Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1920 | 1921 | (Page 1922) | 1923 | 1924 | .... | 3270 | newer

  0 0


  Na. Angela Msimbira- TAMISEMI.

  Katibu Mkuu Ofisi ya Ras Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe amesema kuwa zaidi ya kaya 438 za watumishi wa umma watakaohamia Dodoma na wenye sifa ya kupatiwa nyumba na Serikali watakuwa na uhakika wa kupata nyumba zilizokuwa zikimilikiwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA)

  Akikabidhi Nyumba zilizokuwa zikimilikiwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu kwa Wakala wa Majengo (TBA) Mhandisi Mussa Iyombe amesema, nyumba hizo zitakuwa maalum kwa watumishi wenye sifa kulingana na miundo ya kitumishi.

  ‘’Nyumba ambazo zinakabidhiwa kwa Wakala wa Majengo ni nyumba za kuishi ambazo awali zilimilikiwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu na kuhamishiwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma” Amesema Mhandisi Iyombe.

  Akitoa Maelezo ya awali Mhandisi Musa Iyombe amesema baada ya kuivunjwa kwa CDA iliagizwa kuwa watumishi wote waliokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kupangiwa kazi kwenye Ofisi za Serikali na kipaombele cha kwanza kilikuwa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuchagua watumishi wanaomfaa kwa ajili ya kuendeleza kazi zilizokuwa zikifanywa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kazi ambayo kwa sasa imekamilika.

  Katibu Mkuu Mkuu OR-TAMISEMI,Mhandisi Mussa Iyombe, pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa majengo nchini, Msanifu Majengo Elius Mwakalinga, wakiweka saini makubaliano ya kukabidhiana zilizokuwa nyumba za CDA.

  .Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe, akipokea Nyaraka kutoka kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma kabla yakuzikabidhi kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa majengo Tanzania.

  Katibu Mkuu Mussa Iyombe akifanya makabidhiano rasmi na Mtendaji mkuu wa Wakala wa Majengo nchini. TBA.

  Baadhi ya washuhudiaji wakiwa katika makabidhiano hayo hapa wakishuhudia.


  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0


  0 0

  "Serikali yasema ipo tayari kugharamia matibabu zaidi ya Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Antiphas Lissu popote Duniani, pindi itakapopata maombi kutoka kwa familia pamoja na taarifa kutoka kwa madaktari kuhusu mahitaji ya matibabu zaidi ya mgonjwa",Waziri Ummy Mwalimu.

  0 0


  0 0

  SERIKALI imesema kuwa ipo tayari kuingia kugharama zozote ili kumpeleka kwenye matibabu mahali popote duniani Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu iwapo watapokea maombi kutoka kwa ndugu na familia yatakaothibitishwa na daktari kuwa anahitaji huduma ya madaktari wa bingwa zaidi.

  Akitaka apelekwe Marekani,Ujerumani na mahali mengine ikiwemo India tunaweza kumpeleka iwapo watapeleka maombi kwa serikali kutaka ifanye hivyo ili  kuhakikisha anapata matibabu stahiki. 

  Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Tanga ambapo alisema wakipita maombi watatekeleza suala hilo haraka iwezekanavyo.

  "Serikali haitakataa wala kushindwa kumuhudumia Tindu Lissu yeye ni Mtanzania kama wanavyohudumiwa wengine hivyo wao wapo tayari kuhakikisha anapata matibabu bora nje ya nchi "Alisema .Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga wakati akitangaza kuwa serikali ipo tayari kumpeleka kwenye matibabu mahali popote duniani mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lisu. 


  0 0

  Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa jumuiya ya madola utakaofanyika kuanzia Septemba 24 hadi 28 mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Benki ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam.

  Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa jumuiya ya madola utakaofanyika kuanzia Septemba 24 hadi 28 mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Benki ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jaji Kiongozi Fednand Katipwa.

  Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa jumuiya ya madola utakaofanyika kuanzia Septemba 24 hadi 28 mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Benki ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jaji Kiongozi Fednand Katipwa. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili, Ignas Hatusi.

  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii. 


   Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
  KWA MARA ya kwanza, nchi ya Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa jumuiya ya madola utakaofanyika kuanzia Septemba 24 hadi 28 mwaka huu (2017)jijini Dar es Salaam ambapo washiriki kutoka nchi mbali mbali wapatao 354 wanatarijiwa kukuwepo.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mahakama ya rufaa, leo jijini Dar es Salaam Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma amesema, mkutano huo utakaofanyika katika ukumbi wa benki kuu jijini hapa utafunguliwa Septemba 24 na Makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Samiah Suluhu Hassan na kufungwa na Rais wa Zanzibar Dkt, Mohamed Ali Shein siku ya Alhamis Septemba 28.

  Amesema, mkutano huo wenye maudhui “Mahakama Madhubuti, inayowajibika na Jumuishi” yanayoendana na misingi ya utekelezaji wa mpango mkakati wa mahakama na nguzo zake tatu utakuwa wa kihistoria kwani tangu kuanzishwa kwake mwaka 1970, kwa mara ya kwanza Tanzania inakuwa mwenyeji.

  Amesema, majaji wakuu 13 kutoka nchi mbali mbali na watu mashuhuri wapatao sita ambao ni marais na majaji waandamizi wa mahakama za juu na rufaa kutka Australia, Afrika Mashariki, Pakistani na Zambia wanatarajiwa kushiriki pia huku Mahakama ya Tanzania ikiwakilishwa na wajumbe 50 ambao watakuwa ni majaji na mawakili kutoka Tanzania bara na visiwani.

  Ameongeza kuwa, lengo kubwa la mkutano huo ni pamoja na kuwajengea uelewa wajumbe kuhusiana na masuala ya uhuru wa mahakama, mikataba ya kimataifa maendeleo ya kisheria upatikanani wa huduma ya haki, maendeleo ya chama na chagamoto zake katika usikilizaji wa mashauri ambapo pia “Mahakimu na majaji wetu watapata fursa ya kujengewa uwezo na kupata uzoefu juu ya sheria mbali mbali.

  Amesema, katika mkutano huo, Tanzania itapata fursa ya kujitangaza kiutalii na vivutio vyake na vile vile itakuza biashara kwa kuongeza kipatao hasa katika mahoteli ambapo wajumbe wengi watafikia.
  “Katika kuhakikisha utalii wetu unajitangaza, tumefanya maandalizi ya kutosha na wizara ya mambo ya nadani, wizara ya mambo ya nje na ile ya utalii zinashiriki vema, kwani tunaimani baada ya mkutano huu wageni wengi watabaia nchini na kutembelea vivutio vya utalii na sehemu mbali mbali kama Zanzibar na Bagamyo”.

  0 0

  NA BALTAZAR MASHAKA,MWANZA
  TAASISI ya The Desk & Chair Foundation (TD&CF) imekabidhi hundi mbili zenye thamani ya zaidi sh. 2.5 kwa vituo vya Karibu Foundation na Nitetee Foundation ili kuwawezesha  watoto 50 wanaolelewa kwenye vituo hivyo kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF).
  Akizungumza jana baada ya kukabidhi hundi hizo Mwenyekiti wa TD & CF Sibtain Meghjee alisema fedha hizo zitatumika kugharamia matibabu ya watoto hao kwa kipindi cha mwaka mmoja.
  “ Watoto wanaolelewa kwenye vituo vya Nitetee Foundation na Karibu Foundation,  wengi wao wanatoka kwenye familia duni na wanaishi katika mazingira magumu.Tumeona tuwasaidie kwa kuwakinga na magonjwa kwa kuwalipia mchango wa uanachama wa Bima ya Afya wa sh. 54,000 utakaomuwezesha mtoto kutibiwa kwa mwaka mzima ambapo kila kituo kimepewa sh. 1, 260,000 kwa ajili ya watoto 25 ambao wamesajiliwa tayari, ”alisema. 
   Meneja wa kituo cha Nitetee Foundation, Johaness Emmanuel akipokea hundi ya sh. 1,260,000 za malipo ya mchango wa uanachama wa bima ya afya kwa watoto 25 wa kituo hicho kutoka kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana, kulia mwenye kinasa sauti ni Mwenyekiti wa Taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania Sibtain Meghjee ambayo imetoa fedha hizo kwa kituo hicho na Karibu Foundation.Kulia mwenye shati ya draft ni Meneja Matekelezo wa NHIF Mkoa wa Mwanza Calistus Mpangala. Picha ya Baltazar Mashaka.
   Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Mkoa wa Mwanza, Castus Mpangala akitoa ufafanuzi wa huduma zinazotolewa na mfuko huo kwa wananchi waliohudhuria semina ya bima ya afya iliyoandaliwa na Taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania ili kuwahamasisha  kujiunga na mfuko huo kwa ajili ya kupata matibabu kwa gharama nafuu. Semina hiyo ilifanyika jijini Mwanza.
   Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella mwenye kofia akiwa ameshika moja ya mashuka yaliyotolewa msaada na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Mkoa wa Mwanza kwa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe. Wa tatu kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dk.Leonard Subi, Meneja wa mfuko huo mkoani Mwanza Dk. Mohamed Kilolile wanne kulia na  kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Uekerewe Estomiah Chang'a.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (mwenye kofia) hivi karibuni akinunua samaki aina ya Furu kutoka kwa akinamama wachuuzi wa samaki katika Soko la Kakukulu lililopo wilayani Ukerewe. Mkuu huyo wa Mkoa alikuwa wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali. Picha na Baltazar Mashaka.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  NA VICTOR MASANGU, KIBAHA .

  VIJANA wajasiriamali zaidi ya 50 kutoka Wilayani Kibaha Mkoa Pwani wamepatiwa mafunzo kwa lengo la kuweza kujifunza stadi mbali mbali za maisha pamoja na namna ya kuweza kujiajiri wao wenyewe kupitia biashara ndogo ndogo wanazozifanya ili kuweza kupambana na wimbi la umasikini na  kujikwamua kiuchumi kwa lengo la kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

  Mafunzo hayo ya vijana ambayo yanafanyika mjini Kibaha kwa muda wa siku 14 yameandaliwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya ushindani na biashara Tanzania  (TECC) kwa kushirikiana na wadau  mbali mbali wa maendeleo kwa lengo la kuweza kuwawezesha vijana hao  ili waweze kupambana na changamoto inayowakabili kwa sasa ya upatikanaji wa soko la  ajira.

  Akizungumza katika uzinduzi wa programu  hiyo ya kuwasaidia vijana wajasiliamari Mkurugenzi mtendaji wa  Taasisi hiyo ya TECC Sosthenes Sambua amesema kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha kwamba inawakomboa vijana hao kwa kuwajengea uwezo wa kuweza kujikwamua kimaisha.

  Naye Meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani Agnes Yesaya amesema lengo lao kubwa ni kuhakikisha inatoa mafunzo zaidi kwa vijana waliopo katika vikundi mbali mbali pamoja na kuwapatia mikopo pamoja na kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo ambayo itaweza kuwapa fursa ya kujiendeleza zaidi katika  kukuza mitaji yao.

  “Sisi kama sido Mkoa wa Pwani lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunawasaidia vijana katika kuwapatia mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali pamoja na stadi za maisha kwa lengo la kuweza kupambana na ajira, hivyo tunatarajia baada ya mafunzo haya yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa vijana wetu ikiwemo kupambana na wimbi la umasikini.,”alisema Yesaya.
   Meneja wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani Agnes Yesaya akizungumza jambo mara baada ya uzinduzi wa progamu ya kuwasaidia mafunzo mbali mbali  vijana wajasiriamali zaidi ya 50  kutoka Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani (PICHA NA VICTOR MASANGU)
   Mkurugenzi mtendaji wa  Taasisi  ya TECC, Sosthenes Sambua ambao ndio waandaaji wa mafunzo hayo ya vijana akizungumzia kuhusina na mikakati ya kuwawezesha vijana hao  ili waweze kutimiza ndoto zao mara baada ya kupatiwa ujuzi katika mafunzo hayo.
   Baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wakiwa wametulia kwa ajili ya kusikiliza mafunzo ya ujasiliamali.
  Mmoja wa vijana wajasiriamali akizungumza na baadhi ya wenzake katika mafunzo hayo kuhusina na jinsi alivyoweza kupata fursa ya kuweza kujiajiri yeye mwenyewe na kupitia mafunzo aliyoyapata hayo awali.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Jaji Mkuu wa Serikali, Profesa Ibrahim Musa akijibu swali la Mwandishi wa habari wakati alipoulizwa kuhusiana na Taarifa iliyotumwa na Chama cha wanasheria Uingereza. Taarifa Kamili ya Chama hicho Soma hapa chini.

   

  0 0

   JESHI la Polisi  Mkoa wa Pwani  wamewakamata watuhumiwa wawili  ambao wameshikwa  wakisafirisha  dawa za kulevya  aina ya Bhangi  magunia nane.
   Watuhumiwa hao walionaswa  na Jeshi la Polisi wamefahamika  kwa  mjina Abraham Michael  mwenye umri wa miaka  31 mkaazi wa Jijini Dar es Salaam na Godfrey  Malakasuka  mwenye umri wa miaka 21 mkaazi wa Kimara  waliokamatwa katika eneo la Ubena Zomozi wakitokea Mkoani Morogoro kuelekea Jijini Dar es Salamaa.
  Akizungumza na  waandishi wa habari  Kamanda wa Mkoa wa Pwani ACP Jonathan Shanna  alisema kuwa watuhumiwa  wamekamatwa na vidhibiti  hivyo wanastahili  kupata adhabu kali pindi watakapofikishwa  mahakamani.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ametoa wito kwa wakazi wa Arusha kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/S Hanil-Jiangsu J/V ili kuweza kukamilisha kwa wakati ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4.

  Akikagua mradi wa ujenzi wa barabara hiyo mkoani humo, Profesa Mbarawa amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutapunguza msongamano wa magari katikati ya jiji hilo na hivyo kuvutia watalii na kukuza uchumi wa mkoa.

  "Kukamilika kwa barabara hii ya Arusha bypass kutapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano kwani magari makubwa ya mizigo yatatumia mchepuo huu na kurahisisha huduma za usafirishaji jijini Arusha", amesema Waziri Mbarawa.Ameongeza kuwa Wizara yake itasimamia kwa ukaribu ujenzi wa barabara hiyo ili ikamilike kwa wakati uliopangwa na viwango vinavyostahili vilivyokubalika.
   Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Cheil Engineering Bw. Shin Soo akimueleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4. Kushoto ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale.
   Mafundi wa Kampuni ya M/S Hanil-Jiangsu J/V wakiendelea na ujenzi wa moja kati ya madaraja makubwa saba yanayojengwa katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4.
   Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) hatua mbalimbali za maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), wakati Waziri huyo alipoikagua, mkoani Arusha.
   Moja kati ya madaraja saba yanayojengwa katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4, jijini Arusha.
   Tingatinga likiendelea na kazi ya ujenzi wa awali ya madaraja katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4, jijini Arusha.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  WADAU katika sekta ujenzi nchini wametakiwa kutumia bidhaa zenye viwango na ubora unaostahili ili kulinda ukuaji wa sekta hiyo na kuleta matokea chanya kwa ustawi na maendelea ya taifa na watu wake.

  Akizungumza kwenye semina iliyowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wahandisi, makandarasi, wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa nyaya za umeme jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwango wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bi. Edna Ndumbaro alisema bidhaa zinazotumika kwenye masuala ya umeme zinahitaji kuwa na viwango na ubora unaostahili.

  “Badiliko la rangi mpya za nyaya za umeme (New Colour Codes) limewaleta wadau hawa muhimu kujadiliana kwa pamoja na kuazimia kwa pamoja namna bora ya utekelezaji wake,” Bi. Ndumbaro alisema. Alisema rangi mpya ya nyaya ya umeme ilishaazimiwa kama kiwango cha lazima kufuatwa tangu mwaka 2016 na hivyo ni vyema kwa wadau na wataalamu wakazingatia kuwa viwango ni jambo muhimu sana likapewa kipaumbele zaidi.

  “Sisi kama TBS tutaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa viwango na ubora kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ikiwemo tovuti ya shirika,” Bi. Ndumbaro alisema na kuongeza kuwa washiriki wa semina hiyo watakuwa walimu wazuri.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwango wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bi. Edna Ndumbaro akisisitiza jambo kwenye Semina ya wadau kwenye semina iliyowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wahandisi, makandarasi, wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa nyaya za umeme jijini Dar es Salaam jana kuhusu matumizi ya Rangi mpya za nyaya za umeme.
  Afisa Viwango wa Viwango wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Henry Massawe akiwasilisha mad kwenye Semina ya wadau kwenye semina iliyowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wahandisi, makandarasi, wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa nyaya za umeme jijini Dar es Salaam jana kuhusu matumizi ya Rangi mpya za nyaya za umeme.

  Baadhi ya washiriki wa semina ya wadau kwenye semina iliyowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wahandisi, makandarasi, wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa nyaya za umeme jijini Dar es Salaam jana kuhusu matumizi ya Rangi mpya za nyaya za umeme semina hiyo imeandaliwa na Shirika Viwango wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

  MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amesitisha mkataba na Kampuni ya Mwamkinga Auction Mart and Brokers iliyokuwa ikifanya kazi ya kudhibiti uegeshaji wa magari katika maeneo yasiyo rasmi kwa Hal
  mashauri ya Temeke na Kigamboni.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mapema leo asubuhi Meya Mwita amesema kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na kampuni hiyo kufanya kazi kwakutozingatia matakwa ya mkataba na hivyo kuanzisha migogoro isiyo ya lazima baina ya halmashauri ya jiji na Wananchi.

  Meya mwita amefafanua kuwa jiji liliingia mkabata na kampuni hiyo Aprili mwaka huu kwa lengo la kufanya kazi hiyo ambapo mkataba huo ulielekeza kufanya kazi kwa weledi mkubwa, kuzingatia sheria, miongozo ,maelekezo, kanuni na taratibu zilizopangiwa bila kusababisha bughudha, uonevu, kero na usumbufu kwa wananchi jambo ambalo halikufanyika.

  “ Hii kampuni imekuwa ikilalamikiwa mno na wananchi, inawasumbua, na sisi kuwapa tenda hii sio kwa ajili ya kuwanyanyasa, kuwasumbua ila ni kufanya kazi kwa weledi”Nakuongeza kuwa” tumefuatilia kwa karibu sana utendaji kazi wao, kutokana na malalamiko ambayo yalikuwa yanatolewa na wananchi, tukajiridhisha, kwa ushahidi uliojitosheleza, hawawezi kunyanyasa watu na mimi kama meya wa jiji hili nikawaachia, hili haliwezekani” amesisitiza Meya Mwita.

  Hata hivyo ameeleza kuwa kampuni hiyo inapaswa kuondoka mara moja kwenye maeneo iliyopangiwa kufanya kazi hiyo na kuhakikisha kwamba katika kuanzia tarehe ambayo mkataba huo umesitishwa iwe imekabidhi mashine zote za kukusanyia mapato kwa halmashauri zikiwa kwenye hali salama.

  Aidha Meya Mwita amesisitiza kuwa hata sita kuzichukulia hatua kampuni nyingine ambazo zimepewa tenda hiyo na kuzionya kuwa iwapo wanatabia hiyo waache mara moja kwani kazi waliyopewa sio ya kusanyanyasa wananchi bali ni kufanya kazi kwa kufuata sheria.

  0 0

  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la UN Alvaro Rogriquez jana akipanda mti wa matumaini ya programu ya pamoja ya kigoma katika kambi ya Nyarugusu juu ya mradi mtambukwa endelevu kwa wakimbizi na wakazi wa wilaya hasa vijiji jirani zinazoishi na wakimbizi Picha na( Magreth Magosso Kigoma).
  Pichani wa tatu kutoka mkono wa kushoto ni Kaimu mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Marco Gaguti akikata utepe wa kuzindua jengo la dawati la jinsia la polisi wilayani kasulu akishuhudiwa na wafadhili wa umoja wa mataifa akiwemo mkurugenzi mkazi wa UN Alvaro Rodriquez .
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Palanjo aliyevaa koti ambaye pia ni Mgeni rasmi akihitimisha kwa kuzindua jiwe la msingi wa mradi wa pamoja kigoma katika Kambi ya wakimbiz na waomba hifadhi ya Nyarugusu wilaya ya kasulu .(Picha na Magreth Magosso )Kigoma.
  Mwakilishi kutoka ubalozi wa watu wa Norway Trygre Bendksby jana katika kambi ya nyarugusu akiumwagilia maji mti alioupanda kama sehemu ya matumaini ya mradi wa programu ya pamoja kigoma yenye vipaumbele sita ikiwemo nishati endelevu na mazingira .Picha na Magreth Magosso kigoma.

  0 0

  Kikao cha wataalamu wa masuala ya teknolojia ya Mawasiliano leo kimeendelea mjini Bagamoyo kwa kuhusisha Wadau wakuu katika masuala ya utoaji huduma nchini zikiwemo Wizara, Taasisi , Mashirika na Makampuni binafsi. 

  Katika kikao cha leo wadau wanajadili mapendekezo ya timu ya wataalamu iliyokutana siku ya kwanza ya kikao hicho kuhusu kuundwa kwa timu ya pamoja ya wataalamu ambayo itapendekeza mfumo rafiki na rahisi utakaorahisisha utoaji huduma nchini na kuboresha maisha ya watanzania kwa kutumia mfumo wa Taifa wa Utambuzi na Usajili wa watu unaosimamiwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). 

  Akichangia katika siku ya pili ya mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Balozi Hassan Yahya Simba amesema ubora wa huduma na maendeleo ya Taifa unategemea uwepo wa mfumo huu ambao ni kwa manufaa si tu ya Serikali lakini pia kwa Sekta binafsi.
  Mwakilishi wa Benki ya Dunia (World Bank) Ndugu Robert Polacious akizungumza kwenye siku ya pili ya kikao cha wadau kuhusu kuundwa kwa mfumo wa kidigitali utakaoungalisha mifumo ya taarifa nchini kwa kutumia Mfumo Mama wa Utambuzi na Usajili wa Watu unaosimamiwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NDIA) 
  Dr. Elias Mturi mtaalamu katika teknolojia ya mawasiliano akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya Wadau Bagamoyo. 

  Amesema kwa sasa Serikali ina kila sababu ya kuwa na mfumo huu kutokana na mahitaji yaliyopo katika kuboresha huduma za Kijamii, kuwezesha wananchi kushiriki kupata huduma za kifedha na Kibenki, kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato, uchaguzi na kuongeza fursa za uzalishaji katika kufikia maendeleo ya haraka. 

  Washiriki wengine wanaoshiriki kuchangia kuundwa kwa mfumo huu ni Kampuni za simu Tanzania, Benki, Mashiriki ya Kimataifa yanayotoa huduma nchini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Wataalamu wa ndani na nje katika masuala ya teknolojia na wakuu wa Taasisi wa nchi za Estonia na India ambazo tayari mfumo wa kuunganisha taarifa kidigitali (Digital ID ecosystem) imeshaanzishwa na kupata mafanikio makubwa. 

  Warsha hii inategemewa kumalizika na maazimio ya pamoja ya namna mfumo huo utakavyoundwa nchini kwa kutumia teknolojia na kushiriki wadau wote muhimu. 
  Wawakilishi wa Umoja wa Makampuni ya Simu Tanzania wakiwasilisha mada na maoni ya wadau katika kuundwa kwa mfumo wa Taifa wa kidigitali unaounganisha mifumo ya taarifa kupitia mfumo Mama wa Utambuzi na Usajili wa Watu unaomilikiwa na NIDA. Katikati ni ndugu Paul Bomani wa AIM Group akiwasilisha mada kwa niaba ya MOAT. 
  Washiriki wa Warsha ya wataalamu na wadau wakijadiliana kwenye vikundi wakati warsha ya kuunda mfumo wa kidigitali wa mawasiliano Tanzania inayofanyika Bagamoyo.

  0 0

  Baadhi ya vijana wajasiliamali katika Manispaa ya kigoma Ujiji mkoani Kigoma, wakimsikiliza mwenzao akinyambulisha dhana ya uwezweshwaji wa vijana kiuchumi kwenye warsha ya kuibua changamoto ya ajira kwa vijana iliyoandaliwa na Akimizi ya kuendeleza wajasiliamali (DTBI) chini ya Tume yaTaifa ya Sayansi uliofanyika leo katika ukumbi wa Redcross uliopo kigoma ujiji.(Picha na Magreth Magosso kigoma).

  0 0

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ laanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Meja Jenerali Michael Isamuyo atua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano.
  Helikopta iliyombeba Meja Jenerali Michael Isamuyo akitua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano. Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ limenanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

  0 0


  MADAKTARI kutoka  Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete kwa ushirikiana na wenzao wa Hospitali ya B.L.K ya nchini India wamewafanyia wagonjwa 64 upasuaji wa moyo  ambao ni wa kufungua na bila kufungua  kifua.

  Kati ya hao wagonjwa nane walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na 52 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua (catheterization)  kwa kutumia mtambo wa Cathlab.

  Pia madaktari hao wamepata mafunzo ya kufanya upasuaji wa milango miwili ya moyo  ambapo awali huduma hiyo ilikuwa haitolewi kwenye taasisi hiyo .Mafunzo hayo ya siku tano yaliyo ongozwa na wataalamu kutoka Hosipitali ya BLK ya Nchini India itasaidia serikali kuokoa zaidi ya milioni 30 ambazo zingetumika kwaajili ya matibabu ya mgonjwa wa moyo wenye uhitaji wa upasuaji wa  milango miwili  ambapo asilimia 25 ya wagonjwa wana uhitaji huo.

  Akizungumza na Waandishi wa habari jana Dar es Salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo  Peter kisenge alisema kupitia kambi ya siku tano ya  madaktari nane wanaotibu maradhi ya moyo ,Wataalamu wa usingizi ,Wataalamu wa kutoa damu kwenye mapafu ,kutoka Hosipitali ya BLK ya nchini India imesaidia kutoa mafunzo ya uwekaji na upasuaji wa milango miwili kwenye moyo kwa wagonjwa wenye matatizo hayo ambapo huduma hiyo itakuwa ya kwanza kutolewa hapa nchini.

  Mbali na huduma hiyo Dk Kisenge alisema tayari madaktari watatu wa taasisi hiyo wanaweza kutoa huduma ya uwekaji wa milango miwili ya damu kwenye moyo  huku Daktari mmoja akipata mafunzo ya miaka miwili  nchini india.Kuanza kwa huduma hiyo alisema watasaidia watoto wadogo ambao milango yao imeziba ambapo awali walikuwa hawafanyiwi upasuaji kutokana kutokuwepo kwa ujuzi wa upasuaji wa milango hiyo.
  Alisema kwa wagonjwa 64 waliofanyiwa upasuaji katika taasisi hiyo wangesafirishwa nchini india serikali ingepoteza zaidi ya bilioni 6 .

  Kwa upande wake Daktari Bingwa Upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Hosipitali ya BLK ya Nchini India Dk Ajal Kajul alisema wataendelea kutoa ushirikiano kwa madaktari hapa nchini ambapo baadhi ya madaktari walioambatana nao watabaki katika taasisi hiyo kwaajili ya kuendelea kutoa mafunzo zaidi.

   Dk. Kaul alisema wataendelea kuonyesha ushirikiano wa kutoa ujuzi kwa madaktari wa hapa nchini ambapo octoba mwaka huu watatoa mafunzo ya upandikizaji wa figo,na wagonjwa wenye matatizo ya mgongo katika Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili. 
   Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Hospitali ya B.L.K ya nchini India Ajal Kajul akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uhusiano wao na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo kwa pamoja wameweza kuwafanyia upasuaji  wa kufungua na bila kufungua  kifua  wagonjwa 64. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Peter Kisenge.
    Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uhusiano wao na Hospitali ya B.L.K ya nchini India   ambapo kwa pamoja wameweza kuwafanyia upasuaji  wa kufungua na bila kufungua  kifua  wagonjwa 64. Kulia  ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Hospitali ya B.L.K ya nchini India Ajal Kajul.


  Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikilliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Hospitali ya B.L.K ya nchini India (hayupo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uhusiano wao na Taasisi hiyo ambapo kwa pamoja wameweza kuwafanyia upasuaji  wa kufungua na kufungua kifua  wagonjwa 64. (Picha na JKCI)

  0 0

  Mwanamuziki John Kitime akizungumza na Michuzi TV jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tamasha la Muziki wa Zamani yaani muziki wa Miaka ya 1960 na 1970 na 1980. Tamasha hilo litkalofanyika katika ukumbi wa Burudani wa Salenda Klabu jijini Dar es Salaam Kesho Ijumaa ya Septemba 22, 2017.

  Amesema kuwa Burudani ya Kutosha itatolewa kuanzia saa moja jioni kwa kiingilio cha shilingi 10,000/= na itakuwa kila Ijumaa ya kila wiki.
  Pia amewakaribisha Vijana wazamani pamoja kwenda katika eneo husika ili kujikumbusha muziki na burudani za zamani.

  0 0

  Ecobank yaja na suluhisho la kufanya malipo salama kwa njia mtandao kupitia MASTERPASS na MVISA . 

  Ecobank katika kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwa suluhisho kwenye sekta ya biashara ya huduma za kibenki hapa nchini leo imezindua applikesheni ya simu za mkononi itakayojulikana kama Ecobank Mobile App – MASTERPASS NA MVISA ili kusaidia wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali kufanya Malipo kwa njia rahisi na kwa usalama zaidi mahali popote.

  Mtanzania yeyote ataweza kutumia teknolojia hii ya mpya ya MASTERPASS QR na MVISA kulipia gharama mbali mbali kwa kutumia simu zao za mkononi kwa kupitisha Quick Response (QR) kwa wauzaji mbalimbali wa bidhaa au watoa huduma ndani na nje ya nchi.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Bi, Mwanahiba Mzee alisema “applikesheni ya Ecobank Mobile App ilizinduliwa Februari mwaka huu lakini kwa sasa imeboreshwa zaidi ili wateja wa Ecobank na wale wasio wateja wa bank hii waweze kutumia applikesheni hii duniani kote”.

  ‘Applikesheni ya Ecobank Mobile App ni njia rahisi ya kujipatia huduma za kibenki ndani ya nchi 33 ambazo Benki yetu inafanya biashara lakini pia unaweza kuitumia ukiwa kokote duniani. Wateja wanaweza kupakua applikesheni Ecobank Mobile App na papo hapo kujifungulia akaunti ya Ecobank kwa njia ya mtandao na kuanza kupata huduma za kibenki kama vile kufanya malipo au kuhamisha fedha bila kutembelea tawi lolote la Benki”, alisema Bi Mzee.

  “Tunayo furaha kwamba applikesheni yetu ni sulushisho la huduma za haraka za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi na bado inaendea kuboreshwa zaidi na zaidi na sasa tunatumia teknolojia ya Masterpass QR na Mvisa kwa kufanya malipo mbali mbali, aliongeza. 
    Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ,Ecobank Tanzania, Mwanaiba Mzee, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi  huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA .Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki  hiyo, Respige  Kimati  na Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Reja reja, Ndabu Sware (kushoto).
   Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Reja Reja wa Ecobank Ndabu Lilian Sware (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi  huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA. Kati kati Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki hiyo Mwanaiba Mzee na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki  hiyo, Respige  Kimati.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakifuatilia kwa umakini wa Uzinduzi  wa huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA. Ecobank Tanzania inakuwa Benki ya kwanza hapa Tanzania kuzindua huduma ya Mobile App ambayo inakuwa ni suluhisho kwa huduma za kifedha.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1920 | 1921 | (Page 1922) | 1923 | 1924 | .... | 3270 | newer