Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

HABARI NA MATUKIO UGHAIBUNI: KIFO CHA MWANASARAKASI MOHAMMED IDI MOHAMMED (“MOHDY”)

$
0
0
Na Freddy Macha
Sarakasi ni kati ya sanaa hatari na za kusisimua sana.  Kwa sasa Ulaya wapo vijana na watu wa makamo mbalimbali waliohamia toka Afrika 

Mashariki (hasa Kenya na Tanzania) wakitumbuiza kadamnasi kwa sarakasi, Uingereza, Ureno,  Ujerumani na Hispania.
Nchini Hispania kuna visiwa vya Grand Canary ambapo Watanzania wachache hurukaruka kuvutia maelfu ya watalii.

 Moja yake ni Lanzarote. Hapa  Mtanzania Mohammed Idi Mohamed aliyehamia  baada ya kuishi Ujerumani kwa kipindi. Mohdy, Muddy au Modi (mwenye rasta fupi pichani) aliwahi pia kufanya kazi Tanzania, Ureno na Uingereza.

Alifariki Jumatatu 18 Septemba, 2017, asubuhi. Sababu za kifo chake zimeelezwa na waganga ni kuvuja damu kutoka mfereji wa koo kwenda mapafu na kutokea tumboni. 
Alipasukwa mshipa huu wa  damu ghafla na kuanguka bafuni akipiga mswaki. Bahati nzuri Muddy alijikatia bima ya maisha ambayo imeondoa tatizo la kusafirisha mwili wake nyumbani kuzikwa. Michango iiliyoombwa kutolewa itasaidia familia yake na gharama nyingine za mazishi.  Tuma kupitia Western Union. Huwa bei nafuu zikitumwa zifike kesho yake badala ya siku hiyo hiyo... Marehemu ameacha watoto wawili na wajukuu. Mungu aiweke roho yake pema peponi. 
Kwa walio Ujerumani, ni Malimbo Saidi Malimbo, simu (+49 ) 1522-4082848.

Uingereza, Saidi Kanda (+44) 4040-66607. Tanzania, Eddy Sengo,  (+255) 656 210 725.


Picha ihsani ya Fab Moses, Lanzarote, Hispania 
-London, 26  Septemba    2017



RPC TANGA apiga marufuku upigwaji vigodoro katika jiji hilo​

Jipatie Engine na spare za Land Rover Discovery kwa bei nafuu

$
0
0
Tunauza Engine na spare za Land Rover Discovery kwa bei nafuu tunaleta kutoka U.K Engine hiyo ya TD5 inauza Milioni 4.7 tunazo za Manual na Automatic pia tunaweza kukupatiya Spare ya aina yoyote kutoka Europe 
wasiliana na sisi kwa maelezo zaidi tupigie +255718030320 +255674782666 
au kwa whatsapp +447723550406

BIMA YA MAYFAIR YAZINDUA MIKATABA KWA LUGHA YA KISWAHILI.

$
0
0




KATIKA kiuenzi lugha ya Kiswahili, kampuni ya bima ya Mayfair imezindua mkataba wa bima uliotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili ili kumuwezesha mwananchi kuelewa haki zake kwa lugha rahisi anayoielewa moja kwa moja.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kamishna Wa bima Tanzania (Tira), Bhagayo Saqware amesema, mkataba huu wa bima wa kiswahili wa Mayfair umeiongezea heshima lugha ya kiswahili kwani wameonyesha wanaiheshimu lugha ya taifa inayotumiwa na watanzania takribani milioni 50.
"Lugha ya kiswahili inazungumzwa na zaidi ya wazungumzaji milioni 200 kutoka ndani na nje ya Tanzania, mktaba huu utawawezesha kwenda mbele zaidi" amesema Saqware.

Ameongeza kuwa mkataba kwa lugha ya kiswahili utawaongezea wananchi wengi uwezo wa ufahamu wa bima na hivyo kufanya shughuli ya mamlaka ya bima kuelimisha jamii juu ya bima itakuwa imepata msukumo

Aidha ametoa wito kwa makampuni mengine ya bima kufanyia mabadiliko mikataba yao kama walivyofanya Mayfair kwa kuandaa mikataba kutoka lugha ya kingereza kwenda kiswahili ambayo ni mabadiliko chanya.
Amesema yakijitokeza makampuni mengi kufanya hivyo, yatasaidia kukuza kiswahili kwani mpaka sasa bima ya Mayfair wameingia katika vitabu vya historia vya ndani na nje ya nchi kwa kukuza lugha ya kiswahili.

Ameongeza, kulikuwa na changamoto kubwa, watu wengi walikuwa hawajui haki zao kupitia mikataba ya kiingereza lakini tafsiri hii sasa itawawezesha kujua haki zao ambapo ili kuhamasisha hilo tunatoa tuzo mbali mbali kwa makampuni yanayofanyia mabadiliko mikataba yao kwa kutoa tozo nafuu katika utoaji wa leseni na kuharakisha.

" Ili mtu uelewe jambo lolote, lazima ulipate jambo hilo kwa lugha yakwako* " kama mtu unaweza kuota usiku kwa njia ya kiswahili basi ujue wewe unajua kiswahili na kama haujawahi kuota kwa kiingereza basi hujui kiingereza" amesema.

Naye.  Mkurugenzi wa bodi UA myfair, William Erio amesema mkataba huo utawezesha watu wengi kunufaika na Huduma za bima ya Mayfair kwani mtu atakuwa anauhakika yuko salama kwa kuelewa nini kipo ndani ya mkataba, "Kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu nchini vhhapa tumepata mafanikio makubwa, Mayfair ni kampuni ya kwanza katika sekta ya bima Tanzania kutafsiri mkataba wa bima ya magari kwa kiswahili.

Kamishna Wa bima Tanzania (Tira), Bhagayo Saqware akizungumza mara baada ya kuzindua mikataba ya bima ya Mayfair mara baada ya kuzidua ambayo imeleta tija kubwa kwa ya matumizi ya Lugha ya Kiswahili pamoja na kukuza Lugha yetu hapa nchini ikiwa ni Mkataba wa Kwanza kuandikwa kwa kiswahili.
 Kamishna Wa bima Tanzania (Tira), Bhagayo Saqware katika akikata utepe wakati wa kuzindua mkataba wa bima wa kiswahili ambao umeiongezea heshima lugha ya kiswahili hapa nchini uzinduzi huo umefanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa bima ya Mayfair,Sanjay Singh na kushoto ni  Mkurugenzi Mkuu wa Sumaria Group,Jayesh Shash.

 Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa bima ya Mayfair,Sanjay Singh akizungumza mara baada ya kuzindua Mikataba ya bima ya Kiswahili hapa nchini ambayo italeta uelewa wa kuelewa vizuri mikataba ya bima wanazokata.Waanzilishi wa Bima ya Mayfair  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mikataba ya kiswahili ya  bima ya Mayfair jijini Dar es Salaam.

JALADA LA KESI YA RAIS WA SIMBA SC,AVEVA NA MAKAMU WAKE BADO LIPO KWA DDP.

$
0
0
JALADA la kesi inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Wakili wa Serikali Mkuu, Vitali Peter ameyaeleza hayo  kwa Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.


Vitalis ameleza kuwa hadi sasa bado wanasubiri kurejeshwa kwa jalada hilo na maelekezo ya kuendelea kama DPP atakuwa amejiridhisha na uchunguzi kuwa umekamilika.

Wakili wa washtakiwa, Evodius Mtawala aliomba ahirisho fupi kwa sababu taratibu za kiofisi haziwezi kuchukua muda mrefu. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 4,2017.

Evans Elieza Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.

Katika shtaka la kwanza, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.

Katika shtaka la pili alidai kuwa Machi 15,2016 katika benki ya CRDB tawi la Azikiwe Ilala Aveva akijua alitoa nyaraka za uongo ambayo ni fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakati akijua ni kosa.

Katika la tatu la kutakatisha fedha, Aveva na Nyange wanadaiwa kuwa kati ya Machi 15 na Juni 29,2016 Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama ya kutakatisha fedha kwa kupata USD 300,000 wakati wakijua ni zao la uhalifu.

Kwa upande wa shtaka la nne la kutakatisha fedha, Aveva anadaiwa kuwa kati ya Machi 15,2016 katika benki ya Baclays Mikocheni alijipatia USD 300,000 wakati akijua zimetokana na kughushi.


Katika shtaka la tano la kutakatisha fedha, mshtakiwa Nyange anadaiwa kuwa Machi 15,2016 katika benki ya Baclays tawi la Mikocheni alimsaidia Aveva kujipatia USD 300,000 wakati akijua fedha hizo zimetokana na kughushi.

Washtakiwa wapo rumande kwa sababu shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili halina dhamana.

MAWASILIANO YAONGEZA KASI YA UKUSANYAJI WA MAPATO YA SERIKALI

$
0
0
Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli imesisitiza kwa taasisi za Serikali, sekta binafsi na wananchi kwa ujumla kulipa kodi kwa wakati ili nchi iweze kuongeza mapato yake kwa lengo la kukuza uchumi, kujenga miundombinu ya barabara, reli, bandari, mawasiliano, kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na kuweza kuwatumika wananchi.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigalla wakati wa ziara ya Kamati yake ya kukagua ujenzi wa minara, ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini na kwenye maeneo yasiyo na mvuto wa kibishara kwenye mikoa ya kanda ya ziwa ya Mwanza na Mara ambapo Serikali imetoa ruzuku kwa makampuni ya simu za mkononi ili ziweze kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi kupitia Mfuko wa Mawasiliao kwa Wote (UCSAF) ulio chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Ameongeza kuwa Kamati yake inasimamia sekta ya miundombinu yote nchini ikiwa ni pamoja na miundombinu ya mawasiliano ambayo inategemewa na Serikali katika kukuza uchumi na kuiwezesha nchi yetu kufikia uchumi wa kati na kuwa nchi ya viwanda. Prof. Norman Sigalla King amesema kuwa miundombinu na huduma za mawasiliano ni moja ya nguzo kuu za ukuaji wa uchumi, inachochea maendeleo ya taifa letu na kuiwezesha Serikali kuhudumia wananchi wake kwa haraka, wakati, kwa ufanisi na kupunguza gharama za Serikali kuwahudumia wananchi na kuokoa muda. “Serikali imepeleka fedha nyingi kwa ajili ya miundombinu mbalimbali ya nchi yetu kupitia Wizara hii kwenye bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2017/2018 ili nchi iweze kusonga mbele”, amesema Prof. Norman Sigalla King.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Kamati ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mnara wa TTCL kwenye kijiji cha Sanga Itinje kilichopo Kata ya Itinje wilaya ya Meatu mkoani Simiyu. Kushoto kwa Mwenyekiti ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Eng. Peter Ulanga.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bwana John Mongella akiongea kuhusu mchango wa mifumo ya mawasiliano katika kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu na watendaji wa kampuni za simu wa mkoani Mwanza (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua ujenzi wa minara, ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini mkoani Mwanza. Aliyeketi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King. 


Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Bwana Abdallah Lugage akitoa taarifa kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mnara wa kampuni hiyo kwenye kijiji cha Sanga Intinje kilichopo kata ya Intinje wilaya ya Meatu mkoani Simiyu. Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Norman Sigalla King.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, watendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, wafanyakazi wa TTCL na wanakijiji wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mnara wa kampuni hiyo kwenye kijiji cha Sanga Intinje kata ya Intinje iliyopo wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.

MBUNGE MUSSA AIPIGA JEKI TIMU YA AFRICAN SPORTS YA TANGA.

$
0
0
TIMU ya African Sports “Wanakimanumanu”imepata msaada wa vifaa vya michezo kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi daraja la pili itakayoanza kutimua vumbi.

Vifaa hivyo ambavyo ni seti ya viatu vilitolewa juzi na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku katika halfa iliyofanyika kwenye viwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo,Mbunge Mussa alisema ameamua kutoa vifaa hivyo ili kuweza kuihamasisha kufanya vizuri katika mashindano hayo na hatimaye kuweza kurudi ilipotoka.Alisema licha ya timu hiyo kushuka daraja hivi sasa wanapaswa  kujiimarisha na kucheza kwa umakini mkubwa ili kuweza kucheza michuano ya ngazi za juu.

“Mimi ni Mbunge lakini pia ni mwana michezo hivyo nitahakikisha nazisapoti timu za mkoa huu kwa lengo la kurejea kwenye makali yao ya zamani kwani michezo ni ajira “Alisema.Nay kwa upande wake,Mweka Hazina wa timu hiyo,Sad Juma alimshukuru mbunge huyo kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia timu hiyo kuondokana na uhaba uliokuwepo.

“Kama unavyojua sisi tulikuwa na uhaba wa vifaa vya michezo hususani viatu na nyenginevyo hivyo alichotupa mbunge tunamshukuru lakini tutakuwa nawe bega kwa bega “Alisema.Hata hivyo alisema hivi sasa wanaendelea na maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na mashindano hayo wakiwa na kikosi imara ambacho kimedhamiria kupata mafanikio.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi viatu Mweka Hazina wa timu ya African
Sports,Sad Juma kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi Daraja la pili makabidhiano hayo yalifanyika uwanja wa CCM mkwakwani mjini Tanga
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi viatu Mweka Hazina wa timu ya African Sports,Sad Juma kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi Daraja la pili makabidhiano hayo yalifanyika uwanja wa CCM mkwakwani mjini Tanga
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akisalimiana na wachezaji wa timu ya Jang'ombe ya Zanzibar ambao wameweka kambi mkoani Tanga wakati alipokwenda kukabidhi vifaa kwa timu ya African Sports.

MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA

$
0
0
Kwa mara nyingine mchezo wa Bahati Nasibu wa Tatu Mzuka, mchezo unaojinyakulia umaarufu mkubwa nchini Tanzania, umetangaza mshindi wake wa droo kubwa ya Juma la nane ambaye amejishindia kitita cha shilingi za Kitanzania milioni 60. Mshindi huyu si mwingine bali Bi. Rebecca Amos mkazi wa Yombo Vituka, jijini Dar es Salaam. 

Bi Rebecca, mwenye umri wa miaka 22, ameibuka na ushindi huu mnono katika mchezo uliofanyika Jumapili iliyopita na kurushwa mubashara katika televisheni.

Kufuatia zawadi hii ya iliyotolewa Juma hili na aina ya washindi wanaoibuka, mchezo wa Tatu Mzuka ni dhahiri umeendelea kuleta mageuzi makubwa katika eneo la michezo ya Bahati Nasibu hapa nchini. Hii inatokana na aina ya washindi wanaopatikana na pia uwezo Tatu Mzuka kutoa zawadi za washindi zinazofikia kiasi cha shilingi milioni 2 kila saa kwa saa 24 kwa siku. Ushindi huu unatolewa ilhali kiasi cha kushiriki katika mchezo huu kikiwa ni kuanzia shilingi 500 tu huku droo za kusaka washindi zikifanyika kila saa.

Akizungumza na vyombo vya habari kuhusu namna mchezo huu wa Tatu Mzuka unavyobadili maisha ya watu, Meneja Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga alisema; “Droo inayofanyika mara moja katika Juma si aina pekee ya kupata washindi katika mchezo huu kwa kuwa kila mtu anapocheza Tatu Mzuka anapata pia nafasi ya kushinda mara 200 ya kiasi alichotumia kucheza kila saa. Droo hizi za kila saa kwa sasa zinatoa washindi ambao wanapata hadi kiasi cha shilingi milioni 300,000 katika Juma, kwa washindi mbalimbali nchini Tanzania.”

  Meneja Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu namna mchezo huu wa Tatu Mzuka unavyobadili maisha ya watu,huku akimtaja Rebecca Amos (pichani kulia),mkazi wa Yombo Vituka aliyejishindia kitita cha shilingi milio 60,picha shoto ni rafiki wa mshindi wa Tatu Mzuka kwa wiki hii,Agness Swai

Maganga  alisema kuwa Droo inayofanyika mara moja katika Juma si aina pekee ya kupata washindi katika mchezo huu, kwa kuwa kila mtu anapocheza Tatu Mzuka anapata pia nafasi ya kushinda mara 200 ya kiasi alichotumia kucheza kila saa. Droo hizi za kila saa kwa sasa zinatoa washindi ambao wanapata hadi kiasi cha shilingi milioni 300,000 katika Juma, kwa washindi mbalimbali nchini Tanzania.”
 Rebecca Amos (pichani kulia),mkazi wa Yombo Vituka aliyejishindia kitita cha shilingi milio 60 za Tatu Mzuka,akitoa ushuhuda wake kuhusiana na mchezo huo na hatimaye nae kuibuka mshindi wa mamilioni.Rebecca amewaasa watu wengine kucheza mchezo huo kwani mmoja wao anaweza akaibuka mshindi na kubadilisha kabisa mfumo wake wa kimaisha kupitia fedha atakazo kuwa ameshinda 
Meneja Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi mshindi Rebecca Amos ,mkazi wa Yombo Vituka aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 60,mapema leo jijini Dar.

IDDA3: Sahara Group advocates digital revolution at UN meeting

$
0
0
Executive Director at the Sahara Group, Tonye Cole has said the industrialisation of Africa in the next decade must be owned and led by Africans with key support from the private sector as well as regional and multilateral organisations.

Citing the need for a robust “digital infrastructure”, Cole urged African leaders to commit to having a digital highway that connects the various nations. “It will form the basis upon which everything else will thrive.

 It will unleash jobs for our teeming youths, deliver education to the uttermost corners of the continent, connect farmers and entrepreneurs to the world, deliver healthcare to remote locations and inspire electrification projects across borders."

Cole who is also co-founder of the leading African energy conglomerate represented the Private Sector on a panel during a session on Africa at the recently concluded 72nd United Nations General Assembly in New York.

Themed: “Third Industrial Development Decade for Africa (IDDA3, 2016-2025): From political commitments to actions on the ground,” the session sought to address, among others, the environmental, social and economic challenges and opportunities that the continent faces in its quest for sustainable development.

WAZEE WILAYA YA UBUNGO WAISHUKURU NIDA KWA KUWATHAMINI NA KUWAJALI

$
0
0
Wazee wa Kata ya Manzese Wilaya ya Ubungo mkoa wa Dar-es-Salaam wamefurahishwa na kitendo cha serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) kuwapatia fursa maalumu ya kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa na wao kutambulika kama Raia sambamba na zoezi linaloendelea sasa la kuwasajili Kadi za Afya mpango ulio chini ya Manispaa ya Ubungo.

Wakizungumza wakati wa Usajili unaoendelea katika kata hiyo ukihusisha ujazaji fomu za maombi ya Vitambulisho, uchukuaji alama za Vidole, picha na Saini za Kielektroniki; wazee hao wamesema hii kwao imekuwa ni fursa ya pekee na kuomba NIDA kuendelea kusogeza huduma hizi kwa wazee waliopo kwenye maeneo mengine nchini.

Mzee Sudi Abdallah Sudi amesema “ Hii ni fursa adhimu sana na tunaomba muendee na moyo huu wa kutujali wazee na kusogeza huduma hii kwa wazee waliopo kwenye Kata zingine kwani itawasaidia wazee. Wazee wengi tunakosa fursa nyingi zikiwemo huduma mbalimbali kutokana na umri wetu mkubwa kwa kushindwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma zilikowekwa”
Baadhi ya Wazee wa kata ya Manzese wakisubiri huduma ya Usajili katika zoezi la kuwasajili wazee linaloendelea Wilayani humo kwa kuratibiwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ofisi ya Wilaya ya Ubungo.
Zoezi la kuwasajili Wazee Kata ya Manzese likiendelea.Katika picha ni mmoja wa wananchi akisubiri kupigwa picha katika moja wapo ya hatia za Usajili na uchukuaji alama za Kibaiolojia.
Ndg. Anthony Mwasiguhu Afisa usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akiingiz taarifa za Bi. Fatuma kwenye mfumo wa Usajili wakati zoezi la kuwasajili wazee likiendelea Kata ya Manzese. 
Bi. Neema Mbila Afisa Usajili Wilaya ya Ubungo akimsaidia Bi.Fatuma kujisajili wakati wa hatua ya uchukuaji alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki wakati wazoezi la kuwasajili wazee linaloendelea sambamba na usajili wa kadi za Afya kwa Wilaya ya Ubungo.



Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO katika Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari Sept 28

$
0
0
Katika ulimwengu wa uchangamano, ufikivu wa habari ni muhimu katika kujenga jamii yenye maarifa, iliyo shirikishi na endelevu. Huu ndio ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari kwa Wote (IDUAI), ukizingatia jukumu muhimu ambalo ufukivu wa habari hufanya katika kuendeleza Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu. 

Ufikivu habari ni haki ya msingi. Inawawezesha wanawake na wanaume kuelewa na kushiriki katika kujenga na kushirikiana ujuzi wanaohitaji ili watoe mchango kikamilifu katika jamii yao. Raia wenye taarifa sahihi huifanya serikali iwajibike. 

Ufikivu Habari ni dereva wa uvumbuzi na ubunifu, kuongeza fursa kwa wote, hasa kwa wasichana na wanawake. Ufikivu habari huanza na kujitolea kwa Serikali kutengeneza, kueneza na kutekeleza sera na sheria zinazohusu haki ya habari na kuhakikisha kuheshimiwa kwa haki hii ya kibinadamu. Hii inahitaji utaratibu wa ufanisi wa utekelezaji na utamaduni wa uwazi katika aina zote za taasisi. 

Wananchi wanahitaji pia kuwa na fikra pana, ujuzi wa kusoma na ujuzi wa kidigitali ambao unahitajika kufikia, kuchambua na kutumia habari kwa njia tofauti, nje na ndani ya mitandao. Hii ndiyo maana UNESCO inaziomba serikali zote na washirika kutumia uwezo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili kusaidia kufikia Lengo la 4, Elimu Endelevu inayolenga kuhakikisha "elimu shirikishi, sawa na ya ubora na kukuza fursa za elimu isiyo na mwisho kwa wote; Ufikivu wa Habari pia unajumuisha kukuza uandaaji wa maudhui yanayofaa, yenye kulenga jamii husika na yanayopatikana kwa lugha mbalimbali. Yote hii inahitaji sera zenye ufanisi na ushirikiano mzuri katika ngazi zote. Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari kwa Wote pia ni fursa ya kurejea ahadi yetu ya uhuru wa kujieleza na usalama wa waandishi wa habari. Vyombo vya habari huchukua nafasi muhimu katika kuwezesha ufikivu wa habari kwa wananchi na katika kufuatilia masuala muhimu ya kijamii na wakati huo huo vikiwaelimisha wafuatiliaji kwa kuwapa ufahamu na ujuzi. 

Haiwezekani kuwepo kwa ufikivu wa habari kwa wote bila kuwepo kwa vyombo vya habari vilivyo huru. Ufikivu wa habari sio tu ni lengo peke yake; pia ni mchangiaji muhimu katika utekelezaji wa malengo mengine yote ya Maendeleo Endelevu. Kwa hiyo ni muhimu tuendeleze juhudi zetu ili kuhakikisha kuwa kila mwanamke na mwanamume wanafurahia ufikivu kamili wa habari.

Marekebisho ya sheria katika sekta ya madini hayatambuliki na kufanya sekta hiyo kukosa mabadiliko –CAG Ripoti

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG) imebainisha kuwa kipengele cha kutotambua marekebisho ya sheria kilichomo kwenye mikataba ya madini kimekuwa kikichangia kutoonekana kwa mabadiliko katika sekta hiyo.

Hayo yamebainishwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Nje wa ofisi ya CAG, Johannes Kisiri wakati wa kutoa mada kuhusu ukaguzi wa hesabu za mashirika ya umma katika sekta ya gesi kwenye warsha ya asasi za kiraia na waandishi wa habari, amesema mikataba mingi ya madini na gesi kuna kipengele ambacho sio muafaka kwa faida ya taifa ambacho kinasema ‘ yatakayobadilika kwenye sheria hayataathiri makubaliano ya awali,” amesema

Kisiri amesema ukaguzi umegundua kuwa Kampuni ya Tanzanite One Tanzania Limited(TML) iliyoingia mkataba wa kuchimba madini ya tanzanite na Shirika la Madini la Taifa(Stamico) imekuwa ikiizuia madini hayo kampuni ya Sky Associates Vila ya bila kuishirikisha stamico.

Amesema ushauri wa CAG kuhusiana na mradi kuazalisha umeme katika Korongo la Stiegler ambao ulikuwa unasimamiwa na Mamlaka ya Uendelezaji Bonde la Rufiji (RUBADA) umefanyiwa kazi kutokana ripoti ya CAG ilianisha kuwa RUBADA haikuwa na uwezo wa kifedha wa kuenesha mradi huo na kushauri kufanywa na taasisi za umma zenye uwezo kama tanesco,” amesema

Mradi huo ambao ungekuwa na manufaa sana kwa gharama za dola za marekani bilioni 2.4 (sawa na Sh trilioni 6) na kutakiwa kuzalisha megawati 2,100 ambapo Bunge limefuta sheria iliyoanzisha RUBADA kupisha taasisi nyingine kuendesha mradi huo.

Mradi huu ulipangwa kutekelezwa katika vipindi vya awamu tatu, ambapo awamu ya kwaza ungezalisha megawati 300, ya pili 600 na awamu ya mwisho ni megawati 300 ambayo ingekamilika mwaka 2028.

Kisiri amesema mikataba inailazimisha tanesco kununua umme kwa Sh 544.65 kwa uniti moja kutoka kampuni binafsi na kuuza kwa Sh 279.35 kwa uniti
 Mkurugenzi Msaidizi wa Ufatiliaji na Tathimini wa CAG, Wendy Masoyi akizungumza katika ufunguzi wa warsha warsha ya Nne ya Asasi zisizo za Kiserikali na waandishi wa habari katika kupata toleo maalum kwa mwaka wa fedha ulioshia Juni 30, 2016 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini wa Ofisi ya CAG, Sarah Reuben akineonesha muundo wa kitabu cha machapisho ya ukaguzi wa CAG kwa mwaka ulioshia Juni 30 ,2016 kwa wana warsha hawapo pichani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkaguzi wa Serikali za Mitaa wa CAG Temeke, Angel Moshi akitoa mada kwa wana warsha hawapo pichani juu ya miradi mbalimbali iliyoangaliwa katika ukaguzi wa CAG kwa mwaka wa fedha ulioshia Juni 30 , ilifanyika jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wadau wakifatilia taarifa katika warsha ya toleo maalum kwa mwaka wa fedha ulioshia Juni 30 ,2016 iliyohusisha Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani pamoja na Dar es Salaam.
Picha pamoja wadau katika warsha ya toleo maalum kwa mwaka wa fedha ulioshia Juni 30 ,2016 iliyohusisha Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani pamoja na Dar es Salaam.

FCS YAWEZESHA AZAKI ZA ZANZIBAR KUFANYA MAFUNZO YA UTETEZI MOROGORO

$
0
0
Meneja wa Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka Foundation for Civil Society, Edna Chilimo, akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wana Asasi za Kiraia kutoka Visiwa vya Zanzibar yaliyofanyika katika ukumbi wa New Savoy mjini Morogoro. 

Makundi washiriki wa mafunzo hayo ni Azaki kutoka Zanzibar na Pemba ambapo wanashiriki mafunzo ya Utetezi na Ushawishi wa Sera kutoka kwa mashirika ya MVIWATA (Muungano wa Vyama vya Wakulima Wadogo Tanzania) na MPLC (Morogoro Para-Legal Center). Mashirika haya mawili yamebobea katika Ushawishi na Utetezi wa haki za kumiliki ardhi kwa makundi mbalimbali mkoani Morogoro. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO).
Mshauri Mwelekezi wa Mradi wa Sera kutoka The Foundation for Civil Society Zanzibar, Salma Maulidi, akiendesha mafunzo hayo ndani ya ukumbi wa New savoy Morogoro.
Mkulima Mwezeshaji wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania MVIWATA Morogoro, Marcelina Kibena akiendesha mafunzo kwa washiri kutoka asasi za Kiraia za Visiwani Zanzibar yaliyofanyika katika Ofisi za MVIWATA zilizopo Viwanja vya Nane Nane mjini Morogoro.
Ofisa Miradi wa Morogoro Para-Legal Center (MPLC) Sakina Nyumayo, akifafanua jambo kwa washiriki hao wakati wa mafunzo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Miss Vyuo Vikuu sasa kufanyika Oktoba mwishoni

$
0
0
Dar es Salaam. Mashindano ya kumsaka mrembo wa vyuo vikuu vya Tanzania “Miss Higher Learning Institution 2017” yaliyopangwa kufanyika kesho Ijumaa ( Septemba 29) kwenye ukumbi wa King Solomoni, Namanga jijini yamehairishwa.

Kuhairishwa kwa mashindano hayo kumetokana na sababu za kalenda na waandaaji kufikia makubaliano ya kusogeza mbele mpaka mwishoni mwa mwezi ujao.Mashindano hayo yameandaliwa na kampuni ya Glamour Bridal Tanzania baada ya kupewa idhini ya waandaaji wa Miss Tanzania, Lino International Agency kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).

Mkurugenzi wa Glamour Bridal Tanzania Muba Saedo alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa kwa lengo la kuboresha zaidi na hatua hiyo itawawezesha kufanya mashindano yenye upinzani wa hali ya juu kutokana na idadi ya vyuo mbalimbali vilivyothibitisha.

“Tumelazimika kusogeza mbele mashindano kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wetu, warembo wataendelea na kambi chini ya mkufunzi wao Clara Michael na ba matron, Blessing Ngowi,” alisema Saedo.

Mbali ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), mashindano hayo yatashirikisha vyuo vya Taasisi ya Uhasaibu Dar es Salaam (TIA), IFM, CBE, UDOM, Tumaini – Makumira na Taasisi ya Uhasibu wa Arusha (IAA) na Chuo Kikuu Cha Ardhi.

Saedo alivitaja vyuo vingine kuwa ni Mzumbe, Chuo Kikuu cha Iringa, Tanzania Aviation University College na Magogoni.
Warembo wa wanaowania taji la mrembo wa vyuo vikuu vya Tanzania “Miss Higher Learning Institution 2017” wakiwa katika picha ya pamoja. Shindano hilo lililopangwa kufanyika Septemba 29, limehairishwa mpaka mwishoni mwa mwezi ujao.
Warembo wa wanaowania taji la mrembo wa vyuo vikuu vya Tanzania “Miss Higher Learning Institution 2017” wakiwa katika picha ya pamoja. Shindano hilo lililopangwa kufanyika Septemba 29, limehairishwa mpaka mwishoni mwa mwezi ujao.

IGP SIRRO AFANYA UKAGUZI WA KUSTUKIZA HOSPITALI YA POLISI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akisalimiana na maafisa wa Jeshi hilo alipowasili Hospitali ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa, kwa lengo la kuzungumza na uongozi na kujionea namna ya utoaji wa huduma za afya kwa wateja.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (wa pili kulia), akimjulia hali mmoja kati ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa, alipofanya ukaguzi wa ghafla katika hospitali hiyo kwa lengo la kuzungumza na uongozi na kujionea namna ya utoaji wa huduma za afya kwa wateja.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza Kamanda wa Kikosi cha Afya (SACP) Paul Kasabago, alipofanya ukaguzi wa ghafla katika Hospitali ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa, kwa lengo la kuzungumza na uongozi na kujionea namna ya utoaji wa huduma za afya kwa wateja.

DTB YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR

$
0
0
Afisa Usimamizi na Ubora wa hospitali ya Amana, Lucy Mbusi (kushoto) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa tiba na dawa kwa hospitali ya Amana, jijini Dar es salaam, vilivyotolea na Benki ya DTB kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti", mwishoni mwa wiki. Katikati ni Muanzilishi wa Doris Mollel Foundation inayojishughulisha na kusaidia watoto njiti, Doris Mollel na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya DTB, Betty Ruppia.

Wafanyakazi wa Benki ya DTB wakiwa na Muanzilishi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel (wa pili kulia) kwa pamoja wakielekea kwenye wadi ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki. Benki ya DTB walifika hospitalini kukabidhi msaada wa vifaa tiba na dawa za kuwasaidia watoto njiti ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto njiti duniani. DTB Bank imekuwa ikitoa misaada ya vifaa tiba kila mwaka kwa hospitali ya Amana na kwa mwaka huu wameamua kuwasaidia watoto njiti. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya DTB, Betty Ruppia.
Afisa Msaidizi wa Kitengo cha Elimu wa Taasisi ya Mariam Gerion, akikabidhi sehemu ya zawadi kwa wakinamama waliojifungua watoto Nditi, katika Wadi ya Wazazi  Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.
Wafanyakazi wa Benki ya DTB wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi ya Doris Mollel, muda mfupi baada ya kumazika kwa zoezi la utoaji wa vifaa tiba na dawa, kwa hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya DTB, Betty Ruppia (kulia) akishirikiana na Rahma Amood kutoka Taasisi ya Doris Mollel pamoja na Afisa Usimamizi na Ubora wa hospitali ya Amana, Lucy Mbusi kupanda mti katika moja ya maeneo ya hospitali hiyo.

ASILIMIA 95 YA MIRADI YA KUBORESHA UMEME WA TANESCO DAR ES SALAAM IMEKAMILIKA:MHANDISI MGAYA

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema, tayari asilimia 95 ya uboreshaji miradi ya umeme katika jiji la Dar es Salaam, imekamilika.

Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi, Mahende Mgaya, (pichani juu), amewaambia waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Septemba 27, 2017 na kwamba ifikapo Desemba mwaka huu wa 2017, wananchi na wakazi wa Dar es Salaam wataona ile hali ya kukatika kwa umeme, mara kwa mara imebadilika.

“Tulikuwa na jumla ya miradi mipya 18 ya kuboresha vituo vya umeme jijini Dar es Salaam ili viweze kutoa umeme wa kutosha na wa uhakika, hadi sasa, vituo vinane vimekamilika kabisa na vinafanya kazi, vimebaki vituo 10 ambavyo navyo viko katika hatua za mwisho za kukamilika, na ifikapo Desemba, 2017 vituo vyote 18 vitakuwa vinafanya akzi.” Alitoa hakikisho Mhandisi Mgaya.
Wakandarasi na mafundi wa TANESCO wakiwa kazini Moja ya vituo ambavyo vimefungwa mitambo mipya ili kuboresha upatikanaji wa umeme jijini Dar es Salaam. Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kisutu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TANZANIA YASIFIWA UN KWA MAGEUZI YA RAIS DKT MAGUFULI-DKT MAHIGA

RAIS NA MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wote wa Halmashauri Kuu,wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Alli Mohamed Shein,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Idd.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Ndg. Phili Mangula akikaribishwa ukumbini katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe  Magufuli akiwasili ukumbini kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

M-KOPA YAIPIGA JEKI SHULE YA SEKONDARI SANDULA ,MBOZI MKOANI SONGWE

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

Wanafunzi wa  shule ya Sekondali Sandula iliyopo wilayani Mbozi imeepukana na changamoto za ukosefu wa umeme pindi wanapojisomea  nyakati za usiku kwa kupatiwa msaada wa vifaa vya umeme wa Jua 'Solar'  kutoka kampuni ya  M-Kopa ikiwa ni mara ya pili kutoa msaada huo katika shule ya sekondari hiyo.

Msaada huo umefanyika  katika Shule ya Sekondari Sandula Wilayani Mbozi  kwa mara ya pili  na shule zingine zilizonufaika na msaada huo ni  shule ya sekondari Mwinyi iliyopo Mkuranga mkoani Pwani  ikiwa ni  kwa ajili kuongeza ufaulu katika shule hizo  kwa kujisomea zaidi katika nyakati za usiku na kuondokana na matumizi ya vibatari vya mafuta ya Taa. 

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa vya Umeme wa Jua , Meneja Mauzo  M-kopa  Richard  Machera amesema kuwa  kwa Shule ya Sandula uligharimu zaidi ya sh. milioni 4.9 kwa kununua taa za LED sola 36, Chajazasimu, Betri za kuhifadhi nguvu ya Jua  Tisa (9), Paneli Tisa (9), Tochi  Tisa (9) na redio za kisasa za sola Tisa (9)

Vifaa hivyo vimefungwa kwenye madarasa mawili, Ofisi ya Mwalimu Mkuu na Mwalimu Mkuu Msaidizi  pamoja na Mabweni.

Mwalimu Mkuu washule ya sekondari Sandula, Witson Mtafya amesema msaada huo utasaidia  wanafunzi  kupata muda wa ziada wa kujisomea na kufanya mijadala kwenye vikundi kwa fasihi zaidi na hatimaye ufaulu wao utaongezeka.  
 Meneja Mauzo  M-kopa, Richard Machera   akikabidhi Msaada huo vifaa vya umeme wa jua  kwa  Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Sandula Witson Mtafya katika viwanja vya Shule ya Sekondari Sandula iliyopo Wilayani Mbozi  mkoani Songwe.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sandula wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Sandula iliyopo Wilayani Mbozi .
 Walimu wa shule wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mauzo  M-Kopa,  Richard   pamoja na wageni waalikwa wengine katika picha ya pamoja. pamoja wakiwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Sandula iliyopo Wilayani Mbozi .
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live




Latest Images