Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1919 | 1920 | (Page 1921) | 1922 | 1923 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Familia ya Ramadhani  Hassan Nyamka wanakumbuka kifo cha baba yao mpendwa Ramadhani Nyamka aliyefariki Septemba 20 1997.

  Ni miaka 2o toka kuondoka kwa Ramadhani Nyamka ambaye aliwahi kuwa Mwemyekiti wa Chama Mkoa Dar es Salaam na Meya wa Jiji la Dar es salaam mwaka 1978-82.

  Unakumbukwa na watoto wako Zuberi, Ibrahim, Sophia, Halima, Shami, Mariam, Maendeleo, Shaban na Mikidadi,  wake zao Mama Shami na Mama Mzee pamoja na wajukuu zako Zainab, Umrathi, Nuru, Salum, Hafidha, Sara na familia nzima kwa ujumla.

  Tunazidi kukuombea kwa Allah azidi kukupa kauli thabiti na makazi mema Akhera.

  Allahuma Amin.  0 0

  Ligi Ndogo ya Wanawake sasa itaanza rasmi Septemba 30, 2017 katika Kituo cha Dar es Salaam badala ya Septemba 22, mwaka huu. 

  Wakati tayari timu zimepewa taarifa rasmi juu ya tarehe hiyo mpya, lakini kwa taarifa hii, timu zilizoko mikoani zisianze safari kwa sasa.Kupelekwa mbele kwa tarahe husika kumetokana na taratibu za mwisho za usajili ambako sasa timu bingwa wa mkoa inayotambuliwa na mkoa, lazima itimize masharti matatu. 

  Kwanza; Ni kuthibitisha kushiriki kucheza ligi ndogo kabla ya Septemba 25, mwaka huu.Pili; kuthibitisha kama imesajiliwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo (Klabu iwe na hati ya usajili) na tatu kuwasilisha majina ya wachezaji wake iliyowasajili kwa . 

  Kama kuna timu bingwa kwa mujibu wa mkoa, na tayari ina majina ya wachezaji iliyowasajili msimu huu, lakini haina hati ya usajili kutoka kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya mchezo, basi klabu hiyo itakosa sifa ya kushiriki.

  Sharti kubwa ni kwamba timu au klabu hiyo lazima iwe imesajiliwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo. Ndio utaratibu. Ligi Ndogo inachezwa ili kupata timu mbili zitakazopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara msimu wa 2017/18 baada ya timu mbili kushuka msimu wa 2016/17. Ligi ya msimu ulipita bingwa ni Mlandizi Queens ya Pwani wakati zilizoshuka daraja ni Viva Queens ya Mtwara na Victoria Queens ya Kagera.
  Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wanawake (TWFA) Amina Karuma.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA.

  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Afrika Kusini zaridhia kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika. 

  Makubaliano hayo yamefanyika tarehe 19/09/2017 baina ya Tanzania na Afrika Kusini yakiwahusisha Mawaziri wenye dhamana ya Utamaduni kutoka nchi hizo pamoja na Mawaziri kutoka Wizara za kisekta zinazohusika na utekelezaji wa Programu hiyo.

  Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  amesema kuwa Tanzania ina mchango wa hali na mali katika harakati za ukombozi wa nchi za Bara la Afrika pamoja na uanzishwaji wa program hiyo inayolenga kuhifadhi Urithi huo kwa kushirikiana na wadau.

  “ Mwaka  2002 programu hiyo iliridhiwa na Mkutano Mkuu wa 33 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) wa mwezi Januari, 2011” ameongeza Dkt. Mwakyembe.

  Aidha, Dkt. Mwakyembe amesema kuwa, moja ya makubalino ni kuendeleza jitihada za kufanya tafiti zaidi baada ya kukamilika kwa utafiti wa Mradi wa Hashimu Mbita na kufanya juhudi za makusudi kuorodhesha nyaraka za iliyokuwa Kamati ya Ukombozi wa Bara la Afrika katika kumbukumbu ya Dunia.

  Kwa upande wake Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika Kusini Nathi Mthethwa amesema kuwa Programu hiyo  itaimarisha ushirikiano katika kuongeza idadi ya maeneo ya Urithi wa Dunia yanayohusiana na Harakati za Ukombozi yanaorodheshwa kwa pamoja baia ya nchi moja na nyingine hususani Urithi wa Ukombozi usioshikika.

  “Kuna baadhi ya vizazi havielewi machungu ya kutawaliwa, hivyo nashauri mifumo ya elimu katika nchi za Afrika izingatie masuala ya ukombozi wa Bara la Afrika ili kuleta uelewa kwa kizazi kilichopo na vizazi vijavyo” ameongeza Mhe. Mthethwa.

  Programu hiyo ina wajibu wa kukusanya, kuweka kumbukumbu, kuhifadhi na kukumbuka nakishi ya Urithi wa Afrika tangu harakati za kupigania Uhuru wa Afrika hadi Bara zima lilipokombolewa.


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe 

  0 0

  Na Evelyn Mkokoi – Dar Es Salaam.
  Garage kubwa yenye kutoa huduma kwa magari ya aina mbalimbali iliyopo katika eneo la mtaa wa viwanda mikocheni jijini Dar es Salaam imefungwa kwa kile kinachodaiwa ni kukikuka sheria ya mazingira na kanuni zake kwa kuharibu mazingira kwa kumwaga mafuta machafu,  kutupa vyuma chakavu na kutelekeza  magari  yaliyochoka.
  Hatua Hiyo imechukuliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupitia Afisa Sheria Mkuu wake  Bw. Vincent Haule, ambapo Bwana Haule Alisema kuwa Garage Hiyo ambayo Mmiliki wake hakutambulika Mara moja inatakiwa kusimamisha shughuli zote za uendeshaji katika eneo hilo ndani ya siku saba pamoja na kuondoa magari yote.
  Bw. Haule aliongeza kwa kusema kuwa Mmiliki wa Garage hiyo anatakiwa kufuata taratibu za serikali kwa kupata vibali vyote vya uendeshaji ikiwa ni pamoja na kibali maalum kutoka NEMC.Baada ya kutozwa faini ya shilingi milioni 10 kwa kiwanda cha Bidco kinachotengeneza bidhaa za sabuni na mafuta ya kula na kutakiwa kuilipa faini hiyo ndani ya wiki mbili, Naibu Waziri Ofisi ya Makami wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, alisema viwanda vinavyochukuliwa hatua kwa uchafuzi wa mazingira vinatakiwa  kutii maagizo ya serikali.
   Mpina pia alitoa maelekezo kwa Manisapaa ya Kinondoni ambapo aliitaka ishughulikie mitaro katika maeneo ya mikocheni pembezoni mwa viwanda husika na kuondosha maji katika njia sahihi.Kwa upande wa wenye viwanda, Mpina aliwata kuacha kutiririsha majitaka katika mazingira na kuyatibu na kuyaunga katika mfumo sahihi wa uondoshwaji maji hayo wa DAWASCO ili kunususru uharibifu wa mazingira na afya ya viumbe hai.
  Aidha, Mpina aliwataka wamiliki wa kiwanda cha Bidco kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuziba matundu yanayotoa maji machafu kutoka kiwandani hapo sambamba na kusafisha mitaro yote kiwandani humo. Ziara ya  siku mbili ya Naibu Waziri Mpina  jijini Dar es Salaam ilihusisha Ukaguzi wa Mazingira na Utekelezaji wa Sheria hiyo.
  Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina(kushoto) akimsikiliza mtaalam  Bw. Filbert Mdonko, kutoka katika kiwanda cha Intergraded Steel Limited kilichopo katika eneo la viwanda Mikocheni Dar es Salaam namna ambavyo Mtambo wa kusafisha Majitaka unavyofanya kazi.
   Sehemu ya eneo la Garage iliyofungwa kwa uchafuzi wa mazingira katika eneo la viwanda Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano a Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, akiongea na kuonyesha maji machafu na yenye sumu yaliyotuwama na maji hayo yanayotoka viwandani katika eneo la Mikocheni Jijini Dar es Salaam alipoendelea na ziara yake ya ukaguzi wa viwanda na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira leo. 

  0 0


  0 0  0 0


  0 0


  0 0

  Na Benedict Liwenga-WHUSM.
  NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura amesema kwamba Mwanzilishi wa Nyumba ya Sanaa pamoja na Vituo mbalimbali vya Sanaa na Utamaduni nchini Tanzania, Marehemu Sista Jean Pruitt atakumbukwa kwa utu, upendo na kujituma wakati wote na kujitoa kwake kwa hali na mali katika kuviendeleza Vituo mbalimbali vya Sanaa na Utamaduni pamoja na kuendeleza maisha ya wenye mahitaji.

  Mhe. Wambura ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karimjee wakati wa Ibada ya kumuaga mtawa huyo aliyefariki dunia siku za hivi karibuni Jijini Arusha.

  Amesema kwamba, mtawa huyo amekuwa akifanya kazi zake kwa bidii kwa kipindi cha zaidi ya miaka 40 kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania na baadhi ya vituo ambavyo alivianzisha ni pamoja na Kituo cha Dogodogo Centre, TAMOFA, Vipaji, Alliance, huku akisaidia maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) katika kukuza vipaji vya vijana mbalimbali nchini.

  "Sista Jean atakumbukwa kwa jinsi alivyojitoa kusaidia na kuleta mabadiliko katika tasnia ya sanaa ikiwemo kutumia Nyumba ya Sanaa katika kuibua na kuviendeleza vipaji vya sanaa kwa Vijana wetu nchini", alisema Mhe. Wambura.

  Aliongeza kuwa, mchango wake katika sanaa ulimwezesha mtawa huyo kupata tuzo mbalimbali zikiwemo, mwaka 1983 alipewa Tuzo Maalum na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo ilikua Tuzo ya Maisha pamoja na Tuzo ya Zeze iliyotolewa na uliokuwa Mfuko wa Utamaduni Tanzania.

  Akisoma wasifu wa mtawa huyo, Mwakilishi wa Shirika la Masista wa Maryknoll, amesema kwamba, Sista Jean Pruitt alikuja Tanzania 1968 akifanya mambo mbalimbali kwa jamii ikiwemo masuala ya sanaa na watoto wadogo hususani wale wanaotoka katika mazingira magumu hivyo kazi zake alitekeleza kwa vitendo kuliko maneno.

  "Sista Jean Pruitt alifanya shughuli mbalimbali ikiwemo miradi kwa vitendo zaidi, pia aliwalea watoto wengi zaidi nchini Tanzania kwa kuwasomesha na kuwasaidia vijana kuibua vipaji vyao", alisema Mwakilishi huyo.

  Marehemu sista Jean Pruitt alizaliwa nchini Marekani Oktoba 17, 1939 katika Jimbo la Michigan na alijihusisha sana na masuala ya ustawi wa jamii akijikita katika masuala ya Sanaa na Watoto hususani nchini Tanzania pia ndiye mwanzilishi wa Nyumba ya Sanaa.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura akiongea na Viongozi mbalimbali pamoja na Watawa wa Shirika la Watawa wa MaryKnoll wakati wa Ibada ya kumuaga Marehemu Sista Jean Pruitt iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi wa watu toka sehemu mbalimbali walioguswa na msiba wa Sista Jean Pruitt wakifuatilia ibada ya kumuombea marehemu huyo katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini Dk. Juma Ally Malewa wa kwanza kushoto akimkabidhi Mhariri Mkuu wa Gazeti la Mtanzania Bw. Kulwa Karedia Cheti cha Kutambua Mchango wa Gazeti la MTANZANIA katika kutangaza shughuli za Maendeleo za Jeshi la Magereza Nchini hususani mchango wa Jeshi hilo katika Uchumi wa Viwanda. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali WMNN.)

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

  MKUU wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama, amesema anachukizwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimtolea maneno machafu ovyo, Rais Dk. John Magufuli hususan kwenye mitandao ya kijamii suala ambalo linaumiza.

  Aidha amelaani vikali vitendo vya matukio ya baadhi ya watu kuwavamia na kuwashambulia kwa risasi viongozi. Pamoja na hayo ,Assumpter hakusita kukemea tabia ya utekaji wa watoto na kisha kupoteza maisha yao ikiwemo tukio lililotokea wiki iliyopita huko Kongowe Kibaha.

   Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na matukio yanayoendelea katika maeneo mbali mbali  alisema, anasikitishwa kuona vitendo kama hivyo vinaendelea kufanyika katika jamii ya watanzania hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kwa wananchi na baadhi ya viongozi kuishi  wakiwa katika hali ya hofu.

  Assumpter alisema kuwa baadhi ya watu kwa sasa  wamekuwa wakiamua kumtolea maneno machafu kiongozi wa nchi bila ya kufahamu kuwa ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi. Alieleza vitendo na tabia kama hiyo haifai hata kidogo katika jamii na badala yake watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo na nchi yao.

  Assumpter alibainisha kwamba, Rais Magufuli anafanya mambo Makubwa tangu kaingia madarakani na kupigania maslahi ya nchi. Alisema kikubwa ni kumuunga mkono na sio kumkebehi na kumtolea maneno machafu ambayo hata nchi na mataifa mengine watabakia kutushangaa.

  "Rais Magufuli anapambana na wabadhilifu, raslimali za taifa ikiwemo madini na maslahi ya taifa kijumla "

  Assumpter alisema, fedha nyingi zilikuwa zikipotea mikononi mwa baadhi ya watumishi wasiowaminifu ambapo yeye ameweza kurejesha mapato, kodi na fedha za wananchi zilizokuwa zikiliwa na wachache kwa maslahi ya matumbo yao.

  “Nachukizwa sana na kuona matukio mbali mbali yaiendelea hapa nchini, kama vile watoto kutekwa nyara, baadhi ya viongozi kupigwa risasi kwa kweli hii sio sahihi huku wengine kutoa maneno machafu kwa kiongozi wetu wa nchi kwa hili mimi nalaani vikali"

  “Napenda kuchukua fursa hii pia kumpa pole mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu kwa kuvamiwa na kushambuliwa na risasi za moto  na kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana"

  "Huyu Tundu Lissu ni kiongozi mkubwa na ni mtu maarufu Tanzania lakini kitendo cha kushambuliwa na risasi sio kizuri na mimi namwombea kwa mungu apone na arudi kuendelea na majukumu yake ya kuwatumikia wananchi wa jimbo lake,”alisema Assumpter .

  0 0

  Mkadiriaji majenzi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara, Qs. Judith Aron, akizungumza na wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita wa Shule ya Sekondari Mahiwa iliyopo kata ya Nyango mkoani Lindi, kuhusu faida za usomaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
  Wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita wa Shule ya Sekondari Mahiwa iliyopo kata ya Nyango mkoani Lindi, wakimsikiliza mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara, Bi Liberatha Alphonce (hayupo pichani), wakati akiwasilisha mada ya umuhimu wa masomo ya sayansi na hisabati kwa Taifa na Dunia kwa ujumla.
  Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara, Bi. Liberatha Alphonce, akifafanua jambo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Mtama iliyopo mkoani Lindi wakati akitoa mada kuhusu uhamasishaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa wasichana.
  Mwanafunzi pekee wa kike wa kidato cha nne anayesoma masomo ya Sayansi, Saumu Abdallah, akitoa maoni yake kwa Wahandisi wa kike kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara kuhusu changamoto zinazokabili shule yao.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mtama mkoani Lindi, Bi. Asha Namjupa, akisisitiza jambo kwa Wahandisi wa kike kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara kuhusu mipango walionao katika kuhamasisha wanafunzi wa kike kusoma masomo ya Sayansi na Hisabati.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini zikiwemo wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.

  Amesema Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

  Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumatano, Septemba 20, 2017) alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Chemba na Kondoa waliomsimamisha katika maeneo ya Chemba, Kalema, Bicha na Bereko akiwa njianu kuelekea mkoani Arusha kwa shughuli za kikazi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Chemba mkoani Dodoma wakati alipolazimika kusimama baada ya kuona umati mkubwa wa wananchi hao waliokuwa wakimsubiri alipokuwa akisafiri kwa Barbara kwenda Arusha akitoka Dodoma Septemba 20, 2017.

  Alisema kwa sasa Serikali imeendelea na uchumbaji wa visima virefu, vifupi pamoja na kuweka mtandao wa mabomba ya kusamba maji katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo na ya wilaya hizo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo karibu na makazi yao.

  Pia Waziri Mkuu alisema wananchi wanatakiwa wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60 ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.

  Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wawachukulie hatua watu wote watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa makazi na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa zinasababisha ukame.

  Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa nishati ya umeme, Waziri Mkuu alisema hakuna kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa huduma hiyo katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kalema wilayani Chemba wakati alipolazimika kusimama baada ya kuona umati mkubwa wa wananchi hao waliokuwa wakimsubiri alipokuwa akisafiri kwa Barbara kwenda Arusha akitoka Dodoma Septemba 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Ameagiza wakandarasi wamalize maeneo yaliyosalia katika REA awamu ya pili ndipo waendelee na awamu ya tatu. Alisema Serikali imetenga sh. trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo.

  “Rais wetu Dkt. John Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na vya wilaya za Chemba na Kondoa. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

  Pia Waziri Mkuu alisema  mwananchi hawatowajibika tena katika kulipia nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

  Waziri Mkuu aliongeza kwamba  lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi.

  Awali mbunge wa Chemba, Bw. Juma Nkamia, Mbunge wa Kondoa Mjini Bw. Edwin Sanda na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji ambaye ni Mbunge wa Kondoa Vijijini waliomba Serikali iwasaidie katika kutatua kero ya maji na umeme.

  Walisema katika maeneo mbalimbali ya majimbo yao wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya umeme pamoja na maji safi na salama hivyo kusababisha wananchi kushindwa kushiriki vema kwenye shughuli za kimaendeleo.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel ambayo inajenga jengo la bweni na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Misitu Olmotonyi kuhusu maendeleo ya mradi huo alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe kumaliza ujenzi wa mradi huo.

  Na Hamza Temba - WMU
  .................................................................
  Chuo cha Misitu Olmotonyi kilichopo mkoani Arusha kimetakiwa kuboresha taaluma na mitaala ya kufundishia iweze kukidhi mahitaji ya jamii ya sasa na ijayo ikiwemo kujibu kero na changamoto zinazoikabili jamii hiyo.  Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipotembelea chuo hicho jana kwa ajili kukagua maendeleo yake na kuzungumza na waalimu pamoja na wafanyakazi ambapo pia alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayojengwa chuoni hapo ikiwemo ya bweni na ukumbi wa mihadhara.  Alisema Tanzania ya leo inahitaji wataalamu watakaojibu kero na kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya uhifadhi nchini ikiwemo ya uharibifu wa misitu kwa njia ya uchomaji wa mkaa, uvunaji haramu wa magogo na vitendo vya uingizaji wa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi nchini. 

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimpa maelekezo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel (kushoto) ambayo inajenga mradi wa bweni na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Misitu Olmotonyi alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe kumaliza ujenzi wa mradi huo.

  "Ni lazima muwafundishe wanafunzi wenu uaminifu na uzalendo wa kutumia rasilimali za misitu kwa njia endelevu, muwafundishe uhifadhi zaidi na sio uvunaji pamoja kutumia sheria ipasavyo katika kulinda na kusimamia rasilimali hizi huku wakitambua kuwa rasilimali hizo zikitoweka hakuna maisha kutokana na umuhimu wake katika maisha ya binadamu" alisema Prof. Maghembe.

  Pamoja na hayo, alikitaka chuo hicho kujiimarisha zaidi katika mafunzo kwa vitendo kufikia viwango bora vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na kuendeleza waalimu kitaaluma kwa kutumia fursa mbalimbali ikiwemo za mafunzo ya nje ya nchi kwa mfumo wa "Scholarships". 

  Aidha, alikitaka pia chuo hicho kujikita zaidi katika utoaji wa huduma kwa jamii katika sekta ya misitu pamoja na kuanzisha na kuimarisha programu mbalimbali za utafiti ambazo pamoja na faida nyingine pia zitakitangaza chuo hicho ndani na nje ya nchi.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na waalimu na wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi mkoani Arusha jana . Kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Christognus Haule.

  Katika hatua nyingine, Prof. Maghembe amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel kukamilisha haraka ujenzi unaoendelea wa jengo la bweni na ukumbi wa mihadhara chuoni hapo. Ujenzi huo upo chini ya mradi wa ECOPRC na jengo la bweni litakua na uwezo wa kuchukua wanafunzi 100 na ukumbi wa mihadhara wanafunzi 200. 

  BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tukuyu, Ezekiel Manyemele, wakifunua kitambaa kuzindua Jengo la Choo cha wanawake katika Hospitali ya Makandana Wilayani Rungwe, jana Sept 20, 2017. Jengo hilo la Choo limegharimu zaidi ya Sh. milioni 50.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akipanda mti na Mwanafunzi wa darasa la Sita wa Shule ya Msingi Segera, Tunza Fred, wakati alipotembelea shule hiyo kukabidhi Vifaa vya ukarabati wa shule hiyo akiwa katika ziara yake Wilaya ya Rungwe jana Sept 20, 2017. Jumla ya miti 160 ilipandwa katika shule hiyo ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akimkabidhi tofali, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Segera, Fred Mfwea (wa pili kulia) na Diwani wa Kata ya Segera (katikati) wakati alipotembelea shuleni hapo kukabidhi Vifaa vya ukarabati wa shule hiyo akiwa katika ziara yake Wilaya ya Rungwe jana Sept 20, 2017.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akicheza muziki 'Ndiyo Maana Tenzele' wa asili wa kabila la Wasafa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Unyamwange, Julius Pascal, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya akiangalisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha afya Kata ya Isongole jana sept 20,2017. tofali.Picha na Muhidin Sufiani.

  0 0

  DAR ES SALAAM
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Amina Makillagi, amewataka wagombea na wajumbe wote wa mikutano mikuu ya wilaya kwenye Uchaguzi wa jumuiya hiyo ngazi ya wilaya utakaofanyika leo, tarehe 21/9/2017 kuzingatia maadili ya Chama na UWT.


   "Kubwa ni kutotoa wala kupokea rushwa. UWT imejiandaa vizuri kuhakikisha inafuatilia nyendo zozote ovu zitakazojitokeza katika Uchaguzi. Mgombea yeyote atakayetoa rushwa atachukuliwa hatua za kinidhamu kabla na baada ya Uchaguzi kuisha ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nafasi ya uongozi iliyopatikana kwa mazingira tatanishi", amesema Makilagi.   Makillagi ambaye amewatakia uchaguzi mwema wanachama wote wa UWT, amesisitiza kuwa rushwa haitavumilika na kwa mjumbe yeyote atakayepokea rushwa na kwamba kanuni zilizopo zitamuwajibisha ipasavyo.

  0 0
 • 09/21/17--01:10: KUMBUKUMBU
 • MAREHEMU CASSIUS O. MDAMI 

   Tangu umetuacha tumetafakari mengi tukidhani umesafiri utarudi lakini kumbe haikuwa hivyo. Kuwa kwako mbali na familia kumetufanya kujifunza mengi kuhusu maisha na kutafakari muda ambao tulikuwa pamoja katika maisha ya hapa duniani wakati wa furaha na uchungu. Unakumbukwa na mke wako Rose na watoto wako Martina, Grace, Gideon, Gonsalver na Gibson. 

  Umetimiza mwaka sasa tangu umetuacha; pengo lako ni kubwa katika kila kona ya maisha na hata katika Tasnia ya Habari uliyoitumikia katika muda mwingi wa maisha yako kwa kutuonyesha kwa vitendo maana ya kuipenda na kuithamini kazi katika maisha. 

  Tumekosa simulizi za kusisimua za Utalii wa Ndani, ulichimba na kuchimbua mengi ambayo kama si kwa jitihada zako binafsi tusingeyajua kamwe… tumebaki na msemo wako maarufu “Falsafa ya Ufagio ni Unyenyekevu”. 

  Faraja yetu ni Mungu aliye Baba wa Yatima na mume wa Wajane (Kutoka 22:22-24). Tunaamini katika Ufufuo na Uzima na siku moja tutafurahi nawe mbinguni (Yohana 11:25-26). 

  Mungu akupe pumziko la Milele, upumzike kwa Amani - Amina

  0 0

  Waomboleaji wakiwemo ndugu,jamaa na marafiki wakiwa wamebeba jeneza ambalo lina mwili wa Kaka yake Mufti wa Tanzania,Shekhe Saad Zubeiry Ally ambaye amefariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam wakijiandaa kuliingiza kaburini wakati wa mazishi yaliyofanyika jana (Septemba 21) kwenye makaburi ya familia eneo la Kwamndolwa wilayani Korogwe Mkoani Tanga.
  Mufti wa Tanzania Shekhe Aboubakar Zubeir katika akizungumza wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika katika eneo la Kwamndolwa wilayani Korogwe Mkoani Tanga.
  Mufti wa Tanzania Shekhe Aboubakar Zubeir kulia akiteta jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu wakati wa maziko ya kaka yake Mufti yaliyofanyika kwenye eneo la Makaburi ya familia eneo la Kwamndolwa wilayani Korogwe kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira,January Makamba wakati wa maziko hayo.


  0 0

   Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeandaa tamasha la kimataifa la 36 la Sanaa na Utamaduni litakalofanyika Septemba 23 hadi 30 katika viwanja vya TaSUBa mjini Bagamoyo mkoani pwani.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Dk. Herbert Makoye amesema Tamasha la Kimataifa la 36 kwa mwaka huu litakuwa la kipekee kutokana na kupiga vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya ambayo dunia inapambana nayo.

  Dk. Makoye amesema kaulimbiu ya ya Tamasha hilo ni “Sanaa na Utamaduni katika Kupiga Vita Madawa ya Kulevya” ikiwa ni mahsusi katika kuunga mkono mapambano ya vita dhidi ya usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya hapa nchini.
  Tamasha la Kimataifa Sanaa na Utamaduni Bagamoyo hufanyika kila mwaka na huandaliwa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ikiwa na malengo ya Kutunza na kuenzi sanaa na utamaduni wa Mtanzania, Kutengeneza jukwaa ambalo wanafunzi wa Tasuba wanalitumia kupima kiwango chao cha umahiri katika sanaa kwa mwaka katika fani za sanaa za maonyesho na zile za ufundi.

  Amesema malengo mengine ya tamasha Kukutanisha watu wa tamaduni mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali za dunia ili kuonyesha utajiri wao wa sanaa na utamaduni, Kutengeneza jukwaa ambalo ni kiungo cha kujenga mahusiano ya wasanii wa ndani na nje ya nchi kupitia maonyesho ya sanaa na pia kubadilishana uzoefu na mawazo katika kuendeleza tasnia ya sanaa.

  Aidha amesema tamasha la mwaka huu linafanyika kwa mara ya 36 na litapambwa na ngoma za asili, muziki, sarakasi na maigizo pamoja na maonyesho ya sanaa za ufundi. Pia kutakuwa na warsha na semina zitakazohusu mambo mbalimbali ya kijamii. Jumla ya vikundi vya Sanaa 68 vimethibitisha kushiriki na kati ya hivyo vikundi Saba ni kutoka nje ya nchi (Kenya, Ufaransa, Korea Kusini, Uingereza, Zimbabwe na Mayyote).

  Mgeni rasmi wa ufunguzi wa tamasha hilo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dk Harrison Mwakyembe (Mb), wakati Ufungaji wa Tamasha utafanyika na Naibu Spika Dk. Tulia Ackson.
  Kampuni ya Michuzi Media Group ni moja ya wadhamini wa kufanikisha tamasha hilo la Kimataifa la 36
  Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dk. Herbert Makoye (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza tamasha la kimataifa la 36 taasisi hiyo litakalofanyika mjini Bagamoyo , kushoto ni Mwenyekiti wa Tamasha, John Mponda , wa pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Rodney Thadeus kulia ni Afisa habari wa TaSUBa, Sophia Mtakasimba

  0 0

  Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii,Kigoma

  MASHIRIKA 16 ya umoja wa Mataifa yamezindua programu ya pamoja mkoani Kigoma, ikiwa ni mpango wa pamoja utakaohusisha sekta mbalimbali kwa lengo la kuimarisha maendeleo na usalama kwa watu wa Kigoma.

  Akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi wa programu hiyo iliyofanyika katika viwanja vya soko la pamoja lililopo katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilayani Kasulu ,Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Paranjo alisema kuwa mpango wa programu ya pamoja utatumia njia kamilifu kutatua masuala mbalimbali yanayowakabili wakimbizi,wahamiaji pamoja na jamii za wenyeji wanaoishi Mkoa humo.

  Paranjo alisema kuwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma wamekuwa wakiishi na wakimbizi kwa kipindi cha muda mrefu hivyo kupitia programu hiyo na wao watanufaika.Alisema ingiwa programu hiyo ilianza Julai 1 2017 lakini uzinduzi rasmi umefanyika leo pia mpango huu utadumu kwa muda wa miaka minne.

  Mkuu wa mahusiano kutoka ubalozi wa Norway Trygue Bendiksy alisema kuwa mpango huo una bajeti ya dola za kimarekani milioni 55,ambapo mpaka sasa kiasi cha dola milioni 12 kati ya hizo tayari zimeshapatikana hivyo aliwaomba wadau kuendelea kujitokeza kusaidia ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa katika programu hiyo.

  Alisema mashirika hayo 16 ya umoja wa mataifa katika programu hiyo watashirikiana katika nyana za nishati na mazingira endelevu,uwezeshwaji wa kiuchumi wa vijana na wanawake,vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,elimu inayolenga wasichana wenye umri wa kuvunja ungo,maji safi pamoja na kilimo.

  Mkuu wa kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Abiudi Saidaye alisema hivi sasa kambini hiyo ina jumla wakimbizi na waomba hifadhi 143608 kutoka nchi ya Burundi na Congo.Alisema mpango wa programu wa pamoja ya Kigoma utasaidia kutatua masuala mbalimbali yanayowakabili wakimbizi ikiwa ni sambamba na kuwaendeleza kimaendeleo.

  Rais wa wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu Abilola Angelique kwa niaba ya wakimbizi na waomba hifadhi wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na umoja wa Mataifa kwa kitendo cha kuwapokea na kuwahudimia kwa kipindi chote walichokuwa nchini. 
   Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Paranjo wakifurahi na baadhi ya wawakilishi wa mashirika ya umoja wa Mataifa baada ya kuzindua programu ya pamoja ya Kigoma
   Wawakilishi wa shirika la FAO wakishirikiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma wakikabidhi zana za kilimo wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu kwaajili ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya Kigoma
   Wawakilishi wa shirika la kimataifa la UNESCO wakikabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa utekelezaji wa programu ya pamoja Kigoma. 
  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa programu ya pamoja Kigoma Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Charles Paranjo akisoma risala yake kwenye viwanja vya soko la umoja katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilayani Kasulu. 
   Rais wa kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilayani Kasulu Abilola Angelique akiongea neno la shukrani baada ya uzinduzi wa programu ya pamoja ya Kigoma
   Kikundi cha ngoma ya asili kutoka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wakitumbuiza ngoma ya asili ya kabila la warundi wakati wa uzinduzi wa programu ya pamoja ya Kigoma

older | 1 | .... | 1919 | 1920 | (Page 1921) | 1922 | 1923 | .... | 3285 | newer