Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

MHE KINGU AWAOMBEA MAJI WAKAZI WA JIMBONI KWA LISSU

0
0
Na Mathias Canal, Singida

Pamoja na Changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi katika Jimbo la Singida Mashariki Wilayani Ikungi Mkoani Singida lakini uhaba wa upatikanaji wa huduma ya maji ni kikwaz kikubwa kwa wananchi kwani wanatumia umbali na muda mrefu kutafuta maji.

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu ametoa ombi hilo mbele ya Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe wakati akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Ikungi kwenye kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.

Mhe Kingu alisema kuwa Jimbo lake lina changamoto ya maji ambayo kwa kiasi kikubwa serikali inaendeleza juhudi za kuzitatua, huku akisema kuwa katika Jimbo jirani la Singida Mashariki linaloongozwa na Mhe Tundu Lissu hali ni mbaya zaidi katika upatikanaji wa miundombinu ya maji kwa wananchi wake. 

Alisema kuwa hivi karibuni alipita katika jimbo hilo na kujionea adha inayowakumba wananchi jambo amablo lilimfanya kujipanga kuwaombea maji wananchi hao katika kipindi cha Bunge lijalo. Alisema kuwa wananchi hao wamebaki wakiwa utadhani hawana muwakilishi wa Jimbo kwa kipindi cha miaka 10 jambo ambalo linafanya kuteseka na huduma za utafutaji maji kwa kutumia muda mwingi na umbali mrefu. Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Ikungi mara baada ya kupita Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akielekea Manispaa ya Singida kwa ajili ya mapumziko, Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu (Kushoto) akimfatilia kwa makini Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe wakati wa kikao cha pamoja na watumishi wa Wilaya ya Ikungi, Mwingine ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Ndg Elieza.


BENKI YA CRDB YACHANGIA MILIONI MBILI UKARABATI WA SHULE YA MSINGI GEZAULOLE, JIJINI DAR

0
0
 Katibu wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi wa Maswala ya Kampuni, John Rugambo akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni mbili (2,000,000) kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Mshingi Gezaulole, Bundala Maganga ikiwa ni mchango wa benki hiyo kusaidia ukarabati wa madarasa ya shule hiyo, leo Septemba 27, 2017. Wengine pichani ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mariam Kinande (kulia) na kushoto ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Kamati ya Shule ya Mshingi Gezaulole,Martin Madama.
Katibu wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi wa Maswala ya Kampuni, John Rugambo akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni mbili (2,000,000) kwa Wanafunzi, Kelvin James na Swaum Mohamed wa darasa la sita Shule ya Msingi Gezaulole, Kigamboni jijini Dar es salaam ikiwa ni mchango wa benki hiyo kusaidia ukarabati wa madarasa ya shule hiyo, leo Septemba 27, 2017.
 Katibu wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi wa Maswala ya Kampuni, John Rugambo akizungumza kabla ya kabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni mbili (2,000,000) kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa madarasa ya shule hiyo, leo Septemba 27, 2017. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mariam Kinande na kushoto ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Kamati ya Shule ya Mshingi Gezaulole,Martin Madama.
Katibu wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi wa Maswala ya Kampuni, John Rugambo akizungumza na baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Gezaulole, iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam.

Katibu wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi wa Maswala ya Kampuni, John Rugambo  akiwa katika picha ya pamoja na Walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Gezaulole, iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam.

WATANZANIA WAMETAKIWA KUENZI UTAMADUNI WETU KUKUZA FURSA ZA UTALII WA KIUTAMADUNI

0
0
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mbulu

Watanzania wametakiwa kuenzi mila na desturi ambazo ni chanya wazitunze na kuzitumia ili kujenga jamii yenye maadili mema nchini kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alipotembelea Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom wilaya Mbulu mkoani Manyara ambapo amejionea utajiri wa kiutamaduni wenye fursa za utalii wa kiutamaduni.

“Nimetembelea nyumba za asili zilizopo hapa katika kituo hiki nimefurahishwa sana na utajiri wa kiutamaduni uliopo hapa, wazee walizingatia maadili katika kuwalea watoto wao kulingana na mila na desturi zao, ni vema tuenzi utamaduni wetu, huo ni msingi wa maadili mema ya jamii” alisema Naibu Waziri Wambura

Akitolea mfano wa maadili mema yanayopaswa kurithishwa aliyojionea katika kituo cha 4CCP na namna ambavyo watoto waliheshimu nyumba za wazazi wao, Naibu Waziri Wambura amesema kuwa kwa mujibu wa mila na desturi za Kitanzani suala la ulevi na utumiaji wa tumbaku kwa vijana ilikuwa ni mwiko hadi kijana afikie umri wa utu uzima ambapo anaweza kuwa na maamuzi sahihi katika maisha yake yenye kuwa na tija kwa familia.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (wa pili kushoto) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Ulinzi na Usalama mara baada ya kuwasili Wilayani Mbulu kwa ziara ya kikazi ya siku mbili wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura kuongea na wananchi waliokuwa katika tamasha la utamaduni katika Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom mara baada ya kuwasili Wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili wilayani humo.
Baadhi ya Washiriki wa tamasha la utamaduni katika Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom, wilaya ya Mbullu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (hayupo pichani) alipotembelea kituo hicho.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akitoka ndani kujionea moja ya nyumba za asili ya Wabantu Wanyiramba na Wanyisanzu iliyopo Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) kilichopo Haydom.)

Msafiri Zawose awaomba Watanzania kumpigia kura Tuzo za Afrima

0
0
 Na Humphrey Shao

Msanii wa Muziki wa Asili nchini anayetamba katika majukwaa ya kimataifa Msafiri Zawose amewataka watanzania wazidi kumpigia kura hilo aweze kutwaa tuzo ya Afrima katika kipengele cha Muziki wa asili

Zawose ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa Michuzi blog juu ya Mipango yake ya kufanya matamasha nje ya nchi.

"Cha kwanza ni kuwataka watanzania waingie katika website ya afrima kisha kipita katika kipengele cha best tradional music na kumchagua Msafiri Zawose kutoka Tanzania hili niwe mshindi na kuleta heshima kwa taifa" amesema Zawose.

Ametaja kuwa mafanikio makubwa     uanzia Nyumbani hivyo ni wakati wa  Watanzania kumuunga mkono katika kutambulisha utamaduni wetu kimataifa.
Ametaja kuwa huu ndio muda wa kuweza kuionyesha Dunia  namna tulivyojaliwa vitu vya asili ambavyo vinaweza kuwavutia watalii kuja nchinini.

Zawose amemaliza kwa kusisitiza kuwa ni vyema kila mmoja kimpigia kura kadri awezavyo hilo awe kuibuka mshindi

MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA WAKABIDHI CHUPA ZA DAMU 300 HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

0
0
 Mpango wa Taifa wa Damu salama kanda ya mashariki Dar es Salaam jana ulikabidhi chupa za Damu 300 kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.  Akizungumza wakati wa makabidhiano Afisa uhusino Mpango wa Taifa wa Damu Salama Bw. Rajab Mwenda alisema chupa hizo za Damu zitasaidia kuokoa maisha ya wahitaji hospitali na zimepatikana kutokana na kampeni ya kukusanya Damu ambayo imeanza wiki hii ambapo mkoa wa Dar es Salaam mpaka jana ulikuwa umeisha kusanya zaidi ya  chupa za damu 500.  
 Bw. Rajab alitumia fursa ya makabidhiano kuwashukuru Jumuiya ya Khoja shia kwa mwitikio wao mkubwa wa kuchangia Damu kwa hiari siku ya Ashura 24/9/2017.  Siku ya Ashura ni siku ambayo Jumuiya ya Khoja shia kila mwaka huwa wanaadhimisha kifo cha Imam Hussein kwa kuchangia Damu. Pia alitoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kuchangia damu kama Ishara ya kuunga mkono jitihada za Mpango kuhamasisha jamii kuchangia Damu ili kupunguza vifoo vinavyoweza sababishwa na uhaba wa Damu

Mwakilishi wa Hospitali ya Muhimbili Bw. Hamisi Shabani Kubiga alishukuru Mpango wa Taifa wa Damu salama kwa kugawia Hospitali ya muhimbili kiasi hicho cha chupa za Damu, chupa hizo zitasaidia kutibu kina Mama na watoto wenye uhitaji wa Damu, Majeruhi wa ajali na magonjwa mengine alisema Bw. Hamisi

AZAM FC YAANZISHA LIGI YA VIJANA U-15, KUANZA OKTOBA 7 CHAMAZI

0
0
KLABU ya Azam FC inatarajia kuanzisha Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 15 (Azam Youth League U-15), itakayoanza kutimua vumbi kuanzia Oktoba 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Hiyo ni ligi ya pili kwa vijana baada ya ile ya chini ya umri wa miaka 13 (Azam Youth League U-13) iliyomalizika Julai mwaka huu ikishuhudiwa Bom Bom FC ikiwa mabingwa na Azam U-13 ikishika nafasi ya tatu.

Akitangaza ligi hiyo Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Tom Legg, alisema kuwa ligi hiyo itakuwa ikifanyika kila Jumamosi kwa muda wa wiki kumi huku akizitaja timu zinazoshiriki kuwa ni Bom Bom SC, JMK Park Academy, Rendis FC, New Talent na Florida Academy.

“Kwa muda wa wiki 10 timu zitacheza nyumbani na ugenini, ligi ya U-15 itahusisha wachezaji 11 dhidi ya 11 tumeziboresha baadhi ya kanuni ili kuhakikisha kuwa wachezaji wanacheza na vilevile kujifunza ndani ya wiki hizo 10,” alisema.

Alisema kuwa kama walivyofanya kwenye michuano iliyopita kudhibiti umri wa wachezaji, pia safari hii wamejipanga vilivyo kuhakikisha wachezaji wote wanaocheza michuano hiyo wanakuwa kwenye umri unaotakiwa wa chini ya miaka 15.

“Kila mchezaji atayeshiriki michuano hiyo atapimwa na mimi na baadhi ya watu wa benchi la ufundi katika siku ya usajili, kila mchezaji atatakiwa kuonyesha nakala ya cheti chake cha kuzaliwa au uthibitisho wowote na taarifa zote zitawekwa mtandaoni na kila kocha wa timu zote ataweza kujionea taarifa hizi,” alisema.

Legg alisema kuwa wanatarajia kuitanua ligi hiyo Tanzania nzima kwenye vituo vyao maalumu watakavyovianzisha hapo baadaye ikiwa ni mipango ya muda mrefu, lakini katika mipango ya muda mfupi wameamua kuanza na mkoa wa Dar es Salaam.

Katika kujiandaa na ligi hiyo, tayari kikosi cha Azam FC U-15 kinaendelea na mazoezi makali kila siku za Jumanne, Alhamisi na Jumamosi, ikicheza mechi za kujipima ubavu.
Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Tom Legg akizungumzia ligi ya vijana 

RC MAKONDA ATANGAZA NEEMA KWA WAMILIKI WA VIWANDA VIDOGO, DAR

WATEJA WA CBA BENKI WAENDELEA KUNUFAIKA NA PROMOSHENI YA"WEKA AMANA USHINDE"

0
0
  Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki wa Benki ya CBA kwa wateja binafsi, Julius Konyani, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa kuchezeshwa droo ya tatu ya ya promosheni ya akiba inayojulikana kama ‘Weka amana ushinde’ zaidi ya milioni 20 zinaendelea kushindaniwa na wateja wa benki hiyo, Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemedi na kushoto ni Mkuu wa Mauzo na Mahusiano ya Kibenki wa CBA, Godson Biyengo.
 Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki wa Benki ya CBA kwa wateja binafsi, Julius Konyani, akibonyeza kitufe cha kompyuta kwa ajili ya kuchezesha droo ya kuwapata washindi wa promosheni ya akiba inayojulikana kama ‘Weka amana ushinde’ zaidi ya milioni 20 zinaendelea kushindaniwa na wateja wa benki hiyo , Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemedi na kushoto ni Mkuu wa Mauzo na Mahusiano ya Kibenki wa CBA, Godson Biyengo.
 Mkuu wa Mauzo na Mahusiano ya Kibenki wa CBA, Godson Biyengo, akimuonesha Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki wa Benki ya CBA kwa wateja binafsi, Julius Konyani (katikati) na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemedi, mshindi wa droo ya tatu ya ya promosheni ya akiba inayojulikana kama ‘Weka amana ushinde’ zaidi ya milioni 20 zitashindaniwa na wateja wa benki hiyo, mara baada ya kuchezeshwa, Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki wa Benki ya CBA kwa wateja binafsi, Julius Konyani, akizungumza na mmoja wa washindi aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 2/- kwenye droo ya tatu ya ya promosheni ya akiba inayojulikana kama ‘Weka amana ushinde’ zaidi ya milioni 20 zinashindaniwa na wateja wa benki hiyo, Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemedi na kushoto ni Mkuu wa Mauzo na Mahusiano ya Kibenki wa CBA, Godson Biyengo.

INTRODUCING RAPSAM - TUGENDE (OFFICIA VIDEO)

SOKO LA NDIZI LA KIMATAIFA LATARAJIWA KUJENGWA WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA

MAKAMISHNA WA UPELELEZI WA KODI AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA DAR

0
0
Kaimu Naibu Kamishna Upelelezi wa Kodi, Eustacio Makala akisalimiana na Meneja Elimu kwa mlipa kodi, Diana Masala kabla ya kuanza kwa mkutano wa watendaji waandamizi wa Mamlaka za mapato za jumuiya ya Afrika Mashariki kwa makamishna wapelelezi kwa maswala ya kodi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Washiriki wa mkutano huo wakianza kwa kumtanguliza Mungu kwanza. 
KAIMU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Gerald Mwanilwa akisoma hotuba ya Kamishna Mkuu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa makamshina na watendaji waandamizi wa Mamlaka za mapato za jumuiya ya Afrika Mashariki kwa makamishna wapelelezi kwa maswala ya kodi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. 
KAIMU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Gerald Mwanilwa (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya watendaji waandamizi wa mamlaka hiyo wakati wa mapumziko ya Mkutano wa Mamlaka za mapato za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa makamishna wapelelezi kwa maswala ya kodi uliofunguliwa jijini Dar es Salaam leo Septemba 27 2017. Kutokea (kushoto) ni Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi, Salim Kessi, Kaimu Naibu Kamishna Upelelezi wa Kodi, Eustacio Makala na Meneja Elimu kwa mlipa kodi, Diana Masala. 

WAFANYABIASHARA SOKO LA ILALA MCHIKICHINI JIJINI DAR ES SALAAM WAPEWA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

0
0
WAFANYABIASHARA katika Soko la Ilala Mchikichini wamepatiwa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa jinsia masokoni .

Katika hatua nyingine wafanyabiashara wanaume wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia na wanawake wametakiwa kwenda kushitaki ofisi za masoko husika ili sheria ichukue mkondo wake kwa wahusika waweze kujirekebisha.

Mwito huo umetolewa na Mwezeshaji wa Sheria masokoni, Khadija Mohamed kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG) wakati wanasheria wa shirika hilo wakitoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wafanyabiashara wa Soko la Ilala Mchikichini Dar es Salaam leo hii.

"Wakina baba mnapofanyiwa vitendo vya kijinsia na wanawake katika masoko msione haya nendeni kushitaki kwa viongozi wa masoko ili watuhumiwa waweze kukamatwa na kujirekebisha" alisema Mohamed.

Mohamed alisema vitendo vya ukatili wa jinsia hawafanyiwi wanawake pekee bali hata wanaume wamekuwa wakifanyiwa lakini wanaona aibu kwenda kushitaki.Mwezeshaji wa Sheria Batuli Mkumbukwa alisema vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo vimeshamiri hivyo alitoa mwito kwa wafanyabiashara wa soko hilo kuviacha. 
Mwezeshaji wa kisheria kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG), Amina Mussa akitoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa jinsia kwa wafanyabiashara wa Soko la Ilala Mchikichini Dar es Salaam leo. 
Mfanyabiashara Shikei Ngosi, akielezea changamoto zinazotokana na ukatili wa kijinsia katika soko hilo.
Mwezeshaji Khadija Mohamed akitoa elimu ya upingaji wa ukatili wa kijinsia.

DUNIA, AFRIKA, NA TANZANIA INAJUWA MCHELE MZURI NI KYELA, RC MAKALLA MBEYA

KAULI ZA MADIWANI WA ARUSHA WALIOHAMIA CCM

WATANZANIA KIZIMBANI KWA KUSAFIRISHA RAIA WA ETHIOPIA, NA RAIA HAO KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

0
0

 Wahamiaji Haramu wakisubiri kusomewa mashtaka ya kuingia nchini kinyume cha sheria bila ya kuwa na kibali leo jijini Dar es Salaam Katika Mahaka ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 Wahamiaji 40 kutoka Ethiopia  wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salam leo na kukutwa na mashtaka ya kuingia nchini kinyume cha sheria bila ya kuwa na kibali.
 Wahamiaji haramu wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kuwasiri tukoka walipokuwa wamehifadhiwa.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii. 

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii. 
WATANZANIA wawili, Ibrahim Abdallah dereva wa gari aina ya Nissan Civilian namba T 669 DJH na kondakta  Christopher Steven wamepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha binadamu kimagendo ambao raia 31 wa Ethiopia.


Aidha raia hao 31 wa Ethiopia wamesomewa mashtaka matano ya kuingia nchini kinyume cha sheria bila ya kuwa na kibali.


Mwendesha mashtaka wakili wa serikali kutoka Uhamiaji Novatus Mlay amedai Septemba 25, mwaka huu, huko Tuangoma wilaya ya Temeke watanzania hao walikutwa wakiwasafirisha raia hao 31 wa Ethiopia  kimagendo na kuwaingiza nchini kwa nia ya kuwapitisha na kuwasaidia kutoka Tanzania kwenda Afrika Kusini.

Hata hivyo, watanzania hao wamekana kuhusika na kosa hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 11, mwaka huu huku upande wa mashtaka ukieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika huku watuhumia hao 31 wa Ethiopia wakikubali mashtaka yote waliyosomewa na kesi iendelea Oktoba 11, 2017 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.


Wakati huo huo, watanzania  watatu akiwamo dereva wa kampuni ya Dangote Cement Ltd, Khalid Abdallah, Hussein Hamad Hassan na Jumanne Mtambo pamoja na wahamiaji nane raia wa Ethiopia wamesomewa mashtaka matano likiwemo shtaka la kusafirisha kimagendo binadamu na kuingia nchini kinyume cha sheria.


Wakili Mlay amedai mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa kuwa, wahamiaji Solomon Ertiso, Gazahegn Tiroro , Haire  Latso, Thadius Lilanso, Dawit Habtam, Deznet Godebo, Feraru Gurana na Elioj Akola, Septemba 20,2017 katika eneo la Kongowe Mbagala walikamatwa wakiingia nchini bila ya kuwa na kibali.


baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hao wote walikubali kuyatenda  makosa hayo huku  watanzania hao ambao wanakabiliwa na tuhuma za kusafirisha binadamu wanao wanadaiwa kuwasafirisha kimagendo wahamiaji hao haramu.


Mlay alidai kuwa siku hiyo ya tukio ya Septemba 20, 2017  huko Mbagala Kongowe Khalid, Hussein  na Jumanne wakiwa raia wa Tanzania  walikutwa wakiwasafirisha wahamiaji hao haramu kimagendo.


Alidai kuwa raia hao watatu wa Tanzania waliwasafirisha  kimagendo wahamiaji hao haramu kwa kutumia gari yenye namba za usajili T 961 DKA mali ya kampuni ya Dangote Cement Ltd kwa kuwatoa Tanzania kwenda nchini Afrika Kusini.


Pia washtakiwa hao, kuwa siku hiyo walikutwa wakisaidia kuwasafirisha wahamiaji hao ambao ni raia wa Ethiopia kimagendo  kwa kuwaingiza ndani ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.


Watanzania hao wamekana tuhuma hizo na kesi hiyo itaendelea Octoba 10 kwa ajili ya kutajwa huku Octoba 11 Raia hao wa Ethiopia watasomewa maelezo awali baada ya kukubali kutenda makosa hayo.

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA MAJAJI NA MAHAKIMU WAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

0
0
Waziri wa Katiba Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ally Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunga mkutano Mkuu wa Majaji na Mawakili uliokuwa ukifanyika jijini Dar es Salaa kuanzia Septemba 25-28, 2017 Ambpo alifunga Mkutano huo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.
Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania Mhe. Jaji Ignas Kitusi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufunga mkutano Mkuu wa Majaji na Mawakili wa wanachama wa Jumuiya ya Madola.
 Wawakili na Majaji wakiwa katika Mkutano wa mwaka ya wanachama wa Jumuiya ya madola jijini Dar es Salaam leo.
 Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

RAIS wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania, Jaji Ignas Kitusi amesema, Serikali inamchango mkubwa katika kuiwezesha mahakama  kutimiza majukumu yake ili iweze kusonga mbele katika maendeleo, 
huku majaji na mahakimu wakizungumzia miiko ya utendaji kazi mahakama.

Jaji Kitusi amesema hayo leo wakati wa ufungaji wa mkutano mkuu wa mwaka wa majaji na mahakimu wa Jumuiya ya madola uliomalizika leo jijini Dar es Salaam.

amesema kuwa,  katika mkutano huo wamejadili mbalo mbali moja wapo zikiwa ni changamoto wanazokutana nazo mahakimu na Majaji zikiwepo changamoto za kimtandao, usafirishaji wa binadamu ambayo pia ni changamoto.

Amesema ili kujua kama kila mwanachama wa mkutano huo amezingatia maazimio waliyofikia, mkutano mwingine mkubwa utafanyika nchini Australia ili kujipima ambapo moja kati ya maazimio waliyofikia ni  kuzingatia miiko ya kazi na kiutendaji kwa ujumla, "kwani  kila nchi imetengeneza sheria na vitabu vyake vya kanuni na maadili vinavyoongoza majaji na mahakimu.

Aidha amesema kuwa, katika mkutano huo pia wamezungumzia changamoto za ucheleweshaji wa mashauri na kuongeza kuwa kwa kuiga nchi mbali mbali ambazo zimefanya vizuri katika sekta hiyo, ni wazi kuwa nchi ambazo ziko nyuma zitaiga mfano Wa nchi hizo ili kupunguza msongamano wa mashauri mahakamani.

. Changamoto ya kifedha ambayo inahitaji ushiriki Wa serikali katika kuwezesha mahakama kutimiza majukumu yaliyopo, maadili, rasilimali watu.

alisema kuwa, kuna changamoto nyingi zinazowakabili mahakimu au majaji zikiwemo za kimaadili na kutoa wito kwa Jamii nzima kuiacha mahakama ifanye kazi bila kuiingilia na pia majaji na mahakimu wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na ushahidi bila kuruhusu kuingiliwa na vishawishi kwa namna yoyote.

Aidha alisema, Serikali inaowajibu wa kuangalia kazi za majaji na mahakimu kwani kazi zao mara nyingine zinawaweka hatarini, na ni jukumu la serikali kutoa hali ya usalama kwao Ili waweze kusikiliza kesi zao bila ya kuwa na wasiwasi na usalama wa maisha yao.

JUMIA TRAVEL YAUNGANA NA DUNIA KUADHIMISHA SIKU YA UTALII

0
0

Kila ifikapo Septemba 27 ya kila mwaka dunia huadhimisha siku ya utalii duniani. Maadhimisho hayo hufanywa na kila nchi ambapo kunakuwepo na shughuli kadhaa zikiongozwa na malengo na kauli mbiu tofauti zilizoazimiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO).

Mnamo mwaka 2015, Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa uliutangaza mwaka 2017 kama Mwaka wa Kimataifa wa Utalii Endelevu kwa Maendeleo. Na hivyo kuifanya kauli mbiu ya mwaka huu kuwa ni ‘Utalii Endelevu kwa Maendeleo.’

Maeneo matano ambayo yanaangaziwa na kufanyiwa kazi mwaka huu ni; Ukuaji wa uchumi endelevu na wa pamoja; Ujumuishwaji wa jamii, ajira na kupunguza umasikini; Ufanisi wa rasilimali, utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa; Amali za kiutamaduni, utofauti na urithi; na Maelewano ya pamoja, amani na usalama.

Katika kuunga mkono maadhimisho haya, Jumia Travel ikiwa ni mdau wa masuala ya utalii Tanzania na Afrika kwa ujumla imekuwa ikifanya jitihada za kukuza ufahamu juu ya maeneo na vivutio mbalimbali vya utalii nchini.

Hivi sasa kuna kampeni inayoendelea kwa jina la ‘Destinations Campaign’ ikiwa inalenga kukuza ufahamu juu ya maeneo tofauti nchini ambayo watanzania hawafahamu kama ni vivutio vya kitalii.

Tanzania imebarikiwa kuwa na maeneo mengi lakini hayapewi kipaumbele wala kutangazwa vilivyo. Na endapo ikiwa yanatangazwa, sio yote yanayopata fursa sawa kama vile Zanzibar, Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo watu wengi nchini na duniani wanayafahamu.

Jumia Travel imeamua kuitumia fursa ya kufanya kazi na maelfu ya hoteli nchini na Afrika kuyaangazia maeneo hayo na sehemu ambazo wageni wanaweza kulala. Kikubwa kinachofanyika ni kuwafahamisha watanzania juu ya shughuli tofauti wanazoweza kuzifanya pindi wakitembelea maeneo hayo. Mbali na hapo wamiliki na mameneja wa hoteli huhojiwa juu ya masuala wanayoona yanaweza kuwavutia wateja kwenye hoteli zao.

Jitihada za kukuza ufahamu na kutangaza maeneo mbalimbali nchini zinafanywa pia na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Bodi ya Utalii imekuja na mkakati na mbinu mpya kwa kuyatenga maeneo ya usimamizi wa wanyama tofauti na ya kawaida yaliyozoeleka na watalii wengi.

Kwa mfano, hivi sasa TTB inafanya jitihada kubwa za kukuza maeneo matano yaliyomo kwenye mpango wa usimamizi huo ambayo ni Burunge ipo Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, Randilen ipo Wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha, Ikona ipo katika Wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara jirani na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Ipole ipo katika Wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora na Mbomipa ambayo ni muunganiko wa vijiji zaidi ya 21 vya tarafa  za Idodi na Pawaga vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Kwa kufanya hivyo inatoa fursa kwa watalii kuwa na machaguo ya sehemu za kutembelea tofauti na yaliyozoeleka. Kwa sababu hata kwenye maeneo haya watalii wanaweza kukidhi haja zao kwa kuwaona wanyama na kufanya shughuli nyinginezo za kitalii.

Kwa mujibu wa ripoti ya utalii ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii Duniani, Mwaka 2016 umethibitisha kuwa ni mwaka mwingine wa mafanikio katika sekta ya utalii kimataifa licha ya changamoto kadhaa. Idadi ya watalii kimataifa imekuwa kwa mwaka wa saba mfululizo na kufikia bilioni 1.2, idadi ya ukuaji ambayo haijawahi kutokea tangu miaka ya ‘60’ (1960). Ukuaji mkubwa zaidi umeonekana kwenye sehemu za Afrika, Asia na Pasifiki.
Tunakukaribisha katika kuungana nasi na kusherehekea Mwaka wa Kimataifa wa Utalii Endelevu kwa Maendeleo 2017.

SERIKALI YAIPONGEZA COSTECH-OFAB KWA KUANDAA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI 2017

0
0

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka waandishi wa habari nchini kutumia taaluma zao kuelimisha jamii kuhusu habari za sayansi na teknolojia ili kuleta maendeleo nchini.

Akizungumza wakati wa utoaji tuzo za umahiri katika uandishi wa habari za Sayansi zilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknlojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknojia (OFAB), Waziri Ndalichako alisema tuzo hizo iwe ni chachu za kuandika habari za sayansi kwa undani ili kuwajengea uelewa wananchi wa.kawaida.

Alisema ufundi wa waandishi katika.kuandika habari za sayansi utasaidia kutangaza ubunifu na kuongeza tija thamani katika teknolojia mbalimbali."Wananchi wanahitaji teknolojia za kisasa katika kurahisisha utendaji kazi hivyo uandishi wenu utasaidia kuinua sekta ya kilimo na mifugo ambayo ndio kundi.muhimu katika jamii hasa katika kuelekea uchumi wa viwanda,"alisema Ndalichako.

Aliwataka Costech na taasisi nyingine kuendelea kushirikiana na wanahabari kuelimisha jamii katika masuala ya sayansi.Ndalichako alipongeza COSTECH na OFAB kwa kuandaa tuzo hizo kwani zitaongeza mori kwa wanahabari wa kuandika habari za sayansi.

Akielezea ushiriki wa.waandishi katika shindano hilo lililoanza Januari hadi Agosti mwaka hii, Mkurugenzi Mkuu wa COTECH, Dk.Hassan Mshinda alisema, shindano hilo hapa nchini sasa ni mara ya tisa kufanyika na kwa upande wa Afrika ni la kumi.
Mwandishi wa Habari wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu akipeana mkono na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa kwanza kwenye kuandika na kuelimisha umma kuhusu matumizi ya sayansi, Teknolojia na ubunifu hususani Bioteknolojia katika kuendeleza kilimo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda
Waziri Ndalichako akihutubia katika hafla hiyo.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz akitoa hutuba katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa COTECH, Dk.Hassan Mshinda akizungumzia tuzo hizo

UJUMBE KUTOKA KWA MKURUGENZI WA RASILIMALI WATU TRA

CRDB BANK YASHIRIKI VEMA KONGAMANO LA UWEKEZAJI MBEYA

Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images