Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MASENETA WA BARAZA LA MAREKANI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Seneta James Inhofe pamoja na Maseneta wa Baraza la Marekani  walipotembelea na kufanya mazungumzo  Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji Charles Mwijage, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamiss Kigwangala, Naibu Waziri wa Mambo ya nje Suzane Kolimba pamoja  Maseneta wa Baraza la Marekani wakiongozwa na Seneta James Inhofe mara baada ya kufanya mazungumzo  Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama kitabu cha Seneta James Inhofe kilichoonyesha picha za maeneo mbalimbali ya Tanzania alipotembelea mwaka mmoja na nusu uliopita, tukio hilo limefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Seneta James Inhofe pamoja na Maseneta wa Baraza la Marekani walipotembelea na kufanya mazungumzo na mhe, Rais Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta  jambo na kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na kiongozi waJumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.

Picha na Ikulu

WATANZANIA WATAKIWA KUMUENZI MWALIMU NYERERE KWA KUTUMIA MAPINDUZI YA VIWANDA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
WATANZANIA wametakiwa kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli katika adhma yake ya kufanya nchi hii kuwa na uchumi wa viwanda kwa kuendelea kusimamia mawazo wa aliyekuwa Rais wa kwanza nchini Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, William Tata Ole Nasha alipokuwa akifungua kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius .K. Nyerere lilifanyika katika ukumbi wa Utamaduni wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere anakumbukwa kwa mtazamo wake wa kuanzisha ,kuendeleza na kudumisha viwanda vya ndani ya nchi kukidhi mahitaji ya wananchi pasipo kutegemea Zaidi uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi .uthubutu wa kuanzisha Viwanda vya nguo kama vile Kiwanda cha Urafiki ,Mwatex , Mbeyatex na Mutex ni hatua inayokisi mtazamo wake juu ya Viwanda.” Amesema Ole Nasha.

Amesema hivyo kwa namna ya pekee nimpongeze Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, anavyosimamia utekelezaji wa mpango huu kwanza kwa kurejesha maadili kwa viongozi na kusimamia matumizi ya rasilimali bora za nchi.

Kwa upande wake mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ,Prof. Shadrack Mwakalila amesema Baba wa Taifa alisema Julai 29 mwaka 1961 wakati wa ufunguzi wa chuo hicho kuwa alisema kuwa wale wote watakaopata nafasi ya kusoma na kufuzu kivukoni watafanana ma hamira katika mkate. Haiwezekani kutenga hamira katika mkate bali tunajua hamira ipo kwa kutazama jinsi ilivyomua mkate.
Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof Mark Mwandosya akizungumza wakati wa Kongamano la la mahadhimsho ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika katika chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kongamano la Mahadhimisho ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mama Anna Makinda akizungumza wakati akifungua mdahaloi huo.
Kaimu Balozi wa Jamhuri ya watu wa China nchini akikabidhi zawadi ya Vitabu zinavyomzungumzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika kongamano la Maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni.
Sehemu ya Wajumbe walio hudhulia Kongamano la kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

RAIS DKT SHEI ASHIRIKI MAONESHO KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) alipokuwa akiangalia Friji la mbao na Vifaa mbali mbali mbali vilivyotengenezwa na Jeshi la JKU wakati alipotembelea katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (wa pili kulia) Waziri wa kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe.Hamada Rashid Mohamed.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiangalia Meza za Skuli (Madeski) na Makabati yaliyotenmgenezwa na JKU wakati alipotembelea maonesho mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (kushoto) Waziri wa Nchio Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kher.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiangalia Mashine ya kuchambulia Mahindi ya Taasisi ya Kilimo ya EGYPT ZANZIBAR JOINT FARM wakati alipotembelea maonesho mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (kushoto) Meneja wa mradi Dr.Reda Abdalla Abdelaziz.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa mradi Dr.Reda Abdalla Abdelaziz,(wa pili kulia) katika Taasisi ya Kilimo ya EGYPT ZANZIBAR JOINT FARM wakati alipotembelea maonesho mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiangalia Asali wakati alipotembelea banda la JKU katika maonesho mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (kushoto) .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Nahodha Khamis Mnungwi (kulia) kuhusu masuala ya Uvuvi mara alipokuwa akiangalia Samaki wakati alipotembelea banda la JKU katika maonesho mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (katikati) Waziri wa kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe.Hamada Rashid Mohamed
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Hoska Gonza Mbilinyi Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Kusimamia Umuhimu wa Bahari Kuu wakati alipotembelea banda la Taasisi hiyo katika maonesho mbali mbali katika maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana (kushoto) Waziri wa kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe.Hamada Rashid Mohamed,

Picha na Ikulu.

VIGUTA WAWAPATIA UZALENDO KWANZA VIWANJA, NYUMBA MKOANI PWANI

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vicoba Tanzania (Viguta) Taifa, Dk. Dauda Salmin (kulia) akishikana mikono na Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere mara baada ya kusaini mkataba wa ushirikiano ya kufanyakazi pamoja ambapo UZALENDO KWANZA NA VIGUTA watakuwa bega kwa bega kutoa elimu ya ujasiliamali Tanzania nzima katika hafla iliyofanyika jana Kijiji Cha Kwala - Chalinze. Mwenyekiti wa Umoja wa Vicoba Tanzania (Viguta) Taifa, Dk. Dauda Salmin (kulia) wakisainisha mkataba wa ushirikiano na Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere ili kuendelea kutoa elimu ya ujasiliamali Tanzania nzima katika hafla iliyofanyika jana Kijiji Cha Kwala - Chalinze.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vicoba Tanzania (Viguta) Taifa, Dk. Dauda Salmin (kulia) akipongezana na Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere mara baada ya kumaliza kusaini makubaliano.
Salamu za pongezi zikiendelea kutolewa mara baada ya kumaliza zoezi la kusaini mkataba. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SITAHAMISHA MTUMISHI, NITATENGENEZA – WAZIRI JAFO

$
0
0

NTEGHENJWA HOSSEAH – TAMISEMI, DODOMA 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Said Jaffo amesema hatahamisha Mkuu wa Idara wala Kitengo katika Wizara hii lakini atamtengeneza awe kama anavyotaka ili aweze kuendana na kasi ya utendakaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano. 

Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati wa kikao chake na Watumishi wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara hii ambapo aliambatana na Manaibu Waziri wa OR-TAMISEMI . 

Waziri Jaffo alisema kuwa “Siwezi kuhamisha matatizo kutoka eneo kwenda lingine cha msingi ni kuhakikisha tunamtengeneza hapa hapa awe kama tunavyotaka kulingana na mahitaji yetu na aweze kuendana na kasi ya Serikali hii sasa hivi kasi yetu sio ya kutembea bali ni kukimbia na lazima wote twenda pamoja”. 

Aliongeza kuwa nahitaji “Consistency of information” kutoka kwa watalaam wanaofahamu vizuri maeneo yao ya kazi sio kila siku unahamisha unaanza na mtu mpya naye anakuwa hana taarifa za kutosha kuhusu kazi za awali hivyo inachukua muda kuanza kwenda sawa kwangu mimi nasema ntamnyoosha yeyote ambaye haendani na viwango vyangu akiwa hapa hapa na si kwingineko”. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akiwa na Naibu Mawaziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kakunda (kulia) pamoja na Naibu Waziri Mhe. George Joseph Kakunda mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za OR TAMISEMI mjini Dodoma na kufanya kikao na Watumishi.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma (hawapopichani) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara hiyo, kulia ni Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege pamoja na Naibu Waziri Mhe. George Joseph Kakunda
Watumishi wa OR-TAMISEMI wakifuatilia kikao na Waziri pamoja na Naibu Mawaziri (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za TAMISEMI –mjini Dodoma.
Katika picha ya pamoja ni viongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI (katikati) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Selemani Jafo kushoto akifuatiwa na Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege (Afya,Miundombinu,ViwandanaUwekezaji, naSerikalizaMitaa),KatibuMkuu OR-TAMISEMIMhandisiMusa Iyombe, Naibu Katibu Mkuu (Afya) Zainab Chaula na kulia n iNaibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda (Elimu, Maji, Kilimo, MifugonaMaliasili), NaibuKatibuMkuu –ElimuTixonNzunda(Elimu) pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi ya Walimu Tanzania (TSC) Winfrida G.Rutaindurwa.


Waziri Dkt. Mwakyembe Akutana na Wasambazaji wa Matangazo Katika Vyombo vya Habari

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wasambazaji wa Matangazo kwenye Vyombo vya Habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Daniel Shonza.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) na Wasambazaji wa Matangazo kwenye Vyombo vya Habari leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo wakati wa kikao baina yake na Wasambazaji wa Matangazo kwenye Vyombo vya Habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Daniel Shonza na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus.
Mmoja wa wawakilishi wa Kampuni za Usambazaji wa Matangazo kwenye Vyombo vya Habari kutoka Kampuni ya OMD Tanzania Bw. Enos Otieno akichangia hoja wakti wa kikao baina yao na Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe leo jijini Dar es Salaam.


Picha na: Frank Shija – MAELEZO

MAKAMU WA RAIS SAMIA AKUTANA NA MABALOZI WA SAUDI ARABIA, IRELAND NA MOROCCO KWA NYAKATI TOFAUTI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Paul Sherlock, Ikulu jijini Dar Es Salaam.
Balozi alizungumzia masuala mbalimbali yakiwemo kuwawezesha wanawake katika nafasi za kisiasa, Masuala ya Mimba za utotoni  na namna ya kukabiliana na vifo wakati wa kujifungua.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliiomba nchi ya Ireland kuendelea kusaidia Tanzania katika kutoa elimu ya uzazi ili kupunguza Vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua.
Wakati huo huo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amkutana na kuzungumza na Balozi wa Morocco nchini Mhe. Abdelilah Benryane mwenye makazi yake mjini Nairobi,Kenya.

Katika mazungumzo yao, Balozi wa Morocco alimpatia taarifa ya utekelezaji wa yote yaliokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco na kumueleza Makamu kwamba utekelezaji wa mambo hayo umefikia hatua nzuri.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais alimpongeza Balozi kwa kusimamia utekelezaji huo ndani ya muda mfupi.

Makamu wa Rais alimueleza Balozi huyo wa Morocco kuwa uhusiano uliopo kati ya nchi mbili hizi ni wa kudumu na utasaidia katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo katika nchi hizi.Mwisho Kabisa Makamu wa Rais alikutana na kuzungumza na Balozi wa Sausi Arabia Mhe. Mohammed Almalik .
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia Mhe.Mohammed Almalik(kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar Es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Paul Sherlock alimtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Morocco Mhe. Abdelilah Benryane (kushoto), Ikulu jijini Dar es salaam. 

11:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa kutoka kwa Balozi wa Morocco Mhe. Abdelilah Benryane (kushoto), Ikulu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya makamu wa Rais).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI UMMY ATOA MIEZI SITA KUANZISHWA MADAWATI YA ULINZI WA WATOTO SHULEN

$
0
0

Na Mwandishi Wetu Tarime- Mara.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametoa miezi sita kwa Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kuanzisha Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto kwa ajili ya kusikilizamatatizo ya wanafunzi hasa wanafunzi wa kike.
Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa KikeKitaifa iliyofanyika katika wilaya ya Tarime mkoani Maraamewasisitiza wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kuzingatia uwepo wa dawati la ulinzi na usalama wa mtoto  kike katika shule zao ili kuwa salama na kuwa na mahali pa keleza matatizo yao.
Mhe. Ummy ameongeza kuwa suala la kumlinda mtoto wa kike ni jukumu la kila moja katika jamii na kuwapongeza wadau wa maendeleo ya watoto kwa jitihada zao na kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa wanajamii kuhusu madhara ya mimba za utotoni, ukeketaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua kampeni ya kitaifa ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” "Najitambua Elimu ndio Mpango mzima". 
 Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akibonyeza kitufe kuzindua ujumbe wa radio wa kampeni ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima” 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto, wadau na madereva bodaboda wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara muda mfupi baada ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika kitaifa wilayani Tarime mkoani Mara. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KIONGOZI WA JUMUIYA YA ISMAILI DUNIANI H.H. PRICE KARIM Al-HUSSAYNI AGA KHAN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta  jambo na kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na kiongozi waJumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pome Magufuli na viongozi wengine wa serikali katika picha ya pamoja na kiongozi waJumuiya ya Ismailia duniani H.H. Prince Karim al-Hussayni Aga Khan na ujumbe wake alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 11, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia duniani H.H. Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 11, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia duniani H.H. Prince Karim al-Hussayni Aga Khan wakiongea na wanahabari (hawapo pichani) mgeni huyo alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 11, 2017.


PICHA NA IKULU

RC SHIGELLA AFUNGUA KIKAO CHA RCC LEO MKOANI TANGA

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akifungua kikao cha kamati ya ushauri cha Mkoa huo (RCC) kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi akizungumza katika kikao hicho leo 
Katibu Tawala Msaidizi Upande wa Miundombinu mkoa wa Tanga,Monica Kinala akifafanua jambo kwenye kikao hicho wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akielezea mikakati ya Bandari hiyo kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tanga (RCC) 
MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Steven Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Gabriel Robert.


MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE MKOA WA SHINYANGA OKTOBA 11,2017

$
0
0
Mkoa wa Shinyanga leo umeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 11 mwezi Oktoba.



Maadhimisho ya  siku ya kimataifa ya mtoto wa kike katika mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.

Sherehe za maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike yamehudhuriwa na watoto kutoka maeneo na shule mbalimbali mkoani Shinyanga,viongozi wa serikali na vyama vya siasa,wananchi na mashirika na taasisi zisizokuwa za kiserikali likiwemo shirika la kimataifa la Save the Children.

Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu ya “Tokomeza Mimba za utotoni,Tufikie uchumi wa viwanda”.
Akitoa hotuba kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza kwa mimba za utotoni nchini hivyo jitihada mbalimbali zinahitajika kuhakikisha mimba za utotoni zinatokomezwa mkoani humo.
Mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya  siku ya kimataifa ya mtoto wa kike,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,akitoa hotuba katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini leo Oktoba 11,2017.Picha zote Kadama Malunde- Malunde1 blog
Meneja wa Shirika la Kimataifa la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima aliwataka wananchi kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati ikiwemo ya Chagulaga ambayo wanaume hutumia fursa kuchagua mchumba na kusababisha watoto wa kike waolewa bila ridhaa yao.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Ngassa Mboje akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Iselamagazi wakiimba na kucheza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

EFM REDIO KUWASHA MZIKI CCM KIRUMBA MWANZA

BALOZI SEIF ALI IDDI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA SWEDEN

$
0
0
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi amesema uzoefu wa Sweden wa miaka mingi katika kuendesha serikali za Mitaa unaweza kuisaidia Zanzibar katika kipindi hiki cha ugatuzi.

Balozi Seif amesema hayo afisini kwake vuga wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe wa watu wanane kutoka sweeden ukiongozwa na Spika wa Manispaliti ya Sundsvall Bibi. Arianne Sundman ambaye yupo nchini kwa ziara ya wiki moja.

Amesema Zanzibar hivi sasa inapitia katika kipindi cha mageuzi ya serikali za mitaa unaojulikana kwa jina la ugatuzi ili kuyafanikisha mageuzi hayo ni vyema kujifunza kutoka nchi mbali mbali zenye uzoefu.

Balozi Seif amefurahishwa na uhusiano uliopo kati ya Wadi ya Makunduchi na Manispaliti ya Sundsvall na kutaka uhusiano huo uimarishwe zaidi. Naye Spika wa manispaliti ya Sundsvall Bibi. Arianne Sundman amesema Manispaliti yake iko tayari kubadilishana uzoefu na Zanzibar katika sekta mbali mbali ikiwemo elimu.

Akielezea uhusiano uliopo kati ya Manispaliti yake na Wadi ya Makunduchi, Bi Arianne amesema ameridhishwa na uhusiano huo ambao unaimarika siku hadi siku. Wakati huohuo spika wa baraza la wawakilishi mh zubeir ali maulid amesema ujio wa wa ujumbe huo ni hatua muhimu ya kuimarisha uhusiano katika masuala muhimu ya maendeleo.

Akielezea shughuli zinazo fanywa ba baraza la wawakilishi mh zubeir amesema ni pamoja na kutunga shera, kupitisha bajeti, masuali na majibu pamoja na kupitisha mipango ya maendeleo. Nae spika wa manispaa ya sundsval ametoa shukrani kwa mapokezi mazuri waliyoyapata na kuahidi kuimarisha uhusiano kwa wawakilishi katika kubadilishana mawazo katika utekelezaji wa kazi zao za kila siku.

Mapema ujumbe huo ulipata nafasi ya kusikiza kipindi cha masulaa na majibu katika kiao cha baraza la wawakilishi kichoendelea na kutembelea sehemu mbali mbali za baraza ikiwepo chumba acha hansard. 
 Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na ujumbe wa Manispaliti ya Sundsvall Sweden
 Balozi Seif akitoa Zawadi ya kasha kwa Bibi Arianne Sundman, Spika wa Manispaliti ya Sundsvall, Sweden

picha ya pamoja na ujumbe wa Sundsvall ukiongozwa na Spika.

WANANCHI WA HALMASHAURI YA MJI WA MADABA WAFURAHIA UJIO WA UMEME

$
0
0

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MADABA.

WANANCHI wa Halmashauri ya mji wa Madaba, mkoani Ruvuma, wameipongeza serikali kwa kuwafikishia umeme kwenye eneo lao ambapo wamesema utabadilisha maisha yao.

Pongezi hizo zimetolewa Oktoba 11, 2017, kufuatia kukamilika kwa kazi ya kujenga njia ya kusafirisha umeme kwenye eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka mtandao wa nyaya (wiring), kwenye eneo hilo na kwenye nyumba za  wananchi kazi iliyokwenda sambamba na ufungaji wa  transofoma pozo.

Kwa sasa Serikali kupitia Shirika lake la Umeme, TANESCO inatekeleza mradi mkubwa wa umeme wa Makambako-Songea ambao unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa  msongo wa kilovolti 220Kv Transmision Lines na usambazaji umeme vijijini (Rural electrification), katika vijiji vya mkoa wa Njombe na Ruvuma ikiwa ni pamoja na kujenga vituo viwili vipya vya kupoza umeme, huko Madaba na Songea na upanuzi wa kituo kingine mjini Makambako.

“Nimefurahi sana eneo letu kupata umeme, kwa muda mrefu sana tumekuwa tukitegemea umeme wa solar, sasa nina matumaini makubwa nimeona kazi zinavyoendelea hapa za kuweka nguzo za umeme, kutandaza nyaya majumbani na kuweka transofa, na tumeambiwa tukae mkao wa kula kwani umeem utawaka muda wowote kuanzia hivi sasa.” Anasema  Rehema Maluwa, (pichani juu).
 Nyumba zikiwa na madishi ya tv kwenye Halmashauri ya mji wa Madaba mkoani Ruvuma ambazo bila shaka kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutokana na matumizi ya jenereta kupata umeme lakini ujio wa umeme wa TANESCO utapunguza gharama za uendeshaji.
 Maendeleo ya ujenzi wa msingi wa kufungia mashine kituo cha Madaba, ukiendelea Oktoba 11, 2017.
  Maendeleo ya ujenzi wa msingi wa kufungia mashine kituo cha Madaba, ukiendelea Oktoba 11, 2017.
 Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.
  Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Matumizi ya mkaa wa mawe wa kupikia yatapunguza ukataji miti ovyo na kuepusha uharibifu wa mazingira.

$
0
0
Jonas Kamaleki-MAELEZO

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Meneja wa Kampuni ya Accaso International Limited, William Kafipa katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.

Kafipa amesema mkaa wa mawe wa kupikia unatumika kwa kiasi kidogo na unawaka kwa muda wa saa nne mfululizo hivyo kuwezesha mtumiaji kupika vitu vingi kwa mkaa kidogo ukilinganisha na mkaa unaotokana na miti.

“Mkaa huu ni bora sana na watu wengi wakiutumia wataachana na kukata miti ovyo hivyo kutunza mazingira na kuepusha nchi kuwa jangwa,”alisema Kafipa.

Aliongeza kuwa badala ya kutumia gunia moja la mkaa wa kuni ambalo gharama yake ni kati ya shilingi 60,000/= na 85,000/=, unaweza kutumia boksi mbili hadi tatu za mkaa wa mawe kwa matumizi sawa na gunia hilo ambayo jumla yake ni shilingi 36,000/=. Kwa kufanya hivyo mtumiaji ataokoa fedha yake na pia atatunza mazingira kwani hatalazimika kukata miti ili kupata mkaa.

Kwa upande wake, Afisa Masoko na Mauzo wa Accaso, Monica Cornelius amesema mkaa wa mawe utampunguzia mwanamke adha ya kutembea mwendo mrefu kutafuta kuni endapo atatumia mkaa huo ambao bei yake ni nafuu hata kwa mtu wa kipato cha chini.

“Mkaa huu hautoi moshi jambo ambalo ni zuri kwa mazingira na kwa kwa afya ya mtumiaji, hii itaepusha pia mauaji ya vikongwe ambao walikuwa na macho mekundu kutokana na kupikia samadi au kuni mbichi,” alisema Monica.Monica ameongeza kuwa akina mama na watu wengine waipokee teknolojia hii mpya ya mkaa wa mawe wa kupikia ili iweze kubadilisha maisha yao.


TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI

$
0
0
 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi  wa baraza hilo  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mkutano wa kuzindua baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ukiendelea.
Picha na JKCI
 Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi akizindua baraza la Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya JKCI Prof. William Mahalu na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa baraza la Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Restituta Rugaganya mara baada ya kuzindua baraza hilo leo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi akimpongeza  Katibu wa baraza la Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Samweli Rweyemamu mara baada ya kumkabidhi vitendea kazi wakati wa uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO OCTOBER 12, 2017

Nitaanza na Rushwa, Uzembe Katika Ofisi za Umma – Waziri Mkuchika

$
0
0

Na: Thobias Robert- MAELEZO

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa atashughulikia suala la rushwa pamoja na udanganyifu wa umri unaofanywa na baadhi ya watumishi wa umma hapa nchini.

Mkuchika aliyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika mkabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo ambaye kwa sasa ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki katika ukumbi wa wizara hiyo.“Tutaongeza kasi ya kurejesha nidhamu, maadili na mapambano dhidi ya rushwa hapa nchini,” alifafanua waziri Mkuchika

Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro pamoja na watumishi wa wizara hiyo, Waziri Mkuchika alisema kuwa atahakikisha anashughulikia suala la watumishi kupandishwa madaraja pamoja na kuongezewa mishahara baada ya kukamilika zoezi la ukaguzi la watumishi hewa.

Aidha alisema kuwa suala la rushwa linatakiwa kujengewa msingi kutoka ngazi ya chini, hivyo ataongea na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ili kuweka somo la rushwa katika mitaala ya elimu hapa nchini kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu.
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye sasa amekuwa Waziri wa Madini Angelah Kairuki (kushoto) akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora George Mkuchika wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya ofisi leo jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni watumishi wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam katika hafla ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo Angellah Kairuki ambaye sasa amekuwa Waziri wa Madini 
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye sasa amekuwa Waziri wa Madini Angelah Kairuki akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari katika hafla ya kumkabidhi ofisi mrithi wake Waziri George Mkuchika leo Jijini Dar es Salaam .
Aliyekuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angelah Kairuki akimkabidhi nyaraka za ofisi Waziri aliyeteuliwa kuongoza Wizara hiyo George Mkuchika katika hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angelah Kairuki akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari katika hafla ya makabidhiano ya ofisi na waziri aliyeteuliwa kuongoza wizara hiyo George Mkuchika leo jijini Dar es Salaam.Picha na: Thobias Robert – MAELEZO.



MAMA SALMA-AUTAKA MKOA WA PWANI KUPAMBANA NA MAFATAKI KUOMDOA TATIZO LA MIMBA ZA UTOTONI

$
0
0

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

MKE wa rais mstaafu ,mama Salma Kikwete,amesema mkoa wa Pwani upambane na mafataki wanaoteka fikra za watoto wao wa kike ili kuondokana na mimba za utotoni ambapo mkoa huo ni kati ya mikoa kumi inayoongoza kwa mimba hizo kitaifa.

Aidha amekemea tabia inayofanywa na mashuga dadi wanaojiona mahodari wa kutongoza na kunyemelea watoto wa kike wanafunzi na wengine kuwakatisha masomo kwa kuwatia mimba na kudai anaejiona hodari wa kutongoza dunia aende kwa wanawake wakubwa huko mitaani.

Pamoja na hilo,Mama Salma ,ameitaka jamii kuachana na mila na desturi zinazochochea mimba ,na kusema lazima zitazamwe ili kuwawezesha watoto hao waendelee na masomo yao.

Aliyasema hayo,wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimkoa,yaliyofanyika wilayani Kibaha mkoani Pwani,ambayo yamefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Room To Read.

MKE wa rais mstaafu ,mama Salma Kikwete ,akiwa katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimkoa Mkoani Pwani yaliyofanyika Kibaha na kufadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Room To Read linalotekeleza mradi wa kumwendeleza mtoto wa kike.Picha na Mwamvua Mwinyi.


Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images