Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1924 | 1925 | (Page 1926) | 1927 | 1928 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika Kituo cha Forodha Bandarini, kilichoko katika Bandari ya Dar es Salaam na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, kufanya mabadiliko makubwa ya watumishi walioko katika idara ya upimaji na ukaguzi wa mizigo baada ya kubainika kuwa baadhi yao wanajihusisha kwa namna moja au nyingine na upotevu wa mapato ya Serikali.

  Dokta Mpango ametoa muda wa siku saba kwa TRA kumpa taarifa kamili ya utekelezaji wa maagizo hayo, ikiwemo kuwahamisha watumishi wote waliokaa muda mrefu kwenye eneo hilo la upimaji na ukaguzi wa mizigo ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya Serikali katika Bandari hiyo.

  Ameshangazwa na kitendo cha Mapato katika Bandari ya Dar es Salaam kutoongezeka licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, kuboresha Bandari hiyo kutokana na baadhi ya watumishi wasio waaminifu kushirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa kodi ya serikali.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) akiwa katika kikao na Maafisa Waandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) alipofanya ziara ya kukagua utendaji ambapo aliwataka kuchukua hatua dhidi ya watumishi wasiowaaminifu wanaolikosesha Taifa mapato stahiki.
  Meneja wa Idara ya Forodha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bandari ya dar es Salaam, Bw. John Micah (kulia) na Meneja anaye husika na suala la Mafuta Bw. Stephen Malekano (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani) alipofanya ziara Idara ya Forodha, Bandarini, Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Maafisa waandamizi wa Mamlaka ya mapato Tanzania-TRA, alipofanya ziara ya kushitukiza bandari ya Dar es Salaam na kuagiza kitengo cha ukaguzi na upimaji wa mizigo bandarini kifumuliwe baada ya watumishi wake kutofanyakazi ya kukusanya mapato ya Serikali ipasavyo
  Afisa Kitengo cha Bandari Majahazi, Bw. Mahmood Makame, akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) kuhusu changamoto ya elimu kuhusu masuala ya kodi kwa wateja wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam, alipofanya ziara ya kushitukiza katika ofisi hiyo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).


  0 0

  04 AUGUST 1930 – 22 SEPTEMBER 2009

  Days, weeks, months and years came and gone. It is now 8 years since you left us, desolate and bereft. Mama your bountiful, unconditional and unwavering Love and support to your husband, children, grandchildren and family members gardened you unprecedented admiration from the Marealle and Lyimo Clans, then and always! You left a foot print in this earthly world of ours. We loved you Mama, and will forever Love You.

  Rest in Eternal Bliss Mama.

  0 0
  0 0


  0 0

  WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage Septemba 9, 2017 alifungua tawi la Kiwanda cha mabati ALAF katika mkoa wa Dodoma eneo la Kizota kitalu namba 148.

  Kufunguliwa kwa tawi hili katika mkoa wa Dodoma ni kutokana na maamuzi ya serikali  kuamia makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kwa vitendo  na  kuunga mkono kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais John Magufuli katika“ USHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA TAIFA”.

  Kufunguliwa kwa tawi hili  kutaimarisha maendeleo ya mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani.

  Wateja kutoka Dodoma na Singida  sasa wataweza  kupata suluhisho la mahitaji ya bidhaa za uezekaji kutola ALAF.

  Tunauza  bidhaa zilizo tayari kwa matumizi kulingana na mahitaji ya mteja hasa mabati ya rangi  pamoja na kutoa ushauri wa kiufundi na kiutaalamu.

  Kwa sasa kiwanda chetu cha ALAF kina matawi manne Mbeya, Mwanza, Arusha na Dodoma.

  Kuhusu kampuni ya ALAF
  Kampuni ya ALAF ni sehemu ya kampuni ziliyoko chini ya Kampuni   ya SAFAL, kampuni inayoongoza bila mpinzani ktika utoaji wa bidhaa bora za uezekaji barani Afrika.Kampuni ya SAFAL inaendesha shughuli zake katika nchi 13 kuanzia mashariki,kati na kusini mwa bara la Afrika.

  Tukiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 50 katika biashara, ALAF tunaongoza  katika uzalishaji  wa bidhaa za  uezekaji za chuma.Katika kuongezea bidhaa zake za upauaji, bidhaa za kitaalamu pia zinauzwa na ALAF kama misumari (fixtite fastener), steel pipes, na Hollow section pamoja na viambatanisho muhimu kwa uezekaji.

  Baadhi ya bidhaa zinazotolewa na ALAF ni Lifestile, Romantile, Versatile, Tekdek (It5), Resincot na Simba Dumu.
  Wasilana nasi kwa namba hizi  Dar es Salaam- O768 555 560, Arusha - 0763 707 071, Mbeya - 0765 555 560,  Dodoma - 0764 131442  na Mwanza 0682 808 080. 


  Tunapatikana pia kuitia mitandao ya kijamii Facebook -Alaf Limited na Instagram - Alaf Limited


  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage akifungua tawi la kampuni ya mabati ya ALAF  Dodoma. Kushoto ni meneja mkuu Upauaji  (roofing) wa Kampuni ya mabati  ALAF, Dipti Mohanty  akishuhudia ufunguzi huo.

  0 0


  KITUO cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC kimezinduwa mradi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, yaani Kinondoni na Ubungo.

  Akizungumza na wadau wa mradi huo yaani baadhi ya wasaidizi wa sheria, maofisa ustawi wa jamii, wanasheria, mahakimu, Askari Polisi Dawati la Jinsia, maofisa watendaji wa mitaa kutoka wilaya za Kinondoni na Ubungo, Mwenyekiti wa CRC, Saida Mukhi aliwataka wadau hao kushirikiana ili kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinakomeshwa na kupungua.

  Alisema lengo la mradi huo unaofadhiliwa na shirika la Legal Service Facilities (LSF) ni kuhimarisha zaidi upatikanaji wa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. Aliongeza kuwa mradi huo utajikita zaidi katika utoaji wa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa waathirika na kuhakikisha mfumo wa upatikanaji wa haki unafanya kazi vizuri.

  “…wadau katika maeneo hayo mnatakiwa kuhakikisha tunapinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vinaweza kusababisha madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii, ikiwa ni pamoja na wahusika kunyimwa uhuru,” alisema Bi. Saida Mukhi akifungua warsha ya wadau hao.

  Kwa upande wake, Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo akifafanua zaidi kwa washiriki wa semina hiyo alisema mradi huo utaendeshwa katika Kata za Makumbusho na Kawe kwa Wilaya ya Kinondoni huku kwa Wilaya ya Ubungo utajikita kwenye Kata ya Saranga.

  Alisema CRC itashirikiana na wadau katika maeneo hayo kuhakikisha inapiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo mara nyingi vimekuwa na madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii na mara nyingine kuwanyima uhuru.
  Mwenyekiti wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Saida Mukhi akizungumza na washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni na Ubungo. Kulia ni Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo.Mwenyekiti wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Saida Mukhi (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
  Ofisa Mradi wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Suzan Charles akitoa ufafanua juu ya mradi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam.Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi akichangia mada.


  0 0

  Familia ya Alhaj Sudi Suleiman Madega, Katibu Mkuu (Mst) Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU).

  Inapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa msaada wa hali, mali na faraja walioipatia familia katika kipindi kigumu cha kuuguza, msiba na hatimaye kumpuzisha kwenye nyumba yake ya milele mpendwa wao Hajat Mwalimu Batoul Abdallah Mbarouk aliyefariki tarehe 16 Agosti, 2017 na kuzikwa tarehe 17 Agosti, 2017. 

  Hajat Batoul A. Mbarouk alikuwa Mke wa Sudi S. Madega; na Mama wa Suleiman, Amir, Dr. issa, Maryam, Zuhura na Asha Madega. Pia, Mkwe wa Maryam Hamza Chum, Nuru Kassim Kisesa, Daud Buswelo na Hawa Kadyanji.

  Kwa kuwa ni ngumu kumshukuru kila mmoja, itoshe kusema ahsanteni sana nyote. Hata hivyo, kipekee familia inapenda kufikisha salamu maalum kwa wafuatao:-

               i.        Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wa Taasisi ya Saratani Ya Ocean Road ambako marehemu alikuwa akitibiwa tangu mwaka huu mwanzoni na hatimaye kuaga dunia tarehe 16 Agosti, 2017. Hususa, Dr. Steve, Dr. Kezia , Dr. Mathew, Dr. Chacha, Dr. Ruta  Dr. Abdi Sangali , Sister Sapine,  Sister Wema , Sister Ester , Sister Doris , Sister Kimath , Sister Eliza , Joel Makanyaga, Mkulia, Alawi, Solomon na wengine wote;

              ii.        Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako marehemu alikuwa akitibiwa tangu mwezi Agosti, 2016;

             iii.        Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais (Mst) wa Jamhuri Muungano wa Tanzania na mkewe Mh. Mwl. Salma Rashid Kikwete (Mb) na familia yao;

            iv.        Katibu Mkuu, Uongozi na Wafanyakazi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU);

              v.        Katibu Mkuu, Uongozi na Wafanyakazi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT). Hususan, Makao Makuu, Mkoa wa Dar es Salaam, Mkoa wa Pwani na Walimu wote;

            vi.        Mh. Jaji (Mst) Harold R. Nsekela (Kamishna wa Maadili), Uongozi na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

           vii.        Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndg. Kailima Ramadhani na Mkurugenzi wa Utawala Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndg. Hamis A. Mkunga;

          viii.        Alhaji Masoud Msangi, Mkurugenzi Mtendaji Nduvini Auto Works;

            ix.        Majirani wa marehemu wa Mbagala, Mbezi na Chang’ombe;

              x.        Vile vile, tunapenda kutambua familia zifuatazo:-

  Ukoo wa Kanyama na Mbarouk popote pale walipo, Familia ya Mh. Luteni (Mst) Abdallah Kihato, familia ya Mh. Mohamed S. Jegame, familia ya Marehemu Balozi Isaya Bakari Chialo, familia ya Dr. Hamza Juma Chum, familia ya Brigedia Jenerali (Mst) Ussi Khamis wa Zanzibar, familia ya Kassim Kisesa, familia ya Masoud Sultan, familia ya Bakari O. Sangali, familia ya Issa Sechonge, familia ya Kisarazo, familia ya Idris Mavura, familia ya Marehemu Mwl. Hemed Ally Kimeah, familia ya Mbaruku Nguzo, familia ya Mbegu na wengine wote.


  Pamoja na salamu hizi, familia inawaarifu na kuwaalika rasmi katika Arobaini ya Marehemu Mwalimu Mbarouk itakayofanyika nyumbani kwake Mbagala siku ya jumapili tarehe 24 Septemba, 2017 kuanzia saa 5 asubuhi mpaka 8 mchana.


  Kwa mawasiliano tafadhali wasiliana na Ndg. Amir Sudi Madega kupitia Namba 0716875737.


  Innalilahi Wainailahi Rajioun,

  Ahsanteni Sana


  0 0

  Mwanamuziki nguli wa miondoko ya Bongo Fleva nchini Ali Kiba amesema moja ya mafanikio anayojivunia nayo katika kazi ya muziki kwa mwaka huu ni ushiriki wake tena katika onyesho la Coke Studio msimu wa mwaka huu. Ali Kiba ambaye amefanya kolabo kwa kushirikiana na mwanamuziki nguli kutoka Nigeria, Patoranking, amesema katika mahojiano hivi karibuni kuwa anajivunia kuwa miongoni mwa wanamuziki wanaoshiriki kwenye msimu wa tano wa Coke Studio unaoendela ambapo kwa hapa nchini onyesho lake linarushwa na luninga ya Clouds kila Jumamosi saa 12 jioni. 

   Anasema ushiriki wake kwa mara ya moja ya kwenye mafanikio kwani rekodi yake imezidi kuongezeka katika anga la kimataifa na ameweza kujiongezea washabiki ambao wanafuatilia shindano hili kupitia luninga,vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Mbali na kuongelea mafanikio ya kupata washabiki amesema kuwa amefurahi kufanya kolabo na msanii wa nje ya nchi kwa kuwa ameweza kujifunza mengi kupitia ushiriki wake kwenye Coke Studio.
  “Jambo lingine ambalo naliona ni kubwa kama msanii ni kukubalika kufanya kazi na kampuni kubwa kama Coca Cola kazi hii imenifanya nizidi kujiongezea mashabiki na umaarufu wangu kuongezeka”Alisema. Alisema onyesho la Coke Studio linadhihirisha kuwa muziki wa Bongo Fleva unazidi kukua na kuwa maarufu sehemu mbalimbali barani Afrika kutokana na jinsi linavyofuatiliwa na idadi kubwa ya watu hususani vijana. 

   Aliwataka wanamuziki wachanga wanaochipukia kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanapata mafanikio na kuongeza kuwa mafanikio yanapatikana kwa kufanya kazi na makampuni makubwa ya biashara mojawapo ikiwa ni kushiriki kwenye maonyesho makubwa kama haya. “Fani ya muziki inazidi kukua kiasi kwamba wakati wa kufanya muziki wa ndani tu imekwisha na inabidi kuvuka mipaka na kolabo kama hizi za Coke Studio zinasaidia kupata uzoefu na kufungua milango ya mafanikio”.Alisema. Alimalizia kwa kuwapongeza wanamuziki wenzake kutoka Tanzania ambao yuko nao katika msimu wa Coke Studio mwaka huu.Wanamuziki hao ni , Rayvanny, Izzo Bizness, na Nandy.

  0 0

  Ujumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ukiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bibi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga wamefanya ziara katika migodi ya Mpipiti pamoja na Sekenke iliyopo katika Wilaya ya Singida vijijini na Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.

  Dhumuni ni ziara hiyo ni kujifunza na kuangalia kwa ukaribu jinsi Wachimbaji hao wanavyofanya shughuli zao za kila siku hususan katika suala zima la mazingira. Wakiwa aktika ziara hiyo waliongea na Viongozi wa Wachimbaji hao wadogo na kujionea shughuli hizo za uchimbaji katika migodi hiyo zinavyokwenda. Viongozi hao wa Wachimbaji walitoa changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika uchimbaji ikiwemo miundombinu mibovu , umeme na garama za ukodishaji wa mashine za kuvutia maji(pampu) na kompresa.

  Kabla ya kuanza ziara hiyo ujumbe huo ulipata nafasi ya kumtembelea Katibu YTawala wa Moa wa Singida Dkt. Angela Mageni Lutandula Ofisini kwake na kujitambulisha na kumweleza dhumuni la safari yao mkoani humo. Akiongea Katibu Tawala aliwakaribisha Wajumbe hao mkoani Singida na kuwasititiza wakajionee wao wenyewe shughuli hizo za uChimbaji wa madini kwa Wachimbaji wadogowadogo mkoani kwake.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi (katikati) akiongea na ujumbe wa Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais walipomtembelea Ofisini kwake kwenda kujitambulisha kabla ya kuanza ziara ya kutembelea Wachimbaji wadogo wadogo katik Mkoa wa Singida.
  Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji (katikati) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga(wa mwisho kushoto) toka Ofisi ya Makamu wa Rais wakipata maelezo jinsi Wachimbaji wadogo wanavyoingia kwenye mashimo kwa kutumia kamba kutoka kwa Kiongozi wa Mgodi wa Wachimbaji wadogo wa Mpipiti katika Wilaya ya Singida Vijijini Bwana Geston Ali.
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga akiangalia jinsi dhahabu inavyochujwa kutolewa katika udongo kwa kutumia maji katika mgodi mdogo wa Mpipiti uliopo wilaya ya Singida Vijijini.
  Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji (katikati) , Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga pamoja na Afisa Afya Mazingira Bi Suzan Nchala wakionyeshwa na Bwana Athman Mrisho (Mkurugenzi wa mgodi) jiwe linakuwa kabla ya kuingizwa kwenye mashine kwa kuvunjwavunjwa katika mgodi mdogo wa Sekenke wilayani Iramba mkoani Singida.

  0 0

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kufikisha huduma za mawasiliano kwenye vijijini vyote nchi nzima na maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara ili kuchochea ukuaji wa uchumi na utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi wote, kwa wakati, uhakika na muda wote.

  Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga wakati wa ziara iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia UCSAF ya kuwapeleka wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kukagua maendeleo ya ujenzi wa minara ya simu za mkononi, hali ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi na changamoto zilizopo kwa wananchi wa maeneo husika. Wakiwa kwenye ziara hiyo kata ya Jipe iliyopo Wilaya ya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro Eng.

   Ulanga amesema kuwa mnara wa Vodacom uliojengwa kwenye eneo hilo unahudumia zaidi ya wananchi 1,200 kwenye vijiji zaidi ya nane. Hadi hivi sasa UCSAF imejenga minara ya simu za mkononi kwenye maeneo saba yaliyopo Wilaya ya Mwanga na Same mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na kampuni za simu za mkononi. Vile vile, Kamati imetembelea minara iliyopo kata ya Nkalamo iliyopo Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

  Eng. Ulanga ameongeza kuwa Serikali kupitia UCSAF inaendelea kutoa ruzuku kwa kampuni za simu za mkononi ili ziweze kufikisha mawasiliano kwenye vijiji vyote nchi nzima ambapo hadi hivi sasa UCSAF imetoa jumla ya dola za marekani milioni 41.5 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 93.3 kwa ajili ya kufikisha huduma za mawasiliano vijijini kwenye kata 518 ambazo zitajengwa minara ya mawasiliano. Mpaka sasa jumla ya kata 391 kati ya kata 518 zimefikishiwa huduma ya mawasiliano katika kipindi cha miaka minne kuanzia mwezi Machi 2013 mpaka mwezi Agosti 2017 mwaka huu.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa alipofanya ziara ya mawasiliano vijijini kwenye Wilaya ya Bahi, Chamwino mkoani Dodoma na Gairo kwenye mkoa wa Morogoro, ameziagiza kampuni za simu kuhakikisha kuwa huduma za mawasiliano vijijini zinapatikana masaa yote 24, siku saba za wiki na katika kipindi cha mwaka mzima bila kukatika, kwa uhakika na kwa wakati wote. 

  Hali ya ukosefu wa mawasiliano kwa nyakati za usiku imekuwa ikijitokeza kwenye baadhi ya maeneo ya vijijini ambako hakuna nishati ya uhakika ya umeme ambapo kampuni za simu zinatumia umeme wa jua kuendesha minara ili iweze kutoa mawasiliano kwa wananchi.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigalla King (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha Kweinsewa kilichopo kata ya Nkolamo, wilaya ya Korogwe Vijijini mkoani Tanga wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua ujenzi wa minara na upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwenye vijiji.
  Bibi Mwanafuraha Nyange, mkazi wa kijiji cha ziwa Jipe kilichopo Kata ya Jipe wilaya ya Mwanga kwenye mkoa wa Kilimanjaro akieleza umuhimu wa mawasiliano vijijini kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara yao ya kukagua ufikishaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini.
  Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu na wakazi wa kijiji cha ziwa Jipe kilichopo wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Norman Sigalla King.


  0 0  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella, akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mapema jana mjini Tanga. PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG - TANGA. 

   Vifaa vilivyotolewa na wasanii na wachezaji hao katika uwanja wa Tangamano ikiwa ni Kampeni ya Uzalendo kwanza ni pamoja na Ultra Sound, mashine ya X- Ray, Wheel Chair, Magongo ya walemavu na craches. Shigella amepokea vifaa hivyo ikiwa ni moja ya Kampeni ya UZALENDO KWANZA ambayo inaongozwa na wasanii na wacheza mpira ikiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuchangia maendeleo ya nchi. Ambapo vifaa hivyo vinagawiwa katika hospitali za Ngamiani, Makorola, Pongwe na Mikanjuni.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella, akitokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Mwenyekiti wa UZALENDO KWANZA, Steve Nyerere wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Manno mjini Tanga.
  Vijana wazalendo wa UZALENDO KWANZA wakibeba vifaa Tiba ambavyo walitoa kwa ajili ya hospitali za mkoa wa Tanga.


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack amezindua kampeni ya upandaji miti katika wilaya ya Shinyanga yenye kauli mbiu ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ ili kuboresha mazingira Shinyanga na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha jangwa. 

  Kampeni hiyo inayoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, imezinduliwa leo Jumamosi Septemba 23,2017 katika manispaa ya Shinyanga ,kwa lengo la kuboresha mazingira ya mji wa Shinyanga,maeneo ya taasisi,maeneo ya wazi,maeneo yanayozunguka kaya,kandokando ya barabara na sehemu zingine ambazo hazina miti. 

  Akizungumza wakati wa kuzindua kampeni hiyo,Telack alisema kutokana na mvua haba katika mkoa wa Shinyanga, kumekuwepo na mabadiliko ya tabia nchi hali inayosababisha kuwepo na hali ya jangwa. Telack aliwataka wananchi na wadau wote kuhakikisha wanatunza miti hiyo na kuzuia mifugo kuzurura ovyo mitaani. 

  “Tutakuwa wakali,kuanzia sasa ni marufuku kwa mifugo kuzurura mitaani,ikikamatwa kwa kila mfugo faini ni kati ya shilingi 50,000/= na 100,000/=,iwe ng’ombe,mbuzi,kondoo au punda, tukikuta mti umekauka faini ni shilingi 50,000/=”,alieleza mkuu huyo wa mkoa. 
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizungumza wakati wa kuzindua kampeni ya upandaji miti ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ leo katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga.Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi.
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro wakati wa uzinduzi huo. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya upandaji miti ambapo alisema miongoni mwa malengo yake ni kuhifadhi ardhi na kuiongezea thamani,kuzuia mmomonyoko wa adhi na kuboresha mazingira
  Wananchi wakiwa wameshikilia vijiti vinavyotumika katika zoezi la upandaji miti.
  Uzinduzi unaendelea
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akichomeka vijiti kwenye mti aliopanda.


  0 0

  Kikao cha Baraza la wafanyabiashara wilaya ya kigoma kilichofanyika  jana ambacho kilikuwa kikao maalum cha madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na halmashauri ya wilaya ya kigoma mkoani kigoma, wakisikiliza ajenda mbalimbali zinazowasirishwa na baraza hilo na namna ya kutumia fursa ya mradi wa ( LIC) unaolenga kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara kwa wafanyabiashara wadogo,kati na wakubwa ili kukuza uchumi katika sekta ya viwanda mkoani humo.Picha na Magreth Magosso Kigoma.

  0 0


  Wakati serikali ikishirikiana na wahisani mbalimbali wa afya katika kuondoa changamoto ya ugonjwa wa malaria unaoenezwa na Mmbu jike aitwaye anofeles,  baadhi ya wakazi wa Manispaa ya kigoma ujiji wamekuwa wakitumia vyandarua  kuhifadhi vifaranga vya kuku ili wasiliwe na mwewe,picha kama ambavyo imenaswa na mpiga picha wetu Magreth Magosso kigoma Chandarua kikitumika kuwalinda Vifaranga hao wasiliwe na Mwewe,kimsingi Elimu bado inahitajika kwa jamii katika suala zima la matumizi bora na sahihi ya Vyandarua katika suala zima la kupambana na ugonjwa wa Malaria. 

  0 0

  Globu ya Jamii inampongeza Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brig Gen Emmanuel Maganga na mkewe Mama Love Maganga kwa binti yao Asteria kuwa mmoja wa maafisa wapya 422 waliotunukiwa Kamisheni leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Hongereni sana familia ya Maganga

  0 0

  BAADA  ya kupata pointi 4 ugenini Yanga yarudi kwa kasi na kufanikiwa kunyakuwa pointi tatu ikiwa nyumbani kwa kuifunga Ndanda ya Mtwara goli 1-0.

  Yanga wakiwa nyumbani waliweza kumiliki mpira kwa dakika zote 45 za kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Ibrahim Ajib dakika ya 35.

  Kutokana na matokeo ya leo Yanga wanakuwa sawa na Simba kwa pointi wakitofautiana kwa magoli ya kufunga.

  Kwa upande wa kocha msaidizi wa Yanga, Shedrack Nsajigwa amesema watafanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza licha ya kupata pointi 3.

  Nae kocha msaidizi wa Ndanda Musa Mbaya amesema kushindwa kwao leo ni kutokana na ugeni wa wachezaji ambao wameingia kwenye kikosi chao na kupelekea kutoweka muunganiko mzuri hivyo makosa hayo  watayafanyia kazi mapungufu hususani kwenye upande wa ushambuliaji.
   Mshambuliani wa Timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu, akiachia shuti kali kueleka langoni mwa timu ya Ndanda "Wanakuchele", katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyochezwa jioni ya leo kwenye dimba la Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 1-0.
   Mabeki wa timu ya Ndanda, wakimdhibiti vilivyo, mshambuliani wa timu ya Yanga, Obrey Chirwa katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyochezwa jioni ya leo kwenye dimba la Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 1-0.


  0 0  aru1
  aru2
  IMGS0864
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride  katika sherehe ya kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya 422 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017. (PICHA NA IKULU)
  IMGS0869
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride  katika sherehe ya kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya 422 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017
  Picha na IKULU
  IMGS0943
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na jukwaa kuu katika sherehe ya kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya 422 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017
  IMGS0945IMGS1062
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 422 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017
  IMGS1065
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 422 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017
  IMGS1305
  Sehemu ya umati wa maelfu ya wananchi ukimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania an Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017
  IMGS1361
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania an Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017
  IMGS1586IMGS1604
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na madiwani na waliowahi kuwa madiwani wa CHADEMA walioamua kuhamia CCM wakati wa sherehe za kukamisheni maafisa wapya wa kijeshi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017


  0 0

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wakicheza pamoja na wasanii wa kikundi cha Ngoma cha Wasonjo kutoka Ngorongoro, wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. Picha na Muhidin Sufiani
  Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Masebe Rungwe, wakicheza jukwaani wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. Picha na Muhidin Sufiani
  Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Kanengwa, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. Picha na Muhidin Sufiani
  Wasanii wa Kikundi cha Ngoma cha Lipango Mbozi Mkoa wa Songwe, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, jana Sep 22, 2017. Picha na Muhidin Sufiani
  Majaji wa shindano la ngoma Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, wakifuatilia burudani zilizokuwa zikiendelea jukwaani wakati wa Tamasha hilo kwenye Uwanja wa Tandale, Tukuyu. Picha na Muhidin Sufiani
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kulia) akiwaongoza baadhi ya viongozi na wadau kucheza Kwaito jukwaani wakati wa Tamasha hilo. Picha na Muhidin Sufiani.


  0 0

  Wachimbaji wadogo wa migodi wametakiwa kutunza mazingira katika maeneo yote yanayozunguka migodi pamoja na usalama kwa Wafanyakazi katika katika migodi hiyo. Rai hiyo imetolewa na ujumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ulipotembelea mgodi wa Igulubi ulioko katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora katika ziara inayofanywa na Ujumbe huo wa kutembelea migodi ya Wachimbaji wadogo. 

  Wakiongea katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji na Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Bi Magadalena Mtenga walisema kuwa utunzaji wa mazingira ni kitu cha muhimu sana na pia usalama kwa Wafanayakazi katika migodi hiyo ni muhimu pia. Walimshauri Mkurugenzi wa mgodi huo Bwana Steven Siame kuwa karibu na Taasisi za Serikali ili kuweza kufahamu mambo yote yanayotakiwa katika suala zima la uchimbaji ikiwemo Baraza la Usimamizi wa Mazingira kwa ajili ya kujua kanuni za utunzaji wa mazingira.

  Ujumbe huo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais upo katika ziara ya kutembelea migodi midogo inayomilikiwa na Wachimbaji wadogo kwa ajili ya kujifunza na kuona shughuli hizo za Uchimbaji zinavyofanyika katika migodi hiyo likiwemo na suala la utunzaji wa Mazingira kwa ujumla. 
   Mkurugenzi  wa sera na Mipango toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga wakiangalia mashine  ya kuingia shimoni inayotumiwa na Wachimbaji wadogo wa mgodi wa Igulubi ulioko katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

   Mkurugenzi wa sera na Mipango toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga wakionyeshwa na Afisa madini kanda ya Taabora Injinia Kasweke aina za mawe  yenye dhahabu yanayopatikana katika Mgodi mdogo wa Igulubi wilayani Igunga mkoa wa Tabora.

    Mkurugenzi wa sera na Mipango toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga na Afisa Mazingira Bi Suzan Nchala wakiangalia sehemu ambapo mawe yaliyopondwa husafishwa ili kupata dhahabu walipotembelea mgodi wa Igulubi wilayani Tabora.

  Mmiliki wa mgodi mdogo wa Igulubi Bwana Steven Siyame akiwaonyesha wajumbe toka Ofisi ya Makamu wa Rais waliofanya ziara katika mgodi huo uliopo Igunga Tabora jinsi mashine ya kuvunjia mawe inavyofanya kazi( haipo pichani).

older | 1 | .... | 1924 | 1925 | (Page 1926) | 1927 | 1928 | .... | 3272 | newer