Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live

TANGA CEMENT YATOA MIFUKO ELFU MOJA YA SARUJI KWA AJILI YA UJENZI NYUMBA ZA POLISI ARUSHA

$
0
0
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani hapa, limepokea jumla ya tani hamsini sawa na mifuko elfu moja ya Saruji yenye thamani ya shilingi Milioni kumi na Mbili na Laki Tano toka kampuni ya Saruji yaTanga (Tanga Cement) ili ziweze kusaidia ujenzi wa nyumba za Askari wa Jeshi hilo ambalo hivi karibuni walipatwa na majanga ya moto yaliyosababisha nyumba za familia 13 kuungua na kuteketeza karibu kila kitu. 
Akipokea shehena hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo aliishukuru Kampuni ya Tanga Cement kwa kujitoa na kutambua mchango wa askari katika kuimarisha usalama, na kuahidi kusimamia ili ujenzi huo kasi yake iongezeke.
Alisema mbali na Kampuni hiyo pia aliwaomba watu wengine binafsi pamoja na Makapuni mengine waige mfano toka kwa kampuni hiyo kuisaidia jamii hasa katika sekta mbalimbali kama vile elimu, afya  na majanga kama haya.
Kamanda Mkumbo pia alitumia fursa hiyo kushukuru watu binafsi , makampuni,  taasisi pamoja na majeshi ya Ulinzi na Usalama kama vile Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jeshi la Polisi Kilimanjaro, Chuo cha Polisi Moshi na Jeshi la Magereza.
Wengine ni kiwanda cha Magodoro cha Tanfoam, kiwanda cha A to Z, Ofisi ya Mwanasheria mkoani hapa, Green Valley School na Kampuni ya Otterlo Business Corporation Ltd (OBC) pamoja na watu binafsi ambao walitoa msaada wa fedha, Chakula, Saruji nguo pamoja na Magodoro.
Kwa upande wake Meneja Biashara wa kampuni hiyo Bw. Peet Brits alisema kwamba, wao kama kampuni wameweka mkazo kusaidia katika elimu, afya, maendeleo ya Jamii pamoja na mazingira lakini kwenye majanga mbalimbali kama vile ajali za moto.
Alisema kwamba anafahamu kazi zinazofanywa na Jeshi la Polisi katika kudumisha usalama ambapo unasaidia kuvutia mazingira mazuri ya kibiashara hapa nchini. Alisema wametoa msaada huo ili usaidie kujenga makazi ya familia za askari.
Bw. Brits alisema anajua walichochangia hakiwezi kutosheleza lakini wanaamini kitasaidia kwenye ujenzi wa nyumba hizo na kuzitaka kampuni pamoja na taasisi  kusaidia Jeshi la Polisi ambalo linaimarisha usalama hali ambayo inasaidia kuweka mazingira mazuri ya kibiashara.
 Meneja Biashara wa Tanga Cement Peet Brits akimkabidhi Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo mifuko ya Saruji iliyotolewa na Kampuni hiyo ili iweze kusaidia ujenzi wa nyumba za Polisi zilizoungua moto hivi karibuni (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 Baadhi ya mafundi na wasaidizi wao wakiendelea kujenga nyumba za Polisi jijini hapa (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Moja ya lori lililobeba mifuko ya Saruji iliyotolewa na kampuni ya Tanga Cement kwa Jeshi la Polisi mkoani Arusha.
Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)


Introducing "I Miss You" (Official Video) by Lady Jaydee

$
0
0
The much awaited video for "I Miss You" is finally out. Lady Jaydee finally drops the video she had promised her fans,  former latest single. The song has had everyone buzzing on the social media, trying to sing along, has also caught heat in the airwaves as its already on numerous raid charts. 
Hopefully these visuals from Justin Campos will propel the song all the way to the deservedly top spot and maybe even entertain the idea of a remix. A song written by Lady JayDee, Domokaya and One The Incredible, Produced by Man Water at Combination Sounds, and the video was shot on location in Johannesburg, SA.
Twitter: @jidejaydee
Instagram: @jidejaydee
Facebook: @ladyjaydee

UHURU KENYATTA AONGEA BAADA YA RAILA ODINGA KUJITOA KATIKA UCHAGUZI WA MARUDIO

MAMA ZAKHI A MEGHJI AFUNGUA MKUTANO WA 36 WA CHAMA CHA GIRL GUIDES & GIRL SCOUTS DUNIANI NCHINI INDIA

$
0
0
  Mjumbe wa Bodi ya  Udhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA),  Mama Zakhia Meghji  akiwa na vioongozi wa Girl Guides na Girl Scouts wa Ulimwengu (WAGGGS) akiwasha mshumaa  kuashiria ufunguzi rasmi wa Mkutano Mkuu wa wa 36 wa WAGGGS nchini India. Meghji alimwakilisha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyepangwa kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo wa kimataifa. Mama Samia ni Mlezi wa TGGA.
Mkutano huo hufanyika kila baada ya miaka mitatu na mara ya mwisho ulifanyika Honkong. Kuwashwa mshumaa ni  nuru ya moyo wa kujitolea katika juhudi za kuwafikia wasichana wengi zaidi popote walipo mjini na vijijini. Mkutano huo ulifanyika kuanzia Septemba 18 hadi 23 mwaka huu.

  Mama Zakhia Meghji  akiwa na Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda wakipambwa kwa nyimbo walipokuwa wakiingia ukumbini.
 Mjumbe wa Bodi ya  Udhamini ya Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA),  Mama Zakhia Meghji  akisoma hotuba wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano Mkuu wa wa 36 wa WAGGGS nchini India.
 Waliokaa  kutoka kulia ni Balozi  wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda, Mama Zakhia Meghji, Mama Martha Qorro ambaye ni Mwenyekiti wa TGGA. Waliosimama wa pili kushoto ni  Aika wa Afrika Kusini,  kushoto kwake ni Maryam Mjema wa TGGA Kamishna wa Mambo ya Nje, Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi Nicola  Grinstead Mwenyekiti wa Bodi ya WAGGGS.

Dkt. Mwakyembe Azindua Tuzo za Filamu ya Sinema Zetu

MAHAKAMA KUU ARUSHA YAMALIZA MASHAURI YALIYOSAJILIWA JANUARI MPAKA AGOSTI MWAKA HUU

$
0
0
Na Lydia Churi- Mahakama, Arusha

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imefanikiwa kusikiliza na kumaliza kwa zaidi ya asilimia 90 ya mashauri yaliyofunguliwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Agosti mwaka huu.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha Mhe. Angelo Rumisha, jumla ya mashauri 737 kati ya 805 yaliyosajiliwa kuanzia mwezi Januari hadi Agosti 2017, yamemalizika.

Alisema haya ni mafanikio ya kuridhisha kwa Mahakama Kuu kanda ya Arusha ambapo kila Mhe. Jaji amesikiliza na kumaliza wastani wa mashauri 245. Hivi sasa, Mahakama Kuu kanda ya Arusha ina jumla ya majaji watatu.

Katika kuhakikisha inaondokana na mlundikano wa mashauri kwenye Mahakama mbalimbali nchini, Mahakama ya Tanzania ilipanga idadi ya mashauri yatakayosikilizwa na Majaji na Mahakimu. Kwa mujibu wa mpango huo, kila Jaji anatakiwa kumaliza mashauri yasiyopungua 220 kwa mwaka na hakimu Mashauri 250.

Akifafanua takwimu za mashauri, Naibu Msajili alisema hadi kufikia Agosti 31, mwaka huu, Mahakama hiyo imebakiwa na mashauri 809 ambapo  kati ya mashauri hayo, 788 yana umri wa kati ya miaka 1-2, mashauri 17 yana umri kati ya miaka 3-5, mashauri 2 yana umri kati ya miaka 5-10 na mashauri mengine 2 yana umri wa zaidi ya miaka 10.

Alisema mashauri yote yenye miaka 10 na zaidi ni yale yaliyorudishwa kutoka Mahakama ya Rufani baada ya kikao cha Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kilichofanyika April mwaka huu.

Akizungumzia Mahakama za Hakimu Mkazi na za Wilaya kwa Mikoa ya Arusha na Manyara, Mhe. Rumisha alisema jumla ya mashauri 223 yana umri zaidi ya miezi 12, kati ya mashauri hayo, ni mashauri mawili tu ndiyo ambayo Mahakama zina mamlaka nayo ikiwa ni sawa na asilimia 1.3 ya mashauri yote yenye umri zaidi ya miezi 12 hivyo mashauri mengi ya mlundikano ni yale ambayo Mahakama hazina mamlaka nayo.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha Mhe. Angelo Rumisha
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha Mhe. Sekela  Moshi.
Wakati huo huo, Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha Mhe. Sekela Moshi amesema hivi sasa kanda yake imeanza kutekeleza Mikakati iliyojipangia ya kuondoa mashauri yote yenye muda mrefu Mahakamani.

Akiitaja mikakati hiyo, Kaimu Jaji Mfawidhi alisema tangu Oktoba 2 mwaka huu, kanda ya Arusha imekuwa ikifanya vikao vya kumaliza mashauri ya zamani ya madai ambapo mpango huo unatarajiwa kukamilika Oktoba 13, 2017.  

Alisema baada ya kukamilika kwa mkakati huo, kanda yake itaanza mkakati mwingine uliopangwa na Mahakama ya Tanzania wa kumaliza mashauri ya zamani chini ya mradi wa Benki ya Dunia unaotarajiwa kuanza Oktoba 16 na 17 mwaka huu.

Alisema kanda ya Arusha ina mashauri ya zamani machache hivyo wanatarajia ifikapo Novemba  14, 2017 mashauri yote ya muda mrefu yatakuwa yamemalizika.

RAIS DK. SHEIN AFUNGUA MAONESHO YA KILIMO KIZIMBANI LEO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kufungua   Maonesho ya Maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani leo katika Viwanja vya eneo maalum lililotengwa Kizimbani Wilaya ya Magharibi "B" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja (kulia) Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitoa hutuba yake kwa Wananchi mbali mbali na Viongozi waliohudhuria katika maonesho ya Maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani katika Viwanja vya eneo maalum lililotengwa Kizimbani Wilaya ya Magharibi "B" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja alipoyafungua leo
 Baadhi ya Viongozi mbali mbali na Wananchi waliohudhuria katika sherehe za Ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani katika Viwanja vya eneo maalum lililotengwa Kizimbani Wilaya ya Magharibi "B" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mhe.Mama Mwanamwema Shein (katikati) akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma (kulia) pamoja na  Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed katika sherehe za  Ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani yaliyofunguliwa leo katika Viwanja vya eneo maalum lililotengwa Kizimbani Wilaya ya Magharibi "B" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
 Baadhi ya Vijana waliovalia sare na Wananchi wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani katika Viwanja vya eneo maalum lililotengwa Kizimbani Wilaya ya Magharibi "B" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
  Wanafunzi wa Skuli ya Dole wakiwa katika  sherehe za Ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani katika Viwanja vya eneo maalum lililotengwa Kizimbani Wilaya ya Magharibi "B" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAGAZETI YA JUMATANO LEO OCTOBER 11,2017


BLOGGER WA JAMVI LA HABARI AMEREMETA

$
0
0
Blogger mashuhuri wa blog ya Jamvi la Habari ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SAUT-Songea Willy Migodela tarehe 07/10/2017 alifunga ndoa na Lightness Ngenzi katika kanisa la KKKT Msharika wa Mbarali mkoani Mbeya. Globu ya Jamii inampa pongezi Will na shemela kwa kumeremeta.

Pichani Bwana Harusi Willy Migodela na Bibi Harusi Lightness Ngenzi
Pichani Bwana Harusi na Bibi Harusi wakiwa na wasimamizi wao Mr & Mrs Pambano Myula
Pichani Bwana na Bibi Harusi wakiwa katika picha ya pamoja na wapambe wao.

Bwana na Bibi Harusi wakiwa katika tabasamu la kufurahia ndoa yao



KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

UHURU FM LEO TENA WAMWAGA MSAADA KUPITIA KAMPENI YAO YA 'GUSA MAISHA YAO' KUMUENZI BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE

$
0
0
Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Peoples Media inayoendesha Kituo cha Radio cha Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam, Paul Mng'ong'o (wanne kushoto), akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula kwa Mwanzilishi wa Kituo cha kujeresha katika maisha ya kawaida waraibu wa dawa za kulevya cha Pili Misana Foundation, Pili Misana, kilichopo Kigamboni, dar es Salaam, leo, ikiwa ni mwendelezo wa Uhuru FM kutoa misaada kupitia kampeni yao ya 'Gusa Maisha yao' kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere. Wengine katika picha ni baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru FM na Vijana wanaoishi katika kituo hicho. 
Aina ya msaada uliotolewa 
Dereva akiliungurumisha basi kupitia daraja la Kigamboni kwenda kwenye kituo hicho 
Baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa katika basi kwenda kwenye kituo hicho cha kusaidia waraibu wa dawa za kulevya kurejea katika maisha ya kawaida, baada ya kufika wafanyakazi hao wakaanza kushuka na vitu vya msaada, mmoja baada ya mwingine .

MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191

$
0
0
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MAKAMBAKO

KUKAMILIKA kwa Mradi wa ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 220kV, na usambazaji umeme vijijini kutoka Makambako-Songea kupitia Njombe, unatarajiwa kuondoa kabisa tatizo la upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wa mijini na vijiji vipatavyo 191, Meneja wa Mradi huo Mhandisi Didas Liyamuya,(pichani juu), amesema leo Jumanne Oktoba 10, 2017 wakati wa ziara ya Wahariri wa vyombo vya habari nchini.

Sambamba na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme pia utahusisha upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Makambako cha msongo wa umeme wa kilovolti 220/132/33Kv, na ujenzi wa vituo vingine vipya viwili, vya Madaba na Songea vya msongo umeme wa kilovolti 220/33kV, halikadhalika ujenzi wa mfumo wa usambazaji umeme wa msongo wa kilovoti 33 pamoja na kuunganisha wateja 22,700, katika mikoa hiyo alisema Mhandisi Liyamuya.

Akifafanua zaidi, katika mkoa wa Njombe, umeme utasambazwa katika maeneo ya Makambako na viunga vyake, Njombe yenyewe, na Ludewa, wakati mkoa wa Ruvuma umeme utasambazwa katika mji wa Songea na vijiji vilivyo katika wilaya ya Mbinga, Namtumbo na Madaba, na kuongeza kuwa umeme utakuwa wa msongo wa kilovolti 33 pamoja na ujenzi wa mawasiliano “OPGW”.

“Lengo la mradi huu ambao unafadhiliwa na Serikali ya Swedena kupitia Shirika lake la Misaada ya Kimaendeleo SIDA, Serikali ya Tanzania na Shirika la Umeme Nchini, TANESCO, ni kuboresha hali ya upatikanaji umeme katika maeneo ya uzalishaji na majumbani.” Alifafanua.
Mmoja wa wakazi wa kitongoji cha Lyamkena, mji wa Makambako mkoani Njombe, ambaye ni mteja mpya wa TANESCO, Bw.Thomas Kiwale, (kulia), akihakikiwa wakati wa zoezi la kuwahakiki wateja walioomba kuunganishiwa umeme kwenye eneo hilo, na afisa wa TANESCO, Bi.Atuokoe Mhingi, Oktoba 10, 2017
Wahariri na mafundi wa TANESCO, wakipita chini ya moja ya transofa zinazoednelea kufungwa kwenye mji wa Makambako Oktoba 10, 2017.
Moja ya minara ya kusafirisha umeme wa 220kV. ambao tayari umejengwa nje kidogo ya mji wa Makambako.
Kazi ya ujenzi wa msingi wa kufunga mitambo kwenye eneo la upanuzi wa kituo cha kupoza umeme wa 220kV Makambako ikiendelea.

SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA AFRICAID KUPITIA MRADI WA KISA LAWAKUTANISHA WASICHANA WA KIDATO CHA TANO NA SITA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
 Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.


WASICHANA walioko shuleni  wametakiwa kuacha kuchagua kazi za kufanya pindi wamalizapo masomo na badala yake wafanye maandalizi ya kujiajili kwa kufanya shughuli za ujasiliamali wakati wakiendelea na harakati za kutafuta kazi.

Mbali na hayo wasichana pia wametakiwa kujenga tabia ya kujiamini na kuacha tabia ya kuwa tegemezi ili kuondokana na mfumo uliopo katika jamii kwa sasa ya kuwa mtoto wa kike ni wa kuwezeshwa na kuhurumiwa.

Hayo yameelezwa na wawezeshaiji wakati wa kongamano lililofanyika katika Chuo cha Wanyapori (Mweka) na kuandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Africaid kupitia mradi wake wa KISA na kukutanisha zaidi ya wanafunzi 1400 kutoka shule 11 za mkoa wa Kilimanjaro .

Stumai Simba ni miongoni mwa wasichana walioamua kujiajiri na baadae wanatumika katika kutoa hamasa kwa wasichana hasa wanaojiandaa kuhitimu masomo yao ya ngazi ya sekondari kushiriki kuondoa mfumo dume katika jamii amewataka wasichana kutokata tamaa.

Muwasilishaji wa mada katika kongamano lililowajumuisha Wasichana wanaosoma kidato cha tano na sita katika shule mbalimbali mkoani Kilimanjaro,Nyamagesa Laban akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika Chuo cha Wanyamapori Mweka. 
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa karibu ujumbe uliokuwa ukitolewa na Nyamagesa ambaye pia ni mwandishi wa vitabu.
Baadhi ya wananfunzi walioshiriki kongamano hilo wakiuliza maswali kwa Nyamagesa mara baada ya kumaliza kutoa ujumbe kwa wanafunzi hao.
Muwasilishaji wa mada katika kongamano la Wasichana wa Shule za Sekondari mkoni Kilimanjaro,Stumai Simba akizungumza katika kongamano hilo.

Kesi ya kumtusi Rais dhidi ya Mdee kuanza kuunguruma mwezi ujao.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Kesi ya kutumia lugha chafu ya Matusi dhidi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli inayomkabili mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee kuanza kusikilizwa Nivemba 8, huu.

Hatua hiyo inakuja baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali, Janeth Magoho kuiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo umekamilika na kumsomea mshtakiwa huyo maelezo ya awali (PH).

Kabla ya kusomewa PH, Halima alikumbushwa shtaka hilo linalomkabili, kuwa alitenda kosa Julai 3 mwaka huu, katika Makao Makuu ya Chadema Kinondoni.

Anadaiwa kumtusi Rais kiwa "anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa Amani.

Akisomewa PH, Halima amekubali maelezo yake binafsi likiwamo jina lake, anaishi Makongo, yeye ni Mbunge na Siku ya tukio ya Julai 3,2017 alikuwa katika fisi ya Chadema.

Aidha, amekanusha kumtukana Rais wa Januhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli.Akiendelea kusomewa PH na wakili Magoha mshtakiwa Halima alikubali kuwa Julai 4, mwaka huu alikamatwa katika eneo la Kibangu wilaya Kinondoni na kupelekwa kwa katika ofisi ya ZCO kwa mahojiano.

Hata hivyo, Halima alikana maelezo ya kuwa wakati akihojiwa alikubali kuwa alitoa lungha ya matusi dhidi ya Raid Magufuli.Kitu kingine alichokubali ni kufikishwa mahakamani kukabiliana na kesi inayomkabili. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 8, itakapoanza kusikilizwa.

TAMKO LA WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO UMMY MWALIMU KUHUSU SIKU YA SIKU YA AFYA YA MACHO DUNIANI


WATENDAJI WAZEMBE KUSIMAMISHA: BENJAMIN SITTA

$
0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amefungua semina ya mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa mtaa, kata na wenyeviti wa mtaa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali katika maeneo yao kabla hayajafika ngazi za juu.

Akizungumza mara baada kuzindua mafunzo hayo mstahiki meya Benjamin Sitta amesema kuwa kuna kero nyingi sana katika manispaa ya Kinondoni hivyo kupitia semina hiyo watakumbushwa wajibu wao katika kuwahudumia wananchi na hatimae kero hizi zitaishia ngazi ya chini kwani zipo ndani ya uwezo wao.

"Tumeshuhudia viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya, mkuu wa mkoa na Rais John Pombe Magufuli wakisimamishwa na wananchi na wakiambiwa kero ambazo zipo chini ya uwezo wa viongozi wa kata jambo ambalo si sahihi" Alisem Meya Sitta.

Katika hatua nyingine Mstahiki Meya Sitta ameahidi kutowafumbia macho watendaji wazembe kwani wanarudisha nyuma kasi ya maendeleo inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli.

"Tutawachukulia hatua kali watendaji wazembe ikiwemo kuwasimamisha tumeisha anza na mmoja na wengine watafuata kwani manispaa imelipa fidia ya zaidi ya bilioni 10 kutokana na watendaji wasio tambua majukumu yao, ila wale wenye kufanya vyema tutawapongeza kwa kutambua mchango wao" Alisema Meya Sitta.

Kwa upande wake Marry Asei Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema mafunzo hayo ni matunda ya ziara ya Dar Mpya chini ya Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akizungumza katika semina ya mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa mtaa, kata na wenyeviti wa mtaa  lengo ni kuwajengea uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali, leo jijini Dar es Salaam.


Sehemu ya watendaji wa mtaa, kata na wenyeviti wa mtaa wakimsikiliza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

VIGOGO WAWILI CHUO CHA UHASIBU (TIA) WAPANDISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Vigogo wawili wa chuo cha uhasibu (TIA) jijini Dar es Salaam, leo wamepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka mawili, la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni moja.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa, Leornad Swai amewataja watuhumiwa hao kuwa ni, Shaha Mussa Hanzuruni na Onesphory Ambangile Luhungu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba imedaiwa, kati ya January Mosi 2012 na Desemba 30 2014, katika chuo hicho cha TIA kilichopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam washtakiwa hao walitenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka.

Imedaiwa, washtakiwa, walitumia vibaya madaraka yao kwa kutofuata taratibu za manunuzi katika ununuzi wa ardhi wa chuo hicho (TIA) kampasi uya Mwanza na kimsababishia Vedasto Lupungo kupata manufaa ya Sh.1,097,681,107./-

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo washtakiwa hao kwa ridhaa zao na matendo yao waliisababishia TIA Hasara ya Sh. 1,097,681,107/- kwa kutokifuata sheria za manunuzi wakati wa kusaini mkataba wa ardhi Wa eneo la TIA kampasi ya Mwanza.

Kwa kuwa DPP ameipa mamlaka mahakama ya Kisutu kisikiloza kesi hiyo ya uhujumu uchumi, washtakiwa walipata nafasi ya kijibu juu ya tuhuma hizo ambapo wote wamekana kutenda makosa hayo na mahakama ikawasomea masharti ya dhamana kwa kuwa kesi hiyo inadhaminika

Akisoma masharti ya dhamana, Hakimu Simba amewata washtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaoweka bondi ya milioni 250 kila mmoja, pia amemtaka mdhamini mmoja kati ya hao kuweka mahakamani pesa taslimu, milioni 250 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha ambayo Ipo ndani ya mkoa wa DSM.

Pia wametakiwa kuwasilisha Pasi zao za kusafiria vilevile hawaruhusiwi kusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila ruhusa ya maandishi kutoka mahakamani hapo.

DC ARUSHA MJINI AWATAKA WANANCHI KUJIANDIKISHA VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Fabian Daqqaro amewataka wananchi wa wilaya ya Arusha Mjini Kuchangamkia zoezi la Uandikishwaji Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambalo linaendelea katika kata tatu za Wilaya hiyo.
 Akizungumza katika kipindi cha Goodmorning Tanzania kinachorushwa na kituo cha Matangazo cha Redio cha Redio 5 Arusha Daqqaro, amesema kuwa zoezi hili lina manufaa makubwa kwa wananchi na watanzania kwa ujumla lakini pia vitambulisho hivyo vitawawezesha watanzania kutambulika kila mahala, pamoja na raia wa kigeni kufanya shughuli zao bila usumbufu ikiwa ni pamoja serikali kuwa na taarifa sahihi za wananchi.
 Aidha amesema kuwa wananchi wasisubiri mpaka zoezi hilo kufikia tamati ndio kujitokeza Kwa wingi  kwa kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha msongamano na usumbufu mkubwa kwa wananchi.
“Naomba niwafahamishe na kutoa rai kwa wananchi wangu wajitokeze kwa wingi katika zoezi hili na wasisibirie siku kubaki chache ndio wajitokeze kwa kuwa kunapelekea usumbufu mkubwa sana hivyo,zoezi hili pia litakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi”alisema fabian

 Pia ametaka kila mwananchi kushiriki zoezi hilo na kutolihusisha na masuala ya kisiasa kutokana na umuhimu wake,kwa kuwa lengo ni kutambua na kusajili na kutoa vitambulisho vya taifa.

Afisa kutoka mamlaka hiyo wilaya ya Arusha Mjini  Juliette Raymond  Amesema lengo la zoezi hilo ni kuwezesha serikali kutambua wananchi wake wapo wapi na wanafanya nini ilimradi  anaishi ndani ya mipaka ya Tanzania ,hivyo zoezi hilo ni  lazima kwa kila mtu kwa Mujibu wa sheria.

Kwa wilaya ya Arusha Mjini zoezi hilo linaendelea katika kata ya Sombetini,Sekei na Themi ambapo zoezi hilo linafnyika katika Halmashauri ya Jiji la Arusha katika kata ya Sekei,Themi katika viwanja vya nane nane na Sombetini Ofisi za Mtendaji kata eneo la Mbauda Sokoni.

MAMBO SITA MUHIMU UNAPOPEKULIWA NA ASKARI.

$
0
0


Na Bashir Yakub.

napopekuliwa yapo mambo ambayo usipoyazingatia wewe unayepekuliwa basi yatakuingiza matatani mbeleni au hata kama umebambikiziwa kosa itaonekana ni kweli na waweza kwenda jela bila kuwa umetenda kosa lolote.

Kawaida wanaopekua ni askari. Usitarajie huyu anayekuja kukupekua awe ndiye wa kukwambia haki zako . Badala yake wewe unayepekuliwa ndiye uwe wa kumwambia askari kuwa hiki ndicho hiki hapana.

Askari anapokuja kukupekua tayari wewe unashukiwa na hivyo ni rahisi kwake kuacha kufuata au kuongeza jambo lisilokubalika ilimradi atimize lengo lililomleta. Wewe ndiye wa kusema hili ndio na hili hapana. 

Hivyo basi ni muhimu sana kwako kujua kuhusu kupekua na mambo gani ya msingi ufanyiwe au usifanyiwe ili kuepuka uwezekano wa kwenda jela bila kosa. 

Usiseme mimi sina haja ya kujua kuhusu kupekua kwasababu ni mwema sana na hivyo si rahisi kutakiwa kupekuliwa. Laa hasha, kupekuliwa na kukamatwa na polisi humkumba yeyote awe mwema ama vinginevyo. Kujua ni silaha na hivyo ni muhimu kukaa na silaha hii. 

Makala yatapitia sura ya 20, vifungu vya 38 hadi 45 vya Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai . 

1. NANI ANARUHUSIWA KUKUPEKUA.

Askari ndiye anayeruhusiwa kukupekua. Hata raia wanaweza kumzuia raia mwenzao wakampekua ikiwa wana taarifa kuhusu kuficha au kumiliki kitu ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria. Isipokuwa ni haramu kabisa kwa raia kumpekua raia mwenzake bila kuwa na kibali maalum. 

2. VITU GANI VINAWEZA KUPEKULIWA. 

Mtu kama mtu anaweza kupekuliwa, kwa maana nguoni mwake kama mifukoni nk. Pia vifaa kama gari, ,meli, nk navyo vyaweza kupekuliwa. Halikadhalika nyumba kama nyumba nayo yaweza kupekuliwa pamoja navyo vifaa vingine. 


BINTI FOUNDATION YATOA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE,SHUELE YA MSINGI HANANASIFU JIJINI DAR

$
0
0

 Mkurugenzi wa taasisi ya Binti Foundation Johari Sadiq akizungumza mapema leo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),Katika hafla fupi ya utoaji wa msaada wa vifaa vya shule mbalimbali katika shule ya msingi ya Hananasisifu,jijini Dar,ikiwa ni sehemu yao ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike,ambapo Kitaifa inaadhimishwa mkoani Mara,Pichani kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Hananasifu  Idda Uisso.
 Mkurugenzi wa taasisi ya Binti Foundation Johari Sadiq akimkabidhi Mwalimu Mkuu Idda Uisso baadhi ya vifaa vya shule ikiwemo Madaftari,Sale za Shule,Kalamu na vinginevyo kwa ajili ya wanafunzi ambao wanaishi katika mazingira magumu na hawajiwezi.Binti Foundation imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike,ambapo Kitaifa inaadhimishwa mkoani Mara.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Hananasisifu Idda Uisso akitoa neno la shukurani kwa taasisi ya Binti Foundation kwa msaada wao walioutoa kwa shule hiyo,Mwalimu Idda ameziomba taasisi nyingine zenye uwezo kujitokeza kuwasadia watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi wasiojiweza.
Mkurugenzi wa taasisi ya Binti Foundation Johari Sadiq na baadhi ya wadau wa taasisi hiyo wakishiriki kwa pamoja kugawa vifaa vya shule kwa wanafunzi mbalimbali ambao wanaishi katika mazingira magumu na hawana uwezo.
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live




Latest Images