Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1918 | 1919 | (Page 1920) | 1921 | 1922 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Mary Gwera, Mahakama

  Mwakilishi ‘Practice Manager’ kutoka Benki ya Dunia (WB), Bw. George Larbi ameisifu Mahakama kwa utekelezaji wake wa Mradi wa Maboresho wa huduma za Kimahakama.

  Bw. Larbi aliyasema hayo mapema Septemba 19, alipokutana na Mhe. Jaji Mkuu ofisini kwake Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam ambapo alipata nafasi ya kuongea na Mhe. Jaji Mkuu na Viongozi wengine wa Mahakama akiwemo Mtendaji Mkuu na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

  “Mradi huu unaotekelezwa na Mahakama ni mradi wa mfano ambapo mafanikio yake yanatarajiwa kuigwa nan chi nyingine,” alisema Bw. Larli.

  Bw. Larli ambaye amewasili nchini kutokea Washington D.C zilipo ofisi cha Benki ya Dunia amefanya ziara yake kwa lengo la kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Benki ya Dunia (WB).

  Alisema Mradi huu unaotekelezwa na Mahakama ni Mradi wa pili kwa nchi za Afrika ambapo Benki ya Dunia inashirikiana moja kwa moja na Mahakama katika kuboresha huduma ya utoaji haki.

  Maeneo muhimu yanaotekelezwa na Mradi wa Benki ya Dunia (WB) ni pamoja na; Mapambano dhidi ya Rushwa; ni kwa jinsi gani Mahakama pamoja na wadau wengine wanaweza kushirikiana katika kupiga vita vitendo vya rushwa.Maeneo mengine ni ushirikishaji wa wadau katika masuala yote ya utoaji haki na kusogeza huduma ya utoaji haki karibu na wananchi.
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibarhim Hamis Juma (kulia) akiongea neno na Bw. George Larbi kutoka Benki ya Dunia (katikati) wa kwanza kushoto ni Bw. Denis Biseko 'Co-Team Task Leadear' wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Kimahakama.
   Bw. George Larbi, kutoka Benki ya Dunia (WB) (katikati) akiongea na Mhe. Jaji Mkuu (kulia).

   Mhe. Jaji Mkuu (aliyeketi wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Wageni kutoka Benki ya Dunia (wawili walioketi katikati) wa tatu kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, wa pili kushoto ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mradi wa Maboresho wa Huduma za Mahakama, Mhe. Zahra Maruma.

   Ukaguzi: Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Mahakama cha Mahakama-Kisutu unaojengwa kwa fedha za Benki ya Dunia Bw. George Larbi kutoka Benki ya Dunia pia alipata fursa ya kutembelea Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Mahakama unaofanyika katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa sasa kazi ya upakaji rangi katika jengo hilo inaendelea.
   Mafundi wakiendelea na kazi ya upakaji rangi katika jengo la Kituo cha Mafunzo linalojengwa Kisutu-Dar es Salaam (Picha na Mary Gwera, Mahakama) 

  0 0

  Na Fredy Mgunda,Iringa.

  Halmashauri ya wilaya ya Iringa imetumia shilingi milioni mia moja na tisini (190,000,000 ) kupambana na tatizo la milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu katika tarafa ya pawaga na Idodi mkoani Iringa na ni miongoni mwa halmashauri 156 zinazotekeleza kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira Tanzania bara.

  Akizungumza wakati wa utoaji elimu ya matumizi ya vyoo bora katika tarafa ya pawaga afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya aliwataka wananchi kuanza kutumia vyoo bora ili kumaliza tatizo la milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu ambao umekuwa ukiwakumba mara kwa mara.

  “Jamani chanzo mmoja wapo cha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ni matumizi ya vyoo ambavyo sio bora hivyo mnatakiwa kutumia vyoo bora na kutoa elimu kwa wananchi wenu maana nyinyi ndi wenye wananchi na leo tunawapa hii elimu nyie viongozi tunaomba muifikishe elimu kwa wananchi”alisema Nkya

  Nkya alisema walitoa elimu ya uboreshaji wa miundombinu ya vyoo na kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka kwa sabuni mara ya kutoka chooni kwa ngazi ya kaya na shule za msingi na sekondari,Vyuo,taasisi za kidini,taasisi binafsi,taasisi za kiserikali kama ofisi za serikali na vituo vya afya lengo likiwa ni kutokomeza kabisa ugonjwa wa kipindupindu.


  Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akizungumza na viongozi wa vijiji wa tarafa ya pawaga kuhusu uboreshaji wa vyoo bora kwa lengo la kutatua tatizo la ugonjwa wa kipindupindu ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika tarafa hiyo walianza kutoa elimu kwa viongozi wote na baadae wakahamia kwa wananchi.
  Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akizungumza na mama moja ambaye hana choo bora na kutundikiwa bendera ilikuwa inamuonyesha kuwa hana choo bora katika kijiji cha mboliboli tarafa ya pawaga mkoani Iringa.
  Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akisimamia zoezi la utundikaji wa bendera kwa wasio na vyoo bora.


  0 0

  Mamia ya wadau wa sanaa wamejitokeza kwa wingi Jumanne hii jioni katika Uwanja wa ndege wa JK Nyerere jijini Dar es salaam kumuaga msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto ambaye ameelekea nchini China kwaajili  ya kuiwakilisha Tanzania katika tamasha la utalii wa sanaa duniani.

  Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo, Kitendawili alitangaza katika mitandao yake ya kijamii kwamba atasafiri Jumanne hii kuelekea nchini China hali iliyopelekea mashabiki wengi kumimika uwanjani hapo kwaajili ya kumuaga.

  Akiongea na waandishi waliojitokeza uwanjani hapo, Mpoto alisema anawashukuru mamia ya watu waliojitokeza uwanjani hapo kwaajili ya kumuaga kwenda kuiwakilisha nchi katika masuala ya kiutalii nchini China.

  “Sikutegemea kama watu watakuwa wengi hivi, huu ni upendo wa dhati sana na nawashukuru sana kwa moyo huo na upendo mliouonyesha, nakwenda China kwaajili ya Watanzania, sio Mpoto lakini nakwenda kuuonyesha ulimwengu kwamba Tanzania tuna utajiri wa sanaa, Tanzania tuna makabila zaidi ya mia moja na ishirini hiki ni kitu kikubwa sana, tunaenda kuwatambia usalama tuliokuwa nao,” alisema Mrisho.

  Muimbaji huyo amedai haikuwa kazi rahisi kupata kazi hiyo na kuwa muakilishi pekee wa Tanzania kwenye maadhimisho hayo ya utalii duniani ambayo yanawakutanisha mataifa mbalimbali duniani.

  Aliongeza, “Mungu bado anaendelea kutuona, kati ya nchi zote za Afrika ni nchi tatu tu ambazo zimepata mualiko huu ikiwemo Tanzania na Kenya. Hii ni ishara nzuri sana duniani na Afrika nzima kwa sababu wadau ambao watatembelea mahadhisho hayo washuhudia vitu vyetu vya asili, ngoma, nyimbo, ala za muziki pamoja na mitindo mbalimbali ya upigaji wa ngoma,”

  Alisema safari hiyo imewezeshwa na  Ubalozi wa Tanzania China, Wizara ya Utamaduni, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, TANAPA, TTB, BASATA pamoja na Leopard Tours.

  0 0  0 0

  Na Karama Kenyunko.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtaka aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake wawili kuwa na imani pamoja na subira dhidi ya upelelezi wa kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili kwa kuwa unakaribia kufika mwisho.

  Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema hayo  leo asubuhi kesi hiyo ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa huku upande wa Jamhuri ukidai kuwa upelelelezi bado haujakamilika.

  Kabla ya Hakimu Mkeha kusema hayo, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali Mutalemwa Kishenyi ulidai kuwa, mara ya mwisho kesi hiyo ilipotajwa waliomba siku 14 ili waweze kuelezea Hali ya upelelezi dhidi ya kesi hiyo lakini muda walioomba haujawatosha kukamilisha malengo hayo hivyo wakaomba kuongezewa siku 14  ili kukamilisha na waje kueleza hali ya upelelezi.

  "Mheshimiwa tunafanya jitihada kuona upelelezi unakamilika, tunaomba tuongezewe muda wa siku 14" amedai Kishanyi.

  Hata Hivyo jopo la mawakili wa utetezi likiongozwa na wakili Masumbuko Lamwai amedai "kesi hiyo imekuwa kama ya kukomoana komoana", akaongeza kudai kuwa, Wateja wao wamekaa gerezani kwa takribani mwaka mmoja na nusu kwani kwa mujibu wa hati ya mashtaka washtakiwa walifikishwa mahakamani Aprili Mosi mwaka jana.

   Amedai uchunguzi katika mashtaka dhidi ya Wateja wao unahusu nyaraka ambazo upande wa mashtaka wanazo na hakuna uchunguzi zaidi ya nyaraka.

  "Shtaka la utakatishaji wa fedha dhidi ya washtakiwa limewekwa kwa makusudi ili washtakiwa waendelee kukaa gerezani, kwa mtu aliyekaa gerezani kwa takribani mwaka mmoja na nusu ukimwambia upelelezi bado inaleta mshangao.

  Amesema, washtakiwa ni watu wazima wanashughuli zao ambapo zingine zimefilisika kwa kukosa usimamizi, " Tunajua mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi hii lakini upande wa mashtaka wanatumia vibaya taratibu za kimahakama.

  Akijibu hoja hizo, Hakimu Mkeha amewaambia washtakiwa kuwa upelelezi unaofanywa unakaribia mwisho, naomba muwe na imani, nimejiridhisha Mimi Jana kwa macho yangu kuwa upelelezi unakaribia kufika mwisho, tuwe na subira. Amesema Mkeha

  Kitilya na wenzake, aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na Sioi Solomon wanashtakiwa kwa utakatishaji wa fedha dola milioni 6.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Octoba 5, 2017.

  0 0  0 0


  Walimu wa masomo ya Sayansi mkoani Lindi wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka za kuandaa na kuimarisha miundombinu bora kwa shule za Sekondari zinazofundisha masomo hayo ili kuendeleza na kufufua vipaji vya wanafunzi.

  Akizungumza kwa niaba ya walimu hao wakati wa ziara iliyofanywa na wahandisi wa kike kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kupitia Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara katika shule za mkoa huo,   Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mchinga iliyopo  mkoani humo, Bw. Makopa Selemani , amesisitiza kwa Serikali kuona namna ya kujenga maabara  nyingi za sayansi ambazo zitakuwa na vifaa na kuongeza walimu wa Sayansi ambao wameonekana kuwa ni wachache katika mkoa huo.

  "Tunaiomba Serikali kutazama kwa jicho la pekee shule za mkoa huu hususan zenye michepuo ya sayansi kwani si kwamba wanafunzi hawapendi masomo haya bali miundombinu hairidhishi", amesema Mwalimu Mkuu.
  Aidha, Mwalimu Mkuu ameongeza kuwa ili kuwasaidia wanafunzi wa kike katika mkoa huo serikali iwajengee mabweni wanafunzi hao ili kuepusha kupata vishawishi kwani wengi wao wanaishi mbali na shule.

  Mwalimu Mkuu Selemani, ameelezea baadhi ya mikakati ya shule yake katika kuhamasisha wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi ikiwemo kufanya vikao vya mara kwa mara na wanafunzi hao ili kujadili changamoto zao na kuzitatua.
   Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara, Bi. Liberatha Alphonce, akionesha mfano wa picha iliyochorwa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mchinga mkoani Lindi (hawapo pichani), ili kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.
   Wahandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara, wakisikiliza maoni kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mchinga mkoani Lindi walipotembelea shule hiyo kuhamasisha usomaji wa masomo ya Sayansi kwa wasichana.
   Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mchinga mkoani Lindi, wakionesha ndoto zao kwa Wahandisi wa kike kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara, walipotembelea shule hiyo kuhamasisha usomaji wa masomo ya Sayansi kwa wasichana.
  Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara, Bi. Rahma Mwinyi, akigawa zawadi ya madaftri kwa wanafunzi wa shule ya Mkonge mkoani Lindi ili  kuhamasisha wanafunzi  hao kupenda masomo ya sayansi.


  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipokea taarifa ya utendaji kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alipofanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Pwani kwa lengo la kuangalia namna zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma lilivyofanyika.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akitoa maelekezo wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuangalia namna zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma lilivyofanyika.
   Baadhi ya watendaji wa Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuangalia namna zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma lilivyofanyika.
  0 0

  Na Tiganya Vincent.

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amefanikiwa kumaliza mgogoro kati ya waliokuwa wafanyakazi 11 wa Kampuni ya Ujenzi ya Ceytun iliyokuwa ikipanua Uwanja wa Ndege wa Tabora na wamiliki wake juu ya kulipwa madai ya malipo ya muda wa ziada na mapunjo ya mishahara.

  Mgogoro huo ulimalizika jana mjini Tabora baada ya Wamiliki wa Kampuni hiyo kukubali na kulipa madeni ya wafanyakazi wake ambapo  malipo yalifanyika mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Mkuu wa Wilaya ya Tabora.
  Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuamuru kuwang’anywa Hati za kusafiria za viongozi wake wawili wa Kampuni hiyo na kuzuiwa kwa vifaa vyake vya  ujenzi baada ya kuonekana kuwa anataka kuondoka bila kulipa malipo ya wafanyakazi hao.

  Akizungumza mara baada ya Kampuni hiyo kuwalipa waliokuwa  wafanyakazi wake Mwanri alisema kuwa amelizika na kazi iliyofanyika na hivi sasa wanaweza kuchukua hati zao za kusafiria na wako huru kuondoa vifaa vyao vya ujenzi kwa sababu wamemalizana na watumishi hao bila kinyongo.

  Aliomba Kampuni hiyo ikipata kazi nyingine isisite kuwapa ajira waliokuwa wafanyakazi wake licha ya mvutano uliotokea na kuongeza kuwa kilichotekea ndio mwanzo wa kuboresha mahusiano katika siku za baadaye.
  Mwanri alisema kuwa uungwana waliouonyesha kukabali kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao na waliokuwa wafanyakazi wao umeonyesha ni Kampuni inayostahili kuendelea kupewa kazi nyingine hapa nchini.

  Aliwataka kutofunga milango kwani inawezekana wapo waliokuwa wafanyakazi wao ambao walisahaulika na wameshaondoka na pindi watakapokuja na vielelezo vinavyoonyesha kuwa bado wanadai basi wasaidiwe na walipwe haki zao.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  WAWEKEZAJI katika sekta ya kilimo na mifugo wamelalamikia ushindani unaoletwa na bidhaa kutoka nje kutokana na serikali kushindwa kuzidhibiti kwa njia ya kupunguza kodi na tozo mbalimbali katika uzalishaji.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wawekezaji hao ambao pia ni sehemu ya wabia wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo, Maji na Umwagiliaji katika Kongani ya Ihemi mkoani Iringa na Njombe, walisema ipo haja serikali ikaangalia suala hilo kwa jicho pana ili kulinda bidhaa za ndani.

  Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha ASAS Dairies Limited kilichopo mkoani hapa, Bwana Fuad Abri alisema haiwezekani Tanzania iwe nchi ya pili kwa idadi ya ng’ombe barani Afrika baada ya Ethiopia lakini bado inapitwa katika uzalishaji na uingizaji maziwa nchini.

  “Wenzetu Kenya wanazalisha lita 1,500,000 za maziwa kwa siku lakini Tanzania inazalisha lita 120,000 kwa siku. Wakati huohuo sisi tunawapita kwa umbali katika idadi ya ng’ombe, kama hiyo haitoshi bidhaa za maziwa kutoka mataifa jirani zinaingia kwa wingi na kutoa ushindani mkubwa na bidhaa za ndani,” alisema Bw. Abri.

  Alisisitiza kuwa zipo namna nyingi za kuzuia ushindani huu kwa sababu Serikali ya Kenya inashirikiana kwa kiasi kikubwa na wazalishaji maziwa na ndiyo maana wana uwezo wa kusafirisha nje kwa bei shindani.

  “Katika biashara hii ya maziwa kitu kikubwa kinachotakiwa kuangaliwa ni namna gani unapata maziwa yako, bei utakayonunulia ikupe faida lakini faida yenyewe iwe katika soko shindani,” alisema Bw. Abri.
   Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha ASAS Dairies Limited mkoani Iringa, Bwana Fuad Abri akitoa mada juu ya uendeshaji wa kiwanda chake na ubia wao na Kituo cha Kuendeleza kilimo Nyanda za juu kusini mwa Tanzania (SAGCOT) alipotembelewa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo,Mifugo , Maji na Umwagiliaji. Lengo la ziara ya Kamati hiyo ni kujionea na kujifunza juu ya Kongani ya Ihemi na shughuli za SAGCOT.
  Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha ASAS Dairies Limited, Bwana Fuad Abri (kulia)akitoa maelekezo ya uendeshaji wa kiwanda chake alipotembelewa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo,Mifugo , maji na umwagiliaji. Ikiwa ni sehemu ya ziara ya kamati hiyo kujionea na kujifunza juu ya kongani ya Ihemi na shughuli mbalimbali za Mpango wa Kuendeleza Kilimo Nyanda za juu kusini mwa Tanzania(SAGCOT). Wapili kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa Maswa Magharibi, Bwana Mashimba Ndaki. Watatu kulia ni Mjumbe wa kamati ambaye pia Mbunge wa viti Maalum Bibi Khadija Hassan Aboud. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT , Bwana Geoffrey Kirenga.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imeshindwa kuendelea kusikiliza ushahidi dhidi ya kesi ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya kazi yake, inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo na mwanahisa wa mtandao huo, Mike Mushi kwa sababu shahidi alikuwa hajaandaliwa.

  Aidha upande wa Mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa serikali, Nassoro Katuga ulidai kuwa jalada la kesi hiyo lipo Polisi, na kwamba  mawakili wa serikal wanaosikiliza kesi hiyo wanamajukumu mengine ya kikazi katika mahakama tofauti.

  Wakili Katuga amedai hayo yote mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

  Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi October 17, 2017 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

  Katika kesi hiyo, Melo na mwenzake wanakabiliwa na kosa moja la kuzuia jeshi la polisi kufanya kazi yake.

  Inadaiwa washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya Aprili 1 na Desemba 13, mwaka jana katika maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Sylvester Simfukwe (katikati)  akisisitiza jambo wakati akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya TEHAMA na Elektroniki wa wakala huo kabla ya kuwatunuku vyeti baada ya kumaliza mafunzo hayo. Kulia ni Mhandisi Aurelia Ngopa na kushoto ni mkuu wa chuo hicho Mhandis Lucius Luteganya. Mafunzo hayo yaliendeshwa katika kituo hicho kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam na yalihusisha jumla ya watumishi 15 wa TEMESA.
  Mkuu wa chuo cha VETA Kipawa ICTC Mhandisi Lucius Luteganya (wa pili kushoto aliyesimama) akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya TEHAMA na Elektroniki kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) waliofuzu mafunzo hayo katika zoezi la kuwatunuku vyeti lililoandaliwa na Kituo hicho. Mafunzo hayo yaliendeshwa katika kituo hicho kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam na yalihusisha jumla ya watumishi 15 wa TEMESA.
   Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya TEHAMA na Elektroniki kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wakisubiri kukabidhiwa vyeti vyao mara baada ya kumaliza mafunzo hayo katika chuo cha VETA Kipawa ICTC. Mafunzo hayo yaliendeshwa katika kituo hicho kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam na yalihusisha jumla ya watumishi 15 wa TEMESA.
   Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Sylvester Simfukwe akimkabidhi cheti cha kuhitimu mfanyakazi wa wakala huo Jane Wilson Sawala mara baada ya kuhitimu mafunzo ya TEHAMA na Elektroniki katika chuo cha VETA Kipawa ICTC. Wa kwanza kulia anayetazama ni Mhandisi Aurelia Ngopa. Mafunzo hayo yaliendeshwa katika kituo hicho kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam na yalihusisha jumla ya watumishi 15 wa TEMESA.
   Wahitimu waliofuzu mafunzo ya TEHAMA na Elektroniki katika chuo cha VETA Kipawa ICTC wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Sylvester Simfukwe (katikati aliyekaa) mara baada ya kutunukiwa vyeti vyao baada ya kumaliza mafunzo hayo. Kulia aliyekaa ni Mkuu wa chuo hicho Mhandisi Lucius Luteganya na kushoto ni Mhandisi Aurelia Ngopa. Mafunzo hayo yaliendeshwa katika kituo hicho kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam na yalihusisha jumla ya watumishi 15 wa TEMESA.

  Na Alfred Mgweno, TEMESA
  Jumla ya watumishi 15 kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), jana (Septemba 19, 2017) wamehitimu mafunzo ya TEHAMA na Elektroniki kutoka katika Chuo cha TEHAMA VETA   (Kipawa Information and Communication Technology Center) kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yalihusisha watumishi kutoka mikoa ya Dodoma, Kigoma, Njombe pamoja na Dar es Salaam. 

  Akizungumza katika sherehe za Mahafali hayo, Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Sylvester Simfukwe , alitoa wito kwa wahitimu hao kuhakikisha wanautumia ujuzi walioupata chuoni hapo kuundeleza wakala kutoa huduma kwa ufanisi mkubwa  unaoendana na mabadiliko ya kiteknolojia na pia kuwa mabalozi wazuri popote watakapokwenda.

   “Lengo la kuwaleta kwenye mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa mnaendana na mabadiliko ya teknolojia inayobadilika kila wakati na pia kuwafanya muwe wabunifu wa mifumo mipya kila inapotokea”
  Aidha, Mhandisi Simfukwe,  alimshukuru Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi Lucius Luteganya kwa mapokezi mazuri aliyowapatia watumishi wa wakala  pamoja na kukubali kuwapa mafunzo hayo pamoja na wakufunzi kwa ushirikiano waliouonyesha kwa wahitimu hao, pia aliwahimiza waendelee kutoa mafunzo kwa weledi na ubunifu,kwa Watanzania wanaofanya nao kazi, ili kuongeza wajuzi wa fani hizo za TEHAMA.

  Kwa upande wake, Mkuu wa chuo hicho, Mhandisi Lucius Luteganya, alitoa historia ya Kipawa ICTC, na kusema kuwa, Serikali iliamua kuwekeza katika Kituo hicho kwa malengo ya kutoa mafunzo ya TEHAMA na kukifanya chuo hicho kua kisima cha taaluma na ujuzi hapa nchini. 

  Mafunzo hayo yalihusisha Usambazaji wa mifumo ya nyaya, Uunganishaji wa nyaya za kubebea mifumo ya TEHAMA, Mpangilio wa vifaa vya kielektroniki vya kuzuia uingiaji kwenye jengo, Kamera za ulinzi, Mifumo ya mawasiliano isiyotumia nyaya, Mfumo wa mahudhurio wa kielektroniki, Mfumo wa mawasiliano ya kitoa nakala, Viashiria vya moto pamoja na Vizimia moto.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 20 Septemba, 2017 ameondoka jijini Dar Es salaam kuelekea mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi.

  Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA,Rais Dkt. Magufuli ataanza ziara yake Mkoani Manyara kwa kufungua barabara ya Kia - Mererani yenye urefu wa kilomita 26, na kuzungumza na wananchi wa mkoa huo.

  Tarehe 23 Septemba 2017, Rais Dkt. Magufuli atatunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

  Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar Es salaam , Rais Dkt. Magufuli ameagwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda.

  Jaffar Haniu
  Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar Es Slaam.
  20 Septemba 2017. 


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akielekea kupanda ndege kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya kikazi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akielekea kupanda ndege kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya Kikazi. PICHA NA IKULU
   

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa kwa furaha na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera alipowasili kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia maelfu ya wananchi alipowasili Mererani kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017.
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mbunge wa Simanjiro Mhe. James Ole Milya kwenye sherehe ya kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017.
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa Mererani wakati wa kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017.
  0 0

  Na. Honorius Mpangala.

  Mwalimu ni fani pana ambayo imekuwa na majina tofauti mengi ambayo hutumika katika kitendo cha kufundisha.Licha ya kuwa kama jina la fani ya kuhawilisha maarifa toka kwa anayejua kwenda kwa asiyejua. Ila yapo majina mengi katika nyanja nyingi ambayo hutumika katika matendo hayo ya kuhawilisha maarifa.

  Wako walimu wa mambo mbalimbali,pia kwavile wafanyao kazi hizo ni binadamu basi changamoto hutoke pia. 

  Katika mchezo wa soka kuna kocha ambaye hufanya kazi hiyo ya kufundisha wachezaji. Kwa miaka mingi fani hii ya ualimu wa soka ilichukuliwa kama fani ambayo wanaoweza kuitenda vyema ni wale waliocheza soka kwa madaraja ya Juu. 

  Lakini kwa kadiri miaka ilivyoweza kusogea mapinduzi ya dhana hiyo yalianza kutoweka taratibu baada ya kuona wako makocha ambao wanafanya vyema pasipo hata kucheza madaraja ya juu katika soka. Wako makocha ambao wametoa mafanikio kwa vilabu vikubwa wakati wao wamecheza katika madaraja ya chini.

  Katika ulimwengu wa soka imekuja kuonekana,kucheza soka ni kama kitu cha nyongeza kwa kocha lakini kitu muhimu ni kuweza kufundisha soka. Kutokana na dhana hiyo tumeweza kuwaona makocha wengi vijana wakifanya vyema katika vilabu tofauti duniani. Kuonekana kwao kunafanya kuondoa ile dhana ya awali kuwa ili uwe kocha mzuri lazima upitie katika kusakata soka katika madaraja ya juu.


  André Villas-Boas

  Mohammed Kijuso

  Katika klabu ya Mbeya City kwa muda mrefu Mara tu ya kuondoka kocha msaidizi Maka Mwalwisi waliamua kumpa jukumu lile aliyekuwa mchezaji wao Mohammed Kijuso.Akiwa kama kocha msaaidizi alifanya kazi na Juma Mwambusi kama kocha mkuu na baadae Kufanya kazi na Kinnah Phiri. Kwasasa baada ya klabu kuachana na kinnah Phiri majukumu yanakabidhiwa kwa Kijuso.

  Akiwa na umri wa miaka 38, usije ukashangaa matokeo bora uwanjani yakawafanya halmashauri ya jiji la Mbeya kuamua kumpa jukumu la kocha wa klabu.Japo Kijuso amecheza soka katika daraja la juu kabisa kwa Tanzania lakini umri wake unamfanya aonekane kocha kijana na kubeba majukumu katika klabu yenye mashabiki wenye ushawishi mkubwa katika klabu yao.


  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  WATUMIAJI wa Simu na mitandao wameaswa kuwa waangalifu katika kujiepusha na matepeli wanaotumia mitandao hiyo katika kujipatia kipato.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Mawasiliano kwa Umma, Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Semu Mwakyanjala amesema kuwa simu na mitandao inatakiwa kutumika kwa uangalifu zaidi ili mawasiliano yawe na tija kwa mtumiaji.

  Amesema wizi katika mitandao umkeuwa ukifanyika kila siku,hivyo kila mtu akiona taarifa tofauti anatakiwa kuripoti katika vyombo vya dola ili wizi huo usiweze kufanyika na mtu anayefanya hivyo kuanza kufuatiliwa.

  Mwakyanjala amesema TCRA inafanya uchambuzi wa taarifa za matukio ya usalama wa mitandao kutoka katika vyanzo mbalimbali vya nchini , kimataifa na matokeo ya uchambuzi huo kuongeza usalama wa matumizi ya mawasialiano ya simu, komputa pamoja na Internet.

  Aidha amesema TCRA inafanya tathimini ya udhaifu wa mifumo ya komputa ya mitandao ya wadau wake isiweze kusambaza ujumbe wa chuki maudhi au uchochezi unapotokea kwa mtu mwingine na kinachotakiwa kufanyika ni kufuta pale aunapoona taarifa haikidhi vigezo katika mawasiliano.
  Kaimu Meneja Mawasiliano kwa Umma, Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Semu Mwakyanjala akizungumza na waandishi wa habari juu ya mamlaka hiyo inavyofanya kazi leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa habari wa idara ya habari MAELEZO, Fatma Salum.

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi (aliyesimama) akizungumza na wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana alipokua akifungua kikao cha kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule leo Jijini Dar es Salaam.

  Na Genofeva Matemu - Maelezo 

  Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu imewakutanisha wadau mbalimbali kutoka Asasi zinazojishughulisha na masuala ya vijana ili ziweze kushirikiana na serikali kupitia na kuboresha Mwongozo Sanifu wa Stadi za Maisha kwa Vijana kwa kubadilishana uzoefu walionao na kuuwezesha mwongozo huo kumsaidia kijana katika mazingira ya sasa.

  Akifungua kikao cha wadau hao Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi amesema kuwa msingi mkubwa wa kuboresha mwongozi sanifu wa stadi za maisha kwa vijana ni pamoja na kuangalia namna gani serikali inaweza kuwasaidia vijana kwa kuwawezesha kujitambua, kujiendeleza wenyewe na kukuza uchumi wa nchi yetu.

  "Mwongozo wa stadi za maisha umekua ukiwajenga vijana kwa kuwaandaa kujitambua ili waweze kuhimili changamoto mbalimbali zilizopo kama vile vishawishi mbalimbali vinavyowakabili, magonjwa, matumizi ya madawa ya kulevya, mimba za utotoni pamoja na ukosefu wa ajira" amesema Bw. Shitindi kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia, kiuchumi, kisayansi na kijamii serikali imeona ni vyema kukaa pamoja na wadau hao kuangalia yale yaliyomo kwenye Mwongozo wa mwaka 2009 na kufanya uchambuzi yakinifu kwa kila eneo ndani ya mwongozo huo.

  aidha Bw. Kajugusi amewashukuru wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana kwa kuisaidia serikali kufikisha elimu ya stadi za maisha kwa vijana kulingana na mipango na programu zao na kuwahaidi kuendelea kufanya nao kazi katika kujenga taifa lenye vijana wanaojitambua.

  Naye Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Shirika la Kimataifa la Idadi ya watu Bibi. Tausi Hassan ameishukuru serikali kuwakutanisha wadau wanaofanya kazi na vijana moja kwa moja kushirikiana katika kuboresha Mwongozo wa Stadi za Maisha kwa vijana kwani ushirikiano huo utalenga nyanja zote hivyo kupata mwongozo unaokidhi matakwa ya vijana kitaifa.
  Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi (katikati) akifafanua jambo wakati wa kikao na wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Msaidizi Ushauri Nasaha Bw. Juma Mswadiku (kushoto) akitoa hoja wakati wa kikao na wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule leo Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule wakifuatilia mada zilizokua zikiendela leo wakati wa kikao na wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana.
  Mwezeshaji kutoka Chama cha Stadi za Maisha (LISA) Bw. Elemeth Oloo akitoa mada kwa wadau kutoka Asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya vijana wakati wa kikao cha kupitia mwongozo wa Stadi za Maisha wa mwaka 2009 kwa vijana walio nje ya shule leo Jijini Dar es Salaam. Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo

  0 0

  Mkuu wa Polisi Nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wanachi wa Mererani Mkoani Manyara leo baada Rais Dk. John Magufuli kufungua barabara ya kiwango cha lami cha kilometa 26 iliyoanzia KIA kuelekea mererani Mkoani humo.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna wa Polisi DCP Charles Mkumbo (kulia) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi ACP Hamisi Seleman Issah katika uwanja wa Ndege KIA wakati wanamsubiri Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli akitokea jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi mikoa ya Arusha na Manyara. PICHA KWA HISANI YA JESHI LA POLISI.


  0 0

  Na Tiganya Vincent.

  SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeagiza kukamatwa na kuwekwa ndani kwa watumishi wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga na Mzabuni Muhoro Traders kwa tuhuma za udanganyigu wa ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 23.2.

  Agizo hilo limetolewa leo mjini Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
  Amesema kuwa kwa nyakati tofauti za kuanzia Januari  na Machi mwaka huu watumishi walikula njama na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu jumla ya shilingi milioni 23,202.500.00 mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.

  Mwanri anaongeza kuwa watumishi hao waliagiza vifaa hivyo kutoka kwa Mzabuni Muhoro Traders wa Igunga vifaa , lakini havikuwahi kupokelewa na Halmashauri ya Igunga lakini kwenye vitabu vya Afisa Ugavi na yule wa Bohari walikiri kupokea katika vitabu vyao.

  “Naagiza watumishi hao wanne wasimamishwe kazi na wakamatwe wao na Mzabuni Muhoro Traders kisha wawekwe ndani kwa ajili ya kufikishwa  Mahakamani ili wajibu tuhuma zinazowakabili” anasema Mkuu huyo wa Mkoa.
  Anasema kuwa katika hati namba ya malipo namba 2071-1457 watuhumiwa walichukua shilingi 9,250,000/-, hati namba 2017-1457 walijipatia shilingi 6,850,000/- na hati ya malipo namba 2017-1453 shilingi 7,102,500/- na kusababishia Halmashauri hasara hiyo.

  Mwanri amewataja walikamatwa ni pamoja na aliyewahi kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga Gidfrey Mgongo, Afisa Ugavi Mohamed Mtao, aliyekuwa Mhasibu wa Idara ya Afya sasa yuko TARURA Richard Byelembo, Boharia wa Idara ya Afya Jones Lotto.

  Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza pia Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga wa sasa Dkt. Bonaventura Kalumete ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.

  Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mwanri amewaagiza kushughulikia tatizo la ukosefu wa dawa katika Zahanati kwa sababu tayari Halmashauri hiyo imepokea miliomi 550 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.

  0 0


  Na. Paschal Dotto- MAELEZO.

  Serikali ya Awamu ya Tano chini ya  uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya rushwa katika ofisi za Serikali, taasisi na mashirika ya umma na kuweka usawa katika  upatikanaji wa huduma kwa jamii.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam  na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John  Mbungo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kuhusu rushwa katika taasisi na mashirika ya umma kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

   Brigedia Jenerali Mbungo alisema kuwa lazima watumishi wajifunze kuwa waadilifu, kwa hiyo kile watakachokipata kutoka katika mkutano huo kikafanye kazi kuleta haki kwa wananchi wakati wa kupata huduma katika ofisi zao ili kuendana na sera ya Awamu ya Tano ya kutokuvumilia vitendo vya rushwa nchini.

  “Tumieni fursa katika kikao hiki ili kuweza kupata elimu itakayosaidia wananchi kuelimika juu ya vitendo vya rushwa na kupata haki zao za msingi wanapopata huduma katika ofisi zenu”,alisema Brigedia Jenerali Mbungo.
  Kikao kazi hiki ni cha kwanza ambacho kinafuatia mkakati wa awamu wa tatu  utakaokuwa wa miaka mitano kuanzia  Julai, 2017 unaolenga kuanzia ngazi za vijiji, wilaya, mkoa, mpaka taifa ili kudhibiti uadilifu, nidhamu na utendaji kazi wenye kuzingatia haki katika ofisi mbalimbali nchini.

  Aidha Brigedia Mbungo alisema kuwa kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali, hali ya rushwa nchini imepungua kwa kiasi kikubwa kwani malalamiko yamepungua katika ofisi, taasisi na mashirika ya umma.

  “Hali ya rushwa sasa hivi imepungua kwa sababu Serikali kwa kutumia juhudi  mbalimbali imedhibiti hali hii, Tanzania ina viwango vya chini sana vya rushwa ikilinganishwa na nchi nyingine za maziwa makuu kwa hiyo naweza kusema kiwango kimepungua sana hususani kwa Jiji la Dar es Salaam ambapo vitendo hivi vilishamiri sana, hivyo katika awamu hii ya tatu ya mkakati huu tunatarajia viwango vitashuka zaidi”, alisisitiza Brigedia Jenerali Mbungo.
  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Theresia Mmbando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo.
    Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bibi. Theresia Mmbando akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) leo jijini Dar es Salaam.
   Mratibu wa Kitengo cha Utawala Bora kutoka Ofisi ya Rais Bi. Christina Maganga akitoa neno la utangulizi kuhusu mkakati wa taifa dhidi ya rushwa awamu ya tatu wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wajumbe wa kamati za kudhibiti uadilifu kuhusu utekekelezaji wa mkakati huo leo jijini Dar es Salaam.

   Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudhibiti uadilifu kutoka mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia wakifuatila mada wakati wa kikao kazi cha wajumbe wa kamati hizo kuhusu utekekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa, awamu ya tatu (2017-20120) leo jijini Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1918 | 1919 | (Page 1920) | 1921 | 1922 | .... | 3286 | newer