Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

WAZIRI MBARAWA ATOA MAAGIZO KWA TANROAD KUSIMAMIA UJENZI WA DARAJA LA MLALAKUWA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Na Ismail Ngayonga

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameiagiza Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) kusimamia viwango, muda na gharama inayolingana na thamani ya mradi kwa Kampuni ya Milembe KIKA JV inayojenga Daraja la Mlakakuwa lililopo Barababa ya Mwai Kibaki Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mbarawa aliyasema hayo leo Jumanne (Septemba 26, 2017) Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi ujenzi wa Daraja hilo ambao ni sehemu ya upanuzi wa barabara ya Mwai Kibaki yenye urefu wa Kilometa 5.3 inayopanuliwa kutoka njia mbili za sasa hadi njia nne.

Profesa Mbarawa alisema malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa Daraja hilo linakuwa imara na kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kipindi kirefu zaidi, hivyo ni wajibu wa TANROAD kuhakikisha kuwa Mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo anaikamilisha kazi hiyo kwa kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.

“Malengo yetu ni kuhakikisha hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu upande mmoja wa njia mbili unafuguliwa mradi huo unaopaswa kukamilika katika kipindi cha miezi 24 kulingana na Mkataba tuliosaini na Watanzania wanasubiri kwa hamu kukamilika kwa mradi huu kwa kuwa utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la msongamano”

Waziri Mbarawa anasema hadi sasa Serikali imeshatoa kiasi cha Tsh. Bilioni 1.1 kati ya Tsh. Bilioni 4.8 zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao hadi sasa umefikisha asilimia 20 ya kukamilika kwake na hivyo aliigiza TANROAD kuhakikisha kuwa Mkandarasi wa mradi anaikamailisha kazi hiyo kwa wakati.

Alisema Serikali ina imani kubwa na Mkandarasi wa Mradi huo Kampuni ya Milembe Kika JV kuwa itafanya kazi hiyo kwa uzalendo mkubwa kwani kufanikiwa kwao katika kutekeleza mradi huo kutawawezesha kupata zabuni nyingine za kazi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma.

Kwa upande wake Mhandisi Miradi wa TANROAD Mkoa wa Dar es Salaam, Julius Ngusa alisema mradi huo ulianza Oktoba mwaka 2016 na unatarajia kukamilika Oktoba 2018, ambapo mpaka kufikia Mwezi Agosti 2017 Mkandarasi amekamilisha ujenzi wa nguzo 56 za awamu ya kwanza.

Aliongeza Daraja hilo litakuwa na njia mbili za magari na njia ya waenda kwa miguu na baiskeli pamoja na daraja la Mabasi yaendayo haraka (BRT) litakalojengwa katikati ya madaraja yatakayojengwa.

Kwa mujibu wa Ngusa alisema awali mradi huo ulikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mvua zilizonyesha kuanzia Mwezi Machi  hadi Juni mwaka huu, ambapo hata hivyo katika kufidia muda uliopotea Mkandarasi huyo amekuwa akifanya kazi kwa kipindi cha masaa 24 kila siku kabla ya kuanza kwa mvua za Mwezi Desemba.

Naye Mkandarasi wa Kampini ya Milembe KIKA JV, Epharaim Kakubanga alisema kampuni hiyo imejipanga kikamilifu kutekeleza mradi huo kwa mujibu wa mkataba walioafikiana baina yao na Serikali ikiwemo kuzingatia muda, ubora na kiwango cha ujenzi wa mradi wa Daraja hilo.

Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga

0
0
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla mapema jana Mei 28.2017 amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) na vifaa vya Hospitali ikiwmo vitanda na Magodoro katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani.

Dkt. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, mbali na kukabidhi gari hilo la wagonjwa na vifaa hivyo vya Hospitali kwa uongozi wa Hospitali na Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo hilo, aliweza kufanya ukaguzi wa ghafla kujionea mazingira ya Hospitali hiyo na kubaini mapungufu mbalimbali ambayoo ametoa maagizo kupatiwa ufumbuzi kabla ya kuchukuliwa hatua kwa uongozi wa Hospitali hiyo. 
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikata utepe wakati wa kukaabidhi gari la wagonjwa hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.

Miongoni mwa changamoto hizo alizobaini katika Hospitali hiyo ni pamoja na kuwa na mfumo mbovu wa uhifadhi wa taka, pamoja na uchafu katika wodi ya wazazi jambo ambalo linaweza kusababisha hatari ya maambukizi kwa Wagonjwa na wahudumu wenyewe wa Afya. 

Awali wakati wa kukabidhi gari hilo ambalo limenunuliwa kwa nguvu ya Madiwani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na Mbunge wa jimbo hilo la Mkuranga, Abdallah Ulega aliwataka kulitumia kwa uangalifu wa hali juu huku likitakiwa kufanya shughuli zilizokusudiwa katika kusaidia wananchi wake. 

“Nimesikia kileo chenu ambacho ni kupatiwa mashine ya X-Ray na na vifaa vingine muhimu. Wizara yetu inalishughulikia hilo na tunawaomba muwe na imani na Mbunge wenu ambaye amekuwa akinisisitiza juu ya jambo hilo. Hospitali ya Mkuranga ni moja wapo ambayo itafaidika na msaada wa vifaa ikiwemo mashine hiyo ya X-Ray” alisema Dkt. Kigwangalla wakati akizungumza na wananchi mbalimbali ambao pia walipata fursa ya kuuliza maswali katika tukio hilo.

Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhi vifaa vya hospitali katika tuko la sherehe hizo za kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.

  

Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa ndani ya gari la wagonjwa hospitali ya Wilaya ya Mkuranga mara baada ya kulikabidhi.

MIKOA INAYOLIMA PAMBA IONGEZE UZALISHAJI - MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa 11 inayolima pamba nchini wahakikishe wanasimamia vizuri  wakulima wa zao hilo ili kuongeza uzalishaji na kuwaletea tija wananchi. Agizo hilo limetolewa leo (Jumanne, Septemba 26, 2017) na  Waziri Mkuu wakati akizungumza na wakuu hao wa mikoa kwenye kikao alichokitiisha mjini Dar es Salaam kujadili maendeleo ya zao hilo.

Kikao hicho ni muendelezo wa kikao alichokitiisha mjini Dodoma  (Ijumaa, Septemba 8, 2017) kujadili mbinu za kufufua zao hilo.

Wakuu wa mikoa walioitwa kwenye kikao hicho ni kutoka mikoa ya Shinyanga, Singida, Kagera, Tabora, Morogoro, Mara, Mwanza, Simiyu, Katavi, Kigoma na Geita. Waziri Mkuu amesema katika kipindi hiki ambacho msimu wa maandalizi ya kilimo cha pamba umeanza ni vema kwa Maofisa Kilimo na Wagani wakawasimamia wakulima kwa ukaribu ili wahakikishe wanafuata mbinu bora za kilimo.

Amesema iwapo wakulima watapata usimamizi mzuri kutoka kwa Maofisa Ugani waliopo kwenye maeneo yao kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba yao itawasaidia katika kuongeza  tija, kwenye uzalishaji wao.

“Serikali inawataka Maofisa Kilimo na Wagani wawasimamie wakulima kuanzia maandalizi ya shamba, kupanda, matumizi ya pembejeo na dawa, kuvuna na kutafuta masoko ili kilimo cha zao hilo kiweze kuwaongezea tija.”

Amesema Maafisa Kilimo wote walioko kwenye kila Halmashauri ni lazima wahusike kikamilifu katika kuwaelekeza wakulima namna ya kutumia mbinu bora za kilimo ili waweze kupata mazao mengi , hivyo kujikwamua kiuchumi. Pia Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Vyuo vya Kilimo nchini wahakikisha wanakuwa na mashamba darasa yatakayotumika na wakulima na wanafunzi wao kujifunza mbinu bora za kilimo kwa vitendo.

 Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba; Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI; Bw. Suleiman Jafo, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Kilimo, Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dkt. Tito Haule na Mkurugenzi Uhamasishaji Mazao, Bw. Twahir Nzallawahe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa inayolima zao Pamba kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 26, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NMB YAWAFUNDA WAFANYABIASHARA MKOANI WA IRINGA

0
0
NMB Bank imeendesha mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 600 wa Iringa mjini na wilayani Mafinga yenye lengo la kuwapa ujuzi wa jinsi ya kukuza biashara zao kwa maendeleo ya kiuchumi nchini.

Wafanyabiashara hao walipewa mafunzo yanayohusu bidhaa zinazotolewa na NMB kama jinsi ya kutunza vitabu vya mahesabu, elimu ya masoko na pia elimu ya mlipa kodi na matumizi bora ya mikopo wanayopatiwa na benki ya NMB. Akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara zaidi ya 300 wa mjini Iringa, Meneja Mahusiano ya Wateja wa NMB, Wogofya Mpafalamagoa alisema kuwa katika kuwajaliWateja wake wadogo na wakati, NMB imekuwaikiendesha mafunzo ya wajasiliamali nchi nzima ili kuwapa elimu ya jinsi ya kukuza biashara zao.

“kuna wafanyabiashara hapa wameanza na mitaji midogosana, wameanza kwa kukopa shilingi laki 5 tu na kuziwekeza kwenye biashara, kupitia mafunzo haya na pia ushauri tunaowapa, wamekuza mitaji yao na wengine sasa wanakopa mabilioni NMB.” Alisema Mpafalamagoa. Mafunzo hayo ya wajasiliamali yalifanyikakwa klabu za biashara za Iringa mjini na Wilayani Mafinga ambapo zaidi ya wafanyabiashara 600 walihudhuria na kunufaika na mafunzo kutoka NMB.
Meneja Mahusiano ya Wateja wa NMB – Wogofya Mpafalamagoa akitoa mada kwenye mkutano wa wajasiliamali uliondaliwa na benki ya NMB. Zaidi ya wafanyabiashara zaidi ya 300 wa wilayani Mafinga walihudhuria mkutano huo ambapo pia walipewa mafunzo ya jinsi ya kukuza biashara zao.

NMB ina business club 34 nchi nzima zenye wanachama zaidi ya 10,000 ambao wamekuwa wakifaidika na mafunzo mbalimbali kutoka NMB yanayohusu bidhaa zinazotolewa kwao na benki kama jinsi ya kutunza vitabu vya mahesabu, elimu ya masoko na pia elimu ya mlipa kodi. Mpafalamagoa alisisitiza kwamba lengo kugawa  vilabu hivyo vya biashara vimeundwa kuhakikisha wafanyabiashara nchini wanakuza mitaji yao, kuajiri watanzania wengi zaidi na pia kuchangia uchumi wa taifa hili kupitia ulipaji kodi.

Mpafalamagoa aliongeza kuwa ilikuhakikisha benki hiyo inachangia ukuaji wa sekta ya biashara nchini, imeanzisha vilabu vya wafanyabiashara (NMB Business Clubs) ambao ndio walengwa wa vituo vya biashara. 
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mafinga, Daniel Mwasela aliwataka wafanya biashara wa wilaya ya Mufindi kujengaurafiki wa karibu na benki ya NMB Ili waweze kukuza biashara zao kupitia mikopo ya ainambalimbali ambapo yoteinalengakumkwamua kiuchumi mjasiliamali. Wafanyabiashara wadogo na wakati wanawakilisha asilimia 14 ya biashara ya NMB. NMB imeanza kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachama wake wanafikia idadi ya 25,000 kufikia mwishoni mwamwaka2017.

Wanachama wa klabu ya Biashara (NMB Business club) niwajasiliamaliambao wamekuwa wakiwezeshwa mara kwa mara na benki kwaajili ya kuendeleza biashara zao. Nje ya mafunzo na vituo hivisitavya wafanyabiashara, Wajasiriamalihawawanapatafaida ya kutumia mtandaompana zaidi wa matawi zaidi ya 200 ya NMB na ATM zaidi ya 700 nchi nzima.
Sehemu ya Wajasiliamali wadogo wakiwa kwenye mkutano wa klabu ya Biashara mjini Iriga juzi. Zaidi ya wafanyabiashara zaidi ya 300 wa wilayani Mafinga walihudhuria mkutano huo ambapo pia walipewa mafunzo ya jinsi ya kukuza biashara zao.

KAIMU MKURENGENZI MKUU WA TAA AMTEMBELEA MKUU WA MAJESHI OFISINI KWAKE

0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),Ndugu Richard Mayongela  amtembelea Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance S.Mabeyo  Ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi Upanga jijini Dar.(Picha na Ofisi ya  Mkuu wa Majeshi)

MAJALIWA AMTEMBELEA JAJI WARIOBA

0
0




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati alipomtembelea Jaji Warioba, Nyumbani kwake, Oysterbay Jijini Dar es salaam Septemba 26, 2017.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

TUNA HAZINA YA WACHEZAJI WENYE UWEZO WA KUCHEZA KOKOTE DUNIANI -KIM PAULSEN

0
0


Kocha Mkuu wa timu za vijana Tanzania, Kim Paulsen, amevutiwa na uwezo wa vijana wanaoibuka kila mwaka katika soka nchini na kusema tuna hazina ya wachezaji wenye uwezo wa kucheza mahala popote duniani.

Poulsen amewaambia waandishi wa habari leo Jumanne Septemba 26, 2017 jijini Dar es Salaam kwamba wamefanikiwa kuona uwezo wa vijana kwa wakati wote, lakini umahiri umekuwa ukiongezeka kwa kila timu mpya inapoitwa.

Kwa takribani mwezi mmoja, Kocha Poulsen akishirikiana na Oscar Mirambo walikuwa kwenye programu ya kuinoa Serengeti Boys mpya.
“Hii Serengeti mpya inayokuja, nayo ni bora kama ilivyo kwa wale waliopita. Bado naona kuna vipaji vikubwa sana. Ni kulea tu hawa vijana kazi ambayo tutaendelea nayo.”

Poulsen - Raia wa Denmark amesema kambi ya vijana 57 walioripoti na kufundishwa na makocha hao, wameonesha uwezo mkubwa, lakini kiufundi wamepunguza hadi hadi kubaki 27. 
Amesema hao waliobaki watapangiwa kambi nyingine itakayoanza Novemba 19, 2017 na itafikia mwisho Desemba 19, mwaka huu baada ya kuivunja kambi ya muda jana Septemba 25, mwaka huu.

Katika programu ya kambi hiyo mpya ya Novemba na Desemba, Kocha Kim ametaka angalau mechi moja ya kirafiki ya kimataifa huku akisisitiza apate timu ya nchi iliyowekeza hasa katika soka la vijana: “Ikiwezekana hata mbili.”

Akizungumzia kuhusu ujio mpya wa timu ya taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 - Ngorongoro Heroes, Kocha Kim amesema itaitwa kambini wakati wowote kuanzia Oktoba mwanzoni kwa kambi ya wiki tatu.

“Timu ya Serengeti Boys iliyopita ilifanya vizuri sana. Ni matarajio yetu hata hii itafanya vizuri, lakini hapa nataka nizungumzie ile iliyoshiriki fainali za AFCON u17 nchini Gabon…

“…kwa hiyo kambi itakayoitwa ya Ngorongoro Heroes, tutaita wale wote waliounda Serengeti Boys iliyopita. Hata wale ambao hawakubahatika kwenda Gabon tutawajumuisha kwa ajili ya kambi ya wiki tatu mwezi Oktoba,” amesema Poulsen.

Amesema kwamba sababu za kuita nyota wale wa Serengeti Boys katika Ngorongoro Heroes ni kuwapa nafasi ya kwanza wao kuonekana kama wangali na uwezo wa kupambana kama ilivyokuwa zamani na kwa wale wenye uwezo tu, ndio watakaochukuliwa,” amesisitiza.

VITAMBULISHO VYA TAIFA VYABISHA HODI MKOA WA NJOMBE

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka amezindua rasmi kuanza kwa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa huo, zoezi ambalo linaendeshwa katika Wilaya zote za mkoa huo ambazo ni Ludewa, Njombe Mjini, Makete pamoja na Wanging’ombe.

Akizungumza katika sherehe fupi ya uzinduzi wa zoezi hilo kimkoa Mhe. Ole Sendeka amewataka Wakuu Wote wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa, Watendaji Kata na Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa/Vijiji kushirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kufanishika zoezi hilo Msingi ili kutimiza malengo ya Serikali ya Kuwasajili Wananchi wake wote ifikapo Desemba 2018.

Amesema manufaa ya Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi ni mengi na hasa upatikanaji wa huduma kirahisi na kuimarisha ulinzi na Usalama wa nchi.zinduzi huo ulihudhuriwa na Wakuu wote wa Wilaya, kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa za Mkoa wa Njombe, Viongozi wa dini na wananchi.

Zoezi la Usajili katika Mkoa wa Njombe litahusisha uchukuaji na ujazaji wa fomu za maombi ya Vitambulisho, uchukuaji wa alama za Kibaiologia, saini ya kielektroniki, kupigwa picha na zoezi la uhakiki na mapingamizi litakalohusisha Kamati za Ulinzi na usalama na wananchi. Mkoa huo unategemea kusajili jumla ya Wananchi 426,083 kwa kipindi cha Miezi 2 kwa mpango maalumu ambao utahusisha usajili wa Mkupuo (Mass-Registration).



kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Njombe wakifuatilia kwa Karibu yale yaliyokuwa yakizungumzwa na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wakati wa Uzinduzi wa zoezi la Usajili na Utambuzi linaloendela wakati huu Mkoani humo pamoja na Wilaya zake zote.

Wakiwa kwenye Picha ya Pamoja ni Mkuu wa Mkoa wa njombe Mh. Christopher Ole Sendeka, Wakuu wa Wilaya za Njombe, kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Njombe, Afisa Usajili Mkoa wa Njombe Ndugu. Odoyo Godwin Albetus pamoja na Paroko wa KKKT jimbo la Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Christopher Ole Sendeka akihutubia Viongozi wa Mkoa na Wilaya pamoja na Wageni waalikwa katika shughuli ya Uzinduzi wa Zoezi la Usajili na Utambuzi Mkoani Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Ndugu Ali Kasinge ambae alimuwakilisha Mwenyeji wa Uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Lucy Msafiri, akimkaribisha Mkuu wa Mkoa pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa na wageni waalikwa katika Uzinduzi wa Usajili na Utambuzi wa Vitambulisho vya Taifa lililofanyika Njombe Mijini.
Afisa Usajili Mkoa wa Njombe Ndugu. Odoyo Godfrey Albetus akisoma Taarifa fupi ya zoezi la Usajili pamoja na Mpango kazi utaotumika kukamilisha zoezi hilo na kufikia Malengo tarajiwa ya Kusajili Wananchi 426,083 katika Mkoa huo wa Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bi. Zaina Mlawa akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya wakati wa Uzinduzi wa zoezi la Usajili na Utambuzi Mkoani Njombe.

Dkt. Mwakyembe Azindua Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mtwara na Lindi

0
0
Na Benedict Liwenga-WHUSM.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. John Palamagamba amezindua Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mikoa ya Mtwara na Lindi.
Uzinduzi huo umefanyika leo katika Viwanja vya Matogolo Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara ukiwa na lengo la kuwasajili watoto waliochini ya umri miaka mitano pamoja na kuwapatia vyeti ambavyo vitawasaidia kutambulika kwao na kisha kupewa nyaraka za uthibitisho yaani  vyeti vya kuzaliwa.
Waziri Mwakyembe amesema kwamba, katika kupanga maendeleo ya nchi kunahitajika takwimu sahihi za matukio muhimu za Watanzania ambazo zinaelezea taarifa zao za kuzaliwa ikiwemo za vifo kwakuwa takwimu hizo zinasaidia kujua mahitaji ya wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, lishe pamoja na sehemu nyinginezo.
“Mpango huu utaondoa utegemezi wa takwimu za kuhisia, takwimu za kukadilia ndugu zangu mfumo tulionao sasa unategemea Sensa ambayo hufanyika kila baada ya miaka 10, na matukio bado yanatokea, hivyo kutumia Mpango huu kutasaidia kupata takwimu sahihi na halisi za Watanzania wote”, alisema, Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza kuwa, Mikoa ya Lindi na Mtwara itanufaika na mpango huo kwakuwa Serikali itakuwa inatambua mahitaji halisi ya wananchi kupitia taarifa zitakazochukuliwa za uandikishaji wa watoto hao, huku akisisitiza kuwa, anaamini kwamba mikoa hiyo itakuwa chachu ya kuongezeka kwa idadi ya watoto watakaoandikishwa kama ilivyofanyika katika baadhi ya mikoa mingine ya Tanzania.
PICHA 1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na Wakazi wa Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara leo 26 Septemba, 2017.PICHA 3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe katika Kitabu cha Usajili pamoja na Simu kuashiria Uzinduzi wa Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara leo 26 Septemba, 2017.PICHA 4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Wadau mbalimbali wanaosaidia Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano mara baada ya kuuzindua leo Wialayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, 26 Septemba, 2017.PICHA 5
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiwakabidhi vyeti Wazazi kwa niaba ya watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano leo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara 26 Septemba, 2017.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKAZI WA BENKI YA DUNIA BI. BELLA BIRD

0
0
Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amkutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais na Mkurugenzi huyo  walizungumzia masuala mbalimbali ya Lishe kwa akina Mama na namna ukosefu wa lishe bora unavyopelekea vifo vya akina mama na watoto wakati na baada ya kujifungua.

Aidha wamesisitiza suala la Elimu ya Lishe Bora kwa wakina mama hao ili kukabiliana na tatizo.

Makamu wa Rais aliishukuru Benki ya Dunia kwa  kuwasaidia wakina mama wa Kitanzania na kuitaka iendelee kufanya hivyo hasa wakati huu ambapo nchi inaenda kwenye uchumi wa viwanda.​
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird ambaye alimtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI AKAGUA MPAKA KATI YA TANZANIA NA UGANDA MTUKULA MKOANI KAGERA

0
0
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala akikagua Mpaka wa Tanzania na Uganda katika Kituo cha Mpakani cha Mtukula mkoa wa Kagera, Katikati ni Kamishna wa Udhibiti wa Mipaka Samuel Magweiga ambaye ameambatana na Dk. Makakala katika ziara hiyo inayolenga kufanya ukaguzi katika Mpaka wa Tanzania na Uganda ili kujionea utekelezaji wa majukumu ya Idara yake katika Mpaka huo.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala akisalimiana na baadhi ya Maofisa wa Uhamiaji wanaofanya kazi katika Kituo cha Uhamiaji cha Mtukula mkoa wa Kagera alipofanya ziara kukagua Mpaka wa Tanzania na Uganda ili kujionea utekelezaji wa majukumu ya Idara yake katika Mpaka huo.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa pili kushoto akimsikiliza mmoja kati ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera alipotembelea kiwanda hicho ili kujionea shughuli za uzalishaji wa sukari ambapo alisisitiza dhana ya Uhamiaji na Maendeleo. Dk. Makakala ameambatana na Maafisa mbalimbali wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala akimsikiliza Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera Bw. REO B.M alipotembelea Kiwanda hicho. Dk Makakala amewasisitiza Watendaji Wakuu wa Kiwanda hicho kuhakikisha wanafuata Sheria za Uhamiaji mara wanapoajiri wageni kutoka nje ya nchi. Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Makakala yupo Mkoani Kagera kwa ajili ya kufanya Ukaguzi katika Mpaka wa Tanzania na Uganda ili kujionea utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Uhamiaji. 
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala akimkabidhi kipeperushi chenye taarifa mbalimbali za huduma zinazotolewa na Idara ya Uhamiaji Nchini, Mkuu wa wilaya ya Bukoba aliyepokea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera mara baada ya Kamishna Jenerali Dk. Makakala kutembelea Ofisi hiyo akiwa ziarani Mkoa wa Kagera kukagua mpaka wa Tanzania na Uganda.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

SUMATRA PWANI YASISITIZA NAULI MBEZI -KIBAHA NI SH.500/MBEZI-MLANDIZI SH.1,600

0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

MAMLAKA ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA),mkoani Pwani ,imewaasa wamiliki wa mabasi madogo ya abiria(daladala) yanayofanya safari zake Mbezi -Kibaha kuacha kupandisha nauli tofauti na zilizotangazwa kisheria.

Imesisitiza nauli halali kutoka mbezi hadi Kibaha ni 500 badala ya 800 wanayoitoza kwa sasa kwa abiria na Mbezi-Mlandizi ni sh.1,600 badala ya 1,800/2,000 inayolipishwa.

Aidha kuanzia sasa basi litakalobainika kutoza nauli tofauti na elekezi atafikishwa mahakamani ama kutozwa faini.
Hayo aliyasema na ofisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA)mkoani Pwani, Omary Ayubu,mjini Kibaha baada ya kufanya zoezi la kushtukiza kukamata magari yenye makosa mbalimbali,kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani hapo kupitia kitengo cha usalama barabarani.

Alisema wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kutoka kwa abiria kuwa wanatozwa nauli kubwa suala amabalo ni kinyume na sheria.
Ayubu alitaja viwango vya nauli vinazopaswa kulipwa kuwa ni Mbezi- Kiluvya kwa Komba sh.400 badala ya sh.700 na Mbezi-Picha ya Ndege sh.700 badala ya 900.

Maeneo mengine ni Mbezi hadi Mlandizi sh.1,600 badala ya 1,800/2,000, Mbezi- Kongowe sh.1,100, Mbezi-Vigwaza 2,100, Mbezi-Chalinze 3,200, Mbezi-Lugoba 4,100 na Mbezi-Msata 4,600 .
“Leo katika operesheni hii tumekamata magari 21 kutokana na makosa ya kutokuwa na ticket na kutoza nauli kubwa “

“Madereva nane watapelekwa mahakamani kutokana na kuzidisha nauli kinyume cha sheria na tunawataka wamiliki kuzingatia masharti ya leseni,” alisema Ayubu.
Alisema wataendelea kuwachukulia hatua za kisheria madereva wanaokiuka sheria na ameshukuru wananchi kwa ushirikiano wao wa kutoa taarifa juu ya magari yanayoendelea kutoza nauli ambazo ni kinyume cha utaratibu.

Ayubu aliwataka madereva kuwa na katabia ka kugomo kwani haina faida na badala yake mwenye malalamiko aende ofisini na kuandika barua ndani ya mwezi mmoja ili malalamiko yao yaweze kutafutiwa ufumbuzi.

Nae kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Pwani,Salum Morimori alisema kuwa walifanya ukaguzi kwenye mabasi hayo ili kuangalia ubora wa magari .
Alieleza kumekuwa na malalamiko toka kwa abiria kutopewa tiketi, abiria kuchanganywa na mizigo ,ubovu wa magari,matairi mabovu na kuchakaa kwa viti kwenye magari hayo.

Morimori alisema ,hadi sasa magari 35 yamekamatwa ,kati yake 21 ni makosa yanayosimamiwa na SUMATRA na 14 ni ya kiusalama barabarani.

“Tumefanya zoezi hili la kusthtukiza kwa kushirikiana na wenzetu SUMATRA ili kuwajengea kumbukumbu madereva kufuata sheria za usalama barabarani,” alisema Morimori.
Hata hivyo, alisema kuwa lengo ni kuhakikisha usalama wa wanajamii hasa wanaotumia vyombo vya moto wabaki salama.

“Wamiliki na madereva wahakikishe wanaboresha vyombo vyao viko salama kwa kufanya marekebisho hasa mipira na tunahitaji wanajamii kushirikiana nasi ili kukabiliana na madereva ambao wanakiuka sheria za usalama barabarani” alisema Morimori.

Tamasha la Wanawake Wajasiriamali kufanyika Mwezi Oktoba Jijini Dar es Salaam

0
0
Na.Neema Mathias –MAELEZO.

Umoja wa wanawake wajasiriamali (MOWE) wameandaa tamasha la 11 kwa wajasiriamali litakalofanyika kuanzia tarehe 24-30 oktoba , 2017 katika viwanja wa mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam lengo ikiwa ni kupanua wigo wa masoko pamoja na kuonyesha bidhaa na fursa mbalimbali za kijasiriamali zinazopatikana hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati ya tamasha hilo, Bi. Zubeda Kiluwa amesema kuwa, tamasha hilo litakuwa na kauli mbiu isemayo‘Mwanamke mjasiriamali funguka shiriki kujenga Tanzania ya viwanda’

“Tunawaalika wanawake wote popote walipo kushiriki maadhimisho na maonyesho haya kwani yatawahusiha wadau mbalimbali wa maendeleo ya wanawake, Wizara pamoja na taasisi za serikali na mashirika binafsi,”alisema Kiluwa.

Tamasha hilo litafunguliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwaijage ambapo wadau watakaoshiriki kutoa elimu za kijasiriamali katika tamasha hilo ni pamoja na Wakala wa Usajili Biashara na utoaji leseni (BRELA), TRA, GSM, SIDO, TBS, TFDA pamoja na wawakilishi kutoka katika benki mbalimbali ambao kupitia semina hiyo watatoa elimu juu ya ujasiriamali.

Aidha Bi.kiluwa ameleza kuwa gharama zitakazotozwa kwa wajasiriamali watakaoshiriki katika maadhimisho hayo ni shillingi 50,000 kila mmoja, na kwa yeyote atakayeshiriki kwaajili ya uzinduzi, ununuzi na kujionea bidhaa mbalimbali hawatatozwa gharama yoyote.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya tamasha hilo Bi.Anna Matinde amaesema kuwa tamasha hilo halitawahusisha wajasiriamali peke yake bali litawahusisha watu wote lengo likiwa ni kubadilishana mawazo ya kimaendeleo katika kuunga mkono sera ya Tanzania ya viwanda.

“Tanzania itajengwa na watu wengi, kupitiwa mawazo ya wajasiriamali na wale wasio wajasiriamali watapata kujua mambo mbalimbali juu ya elimu ya ujasiriamali, namna ya kujiajiri na kuondokana na wimbi la ukosefu wa ajira,” alifafanua Bi. Matinde.

Aidha Bi. Matinde amefafanua kuwa tamasha hilo halitowahusisha wanawake pekeyake bali hata wanaume wenye fursa mbalimbali za ujasiriamali wanakaribishwa kutangaza kazi zao na kujipatia elimu itakayotolewa .
Mwenyekiti na mjumne wa kamati ya maandalizi ya tamasha la 11 la Wanawake Wajasiriamali(MOWE) Bi.Anna Matinde akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wajasiriamali Bi.Zubeda Lous na kushoto ni mjumbe wa Umoja huo wakati wa utambulisho wa tamasha na semina kubwa ya 11 litakalofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 24-30 oktoba ,2017 utambulisho huo ulifanyika hivi leo katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Umoja wa Wanawake Wajasiriamali (MOWE) Bi.Zubeda Sembo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kushoto ni Katibu wa Umoja huo Bi. Naomi Kamba na kutoka kulia ni mjumbe wa MOWE wakati wa utambulisho wa tamasha na semina kubwa ya 11 litakalofanyika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaa kuanzia tarehe 24-30 oktoba ,2017 utambulisho huo ulifanyika hivi leo katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam.
Picha na Paschal Dotto-MAELEZO

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 26.09.2017

JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA

0
0
Na.Thobias Robert- MAELEZO.

Serikali imelipongeza Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa ushirikiano wake na Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta za Kilimo Afya na Maendeleo ya Jamii kwa kutumia wataalam na uzoefu kutoka Japan.

Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Msaidizi wa ushirikiano wa kiufundi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.Msafiri Marwa alipokuwa akiwaaga vijana wa kijapani waliokuwa wanajitolea katika sekta ya Kilimo na Maendeleo ya jamii hapa nchini.

“Serikali ya Japan kupitia shirika lake la JICA imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania katika sekta mbalimbali kama vile kuwajengea uwezo Watanzania kupitia ufadhili wa masomo ya elimu ya juu nchini Japan na kuleta watu wa kujitolea katika miradi ya maendeleo hapa nchini,” alieleza Bw. Marwa.

Aidha, Bw.Marwa ambaye alimuwakilisha Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bi. Suzani Mlawi aliipongeza Japan kwa kutumia rasilimali watu pamoja na rasilimali fedha kupitia JICA kufadhili utoaji wa huduma za kijamii jambo ambalo ni kipimo cha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

Amewapongeza vijana wa kijapan kwa kazi nzuri waliyoifanya hapa nchini katika kipindi chote cha miaka miwili ya kuwahudumia watanzania hasa katika sekta ya Kilimo na Afya.

“Kwa niaba ya serikali niwapongeze vijana wote mliokuja hapa nchini kwa kufanya kazi na jamii ya Watanzania, mmefanya kazi kwa jitihada kubwa wakati mwingine katika mazingira magumu, niwahakikishie kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha mazingira ya ushirikiano ili kuendeleza uhusiano ” alifafanua Marwa.
Mkurugenzi Msaidi wa Ushiririkiano wa Kiufundi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Msafiri Marwa akimkabidhi zawadi kijana wa Kijapan aliyemaliza muda wake wa kujitolea hapa nchini Bw. Yusuke Sakakibara.
Mkurugenzi Msaidi wa Ushiririkiano wa Kiufundi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Msafiri Marwa akimkabidhi zawadi kijana wa Kijapan aliyemaliza muda wake wa kujitolea hapa nchini Kyoko Tada katika hafla ya kuwaaga vijana watatu wa kijapan waliomaliza muda wao wa kujitolea hapa nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Raia wa Japan waliokuwa wakijitolea nchini kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) wakiwa katika hafla ya kuwaaga baada ya kumaliza muda wao leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Yusuke Sakakibara akiifanya Wilayani Masasi, Shu Sato, Kyoko Tada Mratibu wa vijana wa kujitolea Kutoka JICA nchinI Tanzania Bw. Ichiro Owa mara baada ya hafla kuwaga leo jijini Dar es Salaam.
Picha na: Paschal Dotto – MAELEZO


OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU IMEPOKEA TABLETS 500 ZENYE THAMANI YA SH. MILIONI 400 KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI TANZANIA BARA 2017/18

0
0
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imepokea Tablets 500 zenye thamani ya Shillingi milioni 400 kutoka Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya tablets hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema kupatikana kwa tablets hizo kutasaidia kurahisisha zoezi la ukusanyaji wa taarifa muhimu za Mapato na Matumizi ya Kaya pamoja na kupunguza gharama ambazo zingetumika kuchapisha madodoso ya karatasi.

“Ofisi ya Taifa ya Takwimu leo tumepokea tablets 500 kutoka Benki ya Dunia ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Tablets hizi zitasaidia kurahisisha kazi na kupunguza gharama ambazo tungetumia kuchapisha madodoso ya karatasi,” amesema Dkt. Chuwa.

Dkt. Chuwa amesema utafiti huu utahusisha maeneo wakilishi 796 na kaya wakilishi 9,552 zilizochaguliwa kitaalamu kuweza kutoa matokeo ya viashiria vya umaskini na viashiria vingine.
Amesema utafiti huu utatoa takwimu za msingi kwa viashiria vya kiuchumi na kijamii ambavyo vitasaidia kusimamia na kutathmini mwelekeo wa serikali katika harakati zake za kupunguza umasikini. Taarifa za utafiti huu pia zitasaidia kupima utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Awamu ya Pili (FYDP-II) 2016/17 – 20/21 na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs 2030), pamoja na kuwezesha kufanyika kwa tafiti mbalimbali zinazohusu mwenendo wa hali ya umaskini katika ngazi ya Mikoa na Wilaya.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird amesema Benki ya Dunia imetoa tablets hizo kwa NBS ili kurahisisha ukusanyaji wa taarifa kwa kutumia teknolojia ya kisasa badala ya kutumia njia ya madodoso ya karatasi ambayo ni gharama kubwa.
Amesema Benki hiyo kwa muda mrefu imekuwa ikishirikiana na NBS katika tafiti mbalimbali na hivyo vifaa hivi ni mwendelezo wa ushirikiano huo katika upatikanaji wa takwimu rasmi nchini ambazo pia hutumika kimataifa katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Kukamilika kwa utafiti huu kutasaidia kupatikana kwa takwimu rasmi zinazohusu Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi zitakazotumika kwa ajili ya kusimamia na kutathmini program mbalimbali za Kitaifa, Kikanda na Kimataifa.
tafiti huu unafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na idara mbalimbali pamoja na Wadau wa Maendeleo.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (kushoto) akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhiwa tablets kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kufanyia Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Kulia ni Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Nadia Belhaj Hassine Belghith
Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Nadia Belhaj Hassine Belghith (kulia) akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi tablets katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kufanyia Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Kulia ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mayasa M. Mwinyi.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (kushoto) akipokea tablet kutoka kwa Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Nadia Belhaj Hassine Belghith (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Ofisi ya Taifa ya Takwimu imekabidhiwa tablets hizo kwa ajili ya kufanyia Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia hafla ya kukabidhiwa tablets Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Benki ya Dunia leo jijini Dar es Salaam. Ofisi ya Taifa ya Takwimu imepokea tablets hizo kwa ajili ya kufanyia Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18.
PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA


MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 27,2017

MIKOA INAYOLIMA PAMBA IONGEZE UZALISHAJI-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa 11 inayolima pamba nchini wahakikishe wanasimamia vizuri wakulima wa zao hilo ili kuongeza uzalishaji na kuwaletea tija wananchi.

Agizo hilo limetolewa leo (Jumanne, Septemba 26, 2017) na Waziri Mkuu wakati akizungumza na wakuu hao wa mikoa kwenye kikao alichokitiisha mjini Dar es Salaam kujadili maendeleo ya zao hilo.Kikao hicho ni muendelezo wa kikao alichokitiisha mjini Dodoma (Ijumaa, Septemba 8, 2017) kujadili mbinu za kufufua zao hilo.Wakuu wa mikoa walioitwa kwenye kikao hicho ni kutoka mikoa ya Shinyanga, Singida, Kagera, Tabora, Morogoro, Mara, Mwanza, Simiyu, Katavi, Kigoma na Geita.

Waziri Mkuu amesema katika kipindi hiki ambacho msimu wa maandalizi ya kilimo cha pamba umeanza ni vema kwa Maofisa Kilimo na Wagani wakawasimamia wakulima kwa ukaribu ili wahakikishe wanafuata mbinu bora za kilimo.Amesema iwapo wakulima watapata usimamizi mzuri kutoka kwa Maofisa Ugani waliopo kwenye maeneo yao kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba yao itawasaidia katika kuongeza tija, kwenye uzalishaji wao.

“Serikali inawataka Maofisa Kilimo na Wagani wawasimamie wakulima kuanzia maandalizi ya shamba, kupanda, matumizi ya pembejeo na dawa, kuvuna na kutafuta masoko ili kilimo cha zao hilo kiweze kuwaongezea tija.”

Amesema Maafisa Kilimo wote walioko kwenye kila Halmashauri ni lazima wahusike kikamilifu katika kuwaelekeza wakulima namna ya kutumia mbinu bora za kilimo ili waweze kupata mazao mengi , hivyo kujikwamua kiuchumi.Pia Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Vyuo vya Kilimo nchini wahakikisha wanakuwa na mashamba darasa yatakayotumika na wakulima na wanafunzi wao kujifunza mbinu bora za kilimo kwa vitendo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba; Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI; Bw. Suleiman Jafo, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Kilimo, Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dkt. Tito Haule na Mkurugenzi Uhamasishaji Mazao, Bw. Twahir Nzallawahe.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMANNE, SEPTEMBA 26, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa inayolima zao Pamba kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 26, 2017.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

JAFO AAGIZA MAAMUZI YA HARAKA YA UPANUZI WA HOSPITALI YA TUMBI

0
0
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi ameutaka Uongozi wa Shirika la Elimu Kibaha na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani kukaa pamoja na kufanya Maamuzi ya haraka ndani ya wiki moja wafikie makubaliano ya uendelezaji wa ujenzi wa jengo jipya la upanuzi wa hospital ya Tumbi ambayo ni hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani.

Jafo ameoneshwa kukerwa na ugoigoi wa kufanya maamuzi unaoendelea licha ya serikali kupeleka fedha kiasi cha sh.milioni 685 katika mwaka wa fedha 2016/2017 lakini mpaka sasa wameshindwa kufanya Maamuzi.

Naibu Waziri Jafo amesema kitendo hicho kinachelewesha kuwapatia huduma bora wananchi.Kutokana na hali hiyo, Jafo amewaonya watendaji hao na kuagiza hadi wiki ijayo wawe wamekamilisha mkataba wa makubaliano na ujenzi uanze mara moja.

Upanuzi wa hospitali ya Tumbi unalenga kuimarisha miundombinu ili hospitali hiyo iweze kutoa huduma bora kwa wananchi mbalimbali wa mkoa wa pwani na mikoa mingine hapa nchini kwani kwa muda mrefu hospitali hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa wengi kwa siku ikihusisha pia majeruhi wengi wanao pata ajali katika barabara ya Morogoro.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maagizo kwa uongozi wa mkoa wa Pwani na watendaji wakuu wa Shirika la Elimu Kibaha ambao Hospitali ya Tumbi ipo chini yao.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ramani ya upanuzi wa jengo la hospitali ya Tumbi Kibaha.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akimsalimiana na mgonjwa ambaye ni mlemavu wa viungo katika Hospitali ya Tumbi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo kutoka kwa mganga mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Tumbi iliyopo mkoani Pwani.

WADAU KUKUTANA KUJADILI KANUNI ZA MAUDHUI YA UTANGAZAJI NA MITANDAO YA KIJAMII

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images