika," alisema

  Bi Mzee aliwaambia wadau na wateja kwenye mkutano huo kwamba Ecobank pia inatoa huduma ya kifedha wakati wa kuagizwa kwa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi, huduma ya kifedha wakati wa kusafirishwa kwa bidhaa na huduma nje ya nchi, huduma za kifedha wakati wa kusafirisha bidhaa au mizingo, na kurahishiza Malipo ya Ankara na haya yote yanafanyika ili kuokoa muda na kupoteza rasilimali zaidi.

  Mkutano huo pia ulitoa nafasi kwa wateja na wadau mbalimbali wa benki hiyo na kuweza kutoa maoni na pongezi zao   kwa benki hiyo.

  Akizungumzia juu ya mkutano huo, mmoja wa mteja wa benki hiyo......, alisema, "natoa shukrani za dhati kwaa Ecobank kwa fursa hii ambayo wametupa kwa sababu tumejifunza mambo mengi kuhusu masuala ya kifedha na hasa pale tunapofanya biashara nje ya nchi yetu.

  "Hii ni hoja na mpango mzuri sana kutoka kwa Ecobank Tanzania. Kuonyesha kumjali mteja binafsi kama sisi kunachochea na kuongeza uhusiano uliopo kati yetu sisi na benki. Mbinu hii imekuwa suluhisho linapokuja kushughulikia mahitaji yetu na tunafurahi sana na huduma zao. "Aliongeza.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia ukimwi kwa misaada yake ambayo imesaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini.

  Makamo wa Pili wa Rais ameyasema hayo Afisini kwake Vuga wakati wa mazungumza yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Shilika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Ukimwi ndugu Michel Sidibr Amesema misaada ya Shirika hilo la UNAIDS imesaidia kuendesha kampeni mbali mbali ambazo zimejenga ualewa miongoni mwa wananchi kuhusu kuwepo kwa ukimwi nchini.

  Hata hivyo balozi Seif ametoa wito kwa viongozi kuendelea kuwahimiza wananchi kujiepusha na vitendo vinavyoambukiza ukimwi pamoja na kuwashajihisha kupima mara kwa mara.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Zanzibar ni kigezo cha kujivunia kwa nchi nyingi kutokana na mafanikio yake ya kupungunza kwa kiwango kikubwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto.

  Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema mafanikio ya Zanzibar ya kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto yakiendelezwa hakutokuwa na mtoto anayeambukizwa virusi vya ukimwi katika kipindi kifupi kijacho.

  Wakati huo huo Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Oman anayeshughulikia Mafuta na Gesi Dkt. Mohammed bin Hamed.

  Katika mazungumzo yao Balozi Seif ametoa shukrani zake kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Oman kwa misaada yake katika miradi mbali mbali ya maendeleo.

  Balozi Seif ameiomba Oman kusaidia katika upanuzi wa uwanja wa ndege wa Pemba na kuwa wa kimataifa, ombi ambalo Serikali ya Oman imesema italifikiria.

  Balozi Seif amesema uwanja huo utasaidia kukuza biashara ya utalii na viungo kati ya nchi hizo mbili pamoja na kuwauganisha kwa karibu zaidi watu wa Zanzibar na Oman ambao kwa asili ni ndugu.

  Kwa upande wake Waziri huyo wa Mafuta na Gesi Dkt Mohammed bin Hamed safari yao ya meli kuja kwa ndugu zao wa Zanzibar kuna lengo la kufungua ukurasa mpya wa mashirikiano kati ya pande hizo mbili. Amesema kuna mambo mengi ya kuwaunganisha watu wa pande hizo mbili kuliko mambo ya kuwatenganisha.

  Kuhusu ombi la Zanzibar la kukarabati kumbusho la Beit-al- ajab na kumbusho la Palace, Serikali ya Oman imesema iko tayari kuyafanyia matengenezo makubwa majengo hayo kwani ni rasilimali ya ulimwengu mzima.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi (UNAIDS) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Michel Sidibr.

  0 0

  SHULE mbili za manispaa ya Kinondoni shule ya Kigogo na Mkwawa zaadhimisha siku ya unawaji mikono ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba 13 ikiwa na kaulimbiu ya mikono safi kwa manufaa ya sasa na ya baadae.

   Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta amesema kuwa kila mtoto anatakiwa kunawa mikono kabla na baada ya kula pamoja na watokapo masalani ili kuepukana na maradhi ya kipindupindi na maradhi yaletwayo kwa kula uchafu.

  Amesema kuwa siku hii ni muhimu hasa kwa watoto wanaokurupuka kumegeana vyakula au vitafunwa wawapo shuleni bila ya kunawa mikono yao na bila ya kujua ni nini madhara ya kula bila kunawa.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya kunawa mikono iliyofanyika katika shule ya Msingi Mabibo na shule ya Msingi Mkwawa jijini Dar es Salaam leo.
  Pia amewaasa wanafunzi wa shule za msingi Kigogo pamoja na Mkwawa kunawa mikono mikono kila wanapotaka kula na baada ya kula pia marabaada ya kutoka maeneo ambayo wanashika uchafu.
   Wanafunzi wa shule ya Msingi Kigogo na shule ya msingi Mkwawa wakiwa katika siku ya kunawa mikono iliyoadhimishwa shuleni hapo kwaajili kuelewa manufaa ya kunawa mikono kabla ya kula, baada baada ya   kula,  na baada ya kutoka msalani kwaajili ya kujikinga na maradhi yanayoletwa na kuto kunawa mikono.
   Mwanafunz wa chuo Kikuu cha Muhimbili Kerobe  TEHSA akiwafundisha watoto jinsi ya kunawa mikono kwa kutumia kibuyu chirizi ambacho ni rahisi zaidi kuliko kuchota maji kwa kutumia kikombe ambayo ni kwaajili ya kunawa mikono kabla na baada ya kula na wakati watokapo msalani hii ikiwa ni siku ya unawaji Mikono iliyoambatana na kauli mbiu ya Mikono safi kwa manufaa ya sasa na yabaadae.

older | 1 | .... | 1959 | 1960 | (Page 1961) | 1962 | 1963 | .... | 3284 | newer