Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

TID AFUNIKA TAMASHA LA EFM MZIKI MNENE KIMARA

$
0
0

 Mwanamuziki mkongwe wa bongo fleva Khalid Mohammed 'TID Mnyama' Akiwa amebebwa juu na Mashabiki waliofia Kilimani bara wakati wa Tamasha la Mziki Mnene linaloendeshwa na Rdio ya EFM kupitia programu ya nje ndani.

 Mwanamuziki mkongwe wa bongo fleva Khalid Mohammed 'TID Mnyama' akiimba na Mashabiki wakati wa Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
 RdJ Mamy akifanya vitu vyake katika Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
 RDJ Majey Majizo akicheza na Tantable wakati wa Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
 Msanii wa Muziki wa Singeli Manfongo akiimba wakati wa  Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
 Msanii wa Bongo Fleva Shetah akiimba na Mashabiki wakati wa Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
 RDJ SPUR akionyesha ufundi wa kuchez ana mashine wakati wa Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
 Mkali wa Muziki wa Singeli nchini , Virus Mdudu akifanya mashambulizi katika jukwa la Mziki Mnene  lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam
 Mtangazaji wa Kipindi cha Genge , Pido akifanya yake kwenye Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam

Mashabiki walifika katika Tamasha la Mziki Mnene  lililofanyika Kilimani Bar Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam

NDOA YA MENEJA WA GLOBAL PUBLISHERS, ABDALLAH MRISHO ILIVYOFANA JIJINI DAR

$
0
0
Meneja Abdallah Mrisho na mkewe, Catherine Mdamu wakiwa katika pozi la furaha, muda mfupi baada ya kufungwa kwa ndoa yao.Bibi Harusi, Catherine (katikati) akiwa na wanafamilia (wenye nguo nyeupe) na wafanyakazi wenzake, Women With Voices (WWV) wenye nguo za bluu.Daaab! Maharusi na wanafamilia wakiwa katika pozi maarufu kwa jina la dab!

Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, jana (Jumamosi, Sept. 30,2017) alifunga ndoa ya kifahari na Catherine Mdamu, iliyolifanya Jiji la Dar es Salaam lisimame kwa muda, ikifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City.Katika sherehe hiyo, wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers wakiongozwa na mkurugenzi wao, Eric Shigongo, jamaa na marafiki, walijumuika kula, kunywa mpaka kusaza na kucheza muziki mzuri, mpaka usiku sana huku kukiwa na 'special appearance' ya Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Harusi ya Abdallah na Catherine, Mlimani City - Part 1

Harusi ya Meneja Abdallah na Catherine, Mlimani City - Part 2

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Kitaifa Kufanyika Tarime

$
0
0


 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Watoto toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Margaret Mussai akielezea jambo wakati wa kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba Tarime,  Mkoani Mara. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali, Save the Children Tanzania Bi. Jasminka Milovanic
MK1aMK2
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali, Save the Children Tanzania Bi. Jasminka Milovanic akifafanua jambo wakati wa kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba Tarime,  Mkoani Mara. Kukulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Watoto toka WizaraMaendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Margaret Mussai.
MK3
Afisa Habari wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bw. Anthony Ishengoma akisisitiza jambo wakati wa kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba Tarime,  Mkoani Mara.
MK4.
Mwakilishi kutoka asasi ya kiraia ya CAMFED Bi. Theresia Moyo akielezea jambo mbele ya Wahariri wa Habari (hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba Tarime,  Mkoani Mara. Kutoka kulia ni Mwezeshaji wa Kitaifa toka Taasisi ya Tanzania Girl Guides Bi. Emiliana Stanslaus na Mwakilishi wa Room to Read Bi. Rachel Mbushi.
MK5
Mtaalam wa Haki za Watoto toka Shirika lisilo la Kiserikali, Save the Children Tanzania Bi. Neema Bwaira akisisitiza jambo wakati wa kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba Tarime,  Mkoani Mara. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Familia toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Rose Minja.
MK6
Mhariri wa Habari kutoka kituo cha televisheni cha Channel Ten Bibi. Esther Zelamula akichangia mada wakati wa wa kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika tarehe 11 Oktoba Tarime,  Mkoani Mara.

VIONGOZI WA DINI WAWAPINGE WANAOTAKA KUVURUGA AMANI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba Viongozi wa Jumuiya na Taasisi zote za kidini nchini wahakikishe wanawapiga vita watu wote wanaopanga na kutaka kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini kwa sababu watakwamisha maenendeleo. 

Amesema Serikali inaelewa kwamba dini ni miongoni mwa vyanzo muhimu vya maendeleo ya ustaarabu wa mwanadamu kwani inatoa elimu ya maadili mema yenye kuwafanya waumini waepukane na maovu mbalimbali.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Oktoka 01, 2017) wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa 48 wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya uliofanyika katika eneo la Kitonga kata ya Msongola wilayani Ilala, Dar es Salaam. Amesema kila Mtanzania anatakiwa ahakikishe anadhibiti matukio yote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani kwa kutoa taarifa katika mamlaka husika.”Tanzania ni nchi salama na yenye utulivu, hivyo ni lazima wote tushirikiane kuitunza.”

“Napenda niwahakikishieni kuwa Serikali inaunga mkono juhudi za Jumuiya  za kidini katika kupiga vita maovu ya kila aina; mathalan utumiaji wa dawa za kulevya, wizi, rushwa, uzinzi ambao husababisha madhara mengi ukiwemo ugonjwa wa UKIMWI.” Amesema iwapo dini zetu zitatumika vizuri tutaweza kwa haraka sana kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli la ‘Hapa kazi tu’ kwani kila mtu ataepuka uzembe na kuwajibika ipasavyo.

Waziri Mkuu amesema ana imani kwamba jumuiya hiyo kama zilivyo taasisi zingine za kidini itaendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii yetu kwa kuwapatia waumini wao na wananchi kwa ujumla elimu na maarifa ya kuboresha tabia zao na maadili yao kiroho.Amesema amani na utulivu uliopo nchini unatokana na mambo mengi ikiwemo na wananchi kupata ustawi, kuweza kufanya shughuli zao vizuri na kuwa na imani na Serikali yao, ambayo imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wananchi hususan wanyonge wanapata faraja ndani ya nchi yao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na kiongozi na mbashiri mkuu  wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania,Tahir Mahmood, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa jumuiya hiyo Mbande, Temeke, Jijini Dar  es salaam Oktoba 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waumini wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo huko Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waumini wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo huko Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kitabu kutoka kwa Katibu wa Malezi Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania, Mahmood Hamsin, baada ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa jumuiya hiyo Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017. (kulia) ni. kiongozi na mbashiri mkuu wa  Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania,Tahir Mahmood. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

VIJANA WASHAURIWA KUWATUNZA WAZEE

$
0
0

Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Vijana nchini wameshauriwa kujitolea na kuwatunza wazee katika maeneo yao ili kupata ushauri na busara za wazee hao kwa maendeleo yao na taifa.

Hayo yamesemwa Mjini Dodoma na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi alipokuwa akizungumza na wazee katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yanayofanyika kila Oktoba Mosi ya kila mwaka. Mhe. Mwinyi amesema kuwa jukumu la kuwatunza na kuwalea wazee sio la Serikali pekee bali jamii pia ina nafasi yake katika kuwatunza wazee hasa Vijana.

Mhe. Mwinyi ameongeza kuwa Serikali imejitaidi sana kuweka mazingira mazuri kwa wazee kwa kuwapatia huduma za Afya na kuwatunza wazee wote ambao hawana ndugu wa kuwatunza katika makambi mbalimbali ya wazee nchini. “Niwaombe vijana mtutunze sisi wazee kwani na sisi tulikuwa vijana kama ninyi na mkiweka utamaduni huu utawasaidia na ninyi mkiwa wazee hapo baadae” alisema Mhe. Mwinyi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akitoa zawadi kwa mmoja wa wazee wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017. 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiangalia moja ya bidhaa zinazozalishwa na wazee katika moja ya banda la Maonesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW .



Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwapungia mkono wazee wakati wakiingia kwa maandamano kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akitoa salamu za Mkoa kwa Mgeni Rasmi wa Siku ya Wazee Duniani Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003 kwa Mgeni wa Siku ya Wazee Duniani Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017. 

DC HAPI ATEMBELEA KITUO CHA MABASI MAKUMBUSHO

DK.KIKWETE -HALI YA MIUNDOMBINU KIBAHA SEKONDARI HAIRIDHISHI TUSHIRIKIANE KUITATUA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha 

Rais mstaafu wa awamu ya nne ,dk.Jakaya Kikwete ,ametoa rai kwa wadau na viongozi ambao wametokea katika chimbuko la shule ya sekondari ya Kibaha;” ,Kuangalia namna ya kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa ambayo inasababisha mlundikano wa wanafunzi madarasani.

Aidha amesema mbegu ya kuwa yeye mwanasiasa ilipandwa shuleni hapo, baada ya kuchaguliwa kiongozi wa baraza la shule kutokana na harakati zake za kutetea haki za wanafunzi .

Dk.Kikwete aliyasema hayo shirika la elimu Kibaha ,wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha ambako alipata elimu yake ya sekondari mwaka 1966 hadi 1969. Alisema ,atashirikiana na wadau mbalimbali kuona namna bora ya kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa madarasa .

Dk.Kikwete alisema , haipendezi na hajafurahishwa na hali ya miundombinu ilivyokuwa chakavu hali inayoathiri mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji . Rais huyo mstaafu wa awamu ya nne ,alieleza changamoto hizo si sababu ya kushindwa bali uwepo wa changamoto huongeza umakini ,bidii na ubunifu ili kukabiliana nazo .
Rais mstaafu wa awamu ya nne dk.Jakaya Kikwete ,akitoka kutembelea bweni alikuwa analala wakati akisoma shule ya sekondari Kibaha mwaka 1966-1969, wakati wa mahafali ya 50 ya kidato cha nne shuleni hapo,huku akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa pili kushoto,na viongozi wa shule ya sekondari Kibaha na shirika la elimu Kibaha.(picha na Mwamvua Mwinyi)

Baadhi ya wahitimu wakiimba wimbo maalum katika mahafali hayo. 
Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha aliyochorwa na mmoja wa wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha, Mkoani Pwani, wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo .

Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha, wakati wa mahafali ya 50 ya kidato cha nne shuleni hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi) .

TPB YAFUNGUA TAWI JIPYA MTO WA MBU – ARUSHA

$
0
0

Benki ya TPB imeendelea kusogeza huduma zao karibu zaidi na wateja kwa kufungua tawi jipya Mto wa Mbu, Wilayani Monduli, Mkoani Arusha.

Lengo la kufungua tawi hilo ni kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi na wao kupata fursa ya kutoa huduma kwenye mazingira bora na ya kisasa zaidi, ili wakazi wa mkoa huo waendelea kufaidika na huduma bora zenye gharama nafuu.

Akizungumza wakati wa kuzindua tawi hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya alisema tawi hilo jipya litaongeza idadi ya wateja kwenye benki yao.Alisema pia wananchi wa Arusha, watafaidika na mikopo mbalimbali inayotolewa na TPB inayokidhi mahitaji ya vikundi, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, mikopo ya wafanyakazi na hata wastaafu.

‘Ni matumaini yangu kuwa tawi hili litaongeza idadi ya wateja watakaofika kupata huduma mbalimbali tunazozitoa, kwani TPB tunatoa huduma bora na zenye kukidhi matakwa ya kila mwananchi katika jamii ikiwemo mikopo kwa vikundi visivyo rasmi,’ alisema Profesa Rutashobya.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la benki ya TPB Mto wa Mbu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB Profesa Lettice Rutashobya. Uzinduzi wa tawi hilo la Mto wa Mbu ulifanyika jana huko Mto wa Mbu, Arusha.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja, Ester Mfuru, wa tawi la Benki ya TPB huko Mto wa Mbu, wakati wa uzinduzi wa tawi hili. Kutoka kushoto ni Meneja wa tawi hilo Selestine Mteta na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta. Kulia ni Afisa Mtendaji wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya TPB Prof. Lettice Rutashobya.
Mwenyekiti wa Bodi ya TPB Bank Profesa Lettice Rutashobya, akikabidhi zawadi ya ngao kwa Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango, kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la benki hiyo lililopo Mto wa Mbu Arusha. Akitazama ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi.
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya TPB Mhe. Dkt. Philip Mpango (c) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa benki hiyo. Kutoka kulia waliokaa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshigi na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Profesa Lettice Rutashaobya. Kushoto ni Meneja wa tawi hilo Selestine Mteta na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta. Waliosimama nyuma ni baadhi ya viongozi waandamizi wa benki hiyo. 


Rais Magufuli kutohudhuria Kongamano la Kumbukizi ya Mwl Nyerere

Meya wa jiji la Dar azishauri Taasisi za kibenki kuwapatia walemavu wasioona mikopo

$
0
0
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akipata maelekezo ya bidhaa zinazo tengenezwa na kikundi cha wanawake wenye ulemevu wa kusikia (Viziwi) wakati wa kufunga wiki ya maadhimisho ya wiki ya wanawake wenye ulemavu yaliyofanyika jana jijini hapa.wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa FUWAVITA Aneth Jerana.

NA CHRISTINA MWAGALA.

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amezishauri Taasisi za kibenki kuwasaidia watu wenye ulemavu wasioona ili waweze kuondokana na changamoto mbalimbali ili waweze kujitegemea wenyewe.

Meya Mwita ametoa kauli hiyo jijini hapa jana wakati akifunga maadhimisho ya wiki ya wanawake wenye ulemavu wakusikia (Viziwi) (FUWAVITA) yaliyofanyika katika viwanja vya Biafra jijini hapa.

Meya Mwita alisema kuwa walemavu wananafasi kubwa ndani ya jamii kutokana na ushiriki wao katika shughuli za kimaendeleo na kwamba wanapaswa kupewa fursa zamikopo na Taasisi za kibenki ili waweze kujiondoa kwenye changamoto za kimaisha.

"Ulemavu sio ugonjwa, kuwa mlemavu haimaanishi kwamba ndio wasisaidiwe, makundi kama haya ambayo yameonyesha nia ya kujitafutia weyewe , wanapaswa kuungwa mkono na kila mmoja " alisema Meya Mwita.

" Makundi haya yamesahaulika katika jamii yetu, ni muda wetu huu kuwakumbuka, vyombo vya habari pia vitumike kutangaza bidhaa ambazo zinazalishwa na makundi haya, wananchi nao wajitokeze kuunga mkono jitihada zao" aliongeza .

Awali akijibu risala iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa FUWAVITA  Anethi Jerana ,Meya Mwita alisema kuwa jiji litawapatia mkopo wa shilingili milioni tatu kama walivyoomba na kuwakaribisha kuomba tena iwapo watahitaji.

Katika hatua nyingine Meya Mwita aliipongeza Benki ya NMB kwakudhamini maonyesho hayo sambamba na kutoa huduma ya kuwafungulia akaunti za kifedha na kutumia nafasi hiyo kuzishauri Benki nyingine kuiga mfano huo.

Mapema mwenyekiti wa FUWAVITA akisoma risala mbele ya Mstahiki Meya Mwita aliomba Halmashauri ya Jiji iwasaidie mkopo wa shilingi milioni tatu , ili waweze kuendeleza shuguli zao za kuzalisha bidhaa mbalimbali kwenye kikundi chao.

Mbali na mkopo huo, pia waliiomba Halmashauri ya Jiji kuwapatia vyumba vilivyopo kwenye viwanda vidogo  Mwananyamala ambavyo vilizinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 2,2017

MSAMA AUCTION MART YAPONGEZA KAULI YA WAZIRI DKT. MWAKYEMBE KUTOKOMEZA KAZI FEKI ZA SANAA.

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Kampuni ya Msama Auction Mart imempongeza Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kwa kauli yake kuhusu wizi wa kazi za sanaa nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Alex Msama amesema kuwa Kampuni yao imeona kuwa Waziri huyo ameonesha nia yakupoteza kabisa kazi feki za Sanaa.

Hatua hiyo ya Waziri pia itawagusa wenye kazi zao ambao ni Wasanii wa kazi hizo ikiwemo Wasanii wa Bongo Fleva, Nyimbo za Injili, Maigizo na Filamu.

Msama amesema kuwa doria za kumaliza wizi huo wa kazi za Wasanii inaendelea kwa nchi nzima, ambapo Mkoa mmoja tu ndiyo wenye ahueni yakupunguza wizi huo ambao ni Mwanza.

"Msama Auction Mart kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo inategemea kuanza zoezi lakumaliza kazi feki za sanaa nchini, zoezi ambalo lisilokuwa na mwisho", amesema Msama.

Pia Msama ameonya wale wote wanaofanya biashara za kuuza kazi feki, ambapo amesema kuwa watakapokamata Kompyuta za kufanyia kazi hizo basi hazitarudi tena kwa wahusika.

Wafanyabiashara wa Filamu za Nje nao wametakiwa kuacha kufanya biashara hizo bila kibali cha mwenye kazi husika, kwani hatua hiyo inaikosesha Serikali mapato.

Introducing new single "Mototo wa Udongo" by Kisamaki Ft Fatuma Mcharuko

SYLVESTER LUBALA ATIMIZA MIAKA 71 YA NDOA NA MKEWE CECILIA LUBALA

$
0
0
 Katibu wa Chama cha Mashujaa wliopigana Vita kuu ya pili ya Dunia ambaye ni Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mzee Sylvester Lubala  na Mkewe Cecilia Lubala wakipunga mkono kwa wageni waalikwa wakati wa hafla yao ya kutimiza Miaka 71 ya ndoa iliyofanyika katika hoteli ya Srena Jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na watu maharufu na Viongozi wa kitaifa


 Naibu Waziri wa Afya nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula akimuweka Sawa mama yake wakati wa hafla ya kutimiza miaka 71 ya ndo yao mara baada ya vita kuu ya pili ya Dunia
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Lukuvi akiwa na Mkewe wakitoa pongezi kwa Mzee Sylvester Lubala mara baad ya kutimiza miaka 71 ya ndoa
  Katibu wa Chama cha Mashujaa wliopigana Vita kuu ya pili ya Dunia ambaye ni Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mzee Sylvester Lubala  na Mkewe Cecilia Lubala wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wao 18 wakati wa hafla ya miaka 71 ya ndoa

KUTAZAMA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

BAADA YA KUTUMBUA BODI YA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI MBOMIPA, WAZIRI MAGHEMBE APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA AGIZO ALILOTOA LA KUUNDWA UPYA KWA KATIBA YA JUMUIYA HIYO

$
0
0

Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akizungumza juzi mkoani Iringa mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa mapema mwezi agosti mwaka huu la kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA na kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo.  Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza.

Na Hamza Temba - WMU

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amepokea taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa la kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA na kuagiza rasimu hiyo ifanyiwe marekebisho ya mwisho kabla ya kuwasilishwa kwa wananchi kwa ajili ya mijadala na hatua zaidi za kukamilisha rasimu hiyo.


Alipokea taarifa hiyo juzi (Ijumaa, Septemba 29, 2017) katika kikao alichokiitisha kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, mjini Iringa. Aliagiza kuundwa upya katiba hiyo alipofanya ziara ya kikazi kwenye eneo la Jumuiya hiyo katika kijiji cha Tungamalenga wilayani Iringa mapema mwezi Agosti mwaka huu.


Kufuatia ziara hiyo pamoja na taarifa ya tume aliyoiunda kuchunguza suala hilo alibaini mapungufu mbalimbali ya kikatiba na kuamua kutoa agizo la kuundwa upya kwa katiba hiyo  na kuvunja kabisa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo. Miongoni mwa mapungufu hayo ni katiba iliyokuwepo awali kukinzana na Sheria mama pamoja na kanuni zake.

Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza juzi mkoani Iringa mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa agizo alilotoa mapema mwezi agosti mwaka huu la kuundwa upya kwa katiba ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA na kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya jumuiya hiyo. 

Katiba kutoeleza namna ya upatikanaji wa viongozi na namna ya kuwawajibisha, kutoeleza majukumu ya bodi ya wadhamini kwa usahihi na namna ya upatikanaji wa bodi hiyo pamoja na kutoleza wajibu wa wawekezaji katika jumuiya kwa jumuiya yenyewe na kwa Serikali kwa ujumla wake.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WADAU SEKTA YA ARDHI WAJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA MIFUMO

$
0
0
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendesha warsha ya kuwajengea uwezo wadau wa masuala ya sekta ya ardhi nchini kuhusu mifumo mbalilmbali inavyotumika katika kutoa huduma kwa wananchi.

Akifungua warsha hiyo Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt. Moses Kusiluka alisema, hadi sasa wizara inatumia mfumo zaidi ya mmoja kutoa huduma za kila siku kwa mwananchi. Uwepo wa mifumo hiyo katika utoaji huduma za sekta ya ardhi ni muhimu kwa ajili ya kurahisisha huduma. Ili kufikia malengo, ni lazima kuwepo na mfumo mmoja utakaounganisha mifumo yote hiyo kwa lengo la kuongeza ufanishi na kuboresha huduma.

Uundaji wa mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (Intergrated Land Management Information System, ILMIS) unatekelezwa na Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishiriana na wataalamu kutoka kampuni ya IGN FI kwa udhamini wa Benki ya Dunia. Uundaji huu ulishaanza na kwa sasa mfumo uko katika hatua ya majaribio.

Dhumuni kuu la uundaji mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi ni kuimarisha usalama katika umiliki wa ardhi kwa kuboresha usahihi katika taarifa za ununuzi ardhi, usajili, upimaji na pia katika kusimamia ardhi kwa ujumla wake. Utekelezaji wa Mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (ILMIS), utahusisha mambo mbalimbali kama vile njia rahisi na rafiki ya kusimamia uundaji na uendelezaji wa mfumo wenyewe, majaribio ya mfumo katika utekelezaji, ubadilishaji wa taarifa za ardhi zilizopo mfano taarifa za upimaji na ramani, hatimilki na kuziweka katika mfumo.

Naye Msajili Msaidizi wa Hati, Appolo Laizer alisisitizia umuhimu wa utumiaji mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (ILMIS) kwa wadau wa sekta ya ardhi alipokuwa akielezea jinsi hatimilki zitakavyotolewa na mfumo huo. Alisema, utoaji wa hati kupitia mfumo utaongeza usalama katika nyaraka za umiliki, huduma sahihi, salama na kwa unafuu zaidi. Mfumo utapunguza muda wa kuhakiki taarifa katika uhamisho wa milki kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, kuongeza ulinzi kwenye maeneo yaliyotengwa kama hifadhi ya barabara, misitu au maeneo ya wazi.

Utoaji wa hatimilki kwa kutumia mfumo utasaidia sana kupunguza kama sio kumaliza kabisa migogoro ya ardhi kwa kulinda umiliki wa mwananchi. Pia mfumo utaondoa migogoro ya umilikishaji wa hati kwa mtu zaidi ya mmoja pamoja na kuongeza ulinzi wa hatimilki katika taasisi za kifedha.
Wadau wa masuala ya sekta ya aAdhi wakiwa katika picha ya pamoja.
Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Wizara ya Ardhi akitoa ufanunuzi juu ya ujenzi wa Mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya Ardhi (ILMIS).
Wadau wa Sekta ya Ardhi wakisiliza taarifa kuhusu mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya Ardhi nchini kutoka kwa mtaalamu (hayuko pichani).

TUMIENI MAFUNDI UMEME WENYE LESENI KWA USALAMA WENU - EWURA

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ni Taasisi ya Udhibiti wa huduma za sekta mtambuka iliyoundwa kwa Sheria EWURA, Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania.

Shughuli kuu za Mamlaka ni pamoja na kudhibiti sekta za Nishati na Maji Tanzania Bara. EWURA ina wajibu wa kuzidhibiti sekta hizi kiufundi na kiuchumi. Sekta ndogo zinazothibitiwa na Mamlaka ni Petroli, Gesi Asilia, Umeme na Maji na Usafi wa Mazingira.

Moja ya majukumu makuu ya EWURA ni kutoa, kudurusu na kufuta eseni za huduma mbalimbali inazozidhibiti ikiwemo leseni za Makandari wa Umeme na wote wanaojihusisha na shughuli za utandazi na ufungaji umeme kwa ngazi/ madaraja mbalimbali.
Mfano wa leseni ya kufunga umeme iliyotolewa na EWURA

Kwa mujibu wa kifungu cha 8(1) cha Sheria ya Umeme ya mwaka 2008, kazi za ufungaji umeme ni shughuli inayohitaji leseni ya EWURA. Kwa mantiki hiyo, ni kosa la jinai kuendesha shughuli za ufungaji umeme bila kuwa na leseni halali iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

PSPF INAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

NUCLEAR IMPROVES RICE QUALITY IN ZANZIBAR

$
0
0
Although economic development in Zanzibar is often associated with tourism, agriculture contributes greatly to the Islands' economy and food security. In fact agriculture is the primary sources of income for roughly 70 percent of the islands’ population.

According to KhatibJumaKhatib, the Rice Research Programme Coordinator at Zanzibar's Agricultural Research Institute (ZARI), rice is the preferred crop in Zanzibar.He also confirmed that the demand is there and that the region has the potential to grow more.

In recent years the demand for the grain was so high that Zanzibar started to import nearly 80% of the rice it needed. Yet the farmers in the region exclaimed that they could close that gap if they had adequate agricultural extension services to guide them on the use of fertilizers and other modern technology.

Zanzibar's Ministry of Agriculture and Natural Resources implemented aspecial strategy with a view of increasing rice production by developing irrigation systems, training farmers and introducing improved varieties of rice.

By employing a mutation induction process, scientists are able to create a new variety of rice which is more resistant to diseases, water shortages or high level of salinity in the soil.Mutation is a natural process, but if left up to nature can take millions of years to occur. With the use of specialized equipment which emits a safe level of irradiation the process is sped up considerably.   

With the support of the IAEA and Food and Agriculture Organization (FAO), Zanzibar has put this technique to good use and a new variety of rice known as "SUPA BC" has been introduced to the region. According to KhatibJuma, the new variety of rice is very popular because it has several advantages over other rice varieties and brings higher yields.

In order to cultivate more and stronger varieties of rice, a special biotechnology laboratory has been set upin Zanzibar. The nuclear technology application is assisting local farmers to create modified seeds which are even moreresilient to diseases.

By increasing the local production of rice through the introduction of improved and new varieties, Zanzibar can reduce its dependence on imports, save money and create more jobs.

KATIBU MKUU DKT. MERU ASTAAFU RASMI UTUMISHI WA UMMA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Dar.

KATIBU Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji anayeshughulikia maendeleo ya viwanda Dkt. Adelhelm Meru, amestaafu rasmi utumishi wa umma baada ya kutimiza umri wa miaka 60.

Dkt. Meru ambaye ni mtaalamu aliyebobea katika masuala ya viwanda na uwekezaji, aliteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais Dkt. John Magufuli, Disemba 2015 na amehudumu katika nafasi hiyo hadi alipostaafu Jumatano wiki iliyopita.

Akizungumza katika hafla ya kumuaga Dkt. Meru, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage licha ya kumpongeza kwa kumaliza salama utumishi wa umma, alimsifu kwa umahiri wake wa kutekeleza sera ya maendeleo ya viwanda.

“Sote tunafahamu Serikali ya Awamu ya Tano inaamini katika viwanda, wewe ulikuwa mstari wa mbele katika kubuni mbinu na mikakati ya kuharakisha ujenzi wa viwanda nchini,” alisema Bw. Mwijage.
Alisema Dkt. Meru alitumia uzoefu wake wa kufanya kazi Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA), kuvutia kampuni mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kujenga viwanda vya uzalishaji wa bidhaa.

Kwa upande wake, Dkt. Meru aliishukuru wizara kwa ushirikiano aliopewa na kuwaomba wafanyakazi wenzake kumpa ushirikiano wa juu Rais Dkt. Magufuli katika dhamira ya kuijenga Tanzania mpya yenye uchumi wa viwanda.

“Tumuunge mkono Rais Magufuli hasa katika ukamilishaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ambayo ina matokeo makubwa kwa uchumi wa taifa hususan mradi wa Eneo Maalum la Viwanda la Bagamoyo (SEZ) na miradi ya Mchuchuma na Liganga.

Alichukua nafasi hiyo pia kumshukuru Rais Magufuli kwa kumwamini katika nafasi hiyo muhimu na kuushirikiano mkubwa alioupata wakati akiwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda.“Kwa kipindi chote tulichikuwa pamoja kuna mengi tuliyakamilisha na pale tulipokosana naamini tulikosana kwa ajili ya kazi, hivyo naamini tumesameheana kwa sababu mimi si malaika na hakuna mkamilifu zaidi ya Mungu aliyetuumba,” alisema Dkt. Meru.

Kabla ya kuwa Katibu Mkuu Viwanda, Dkt. Meru aliwahi kufanya kazi katika viwanda vya NECO na Kilimanjaro Machine Tools vilivyokuwa chini ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC); aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Vilevile alikuwa mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa kwanza Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) pia aliteuliwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Dkt. Meru amewahi pia kuwa Mshauri Viwanda katika Kampuni ya Car & General (Kenya) Ltd, iliyoko Nairobi nchini Kenya.


Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji anayeshughulikia maendeleo ya viwanda Dkt. Adelhelm Meru.
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images