Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

IGP SIRRO AWASILI MKOANI SONGWE KWA ZIARA YA KIKAZI

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, alipowasili mkoa humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia pamoja na kuwakumbusha wajibu wa kutoa huduma bora kwa jamii. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili katika mkoa wa Songwe, kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia pamoja na kuwakumbusha wajibu wa kutoa huduma bora kwa jamii. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo na kupeana mbinu na mikakati namna ya kukabiliana na matukio ya uhalifu ikiwamo upitishaji wa magendo kutoka nchi jirani unaofanywa na watu wasiowema. IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi. 
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, wakiwa katika picha na  Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, baada ya kumaliza kikao kazi cha kupeana mbinu na mikakati namna ya kukabiliana na matukio ya uhalifu ikiwamo upitishaji wa magendo kutoka nchi jirani unaofanywa na watu wasiowema. IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.


MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA KUTANGAZA UTALII THAILAND

0
0

 Mtaribu wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Resorce Afrika Limited, Idrissa Songoro akizungumza kuhusu maandalizi ya ziara ya mafunzo ya Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA),nchi Thailand inayotarajia kuanza katilati ya mwezi ujao Novemba mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo, Adam Ngamange na Mwenyeikiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kisui . Kisui.UJUMBE wa Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) unaokwenda ziara ya mafunzo nchini Thailand, umejiandaa pia  kwenda kuutangaza utalii wa Tanzania.
 Songoro na viongozi wa Mkikita wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanamkikita wanaotarajia kwenda Thailand kwa ziara ya wiki moja.
 Dk. Kisui akielezea jinsi Mkikita ulivyojipanga kwa ziara hiyo, itakayowanufaisha wanachama kwa kukutana ana kwa anakwa mazungmzo  na wafanyabiashara na wakulima wa Thailand pamoja na kuingia nao mikataba mbalimbali. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Ngamange akifafanua jambo kwa wajumbe wa kikao hicho.

MAGIC FM BAMIZA TOP 20 COUNT DOWN 0CTOBER 7TH, 2017

Msimamo wa Askofu Niwemugizi Katiba Mpya Siyo wa Kanisa - Kadinali Pengo

CHUO CHA ST DAVID COLLEGE OF HEALTH: WAHI SASA MUHULA MPYA TAYARI UMEANZA.

0
0
CHUO CHA ST DAVID COLLEGE OF HEALTH KILICHOPO KIMARA TEMBONI DSM NI CHUO CHA KIPEKEE KATIKA UKANDA HUU WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KINACHOTOA KOZI ZA AFYA KWA NGAZI ZOTE ZA CHETI NA DIPLOMA.
PIA KUNA KOZI MAALUMU KWA WOTE WASIO NA VIGEZO KAMILI KUMUWEZESHA KUPAMBANA MPAKA AFIKIE VIWANGO NA KUJIUNGA NA MEDICINE..CA/CO

JIUNGE NA KOZI INAYOTOLEWA ST DAVID COLLEGE PEKEE IITWAYO PRE-MEDICINE PROGRAME KWA KUSHIRIKIANA NA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA NECTA TUMEKUANDALIA NJIA RAHISI KABISA.

FIKA SASA KIMARA TEMBONI ZAMANI MOA AU OFISI ZETU ZILIZOPO MWANANYAMALA A CCM MINAZINI KWA DR DAVID B.MWANGANDA. CHUO NI CHA KUTWA NA BWENI.
SIFA KUU NI UFAULU MASOMO YA SAYANSI IKIWEMO HESABU NA KIINGEREZA ANGALAU ALAMA D.

ADA ZETU NI NAFUU UTALIPA KIDOGO KIDOGO KUKIDHI UWEZO WAKO

KWA MAWASILIANO....0654354949/0716044610 
AU INGIA MTANDAONI www.stdavidcollege.ac.tc



UJENZI MAEGESHO YA KIVUKO LINDI KITUNDA WAKARIBIA KUKAMILIKA

0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa kwanza kushoto) akitazama moja ya malighafi inayotumika katika ujenzi wa maegesho mapya ya Lindi Kitunda unaondelea Mkoani Lindi. Maegesho hayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni na yatasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri wa majini katika eneo hilo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo kwa mkandarasi anayejenga maegesho ya Lindi Kitunda wakati alipokua akikagua maendeleo ya ujenzi huo Mkoani Lindi. Maegesho hayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni na yatasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri wa majini katika eneo hilo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa kwanza kushoto) akitoa maagizo kwa mkandarasi anayejenga maegesho ya Lindi Kitunda wakati alipokua akikagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho hayo Mkoani Lindi. Kulia ni Mtaalamu wa Uchumi kutoka wakala huo Edgar Ruta, Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Mhandisi Japhet Y. Maselle na mkandarasi anayesimamia ujenzi huo Ndugu Evans Martin. Maegesho hayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni na yatasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri wa majini katika eneo hilo.
Mafundi wa kampuni inayosimamia ujenzi wa maegesho ya kivuko Lindi Kitunda wakiendelea na ujenzi wa maegesho hayo upande wa Kitunda mkoani Lindi. Maegesho hayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni na yatasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha huduma za usafiri wa majini katika eneo hilo..

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Dk.Hamisi Kigwangalla: “Tuzidi kuombeana dua tu, sintowaangusha Watanzania”

0
0
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya Maliasili na Utalii hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla amewataka watanzania kuendelea kumuombea dua pamoja na ushirikiano katika majukumu yake mpya.“Nimepokea salamu nyingi za pongezi na shukrani kwa Mungu aliye juu. Sintoweza kumjibu kila mtu, uungwana ni kutambua pongezi zenu na dua tele mlizotuombea, nawashukuru sana ndugu zangu. 

Tuzidi kuombeana dua tu.Tuna kazi ngumu ya kukimbia kukidhi matarajio ya kiongozi wetu Mkuu aliyetuamini na matarajio ya wananchi wenzetu. Binafsi nawaahidi nyote kuwa sintowaangusha! Ahsanteni sana ndugu zangu, natarajia ushirikiano wenu wa kila hali.” Alieleza Dk. Hamisi Kigwangalla. 

Awali taarifa za kuteuliwa kwake katika wizara nyingine, alizipata kupitia kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi kwa njia ya simu wakati akiwa kwenye majukumu ya ziara ya kuboresha mfumo wa afya, akiwa Wilayani Nachingwea, Kata ya Kilimalondo umbali wa zaidi ya kilometa 100, kutoka Makao makuu ya Wilaya hiyo ya Nachingwea, aliweza kusitisha ziara yake hiyo ambayo alitakiwa kuendelea katika Vijiji na Wilaya nyingine ya Liwale.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya Utalii hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua chumba cha upasuaji mkubwa cha kituo cha AAfya Kilimalondo, Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.
Dk.Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa kituo cha Afya Kilimalondo wakati wa ziara hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MWILI WA MWANAMUZIKI SHABANI YOHANA WANTED WAAGWA BOTSWANA

0
0
VIDEO YA WANAMUZIKI NA WAPENZI WA MPIGA GITAA SHABAN YOHANA WANTED WAKIAGA HUKO GABORONE BOTSWANA  KABLA YA SANDUKU LENYE MWILI WA SHABANI KUPELEKWA UWANJA WA NDEGE TAYARI KWA SAFARI YA KUJA TANZANIA. MWILI WA SHABANI UTAWASIRI DAR JUMATATU 9 OKTOBA ALFAJIRI.

MICHANGO INAHITAJIKA KWA AJILI YA KUWEZESHA KUSAFIRISHA MWILI KUTOKA DAR KWENDA  MICHUNGWANI MUHEZA KWA MAZISHI SIKU YA JUMANNE. KAMA UMEGUSWA UNAWEZA KUTUMA  CHOCHOTE NAMBA ZIFUATAZO
0713274747 NA 0763722557, ILI KUFANIKISHA MAZISHI YA MWANAMUZIKI HUYU.
SIKILIZA UMAHIRI ALIYOKUWA NAO KWENYE GITAA LA SOLO KATIKA WIMBO HUU


RC RUVUMA LAZIMA VIONGOZI WA WILAYA MTATUE MATATIZO YA MAENEO YENU.

0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dokta Bilinith Mahenge amefanaya ziara ya kukutana wananchi wa wilaya ya namtumbo kwa lengo la kutatua kero zinazowakabili katika wilaya hiyo,na hapa mkuu wa mkoa Dokt Mahenge anakutana na maswali magumu kutoka kwa wananchi hao huku idara ya maji na kilimo yakipamba moto.

MWANSANSU MWENYEKITI MPYA CHAMA CHA MAPINDUZI -NAMTUMBO

0
0
NA YEREMIAS NGERANGERA -NAMTUMBO

Wanachama wa chama cha mapinduzi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wamemchagua Aggrey Mwansasu kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho kwa kumbwaga aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Benjamini Nindi .

Uchaguzi wa kumpata mwenyekiti huyo ulifanyika katika Bwalo la shule ya sekondari Namtumbo shule ambayo inamilikiwa na jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi kilomita tatu kutoka mjini Namtumbo.

Aidha katika uchaguzi huo awali uliingia dosari baada ya msimamamizi wa uchaguzi huo Zena Rashidi Mijinga kujisahau kwa kutosoma kanuni ya kushinda uchaguzi ni sharti mgombea apate asiliomia hamsini ya kura zitakazopigwa.

Dosari ya kanuni hiyo kutosomwa awali ilijionesha baada ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti kutofikia asilimia hamsini ya kura zilizopigwa na kuwataka wajumbe wa mkutano huo kurudia kupiga kura kwa nafasi ya uenyekiti hali iliyoibua hasira kutoka kwa wajumbe kwa madai ya kutaka kumbeba mgombea mmojawapo katika uchaguzi huo na kuongeza kuwa kanuni hizo kwa nini hazikusomwa kabla ya uchaguzi na badala yake zisomwe wakati uchaguzi umefanyika.

Masauni ataka mkandarasi achukuliwe hatua kwa kuutelekeza mradi wa mabilioni Gereza Idete

0
0
Na Felix Mwagara (MOHA)

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelitaka Jeshi la Magereza kumchukulia hatua kali Mkandarasi wa mradi mkubwa wa umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete wilayani Kilombero endapo atabainika alifanya makosa kwa kuutelekeza mradi huo.

Mradi huo ambao ungesaidia kuendeleza kilimo cha mpunga na mahindi kwa zaidi ya ekari 1000, unathamani ya zaidi ya Bilioni 2.5 ambapo ulianza kujengwa mwaka 2013 mara bada ya Serikali kumpa Mkandarasi huyo wa Kampuni ya Tanzania Building Works ya Dar es Salaam, zaidi ya Bilioni 1 ili kuufanikisha mradi huo katika hatua ya awali. 

Akizungumza mara baada ya kuukagua mradi huo uliopo Idete mkoani Morogoro, Masauni alisema Serikali ya Awamu ya Tano haitakubali uzembe huo kwa fedha za Serikali kuchezewa huku mradi huo haujakamilika.

Masauni alilitaka Jeshi la Magereza kuhakikisha Mkandarasi huyo ambaye fedha alizopewa haziendani na ukubwa wa kazi alizozifanya, achunguzwe haraka iwezekanavyo na endapo ikibainika amefanya makosa hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

“Fedha ni nyingi alizopewa, zaidi ya bilioni moja za Serikali zimetolewa, na ukiangalia ukubwa wa kazi aliyoifanya haiendani na thamani ya fedha hizo, hivyo hatuwezi kuvumilia na kuona fedha za Serikali zikichezewa, nahitaji huyu mkandarasi achunguzwe na ikithibitika amefanya makosa hatua za kisheria zichukuliwe,” alisema Masauni na kuongeza;

“Fedha zilizotumika ni nyingi halafu mkandarasi huyo eti anaondoka kwasababu ambayo inayojulikana akisingizia kuwa ukosefu wa fedha, Serikali haiwezi ikachezewa, tendo la kuchelewa kwa mradi huu ameitia hasara kubwa Serikali.” 

IGP SIRRO AWAJENGEA UWEZO ASKARI WA MBEYA.

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akisalimiana na waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya, aliokutananao Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo leo, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. Picha na Jeshi la Polisi.

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akikagua gwaride maalumu aliloandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wa kutumia silaha za moto cha mkoa wa Mbeya, akiwa kwenye ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akisalimiana na waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya, aliokutananao Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo leo, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. Picha na Jeshi la Polisi.

MSANII SHETTA KUNOGESHA USIKU WA KILIMANJARONIGHT ÖREBRO SWEDEN

MSANII SHETTA KUNOGESHA USIKU WA KILIMANJARONIGHT ÖREBRO SWEDEN

0
0
Kwa wale wakazi wote wa nchi ya Sweden na nchi jirani za skandinavia mtakuwa na usiku wa burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa kimataifa kutokea Sweden Tanzania  Uganda na nchi nyingine kadhaa  kwenye usiku wa kuitangaza nchi ya Tanzania kwa vivutio vyake vya utalii ikiwemo mlima mrefu barani Afrika Kilimanjaro.

Tunayofuraha kwamba msanii nyota wa mziki wa Bongoflaver Shetta atakuwepo kukuletea burudani kabambe ya mziki .
Usikose kuhudhuria ! 

Ni tarehe 14 Oktoba
Ukumbi ni kulturhuset Örebro
Järnvägsgatan 8 Örebro Sweden .
Ukipata ujumbe huu mtaarifu na mwezako.

Je unahitaji Engines na spare parts za aina yoyote?

0
0
Tunauza Engine na spare za Land Rover Discovery kwa bei nafuu kutoka UK. Engine hiyo ya TD5 inauza Milioni 4.7 tunazo za Manual na Automatic pia tunaweza kukupatia spare ya aina yoyote kutoka Europe,
Wasiliana na sisi kwa maelezo zaidi +255718030320 +255674782666 on whatsapp +447723550406

MAMIA WAJITOKEZA KUMUAGA MAMA HAPPYFANIA KOMBA KIJICHI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0

 Marehemu Happyfania Komba enzi za uhai wake. Happyfania Komba alifariki dunia usiku wa kuamkia jana akiwa usingizini. Mazishi yake yatafanyika kesho Tunduru mkoani Ruvuma.
Waombolezaji wakiaga mwili wa Happyfania Komba.

 Mwili wa marehemu ukiagwa.
 Mtoto wa marehemu, Exavery Komba akisaidiwa na wenzake wakati akitoa heshima za mwisho kwa mama yake.
 Shangazi yake marehemu Winfrida Komba akilia kwa uchungu wakati wa kumuaga mpendwa wake.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com simu namba 0712727062)


RC RUVUMA: LAZIMA VIONGOZI WA WILAYA MTATUE MATATIZO YA MAENEO YENU

0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt. Bilinith Mahenge amefanya ziara ya kukutana wananchi wa wilaya ya Namtumbo kwa lengo la kutatua kero zinazowakabili katika wilaya hiyo. Hapa mkuu wa mkoa Dkt.  Mahenge anakutana na maswali magumu kutoka kwa wananchi hao

SABA WANUSURIKA KIFO BAADA YA GARI WALIYOPANDA KUGONGA TRENI JIJINI TANGA

0
0

Watu saba wamenusurika kifo huku wawili  wakijeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo baada ya gari ndogo waliokuwa wamepanda aina ya Carry kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni ya Tanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda, gari hilo baada ya kufika eneo la makutano ya reli wakati likijaribu kusimama  lilifeli breki na kuiparamia treni hiyo.
Ajali hiyo ambayo ilitokea jana eneo la makutano ya reli Kwaminchi Jijini  Tanga iliacha mshangao mkubwa kutokana na mazingira ya namna ilivyotoke ambapo gari ndogo ilikuwa ikitokea eneo la Kwaminchi.
Akithibitisha kutokea tukio hilo jana,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba alisema ajali hiyo ilitokea saa kumi jioni katika eneo hilo ambapo gari hilo ilifeli breki na kuparamia mabehewa ya reli wakati ikipita katika eneo hilo.
Aliitaja gari hiyo aina ya Carry ambayo ilipata ajali hiyo kuwa ni T.343 DCQ  iliacha njia na kuigonga treli iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuingia  kwenye stesheni ya Tanga.
Aidha alisema majeruhi sana waliokuwepo kwenye ajali hiyo walifikishwa  kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo kwa matibabu zaidi huku Dereva wa gari hilo akitokomea.
Kamanda huyo alisema kutokana na kukimbia kwa dereva huyo wataendelea kumsaka ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kamanda huyo alitoa wito kwa madereva kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani kwa kuhakikisha kwenye maeneo ya kivuko cha reli wanakaa mita 50.

 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali jijini Tanga wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi makutano ya reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya kufika eneo la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni Jijini Tanga
 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakishuhudia ajali hiyo leo iliyotokea eneo la Kwaminchi makutano ya reli baada ya gari ndogo aina ya Carry kufeli breki baada ya kufika eneo la reli na kuligonga treni iliyokuwa ikitokea eneo la Pongwe kuelekea Stesheni Jijini Tanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba akikagua gari hiyo jioni hii. 
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Rais Dkt John Magufuli hakufanya kosa katika uteuzi wa Katibu wa Bunge-Dkt Kashililah.

0
0

Katibu wa Bunge wa zamani, Dk Thomas Kashililah amesema, Rais Dkt John Pomebe Magufuli hakufanya kosa katika uteuzi wa Katibu wa Bunge. 

Rais Magufuli jana Jumamosi alimteua Steven Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge, uteuzi ambao umeibua hoja kwamba sheria haikufuatwa. 

Dkt Kashililah akizungumza na Mwananchi leo Jumapili, amesema kwa mujibu wa ibara ya 87(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano mamlaka ya uteuzi haikufanya kosa licha ya sheria ya Bunge kuelekeza utaratibu. 

Amesema, “Mamlaka ya uteuzi iko sahihi… unajua sheria haiko juu ya Katiba na Katiba iko juu ya sheria, hivyo Rais akiamua anaweza kufanya hilo, sheria haiwezi kumzuia,” amesema Dk Kashililah akisisitiza ibara ya 87 iko wazi. 

Ibara hiyo inasomeka: “Kutakuwa na Katibu wa Bunge ambaye atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye madaraka ya juu katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.” 

Dk Kashililah amesema: “Kama aliyeteuliwa angekuwa hayuko kwenye madaraka ya juu hapo sawa, lakini huyu aliyeteuliwa (Kagaigai) ni mtu senior kabisa serikalini na ana vigezo hivyo… kuna watu wanapotosha ukweli.”

Introducing "Dela Delani" by Dudu Baya

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images