Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1923 | 1924 | (Page 1925) | 1926 | 1927 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Mjumbe wa baraza la Ulamaa BAKWATA taifa, ambaye pia ni Imamu Mkuu wa Msikiti wa Manyema jijini Dar es salaam, Sheikh Hamid Jongo akizungumza na wanafunzi, walimu na wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Vuchama iliyopo Ugweno, Mwanga Mkoani Kilimanjaro, katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne.
  Meneja wa shule ya sekondari ya Vuchama, Alhaj Yusuph Mfinanga, akizungumza na wanafunzi, walimu na wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Vuchama iliyopo Ugweno, Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
  Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Vuchama, Mwalimu Juma A. Juma akizungumza na wanafunzi, walimu na wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Vuchama iliyopo Ugweno, Mwanga Mkoani Kilimanjaro,katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne.

  Na Mwamvua Mwinyi, Kilimanjaro

  MJUMBE wa baraza la Ulamaa(BAKWATA)Taifa,ambae pia ni Imamu mkuu wa msikiti wa Manyema jijini Dar es salaam, Sheikh Hamid Jongo, amewataka wanafunzi wa shule za taasisi za kielimu za kidini kusoma kwa bidii na kuwa watiifu badala ya kuwa wajeuri na mafedhuri.

  Ameeleza watoto wanapaswa kujipanga kitaaluma ya ahera na kidunia ili kukua katika misingi iliyo na maadili mema ya kidini na kitaifa. Aidha sheikh Jongo,ameziasa taasisi hizo waache kufundisha uhasi bali zijiongeze,kubuni mbinu mbadala zitakazowezesha kwenda pamoja na ushindani wa kitaaluma kwa lengo la kufaulisha hasa kidato cha nne na cha sita pasipo kushika mkia.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Efm redio imewafikia wakazi wa Kinondoni siku ya leo ya tarehe 22/09/2017, kwa kupitia tamasha lake la Njendani lililofanyika katika uwanja wa Biafra – Kinondoni, ambapo watangazaji wa Kipindi cha Joto la Asubuhi, sports HQ, Uhondo na Ladha 3600 wakitangaza moja kwa moja katika kiwanja hicho pamoja na burudani mbalimbali za muziki ikiambapata na kampeni ya kuchangia damu ilioongozwa na Mpango wa Damu salama katika kuokoa maisha ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo.
  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mheshimiwa Ally Hapi (wa kwanza kulia) akiongea live na wakazi wake kupitia kipindi cha Joto la Asubuhi – Uwanja wa Biafra.
  Mtangazaji wa Kipindi cha sports HQ, akizungumza na wakazi wa Kinondoni wakichambua michezo kwa pamoja.
  Rdj x5 wa kipindi cha Sports Headquarters akifanya yake Biafra.
  Sehemu ya mashabiki wakishuhudia matangazo hayo moja kwa moja.


  0 0


  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Philip Mpango akizungumza na wageni waalikwa jana katika hafla ya uzinduzi rasmi wa uuzaji hisa za Maendeleo Bank PLC uliofanyika jijini Dar esSalaam.

  Wakati Maendeleo Bank ikiwa ni taasisi ya nane ya fedha kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Serikali imesema asilimia 60 ya miamala ya fedha nchini haipiti kwenye mifumo rasmi.


  Hivyo, benki na taasisi za fedha zimetakiwa kuongeza ubunifu ili sekta hiyo iweze kuchochea maendeleo ya uchumi. Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa hisa za Maendeleo Bank PLC na kwamba, kwa sasa ni asilimia 40 tu ya miamala ya fedha hupita katika mifumo rasmi.


  Maendeleo Bank inakuwa benki ya kwanza kuhitimu kutoka dirisha la ukuzaji mashirika machanga (Enterprise Growth Market) na mwaka 2016 ilipata tuzo ya kampuni bora katika makampuni yanayokua kutoka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).


  Dk. Mpango alisema sekta ya benki ni muhimu katika kukuza uchumi na kwamba, kupitia huduma za fedha kwa kutumia simu za mikononi, Tanzania ni kati ya nchi zinzoongoza Afrika kwa kusogeza karibu huduma za kibenki kwa wananchi.. “Kwa hili Benki ya Maendeleo lazima muongeze ubunifu ili kuvutia wateja zaidi kutumia huduma zenu,” Dk. Mpango alitaka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuongeza nguvu ya kuelimisha jamii umuhimu wa umiliki wa hisa.


  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba alisema, tangu benki ianzishwe mwaka 2013 imekuwa namafanikio makubwa ikiwamo kuongeza matawi kufikia matatu.
  Mwangalaba alisema mwaka 2015, benki ilipata faida ya Sh. 175 milioni na mwaka 2016 iliongezeka na kufikia Sh. 555 milioni. Pia, kwa miaka minne imelipa kodi ya Sh. 2.42 bilioni.


  Ailongeza kuwa mwaka 201/16, benki ilipata kibali cha kuuza hisa stahili na ilikusanya zaidi ya Sh. 2.8 bilioni, hivyo kufikisha jumla ya Sh. 7.30 bilioni.“Leo tunashuhudia uzinduzi wa uuzaji wa hisa ukiwa na lengo la kuongeza mtaji kwa Sh. 15 bilioni, ambazo zitatumika kuimarisha shughuli za uendeshaji,” alisema.Tangu benki ianzishwe imefanikiwa kukusanya amana zaidi ya Sh. 39 milioni na kutoa mikopo zaidi ya Sh. 28.0 milioni. Pia, mali za benki zina thamani ya Sh. 49 bilioni.Mwangalaba alisema iwapo watafanikiwa kuuza hisa na kupata ntji wa Sh. 15 bilioni, wanatarajia kuimarisha utendaji wa benki hiyo kwa kiwango kikubwa. 


  Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Philip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa uuzaji hisa za Maendeleo Bank PLC. Pamoja nae kutoka kushoto ni Askofu Ambele Mwaipopo, Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Askofu Dk. Alex Malasusa, Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw. Ibrahim Mwangalaba na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo Bank Bw. Amulike Ngeliama. 

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza haja kwa Ofisi ya Mufti pamoja na viongozi wa misikiti ya kisasa inayojengwa hapa nchini kuwa na mikakati mizuri ya uendeshaji na uangalizi kwani baadhi ya misikiti hiyo iliyojengwa kwa gharama kubwa imekuwa ikipoteza haiba yake kutokana na uchakavu.


  Alhaj Dk. Shein alisema kuwa misikiti hiyo ya kisasa iliyojegwa kwa gharama kubwa imekuwa ikipoteza haiba na kukumbwa na chamgamoto ya uchakavu wa miundombinu muhimu baada ya kipindi kifupi tangu inapokabidhiwa kwa Kamati za Misikiti au wananchi wa maeneo yanayohusika.


  Hayo ameyasema leo katika  ufunguzi wa msikiti wa Jaamiu Zinjibar  ambapo katika  hotuba yake ya ufunguzi wa msikiti huo , Alhaj Dk. Shein alisisitiza kuwa kila inapowezekana ni vyema Ofisi ya Mufti ikawa na ufuatiliaji wa misikiti hiyo inayojengwa kwa gharama kubwa ili kuangalia utunzaji na maendeleo yake.


  Aliongeza kuwa miradi ya ujenzi wa misikiti inayojengwa na ikatunzwa vizuri na kwa uadilifu, huwa wanatiwa moyo wale wenye nia na ari ya kusaidia na kuzidi kufungua milango ya kheri, neema na riziki kwa Waislamu wa maeneo mengine ambao bado hawajafaidika na neema kama hiyo.


  Alhaj Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa shukurani za dhati kwa Serikali ya Oman kwa kukubali kujenga msikiti huo mkubwa, mzuri na wa kisasa hapa Zanzibar na kutoa shukurani kwa wananchi wa Oman chini ya uongozi imara wa Sultan Qaboos Bin Said Bin Al Said.


  Pia, Dk. Shein alimpongeza Balozi Mdogo wa Oman aliyopo Zanzibar Dk. Ahmed Hamoud Al Habsi na wasaidizi wake kwa juhudi walizochukua hadi mradi huo ukakamilika kwa ufanisi mkubwa kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.  Aidha, Alhaj Dk. Shein alisisitiza haja ya kuitumia misikiti ipasavyo na kujiepusha kufanya mambo yanayoweza yakawa shirki sambamba na kujiepusha na mizozo pamoja na mifarakano ambayo haina tija kwa Waislamu.


  Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa kwa bahati mbaya katika miaka ya hivi karibuni, kuna baadhi ya Waislamu katika baadhi ya misikiti walianza kugombania uongozi wa misikiti, walikuwepo waliotishia kuiteka misikiti kwa kuwa katika himaya yao na baadhi yao walifanya uharibifu wa vifaa na nyenzo.


  Aliongeza kuwa wapo waliodiriki kuwafukuza waumini wenzao na kugawana makundi ya waliokuwa na haki na wasiokuwa na haki ya kuongoza na wengine walipoanzisha mizozo yao walidiriki hadi kupigana na kuumizana kwani walighafilika juu ya umuhimu wa msikiti na mwenye msikiti.


  Alieleza imani yake ni kwamba msikiti huo wa Jaamiu Zinjibar utakuwa ni miongoni mwa kiungo muhimu cha kuwaunganisha Waislamu wa Zanzibar kutokana na jina uliopewa na kuwa kitovu muhimu katika kutekeleza ibada ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kukumbushana umuhimu wakutekeleza Hijja.


  Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein aliwahimiza wananchi na waumini wanapopata bahati ya kuwaleta wadhamini na wafadhili wa ujenzi wa misikiti na madrasa na uchimbaji wa visima, wawafikishe wafadhili hao katika sehemu za vijijini, Unguja na Pemba ili nao wazidi kupata neema hiyo kwani misikiti na madrasa nyingi za kisasa bado zinajengwa katika maeneo ya mjini ikilinganishwa na vijijini.


  Pia, Alhaj Dk. Shein alitoa wito kwa Waislamu wote washirikiane katika kujenga madrasa wao wenyewe badala ya kukaa na kusubiri wafadhili katika kutekeleza ibada hiyo muhimu huku akiwataka wazazi kuwa na moyo wa kushirikiana na walimu wa madrasa katika kusomesha na kuwalea watoto.


  Nae Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mmanga Mjengo Mjawiri alitoa pongezi kwa Serikali ya Falme ya Oman na hasa Sultan Qaboos  kwa msaada wa TZS Bilioni 17.9 ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechangia eneo la ujenzi, msamaha wa kodi wa vifaa vyote vya ujenzi vilivyotoka nje ya nchi na msamaha wa malipo ya mkandarasi sawa na TZS Bilioni 3.1.


  Mkataba wa ujenzi wa Msikiti huo ulitiwa saini tarehe 6 Januari mwaka 2014 baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyowakilishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Serikali ya Falme ya Oman iliyowakilishwa na Ofisi ya Diwan of Royal Cort ambapo ujenzi umefanywa na Kampuni ya Esteem Construction ya Dar-es-Salaam na kusimamiwa na Wahandisi wa Ofisi ya Diwan of Royal Cort ya Oman.


  Msikiti huo mkubwa una nafasi ya kusaliwa na Waislamu zaidi ya 4,000 na una sehemu ya kusali wanaume na wanawake, vyumba sita vya madarasa, maktaba, maabara ya lugha na kompyuta, ukumbi wa mihadhara ya shughuli za kidini pamoja na maegesho ya gari.


  Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo msikiti huo wa kisasa ambao unatarajiwa kuendesha ibada na pia kutoa mafunzo mbali mbali ya Dini ya Kiislamu na lugha mbali mbali ikiwemo lugha ya kiarabu.


  Mapema Mwakilishi wa Serikali ya Oman na Katibu Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos, Habib bin Mohammed Al Riyami alisema kuwa ujenzi wa msikiti huo ni njia moya wapo ya kujenga uhusiano na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Zanzibar na Oman na kuahidi kuwa Oman chini ya uongozi wa Mfalme Qaboos itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuendeleza sekta za maendeleo ikiwemo elimu pamoja na kuiimarisha dini ya Kiislamu.


  Mufti Mkuu wa Zanzibar Saleh Omar Kabi alieleza fadhila za kujenga msikiti pamoja na kuendeleza elimu ya dini ya Kiislamu na kusisitiza kuwa wananchi wa Oman wakiongozwa na Sultan Qaboos wameendelea kuonesha udugu wa damu kati yao na wananchi wa Zanzibar kama ilivyokuwa kwa Aus na Hazraj wakati wa Mtume Mohammad (SAW).


  Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Serikali ya Oman, Masheikh pamoja na wananchi walihudhuria katika ufunguzi wa msikiti huo akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Balozi Mdogo wa Oman Dk. Ahmed Hamoud Al Habsi na viongozi wengineo.


   Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar


  Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

   E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


  0 0

  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Septemba 23, mwaka huu kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja tofauti hapa nchini.

  Kesho Jumamosi Young Africans itacheza na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Mwadui ya Shinyanga katika mchezo utaofanyika Uwanja wa Mwadui.

  Mchezo mwingine, utakutanisha timu za Majimaji itakayokuwa mwenyeji wa Njombe Mji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Mechi zote hizo zitaanza saa 10.00 jioni.

  Jumapili Septemba 24, mwaka huu kutakuwa na michezo minne ambako Ruvu Shooting itaialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani huku Stand United ikicheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. Mechi hizo pia zitaanza saa 10.00 jioni.

  Michezo mingine itakuwa ni Singida United itakayoialika Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma saa 10.00 jioni kabla ya Azam kuialika Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi katika mchezo utakaoanza saa 1.00 jioni

  0 0  0 0

  Taarifa kwa Vyombo vya Habari

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa mwili wa marehemu Praiveti Mussa Jumanne Muryery ambaye ameuawa nchini DRC akiwa katika jukumu la Ulinzi wa Amani, utaagwa kwa heshima tarehe 25 Septemba 2017 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kuanzia saa 2:00 asubuhi. 

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa        Dkt.  Florens M. Turuka ataongoza katika kuuaga mwili wa Marehemu.
  Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi Amin.


  Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
  22 Septemba, 2017.

  0 0

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limemkamata mwanamke mwengine akiwa na jumla ya kete 969 zinazosadikiwa kuwa ni madawa ya kulevya zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya DVD.

  Mwanamke huyo ambaye amekamatwa na wenziwe wawili wanaume katika maeneo ya PBZ Chake Chake anakuwa wa pili kukamatwa ndani ya kipindi cha wiki mbili baada ya Septemba 9 mwezi huu kukamatwa mwengine akiwa na jumla ya kete 3621.

  Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Madungu Chake Cheke Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shikhan Mohamed Shikhan amemtaja mwanamke huo ni Asha Mohamed Issa (30) mkaazi wa Wawi Chake Chake, huku wenzake wakiwa ni Ali Nyoro Tirima (32)wa Wawi na Salim Said Kombo 23 mkaazi wa Konde Wilaya ya Micheweni.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shikhan Mohamed Shikhan akizungumzia kukamatwa kwa madawa hayo.
  Mzigo wa madawa hayo.  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,”Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science” Mhe.Habib Mohammed Al-Riyami mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,uliojengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,ambao umejengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,ambao umejengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,ambao umejengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,ambao umejengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipofuatana na Viongozi mbali mbali wakiwemo Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,”Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science” wakati alipotembelea sehemu mbali mbali za Msikiti Masjid Jaamiu Zinjibar baada ya kuufungua rasmi leo,ambao umejengwa Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi kwa Ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Watu wa Oman,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,”Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science” Mhe.Habib Mohammed Al-Riyami wakati alipotembelea sehemu mbali mbali mara alipofungua Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,uliojengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipokea Shahada na Ufunguo kutoka kwa Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,”Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science” Mhe.Habib Mohammed Al-Riyami kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Msikiti Masjid Jaamiu Zinjibar leo uliojengwa kwa Ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Watu wa Oman katika maeneo ya Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi,Picha na Ikulu

  0 0

  WADAU mbalimbali wamejitokeza kuchangamkia fursa za uwekezaji wilayani Kisarawe wakati wa uzinduzi wa kongamano la fursa za uwekezaji wilayani humo. 

  Katika kongamano hilo limehudhuriwa na Wafanya biashara na taasisi mbalimbali ambao wameweza kufahamu fursa nyingi ambapo hapo awali walikuwa hawajui mazuri hayo.

  Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo, Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. Selemani Jafo ameeleza kwa undani mpango wa serikali wa viwanda sambamba na kueleza kwa kina fursa zipi zilizopo Kisarawe.

  Jafo ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa maelekezo yake kwa DAWASA aliyo yatoa miezi michache iliyopita ya kupeleka maji Kisarawe na eneo la uwekezaji wa viwanda ambapo mpango huo utachochea viwanda katika eneo la Visegese lililotengwa kwaajili ya viwanda.

  Katika eneo hilo kwasasa kuna zaidi ya ekari 1000 zilizopimwa na kuchongwa barabara na viwanja 291 vya uwekezaji wa viwanda vikubwa na viwanda cha kati vimeshapimwa na kutengwa tayari kwa uwekezaji.

  Aidha Mpaka sasa tayari viwanda vinane vimeshajengwa ikiwa pamoja na bandari kavu iliyopo itakayosaidia uwekezaji wa kisasa kutokana na kupitiwa kwa reli mbili za TAZARA na Reli ya kati.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akifungua kongamano la fursa na Uwekezaji Kisarawe.
  Wadau mbalimbali walioshiriki kongamano la fursa za uwekezaji wilayani Kisarawe.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye picha na baadhi ya viongozi wa serikali.

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Serikali  imesema kuwa Baraza la Taifa la Ujenzi ni muhimu kwa taifa pamoja na kwa wananchi katika kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu  sekta ujenzi nchini.

  Hayo ameyasema leo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakati akifungua warsha ya Baraza la Taifa la Ujenzi kujadiliana la maboresho ya baraza hilo, uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam, Profesa Mbarawa amesema kuwa hakuna mtu ambaye anajua gharama ya mraba wa mita moja ambapo kazi hiyo ilitakiwa kufanywa na baraza hilo.

  Amesema kuwa wakati mtu anataka kujenga nyumba anaweza kupata gharama katika baraza la ujenzi na kuachana na ujenzi wa mazoea ambao unachukua gharama kubwa.

  Mbarawa amesema  bidhaa zinaingia nchini lakini hakuna anayejua gharama na ubora na kutofautisha na bidhaa zingine za ambapo kazi hiyo baraza la taifa la ujenzi linatakiwa kufanya.

  Amesema kuwa kama mambo hayaendi sawa kutokana na sheria yuko tayari kubadilisha sheria  ili baraza lifanye kazi yake kwa maendeleo ya taifa.

  Aidha Mbarawa amesema warsha hiyo italeta mapendekezo ya kina kutokana na wadau waliopo katika sekta ya ujenzi ili iweze kuleta matokeo chanya.

  Nae  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema warsha hiyo watajadili  katika kuborseha baraza hilo.

  Amesema kuwa wadau wa sekta ya ujezi watakuwa huru na wazi katika uchangiaji masuala mbalimbali ikiwa na malengo ya kuborsesha sekta ya ujenzi.

  Mwenyekiti wa Baraza hilo, Profesa Mayunga Mkunya amesema kuwa kufanyika kwa baraza hilo ni matokeo kile kitachojadiliwa kuwezesha katika kujenga baraza.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya kujadili mabaoresho ya baraza la taifa la Ujenzi lililofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga akizungumza juu ya baraza la Taifa la Ujenzi linavyofanya kazi leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ujenzi,  Profesa Mayunga Mkunya akizungumza juu warsha hiyo itavyoleta matokeo yaliyotokana na majadiliano na wadau leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya wadau ya wakiwa kwenye Warsha ya Baraza la Taifa la Ujenzi kujadiliana maboresho ya baraza hilo, iliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa warsha ya baraza la Taifa la Ujenzi leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam.  

  0 0


  0 0


  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya ujenzi kuanza kuweka twakwimu takwimu zinazohusu masuala ya ujenzi hapa nchini.

  Akifungua warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Prof. Mbarawa, amesisitiza umuhimu wa sekta hiyo kuimarisha taarifa za aina, vifaa, viwango vinavyohitajika kimataifa na gharama katika shughuli za ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, nyumba na miundombinu mingine.

  “Sekta ya Ujenzi ina mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi na kijamii hivyo uwepo wa taarifa mbalimbali unahitajika ili kurahisisha uelewa wa wananchi wa kawaida katika masuala ya ujenzi na gharama zake”, amesema Prof. Mbarawa.

  Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wadau wa sekta ya ujenzi kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha sekta hiyo inakidhi matarajio ya watanzania wengi kwa lengo la kuwajengea miundombinu iliyo bora na imara.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
  Wadau wa sekta ya ujenzi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya sekta hiyo kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (kulia), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.


  0 0


older | 1 | .... | 1923 | 1924 | (Page 1925) | 1926 | 1927 | .... | 3282 | newer