Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

WASHINDI WA PROMOSHENI YA COCA-COLA WAKABIDHIWA ZAWADI

$
0
0
Promosheni ya ‘Mchongo chini ya kizibo’iliyozinduliwa na Coca-Cola mkoani Mwanza wiki iliyopita imeanza kuibua washindi ambapo wakazi wawili wa jijini Mwanza wamejishindia Televisheni na wengine 2 kujishindia fedha taslimu shilingi 100,000/-kila mmoja wao. 
Promosheni hii inahusisha vinywaji vya Coca-Cola, Fanta, Sprite, Tangawizi, Sparleta na Novida na inafanyika mkoani Mwanza na mikoa mingine ya kanda ya ziwa ikiwemo mikoa jirani yake ya Shinyanga na Kigoma na itawawezesha wateja kujishindia zawadi nono za fedha taslimu zaidi ya milioni 400,bodabado 100,televisheni 60 aina ya SONY LED zenye inchi 32,T-shirts , kofia na soda za bure. Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi jijini Mwanza, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi,alisema lengo la promosheni hii kubwa ni kuwazawadia na kuwashukuru wateja wanaotumia bidhaa za kampuni 
“Tumewaletea promosheni hii kwa ajili ya kuwashukuru wateja wetu wote wanaotumia bidhaa zetu kama mnavyoona leo washindi wa promosheni hii wamekabidhiwa zawadi zao,natoa wito kwa wananchi kuzidi kuichangamkia ili kujishindia zawadi kwa kuwa bado kuna zawadi nyingi za kushinda”alisema Kisusi. 
Mmoja wa washindi wa TV,Fred Charles mkazi wa kitongoji cha Buzuruga akiongea kwa furaha alisema kuwa hakuamini macho yake baada ya kunywa soda ya Coca-Cola na kukuta ina kizibo cha zawadi ya TV “Kilichonifurahisha zaidi ni jinsi ambavyo nimeweza kukabidhiwa zawadi yangu kwa haraka,natoa wito kwa wakazi wa Mwanza tuchangamkie promosheni hii tuweze kujishindia zawadi kama nilivyoshinda mimi”alisema. 
Naye Rashid Mlobelo mkazi wa kitongoji cha Nyegezi jijini Mwanza alisema amefurahishwa na zawadi aliyoipata kupitia promosheni ya ‘Mchongo chini ya kizibo’ alisema kuwa fedha alizozipata zitamsaidia kununua mahitaji mbalimbali Washindi wengine waliokabidhiwa zawadi ni Davis Gombanila aliyejishindia TV na Abdul Khalfan aliyejishia shilingi 100,000/-
Mshindi wa kitita cha 100,000/-Abdul Khalfan (kulia) akipokea fedha zake kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola,Mwanza,Samwel Makenge
Washindi wa promosheni ya Mchongo chini ya kizibo wakiwa na zawadi zao baada ya kukabidhiwa jijini Mwanza jana.
Mshindi wa Televisheni, Fred Charles akipokea zawadi aliyojishindia kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola, Mwanza-Samwel Makenge
.Mshindi Davis Gombanila akikabidhiwa zawadi ya televisheni
Mshindi Rashid Mlobelo akikabidhiwa kitita cha shilingi 100,000/-alizojishindia

UTPC yawanoa waandishi wa habari Dodoma

$
0
0
Na.Vero Ignatus,Dodoma

Umoja  wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) inaeendesha mafunzo ya siku (5) ya waandishi  habari za mazingira (27)mkoani Dodoma, kwa waandishi kutoka mikoa yote nchini ikiwa ni awamu wa kwanza

Afisa program wa (UTPC) anayefanya kazi kitengo cha Mafunzo ,Utafiti na Machapisho Victor Maleko amesema kuwa  lengo kubwa la mafunzo hayo ni  kuwapata waandishi waliobobea katika kuandika habari za mazingira katika maeneo yao.

"Unapowapata wabobezi hawa ni rahisi kwa wadau wa habari kutoka mikoani kufanya kazi na waandishi amabao wapo madhubuti kwenye maeneo yao,wapo waandishi wengi makanjanja hawajui wanachokifanya"alisema Victor.

Mafunzo mengine yanayoendeshwa sambamba na haya ni pamoja na  mkoani Pwani yanaendelea mafunzo ya uandishi wa habari za Jinsia ,mkoani Morogoro yanaendelea mafunzo ya uandishi wa habari za Vijijini na mkoani Dodoma mafunzo ya uandishi wa habari za Mazingira

"tunataka tuwapate machampion watakao simamia habari za mazingira peke yayake,Jinsia  pamoja na  waandishi wa habari za vijijini tu"alisema

Amewaasa waandishi wa habari ambao hawajajiunga katika vilabu vya waandishi  habari vilivyopo kila mkoa wajiunge  kwani zinawasaidia kuwakutanisha pamoja watanufaika na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na UTPC ,ambapo amesema  mafunzo kama haya hayawezi kutolewa kwa mwandishi ambaye siyo mwanchama .

Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo Deodatus Mfugale amesema kuwa lazima mwandishi awe na malengo,waandike habari zinazoleta mabadiliko na zinazogusa hisia za jamii kwa ujumla.''Mwandishi kama unaandika kila kitu muda wako unakaribia kwisha"alisema Mfugale.

Amesema kuwa UTPC itaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa habari chini ufadhili wa Ubalozi wa Sweeden hapa nchini kwa muda wa miaka (5) ambapo huu ni mwaka wa( 2) hadi 2020 wataendelea kubadilisha mafunzo hayo kadri ya  uhitaji wa waandishi .
 Muwezeshaji wa mafunzo Deodatus Mfugale akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Centurion Nala Hotel Dodoma
Afisa program wa (UTPC) anayefanya kazi kitengo cha Mafunzo ,Utafiti na Machapisho Victor Maleko akizungumza na waandishi katika Mafunzo hayo mkoani Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo hayo

JAMII ISAIDIE KUTATUA TAZIZO LA UGONJWA WA MDOMO WA SUNGURA

$
0
0
Miss Universe Tanzania, Jihan Dimachk akiwa na wazazi na watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa ugonjwa wa midomo sungura.
 Mmoja wa watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa ugonjwa wa midomo sungura wakati wa siku ya "Smile day" akishiriki katika siku hiyo.
 Miss Universe Tanzania, Jihan Dimachk akiwa na mmoja wa watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa ugonjwa wa midomo sungura wakati wa siku ya "Smile day" kwenye hospitali ya CCBRT ya jijini. anayemfuatia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans.
 
Miss Universe Tanzania, Jihan Dimachk akiwa na 
wafanyakazi wa hospitali ya CCBRT wakati wa 
siku ya "Smile day" iliyofanyikia kwenye 
hospitali hiyo.


Na Mwandishi wetu.
Miss Universe Tanzania ambayo uandaliwa na kampuni ya Compass Communications chini ya mkurugenzi, Maria Sarungi Tsehai, Jihan Dimachk ameiomba jamii kusaidia watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa midomo sungura (Mdomo wazi) kupata matibabu yanayofaa.

Jihan alisema hayo wa maadhimisho ya "Smile day" katika hospitali ya CCBRT ya jijin kwa kushirikiana taasisi ya Smile Train Africa linalojishughulisha na utatuzi wa tatizo la mdomo sungura.

Jihan ambaye ni balozi wa shirika hilo alisema kuwa jamii inatakiwa kuwakubali na kushirikiana katika kutatua tatizo hilo ambao linawaathiri sana watoto wadogo.

Alisema kuwa taasisi ya Smile Train Africa linatambua tatizo la ugonjwa huo kwa watoto ambao ukosa raha katika kula na kufanya mambo mengine muhimu.

"Nimefarijika sana kuwa balozi wa Taasisi ya Smile Train Africa na hasa katika kuondoa tatizo la ugonjwa wa Mdomo Sungura, naomba Jamii iunge mkono juhudi za taasisi hii kwani jukumu letu sisi,"

"Ugonjwa huu upo mikoa mingi na watoto wanahitaji msaada wa kufanyiwa upasuaji na gharama za matibabu na gharama ni kubwa, nimeguswa sana na tatizo hili, " alisema.

Taasisi ya Smile Train Afrika hutoa msaada wa kifedha na vifaa ili kusaidia kufidia gharama kwa ajili ya upasuaji. Uwekezaji wote huu si tu kwamba unawezesha upasuaji mkubwa lakini pia unafanya upasuaji huu uwe salama na wa ubora wa hali ya juu.

TANZIA: FAMILIA YA MZEE MLONDOYE WA MBEYA MJINI WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BABA YAO MZEE RAPHAEL MLONDE

$
0
0
Watoto wa marehemu mzee Raphael Mlondoye Msyaliha wa Mbeya mjini wanasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpendwa mzee Raphael Mlondoye Msyaliha aliyefariki usiku wa kuamkia tarehe 10 Oktoba 2017 katika Hospital ya Rufaa.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Mbeya mjini karibu na hospitali ya Rufaa. Habari ziwafikie watoto wote wa marehemu, wana ukoo wote wa Msyaliha,Shonza,Shura,Mwamlima,Paza,sijabaje,halinga,mgala,ntenga,Ntengwi,Mwashambwa,Njeje na Mwawalo , ndugu wote na jamaa wa marehemu wateja na wadau wote wa Victoria Engeneering.

Mazishi yamepangwa kufanyika Mbozi kijiji cha Igale kata ya Iyula siku ya Alhamis tarehe 12 mwezi wa 10 2017.
Mwenyezi MUNGU ailaze roho ya marehemu baba yetu mahala pema peponi.

WATU WANNE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 30 NA VIBOKO 12.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu  Mkazi Kisutu imewahukumu watu wa nne kutumikia kifungo cha mika 30 jela na kuchapwa viboko 12, sita wakati wa kuingia na sita wakati wa kutoka baada ya kupatikana na hatia dhidi ya kosa la wizi wa kutumia silaha.

Hukumu hiyo iliyosomwa na hakimu Mkazi, Respicious Mwijage imewataja waliofungwa kuwa ni Donald Nzweka, Michael Pascal,Ally Akili na Kurwa Mwakagenda.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mwijage amesema, upande wa mashtaka umeweza kuthiitisha kosa hilo pasipo kuacha shaka na kuwa washtakiwa walishiriki kutenda kosa na kwamba mahakama ilijiuliza kwamba kosa la kutumia silaha ili lithibitike Jamhuri wana wajibu wa kuthibitisha bila kuacha shaka kwamba mshtakiwa kabla ya kutenda awe na kifaha hatari au wawe zaidi ya mmoja na kwamba baada ya tukio hilo walitumia nguvu kwa mtu waliyeporwa.

Katika kesi hii, mlalamikaji na mashahidi wengine walieleza kuwa usiku wa julai 7 majambazi walivunja mlango mkuu wa nyumba yao kwa kutumia bomu ambalo lilitambuliwa na polisi kuwa baruti na kasha kuendelea kuvunja milango mingine ambapo baada ya hapo waliingia katika chumba walichokuwa wamekaa, ambacho kilikuwa na mwanga, mshtakiwa mmoja alishika panga na kuanza  kuwapiga kwa kutumia ubapa.

Amesema, kwa kuzingatia ushahidi huo hakuna shaka kwamba mashahidi waliweza kuwatambua  majambazi na kuwa utetezi wa washtakiwa kwamba walikamatwa maeneo tofauti na kupelekwa oysterbay polisi na kupigwa na kunyanyaswa siyo ya kweli.

Kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo, Hakimu Mwijage aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote na kusema juu ya washtakiwa ambapo wakili wa serikali Gloria Mwenda, alidai washtakiwa ni  wakosaji wa mara ya kwanza na akaomba wapewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa jamii.

“Nimeridhika ushahidi wa mashahidi 11 walioletwa na upande wa mashtaka ambao wameweza kuthibitisha bila ya kuacha shaka kuwa mlitenda kosa, nawahukumu kwenda jela miaka 30 na kuchapwa viboko 12, sita siku mnaingia na sita siku ya kutoka" amesema Mwijage.

Awali ilidaiwa, Julai 7 ,2013 huko maeneo ya Boko Magengeni, jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao waliiba simu nne pesa taslimu  150,000 na cheni za dhababu mbili ambapo vitu vyote vina thamani ya  2050,000 mali ya Hobokela Mwakijambile.

BAADHI YA WANAFUNZI WAKIKE WANUFAIKA NA ELIMU TOKA VODACOM TANZANIA YA KUSHIKA NYADHIFA MBALIMBALI KATIKA JAMII KUELEKEA SIKU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE KESHO.

$
0
0
IKIWA ni kuelekea siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho,Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, Imeanza kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa kutoa elimu ya uwezo wa mtoto wa kike kuweza kushika nyadhifa mbalimbali katika jamii ikiwa ni matayarisho ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho kwa baadhi ya wanafuzi wakike wa Shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo mbezi Beach jijini Dar as Salaam.

"Akiongelea kuhusiana na mafunzo waliyokuwa wanayatoa kwa wanafunzi hao,Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Jacquiline Materu alisema wamefurahia sana kupata frusa ya kuwafundisha wasichana hao na kuwapa motisha kwamba hakuna mipaka ya kufikia malengo yao ya hapo baadaye bali ni juhudi zao wenyewe kamwe wasije kukata tamaa kwani wanaweza"Alisema Materu.

Mkuu huyo alifafanua zaidi kwamba pamoja na kuwawezesha wanawake na kukuza usawa wa kijinsia ni muhimu kuharakisha maendeleo endelevu. Kumaliza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana ili haki za msingi za kibinadamu ziweze kufanyiwa kazi kwani kuna athari nyingi kwa maeneo ya Taifa letu. Alisema.

"Bado hakuna usawa katika upatikanaji wa ajira na ulipwaji wa mishahara ulimwenguni na bado kuna mapungufu makubwa kati ya wanaume na wanawake katika soko la ajira"

Mkuu wa kitengo cha ripoti na taarifa M-Pesa,Nelusigwe Mwangota(kushoto)akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wakike wa shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo kunduchi beach jijini Dar es Salaam,kuhusiana na uwezo wa mtoto wa kike kuweza kushika nyadhifa mbalimbali katika jamii ikiwa ni matayarisho ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho ikiwa ni chini ya lengo namba tano la mpango wa maendeleo- Usawa wa Kijinsia ,Wanafunzi hao walitembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania PLC moroko jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo kunduchi beach jijini Dar es Salaam waliotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania PLC yaliyopo moroko jijini Dar es Salaam,wakipokea zawadi toka kwa Mkurugenzi wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Harriet Rwakatare baada ya kuwaelimisha juu ya uwezo wa mtoto wa kike kuweza kushika nyadhifa mbalimbali katika jamii ikiwa ni matayarisho ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho ikiwa ni chini ya lengo namba tano la mpango wa maendeleo- Usawa wa Kijinsia.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wanafunzi wakike wa shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo kunduchi beach jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi baadhi ya wanafunzi wakike wa shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo kunduchi beach jijini Dar es Salaam wakati wanafunzi hao walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo moroko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujifunza njinsi ya uwezo wa mtoto wa kike kuweza kushika nyadhifa mbalimbali katika jamii elimu hiyo ilitolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni matayarisho ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho ikiwa ni chini ya lengo namba tano la mpango wa maendeleo- Usawa wa Kijinsia.
Mkuu wa kitengo cha cha maduka ya rejareja ya Vodacom Tanzania PLC, Brigita Stephen(kushoto)akiongea na baadhi ya wanafunzi wakike wa shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo kunduchi beach jijini Dar es Salaam kuhusiana na uwezo wa mtoto wa kike kuweza kushika nyadhifa mbalimbali katika jamii ikiwa ni matayarisho ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani hapo kesho ikiwa ni chini ya lengo namba tano la mpango wa maendeleo- Usawa wa Kijinsia ,Wanafunzi hao walitembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo moroko jijini Dar es Salaam.

TAARIFA KWA UMMA

$
0
0


TAARIFA KWA UMMA

Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya umeandaa Misa Maalum ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itakayofanyika tarehe 14 Oktoba, 2017 katika Kanisa la Holy Family Basilica, Nairobi kuanzia saa 4.00 hadi saa 5.00 asubuhi.

Watanzania wote pamoja na ndugu, jamaa na marafiki mnakaribishwa kushiriki katika Misa hii. Kufika kwenu kwa wingi ndio kufanikisha shughuli yetu sote.



TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU ZA  DHATI.



IMETOLEWA NA:

UBALOZI WA TANZANIA

NAIROBI, KENYA

10 OKTOBA, 2017

ASKARI WAWILI WAFARIKI DUNIA NCHINI CONGO-JWTZ


WALEMAVU WA KUSIKIA MBEYA WAPEWA SOMO NA BENKI KUU JINSI YA KUBAINI NOTI BANDIA.

Zawadi za shs milioni 204 kushindaniwa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC.

$
0
0
 Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbagala,  Sady Mwang’onda (wa pili kulia) na Meneja Bidhaa za Uwekezaji wa benki hiyo, Dorothea Mabonye (wanne kushoto), wakikata utepe kuashirikia uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya NBC. Kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu na kufanyika nchini kote itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi wengine 24 watajishindia kila mmoja zawadi ya pesa taslimu shs milioni moja hivyo kufanya jumla ya zawadi zote kufikia thamani ya shs milioni 204. Hafla hiyo ilifanyika katika tawi hiyo, Dar es Salaam leo. Wengine ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo.
 Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbagala,  Sady Mwang’onda (katikati), Meneja wa Bidhaa za Uwekezaji wa benki hiyo, Dorothea Mabonye (kulia kwake), na Mkuu wa  Bidhaa na Wateja Rejareja, Andrew Lyimo (kushoto kwake), pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo wakishangilia mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya NBC uliofanyika katika tawi hilo, Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu na kufanyika nchini kote itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi wengine 24 watajishindia kila mmoja zawadi ya pesa taslimu shs milioni moja.
  Mkuu Bidhaa na Wateja Rejareja wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo (katikati), akihojiwa na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya NBC uliofanyika katika tawi Mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu na kufanyika nchini kote itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi wengine 24 watajishindia kila mmoja zawadi ya pesa taslimu shs milioni moja.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MABALOZI WA UGANDA, CUBA NA IRAN KWA NYAKATI TOFAUTI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Mabalozi kutoka nchi tatu kwa wakati tofauti ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais alianza kwa kukutana na Balozi Mpya wa Uganda hapa nchini Mhe. Richard T. Kabonero ambaye alifika kuonana na Makamu wa Rais kwa mara ya kwanza ambapo alitumia nafasi hiyo kujitambulisha.

Katika mazungumzo na Makamu wa Rais, Balozi Kabonero alizungumzia nia ni ya dhati ya nchi yake katika kudumisha na kuimarisha uhusiano wa kindugu baina ya Tanzania na Uganda hasa ushirikiano wa kijamii, na kiuchumi ambapo tafiti za mafuta zinazoendelea katika ziwa Eyasi, mashirikiano ya sekta ya anga ili kusaidia kukuza utalii, mradi wa ujenzi ya reli ya kati na mradi wa umeme vijijini pamoja na kuanzishwa kwa jukwaa la biashara la sekta binafsi kutoka nchi husika ili kuweza kunufaika na fursa zitakazojitokeza baada ya kukamilika bomba la mafuta .

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewapongeza wananchi wa Uganda kwa kutimiza miaka 55 ya Uhuru.Pia aliipongeza Uganda kwa kutafiti na kugundua mafuta kwa kutumia wataalamu wazawa ambapo alisisitiza ushirikiano wa kitaalamu na wataalamu wa Tanzania.

Makamu wa Rais amemtakia heri na fanaka katika majukumu mapya ya Ubalozi wa Uganda hapa Tanzania na kumhakikishia ushirikiano wa Serikali.Makamu wa Rais alimalizia mazungumzo yake na Balozi huyo wa Uganda hapa nchini kwa kutoa shukrani zake za dhati kwa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kwa ushirikiano wake walioutoa wakati wa ajali mbaya ya gari iliyowakuta Watanzania waliokuwa wanatoka Harusini ambapo watanzania 13 walifariki.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Uganda nchini Mhe. Richard T. Kabonero aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha na kufanya mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja Balozi mpya wa Uganda nchini Mhe. Richard T. Kabonero mara baada ya kumaliza mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Cuba nchini Mhe. Lucas Domingo Hernandez . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Iran nchini Mhe. Moussa Farhang aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa mazungumzo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kitabu chenye historia ya miji ya Iran ambacho alikabidhiwa na Balozi wa Iran nchini Mhe. Moussa Farhang aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa mazungumzo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

TAARIFA KUTOKA JWTZ: ASKARI WAWILI WA TANZANIA WAUWAWA DRC

MAKUSANYO YA TRA YAVUKA TRILIONI 1 KWA MWEZI

$
0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kutoa taarifa ya makusanyo ya mapato ya kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018. Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2017, TRA imekusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.65.

Makusanyo haya ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.2 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Katika kipindi hicho cha miezi mitatu, makusanyo ya kila mwezi yalikuwa kama ifuatavyo;-

Julai, 2017 Shilingi 1,101,193,417,551.91

Agosti, 2017 Shilingi 1,205,008,256,053.51

Septemba, 2017 Shilingi 1,345, 339,916,757.65
Kwa makusanyo haya, Mamlaka ya Mapato Tanzania, inapenda kuwashukuru wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla kwa kuendelea kulipa kodi na kuiwezesha serikali kutimiza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

Aidha, Mamlaka inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wote kutoa risiti za kielektroniki kwa kila mauzo na kudai risiti kwa kila manunuzi kwani ni njia pekee ya kupata mauzo sahihi yanayoiwezesha TRA kukokotoa kodi sahihi na kwa haki.

“Napenda kuwakumbusha wananchi wote kuhakiki risiti zao ili kuona usahihi wa tarehe na kiasi walicholipa na bidhaa waliyonunua kabla ya kuondoka na risiti hiyo. Endapo utaona haina vigezo tafadhali ripoti kwenye ofisi ya TRA iliyokaribu nawe au piga simu kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa namba0800750075 au 0800780078. anasisitiza Richard Kayombo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi

Vile vile, Mamlaka inawakumbusha wamiliki wa majengo nchini kulipa kodi ya majengo mapema badala ya kusubiri mwishoni mwa mwaka wa fedha ili kuepuka misongamano na usumbufu usio wa lazima.

Pia, wafanyabiashara wa michezo ya kubahatisha wanapewa wito wa kulipakodi zao kwa mujibu wa sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41.
‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu.



Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo akiongea na waandishi wa habari Dar es Salam leo Oktoba 10 2017 alipotoa takwimu za makusanyo ya zaidi ya Trilioni 1 kwa Mwezi kwa mamlaka hiyo kwa miezi ya Julai, Agosti na Septemba 2017. Pamoja naye afisa kodi Mkuu, Julius Ceaser.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo akiongea na waandishi wa habari Dar es Salam leo Oktoba 10 2017 alipotoa takwimu za makusanyo ya zaidi ya Trilioni 1 kwa Mwezi kwa mamlaka hiyo kwa miezi ya Julai, Agosti na Septemba 2017. Pamoja naye Maafisa kodi wakuu, Julius Ceaser (kushoto) na Sydney Mkamba.

NAIBU WAZIRI AWESO AKAGUA MIUNDOMBINU YA MAJI UBUNGO

$
0
0

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji leo amefanya ukaguzi wa miundombinu ya maji eneo la Ubungo na kujionea miundombinu hiyo ambayo mingi imepasuka na kuvujisha maji mengi kutokana na uchakavu au kuhujumiwa miundombinu hiyo.


Katika maeneo aliyopita ameweza kuona upotevu mkubwa wa maji unaotokana na mabomba yaliyopasuka kuvuja, na kusababisha maji mengi kupotea baada ya kuwafikia wananchi kwa ajili ya matumizi.


Naibu Waziri Aweso alisema ipo haja ya kuchukua hatua na kuhakikisha miundombinu hiyo inafanyiwa ukarabati, ili kudhibiti tatizo la upotevu wa maji ambalo limekuwa changamoto kubwa jijini Dar es Salaam.


“Nitakaa na taasisi za DAWASA na DAWASCO tuweke mikakati ya kutatua changamoto hii, ili kuhakikisha kiwango cha upotevu wa maji kinapungua, kwa kuwa ni moja sababu ya wananchi kukosa maji ya uhakika, kwa kuwa mengi yanapotea baadala ya kuwafikia walengwa”, alisema Naibu Waziri.
 Fundi wa DAWASCO akiendelea na kazi ya kurekebisha bomba lililopasuka eneo la Riverside, Ubungo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na msimamizi wa matengenezo wa DAWASCO Kanda ya Tabata, aliyekuwa akisimamia matengenezo katika eneo la Riverside, Ubungo kwenye moja ya miundombinu ya maji iliyoharibika.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa katika eneo la Kibangu, Ubungo akikagua moja ya maeneo yaliyo na miundombinu mibovu ya maji.


WAZIRI KAIRUKI AELEZEA VIPAUMBELE VYAKE

$
0
0
Greyson Mwase na Asteria Muhozya.

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ameeleza vipaumbele  vyake katika Wizara kuwa ni pamoja na  udhibiti wa utoroshaji wa madini nchini, maslahi kwa wafanyakazi huku akiwataka watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu.

Kairuki ameyasema hayo mapema leo tarehe 10 Oktoba, 2017 jijini Dar es Salaam  alipozungumza na  watumishi wa Wizara ya Madini pamoja na taasisi zake, waliopo Dar es Salaam na Makao Makuu  ya Wizara Dodoma. Lengo La kikao hicho lilikuwa ni kufahamiana na kupanga mikakati  ya kushirikiana ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa Uchumi wa nchi.

Taasisi zilizoshiriki katika kikao hicho ni pamoja na  Wakala wa Jiolojia  Tanzania (GST), Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO), Chuo cha Madini Dodoma (MRI) pamoja na Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini na Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji (TEITI).

Amesema kuwa Sekta ya Madini  inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuwataka wataalam wa madini kubuni mbinu za ukusanyaji wa maduhuli pamoja na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye uchimbaji madini.

Katika hatua nyingine aliwataka wataalam hao kubuni mikakati  ya kuzuia utoroshaji wa madini nchini ili nchi ipate mapato stahiki.Amewataka watumishi kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuwa wabunifu ili  sekta hiyo iwe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Naye Naibu  Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewakumbusha  watumishi kuzingatia Dira na Dhima ya Wizara  ikiwemo kufanya kazi kwa tija ili hatimaye  sekta ya madini iweze kuchangia katika uchumi wa nchi kwa kuwa mchango wa sekta husika bado ni kidogo.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki  (kushoto) akitoa maelekezo kwa watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake (hawapo pichani) Kulia ni Naibu  Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa iliyokuwa  Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (kushoto mbele) pamoja na watendaji wengine wa Wizara wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki. (hayupo pichani).
 Sehemu ya  watendaji wa Wizara ya Madini wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
 Naibu  Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia)  akifafanua jambo katika kikao hicho. Kushoto ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAFANYAKAZI WA STAMICO WAPATA MAFUNZO YA UKIMWI

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
SERIKALI imedhamiria kupambana na janga la Ukimwi ikiwa ni pamoja na kuandaa muongozo kwa wafanyakazi kupata elimu juu ya ugonjwa huo jinsi ya kujiepusha.

Hayo ameyasema Kaimu Mkurugenzi Masoko na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico),  Aloyce Tesha wakati akifungua semina ya wafanyakazi wa shirika hilo katika kupata elimu ya Ukimwi pamoja na magonjwa sugu yasiyoambukiza , amesema semina hiyo ni muhimu kwa wafanyakazi katika kuweza kujikinga na magojwa ili waweze kutekeleza majukumu yao.

Tesha amesema kuwa wafanyakazi wakipata elimu wanaweza kufundisha familia zao pamoja na jamii zinazowazunguka katika uchukua tahadhari.

Amesema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo wanakwenda sehemu mbalimbali za madini hivyo lazima wawe na elimu ya Ukimwi na magonjwa yasiyoambukiza.
 Afisa Mwitikio wa Taasisi za Umma kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk. Hafidh Ameir akizungumza wakati akitoa mada ya Ukimwi katika semina wa wafanyakazi wa Stamico.
 Kaimu Mkurugenzi na Uwekezaji wa Stamico, Aloyce Tesha akizungumza katika ufunguzi wa semina ya wafanyakazi wa Stamico juu ya Ugonjwa wa Ukimwi na Magonjwa yasiyoambukiza leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wafanyakazi wakisiliza mada katika semina hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji, Aloyce Tesha akiwa katika picha ya pamoja na wafanyazi wa stamico mara baada ya semina elimu ya ukimwi na Magonjwa yasiyoambukiza.

Sehemu ya kupimia ugonjwa wa kisukari. 

INTRODUCING: KIJANA BY KALA JEREMIEH

NDANDA FC YAUNDA MBINU ZA KUMFUNGA MAJIMAJI

$
0
0
Benchi la ufundi la timu ya ndanda fc umetamba kufanya vizuri katika mchezo wake dhidi ya majimaji fc kutoka mkoani Ruvuma wanalizombe utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii katika uwanja wa nangwanda sijaona mkoani Mtwara

NEWS ALERT: Raila Odinga ajiondoa kwenye uchaguzi mkuu wa marudio Kenya

$
0
0
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kuwa hatashiriki kwenye uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.
Bwana Odinga anasema anataka kufanyika uchaguzi mpya jinsi ilivyoamuliwa na mahakama ya juu.Uchaguzi huo wa tarehe 26 utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Bw. Odinga anasema amejiondoa ili kuipa tume ya uchaguzi IEBC muda wa kutosha kufanya mabadiliko ambayo yatawezesha kufanyika uchaguzi kwa njia nzuri.Awali tume ya uchaguzi ilikuwa imemtangaza rais wa sasa Uhuru Kenyatta kuwa mshindi.Ilisema kuwa Bw. Kenyatta alishinda uchaguzi huo kwa kura milioni 1.4.Upinzani nchini Kenya awali ulikuwa umetangaza wazi kuwa ungeshiriki kwenye uchaguzi mkuu ikiwa mabadiliko yanayostahili yangefanyika.

Upinzani unaamini kuwa uchaguzi unastahili kufutwa baada ya Odinga kujiondoa, na kutoa muda wa kutosha kufanyika mabadiliko yanayostahili ili uchaguzi kufanyika kuambatana na sheria na katiba.

Serikali imekuwa ikisema kuwa uchaguzi utafanyika na rais kuapishwa.Bw. Odinga pia ametoa wito kwa watu kuandamana kesho Jumatano kwa kutumia kauli mbiu "hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi".
Mwezi Septemba mwendesha mashtaka mkuu nchini Kenya Keriako Tobiko, aliamrisha polisi na tume ya kupambana na ufisadi kuchunguza ikiwa wanachama wa tume ya uchaguzi walihusika na uhalifu wowote.
Alitaka wachunguzi kuchunguza madai kuwa maafisa wawili wakuu wa upinzani walikuwa wamedukua mitandao ya tume ya uchaguzi.
Baadhi ya Viongozi wa NASA walipokuwa wakizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo kuhusiana na kujiondoa kwao kwenye uchaguzi mkuu  wa marudio. 

Introducing new single "Why" by Samatwizzy x Kyddo Brown

Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images