Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

ALIYEMTUSI RAIS MAGUFULI MTANDAONI AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI 12 AU KULIPA FAINI YA MILIONI TANO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
MHASIBU wa Shule ya Sekondari ya St Joseph Cathedral, Elizabeth Asenga leo amehukumiwa kulipa faini ya Sh Milioni tano au kwenda jela miezi 12 baada  ya kukutwa na hatia ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Dk, John Magufuli.
 
Mhasibu huyo anadaiwa kumuita Rais Magufuli  kilaza kupitia mtandao wa WhatsApp.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema mshtakiwa amepatikana na hatia baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na pande wa Jamuhuri kwa kuleta mashahidi saba na kumuona mshitakiwa  ana hatia.

"Upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa umetenda kosa hivyo mahakama  inakutia hatiani kwa makosa uliyoshitakiwa nayo" 

Akimsomea adhabu yake amesema "utatakiwa kulipa  faini ya Sh Milion tano au kutumikia kifungo cha miezi 12 jela," alisema Hakimu Shaidi. 

Kabla ya kutolewa adhabu, mshitakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa mama yake mzazi ni mzee anamtegemea na ana watoto wanaomtegemea.

Hata hivyo, mshtakiwa amelipa faini na amefanikiwa kukwepa kwenda jela

Katika kesi ya msingi, inadaiwa   Agosti 6, mwaka jana mshtakiwa huuo aliwasilisha maneno kinyume cha sheria kupitia mtandao wa WhatsApp katika group la wafanyakazi la STJ kwa nia ya kumtusi Rais.

Mshtakiwa alinukuliwa kuwa "Habari za asubuhi humu hakuna rais kilaza kama huyu wetu duniani angalia anavyompa Lissu umashuhuri,  fala yule picha yake ukiweka ofisini  nuksi tupu ukiamka asubuhi ukikutana na picha yake kwanza siku inakua ya mkosi mwanzo mwisho." 

MWENGE WA UHURU WAZINDUA DUKA LA BIMA YA AFYA LA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

$
0
0
 Sehemu ya muonekana kwa ndani duka la Bima ya Afya la Halmashauri ya Jiji la Tanga
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akiwa nje ya duka hilo akisubiri mapokezi ya mwenge wa uhuru kwenye duka hilo
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akiwa na watumishi wa mfuko huo mara baada uzinduzi wa duka hilo katikati ni Macrina Clemence ambaye ni Afisda Matekelezo wa Mfuko huo na kulia ni DaktariLuiza Mtafi 
 Sehemu ya watumishi wa NHIF Mkoani Tanga katikati ni daktari Luiza Mtafi kushoto ni Afisa Madai NHIF Mary Daniel na kulia ni Afisa Matekelezo,Macrina Clemence
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu wakifuatilia uzinduzi huo.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MATAPELI WA ARDHI WILAYANI KINONDONI KUKIONA-DC HAPI.

STARTIMES WASHEREKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUZINDUA CHANELI MPYA KWA WATEJA WAKE

$
0
0
KATIKA kusherekea wiki ya huduma kwa wateja kampuni inayotoa huduma za ving'amuzi Tanzania Wamezindua chaneli mpya kwa wateja wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es aSalaam leo, Mkurugenzi wa uendeshaji wa Startimes, Carter Luoh amesema kuwa kampuni hiyo wameongeza chaneli mpya katika king'amuzi ambapo wanajisogeza karibu na wateja wake.

Pia amesema kuwa Startimes inafuraha kubwa kutoa huduma za kidijitali kwa mikoa 17 kwa kutoa huduma za ving'amuzi ambayo imewafikia wateja wa mikoa zaidi ya 17 hapa nchini kwa kuwafikia wateja kwa kufungua zaidi ya mawakala 300.

Kwaupande wake Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa Ngowi amesema kuwa katika wiki hii muhimu ya huduma kwa wateja wamezindua chaneli nyingine mpya kwenye king'amuzi cha startimes pamoja na pamoja na chaneli zitakazokuwa kimetafsiliwa kwa kiswahili pamoja na movi za kihindi.
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh (katkati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Kampuni ya Startimes kuzindua chaneli mpya katika king'amuzi cha Startimes wakati wa kuzindua wiki ya huduma kwa wateja na kujiweka karibu zaidi na wateja wake. Kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja wa Startimes, Henry Ngailo na Kushoto ni Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa ngowi.
Meneja uendeshaji wa Startimes, Gaspa ngowi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua chaneli mpya ya king'amuzi cha Satrtimes katika kusherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba ikiwa ni kujiweka karibu zaidi na wateja wake. Amesema kuwa sherehe hizi zinaambatana na uongezwaji wa chaneli mpya kama vile ST Bollywood Afrika, ST Bollywood na FOX life. katikati ni Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh (katkati) na Kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja wa Startimes, Henry Ngailo.
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Startimes jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua chaneli mpya ya kwenye king'amuzi cha Startimes katika wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Star Media (T) Ltd, Carter Luoh akikata keki kwa pamoja na wateja wa king'amuzi cha Startimes kwaajili ya kusherekea wiki ya huduma kwa wateja.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

PICHA ZA UNYANYASAJI WA KINGONO ZATAKIWA KUTOLEWA TAARIFA ZIWEZE KUONDOLEWA -TCRA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Taasisi ya kutetea watoto ya C-SEMA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano nchini wamefungua dirisha 'portal' kwa ajili ya picha zinazohusu matukio ya watoto,  zenye maudhui ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto,  kuondolewa katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza katika ufunguzi wa dirisha, Meneja Huduma wa Simu ya Mtoto , Thelma Dhase amesema kuwa picha za matukio za ukatili wa watoto hazitakiwi kuendelea kusambaa katika mitandao.

Amesema kuwa mfumo huo umeanza nchini lakini mradi huo unafanywa duniani nchi 18, ambapo kwa Afrika Tanzania ni ya Nne kuwa na mpango huo katika kutoa taarifa za picha za unyanyasaji wa kingono katika mitandao.

Dhase amesema kuwa mradi huo utasaidia kuongeza usalama wa watutmiaji wa mitandao kuhakikisha watoto waliothirika na picha za unyanyasaji wa kingono hawapitii unyanyasaji zaidi katika mitandao ya kijamii.

Kwa upande wa Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, Semu Mwakyanjala amesema picha za watoto zinaonesha ukatili au udhalilishaji wa watoto, hazitakiwi kusambazwa katika mitandao ya kijamii na mtu akipata picha hizo anatakiwa kutoa taarifa ziweze kutolewa katika mitandao.

Mwakyanjala amesema picha zinazodhalilisha watoto hazitakiwi kutokana na picha hizo zitaawathiri kisaikolojia wakishakuwa watu wazima.

Mradi wa kutolea taarifa za unyanyasaji wa kingono kwa watoto unaendeshwa na Internet Watch Foundation ambao unatekelezwa nchi 18 duniani.

.Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Semu Mwakyanjala akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa watumiaji wa mitandao kutoa taarifa juu ya picha za unyanyasaji wa kingono kwa watoto iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa huduma wa simu ya mtoto wa C-SEMA, Thelma Dhase akizungumza juu utoaji wa taarifa zinazohusiana na picha za unyanyasaji wa kingono kwa watoto kuweza kuondolewa katika kulinda watoto wengine leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waandushi wa wakiwa wadau katika ulinzi wa watoto katika kutoa taarifa za picha za unaynyasaji wa kingono kwa watoto leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, Semu Mwakyanjala akiwa katika picha ya pamoja na Taasisi ya C-CEMA.
.

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA WABUNGE WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUTOKA TANZANIA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. 
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. 
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mheshimiwa Abdullah Makame (katikati) ambae ni kiongozi wa msafara wa Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. ujumbe huo uliongozwa na Mheshimiwa Abdullah Makame (wa tatu kulia) ambae ni kiongozi wa msafara huo.PICHA NA OFISI YA BUNGE

TIMU ZA TANZANIA KIKAPU ZAANZA VIBAYA MICHUANO YA KANDA YA TANO AFRIKA

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Timu tatu za Tanzania za mpira wa kikapu zimeshindwa kutamba mbele ya timu kutoka nchi zingine katika mashindano ya klabu bingwa kanda ya tano yanayoendelea katika jiji la Kampala nchini Uganda.

Michuano ya Klabu Bingwa kanda ya tano (Zone 5) yameanza jana huku timu za Tanzania zikionekana kuanza vibaya, wanaume wakianza kwa hatua ya makundi na wanawake wakianza kwa mtoano. 

Tanzania imewakilishwa na Savio na ABC kwa upande wa wanaume na DB Lioness kwa upande wa wanawake. Matokeo ya siku mbili ya michuano ya kanda ya tano yanayoendelea jiji la Kampala.

Day 1 

APR 45 (Rwanda ) /KCCA (Uganda) 57 -wanawake 
UCU 108 (Uganda) /Horseed 42 (somalia) -wanawake
Equity Bank 70 (Kenya) / DB Lioness 48 (Tanzania) -wanawake
Hawasa 43(Ethiopia)/ Patriot 110 (rwanda) -wanaume
KPA 108 (Kenya) /Gonder city 35 (Ethiopia) -wanaume 
City Oilers 93 (Uganda)/ Savio 46 (Tanzania) -wanaume
Betway Power 87 (Uganda) / ABC 55 (Tanzania) -wanaume 

Day 2

APR 84 (Rwanda ) /DB Lioness 48 74 (Tanzania) - wanawake 
KPA 81 (Kenya) /ABC 77 (Tanzania ) -wanaume
Patriots 77(Rwanda) /Savio 48 (Tanzania ) - wanaume 
KCCA 51 (Uganda) /Equiyt Bank 56 (Kenya) - wanawake 
UCU 69 (Uganda) /KPA 68 (Kenya) - wanawake 
City Oliers 111 (Uganda) /Hawasa City 41 (Ethiopia) - wanawake
Betway Power 113 (Uganda) /Gonder City 31 (Ethiopia) - wanaume

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yatakiwa kusimamia weledi katika utoaji mikopo

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

SERIKALI imesema kuwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imetakiwa kusimamia weledi katika utendaji wao wa kazi na kuacha kujifanya Miungu watu kama ilivyokuwa zamani, hali iyowakatisha tamaa baadhi ya wanafunzi kuomba mikopo katika bodi hiyo.

Hayo ameyasema leo Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profes Joyce Ndalichako wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) mpya ,amesema kuwa bodi ilikuwa inaona kero katika kuwahudumia watoto kupata mikopo na wengine walikuwa ndio sehemu ya wahitaji wa mikopo hiyo kutokana hali ya uchumi waliokuwa nao.

Amesema kuwa bodi iwaangalie watu wenye mahitaji ya kupata mikopo wapate bila kusumbuliwa katika upataji wa mikopo hiyo.Profesa Ndalichako ameitaka Bodi kusimamia vyema makusanyo ya madeni kwa wanafunzi waliosomeshwa kwa mikopo ili iweze kusaidia wengine walioomba kwa ajili ya kujiendeleza na elimu ya juu nchini kutokana na mahitaji ya waombaji ni wengi.

Amesema mpaka sasa tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo mwaka 2014 serikali imetoa kiasi cha fedha shilingi Trilioni 3.1 huku makusanyo yakiwa Bilioni 217.Aidha amesema kulikuwa na ubadhilifu uliokuwa ukifanywa na watendaji wa bodi ya mikopo iliyopita ambayo ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alibainisha hivyo hatarajii utokee tena.

Profesa Ndalichako amesema kuwa hakuna hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kwa majina hewa, mtu anarekodiwa kuwa amechukua fedha huku akiwa marehemu lakini fedha zikiendelea kuchukuliwa hali ambayo haitajiki kujirudia.Makamu Mwenyekiti Madina Mwinyi alimuhakikishia Waziri kwamba wataweka taswira nzuri katika bodi hiyo na kuondoa changamoto zilizokuwa zikikabili hapo awali.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa (HESLB) Abdul –Razak Badru alimshukuru Waziri huyo huku akimuahidi kufanya kazi kwa kushirikiana kwa lengo la kujenga Taifa katika kuangalia vipaumbele vya mikopo.
 Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza katika uzinduzi wa bodi ya mikopo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Mikopo , Madina Mwinyi akitoa maelezo jinsi bodi hiyo itavyofanya kazi leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa (HESLB) Abdul –Razaq Badru akizungumza juu ya kushirikiana na bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha pamoja na bodi ya mikopo leo jijini Dar es Salaam.

STARS WAJICHIMBIA NJE YA MJI KUJIANDAA NA WAMALAWI JUMAMOSI UWANJA WA UHURU

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

TIMU ya Taifa Tanzania Taifa Stars wameingia kambini jana kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi kuanzia saa 10 alasiri katika dimba la Uhuru.
 
Stars inakutana na Malawi ikiwa ni mara ya pili kwa mwaka baada ya kuvaana nao June 25 mwaka huu katika michuano ya COSAFA yaliyofanyika nchini Afrika Kusini na kufanikiwa kupata wa ushindi wa goli 2-0. 

Timu hiyo chini ya Salum Mayanga inafanya mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na tayari Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta tayari ametua nchini kuungana na nyota wengine wa Tanzania katika mazoezi ya pamoja. 

Kocha Mayanga mapema wiki iliyoisha aliita kikosi kitakachounda Taifa Stars kwa ajili ya kuvaana na Malawi siku ya Jumamosi na akiwajumuisha nyota mbalimbali na akimrudisha Ibrahim Ajib baada ya kutokumuita kwa muda mrefu sambamba na golikipa Peter Manyika. 

Mayanga aliteuliwa Januari 4, mwaka huu ameita nyota watano wanacheza soka nje ya mipaka ya Tanzania akiwamo nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Ally Samatta.

Kikosi hicho kina makipa Aishi Manula (Simba SC), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Singida United).Mabekii ni Gardiel Michael (Yanga), Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC) na Adeyum Ahmed (Kagera Sugar). 

Viungo ni Himid Mao ambaye pia ni Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba SC), Raphael Daud (Yanga), Simon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya) na Morel Orgenes (FC Famalicao/Ureno). 

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Ibrahim Hajib (Yanga) na Mbaraka Yussuph (Azam FC). 

Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Ame Ninje (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa). 

Shirkisho la mpira wa miguu nchini wamewataka watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuja kuishangilia timu ya Taifa kwa kujenga dhana ya mchezaji wa 12 uwanjani wakati wale 11 akiwamo Msuva, Ajib, Mbaraka wakileta faraja ya mabao.

WAZIRI DKT Mwakyembe Awataka Wasanii wa Nyimbo za Dini Kuliombea Taifa Kudumisha Amani

$
0
0



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea wa ujumbe wa Uongozi wa kwaya wa Furahini kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida walipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma ambapo amewapongeza kwa uimbaji wao na kuliombea taifa kudumisha amani.
02
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kwaya wa Furahini Benjamini Ng’imba (wa pili kushoto) kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida walipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma.
03
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akimsikiliza Mlezi wa wa Kwaya wa Furahini Zakayo Munyawi (wa kwanza kushoto) kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida walipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma.
04
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Uongozi wa kwaya wa Furahini kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida walipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma ambapo amewapongeza kwa uimbaji wao na kuliombea taifa kudumisha amani.Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma

CRDB TAWI LA QUALITY CENTER WAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na wateja wa benki hiyo tawi la Quality Center jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa  Wateja  Duniani. (Na Mpiga Picha Wetu).
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo, akizungumza na Wateja wa Benki hiyo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi hilo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa wameshika keki maalumu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi la Quality Center Barabara ya Nyerere Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya CRDB, tawi la Quality Center, Clementine Kinabo (kushoto), akimkabidhi tuzo maalumu, Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Master Mind Tobacco, Joseph Dominic, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, iliyofanyika iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN UZINDUZI WA MAKUMBUSHO MPYA YA OLDUVAI - NGORONGORO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wanaoishi kwenye bonde la Ngorongoro kuwa mstari wa mbele katika kuhifadhi na kutunza mazingira ya bonde hilo ili liwe na manufaa kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Makamu wa Rais aliyasema hayo leo wakati wa ufunguzi rasmi wa Makumbusho mapya ya Olduvai - Ngorongoro. Katika ufunguzi huo Makamu wa Rais pia alipata nafasi ya kuzindua tovuti maalum kuhusu masuala ya utalii katika bonde la Ngorongoro. “Ufunguzi huu ninaoufanya leo unaendana na malengo tuliyojiwekea ya kuongeza na kukuza vivutio vya utalii ili kuvutia wageni (watalii) wengi zaidi kutembelea nchi yetu” alisema Makamu wa Rais.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika tukio la ufunguzi wa Makumbusho hayo, Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema anatamani kuona kinachofanyika Ngorongoro kinafanyika pia katika maeneo mengine yenye rasilimali za kihistoria kama vile mapango ya Amboni (Tanga), Michoro ya Miambani ya Kondoa (Dodoma), miji mikongwe ya Zanzibar, Bagamoyo, Kilwa Kisiwani na Songo Mnara.

Pia Mheshimwa Makamu wa Rais aliwaagiza viongozi wa Serikali, hususani Wizara ya Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kutambua, kulinda, kuhifadhi na kuendeleza vivutio vyote vya kiutamaduni na kijiolojia vilivyopo nchini. “Nataka kuona shughuli za kiutalii zikiibuka katika ngazi ya wilaya kupitia Halmashauri zetu na ofisi za Wakuu wa Wilaya ili kuongeza ajira za vijana nchini” alisisitiza Makamu wa Rais. 

Makamu wa Rais alitoa rai kwa wananchi wote wanaoshi pembezoni au karibu na rasilimali za kitamaduni kutunza rasilimali hizo muhimu kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo. Makamu wa Rais alisema ”ninyi ni mashuhuda wazuri wa namna rasilimali hizi zilivyo muhimu kwa ustawi wa uchumi wenu, ajira mnazopata, heshima ya kutambuliwa utamaduni wenu kimataifa pamoja na fedha za kigeni zinazopatikana kupitia utalii unaotokana na rasilimali hizi ambazo husaidia kujenga huduma za kijamii kama vile mahospitali, mashule, barabara na miundombinu ya maji”. 

 Aidha alisisitiza kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa viongozi wa serikali, wataalam na wananchi watakaosababisha uharibifu wa rasilimali muhimu kwa kutotekeleza majukumu yao sawasawa au kuvunja sheria na taratibu za uhifadhi wa rasilimali hizo.

Mwisho, Makamu wa Rais aliwashukuru wote waliohusika katika ujenzi wa Makaumbusho hii mpya na ya kipekee duniani hususan Umoja wa Ulaya ambao wamechangia kiasi kikubwa cha fedha za kukamilisha ujenzi huo.

Ufunguzi wa Makumbusho ya Olduvai uliohudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe(MB), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo, Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Ole Nasha (MB), Balozi wa Umoja wa Ulaya na Balozi wa Hispania pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro, wengine pichani ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia). ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia) mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipata maelezo mbali mbali kuhusu maisha ya binadamu na wanyama wa kale kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale kutoka Makumbusho ya Taifa Dkt. Agness Gidna mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia historia kuhusu maisha ya binadamu na wanyama wa kale iliyopo kwenye Makumbusho ya Olduvai mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

BENKI YA CRDB TAWI LA QUALITY CENTER WAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na wateja wa benki hiyo tawi la Quality Center jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani. (Na Mpiga Picha Wetu). 
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo, akizungumza na Wateja wa Benki hiyo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi hilo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NN General Supplies, Selina Letara, akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei,wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi Quality Center.

MAGAZETI YA JUMATANO LEO OCTOBER 4,2017

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


ARUMERU WASHIRIKI KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA STAILI YA AINA YAKE

$
0
0
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wananchi katika Wilaya ya Arumeru Kata ya Makiba kijiji cha Valeska mkoani Arusha; wameonyesha kuelewa umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa kiasi cha kujiwekea mkakati wa kuhakikisha nishati ya umeme muda wote inakuwepo ili zoezi la Usajili linaloendelea kutosimama.

Pengine hii ni tofauti na mazoea ya siku zote katika uendeshaji wa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu kwa maeneo ambayo zoezi kama hilo limewahi kufanyika kiasi cha kuamsha morali zaidi kwa watumishi kutokana na mwamko mkubwa wa wananchi kushiriki zoezi hilo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kata hiyo; mtendaji wa Kata hiyo amesema wao kama Kata wamehamasisha wananchi kujitokeza kusajiliwa na kutokana na ushirikiano mkubwa ulioonyeshwa na wananchi wana imani Kata yao watakamilisha zoezi la Usajili ndani ya muda uliopangwa.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Mdami akikagua fomu ya Bwana Kitomari baada ya kukamilisha hatua ya kwanza ya usajili Vitambulisho vya Taifa kabla ya kwenda kwenye hatua ya upigaji picha. Hapa ni Kata ya Makiba kituo cha CCM Arumeru Arusha ambako zoezi hilo linafanyika.
Hawa ni Watendaji katika vitongoji viwili vya Kijiji cha Valeska wakiendelea na zoezi la kuwahakiki wananchi wao na kuwathibitisha kuwa ni wakazi halali wa eneo lao kabla ya kuwaidhinisha kupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole wakati wa zoezi la Usajili linaloendelea Wilayani Arumeru.
Huu ni muonekano wa nje ya jengo ambako usajili wa Vitambulisho vya Taifa unaendelea Kata yaMakiba kijiji cha Valeska. Baadhi ya wananchi wakiwa wanabadilishana mawazo huku wakisubiri kupatiwa huduma.
Afisa Usajili Wilaya ya Arumeru ndugu Edward Bujune akitoa maelezo kwa wananchi kuhusu umuhimu na faida za Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi la kuwasajili wananchi wa Wilaya ya Arumeru likiendelea.
Meneja Mifumo ya Komputa ndugu Mohamed Mashaka akirekebisha moja ya Kamera ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa zoezi la Usajili Wilayani Arumeru.

Bonde la Eyasi Wembere laonyesha dalili ya uwepo wa Mafuta

$
0
0
Na Teresia Mhagama, Tabora

Imeelezwa kuwa miamba iliyo katika Bonde la Eyasi Wembere hususan mabonde madogo (sub basin) ya Wembere na Manonga yaliyopo katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, Singida na Simiyu inawezekana kuwa na mafuta kutokana na sifa zake za Kijiolojia na Kijiofizikia.

Hayo yameelezwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini (Uganda), Robert Kasande na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (Tanzania), Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo katika Mkutano na Wananchi uliofanyika katika kijiji cha Mwashiku wilayani Igunga mkoani Tabora. Mkutano huo uliandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry.

Viongozi hao walitoa kauli hiyo baada ya timu ya wataalam kutoka Uganda na Tanzania kufanya ziara katika Bonde hilo hususan mabonde madogo ya Wembere na Manonga na kutembelea miamba inayoonekana katika maeneo ya Sekenke mkoani Singida, na vijiji vya Mwanzugi na Kining'inila mkoani Tabora.
Sehemu ya Bonde la Manonga mkoani Tabora ambalo miamba yake inaonesha uwezekano wa kuwa na viashiria vya Mafuta kutokana na sifa zake za Kijiolojia na Kijiofizikia. 
Timu ya wataalam kutoka Uganda na Tanzania wakiwa katika miamba inayoonekana katika kijiji cha Mwanzugi wilayani Igunga ikiwa ni ikiwa ni maandalizi ya shughuli za Utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi Wembere na Ziwa Tanganyika. 
Timu ya wataalam kutoka Uganda na Tanzania wakiwa katika Bonde la Manonga lililopo katika kijiji cha Kining’inila mkoani Tabora ambapo pia walichukua sampuli za miamba katika Bonde hilo ikiwa ni maandalizi ya shughuli za Utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi Wembere na Ziwa Tanganyika. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
Timu ya wataalam kutoka Uganda na Tanzania wakiwa katika eneo la Sekenke mkoani Singida ambapo miamba ya Bonde la Wembere inaonekana ikiwa ni maandalizi ya shughuli za Utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi Wembere. Wa Tano kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini (Uganda), Robert Kasande, wa Pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (Tanzania), Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo na wa kwanza kushoto ni Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga.

WATANZANIA WAISHIO BOTSWANA WASIFU JUHUDI ZA RAIS DKT.MAGUFULI

$
0
0
Watanzania waishio nchini Botswana wamesifu juhudi zinazochukuliwa na Rais Magufuli za kupambana na mafisadi, wizi wa mali za umma, wafanyakazi hewa, mikataba mibovu na uporaji wa mali za nchi hasa madini. Hayo yalisemwa kwenye mkutano mkuu wa 24 wa chama cha watanzania waishio nchini Botswana uliofanyika mjini Gaborone kwenye kumbi za mikutano za Maharaja jumamosi iliyopita. 

Mgeni rasmi kwenye mkutano huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ambaye pia anaiwakilisha Botswana, Balozi Silvester Ambokile. Wageni wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na wawaikilishi kutoka NSSF, CRDB, NHC (T) LTD na Solomon Stocker Brokers.

Akimkaribisha Mh. Balozi Ambokile ili afungue rasmi mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama Cha Watanzania Botswana, Bw. Nieman Kissasi, alisema kuwa Watanzania waishio nje kwa ujumla wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano za kuinua uchumi wan chi na kuleta nidhamu mahali pa kazi.

 Aidha Bw. Kissasi aliendelea kusema kuwa maendeleo yaliyoko kwenye nchi za kusini mwa Afrika yanaletwa na tabia ya viongozi na wananchi wa nchi hizo kuwa na nidhamu ya kutumia kwa uaminifu kile kidogo wanachokipata. Bw. Kissasi alisisitiza umuhimu wa Watanzania kutoa ushirikiano kwa serikali ili maendeleo ya kweli yaweze kupatikana kwa haraka.

Kwa upande wake Mh. Balozi aliwahakikishia watanzania wa Botswana kuwa serikali ya awamu ya tano itatumia uwezo wake wote ili kuwaletea watanzania maendeleo. Aidha aliwasihi watanzania waishio nje kufuata sheria na taratibu za nchi wanazoishi. Pia aliwasihi kuwekeza nyumbani na kudumisha utamaduni wa kitanzania hasa kueneza lugha ya Kiswahili.

 Mh. Balozi pia alikuwa na mkutano na watanzania wote siku iliyofuata. Mkutano huu ulifanyika kwenye hoteli ya Crystal Palace na ulifuatiwa na maonyesho ya huduma zitolewazo na mashirika ya NSSF, NHC, CRDB na Solomon Stock Brockers. 

Mh. Balozi alifunga mikutano hii kwa kuwapongeza watanzania waishio Botswana kwa kuwa na umoja miongoni nao na kuwasihi wale ambao hawajajiunga na umoja huo kufanya hivyo kwani ni umoja imara na uthabiti unaostahili kuigwa na watanzania waishio nchi zingine.
 PICHANI: Mh. Balozi akiongea na watanzania kwenye Hoteli ya Crystal Palace. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Watanzania Botswana, Bw. Nieman Kissasi.

 Meneja wa huduma za Diaspora wa CRDB, Bi Lucy Naivasha, akielezea huduma zitolewazo  kwa watanzania waishio nje nchi.

 Meneja wa NHC (T) LTD, Bi Sophia Mwema, akielezea huduma zitolewazo na NHC baada ya mkutano mkuu kwenye kumbi za mikutano za Maharaja mjini Gaborone
Mh. Balozi Ambokile, wa nne kulia akiwa na baadhi ya wageni na wanachama baada ya mkutano. Pamoja naye ni mwenyekiti wa Watanzania, Bw. Kissasi, wa tatu kushoto, Meneja wa CRDB, Lucy Naivasha, wa kwanza kushoto, Meneja wa NSSF, Bi. Halima Mjala, wa pili kushoto na mwakilishi wa Solomon Stock Brockers, wa tatu kulia.

FILAMU YA BEI KALI KUZINDULIWA RASMI KESHO MLIMANI CITY

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

FILAMU ya Bei Kali inatarajiwa kuzinduliwa kesho katika ukumbi wa Mlimani City Golden Premier huku wasanii wakijinasibu kuwa ni moja kati ya filamu bora ndani ya soko la filamu.

Filamu hiyo inayojulikana kwa jina la 'Bei Kali' itazunduliwa rasmi kesho kuanzia saa moja usiku ikiwa mbashara kupitia kituo cha televisheni cha Azam Tv kwenye chaneli ya Sinema zetu na kuanza kuingia mtaani.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Daud Michael 'Duma' amesema kuwa filamu hiyo iliyofanywa chini ya Kwetu Studio imeweza kuchukua waigizaji wakubwa akiwemo Irene Uwoya, Hemed Suleiman, Patcho Mwamba na Kaptu Rado.
Duma amesema kuwa filamu hiyo inayoelezea maisha ya kawaida yenye mahusiano ndani yake yakimuhisha mwanadada aliyetoroshwa na mwanaume mwingine na kuletwa mjini lakini alipofika akajiingiza katika mahusiano mengine tofauti na baadae mumewe akaja kumtafuta mjini.

Ameeleza kuwa, filamu hiyo imejaa uhalisia zaidi na ana imani wapenzi wa filamu za kitanzania wataoendezewa nayo kwani imeweza kugusa maisha hali ya kitanzania hasa katika mahusiano na ndoa.

Filamu hiyo, imesimamiwa na Kaptu Rado sambamba na Rashidi Mrutu ambapo Duma amesema itakuja kuwakamata mtaani kwa ubora mzuri na hata waigizaji wake wameweza kutendea haki sehemu walizopatiwa.

TFS, Wizara ya ardhi, watakiwa kumaliza migogoro ya mipaka ya misitu nchini

$
0
0
Na Tulizo Kilaga, Kilwa

MKUU wa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Christopher Ngubiagai amewataka wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi kushirikiana kwa ukaribu na kwa uharaka na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kutatua migogoro ya mipaka ya misitu ili kuepusha migogoro.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya huyo alipokua akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Prof. Dos Santos Silayo anayefanya ziara yake katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Ngubiagai amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ina tatizo kubwa la suala la mipaka ya misitu kati ya kijiji na kijiji, TFS na kijiji na hasa baada ya vijiji kunufaika na mapato yatokanayo na uhifadhi wa misitu ya hifadhi, vijiji n.k.

“Mara ya mwisho nilikwenda kijiji cha Mchakama ambapo ramani zinaonyesha kabisa wananchi watakiwa wawepo katika eneo hili lakini wananchi wanasema hapana sisi mpaka tunaoutambua ni huu hivyo tunaomba Wizara ya Ardhi watusaidie kutatua tatizo ili tuweze kuendelea mbele zaidi,” alisema Ngubiagai.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TFS Prof. Dos Santos Silayo alisema wakati mwingine migogoro inatokea kutokana na kutokushirikishana na hasa kwa NGOs zinapokwenda kusaidia miradi katika vijiji bila kujali kuwa kuna mamlaka nyingine zenye mashiko na ardhi husika na hivyo kusababisha misuguano.

Prof. Silayo aliomba Wakuu wa Wilaya nchini kuwabana wale wote wanaoanzisha miradi kwenye maeno yao pasipo kuwa na ushirikishwaji wa kutosha wa wataalamu wao na hivyo kuigombanisha serikali na wananchi wake pindi wananchi wanapotakiwa kuondoka kwenye maeneo waliyovamia na hasa katika maeneo ya misitu.

Mkazi wa Kilwa Masoko, Ramadhani Hamisi alisema migogoro mingi ya ardhi katika maeneo ya misitu inatokana na sekta ya misitu hapo nyuma kushindwa kutekeleza majukumu yake hali iliyopelekea maeneo mengi ya msitu kugeuzwa shamba la bibi hadi pale ilipoanzishwa TFS na kujengewa uwezo wa kusimamia misitu hali iliyorudisha hadhi ya misitu mingi nchini.

Desemba 2015 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa wanaongeza udhibiti na usimamizi wa migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao husika.
MKUU wa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Christopher Ngubiagai (dulia) akimwelezea Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Prof. Dos Santos Silayo changamoto mbalimbali za uhifadhi wa misitu iliyopo Kilwa mapema wiki hii, Mtendaji kuu yuko kweneye ziara yake katika kikazi katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images