Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1958 | 1959 | (Page 1960) | 1961 | 1962 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (katikati) akiwa na Naibu Mawaziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kakunda (kulia) pamoja na Naibu Waziri Mhe. George Joseph Kakunda mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za OR TAMISEMI mjini Dodoma na kufanya kikao na Watumishi.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Said Jaffo amesema hatahamisha Mkuu wa Idara wala Kitengo katika Wizara hii lakini atamtengeneza awe kama anavyotaka ili aweze kuendana na kasi ya utendakaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

  Waziri  Jaffo ameyasema hayo wakati wa kikao chake na Watumishi wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara hii ambapo aliambatana  na Manaibu Waziri wa OR-TAMISEMI .

  Waziri Jaffo alisema kuwa “Siwezi kuhamisha matatizo kutoka eneo kwenda lingine cha msingi ni kuhakikisha tunamtengeneza hapa hapa awe kama tunavyotaka kulingana na mahitaji yetu na aweze kuendana na kasi ya Serikali hii sasa hivi kasi yetu sio ya kutembea bali ni kukimbia na lazima wote twenda pamoja”.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Joseph kakunda(kushoto) akisaini kitabu mara baada ya kufika Ofisini ‘Ofisi ya Rais –TAMISEMI’ mjini Dodoma

  Aliongeza kuwa nahitaji  “Consistency of information” kutoka kwa watalaam wanaofahamu vizuri maeneo yao ya kazi sio kila siku unahamisha unaanza na mtu mpya naye anakuwa hana taarifa za kutosha kuhusu kazi za awali hivyo inachukua muda kuanza kwenda sawa kwangu mimi nasema ntamnyoosha yeyote ambaye haendani na viwango vyangu akiwa hapa hapa na si kwingineko”. 

  Aidha Waziri Jaffo aliwata  Watumishi wote kuacha kufanya kazi kwa ulegevu na kuwa makini wakati wote wa kazi kwani ndio inayopeleka  kupata ujira wako, kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kutoa huduma bora kwa wananchi,  kutokujali muda hivyo kutumia muda mrefu kukamilisha jukumu ulilopewa ama kutorudisha mrejesho wa kazi na  kutojali utu wa watu wengine.

  “Nataka nione kila mtumishi yuko “busy for something” ili tuweze kuwasaidia Wananchi wetu, na katika hili tutapimana mmoja mmoja katika eneo lake amefanya nini kwa siku, wiki, mwezi mpaka mwaka na yeye mwenyewe atusaidie kujitathmini kuona kama ana umuhimu wowote katika eneo lak ama Lah”
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege akisaini kitabu mara baada ya kufika Ofisini, ‘Ofisi ya Rais –TAMISEMI, mjini Dodoma.

  Wizara hii ni Injini ya mabadiliko katika Nchi yetu hivyo sisi lazima tuwe Wizara bora inayofanya kazi zitakazoleta chachu ya Maendeleo kwa mwanancHi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla, hivyo nitasughulika na watumishi wote mpaka nione mnaendenda kadiri ya kasi ninayoitaka ili mabadiliko chanya yaweze kutokea alisema waziri Jafo.

  “Sitaki kuona mtu anashinda Ofisini Wizara hii ni watekelezaji wa Sera mbalimbali na Sera hizo zinatekelezwa kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa nataka niwaone mkienda kufuatilia utekelezaji na kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa viwango na wananchi wanapata stahiki yao ya huduma bora toka kwenye mamlaka za serikali za mitaa zilizoko kwenye maeneo hayo na sio kushinda Ofisini” Aliongeza Mhe. Jafo.

  Akizungumza wakati wa kikao hicho Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda amesema ninachohitaji toka kwa watumishi wa OR-TAMISEMI tufanye kazi na tuipende Kazi na kwa pamoja tuweze kuisimamia bajeti ya Serikali ambapo Wizara hii tunapata asilimia 20.7 ya bajeti nzima ya Taifa letu ni lazima tuitendee haki kwa sababu Fedha zinakuja kwetu ni nyingi  hii inaonyesha umuhimu wa Wizara hii kwa maendeleo ya taifa.

  Amesisitiza mambo matatu anayoyahitaji toka kwa watumishi kuwa ni “clarity” kuwa na uwezo mkubwa wa kuelewa Majukumu, Sera, Sheria, Program, Miongozo na kanuni mbalimbali sambamba na mazingira wezeshi yatakayomuweza mtumishi kufanya kazi ambayo haya yatatengenezwa na mwajiri pamoja kuwa uwezo wa kufanya kazi ulizopangiwa bila kusimamiwa  “competency”.

  Naye naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Joseph Sinkamba kandege ninachohitaji zaidi toka kwenu ni ushirikiano kwa sababu hata kama mtu anaweza kiasi gani lazima  anahitaji msaada wa mwingine ili aweze kukamilisha kazi yake vizuri hakuna nayeweza peke yake hizi kazi tunategemeana na zaidi ya hapo nahitaji watu wakweli na waaminifu ili tuweze kufikia malengo ya pamoja.

  Kikao hiki na watumishi wa TAMISEMI ni cha pili tangu kuapishwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo pamoja na Manaibu Waziri wake Mhe. Mhe. Joseph Sinkamba kandege pamoja na Mhe. George Joseph Kakunda.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (katikati) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara hiyo, kulia ni Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege pamoja na Naibu Waziri Mhe. George Joseph Kakunda.
  Watumishi wa OR-TAMISEMI wakifuatilia kikao na Waziri pamoja na Naibu Mawaziri (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za TAMISEMI –mjini Dodoma.
  Katika picha ya pamoja ni viongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI (katikati) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo kushoto akifuatiwa na Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege (Afya,Miundombinu,Viwanda na Uwekezaji, na Serikali za Mitaa), Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Musa Iyombe, Naibu Katibu Mkuu (Afya) Zainab Chaula na kulia ni Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. George Joseph Kandege (Elimu, Maji, Kilimo, Mifugo na Maliasili), Naibu Katibu Mkuu –Elimu Tixon Nzunda (Elimu) pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi ya Walimu Tanzania (TSC) Winfrida G.Rutaindurwa.

  0 0

  Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 na Kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya mwaka 2011, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, amefuta uteuzi wa MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NYUMBA NDUGU MOHAMMED HAFIDH RAJAB kuanzia leo tarehe 12 Oktoba, 2017.

  Taarifa hii ni kwa mujibu wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.

  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO
  ZANZIBAR
  12 OKTOBA, 2017

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wake wa kiuchumi na kidiplomasia baina yake na Uganda. Amesema Tanzania na Uganda zinauhusiano wa muda mrefu na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inafarijika na ushirikiano huo.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Oktoba 12, 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Bw. Richard Kaonero jijini Dar es Salaam.

  “Tunaimani kubwa na ushirikiano wetu na Serikali ya Uganda. Tutaendelea kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo tunayoitekeleza kwa pamoja ukiwemo ujenzi wa bomba la gesi.”

  Hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Uganda ili waje kuwekeza kwenye viwanda mbalimbali vikiwemo  vya kuchakata mazao ya  kilimo. Pia amewakaribisha raia wa Uganda kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko nchini Tanzania kama mlima wa Kilimanjaro, fukwe, mali kale na mbuga za wanyama.

  Kwa upande wake, Balozi Kaonero  ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na dhamira ya dhati ya kuimarisha uchumi wake kupitia sekta ya viwanda. Pia Balozi huyo ameiomba Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuanzisha safari ya kwenda Entebe nchini Uganda ili kuimarisha usafiri kati ya nchi hizo mbili.

  Akizungumzia kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, Balozi Kaonero amesema Serikali ya Uganda na Tanzania zinaundugu wa damu na kwamba wataendelea kuudumisha.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Uganda nchini Tanzania Bw. Richard Tumusiime Kaonero, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Oktoba 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0


  Mteja wa benki ya TIB, Irene Kiwia  pamoja na wateja wengine wakishirikiana kukata keki kwaajili ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba.


  BENKI ya biashara  inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania Investment Bank (TIB) inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kibenki zenye ubunifu wa hali ya juu ili kufikia dira ya kuwa benki  ambayo ni chaguo la wateja.

  Hayo yamesemwa ka Mkurugenzi mtendaji wa benki ya TIB, Frank Nyabundege wakati akizungumza na wateja wa benki ya TIB waliofika katika tawi la Samora jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa benki hiyo inatoa huduma za TIB mobile, Utoaji wa bure wa dhamana za kibenki, sms alert, Premier banking, uboreshaji wa kazi za ATM, kutua huduma masaa 24 ya katika tawi la bandari, huduma za malipo ya kodo kirahisi pamoja na JIPANGE Plan.

  Amesema kuwa "Huu ni mwaka ni waka wetu wa pili tangia kupata kibali cha kutoa huduma za kibenki na kuendelea kujenga uwezo wa kuwapa wateja huduma za kipekee."

  Amesema kuwa hudum nzuri kwa wateja ndio kipaumbele katika maendeleo ya benki hiyo.
  Mteja wa benki ya TIB, Irene Kiwia akizungumza na Michuzi TV jijini Dar es Salaam leo wakati alipofika katika benki ya TIB jijini Dar es Salaam wakati wa kuwashukuru wateja wa benki hiyo.
  Mkuu wa masoko na mahusiano wa Benki ya TIB, Theresia Soka akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa benki ya TIB waliofika katika benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. 
  Amewashukuru  wateja wa benki hiyo kufka katika taw la Samora kwaajili ya kusheherekea pamoja wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kuwaomba kutoa maoni yao ili kwenye mapungufu wajirekebisha.
  Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa benki ya TIB wakiwa katika hafla fupi ya kuwashukuru wateja wao katika wiki ya huduma kwa wateja.

  0 0

  Na.Paschal Dotto-MAELEZO

  Mama Maria Nyerere amewaasa vijana kuzingatia utamaduni na michezo ili kuweka sawa akili yao na kuendelea na ujenzi wa taifa kwani michezo hukutanisha watu wengi na kuwawezesha kubadilishana mawazo yenye kujenga katika maisha.

  Akizungumza leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam, Mama Maria Nyerere alisema kuwa michezo ni hatua muhimu ya ukombozi wa fikra kwa vijana kwani wakizingatia michezo wataweza kufanya kazi na kujipatia mahitaji muhumi kama chakula na kuondokana na dhana ya utegemezi.

  “Vijana wamajikita katika mambo maovu, sasa kitakachoweza kusaidia ni michezo kwani inawachangamsha, kuwakutanisha na kuweza kubadilishana mawazo mazuri na kwa sasa wanaendelea vyema na masuala haya ya michezo ambayo yanadumisha pia utamaduni,” alisema Mama Maria

  Aidha, Mjane wa Hayati Baba wa Taifa alisema kuwa kwa sasa vijana wameanza kujirudi katika kudumisha utamaduni kwani walitaka kupotoka na kuacha utamaduni wao, alieleza kuwa watoto wanazaliwa bila ukomavu wa akili katika utamaduni, lakini pia hawapati elimu ya kutosha kutoka kwa wazazi kuhusu utamaduni matokeo yake ni kuishia kuwa na watu wenye tabia za ajabu.

  “Kitakachoweza kuwasaidia vijana wetu ni kuwafundisha utamaduni wetu ili wawe na maadili kwani sasa hivi mtoto anazaliwa hapati elimu ya utamaduni wake, wazazi wametupa utamaduni mbali, ni lazima mtoto atakuwa na tabia za ajabu ajabu,”alisisitiza Mama Maria Nyerere.

  Aliongeza kuwa jukumu la ukombozi wa vijana kutoka katika vitendo vibovu ni la watanzania wote kuweza kuwaelimisha vijana kuhusu michezo ili kuweka akili zao sawa katika kuzalisha na kusaidia kujipatia kipato chao na taifa kwa ujumla.

  Mama Maria Nyerere alisema kuwa kujitegemea kwa vijana hasa katika kufanya kazi kutawawezesha kutimiza ndoto zao na za taifa lenye uchumi wa viwanda kwa ujumla.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO ) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abassi akisikiliza jambo kutoka kwa Mama Maria Nyerere kuelekea kumbukizi ya miaka 18 ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa mahojiano maalum na Mjane huyo nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO ) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abassi akifanya mahojiano na Mama Maria Nyerere kuelekea kumbikizi ya Baba wa Taifa , Mjane huyo aliwasisitiza vijana kuzingatia michezo na utamaduni.Picha na Paschal Dotto- MAELEZO

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Makamishna na Wakuu wa Vitengo vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Masauni alilitaka Jeshi hilo kutoa elimu zaidi kwa umma pamoja na kuongeza kasi ya ufunguaji wa vituo vya zimamoto katika wilaya zote nchini. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, (CGF), Thobias Andengenye, na kulia ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, Michael Shija.

  Na Felix Mwagara (MOHA) 

  NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelitaka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuongeza kasi kufungua vituo vya zimamoto katika wilaya zote nchini pamoja na kutoa elimu kwa umma juu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto.

   Akizungumza na Makamishna na Wakuu wa Vitengo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, Masauni alisema Serikali ya Awamu ya Tano kusudio lake ni kuipeleka nchi katika uchumi wa kati na viwanda hivyo ili maendeleo yapatikane lazima Jeshi hilo lijiimarishe zaidi. “Akikisheni mna peleka maafisa wa zimamoto katika wilaya zote nchini ili wakaweze kutoa elimu kwa umma jinsi ya kuzima moto, kwasababu kinga ni bora kuliko tiba,” alisema Masauni. 

  Aidha, Masauni alisema zipo changamoto kadhaa zinazolikabili Jeshi hilo, ikiwemo magari ya kuzimia moto hayatoshi, vifaa vya mahokozi pamoja na ukosefu wa madawa ya kuzimia moto, lakini Serikali itajitahidi kuzitatua kadiri ya uwezo wake. 

  Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye, alisema amepokea maelekezo hayo kutoka kwa Naibu Waziri, na kumuhakikishia kuwa, Jeshi lake linaona ukuaji wa kasi wa viwanda nchini kunahitaji sana huduma zitolewazo na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. “Tunashukuru kwa ujio wako, maelekezo uliotupa tumeyapokea, tunakuhakikishia kujipanga zaidi katika kuongeza nguvu zaidi katika kukabiliana na majanga ya moto,” alisema Andengenye. 

  Hata hivyo, Andengenye aliiomba Serikali kuiongezean uwezo zaidi Jeshi hilo na kuipatia vitendea kazi vya kisasa pamoja na kuongeza rasilimali watu ili kuipa nguvu zaidi Jeshi hilo katika kutekeleza majukumu yake. Masauni alifanya ziara hiyo ya siku moja kwa lengo la kuzungumza na viongozi wa Jeshi hilo kuhusiana na mipango ya mbalimbali ya Serikali na Jeshi hilo kuhusu kukabiliana na majanga ya moto nchini.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF), Thobias Andengenye akitoa taarifa yake utendaji kazi wa Jeshi lake kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati meza kuu), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mchumi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Boniface Mkumbo alipokua anafafanua mipango mbalimbali ya kuliendeleza jeshi hilo. Kulia kwa Naibu Waziri ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, (CGF), Thobias Andengenye. Katika hotuba yake kwa viongozi wa Jeshi hilo, Masauni alilitaka Jeshi hilo kutoa elimu zaidi kwa umma pamoja na kuongeza kasi ya ufunguaji wa vituo vya zimamoto katika wilaya zote nchini.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Makamishna na Wakuu wa Vitengo vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Masauni alilitaka Jeshi hilo kutoa elimu zaidi kwa umma pamoja na kuongeza kasi ya ufunguaji wa vituo vya zimamoto katika wilaya zote nchini. Kulia kwa Naibu Waziri ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, (CGF), Thobias Andengenye. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Serikali  imesema kuwa itahakikisha rasilimali za bahari zinatumika kwa ajili ya watanzania Wote

  Hayo aliyasema Waziri, Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Ahmad Rashid alipofanya ziara ya ukaguzi wa  meli ya  uvuvi  katika bandari ya Zanzibar mapema leo.

  Rashid amesema  kuwa rasilimali za baharini zikitumika  ipasavyo zinaweza kuleta maendeleo na kuhakikisha uvuvi unaofanyika katika bahari unafuata taratibu  kwa masilahi ya taifa .

  Katika ukaguzi  huo wa meli hiyo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Ahmad Rashid pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo, Abdallah Ulega wametembelea ofisi za utoaji leseni wa meli za uvuvi  ya  serikali ya mapinduzi Zanzibar .

  Amesema sheria iko wazi  kwa hivyo  lazima rasilimali za Tanzania  ikiwemo na bahari iwanufaishe watanzania  wote bila kujali vyama vyao.

  Nae Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvia, Abdallah Ulega amesema  serikali zote mbili zitahakikisha rasilimali za bahari  zinatumiwa na watanzania na sio kwa wageni tu. Amesema watasimamia sheria za uvuvi katika kulinda rasilimali za bahari ili ziweze kuleta maendeleo kwa watanzania.

  Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Zanzibar, Hosea Mbilinyi  amesema  mamlaka imepiga hatua katika  kuhakisha rasilimali za bahari zinanufaisha Tanzania
   Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzabar, Ahmad Rashid akizungumza katika ukaguzi wa Meli ya Uvuvi ya China katika bandari ya Zanzibar.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza baada ya ukaguzi wa meli ya uvuvi wa China katika Bandari ya Zanzibar ili kujionea shughuli za uvuvi katika eneo hilo.
   Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzabar, Ahmad Rashid(kulia) na  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega(kushoto) wakiwa wameshika Samaki ambaye amevuliwa na Meli ya Uvuvi yaa China katika Bandari za Zanzibar .
   Wavuvi wakiendelea na kazi.
  Muonekano wa Meli ya Uvuvi ya China katika bandari ya Zanzibar. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

  0 0


  Na Zuena Msuya, Manyara

  Wizara ya Madini kwa mara ya kwanza itafanya mnada wa madini ya Tanzanite kutoka katika Kampuni nne za uchimbaji na biashara ya madini katika eneo la Mirelani wilayani Simanjiro mkoani Manyara,Mnada huo utafayika tarehe 15, Octoba mwaka huu mkoani Manyara.

  Akizungumza mkoani Manyara, Kaimu Kamishna Msaidizi sehemu ya Uchumi na Biashara ya Madini, Godleader Shoo alisema kuwa utaratibu wa kufanya mnada wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje nchi na pia kuwasaidia wachimbaji kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia.

  Shoo alifafanua kuwa mnada huo utashirikisha wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo atakayefanikiwa kununua madini hayo katika mnada huo ni yule tu atakayeshinda bei iliyowekwa kwa ajili ya kununua madini husika.Alitaja kampuni zitakazouza madini katika mnada huo kuwa ni Kampuni ya uchimbaji madini ya TanzaniteOne, Franone, Glitter Germs pamoja na Classic Gems ambazo zitazouza madini ghafi na yale yaliyokatwa.

  Akizungumzia mnada huo, Shoo alisema zoezi hilo linafanyika kwa njia ya uwazi kwa kushirikisha wachimbaji, wanunuzi, Shirika la Madini la Taifa( STAMICO), Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro pamoja na Wizara ya Madini, ili kuhakikisha kuwa wauzaji na wanunuzi wa madini hayo wanapata kile wanachostahili.

  ” Mnada huu utaendeshwa kwa usalama mkubwa kwani Madini ya Tanzanite yana thamani kubwa. Serikali imeimarisha ulinzi wakati wa zoezi hili ili kujihadhari na watu wasio waaminifu,” alisema Shoo.Aidha mnada huo utaiwezesha Serikali kupata mrabaha stahiki na kodi nyingine za serikali kwa uwazi ili kuchangia pato la taifa; vilevile kuimarisha ulinzi na usalama kwa wauzaji , wanunuzi pamoja na mali zao.

  Alisema kuwa minada kama hiyo pia hufanyika kwa nchi za Afrika zenye madini ya Vito kama vile Zambia( emerald), Zimbabwe ( Almasi) pamoja na Afrika kusini ( Almasi).Washindi wa zabuni za ununuzi wa madini ya Tanzanite wanatarajiwa kutangazwa Octoba 15 mwaka huu mkoani Manyara.
  Madini ya Tanzanite yakipimwa kabla ya kuanza kufanyiwa mnada.
  Vifaa maalum( drum) vilivyohifadhia madini ya Tanzanite.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa , John Nayopa ( aliyesimama)akifatilia zoezi la uthaminishaji, uchambuzi,na ukokotoaji wa mrabaha wa madini yaliyoletwa kwa ajili ya mnada, linalofanywa na watendaji wa Wizara ya Madini.
  Vikosi vya ulinzi na usalama, pamoja na watendaji wa Wizara ya Madini wakihakikisha usalama wa Madini ya Tanzanite yaliyohifadhiwa katika vifaa maalum.
  Usajili wa washiriki wa mnada wa madini ya Tanzanite ukiendelea mkoani Manyara.


  0 0

  Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao(katikati) akikabidhiwa na Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Aggrey & Clifford,Rashid Tenga,Tuzo ya kimataifa ya dhahabu kutoka Spike Asia Festival of Creativity 2017 nchini Singapore iliyotokana na tangazo lililotengenezwa na kampuni hiyo kwa niaba ya Vodacom kuhusiana na kampeni ya kuuza sehemu ya hisa za kampuni hiyo kwa Umma,Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam,Anaeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(kushoto)na Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Aggrey & Clifford,Rashid Tenga,wakimshuhudia Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao,akiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani) Tuzo ya kimataifa ya dhahabu kutoka Spike Asia Festival of Creativity 2017 nchini Singapore iliyotokana na tangazo lililotengenezwa na kampuni ya Aggrey & Clifford kwa niaba ya kampuni hiyo kuhusiana na kampeni ya kuuza sehemu ya hisa za kampuni hiyo kwa Umma,Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo,Ian Ferrao,wakimsikiliza kwa makini Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Aggrey & Clifford,Rashid Tenga,alipokuwa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo ya kimataifa ya dhahabu kutoka Spike Asia Festival of Creativity 2017 nchini Singapore iliyotokana na tangazo lililotengenezwa na kampuni ya Aggrey & Clifford kwa niaba ya Vodacom kuhusiana na kampeni ya kuuza sehemu ya hisa za kampuni hiyo kwa Umma,Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kulia), akimsikiliza kamishna wa Polisi wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi (CP) Alice Mapunda, alipokagua Kamisheni hiyo kwa lengo la kuona namna wanavyofanyakazi pamoja na changamoto wanazokutananazo wakati wanapotekeleza majukumu yao.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia), akiangalia moja kati ya sampuli zinazofanyiwa Uchunguzi wa Kisayansi katika Maabara ya Polisi Makao Makuu, alipofanya ukaguzi kwenye kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi kwa lengo la kuona namna wanavyofanyakazi pamoja na changamoto wanazokutananazo wakati wanapotekeleza majukumu yao.

  Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0

  Si kwa idadi hii ya watu iliyofurika katika Wilaya ya Karatu Kata ya Rhotia ambako Usajili wa Wananchi Vitambulisho vya Taifa unaendelea.

  Kwa mujibu wa Afisa Usajili Wilaya ya Karatu Bi. Rehema Ngomuo takribani wananchi 1200 wamekuwa wakisajiliwa kwa siku na wengine kushindwa kuwasajili na kulazimika kurejea makwao tayari kwa siku inayofuata bila manung’uniko wala ulalamishi; kutokana na umati mkubwa wa wananchi kufurika kwenye vituo vya Usajili kupata huduma hiyo.

  Diwani wa Kata hiyo Bwana Marseli Roli (CCM) ambaye muda wote amekuwepo kituoni hapo kuhakikisha wananchi wake wote wanasajiliwa kwa kuzingatia utaratibu uliopangwa amesema imekuwa ni kawaida ya wananchi katika Kata yake kuitikia wito haraka haswa katika masuala ambayo yana manufaa ya moja kwa moja na maisha yao ya kila siku.

  “ Hili suala la Vitambulisho ni suala muhimu na kila mmoja anatambua umuhimu wake na ndiyo maana hatukupata shida ya kuwahamasisha wananchi kufika kusajiliwa kwa kuwa kila mmoja anatambua thamani ya kuwa nacho. Wengine hapa kama unavyowaona wamefika tangu saa 11 alfajiri” alisema

  Kwa Wilaya ya Karatu Kata ambazo zinashiriki zoezi hili kwa sasa ni Kata ya Rhotia ambayo baada ya siku saba itafuatiwa na Kata za Janakona na Karatu. Wilaya zingine za mkoa wa Arusha zinaendelea na Usajili zikiwemo Arusha, Arumeru, Longido na Loliondo huku Ngorongoro wakiwa tayari kuanza Jumamosi hii.

  Umati wa Watu uliofurika kupata huduma ya Usajili Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi hilo likiendelea katika Kata ya Rhotia. Hawa ni akinamama wajawazito na wenye watoto wachanga wakipatiwa huduma maalumu kwa utaratibu maalumu uliowekwa wa kusaidia wazee, wajawazito na wamama wenye watoto wachanga.
  Afisa Usajili Wilaya ya Karatu Bwana STEVE MBALA akiendelea na taratibu za kuthibitisha uraia wa waombaji na kugonga muhuri wakati zoezi hili likiendelea. utaratibu huu umekuwa ukifanyika kabla ya mwananchi kuruhusiwa kupiga picha, kuchukuliwa alama za vidole na saini ya kielektroniki.
  Foleni hii ni ya Watendaji Kata na Wenyeviti katika Vijiji vya Kata ya Rhotia wakithibitisha makazi ya kila mwananchi anayeishi katika Kata na Kijiji chake kabla ya kutoa idhini ya kuthibitishwa uraia.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa kwa furaha na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari wa ziara ya siku tatu visiwani humo ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere..
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Magharibi Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama janet Magufulki wakisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere.


  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Her Initiative,Lydia Charles akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kawe wakati  wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani kwa kutoa elimu ya afya ya Uzazi na kuwapima afya wanafunzi wa kike wa shule hiyo .
   Mmoja watangazaji wa kipindi cha Mitindo cha Clouds Televisheni akiwa na mmoja wanafunzi wa shule ya Sekondari kawe wakati alipokuwa akitoa somo la afya ya uzazi kwa wanafunzi hao  kupitia programu ya Her Initiative.
   Mtangazaji wa kipindi cha Clouds E, Saida Khalifani(Shadey) akizungumza na wanfunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Kawe juu ya hatua muhimu za kupitia kufikia ndoto zao wakati wa tasisi ya Her Initiative ilipokwenda shuleni hapo katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani.


  0 0


  Aliyasema hayo leo katika kikao cha pamoja baina yake na uongozi wa shirika hilo wakiwemo wadau ambapo alisema watahakikisha wanawahudumia wateja kwa wakati ikiwemo uhakika wa vifaa vyenye bora ili kuwawezesha wananchi kupatiwa umeme kwa haraka zaidi .

  Licha ya hivyo lakini pia Waziri huyo alitilia mkazo suala la madeni yote ya bili za umeme kulipwa kwa wakati kwenye shirika hilo ili kuweza kuwezesha ufanisi mkubwa katika utendaji wa kazi .

  Akizungumza na wazabuni mbalimbali wa miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo,nyaya na mita,Waziri Kaleman alisema kuanzia sasa vifaa vya umeme vitanunuliwa ndani ya nchi kwani kufanya hivyo itapunguza gharama kubwa na kasi ya kuwahudumia wateja."Kwani kufanya hivyo vifaa hivyo vitakuwa karibu kupatikana ndani ya nchi na kutaongeza mapato ndani ya nchi na uzalendo "Alisema.

  Hata hivyo alilipongeza shirika la Umeme nchini Tanesco kwa kufanya kazi kwa bidii na kutoa taarifa kwa wateja juu ya huduma mbalimbali ikiwemo kuwataka kuwajibika kwa kufanya kazi kwa waledi mkubwa.
  WAZIRI wa Nishati,Dkt Medard Kalemani akizungumza na uongozi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco na wadau wa mbalimbali wa umeme ili kuweza kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa uhakika ikiwemo kuwahudumia wateja kwa wakati na kuwepo kwa uhakika wa vifaa vyenye ubora ili kuwezesha 
  Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza katika kikao hicho 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo akiongea katika kikao hicho kushoto ni WAZIRI wa Nishati,Dkt Medard Kalemani 
  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kaleman akiambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Subira Mgalu wamefanya kikao na uongozi wa shirika la Umeme nchini (Tanesco) na wadau mbalimbali wa umeme ili kuweza kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha nishati ya umeme wa uhakika unapatikana.


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi sare za shule kwa wanafunzi 121 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kizumbi na Kitangili katika manispaa ya Shinyanga.

  Zoezi la kukabidhi sare hizo za shule limefanyika leo Alhamis Oktoba 12,2017 katika shule ya msingi Kitangiri.Msaada huo wa sare za shule unatokana na kampeni iliyoanzishwa na mkuu huyo wa wilaya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika wilaya ya Shinyanga.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi sare hizo,Matiro alisema pamoja na serikali kuwa na sera ya elimu bure lakini wamebaini kuwa kuna watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu hivyo wanahitaji msaada kutoka wadau mbalimbali.

  “Tulifanya zoezi la kugawa sare kwa wanafunzi wengine hivi karibuni,na leo ofisi yangu kwa kushirikiana na wadau wengine likiwemo shirika la wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO) nimekuja kukabidhi sare za shule kwa wanafunzi 121 wa kata ya Kitangili na Kizumbi”,alieleza Matiro.Matiro aliwataka wazazi kutimiza wajibu wao wa kulea watoto badala ya kuwatekeleza kwa bibi na babu zao na wao kukimbilia mjini huku watoto wakiteseka na kuishi katika maisha magumu.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza kabla ya kuanza kugawa sare za shule kwa wanafunzi 121 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kizumbi na Kitangili leo katika shule ya msingi Kitangili mjini Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Mratibu wa miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO),Venny Raymond akielezea namna walivyowapata watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kitangili na Kizumbi
  Afisa Elimu kata ya Kitangili Mahmood Ibrahim akizungumza wakati wa zoezi la kugawa sare hizo za shule


  0 0


  Na Thobias Robert

  Naibu Waziri wa Ujenzi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kwandikwa ameitaka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kukusanya na kutumia madeni zaidi ya bilioni 10, inayozidai taasisi, idara na wakala mbalimbali wa sekta za umma na binafsi ili watumie pesa hizo katika shughuli za uzalishaji na maendeleo.

  Waziri ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi kuongea na kuangalia utendaji kazi wa wafanyakazi pamoja na kukagua mitambo inayotumiwa na wakala hiyo iliyo chini ya wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.

  “Madeni ni rasilimali ambayo tunahitaji kuisimamia vyema, chambueni vizuri madeni ambayo taasisi inadai kwenye taasisi, idara na wakala mbalimbali za serikali ili tuweze kuona namna gani tutafanya ili madeni hayo yalipwe, kwa sababu tukikaa na madeni mengi yatatukwamisha katika shughuli zetu,” alisisitiza Waziri Kwandikwa.

  Aidha alisema kuwa wakala na idara zinazofanya kazi na TEMESA zinapaswa kulipa madeni wanayodaiwa ili kuiwezesha taasisi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa kutumia vifaa na miundombinu ya kisasa inayoandana na utoaji wa huduma unaofanya na TEMESA.

  “Nitoe wito kwa taasisi mbalimbali zinazodaiwa na TEMESA ziweze kulipa haraka hayo madeni ili tuweze kufanya kazi vizuri zaidi, maana wangekuwa wanakwenda kwenye kampuni binafsi kama wanadaiwa basi magari yao yangekuwa yanakamatwa, sasa isije tukafika wakati na sisi kuanza kampeni ya kuzuia magari, kwa sababu lazima TEMESA isimame ili tuweze kutoa huduma vizuri,” aliongeza Waziri Kwandikwa.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa (kulia) akipata maelekezo toka kwa Meneja Msaidizi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Peter Bongele (katikati) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Joseph Nyamuhanga.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Joseph Nyamuhanga (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa (katikati) kuzungumza na watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mussa Ngwatu.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa (katikati) akizungumza na watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Joseph Nyamuhanga na kulia ni Mtendaji.Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mussa Ngwatu.
  Baadhi ya watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Vijijini kutoka vilabu mbalimbali vya waandishi wa habari hapa Nchini,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari hapa Nchini(UTPC),chini ya ufadhili wa SIDA yaliyofanyika leo Mkoani Morogoro.(Habari Picha na Pamela Mollel).
  Mwenyekiti wa Morogoro Press Club Nikson Mkilanya ambae alikuwa mgeni rasmi katika kufunga mafunzo hayo,akisisitiza washiriki wa mafunzo hayo kutumia vyema fursa hiyo waliyoipata katika kuibua changamoto mbalimbali za vijijini.
  Mkufunzi wa Mafunzo ya uwandishi wa habari za vijijini Joe Nakajumo akizungumza na baadhi ya wanahabari walioshiri mafunzo hayo leo Mjini Morogoro.
  Mshiriki wa mafunzo Edith Karlo kutoka Kigoma PressClub kikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nekson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo oleo.

  Mshiriki wa mafunzo Pamela Mollel kutoka Arusha Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.


  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  0 0

  WASANII walioalikwa kukaganya zulia jekundu kwenye uzinduzi wa filamu ya 'Mammu' ya msanii Rakheem David 'Kuchie' tayari wameufanya uzinduzi huo kuwa wa ainayake kutokana na kuzungumzia sana katika mitandao kupitia akaunti zao za Facebook, Twitter na istagram. 
  Mmoja ya wasanii waalikwa katika uzinduzi huo,Gabo Zigamba ameweza kupata 'like 'nyingi zinazoonyesha kuwa mwamko wa ujio wa uzinduzi huo ni mkubwa malala baada ya kuweka kava la filamu ya 'Mammu ' katika akaunti yake ya Istagram. 
  "Mambo yanaonekana kwenda vema kwani mashabiki wangu wanaisubiria siku ya uzinduzi wangu wa filamu kwa hamu kubwa,"alisema Rakheem. 
  Alisema uzinduzi nduzi huo utafanyika Otoba 13 katika ukumbi maarufu wa King Hotel iliyopo Sinza maeneo ya Africasana jijini Dar es Salaam na shughuli za uzinduzi zitaanza kuanzia saa 01:00 usiku. 
  Rakheem Aliwataja wasanii wengine waalikwa licha Gabo kuwa ni Mzee Chilo na mama Monalisa 'Natasha Huba'.
  Nyota huyo ambaye tayari ni mwenye umaarufu awali amewahi kufanya vema katika filamu kama iliyoitwa kibajaj iliyoshirikisha nyota wengine kama Mboto, Irene Poul pamoja na nyingine iliyoitwa 'Mama Ntilie 'iliyoshirikisha nyota kama Gabon king Majuto pamoja na Irene. 
  Rakheem  kwa hivi sasa anafanya kweli katika tamthiliya ya Duty inayooneshwa kupitia Star Tv kila siku za jumatano saa 01:00 usiku. 
   Sehemu ya scene za kusisimu katika filamu ya 'Mammu' ya msanii Rakheem David 'Kuchie  0 0

older | 1 | .... | 1958 | 1959 | (Page 1960) | 1961 | 1962 | .... | 3278 | newer