Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1940 | 1941 | (Page 1942) | 1943 | 1944 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Waumini wa kanisa la TAG wakichangia Damu kwaajili ya kuwasaidia watanzania wanye maitaji maalumu.
   Makamu Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Tanzania Assemblies of God  Kinondoni,Greyson Nyantamba (wakwanza kulia)akizungumza na Michuzi blog  juu ya kuchagia damu kwaajili ya kuwasaidia watanzania wenye maitaji ya damu katika maazimisho ya siku ya vijana jijini Dar es Salaam.

   Waumini wa kanisa la TAG wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kuchangia damu.
  (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

  0 0

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umezindua ofisi mpya mbili moja kisiwani Pemba na nyingine kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.

  Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko huo, Bi. Laila Maghimbi alisema, ofisi hizo zimezinduliwa rasmi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

  “Mtakumbuka kwamba wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, huadhimishwa wiki ya huduma kwa wateja duniani, na kwa mwaka huu, Mfuko umzindua ofisi mpya kule Pemba na Ukerewe ili kuboresha zaidi huduma zetu.”

  Akizungumzia mtandao wa PSPF nchini, Bi. Maghimbi alisema, “PSPF ina ofisi kila makao makuu ya mkoa Tanzania Bara na Visiwani.”Bi. Maghimbi alisema, sambamba na ufunguzi wa ofisi mpya,hapa makao makuu mtaona tunaadhimisha kwa kushirikiana na washirika wetu kwenye utoaji huduma mbalimbali, ili kuwapatia fursa wananchama wetu ya kupata huduma kutoka taasisi hizo washirika.
  Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakihudumiwa kwenye ofisi ya huduma kwa wateja makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
  Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akihudumiwa kwenye ofisi ya huduma kwa wateja makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
  Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akihudumiwa na Bi.Elizabeth Shayo, (kulia), makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.


  0 0

  Chaneli ya Sinema Zetu inayopatikana katika Televisheni ya Azam, leo imetangaza rasmi uzinduzi wa Tamasha lake lakutoa Tuzo na mchango wa tasnia ya Bongo Movies maarufu 'Sinema Zetu International Film Festival' litakalofanyika kuanzia January Mosi, 2018 hadi February 28, 2018.

  Katika Tamasha hilo pia kutakuwa na Shindano litalokusanya Filamu zaidi ya 150 kutoka Mikoa mbalimbali kama Morogoro, Mwanza, Dodoma ambapo jumla ya Mikoa nane.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kiongozi Mkuu wa Tamasha hilo, Jacob Joseph amesema kuwa watazunguka Mikoa Sita kwa ajili ya kuzungumza na Wadau wa tasnia hiyo ikiwa sambamba na kutoa elimu yakutosha na kuweka uelewa juu ya Tamasha hilo.

  Mshauri wa Tamasha hilo, Prof. Martin Mhando amesema kuwa Shindano hilo la Filamu katika Televisheni litakuwa na vipengele vitatu ambapo litahusisha Bongo Movies 'Filamu Kubwa', Filamu Fupi za dakika 45, pia Makala za Filamu nazo zitahusika.

  Balozi wa Tamasha hilo, Elizabeth Michael 'Lulu' ameshukuru kupewa ubalozi katika Tamasha hilo ikizingatiwa kwamba yeye ni Msanii atakayebeba Nembo ya Taifa la Tanzania katika nchi jirani zitakazoshiriki Tamasha hilo kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.
   Mshauri wa Tamasha hilo, Prof. Martin Mhando akifafanua jambo kwa Wanahabari kuhisiana na Tamasha hilo linavyoleta mapinduzi katika Lugha ya Kiswahili nchini Tanzania.
   Balozi wa Tamasha hilo la SZIFF, Elizabeth Michael maarufu kama LULU akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari kuhusu Tamasha hilo la Kimataifa la Sinema Zetu na jinsi atakavyoshiriki kama Msanii wa Bongo Movie.
   Kiongozi Mkuu wa Tamasha la Filamu Kimataifa, Jacob Joseph akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar katika uzinduzi wa Tamasha hilo litakaloanza kufanyika January Mosi hadi February 28, 2018.


  0 0


   Madaktari Bingwa wakiendelea kumpa huduma mmoja wa wangonjwa wa macho katika hospitali ya Sokoine Lindi.
  Baadhi ya vifaa tiba na dawa zilizotumika katika zoezi hilo vikikabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa Lindi Bwana Godfrey Zambi.
   Daktari Bingwa wa watoto Martha Mkonyi akimuhudumia mmoja wa watoto waliokuja kupata huduma.

  MWENYEKITI wa Bodi  ya Wakurugenzi wa Mfuko  wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Spika Mstaafu  Anne Makinda amewahimiza watoa huduma katika vituo vya matibabu kujenga utamaduni wa kuwapenda na kuwaheshimu wagonjwa ili kuwapa faraja na huduma bora wanapokwenda kupata matibabu katika vituo vyao.

  Akizunguza wakati wa uzinduzi wa huduma za madaktari bingwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi, Mama Makinda amesema wagonjwa wengi hususan wanawake wajawazito wanaogopa kwenda kupata huduma za mazitbabu katika vituo hivyo kutokana na mapokezi mabaya wanayopata hivyo wanaamua kwenda kwa wakunga wa jadi au kujifungulia majumbani ambako hakuna mazingira salama.

  Amesisitiza kuwa wahudumu wa vituo vya matibabu wanawajibika kuwa na lugha nzuri na huruma kwa wagonjwa kwani kazi wanayofanya inaweza kuwa na mafanikio au madhara makubwa kwa afya za watu wanapwahudumia.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Bernald Konga amesema Mfuko huo umepania kufikisha huduma bora kwa kila mtanzania hivyo hatua ya kupeleka madaktari bingwa katika mikoa yenye mahitaji makubwa ya huduma hiyo ni hatua mojawapo ya kusogeza huduma karibu na watanzania wengi.

  Amesema kuanzia mwaka 2013 hadi sasa Mfuko umeshapeleka madaktari bingwa katika mikoa 17 ambapo mikoa minne imepata huduma hizo mara mbili. Mikoa hiyo ni pamoja na Kigoma, Rukwa, Lindi na Mtwara. 

  Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne cha utekelezaji wa mpango huo katika mikoa ya pembezoni zaidi ya wananchi Elfu Kumi na Tisa wamehudumiwa na madaktari bingwa ambapo zaidi ya Mia saba wamefanyiwa upasuaji wa kibingwa.

  0 0

  TPA imekabidhi jumla ya vitanda saba (7) vya kujifungulia akina mama pamoja na vyandarua mia tatu (300) kwa hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Musoma iliyopo Mkoa wa Mara.

  Hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa tiba hivyo vyenye thamani ya Sh. Milioni 15 imefanyika Jumatatu Oktoba 02, 2017 hospitalini hapo ambapo mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA alivikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Naibu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Lazaro Twange amesema msaada huo ambao umetolewa na TPA ni sehemu ya jitihada za kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuboresha sekta ya huduma za afya.

  Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dk. Vincent Naano ameishukuru TPA kwa kuacha shughuli zake nyingine muhimu na kuamua kutoa msaada huo mkubwa kwa Mkoa wa Mara.

  “Msaada huu hautatumika kwa hospitali kuu tu bali utasambazwa kwa vituo vingine vya afya vya bweri, nyasho, mwangi na nyamatare ambako utasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wanaofika hospitali kuu kwa kukosa huduma vituoni” amesema Dk. Naano.

  Ameongeza kwamba Wilaya ya Musoma inashirikiana kwa karibu na Mamlaka mbalimbali katika kuwaletea Wananchi wake maendeleo na kukumbusha kwamba mwaka juzi (2015) TPA iliisaidia Wilaya yake kwenye ununuzi wa madawati na sasa imesaidia sekta ya afya na kuwaasa wadau wengine kujitokeza kusaidia hasa katika ujenzi wa madarasa ambao kuna upungufu mkubwa.

  Sera ya TPA ya misaada kwa jamii inalenga katika kuchangia huduma za Afya, Elimu na Maendeleo ya Jamii ambapo katika kipindi cha mwaka 2016/2017, yatari Mamlaka imetoa msaada wenye thamani ya Shilingi Milioni 75 kwa bandari zilizopo kwenye Ziwa Victoria pekee.
  Naibu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Lazaro Twange (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa vitanda vya kujifungulia akina mama kwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dk. Vincent Naano (kulia).

  0 0  Asteria Muhozya na Greyson Mwase. 

  Timu ya wataalam kutoka Uganda imewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta. Mbali na kubadilishana uzoefu wataalam hao watafanya ziara Ziwa Eyasi Wembere lililopo mkoani Singida.

  Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo wataalam hao leo tarehe 2 Oktoba, 2017 wamefanya kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani na kuwashirikisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).

  Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kalemani amesema maandalizi hayo ni juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli za kuhakikisha kuwa rasilimali ya mafuta inagunduliwa na kuanza kuleta manufaa kwa wananchi, ambapo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Ujenzi wa Mradi ya Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania tarehe 5 Agosti, 2017 alieleza kuwa wataalam waliogundua mafuta katika Ziwa Abert nchini Uganda kushirikiana na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na Eyasi nchini Tanzania.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha wataalam kutoka Uganda, Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) kabla ya kuanza ziara katika Ziwa Eyas Wembere lililopo mkoani Singida. 
  Wataalam kutoka , Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani). 
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande (kulia) pamoja na wataalam kutoka Uganda wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto mbele) akieleza jambo katika kikao hicho.


  0 0

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
  MKURUGENZI wa Utafiti na Mipango wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Samweli Mvingira na Naibu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Judith Msuya, wamehukumiwa kwenda jela miaka mitatu ama kulipa faini ya Milioni 20  baada ya kupatikana na hatia katika kosa la kutumia madaraka vibaya.

  Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha ambaye amesema upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi washtakiwa pasipo kuacha shaka.

  Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha amesema amewatia hatiani washtakiwa kwa makosa manne ya kutumia madaraka yao vibaya na kuwaachia huru katika kosa la tano ambalo jamuhuri wameshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

  Akisom adhabu hiyo amesema, washtakiwa wanatakiwa kulipa faini ya Milioni 5 kuanzia kosa la kwanza hadi la nne na endapo watashindwa wataenda jela miaka mitatu kwenye kila kosa.

  Katika kesi hiyo washtakiwa walikuwa watatu akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade ambaye alifariki wakati shahidi wa kwanza akitoa ushahidi.

  Inadaiwa, kati ya September 2007 na July 2008, Makao Makuu ya TanTrade Wilaya ya Temeke walitumia madaraka yao vibaya kwa kuagiza gari lililotumika kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma iliyosababisha AL Hamadi Motors FZD kupata faida ya Tsh. 34,895,400.

  Aidha, inadaiwa tarehe hiyo hiyo na mahali hapo, washtakiwa kwa kutumia madaraka yao vibaya, walinunua gari iliyotumika kwa lengo la kumnufaisha Humer Stars kiasi cha Tsh. 32,773,475.
  Washtakiwa wanadaiwa bila kufuata utaratibu wa kushindanisha zabuni kuagiza gari iliyotumika na kusababisha AL Hamad kupata faida ya Tsh. 34,895,400, hata hivyo katika shtaka la nne watuhumiwa walinunua magari bila kufuata utaratibu wa zabuni.

  Pia washtakiwa waliachiwa huru ambapo Jamuhuri ilishindwa kuthibitisha, washtakiwa walidaiwa kutumia madaraka yao vibaya, uzembe na kumsababishia mwajiri wao hasara ya Tsh. 49,145,855.05.
   Hata hivyo, mshtakiwa Mvingira amefanikiwa kulipa faini na yuko huru.

  0 0
  Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewataka wananchi kuzingatia Sheria wakati wa ujenzi wa makazi yao ili kuepuka kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa jambo linalosababisha bomoa bomoa isiyo ya lazima.

  Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Angelina Mabula aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Siku ya Makazi duniani ambayo yalifanyika katika ukumbi wa Karimjee.

  Mhe.Mabula alisema kuwa ni vyema wananchi wazingatie sheria kabla hawajaanza kujenga makazi yao husika kwa kutoa taarifa kwenye ofisi husika ili kuepuka ukiukwaji wa Sheria za nchi katika ujenzi wa makazi.
  “Watanzania tunakumbushwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchi kwa sababu ubomoaji unaofanyika siyo kwa makusudi bali ni kwasababu tu watu wamekiuka Sheria zilizopo na pengine watumishi wasio waaminifu ndani ya Serikali ambao wanawapa watu maeneo pasiporuhusiwa”, alisisitiza Mhe. Mabula

  Akizungumuzia mpango mkakati wa Wizara hiyo Mhe. Mabula alisema kuwa zaidi ya Miji 26 nchini ikiwemo Mtwara, Singida Mwanza na Dar es Salaam iko kwenye mchakato wa kupangilia makazi yake na kuwawezesha wananchi kuondokana na adha ya msongamano wa makazi.
   
  Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula akihutubia katika hafla ya maadhimisho ya 32 ya makazi duniani kutoka kulia ni mkurugenzi wa nyumba Bw.Pius Tesha na wa pili kulia ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala maadhimisho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
  PICHA 1
  Mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi Dkt.Lucas Mataba kulia akitoa salam kwa Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula wa kushoto  katika maadhimisho ya makazi duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam leo wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala.
  PICHA 2
  mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala kushoto akitoa maelezo kwa wadau wa nyumba na makazi katika maadhimisho ya 32 ya makazi duniania yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kutoka kulia ni Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula na wa pili kushoto ni Mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi Dkt.Lucas Mataba.


  0 0


   Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Wauguzi Tanzania  (TANNA)  kutoka sehemu mbalimbali wakiungana na wajumbe wenzao pamoja na viongozi wa Tanna Mkoa wa Lindi jana katika kufanya maandalizi ya Mkutano Mkutano Mkuu  wa 45 unao tarajiwa kufanyika Oktoba 4-6 Kitaifa  ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mh. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.( PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

   Mwenyekiti wa Chama Cha Wauguzi Tanzania (TANNA) Mkoa wa Lindi, Patrick Achimpota (kulia) mwenyeshati la kitenge akisalimiana na mjumbe wa Kamati kuu ya Chama hicho kutoka Arusha, Hosea Naman mara alipofika Mkoani humo kwa niaba ya Mkutano Mkuu wa Chama hicho.


   Wajumbe wa Chama Cha Wauguzi (TANNA) wakiwa katika safari kuelekea Mkoa wa Lindi katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho  unao tarajiwa kufanyika Oktoba 4-6 Kitaifa ambapo unatarajiwa kufunguliwa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa.   Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Lindi, Damasiana Msala (kulia)  akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Wauguzi (TANNA) mara walipowasili katika mkoa huo jana
   Makamu wa Rais wa Chama hicho, Ibrahim Mgoo (wa katikati) akisalimia wajumbe mara baada ya kuwasili katika Mkoa huo jana, kulia ni Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Lindi, Damasiana Msala na kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Sebastian Luziga. 

  0 0

  •   Itashutiwa katika miji ya Berlin, London, Paris, Cape Town, Acapulco na  Mexico
  •  Mastaa wakubwa duniani kama Eric Dane wa Last ship, Gerard Depardieu wa Life of Pie,  Thomas Kretschmann wa Avengers Pearl Thusi  wa  Quantico…kushiriki
  NYOTA ya aliyekuwa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Mtanzania Idris Sultan, inaendelea kung’ara  baada ya ‘kupata shavu’ la kushiriki filamu yenye bajeti ya dola za Kimarekani milioni 17 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 38.
  Idris pamoja na Mtanzania mwingine Ernest Napoleon, wataungana na mastaa wakubwa  duniani kama Eric Dame, mwigizaji Mmarekani, Gerard Depardieu wa Ufaransa, Thomas Kretschmann wa Ujerumani na wengine wengi kucheza filamu hiyo ya ujambazi wa kimataifa.
  Filamu hiyo itakayojulikana kwa jina la ‘The Blue Mauritius’, inahusu majambazi watano wa kimataifa ambao wanasafiri kwenda katika jiji la Cape Town nchini Afrika ya Kusini, kwa ajili ya kuiba vitu mbali mbali vyenye thamani kubwa duniani.
  Idris na mwenzake Ernest Napoleon, watasafiri kwenda katika jiji la Cape Town nchini Afrika kusini mapema mwakani kwa ajili ya filamu hii  kubwa kuwahi kuwahusisha Watanzania. Habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
  Umoja wa Wanawake wa Wanasiasa (WCP-Ulingo) umesema  wanawake wamekuwa wanadhalishwa utu wao katika mitandao ya kijamii Si michuzi Media na kutaka vyombo vya dola kuchukua hatua dhidi ya wanaofanya hivyo.
  Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Sekretarieti ya Umoja huo, Angelina Mtahiwa amesema kuna uovu unafanywa baadhi ya mitandao ya kijamii katika kuwachafua wanawake katika nafasi zao hali ambayo inarudisha nyuma wanawake kuogopa kujihusisha masuala mbalimbali kwa jamii.
  Amesema mitandao ya jamii itumike katika kujenga nchi kuelimisha  masuala ya kijamii ili nchi iweze kusonga mbele kiuchumi pamoja kuwatoa  wanawake katika kushiriki nafasi mbalimbali sio kutumika katika mitandao kwa ajili ya kudhalilishwa.
  Nae Mjumbe wa Sekretarieti hiyo, Swaum Rashidi amesema kwa sasa wanawake wamekuwa wakishiriki shughuli za kuchumi , siasa, biashara  na kuwa sehemu ya mchano katika kuchangia maendeleo ya taifa.
  Swaum amesema wanawake wakidharishwa katika mitandao ya kijamii inawafanya kuwa woga pamoja na kupata wakati mugumu katika familia zao.
  Aidha amesema kuwa watu wanaotengeneza taarifa mbaya za wanawake kupitia mitandao ya kijamii wachukuliwe hatua ili hali hiyo isiweze kujirudia.
  Aidha Swaum amesema kuwa hawawezi kumtaja mwanamke ambaye amesdhalilishwa na katika mitandao kwani kufanya hivyo ni kuendeleza udhalilishaji huo.
   Mjumbe wa Sekretarieti wanawake wanasiasa WCP-Ulingo, Angelina Mtahiwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya udhalilishaji wa wanawake baadhi ya mitando ya jamii si Michuzi Media, kulia ni  Mjumbe  Swaum Rashidi, kushoto  ni Mjumbe Diminatha Rwechungura .
  Mjumbe wa WCP- Ulingo, Swaum Rashidi akizungumzia juu mitandao ya jamii inavyotakiwa kutumika katika maendeleo na sio kuchafua watu kulia ni anawakilisha  Walemavu WCP –Ulingo Agness Mgaya , kushoto ni  Mjumbe wa Sekretarieti wanawake wanasiasa WCP-Ulingo, Angelina Mtahiwa.

  0 0


  0 0

   1.     Je! Unasumbuliwa  na  tatizo sugu na lisilopona la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume ?
  2.             Je, Unawahi  kumaliza  na  kushindwa  kurudia  tendo ?
  3.            Je, Maumbile  yako  yamesinyaa (YAMELEGEA ) kupita maelezo   na kunywea  ama  kuingia ndani na kuonekana  kama ya mtoto  kwa  sababu  ya  kujichua  kwa  muda  mrefu, kuugua  chango la kiume au ngiri ?
  4.             Umejaribu  kutafuta  tiba  ya  tatizo  lako bila  mafanikio, kiasi  cha  kukata  tamaa ya kupona ?
  5.             Unataka  kupata  tiba  sahihi na  ya  uhakika  ya  tatizo  lako ?

  Kama  jibu  lako  ni  NDIO  basi  hii ni  HABARI  NJEMA  SANA  KWAKO !  Tunapenda  kukutaarifu  kuwa  tunayo  dawa  ya  ASILI  kabisa  ambayo  INATIBU  na  KUPONYESHA  KABISA  tatizo  la  NGUVU  ZA  KIUME  ndani  ya  saa AROBAINI  NA  SABA. 
  Tiba  hii  huwasaidia  hata  wanaume    ambao  tatizo  lao  linasababishwa  na  maradhi  ya  kisukari. Tiba  hii  pamoja  na  mambo mengine, husaidia  kuimarisha, kunenepesha  na  kuipa  tena  nguvu misuli ya  uume  ulio  legea  kwa  sababu  ya  kujichua kwa  muda  mrefu, kuugua  chango la kiume, au  ngiri.
  Kama uume  wako  umelegea  na  kuingia  ndani  kwa  sababu  ya  kujichua  kwa  muda  mrefu, kuugua  ngiri, ama  chango la  kiume, tiba  hii  itakufaa  sana na  itakuonyesha  maajabu makubwa.Hukupa  uwezo  wa  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  muda  mrefu na  kurudia  tendo  la  ndoa  bila kuchoka.

  KUJARIBU   NI  BURE 
  Utaratibu  wa  kutumia  tiba    hii upo hivi: Muhitaji  ataanza  kwa  kupewa  BURE, dawa  ambayo  ataitumia  kwa  muda  wa  siku  saba, ili  aone  ufanisi  wake, halafu  baada  ya  hizo  siku  saba  ndio  atalipia dozi kamili ambayo  ataitumia  kwa  muda  wa  siku 40. 

  TUNAPATIKANA   JIJINI   DAR  ES  SALAAM. 
          KWA   MAELEZO  ZAIDI  
  WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA 0787 41 06 18. 

  N.B :  HII  NI  OFFER  MAALUMU  KWA  IDADI  MAALUMU  YA  WATU  NA  KWA  KIPINDI  MAALUMU. WAHI  OFFER  HII  MAPEMA  KABLA  MUDA  WAKE  HAUJAISHA.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mabinti wa Kimasai waliojitokeza wakati wa mapokezi kwenye lango la kuingia kwenye hifadhi ya Ngorongoro ambapo anategemewa kuzindua Makumbusho Mpya ya Olduvai kesho tarehe 3, Oktoba 2017. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya Hifadhi ya Ngorongoro kutoka kwa Msaidizi Mkuu wa Lango Bw. Mansuet Valentine mara baada ya kuwasili kwenye hifadhi ya Ngorongoro ,Makamu wa Rais anategemewa kuzindua Makumbusho Mpya ya Olduvai kesho tarehe 3, Oktoba 2017. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0


  SIMU.TV: Mamlaka za upimaji na kupanga maeneo nchini zimeshauriwa kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya viwanda na makazi kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira; https://youtu.be/ayvV8v94aKc

  SIMU.TV: Mkuu wa magereza nchini kamishina jenerali Dr Juma Malewa ametoa wito kwa askari wa jeshi hilo kutumia kikamilifu rasilimali walizonazo kukuza uchumi; https://youtu.be/s7uddn9hvoE

  SIMU.TV: Kituo cha huduma cha pamoja cha ushuru na forodha cha Rusumo wilayani Ngara kimeanza kufanya kazi kwa masaa 24 ili kupunguza msongamano wa wateja; https://youtu.be/91SBRM0QV9w

  SIMU.TV: Rais wa Zanzibar Dr Alli Shein amewaapisha viongozi wa taasisi mbalimbali visiwani humo ambao aliwateua hivi karibuni; https://youtu.be/SsMSynToREA
  Makamu wa Rais Samia Suluhu amewasili mkoani Arusha kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa makumbusho ya Olduvai Gorge hapo kesho wilayani Ngorongoro; https://youtu.be/qpgoKfLRQ1M

  SIMU.TV: Uongozi wa wilaya ya Kyela umetoa muda wa siku 7 kwa wamiliki wa vibanda vya biashara katika stendi ya Kasumulu kubomoa mabanda yao kupisha ujenzi wa kituo cha kisasa; https://youtu.be/L5d1NFmZDxw

  SIMU.TV: Hifadhi ya taifa ya Ruaha imevunja rekodi ya kutembelewa na watalii wa ndani zaidi ya 160 katika kipindi cha siku mbili; https://youtu.be/0ocNf5kCSOg  

  SIMU.TV: Uzalishaji wa mbaazi unatarajiwa kuongezeka nchini Tanzania kutokana na kupatikana kwa masoko mapya katika nchi za Afrika kusini, Uingereza na mashariki ya kati; https://youtu.be/bC0LSbTVd3c
  SIMU.TV: Mkuu wa chuo cha elimu ya biashara CBE Prof Emmanuel Mjema amevishauri viwanda nchini Tanzania kuzalisha bidhaa zenye ubora kuhimili ushindani; https://youtu.be/RbHsUN1uiv8

  SIMU.TV: Mfuko wa pensheni wa PSPF umeanza kushirikiana na benki mbalimbali nchini ili kuwawezesha wateja kuweza kupata mikopo kwa urahisi; https://youtu.be/pJToIgsiMZY
  SIMU.TV: Fahamu hapa taarifa mbalimbali kuhusiana na kupanda kwa kushuka kwa bei za hisa katika soko la hisa jijini Dar Es salaam maarufu kama DSE; https://youtu.be/p2IbCCjJJ10

  SIMU.TV: Mfuko wa pensheni wa PPF umetumia zaidi ya shilingi bilioni 1.4 kuwasomesha watoto wa wanachama wa mfuko huo waliofariki dunia; https://youtu.be/VWhHbL83y1o
  SIMU.TV: Wakulima wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kuacha mara moja tabia ya ukataji wa miti kwa shughuli za kibinadamu kinyume cha sheria; https://youtu.be/boOzp_K877o

  SIMU.TV: Wakazi wa eneo la Bombambili kata ya Kivule jijini Dar Es salaam wameiomba serikali kuwapelekea huduma za Umeme na barabara nzuri; https://youtu.be/eg_vM7S-vNc

  SIMU.TV: Ujenzi wa barabara ya mita 700 katika mtaa wa Olympio Upanga jijini Dar Es salaam kwa kiwango cha lami umekamilika; https://youtu.be/7x-yTanUPRo  

  SIMU.TV: Mastaa wa Tanzania wanaosakata soka la kulipwa nje ya nchi wameanza kuripoti nchini kujiunga na kambi ya timu ya taifa kuwasubiri Malawi; https://youtu.be/W6ECz52YMXg
  SIMU.TV: Kocha msaidizi wa Ngorongoro Heroes Oscar Mirambo amesema kambi ya timu hiyo imeanza leo kwa ajili ya kupata kikosi bora kutoka kwa vijana 50 walioitwa; https://youtu.be/_5quy0rt9UA

  SIMU.TV: Serikali imewaomba wadau wa michezo kuwekeza katika soka la vijana kwa kuwekeza kupitia mashuleni ambako kuna vipaji vingi zaidi; https://youtu.be/tj56UuDqDVE
  SIMU.TV: Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Alex Masama amewaomba wasanii kuungana na serikali katika harakati za kuwasaka wezi wa kazi za sanaa;  https://youtu.be/3juTI9438HU

  SIMU.TV: Shirikisho la soka barani Afrika CAF limethibitisha nchi za Morocco, Equtorial Guinnea na Ethiopia zimetuma maombi ya kuomba kuandaa michuano ya CHAN; https://youtu.be/vYfMQv9MShY

  SIMU.TV: Katibu mkuu wa wizara ya Maji Prof.Mkumbo ataka jamii zinazoishi pembezoni mwa vyanzo vya maji kupatiwa elimu ta utunzaji mazingira. https://youtu.be/xvwGLmfBoqY

  SIMU.TV: Naibu waziri Luhaga Mpina, akikalia kooni kiwanda cha sukari cha Mtibwa, kufuatia matumizi ya magogo katika uzalishaji licha ya kuzuiwa kufanya hivyo awali. https://youtu.be/91Uiom9zXLs

  SIMU.TV: Hospitali ya rufaa ya Bugando iliyoko mkoani Mwanza yaelezwa kukabiliwa na uhaba mkubwa wa wataalamu na vifaa vya matibabu ya moyo. https://youtu.be/vi3lShsfxds

  SIMU.TV: Vyama vya ushirika nchini, vimeaswa kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili viweze kuleta tija katika ujenzi wa taifa. https://youtu.be/wboV_lNYt2A

  0 0


  0 0

  Na.Vero Ignatus ,Mlandizi

  Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumtha mshana amewaasa wanawake kutokudharau kazi hata kama ni ndogo kwani kwenye hiyo ndogo ndipo nyingine kubwa itafuata.

  Ameyasema hayo Katika Kanisa la RGC lililopo Mlandizi ambapo alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la wanawake lililoambatana na Changizo kwa ajili ya kununua eneo la kiwanja cha kujenga kanisa

  Mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni mchungaji alipata nafasi ya kuhubiri katika kongamano hilo, ambapo amewataka wanawake kujiamini na kuaajibika kwani hata neno la Mungu linasema asiyefanya kazi na asili.

  "Nyumba ambayo mwanamke ni legelege nyumba hiyo haitaendelea kamwe,wanawake changamkeni wajibikeni nyie ndiyo nguzo ya familia hutamchosha mume wako" alisema

  Kwa upande wake Mchungaji Kiongozi Kambi ya Waebrania Mlandizi Mercy Adam Mwakimomyile amesema kuwa Kongamano hilo limebeba kaulibiu isemayo Nguvu ndani ya Mwanamke(Power in Woman)ambapo imewafanya wanawake wajisikie wanaweza

  "Kutokana na uwezo uliopo ndani ya mwanamke basi leo tumeamua kuwa tunaweza kumjengea Mungu madhabahu kupitia kongamano hili" alisema

  Amesema katika kanisa hilo wato watoto zaidi ya elfu moja ambao wanafundishwa maadili kupitia neno la Mungu kuibua vipawa  mbalimbali vilivyopo ndani yao na kuviibua
  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumta Mshama .Picha na Vero Ignatus Blog.
  Mkuu wa wilaya akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kanisa la GRC kambi ya Waebrania Mlandizi àliyepo kulia kwake ni mchungaji kiongozi wa kanisa hilo la Mlandizi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Assumtha Mshama akiwa anaonyeshwa mipaka ya eneo la kiwanja cha Kanisa la GRC Kambi ya Warbrania Mlandizi aliyepo nae ni Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo  Mercy Adam Mwakimomyile.Picha na Vero Igbatus Blog.
  Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe.Assumta Mshama akiwa anaongoza maombi mara baada kuona eneo ambalo linatarajiwa kujengwa kanisa .Picha na Vero Ignatus Blog.Kuna Mama Mtume Deo Rwetaka 


  0 0
  0 0
  0 0


older | 1 | .... | 1940 | 1941 | (Page 1942) | 1943 | 1944 | .... | 3272 | newer