Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Britam Insurance waanza kuadhimisha wiki ya wafanyakazi

$
0
0
Baadhi ya waganyakazi kwa Kampuni ya Britam Insurance wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wafanyakazi wa Kampini hiyo, katika makao makuu yako, Jengo ya PPF Tower, jijini Dar es salaam.
waganyakazi kwa Kampuni ya Britam Insurance wakionekana wenye furaha tele katika wiki ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.


Tigo yasherekea wiki ya huduma kwa Mteja katika duka la Mlimani City

$
0
0

Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Chisel akijadiliana jambo na Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola na msimamizi wa duka la Tigo Mlimani City Joseph Umoti (katikati mapema jana katika duka la Mlimani city.
Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola (kushoto) akisaidiana na msimamizi wa duka la Tigo Mlimani City Joseph Umoti kutoa huduma kwa Happiness Muthali wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Maadhimisho hayo yameanza jana. 
Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola (kushoto) na msimamizi wa duka la Tigo Mlimani City Joseph Umoti wakifurahi jambo na mteja wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Maadhimisho hayo yameanza jana. 

MZEE MANGULA AKUTANA NA KIONGOZI WA PALESTINA

$
0
0
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM - Bara, Philip Mangula akizungumza na Naibu Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (FATAH), Dk. Uri Davis, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 3, 2017. (Picha na Bashir Nkoromo).

TAARIFA KWA UMMA: MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA USAJILI NA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO WA UMRI CHINI YA MIAKA MITANO KATIKA MKOA WA LINDI NA MTWARA

WANACHAMA WA MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA WAKAGUA SHAMBA LA UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA PAPAI RUAHA, IRINGA

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) Mkakati wa Dkt. Kissui Stephen Kissui akielezea malengo ya ziara YA Wakulima wanachama wa mtandao huo walipowasili katika eneo la shamba hilo lililopo Ruaha- Kware, wilayani Kilolo, mkoani Iringa, patakapolimwa zao la kibiashara la Papai. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa mtandao huo, Adam Ngamange, Wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Kilimo na Mifugo wa Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, John Mchopa, na Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya. 

Dk. Kissui amesema lengo ya ziara hiyo ni kuwaonesha Wakulima wanachama wa Mkikita mashamba wanayotarajia kuanza kulima kwa mkataba pia kuutangaza mtandao huo ili watu waanze kuwaza kijani na kila mtu arudi kwenye kilimo.

Alisema kama mtu hawezi kulima mwenyewe kuna wataalamu mbao watawekwa shambani kwa gharama nafuu ambao wataweza kuendeza mashamba hayo.

Pia, Dk. Kissui alisema wanatumia mbegu za kisasa zinazozalisha mara tatu zaidi na mbolea za Organic ambazo hazina madawa na haziharibu ardhi ili kuhakikisha vizazi na vizazi viweze kufurahia. Alisema pia Mkikita husaidia kutafuta masuala ya masoko duniani kabla ya kuanza kulima zao husika.

"Sisi tunaanza kutafuta masoko ya ndani na nje na baadaye tunawaaunganisha wakulima kwenye masoko" Alisema Kissui.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) wakiwasili Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa wakati wa ziara ya kujionea shamba lenye ekari 3000 kwa ajili ya kuwekeza Kilimo cha PAPAI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akielezea miradi ya kuhamasisha kilimo na ufugaji kibiashara wakati wa ziara ya kutembela shamba kwa ajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa.

Chama cha kuogelea kinahitaji Sh milioni 66 kwa ajili ya mashindano ya Cana kanda ya tatu

$
0
0
Wakati mashindano ya kuogelea ya kanda  ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yamebakiza takribani wiki mbili kufanyika, Chama Cha kuogelea nchini (TSA) bado kinasaka kiasi cha fedha taslimu shilling milioni 66 ili kufanikisha mashindano hayo. Mpaka sasa, jumla ya nchi nane  zimethibitisha kushiriki katika mashindano hayo ambayo yanafanyika Tanzania kwa mara ya kwanza katika hisoria ya Tanzania. Mashindano hayo yamepangwa kuanza Oktoba 19 mpaka 21 kwenye bwawa la kuogelea la Hopac la jijini.

Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka alisema kuwa pamoja na maandalizi kuendelea vizuri chini ya mwenyekiti wa  Kamati ya mashindano,  Leena Kapadia, bado hawajatimiza lengo lao kukusanya fedha kwa ajili ya mashindano  hayo. Namkoveka alisema kuwa awali walikuwa wanahitaji Sh milioni 100, hata hivyo kiasi hicho cha fedha kimepungua kutokana na wadhamini mbalimbali kujitokeza kuchangia. Wadhamini hao ni pamoja na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, Swissair, JCDecaux, , Label Promotions , Print Galore na Slipway Hotel.

“ Kamati  imeweza  kutafuta fedha kwa  makampuni 34 na bado tuna imani kati yao watajitokeza kusaidia gharama za maandalizi. Tunatoa wito kwa kampuni zilizopo ndani na nje ya nchi kudhamini mashindano haya ikiamini kuwa licha ya kujitangaza kwa biashara zao itasaidia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa mchezo wa kuogelea katika kanda ya Afrika ya Mashariki na Kati,” alisema Namkoveka.
Alifafanua kuwa viwango vya waogeleaji wa timu ya Taifa vinaendelea kuhimarika hasa kwa kutambua kuwa mashindano kwani  ni sehemu ya kujiandaa kwa mashindano ya Jumuiya Ya Madola yatakayofanyika Huko Australia Mwakani, Olimpiki ya Vijana ya Mwezi Oktoba, na Kufanyika Nchini Argentina.

Alisema kuwa mashindano haya ni sehemu ya maandalizi ya mashindano yatakatotumika kwa ajili kushiriki mashindano ya CANA kanda ya nne yatakayofanyika nchini Malawi. Wakati huo huo; Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea la Dunia (FINA) watatoa dola za kimarekani 10,000 kusaidia gharama za maandalizi.

Namkoveka alitoa  shukrani kwa  Fina  kwa kusaidia kukua kwa mchezo huu hapa Duniani na hakika wanafanya kazi kubwa ya kusaidia mchezo huu kukua. Mchango wao huu utaleta ufanisi katika mashindano haya. Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni nchi za Afrika ya Kusini, Zambia, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan ya Kusini, Djibout, na mwenyeji na  bingwa mtetezi nchi ya Tanzania.
Wakati huohuo, Chama Cha Kuogelea kimeamua kuimarisha usimamizi wa Timu ya Tanzania kwa kuteua Meneja wawili watakaoshughulikia timu ya Tanzania. Chama kimeamua kuteua mameneja wawili kwa kuwa nchi ya Tanzania kwa kuwa ni mwenyeji inaruhusiwa kuwa na timu mbili. Mameneja walioteuliwa ni Priscilla Zengeni na Jones Gouw. Waogeleaji wa Tanzania wapo chini ya makocha Alexander Mwaipasi na Michael Livingstone na baadhi ya wachezaji walioko mikoani wapo chini ya makocha wao wa Klabu au shule.

Alisema kuwa kuna changamoto ya kuweka kambi ya pamoja kwa kuwa wachezaji wanaounda timu hii wengine wanatoka Morogoro, Zanzibar, Arusha, Mwanza na Kilimanjaro na pia ni wachezaji ambao wako mashuleni wanakosoma.

PSPF YAFUNGUA OFISI MPYA PEMBA NA UKEREWE, NI SEHEMU YA WIKI YA UTUMISHI DUNIANI

$
0
0




NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID.

MFUKO wa Pensheni wa PSPF,  umezindua ofisi mpya mbili moja kisiwani Pemba na nyingine kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko huo, Bi. Laila Maghimbi alisema, ofisi hizo zimezinduliwa rasmi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza leo Oktoba 2, 2017.

“Mtakumbuka kwamba wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka,  huadhimishwa wiki ya huduma kwa wateja duniani, na kwa mwaka huu, Mfuko umzindua ofisi mpya kule Pemba na Ukerewe ili kuboresha zaidi huduma zetu.”

Akizungumzia mtandao wa PSPF nchini, Bi. Maghimbi alisema, “PSPF ina ofisi kila makao makuu ya mkoa Tanzania Bara na Visiwani.”
Bi. Maghimbi alisema, sambamba na ufunguzi wa ofisi mpya,
hapa makao makuu mtaona tunaadhimisha kwa kushirikiana na washirika wetu kwenye utoaji huduma mbalimbali, ili kuwapatia fursa wananchama wetu ya kupata huduma kutoka taasisi hizo washirika.
Aliwataja washirika hao ambao wameweka mabanda ya kutoa huduma kuwa ni pamoja na Mfuo wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), benki za TPB, NMB, CRDB na Benki ya Walimu, (MCB).

Alisema, PSPF katika maadhimisho hayo, inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wastaafu wanaofika kujua mafao yao, pia kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS.

Miongoni mwa wanachama wa PSPF waliofika kupatiwa huduma ni pamoja na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi ambaye alisifu huduma za haraka zitolewazo na maafisa wa PSPF.

“Kwa kweli mimi nimeridhishwa na huduma niliyopatiwa hapa, nimefika hapa kufuatilia malipo ya mirathi ya ndugu yetu, na nimepokelewa vizuri na kupatiwa huduma stahiki bila ya ucheleweshwaji, hili ni jambo jema na niwapongeze PSPF kwa uchapakazi wa namna hii.” Alisema Dkt. Msengi.

MKAZI WA CHATO GEITA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UONGO MTANDAONI

$
0
0
 MKAZI wa Chato Geita, Obadia Frank (41), alipokua akingia katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaa leo kusomewa mashtaka yanayomkabili ya Kuchapisha taarifa ya uongo chato Geita.
MKAZI wa Chato Geita, Obadia Frank (41), akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mara baada ya kusomewa mastaka yanayomkabiri jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Na Karama Kenyunko Bloguya Jamii.
MKAZI wa Chato Geita, Obadia Frank (41), mapema leo  amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni.

Akisomewa  hati ya mashtaka na wakili wa serikali Leornad Challo amedai mshtakiwa huyo ambayeni wakala wa Baypot ametenda  kosa hilo gosti 8 mwaka huu, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Mbele ya Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri imedaiwa kuwa siku hiyo mshtakiwa Frank alichapisha taarifa kupitia ukurasa wake wa facebook inayosema,Taarifa kutoka kikao cha mazungumzo kati ya serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia kuwa wanasheria wa upande wetu wanashindwa kutafsiri baadhi ya vifungu vya sheria hadi kufikia kuomba msaada kwa wanasheria wa Acacia sasa huoni hivi ni vituko mwizi anakusaidia sharia haahaa haha.

 Mazungumzo bado yanaendelea lakini wanasheria wetu wamebanwa sana ukizingatia wale jamaa wanavielelezo vyote vya mikataba kiukweli tumuombe mungu maaa serikali ikitaka kkuvunja mkataba na Acacia gharama kubwa zitatuhusu lakini pia kuendekeza vyama itatugharimu sana baada ya Mh. Rais Magufuli angewashilikisha wakina  mawakili wasomi waliokwiva wakili Tundu Lisu, wakili Kibatara na Fatma Karume kwenye mambo muhimu kama haya yeye kaleta uchama sasa itatugarimu// DitectaMagufulimustgo”

Imedaiwa mshtakiwa ametenda hayo huku akijua kuwa taarifa hizo ni uongo na zilikuwa na nia ya  kuipotosha jamii 
Hata hivyo mshtakiwa huyo anayetetewa na wakili Peter Kibatala, amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza mashtari na kesi hiyo itatajwa Octoba 16 mwaka huu. 

Mahakama imemtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wakuaminika ambao walitakuwa kuweka bondi ya milioni tano.

WAZIRI MBARAWA: WAKANDARASI JENGENI BARABARA KWA VIWANGO

$
0
0
Serikali imesema itahakikisha inaendelea kuwasimamia wakandarasi wa Ujenzi wa Barabara kuhakikisha wanajenga barabara zote nchini kwa viwango vilivyokusudiwa na kumaliza kwa wakati ili kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa leo jijini Dar es salaam baada ya kukagua Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano jijini humo ambapo ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wake na kusisitiza kwa Wakala wa Baraba (TANROADS), mkoa wa Dar es salaam kuwa wakali katika usimamizi ili kuhakikisha barabara hizo zinajengwa kwa viwango vilivyokubaliwa kwenye mkataba.

“ Serikali imekuwa ikitumia Fedha nyingi katika kutekeleza miradi hii, hivyo TANROADS hakikisheni mnasimamia wakandarasi hawa kujenga barabara hizi kwa viwango na kwa wakati”, amesema Waziri Mbarawa. Aidha, Waziri Mbarawa amefafanua kuwa utekelezaji wa awamu hiyo unaendelea vizuri ambapo unahusisha barabara ya Kifuru – Msigani (km 4.5) ambayo kwa sasa imefika asilimia 87, Goba – Makongo (km 4.5), nayo imefikia asilimia 52 na Goba – Madale (km 5) yenye asilimia 5.

Profesa Mbarawa ametoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi naTANROADS mkoa wa Dar es salaam wakati mradi huo ukiendeleaa kutekelezwa ili kusaidia kumaliza kwa wakati.

Waziri Mbarawa amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kushughulikia suala la ulipaji wa fidia kwa wananchi wa maeneo hayo ambao wamepitiwa na mradi huo. Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es salaam, Mhandisi Julius Ndyamkama, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa watasimamia mradi huo usiku na mchana ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyo bora.

Mhandisi Ndyamkama amebainisha changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa mradi huo ikiwemo suala la ulipaji wa fidia kwa baadhi ya maeneo hasa katika kipande cha barabara chenye urefu wa kilometa 1 kuanzia Mto Mbezi kuelekea Makongo. Naye, Mratibu wa Mradi wa barabara ya Goba – Madale (km 5), kutoka kampuni ya Ujenzi ya Mwananchi Engineering and Contracting Co. Ltd (MECCO), Mhandisi Crispin Mwombeki, amesema kuwa tayari wameshakamilisha usanifu wa mradi na wanategemea kuanza kazi za Ujenzi hivi karibuni.

Utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya mradi wa Ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano katika jiji la Dar es salaam umeanza mwezi Desemba, mwaka 2016 ambapo umehusisha barabara tatu za Kifuru – Msigani (km 4.5), Goba – Makongo (km 4.5), na Goba – Madale (km 5) na kugharimu Jumla ya Shilingi Bilioni 24.2.

Waziri Kairuki Azindua Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma

$
0
0

Eliphace Marwa-MAELEZO.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amezindua bodi mpya ya mishahara na masilahi katika utumishi wa umma mapema jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo waziri Kairuki ameitaka bodi hiyo kuzingatia misingi iliyopo kwenye hati maalum ya Rais ambayo inawataka kuzingatia vigezo ambavyo ni pamoja na malipo ya mishahara na masilahi kwa watumishi wa Umma yanapatikana na kuwa endelevu.

“Ni vema kuhakikisha utumishi wa Umma unavutia na kubakiza taaluma zinazohitajika katika kuendesha shughuli zake ili kuweza kuleta tija kwa kuzingatia uwazi, usawa na haki mahala pa kazi”, alisema Waziri Kairuki.Aliongeza kuwa endapo bodi itazingatia vigezo hivyo, ushauri watakaoutoa utakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa na hivyo kujenga imani kwa watumishi wa Umma na wadau wengine.

Waziri Kairuki aliahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa bodi hiyo na kusema kuwa Serikali iko pamoja nayo katika kuhakikisha masiilahi ya watumishi wa Umma yanaboreshwa ili kuongeza tija kwa kuwabakiza wataalam katika Utumishi wa Umma.Naye Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Donald Ndagula ameahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zitakazojitokeza kwa kwa kufanya tafiti.

“Napenda kusema kuwa pamoja na changamoto zilizopo katika bodi tutashirikiana na Serikali katika kuboresha hali ya utendaji katika utumishi wa Umma kwa kufanya tafiti kwa lengo la kuishauri Serikali ili iweze kuwapatia maisha ya staha Watumishi wa Umma”, alisema Ndagula.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro na kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa bodi hiyo Bi. Mariam Mwanilwa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akimkaribisha Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki kuzungumza na wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Bodi ya Pili ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma pamoja na Sekretarieti ya bodi hiyo wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA WABUNGE WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUTOKA TANZANIA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mheshimiwa Abdullah Makame (katikati) ambae ni kiongozi wa msafara wa Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.

WAZIRI MBARAWA: WAKANDARASI JENGENI BARABARA KWA VIWANGO

$
0
0
Serikali imesema itahakikisha inaendelea kuwasimamia wakandarasi wa Ujenzi wa Barabara kuhakikisha wanajenga barabara zote nchini kwa viwango vilivyokusudiwa na kumaliza kwa wakati ili kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa leo jijini Dar es salaam mara baada ya kukagua Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano jijini humo ambapo ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wake na kusisitiza kwa Wakala wa Baraba (TANROADS), mkoa wa Dar es salaam kuwa wakali katika usimamizi ili kuhakikisha barabara hizo zinajengwa kwa viwango vilivyokubaliwa kwenye mkataba.

“ Serikali imekuwa ikitumia Fedha nyingi katika kutekeleza miradi hii, hivyo TANROADS hakikisheni mnasimamia wakandarasi hawa kujenga barabara hizi kwa viwango na kwa wakati”, amesema Waziri Mbarawa.

Aidha, Waziri Mbarawa amefafanua kuwa utekelezaji wa awamu hiyo unaendelea vizuri ambapo unahusisha barabara ya Kifuru – Msigani (km 4.5) ambayo kwa sasa imefika asilimia 87, Goba – Makongo (km 4.5), nayo imefikia asilimia 52 na Goba – Madale (km 5) yenye asilimia 5.

Profesa Mbarawa ametoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi naTANROADS mkoa wa Dar es salaam wakati mradi huo ukiendeleaa kutekelezwa ili kusaidia kumaliza kwa wakati.


PPF YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MAABARA

$
0
0
MFUKO wa Pensheni wa PPF umetoa msaada wa vifaa vya maabara vyenye thamani ya zaidi ya shillingi milioni 6.7 kwa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi vifaa hivyo katika mahafali ya tisa ya kidato cha nne shuleni mwishoni mwa wiki,Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio amesema Mfuko umeamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kutengeneza uchumi wa viwanda.

Bw.Erio ambaye pia alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, amebainisha kuwa Mfuko wa Pensheni wa PPF utaendelea kushirikiana na taasisi za elimu nchini katika jitihada za kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Pia Bw.Erio amesema ushirikiano mzuri uliopo kati ya shule ya Canossa na PPF pia ni moja ya sababu kupeleka vifaa hivyo shuleni hapo..

“Shule ya Canossa imekuwa miongoni mwa waajiri wanaowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati bila kuchelewesha,na idadi kubwa ya wafanyakazi wake ni wanachama wa Mfuko wetu,” amefafanua Mkurugenzi Mkuu.
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio akikabidhi moja ya Vifaa vya maabara kwa mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa Mhandisi Magayane Machibya wakati wa mahafali ya tisa ya ka kidato cha nne Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (Kulia) akimkabidhi cheti Joyce Msumari (Kushoto) mhitimu wa kidato cha Nne katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa iliyopo jijini Dar es Salaam.  Joyce Msumari ni mmoja wa wanufaika wa Fao la Elimu linalotolewa na PPF kwa watoto wa wananchama wanaofariki wakiwa katika Ajira.  
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa, Mhandisi Magayane Machibya (Kushoto) na Mkuu wa Shule hiyo Sista Irene Natumanya wakifurahia kupokea vifaa vya maabara kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio (hayupo pichani) 
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Canossa Sista Irene Natumanya (Kulia) akimpa mkono wa shukrani Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio (Katikati) baada ya kukabidhiwa vifaa vya maabara na Mfuko wa PPF mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Shule hiyo Mhandisi Machibya Magayane.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DIAMOND AGAWA VIFAA TIBA NA ZAWADI KWA WAGONJWA HOSPITALI YA AMANA

$
0
0
 Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond) akimsalimia mtoto wa Mama Nadia Iddi ambaye amejifungua katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam ambapo msanii huyo alifika kuwatembelea watoto waliozaliwa hospitalini hapo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa
 Meneja wa Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond), Said Fellaakizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufika katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam kutoa msaada wa Vifaa tiba.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond) akiwa ameongozana na Mtangazaji wa kipindi cha leo Tena Dahuu kwenda kutoa msaada katika hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam
 Msanii wa muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond), akisalimiana na Mmoja ya wamama aliyopo na mtoto wake katika wodi ya watoto ya Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond) akiwa katika maeneo ya Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam
 Msanii wa muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond) akiwa na Mtangazaji wa kipindi cha leo tena cha Clouds Fm Dahuu wakati alipowasili katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam

TUNASUBIRI MASAA 48 TUJUE MAENDELEO YA NGOMA- DAKTARI

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Baada ya kuumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma na kushindwa kufanya mazoezi jana pamoja na kikosi kutokana na maumivu ya misuli siku ya Jumamosi.


Ngoma baada ya kuumia hakuweza kurejea tena uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi, siku ya  jana hakufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenginena kupewa mapumziko na daktari wa timu Hussein Bavu.


Ngoma alipewa saa 24 hadi 48 za uangalizi chini ya daktari wa Yanga ili kuona maendeleo kabla ya kutoa majibu kama anaweza kurudi uwanjani mapema au vinginevyo.


Dakatri wa timu hiyo Bavu amesema kuwa baada ya masaa 24 hadi 48 ndipo wanaweza kutoa majibu sahihi kwani kwa sasa wamempa mapumziko Ngoma ili aweze kurejea katika hali ya kawaida na kuangalia maendeleo yake.


Kwa sasa maendeleo ya Ngoma yanaendelea vizuri na anatembea vizuri ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzo, anaweza kufanya mazoezi binafsi ikiwa ni tiba ya jeraha lake


Yanga inakabiliwa na mchezo wa raundi ya sita ya ligi kuu VPL dhidi ya Kagera Sugar October 14, 2017 kwenye uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.




NEEMA YA MAJI YA DAWASCO YAIVA MBEZI MAKABE MPAKA MSAKUZI

$
0
0
Mmoja wa Vibarua wanaochimba mtaro wa kutandika bomba la maji linaloelekea Mbezi Makabe akiwa anaendelea na kazi ya kuchimba mtaro

Bomba la Maji Safi kutoka Dawasco ambalo limetandikwa ndani ya mtaro kuelekea Mbezi Makabe mpaka Msakuzi kwa ajili ya kupeleka maji safi , Wakazi wa eneo hilo wanapata maji ya Bomba kwa mara ya kwanza katika utawala wa awamu ya tano ya Dk John Pombe Magufuli tangu nchi hii ipate uhuru
Kibarua wa kuchimba mtaro akiendelea na kazi ya kuchimba mtaro kwa ajili ya kupitisha bomba la Maji ya Dawasco katika eneo la Mbezi Makabe mpaka Msakuzi
Bomba la Maji likiwa limetandikwa kwenye mtaro tayari kwa ajili ya kufukiwa kwa ajili ya kupeleka maji Mbezi Makabe mpaka Msakuzi . Picha zote Na Humphrey Shao

VIJANA KATA YA BUZA WAUNGANA KUPAZA SAUTI KATIKA KUJILETEA MAAENDELEO YAO.

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

Vijana wa kata ya Buza katika  mtaa wa Kidagaa wamejitokeza kwenye semina ya mafunzo  ya kujiunga na taasisi ya sauti ya vijana (MYIDC) Temeke  ili kuepukana na changamoto za kukaa mitaani bila kazi maalumu ya kufanya .

Nae Mwenyekiti Mtendaji  MYIDC,  Ismae  Mnikite amesema hayo  katika semina hiyo iliyofanyika mtaa wa Kidagaa  kata ya Buza  halmashauri ya Temeke  amesema kuwa lego la mafunzo hayo ni kutaka kuwafanya vijana waweze kuunda jukwaa la vijana na  baada ya hapo watapatiwa mafunzo kuhusu dira ya vijana na pia lengo likiwa ni kupaza sauti zao katika kuleta maendeleo.

Naye mkazi wa Buza kata ya Kidagaa Fatma Ramadhani  amesema kuwa amepata mwamko huo wa kijiunga  na taasisi hii ya sauti ya vijana (MYIDC) ili kuepukana na changamoto ya kukaa  tu mitaani ameona ni vizuri kutumia fursa zinazotolewa kama kujiunga katika vikundi vya ujasiliamani ili kujikwamua kiuchumi hapa Nchini.

Mkazi mwingine naye Rajabu Charz amesema kuwa  katika mafunzo hayo amejifunza  namna ya kutafuta na kuweka mtaji kwa ajili ya kuanzisha biashara na kuondoa woga wa   kuthubutu katika kafanya jambo la kuleta mafanikio.
 Mwenyekiti Mtendaji  MYIDC,  Ismae  Mnikite akizungumza na waandishi wa habari pamoja na vijana wa mtaa wa Kidagaa kuhusu umuhimu wa mradi wa Sauti ya Vijana (MYID) katika kata ya Buza mtaa wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 Muwakilishi wa Diwani kata ya Buza, Mahmoud Rashidi akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu changamoto  zinazowakabili vijana na kujitahidi kujitokeza kwenye shuhuli kama hizi  kutokana na  kuwa na utayari, pia amewapongeza vijana wa kata hiyo kwa kujitokeza  kuhudhuria mafunzo hayo katika kata ya Buza mta wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 Mkazi wa  Buza  kata ya Kidagaa, Fatma Ramadhani akizungumza na waandishi wa habari kususu kuchangamkia fursa na kutoa pongezi za dhati kwa sauti ya vijana  MDYDC kwa kuona umuhimu wao kama vijana Taifa la kesho katika kata ya Buza mta wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar Es Salaam.
 Mkazi wa kata ya Buza mtaa wa Kidagaa, Rajabu Charz akizungumza na waandishi wa habari katika kata ya Buza mta wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke akitoa wito kwa vijana wenzake kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza  hapa Nchini.
Wakazi wa kata ya Buza mtaa wa Kidagaa waliojitokeza kuhudhuria semina ya mafunzo yaliyotolewa na Mradi wa sauti ya vijana MYIDC ikiwa lengo ni kupata sauti ta vijana pale inapotakiwa kufika ili kuleta maendeleo hapa Nchini.Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 33 WA JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA (ALAT) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu Mhe Kassim majaliwa akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kufungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jaffo mbele ya Rais Dkt magufuli wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiongea machache wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Bw. Gulma Hafeez Muccadam akisoma risala yao mbele ya Rais Dkt magufuli wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.

UWT MKOA WA MBEYA WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI KUELEKEA MAHADHIMISHO YA MIAKA 38

$
0
0

Na Mwandishi wa Globu ya Jamii Mbeya

Umoja wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) wilaya ya Mbeya mjini imendesha zoezi la kutoa elimu ya afya ya uzazi na Maendeleo kwa wanafunzi wa shule ya kutwa ya Mbeya .

akizungumza na Globu ya Jamii Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya , Mary Mwenisongole amesema kuwa kwa kushirikiana na wataalam wa afya na Maendeleo ya jamii,leo tarehe wameshiriki kutoa elimu ya afya na kujitambua kwa watoto wa kike zaidi ya 500 shule ya sekondari ya kutwa Mbeya ikiwa ni sehemu ya maazimisho ya wiki ya miaka 39 ya jumuiya ya wanawake.

'' Sisi kama Jumuiya ya Wanawake wa chama kikongwe hapa nchini tumeona kuwa katika shamra shamra za miaka zaidi ya 38 ya Jumuiya yetu ndani ya chama ni vyema tukaanza kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wa kike waliopo mashuleni kwani wao ndio Viongozi wa UWT ya baadae" amesema .

Akishukuru kwa niaba ya ya Walimu mwalimu wa nidhamu Benson John aliishukuru jumuiya kwa jambo walilofanya na kuomba waendelee kwani tatizo la mimba ni kubwa na kwa mwaka huu 2017 kufikia mwezi wa 9 wanafunz 6 wameshindwa kuendelea na masomo yao kutokana na tatizo la ujauzito.

UWT mkoa wa Mbeya imewahakikishia walimu kuwa zoezi hili lita kuwa endelea na katibu UWT ameahidi kufika mara nyingi iwezekanavyo kupitia mpango wa sauti ya shangazi ambayo imepokelewa kwa shangwe, na wanafunzi wameahidi kutoa ushirikiano kwa SHANGAZI.
Katibu wa UWT mkoa wa Mbeya Mary Mwenisongole akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya katika programu ya Ongea na Shangazi
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mbeya Mjini Mama Mtani akizungumza na na Wanafunzi wa kike wa Mbeya kutwa

REACHING SUSTAINABLE DEVELOPMENT GOALS WITH NUCLEAR ENERGY

$
0
0
With globalized economics and a new era of global interconnectedness all counties and stakeholders share the same responsibilities, to ensure a safe and sustainable future for generations to come. 

In this regard the United Nation has traced 17 Sustainable Development Goals (SDG) to be followed by all nations for all nations. These goals provide clear guidelines to tackle the root causes of poverty, hunger, climate change and unite all necessary efforts to make a positive change for mankind and the planet.



It is generally accepted that science and technological innovations need to play a fundamental role in assisting global leaders to find the answers to pending issues.It is therefore no surprise that nuclear science and innovative nuclear technologies are playing a major role in providing viable solutions to help achieve these ambitious SDG targets. It is well known globally that nuclear technologies have much to offer in the fight against poverty, hunger, dread diseases, and water shortages, not to mention its ability to provide sustainable and environmentally friendly electricity.



Let’s take a closer look these various applications.

Nuclear medicine helps millions of people across the globe to successfully fight cancer and has reducedthe mortality rate of non-communicable diseases by one third. Moreover, nuclear science centers and research facilities are indispensable in the production of radioisotopes which are used in complex medical treatments.



Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images