Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1957 | 1958 | (Page 1959) | 1960 | 1961 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Asasi za kiraia na wadau wa elimu pamoja na Afya wameiomba serikali kutatua changamoto za watoto wa kike zinazofanya washindwe kutimiza ndoto mbalimbali ikiwemo ndoa za utotoni zinazotokana na mila potofu zinazoendelea katika jamii.

  Akizungumza na waandishi habari wakati akimkabidhi mapendekezo ya wadau kwa  Afisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Dora Meena,Meneja wa Miradi ya Utetezi na Sera wa Taasisi ya Healthy Promotion (HDT), Gresmo Mutashobya amesema kuwa wasichana wenye umri kati 10 hadi 19 takribani ya milioni 600 duniani , Tanzania takribani ya asiliamia 18 ya ripoti ya 2016 inaonesha kuwa idadi ya udahili kwa watoto wa kike kwa shule za msingi ilizidi kwa wavulana kwa asilmia 0.1 na udahili wa shule za sekondari ilizidi kwa asilimia 6.1.

  Amesema miaka 10 iliyopita wasichana 550,000 walikatishwa masomo baada ya kupata ujauzito hali iliyosababisha watoto wengine kuathrika katika maisha yao yote kutokana na kukosa elimu.

  Mutashobya ameiomba Serikali kutengeneze mazingira ya usawa ambayo yatahamasisha elimu kwa mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na kuondoa vizuizi katika elimu kwa mtoto wa kike pamoja na kufanya mapitio ya sheria na sera, ili kufanya mabadiliko ya sera na sheria zinazopalilia mila potofu, unyanyasaji na ndoa za utotoni kwa ubadilishaji wa sheria ya ndoa ya mwaka 1977 za mtoto wa kike kuolewa miaka 14.

  Amesema changamoto zingine kwa wazazi wanatakiwa kuzingatia malezi ya watoto wa kike kuwa mstari wa mbele kuondoa dhana ya upendeleo wa kijinsia, pamoja na kuwatia moyo watoto wa kike kuwa wavumilivu kutoingia katika mahusiano ya kimapenzi kabla ya wakati.
  .Meneja wa Miradi ya Utetezi na Sera wa Taasisi ya Healthy Promotion (HDT), Gresmo Mutashobya akizungumza juu ya asasi za kiraia zinavyofanya kazi katika kufanya utetezi kwa mtoto wa kike ili aweze kufikia ndoto zake katika kilele cha Maadhimisho ya Mtoto wa Kike ambayo hufanyika Oktoba 10 kila mwaka, iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
  Afisa wa Vijana Ofisi Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Dora Meena akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Mtoto wa Kike iliyofanyika jana  jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Miradi ya Utetezi na Sera wa Taasisi ya Healthy Promotion (HDT), Gresmo Mutashobya akimkabidhi mapendekezo ya asasi za kiraia juu changamoto za mtoto, Afisa wa Vijana Ofisi Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Dora Meena katika kilele cha Maadhimisho ya Mtoto wa Kike ambayo hufanyika Oktoba 10 kila mwaka, iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wanaasasi na waandishi wakisikiliza taarifa ya kilele cha maadhimisho ya siku mtoto wa kike Duniani.
  Mbunge wa Afrika Mashariki Mhandisi Pamela Massay akizungumza katika maadhimisho ya siku Mtoto wa kike iliyofanyika jana  jijini Dar es Salaam.
  Wanaasasi wakiwa na wameshika ujumbe mbalimbali wa watoto wa kike kuweza kufikia ndoto zao.

  0 0

  Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi, Mh. Abdalah Hamisi Ulega ameitaka Halmashauri ya wilaya Mkuranga kushirikiana na wananchi kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili kupunguza migorogoro ya wakulima na wafugaji.

  Akizungumza na watendaji wa Halmashauri pamoja na kamati ya ulinzi na usalama katika ziara yake ya wilayani Mkuranga mkoani Pwani alisema tatizo la wakulima na wafugaji ni changamoto kubwa kwahiyo ni muhimu kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili wasizagae hovyo.

  Ametaka maafisa mifugo wasikae maofisini bali waende kutoa huduma vijijini na kuwasiliza wananchi kero zao.Ulega amesema vikundi vya wafugaji wakina mama na vijana vipewe kipaumbele, vitambuliwe na kudhaminiwa kwenye utoaji mikopo kwa ajili ya kuinua kipato na kuongeza pato la taifa na la mtu mmoja mmoja

  "Tunahitajika tutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji, na hii ni changamoto tunayotakiwa kuifanyia kazi hatupaswi kuwaacha wafugaji wakihamahama" amesema Ulega. 

  Aidha alisema kuwa Halmashauri inatakiwa kufanya utafiti na kupima ardhi ambayo watawatengenezea miundombinu bora kwa ajili ya wafugaji. Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mkuranga, Filiberto Sanga alisema kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ardhi, wananchi wanauza ardhi kiholela kiasi kwamba wanakosa maeneo ya kilimo hivyo amewataka wananchi kutouza ardhi hovyo. 

  Sanga alisema kuwa agizo la naibu waziri wamelipokea japokuwa wanauhaba wa ardhi lakini wameanisha baadhi ya maeneo yaliyopo tarafa ya Mkamba ambayo watayafanyia utafiti kwa ajili ya wafugaji. 
  Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega akizungumza na watendaji wa Halmashauri pamoja na kamati ya ulinzi na usalama kuhusu kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili kupunguza migorogoro ya wakulima na wafugaji mkoani Pwani.
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, filiberto Sanga akizungumza katika mkutano huo amewataka wananchi kutouza ardhi hovyo ili kupunguza migogoro ya ardhi pamoja na kuwa na maeneo ya kilimo. 
  Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akizungumza na viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi alipokutana nao na kufanya mazungumzo kuhusu usawa na wajibu wa kila mtu ili kufikia malengo ya taifa kiujumla mkoani Pwani.
  Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama hicho leo mkoani Pwani.(Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).

  0 0

  Na Fredy Mgunda,Iringa.

  Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amefanya ziara kwenye baadhi ya shule za msingi za manispaa ya Iringa kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo na kuanza kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuboresha mazingira ya wanafunzi kusomea.

  Akizungumza mara baada ya kumaliza zira hiyo ya wiki moja Kabati alisema kuwa amefanya ziara katika shule ya msingi Kihesa,Igereke,Mtwira na shule ya Kibwabwa na kubaini changamoto nyingi ambazo anaanza kuzitafutia ufumbuzi hivi karibuni.

  “Nimejionea mwenyewe changamoto zilizopo na naona kama changamoto kwa asilimia kubwa zinafanana hivyo ni kazi yangu kuanza kutafuta njia ya kuanza kuzitatua changamoto hizo”alisema Kabati

  Kabati alisema kuwa atakikisha anazikarabati shule hizo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kama nilivyofanya hapo awali katika shule za msingi za Azimio na Kigonzile ambazo kwa sasa zinaubora kama shule za watu binafsi.“Kwa kweli wadau wamekuwa wakinisaidia kufanikisha swala la kukarabati shule za msingi zilizopo hapa manispaa ya Iringa ili kuhakikisha mazingira ya shule zote yanakuwa bora kama shule za watu binafsi” alisema kabati

  Aidha Kabati aliwataka viongozi wa serikali na viongozi wa kisiasa kuzitembelea shule hizo mara kwa mara ili kutatua matatizo haya mapema kwa sababu shule nyingi ni kongwe ndio maana miundombinu imeharibika kwa kiasi kikubwa.
  Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika moja ya shule ya msingi akiwa katika ziara ya kutambua changamoto na kuzifanyia kazi ili ziwe na ubora kama shule za watu binafsi na kuongeza ufaulo kwa wanafunzi wanasoma katika shule hizo.
  Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa darasani na wanafunzi wa shule ya msingi Kibwabwa iliyopo kata ya Kitwiru manispaa ya Iringa
  Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya kuzitambua changamoto za shule za msingi.


  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameahidi kuhakikisha kwamba suala la uharamia wa kazi za filamu za Watanzania nchini unakomeshwa mara moja kwa kuwasaka wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya Sheria.

  Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Wamiliki wa Majumba ya Kuonyeshea Sinema ambapo moja ya changamoto kubwa aliyotajiwa na wamiliki hao ni suala la uharamia wa kazi za sanaa jambo ambalo linawakwamisha wamiliki hao kutokana na ukweli kwamba baadhi ya watu wasio waaminifu wamekuwa wakivujisha filamu mpya kwa kuziuza kiholela mitaani na wengine wakihuisha filamu hizo katika mitandao ya kijamii jambo linalosabibisha hasara kubwa kwa wasanii na wamiliki wa majumba ya sinema.

  Mhe. Mwakyembe amesikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu hao wanaojihusisha na uharamia wa kazi za filamu za Watanzania huku akiapa kuwashughulikia popote walipo watu hao ili kuhakikisha kuwa Wasanii wananufaika na kazi zao na pia Wamiliki wa Majengo ya Sinema wananufaika pia kwa kuonyesha kazi za wasanii hao kwa utaratibu ambao hautomuumiza msanii mwenye kazi yake.

  “Najua baadhi ya Wamiliki wa Majumba ya Sinema mnapata hasara, na hata baadhi ya Wasanii pia, suala hili linanikera sana na kamwe haikubaliki hata kidogo, tutahakikisha kwamba watu wa namna hii wanatoweka katika tasnia yetu, tutawasaka popote walipo na kuwapeleka kwenye vyombo vya Sheria kwani Serikali hii sio ye mchezo na watu wa namna hii”, alisema Dkt. Mwakyembe.

  Ameongeza kuwa, yeye kama Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo atahakikisha kwamba hamasa ya kutosha inatolewa kwa Watanzania ili wawe na utamaduni wa kuangalia sinema zinazotengenezwa nchini katika Majumba ya Sinema yaliyopo nchini.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza (katikati) wakiwa katika moja ya Jumba la Kuonyeshea Sinema lililopo Jijini Dar es Salaam wakati walipokutana na Wamiliki wa majengo hayo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11 Oktoba, 2017. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa wa Wizara hiyo, Bibi Leah Kihimbi.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza (kushoto) wakiangalia moja ya kifaa kikubwa kitumikacho kuonyeshea sinema maarufu kama Projekta wakati walipokutana na Wamiliki wa Majumba hayo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11 Oktoba, 2017.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza (katikati) wakiwa wameongozana na baadhi ya Wamiliki wa Majumba ya Kuonyeshea Sinema wakati walipokutana na Wamiliki wa majengo hayo na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu filamu na uonyeshaji wake 11 Oktoba, 2017.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM).


  0 0


  Jonas Kamaleki- MAELEZO

  Serikali yawataka watanzania kurejesha nchi katika misingi iliyoachwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kuwa na viongozi waadilifu,wazalendo na wenye uchungu na nchi yao.

  Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. William Ole Nasha wakati akifungua Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 18 ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Ole Nasha amesema kuwa kumekuwa na ombwe kubwa la kuporomoka kwa maadili, kushamiri kwa rushwa, ufisadi, kukosekana kwa uzalendo na uwajibikaji, kuwepo kwa wafanyakazi hewa na biashara ya madawa ya kulevya.

  Ameongeza kuwa wengi waliokuwa wakiharibu nchi hii ni watanzania wenyewe kwa ajili ya tamaa na ubinafsi wao. Nimefarijika sana kusikia kuwa Chuo kimeanza kurejesha hadhi yake iliyokuwepo hapo awali kilipoasisiwa kwa kuanzisha program maalum ya Uongozi, Maadili na Utawala Bora,”alisema Ole Nasha.

  Akizungumzia Mada Kuu ya Kongamano ambayo ni Mtazamo wa Mwalimu Nyerere katika Uchumi wa Viwanda na Maendeleo ya Jamii, Naibu Waziri amesema kuwa ni ukweli usiopingika katika uchumi wa maendeleo ya viwanda, Uzalendo, Utaifa, Uadilifu na Uongozi Bora vinapaswa kuzingatiwa. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema kuwa viwanda si maendeleo bali ni matokeo ya maendeleo.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zao ili kuleta mabadiliko makubwa kwa wakulima.

  Akiongea katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea (TFRA) jana na kuwahusisha Watumishi wote wa Taasisi hiyo, Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi hao kuwa na malengo na mpango kazi ambao kila mtu atautekeleza  na atapimwa kutokana na mpango kazi huo.

   Hata hivyo Dkt. Mwanjelwa amewapongeza  kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao kwa sasa, hususan katika zoezi la uagizaji wa mbolea kwa mfumo wa pamoja (Bulk Procurement System) ambao umechangia kwa kiasi kikubwa mbolea hiyo kumfikia mkulima kwa bei nafuu.Pamoja na pongezi hizo Naibu Waziri, Dkt. Mwanjelwa ameitaka  TFRA  kuongeza bidii katika utendaji wao wa kazi na kuhakikisha kuwa wanaondoa kero zinazowakabili Wakulima.

  Aidha ameitaka Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea kuhakikisha kuwa mambo matatu muhimu yanazingatiwa ambayo ni upatikanaji wa mbolea (Availability) ufikishaji wa mbolea karibu zaidi kwa Wakulima (Accessibility) na kwa bei ambayo wakulima wanaweza kumudu kuinunua (Affordability) .“Mhakikishe mbolea inakuwepo nchini kote na wakulima wanapohitaji inapatikana na iwe kwa gharama ambayo Mkulima anaweza akanunua. “Amekaririwa, Naibu Waziri.

  Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa mamlaka hiyo bwana Lazaro Kitandu amemshukuru Naibu waziri kwa kuwatembelea na kuwatia moyo katika utendaji kazi wao na kumhakikishia kwamba TFRA imejipanga vizuri kupambana na changamoto za baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu hasa katika kuzingatia bei elekezi ya mbolea.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza viongozi pamoja na wafanyakazi katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea (TFRA)
   Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akipata maelezo kuhusu sampuli ya mbolea aina ya DAP kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mbolea (TFRA) Bwana Lazaro Kitandu  alipotembelea ofisi hiyo.

  0 0

  KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy leo imekabidhi hundi yenye thamani Tsh milioni 25 kwa waandaaji wa mbio za Rock City Marathon ikiwa ni mwendelezo wa kampuni hiyo kudhamini mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  Akikabidhi hundi hiyo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi, Meneja Mkuu wa  kampuni ya Puma Energy Bw Phillipe Corsaletti alisema udhamini huo unalenga kuunga mkono juhudi za serikali kuhamasisha michezo na utalii wa ndani hapa nchini.

  “Michezo huleta uimara wa afya na uimara huo ndio umetufikisha Puma Energy hapa tulipo kimafanikio. Ni wazi ushiriki wa Puma kwenye mbio hizi utawajaza nishati ya nguvu na ubora washiriki wote’’ alisema.

  Aliahidi kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na waandaaji wa mbio hizo katika kuboresha zaidi mbio hizo kwa miaka ijayo huku akitoa wito kwa  vijana wengi zaidi kutoka mikoa mbalimbali kujiandaa kwa ajili ya mbio hizo.

  Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo, Ngowi alisema uwepo wa kampuni hiyo katika kufanisha Rock City Marathon utaongeza hadhi na ubora wa mbio hizo ili ziende sambamba na ubora wa huduma na bidhaa zinazoandaliwa na kampuni hiyo.

  Naye, Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Bidan Lugoe  alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, Sh mil 2/-  kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu.
  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Bw Phillipe Corsaletti (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 25 kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (wa tatu kushoto) ikiwa ni udhamini wa mbio hizo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Meneja Masoko wa Kampuni ya Puma Energy Bw Machumani Shebe (wa tatu kulia) na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Bidan Lugoe (kulia) 
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Puma Energy Bw Machumani Shebe (kushoto) akizungumza kwenye warsha hiyo. 
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati) akizungumza kwenye warsha hiyo. Pamoja na mambo mengine Ngowi alisema uwepo wa kampuni ya Puma katika kufanisha Rock City Marathon utaongeza hadhi na ubora wa mbio hizo ili ziende sambamba na ubora wa huduma na bidhaa zinazoandaliwa na kampuni hiyo.
  Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Bidan Lugoe akizungumza kuhusiana na maandalizi ya mbio hizo ambazo pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, Sh mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu.
   


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Ndg. Geoffrey Mwambe amesema kwamba taarifa zilizotolewa na Mwandishi wa FT. John Aglionby kuhusu mazingira ya Uwekezaji Tanzania kuwa yanatishia wawekezaji si sahihi na yanalenga kupotosha ukweli kuhusu hali halisi kuhusu Uwekezaji Tanzania.

  Mwandishi huyo wa Financial Times ametoa maelezo ambayo amesema yametolewa na Muwekezaji Aliko Dangote maelezo ambayo yamelenga kusukuma Agenda yake ambayo haijulikani na yenye lengo la kupotosha sera za uwekezaji na kuwaogopesha wawekezaji ambao wameendelea kuiamini Tanzania na kuwekeza mitaji yao mikubwa hapa nchini.

  Hatuamini kuwa Ndugu Dangote anaweza kuwa msemaji wa kuhusiana na sekta ya madini kwa hapa nchini. Amewekeza kwenye sekta ya viwanda na serikali imekuwa mstari wa mbele kusikiliza na kuyafanyia kazi maoni ya mfanyabiashara huyo ili kuweza kuboresha mazingira yetu ya uwekezaji hapa nchini. Serikali yetu imejidhatiti katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na imedhamiria kuhakisha uwekezaji huo unakuwa na faida kwa watanzania nan chi kwa ujumla.

  Tunaamini kuwa kuna umuhimu wa kuhakikisha maelezo yanakuwa na pande mbili ili kuondoa utata utaojitokeza wa maelezo ambayo yanaweza kuathiri na kusababisha utata kwa wafanyabiashara walioiamini Tanzania kama sehemu yao ya kufanya uwekezaji. 

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameitahadharisha Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini kutorudia makosa yaliyokuwa yanafanywa na Halmashauri kabla ya wakala huo kuanzishwa.

  Amesema kuwa matumizi mabaya ya fedha za barabara pamoja na barabara hizo kujengwa chini ya viwango na kuisababishia serikali hasara ya kufanya matengenezo ya mara kwa mara ni miongoni mwa changamoto ambazo serikali imeamua kuzitafutia ufumbuzi kwa kuanzisha Wakala huo.

  “Ukiitwa Injinia na kazi yako iendane na cheo chako, sio unafanya kazi mpaka hata sisi ambao hatuna ujuzi huo tukiona tunasema hii ipo chini ya kiwango, na hapo mwanzo serikali ilikuwa inaelekeza pesa nyingi sana kwenye barabara lakini kiuhalisia barabara hazipo na muda mwingine mvua zinataka kuanza ndio utaona mkandarasi anaingia barabarani kwenda kutengeneza barabara,” Mh. Zelote alifafanua.

  Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha kwanza cha bodi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

  Amesisitiza kuwa kwa kuimarisha sekta ya barabara vijijini ndio miongoni mwa hatua za kuuendea uchumi wa Viwanda ambao ndio kipaumbele cha serikali ya wamu ya tano inayoongozwa na Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

  Hivyo ametoa wito kwa wakala huo kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa uadilifu na kuhakikisha mabadiliko yanaonekana na kuwaasa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na hatimae kurudisha nyuma azma ya serikali ya awamu ya tano. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto) wakati akifungua kikao cha bodi ya barabara, (katikati) Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule pamoja na Katibu tawala wa Mkoa wa Rukwa Bernard Makali. 

  0 0

  Na Tiganya Vincent, RS-Tabora

  SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetoa wito kwa viongozi wa dini mbalimbali mkoani hapa kutumia nafasi zao katika kusaidia mapambano dhidi ya kilimo na matumizi dawa za kulevya aina ya bangi katika jamii. Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji, Wakuu wa Idara na viongozi wa dini mkoani hapa.

  Alisema kuwa vitendo vingine vya uhalifu katika jamii vinasababishwa na matumizi ya dawa za kulevya kama vile bangi ambazo zinawapelekea baadhi ya vijana kuchukua maamuzi mwngine ya kujichukulia sheria mikononi. Mwanri alisema kuwa pamoja na kuwa Serikali ya Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imekuwa ikiendesha zoezi la kufyeka mashamba ya bangi katika mapori mbalimbali bado viongozi wa kiroho wanayo nafasi ya kuwaelimisha Waumini wao kuepuka matumizi na kilimo cha zao hilo haramu ili kuhakikisha vijana wanakuwa katika maadili mazuri na sio yale ya kuelekezwa na bangi.

  Alisema kuwa matumzi ya bangi yamesababisha baadhi ya vijana kukosa hata heshima hata kuwa tayari kupambana na wazee au watu wanaowazidi umri bila kuzingatia kuwa kufanya hivi ni kinyume na utamaduni mwa Mtanzania ambao unawataka vijana kuwa heshimu watu wazima. Mwanri aliongeza kuwa vitendo vya matumizi ya bangi viachwa vikaendelea na hatimaye vikajipenyeza hadi mashuleni upo uwezekano wa kuharibu na wanafunzi na kusababisha vurugu.

  “Tunawaomba sana viongozi wetu wa kiroho mtusaidie kuhusu suala la bangi…utamkuta kijana ameshavuta na kuanza kusema bangi ni bangue …bangi nipe nguvu nikapigane na fulani…jambo linaonyesha kuwa bangi umsababisha kijana kupenda kutafura shari” alisisitiza Mkuu huyo Mkoa.

  Akitoa mada kuhusu hali ya ulinzi na usalama kwa kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa alisema kuwa katika kipindi hicho kumekuwepo na matukio 167 ya watu kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi.

  Alisema kuwa jeshi la Polisi mwaka huu limefanikiwa kukamata dawa nyingi za kulevya ikiwemo bangi kutokana na misako kuongezeka na kufanikiwa kuwakata watuhumiwa na kugundua maeneo ambao wamekuwa wakilimia bangi katika mapori mbalimbali. Aidha Kamando hiyo wa Mkuu wa Tabora alitoa wito kwa viongozi wa kiroho kusaidia kutoa elimu juu ya kuepuka imani ya kishirikina ambazo ndizo zimekuwa zikisababisha mauaji wa wazee na walemavu.

  Kwa upande wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Askofu Mkuu Mihayo Tabora (AMUCTA) Padre Dkt. Juvenalis Asantemungu alisema anakusudia kutunga kitabu kitakachohusu maadili kwa ajili ya kuelimisha jamii ya wakazi wa Tabora na maeneo mengine ili kuzingatia maadili na kuepukana na vitendo vya kuwachoma wazee kwa imani za kishirikina. Alisema kuwa mtu anayezingatia maadili hawezi kutenda uovu huo wa kukatisha maisha ya wazee kwa sababu ya kuona kuwa wamekuwa na macho mekundu kutokana na mazingira wanayoishi.

  Mkutano huo wa siku tatu ambao mada mbalimbali zinajadiliwa na ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora umewahusisha Wakuu wa Wilaya zote, Wakurugenzi Wote , Wakuu wa Idara zote , Taasisi za Umma zote na viongozi wa dini kwa lengo la kumbushana majukumu ya kila mmoja ili kuboresha huduma kwa wananchi.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Wadau wa Usalama Barabarani, kinachojadili mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara, Joyce Momburi na Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Japhet Lusingu.Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Joyce Momburi, akizungumza na wadau mbalimbali wa Usalama Barabarani (hawapo pichani), wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Wadau wa Usalama Barabarani, kinachojadili mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani. Wengine ni Kamishna Msaidizi, Japhet Lusingu (kulia), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Hassan Simba Yahya (watatu kulia) na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Theopista Mallya. Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
  Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Deus Sokoni, akisoma vifungu vya Sheria ya Usalama Barabarani mbele ya wadau mbalimbali wa Usalama Barabarani (hawapo pichani), wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Wadau wa Usalama Barabarani, kinachojadili mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Joyce Momburi na kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Theopista Mallya.Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
  Mdau wa Usalama Barabarani, Henry Bantu, akitoa Historia ya Baraza la Usalama Barabarani wakati Kikao cha Wadau wa Usalama Barabarani, kinachojadili mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani.Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.

  0 0

  Chama cha Wanayansi wa Elimu Bahari ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi (WIOMSA) kimeandaa mashindano ya kazi za sanaa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Tanzania. Dhima ya mashindano hayo ni: “Umuhimu wa Mazingira ya Pwani na Bahari kwa Tanzania”. Chora, paka rangi, tumia program za kompyuta za uchoraji au eleza mawazo yako hayo kwa kutunga wimbo.   

  Vigezo na Masharti ya Kushiriki 
  Uwasilishaji wa ubunifu huo unaweza kufanyika kwa michoro (zikiwemo katuni/vibonzo) au utunzi wa nyimbo. Mwanafunzi anaweza kuwasilisha kazi moja kwa kila njia ya uwasilishaji. 
  i)Majina na mawasiliano. Andika jina lako, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, anuani kamili ikiwemo namba ya simu na jina la shule. 
  ii)Maelezo: Andika maelezo ya sentensi moja kuhusiana na kazi yako ya sanaa.

  Tuzo:
  Tuzo zitatolewa kwa washindi watatu wa mwanzo kwa kila kundi
  i.Cheti 
  ii.Seti ya vitabu vya shule 
  iii.Pesa taslimu: Mshindi wa kwanza 1,000,000/- Mshindi wa pili 500,000/- na Mshindi wa tatu 300,000/-

  Mfumo wa uwasilishaji: 
  i.Michoro: iwe kwa rangi nyeusi na nyeupe au rangi mbalimbali na zichorwe kwenye karatasi ya ukubwa wa A4 (iwe ni ukurasa mmoja tu). Kwa kuwasilisha kupitia mtandao utapiga picha kwa scanner na kuipakia kwenye mtandao kwa muundo wa jpg au pdf).
  ii.Utunzi wa muziki: urekodiwe kwa kuimbwa bila vyombo (acapella) au na vyombo vya muziki (uimbwe kwa muda wa kati ya dakika 1 - 3 tu uhifadhiwe kwenye kwenye mfumo wa mp3 au mp4 kwa ajili ya kupakia mtandaoni au kuwekwa kwenye CD au flash drive kwa ajili ya kutumwa kwa njia ya posta.

  Kazi zote za sanaa ziwasilishwe kabla ya Jumanne 31 Oktoba 2017 kupitia: 
  au
  2.Njia ya posta kwenda: 
  WIOMSA 
  S.L.B 3298, 
  Zanzibar
  au
  3.Namba ya whatsApp: 0767 254 887

  Kwa maelezo zaidi wasiliana kupitia:
   +255 24 2233472 / +255 24 2234597 au secretary@wiomsa.org

  0 0

  Na Tiganya Vincent, RS-Tabora

  WATU watano wakazi wa Wilaya ya Igunga wamefariki duniani katika matukio mawili tofauti kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Tabora.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa amesema hayo leo wakati wa mkutano  na waandishi wa habari. Alisema kuwa katika tukio la kwanza mnamo tarehe 11 mwezi huu, watu wanne wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba waliyokuwa wakiishi kufuatia mvua zilizonyesha kwa kipindi cha siku mbili.

  Kamanda Mtafungwa alisema waliofariki kwa kuangukiwa na ukuta wanatoka kijiji cha Igogo kata ya Nanga na aliwataja kwa majini kuwa ni Kagwa Makenza(80) ambaye pia ni mmiliki wa nyumba iliyosababisha maafa hayo, wengine ni Sande Dule (6), Butonda Shija(3) na Mbula Dule mwenye miezi miwili.

  Alisema watoto wote watatu walifariki dunia wakati wakipata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga.

  Katika tukio la Pili , Kamanda Mtafungwa alisema katika kijiji cha Bulyang’ombe kata ya Nanga mtoto Zenga Tano (5) alifariki dunia baada ya kupigwa na radi mnamo tarehe 10 mwezi huu wakati amelala na wazazi wake.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo alitoa pole kwa familia za waliopatwa maafa na kuwashauri wakazi wa Igunga kufuata utalaamu wa ujenzi wakati wa ujenzi wa nyumba zao ili kuepuka maafa zaidi.

  Alisema kuwa ushauri huo ni pamoja na ujenzi katika sehemu ya miinuko kwa ajili ya kujikinga na maafa zaidi.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.
  UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) umeileza mahakama kuwa, sehemu kubwa ya upelelezi umekamilika bado maeneo machache.

  Wakili wa Serikali, Wankyo Simon alimeeleza hayo leo mbele ya Hakimu Hakimu Mwandamizi, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya kutajwa.

  Wakili Wankyo amedai wanakamilisha upelelezi katika sehemu ndogo iliyobakia na  wamewaelekeza polisi kufanya hill na kwamba tarehe ijayo wataieleza mahakama hatua ya upelelezi ilipofikia

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 26, itakapokuja kwa ajili ya kutajwa

  Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa  kusababisha hasara ya dola za Kimarekani 1,118,291.43 sawa na Sh 2,486,397,982.54.

  Kalugendo ambaye ni Mkazi wa Kinyerezi na Rweyemamu Mkazi wa Mwananyamala wote ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na  Madini.

  Wanadaiwa kati ya Agosti 25 na ,31, mwaka huu, katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, washtakiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiliwa na Wizara ya Nishati na Madini walisababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha.
  Washtakiwa wa kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini  na mthamini wa madini ya almasi, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50)  wakiingia katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu kwaajili ya kusomewa mashtaka yanayo wakabali jijini Dar es Salaam leo.
   Na upande wa mashtaka umeileza mahakama kuwa, sehemu kubwa ya upelelezi umekamilika bado maeneo machache.
  Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) wakitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kusomewa Mashataka yanayowakabiri  jijini Dar es Salaam leo.
   Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 26, itakapokuja kwa ajili ya kutajwa

  0 0

  Video Qeen, Agnes Gerald maarufu kama Masogange akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kusomewa mastaka yanayomkabiri ya matumizi ya Dawa za kulevya na kesi yake kupigwa Kalenda mpaka Novemba 14, 2017.
  Video Qeen, Agnes Gerald maarufu kama Masogange akizungumza na wakili Rouben Semwanza leo mara baada ya kufika katika mahakama ya hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo.

  Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeipiga kalenda kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili  (Video Qeen), Agnes Gerald maarufu kama Masogange hadi Novemba 14 mwaka huu ambapo shahidi wa upande wa utetezi atatoa ushahidi wake.

  Mshtakiwa Masogangea alipaswa kuanza kujitetea leo lakini wakili wa Serikali, Adolf Mkini aliomba  kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine.

   Masogange ataanza kujitetea baada ya mahakama kumkuta na  kesi ya kujibu kwa upande wa mashtaka kuleta mashahidi watatu na kuufunga kesi, Masogange pia anatarajia kuita mashahidi watatu.

  Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam  alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

  Pia anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017  alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

  0 0

   Mkurugenzi wa Shule Direct Faraja Nyarandu akizungumza na washiriki wa mkutano maalum  wa siku ya Mtoto wa Kike Duniani ulioandaliwa na Tasisi ya HDIF kwa wanufaika wake wanaopigania maendeleo ya mtoto wa kike nchini,uliofanyika jana jijini Dar.
   Mkurugenzi wa Shule Direct Faraja Nyarandu akizungumza na washiriki wa mkutano maalum  wa siku ya Mtoto wa Kike Duniani ulioandaliwa na Tasisi ya HDIF kwa wanufaika wake wanaopigania maendeleo ya mtoto wa kike nchini
   Meneja Mipango na Mahusiano kutoka HDIF ,Emma Devies akizungumza na wadau waliofika katika mkutano maalum wa maahdhimsiho ya siku ya mtoto wa kike Duniani,uliofanyika jana jioni jijini dar.
   Wadau walioshiriki katika mkutano huo ulioandaliwa na HDIF  Katika ukumbi wa COSTECH Jijini Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wake wa kiuchumi na kidiplomasia baina yake na Uganda.

  Amesema Tanzania na Uganda zinauhusiano wa muda mrefu na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inafarijika na ushirikiano huo.Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Oktoba 12, 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Bw. Richard Kaonero jijini Dar es Salaam.

  “Tunaimani kubwa na ushirikiano wetu na Serikali ya Uganda. Tutaendelea kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo tunayoitekeleza kwa pamoja ukiwemo ujenzi wa bomba la gesi.”Hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Uganda ili waje kuwekeza kwenye viwanda mbalimbali vikiwemo vya kuchakata mazao ya kilimo.

  Pia amewakaribisha raia wa Uganda kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko nchini Tanzania kama mlima wa Kilimanjaro, fukwe, mali kale na mbuga za wanyama.Kwa upande wake, Balozi Kaonero ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na dhamira ya dhati ya kuimarisha uchumi wake kupitia sekta ya viwanda.

  Pia Balozi huyo ameiomba Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuanzisha safari ya kwenda Entebe nchini Uganda ili kuimarisha usafiri kati ya nchi hizo mbili.

  Akizungumzia kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, Balozi Kaonero amesema Serikali ya Uganda na Tanzania zinaundugu wa damu na kwamba wataendelea kuudumisha.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  ALHAMISI, OKTOBA 12, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Uganda nchini Tanzania Bw. Richard Tumusiime Kaonero, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Oktoba 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt (kulia) katika kikao chake kilichofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais  jijini Dar es Salaam tarehe 12 Oktoba, 2017. Kikao hicho kilishirikisha pia wataalamu kutoka Idara ya Mazingira. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.
   Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya kumtembelea hii leo Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mhe. Balozi amezungumzia namna ya kushirikiana katika sekta ya Mazingira.
  Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt na Naibu Balozi wake Bw.  Ulf Kallstig ambae pia ni Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wakiwa Ofisini kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya kufanya mazungumzo hii leo.

  0 0

  Benki ya TPB imezindua rasmi promosheni ya huduma ya Western Union ambayo itawawezesha watumiaji wa huduma hiyo ya kifedha kushinda fedha, simu za kisasa za mkononi na kompyuta mpakato (laptop). 

  Akizungumza jijini jana, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ukuaji wa Biashara wa Benki ya TPB, Frank Mushi alisema kuwa wameamua kuanzisha shindano hilo kama kuwazawadia wateja wake katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

  Mushi alisema kuwa washindi wanaweza kupata kiasi cha fedha ambacho kitawawezesha kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka, kulipa kodi ya nyumba na ada za watoto wao kwani watumiaji wawili wa Western Union wanaweza kushinda zawadi hadi kufikia sh Milioni 3.

  Alisema kuwa mbali ya benki yao, promosheni hiyo pia itawashirikisha washirika wao kama Shirika la Posta Tanzania (TPC), Benki ya DCB, Benki ya Azania, Benki ya Wakulima ya Kagera, Benki ya Mwanga, Benki ya Amana, Benki ya Uchumi, Benki ya Maendeleo, Benki ya Njombe, Benki ya Mufindi na Benki ya Kilimanjaro.

  ‘’Promosheni tunayozindua leo ni ya miezi mitatu ambayo itaisha mwezi Januari 2018 na inakusudia kuwashukuru na kujiweka karibu zaidi na wateja wetu ambao wanaitumia huduma hii ya Western Union’’, alisema Frank Mushi. 
   Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ukuaji wa Biashara wa Benki ya TPB,  Frank Mushi (Katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya huduma ya Western Union ambayo itawawezesha watumiaji wa huduma hiyo ya kifedha kushinda fedha, simu za kisasa za mkononi na  kompyuta mpakato (laptop). Kushoto ni Kaimu Meneja wa  Huduma za Fedha na Uwakala wa shirika la Posta,  Rehema Mbunda  na kulia ni Kolimba Tawa wa Benki ya TPB ambaye ni Afisa Mkuu wa Uendeshaji
   Wafanyakazi wa TPB Benki na wafanyakazi wengine wa benki hiyo na wadau kutoka Amana Benki, Azania Benki na Shirika la Posta (TPC) wakionyesha baadhi ya zawadi ambazo washindi wa promotion ya Western Union watashinda.
   Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa benki ya TPB, Kolimba Tawa akizungumza katika uzinduzi wa promosheni ya Western Union. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ukuaji wa Biashara wa Benki ya TPB, Frank Mushi (Katikati) na Rehema Mbunda wa Shirika la Posta.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi wapili kushoto akisalimiana na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumh mara baada ya kuwasili kwa Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH wakiwa na ziara ya siku Nne kwa Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi kulia akisalimiana na Mabaharia mara baada ya kuingia katika Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH iliofika katika Bandari ya Zanzibar pamoja na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman kwa Ziara ya Siku Nne ikiwa na lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi katikati akiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumh wa mbele mara baada ya kuingia katika Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH iliofika zanzibar wakiwa na ziara ya siku Nne kwa Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo Zanzibar.
  Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH ikiingia katika Bandari ya Zanzibar ikitokea Oman ikiwa na Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo,ikiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumhi wa Serikali ya Oman.
  Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi wamwanzo kulia akiwa pamoja na Mgeni wake Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumhi kulia yake wakiangalia Ngoma ya Utamaduni (Msewe) baada ya kuwasili kwa Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH wakiwa na ziara ya siku Nne kwa Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi akiwa pamoja na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumhi pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakitembelea vikundi mbalimbali vya Ngoma ya Utamaduni mara baada ya kuwasili kwa Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH wakiwa na ziara ya siku Nne kwa Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo Zanzibar.

older | 1 | .... | 1957 | 1958 | (Page 1959) | 1960 | 1961 | .... | 3286 | newer