Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1916 | 1917 | (Page 1918) | 1919 | 1920 | .... | 3285 | newer

  0 0  0 0

  Na Bearice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Suleiman Jaffo amesema kuwa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika (ALHP) una historia adhimu kati ya Tanzania na Afrika Kusini na itasaidia kuimarisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili.

  Mhe. Jaffo ameyasema hayo leo Wilayani Kongwa, Dodoma wakati wa ziara ya Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na Watalamu wa Programu hiyo kutoka Tanzania na Afrika Kusini  kujionea maeneo yaliyotumika wakati wa  Ukombozi wa Bara la Afrika ikiwemo Afrika Kusini. 

  “Nchi ya Tanzania na Afrika Kusini zina urafiki mkubwa na wa karibu kuliko nchi nyingine yeyote Afrika, hivyo kupitia Programu hii tutazidi kuimarisha udugu na uhusiano uliopo” amefafanua Mhe. Jaffo.

  Ziara hiyo ilihusisha maeneo ya makaburi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini, Kambi walipokuwa wanaishi, mahandaki walipokuwa wanajihifadhi dhidi ya maadui pamoja na madarasa yaliyotumika kwa ajili ya mafunzo kwa wapigania uhuru. 

   Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Suleiman Jaffo akiongea na wajumbe wa Mkutano wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kutoka Tanzania na Afrika Kusini walipokuwa ziarani Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius Ndejembi na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano Serikalini Bi. Plumla Williams akitoa neno kwa niaba ya wajumbe kutoka Afrika Kusini walipotembelea maeneo ya ukombozi yaliyopo Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya agenda ya Mkutano kuhusu utekelezaji wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika.
   Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Suleiman Jaffo (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkurungenzi Mkuu wa Kazi za Umma kutoka Afrika Kusini Bw. Mziwonke Dlabantu (kulia). Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius Ndejembi.
  Baadhi ya Viongozi kutoka Afrika Kusini wakiangalia makaburi ya Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini yaliopo Wilayani Kongwa, Dodoma. Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Iddi Hassan Kimanta leo ameongoza waombolezaji  katika mazishi ya watoto watatu waliofariki dunia kwa mlipuko wa bomu kwenye eneo la mazoezi ya kijeshi wilayani Monduli, mkoani Arusha. 
  Marehemu hao - Johnson Daniel, Lendisi Saitabau na Samweli Nyangusi -walifariki dunia Ijumaa iliyopita katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale walipokuwa wakichunga ng'ombe. Inasemekana walilipukiwa na bomu walipokuwa wakilichezea wakidhani ni mpira.
  Mazishi hayo yamefanyika katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha baada ya shughuli ya kuaga miili hiyo katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli. 

  Wanafunzi wa shule ya msingi Nafcon wakiwa wamebeba majeneza yenye miili ya wanafunzi wenzao mara baada ya kuwasili nyumbani kutokea hospitali ya wilaya ya Monduli kabla ya mazishi  katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha 
   Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Iddi Hassan Kimanta akitoa rambirambi za serikali kwenye mazishi hayo  katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha baada ya shughuli ya kuaga miili hiyo katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli. 
  Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Iddi Hassan Kimnta akifuatiwa na Brigedia Jenerali Athanasi Mbonye, Kamanda wa Brigedi ya Mbuni, na Brigedia Jenerali R.G. Hanti  wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu kabla ya mazishi.

  Ibada ya mazishi katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha 
   Sehemu ya waombolezaji kwenye mazishi hayo
  Askari wa JWTZ wakiwa wamebeba moja ya majeneza ya marehemu hao wakielekea makaburini kwa mazishi. Picha zote na HD TEAM MEDIA.

  0 0

  Siku kama ya leo tarehe 19 September ndio siku ya kuzaliwa mkuu wa bendi ya Ngoma Africa aka FFU ya kule Ujerumani, mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja aka mkuu wa viumbe wa ajabu "Anunnaki Alien" alizaliwa mjini Dar-es-Salaam, akiwa mtoto wa kwanza wa kiume wa Mzee Jumanne Saleh Makunja Ngayonga (RIP) na Bi. Moza Hassan Seifu Mpili (Mama Makunja).
  Mwanamuziki Kamanda Ras Makunja mtunzi na mwimbaji  mahili wa muziki wa dansi leo ndio Happy Birthday yake!!! Hivyo anakukaribisha 
   kuburudika na kusherekea naye katika kambi yao FFU-Ughaibuni  www.reverbnation.com/ngomaafricaband

  0 0

  BODI ya Korosho Tanzania imetangaza bei elekezi kwa msimu 2017/2018 kwa kilo moja ya Korosho ghafi daraja la kwanza (Standard Grade) kitakuwa ni sh.1,450 huku kilo moja ya daraja la pili itakuwa ikiuzwa kiasi cha sh.1,160.

  Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Anna Abdallah wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu ufunguzi rasmi wa soko la Korosho msimu wa mwaka 2017/2018.

  "Niseme tu bei hii elekezi ya korosho imetangazwa na bodi hiyo kwa mamlaka waliopewa chini ya kifungu cha 5(3)(d) ambapo bei hiyo imefikiwa baada ya utafiti wa kupata gharama halisi za kuzalisha kilo moja ya korosho ghafi na kuongeza asilimia 20 kama faida ya mkulima "Alisema.

  Alisema kwa msimu huu gharama ya kuzalisha kilo moja ya korosho ghafi ni 1,208.39 na asilimia 20 ya faida kwa kilo ni sh.241.68 .

  Aidha alisema katika mjengeko wa bei ya korosho ghafi msimu wa 2017/2018 ambapo magunia na kamba vitatolewa na serikali kupitia CBT huku chama cha msingi kikipata sh.90.00,Halmashauri ya wilaya ikipata asilimia 3 ya sh.43.50,mfuko wa wakfu ukipata sh.10.00 ambapo jumla ya gharama ni 143.50 wakati bei elekezi ikiwa ni 1,450.00 na mjengeko wa bei ukiwa ni tsh.1,593.50.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Anna Abdallah katikati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga leo kuhusu bei elekezi ya korosho msimu wa 2017/2018 kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Maokola Majogo 
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martin Shigella akizungumza katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Anna Abdallah kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT)Hassani Jarufu 
  Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia 
  Waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kushoto ni Mbaruku Yusuph wa Gazet la Tanzania Daima,Amina Kingazi wa Gazeti la The Guardian mkoani Tanga,Burhan Yakub wa Mwananchi.


  0 0

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  SERIKALI kupitia Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), imeahidi kusimamia miradi ya umeme Kituo cha Tipper-Kigamboni,  Mbagala na Kurasini ili kuhakikisha inakamilika kwa haraka na kwa wakati na hatimaye wananchi wa maeneo hayo wanaondokana na adha ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, mwishoni mwa ziara yake ya kufuatilia uboreshaji wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na ujenzi wa kituo kipya cha kufua na kusambaza umeme huko Kimbiji  wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam Septemba 18, 2017.

  Waziri pia amekagua ujenzi wa mradi wa maendeleo ya upanuzi na upatikanaji nishati (TEDAP), wa kusafirisha umeme wa 132kv ulioko Gongolamboto nje kidogo ya jiji.

  “Wananchi wanataka umeme, hawahitaji kujua  nguzo za umeme zimepatikana wapi, au upembuzi yakinifu utakamilika lini, nimeagiza baada ya siku tano kuanzia leo (Septemba 18), fanyeni kazi usiku na mchana walau vituo viwili vya kupoza na kusambaza umeme viwe vimekamilika ili wananchi wa Mbagala na Kigamboni wapate umeme wa kutosha.” Alisema Dkt. 
   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wakwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, (wakwanza kushoto), na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo anayeshughulikia Miradi, Mhandisi Khalid James, (watatu kushoto), wakimsikiliza Meneja Mradi wa TEDAP, Mhandisi Emmanuel Manirabona, (aliyenyoosha mkono), wakati Naibu Waziri na uongpozi wa TANESCO, ulipotembelea mradi wa TEDAP wa Gongolamboto jijini Dar es Salaam, Septemba 18, 2017. Mradi huo unahusu upanuzi na uendelezaji wa mradi wa kusafirisha umeme wa 132kv.


  Mbunge wa Kigamboni Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile, (kushoto), akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani ambaye alifuatana naye kwenye ziara hiyo.
  Sakafu ya kufungia transfoma mpya ya umeme wa 15mva kituo cha Tipper-Kigamboni, ikijengwa Septemba 18, 2017
  Mshine mpya kwenye kituo cha Mbagala

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
  0 0


  0 0

  Benki ya NMB imetakiwa kuwasaidia wafanyabiashara Mkoani Singida kuanzisha kiwanda cha kutengenea vifungashio, ili waweze kuhifadhi bidhaa zao katika ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa rai hiyo mapema leo wakati akifungua warsha ya siku moja ya klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB, katika ukumbi wa Kanisa Katoliki mjini Singida.

  Dkt Nchimbi amesema klabu hiyo ya wafanyabiashara itaweka alama kubwa katika maendeleo endapo watajipanga na kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vifungashio hivyo kuliko kuendelea kuvifuata nje ya Singida au nje ya nchi.

  “Uzoefu usipotumika vizuri unaweza ukawa kikwazo cha kuendelea, msizoee kufuata vifungashio na label nje ya singida wakati fursa ipo ya kuanzisha kiwanda hicho Singida”, amesema na kuongeza kuwa. “Wafayabiashara mzipende biashara zenu na kuziweka katika hali ya usafi na yenye kuvutia, wengine wanapenda kujisafisha na kujipendezesha wenyewe lakini ukiangalia biashara zao hazivutii, zimewekwa tu bila kufungashwa vizuri”, amesisitiza.

  Aidha amewataka wafanyabiashara wasiogope kukopa kwakuwa sio jambo la aibu wala fedheha, ila kinachotakiwa ni kuwa na nidhamu ya mkopo na malengo ili waweze kufanikiwa.

  “Akina mama jifunzeni kuwa na nidhamu ya mkopo, sio unakopa leo mara unasikia kapu la mama, jifikirie hayo ndio malengo ya huo mkopo hata kama ni jambo muhimu?, nidhamu ya mkopo inatakiwa ianze kabla ya kukopa na iendelee kuwepo. Dkt Nchimbi pia ameishukuru benki hiyo kwa kushirikiana na serikali katika mambo mbalimbali ya kielimu na afya, pia amewashukuru kwa kutoa mikopo kwa watumishi wa umma jambo ambalo linawasiadia katika mambo mbalimbali.

  Naye Meneja wa NMB Kanda ya kati Straton Chilongola amesema klabu za wafanyabiashara nchini ziko 34 ambazo zimekuwa zikipatiwa mafunzo mikopo kutoka katika benki hiyo. Chilongoloa amesema benki hiyo imekuwa ikitoa mafunzo juu ya ulipaji kodi, ujasiriamali, masuala ya mitaji, leseni na ardhi ili wafanyabiashara hao waweze kukuza mitaji yao. Amesema benki hiyo imefanikiwa kuwakuza wafanyabiashara wengi ambazo wameanza nao wakiwa wafanyabiashara wadogo ambapo sasa wamekuwa wakubwa na wakati huku wakiajiri wengine na hivyo kukuza uchumi.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB Singida Emmanuel Rweyemamu Kyoma amesema wazo la kuanzisha kiwanda cha kutengeza vifungashio wamelipokea vizuri huku wakijipanga kuandaa andiko kwa ajili ya kiwanda hicho. Kyoma amesema kwa ushirikiano na NMB kiwanda hichokitaweza kujengwa Singida huku wakimuahidi Mkuu wa Mkoa kuwa Mkoa wa Singida utazalisha chakula cha kutosha kulisha Mkoa wa Dodoma. Amesema benki ya NMB imekuwa ikishirikiana na wafanyabiashara hao hivyo mipango ya kukuza uchumi kama huo wa kuanzisha viwanda utatekelezeka bila matatizo yoyote.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisalimiana na Mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB Singida Emmanuel Rweyemamu Kyoma mapema leo kabla ya kufungua warsha ya siku moja ya klabu hiyo, katika ukumbi wa Kanisa Katoliki mjini Singida.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akikagua baadhi ya bidhaa za wafanyabiashara wateja wa NMB Singida mapema leo kabla ya kufungua warsha ya siku moja, katika ukumbi wa Kanisa Katoliki mjini Singida.
  Meneja wa NMB Kanda ya kati Straton Chilongola akizungumza klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB Singida mapema leo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja, katika ukumbi wa Kanisa Katoliki mjini Singida.
  Wafanyabiashara wateja wa NMB Singida wakiwa katika warsha ya siku moja katika ukumbi wa Kanisa Katoliki mjini Singida mapema leo.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru (watatu kutoka kulia) akikata utepe katika ufunguzi wa Duka la vifaa vya Ujenzi la Jotun Tanzania, lililopo Mtaa wa Mkwepu, Posta Mpya jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Balozi wa Norway nchini, Bi. Hanne Marie Kaarstad na wa pili kushoto ni Makamu Rais wa JOTUN, Esben Hersve. Kampuni ya Jotun iliyoanzishwa nchini Norway mwaka 1926, ni moja ya kampuni zinazoongoza katika uzalishaji wa rangi duniani, ambapo mwaka 1974 Jotun waliweka uwepo wao katika nchi za umoja wa nchi za kiarabu, tangu wakati huo Jotun imekuwa ikikuwa katika maeneo tofauti, na kuwa kampuni pekee ya uzalishaji rangi  iliyopata tunzo ya vyeti vya viwango vya ubora vyenye  namba  ISO 9001: 2008, ISO 14001 & OHSAS 18001. Kampuni hii pia ina viwanda vya uzalishaji katika nchi ya Abu Dhabi, Dubai, Saudi Arabia, Oman na Misri.
  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dr. Adelhelm Meru, akipewa maelekezo ya namna mashine ya uchanganyaji rangi inavyofanya kazi toufauti kwa dakika moja.
  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dr. Adelhelm Meru, akihutubia katika sherehe za ufunguzi wa duka la rangi ya Jotun Tanzania.

  0 0

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaambia washtakiwa sita wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo  akiwemo mfanyabiashara Yusuf Yusuf (34) maarufu ‘Mpemba’, kuelekeza lawama zao juu ya upelelezi kuchelewa kukamilika kwa mawakili wanaowatetea siyo wa Serikali tu.

  Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema hayo mapema leo asubuhi wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi ilipofika kwa ajili ya kutajwa ambapo Wakili Wa serikali alidai jalada. 

  Wakili Wa Serikali Elia Athanas alidai kuwa taarifa walizopeleka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambazo awali zilikosewa, walizifanyia marekebisho lakini bado hazijarudishwa ili waweze kuwasomea washtakiwa maelezo ya mashahidi (Committal.)

  Hata hivyo, washtakiwa wamelalamika na kudai kuwa kila wakija wanaambiwa jalada halipo, ndipo hakimu akawashauri wawalalamikie pia mawakili wanaowatetea na siyo wa upande wa serikali tu kwani na wao wamekuwa wakikaa kimya tu. 

  "Muwe mnawalalamikia na mawakili wenu pia siyo wa Serikali tu, ili hii kesi iweze kwenda kwa haraka", amesema Simba

  Kesi hiyo imahirishwa hadi Octoba 10 kwa ajili ya kutajwa

  Mbali na mpemba, washtakiwa ni Charles Mrutu (37) mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa (40) mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima (30) mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo (33) dereva na Pius Kulagwa (46) 

  Wote wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubacary bin Zubeiry Ally wakati alipokwenda nyumbani kwake Mtaa wa Ufipa Kinondoni jijini Dar es salaam Septemba 19, 2017 kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Saad Zubeiry Ally kilichotokea kwee hospitaal ya taifa ya Muhimbili Septemba 18, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubacary Zubeiry bin Ally wakati alipokwenda nyumbani kwake Mtaa wa Ufipa Kinondoni jijini Dar es salaam Septemba 19, 2017 kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Saad Zubeiry Ally kilichotokea kwee hospitaal ya taifa ya Muhimbili Septemba 18, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumz na Sheikh Mkuu wa Tanzani, Mufti Abubacary Zubeiry bin Ally wakati alipokwenda nyumbani kwake Mtaa wa Ufipa Kinondoni jijini Dar es salaam Septemba 19, 2017 kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Saad Zubeiry Ally kilichotokea kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili Septemba 18, 2017. Kushoto ni Kadhi Mkuu wa Tanzania , Sheikh Abadallah Mnyasi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Balozi wa Nordic Foundation Tanzania Najma Abdallah akiwasiliana na Frank Athanasi Samson Mkulima wa Mkoani Geita baada ya kuibuka mmoja wa washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu pamoja na familia, katika droo ya kwanza ya Afyabando mchezo uliochezeshwa jijini Dar es Salaam leo Septemba 17 2017.
  Mabalozi wa Nordic Foundation Tanzania Hilary Daudi' Zembwela' na Najma Abdallah wakiwa na Mkaguzi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari Maggid aliysimamia zoezi la kuendesha kampeni ya Afyabando kuwapata washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu pamoja na familia. Mchezo huo umechzeshwa jijini Dar es Salaam leo Septemba 17 2017.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), Hamza Johari akizungumza na wadau wa sekta ya usafiri wa anga  juu sekta hiyo iweze kukua haraka katika umuhimu wake katika ukuaji wa uchumi , katika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
  Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa akiongea na Balozi wa Ufaransa nchini, Bi. Malika Berak mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere katika Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga lililoanza leo.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (mwenye tai nyekundu waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kwanza la Usafiri wa Anga linalofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kushoto kwa Waziri  ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi na kulia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Bw. Hamza Johari. 
  .
  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  SERIKALI imesema kuwa inatatizo la mabaruni wa kurusha ndege hali ambayo inahitaji kusomesha marubani kwa wingi na kuacha kuchukua nje ya nchi.

  Hayo ameyasema Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa sekta ya usafiri wa Anga leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Mbarawa amesema kuwa sasa ni wakati wa kusomesha marubani, mafundi pamoja wahandisi wa ndege kutokana na mahitaji ya hao wote katika kufikia uchumi wa kati wa 2025.

  Amesema kuwa hakuna sababu ya watu hao kuchukua nje ya nchi wakati malengo ya serikali kwenda kwa kasi katika maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga ambayo ndiyo itafanya kuongeza kwa pato la taifa pamoja na uchumi.

  Mbarawa amesema kuwa serikali imejipanga katika ujenzi wa miundombinu ikiwemo miundombinu ya viwanja vya ndege katika na kuweza kufanya Tanzania kuwa kiunganishi kwa safari za ndege za nchi mbalimbali.
  Aidha amesema kuwa wanahitajika wawekezaji makini katika sekta ya usafiri wa anga na sio wawekezaji wa kufanya blablaa na kufanya sekta hiyo ishindwe kukua kwa kasi katika malengo ya serikali.

   Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema kuwa mkutano huo utajadili mada mbalimbali ikiwemo kupungua kwa shehena katika viwanja vya ndege pamoja na bidhaa zinazozalishwa nchini kutumia viwanja nchi jirani ambapo wadau ndio wenye majibu ya kuweza kuitatua changamoto hiyo.

  Johari amesema kuwa katika  mkutano huo ni muhimu katika sekta ya usafiri anga  katika kuboresha huduma ili iweze kwenda kwa kasi katika ukuaji wa uchumi.


  Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege Nchini (ATCL), Ladislaus Matinde amesema mahitaji ya ndege duniani 39620 kwa Afrika ni 10150  huku marubani 617000  duniani na Afrika 22000 na Mafundi 814000, Afrika Mafundi wa Ndege 24000.

  0 0

  Mwakilishi wa Benki ya Dunia (World Bank), Jonathan Marskell akizungumza kutambulisha wageni walioshiriki katika warsha ya wataalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano.
   Mhe. Balozi Hassan Yahya Simba akifungua warsa ya wataalamu wa wataalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano Bagamoyo.
  Washiriki wa Warsha ya Teknolojia ya Mawasiliano Bagamoyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni Rasmi Mhe. Balozi Hassan Yahya Simba baada ya ufunguzi wa Rarsha.

  WATAALAM wa Teknolojia ya Mawasiliano nchini wanakutana katika warsha ya Siku mbili mkoani Pwani kujadili namna ya kutengeneza mfumo wa Taifa wa Kidigitali utakaowezesha mifumo ya Serikali na Binafsi kubadilishana taarifa kwa kutumia Mfumo Mkuu wa Taifa wa Usajili na Utambuzi wa Watu unaosimamiwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA).

  Warsha hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na World Bank na NIDA imefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Balozi Hassan Yahya Simba ambaye amepongeza hatua hii muhimu kwa Taifa ya kuwa na mfumo utakaowezesha kuunganisha mifumo ya Serikali na Binafsi katika masuala ya Utambuzi kwa manufaa mapana ya Taifa.

  Amesema kuwepo kwa mfumo imara wa Utambuzi kutawezesha sio tu maendeleo ya haraka ya Taifa, lakini pia kutaruhusu wananchi kupata haki zao kwa wakati na kuboresha huduma za kijamii; na kusaidia Serikali na sekta binafsi kuwafikia wananchi kirahisi  na kutoa huduma zenye viwango.

  Akizungumza kwa niaba ya Benki ya Dunia (World Bank) ambao wamefadhili warsha hiyo, ndugu  Robert Palacios amesema Benki ya Dunia kwa kutambua umuhimu wa Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa kutambua changamoto kubwa ya idadi kubwa ya wananchi kutotambulika na mifumo rasmi kwa kukosa mfumo rasmi unaowatambua, Benki ya Dunia imeamua kusaidia harakati za nchi za Afrika katika kukamilisha kuanzishwa kwa mfumo wa Utambuzi na kuunganishwa kwa mifumo ya utoaji huduma ili kuwezesha wananchi kupata huduma kwa haraka na kuinua hali za maisha hususani wananchi wanaoshi katika hali ngumu.

  Warsha ya Wataalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano imeanza leo (18 – 19/09/2017) Bagamoyo mkoani Pwani katika hoteli ya Ocenic Bay na inatazamiwa kuibuka na maazimio yatakayoiwezesha Serikali kuwa na Sera na mikakati ya pamoja katika kuunda mfumo wa kidigitali wa matumizi ya Taarifa kwa Serikali na wadau katika utoaji huduma. Miongoni mwa washiriki katika warsha hiyo ni Wizara, Mashirika,  Taasisi na Makampuni binafsi. 

  0 0

   Na Mahmoud Ahmad Arusha
  MKUU wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amekabidhi vifaa vya ujenzi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake alizotoa katika ziara yake ya siku tano iliyomalizika tarehe 15/09/2017.

  Katika makabidhiano hayo Mhe. Gambo amekabidhi jumla ya mifuko 700 ya saruji, nondo za ukubwa wa milimita 16 na 12 tani moja moja na bati 200 kwenda kukamilisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali.

  “Katika ziara yangu nimekutana na wananchi wetu wamejitahidi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo na Halmashauri ya Arusha Vijijini imefanya kazi kubwa, wakaniomba mimi kama Mkuu wa mkoa niweze kuchochea shughuli za maendeleo na msaada huu utaenda kusaidia maeneo mbalimbali mfano ujenzi wa daraja Mateves na nyumba za walimu Oldonyosambu” alisema Mhe. Gambo.

  Mkuu wa Mkoa amemaliza ziara zake za kikazi katika mkoa wa Arusha kwa kutembelea Halmashauri 7 na wilaya zote 6, ziara hizi zikiwa na lengo la kujitambulisha kwa wananchi na kusukuma shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
   Lori lililosheheni mifuko 700 ya saruji tayari kuelekea makao makuu ya Halmashauri yaArusha
  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gamboo akikabidhi mifuko ya saruji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, Charles Mahera (katikati) aliyeambatana na Katibu Tawala wa wilaya ya Arumeru, Timoth Mzava.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akikabidhi mabati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake alizotoa katika ziara yake ya siku tano iliyomalizika tarehe 15/09/2017.
  Nondo tani mbili zikiwa tayari kukabidhiwa kwa wananchi wa wilaya ya Arumeru ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake alizotoa katika ziara yake ya siku tano iliyomalizika tarehe 15/09/2017.

  0 0

  Na Tiganya Vincent.
  WATU saba wa kijiji cha Mwambondo wilayani Uyui wanashirikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwauunguza kwa moto wanawake waanne wakiwatuhumu kuwa wachawi na wanahusika na kifo cha mume wa mmoja wao.

  Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa alizozipata kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa huo Wilbroad Mtafungwa.

  Alisema kuwa chanzo cha vitendo hivyo vya kinyama zilianzia baada ya Mtu mmoja alikuwa akiitwa Mafumba Jirawisi kufariki  kwa sababu ya maradhi lakini baadhi ya watu walianza kumtuhumu mke wa marehemu anayeitwa Manugwa Lutema kuhusika na kifo cha mume wake na kuamua kumpeleka porini na kuanza kumshambulia huku wakitaka awaeleze watu wanaoshirikiana naye kuwafanya vitendo vya kichawi.

  Mwanri alisema kuwa mama huyo baada ya kupiga sana na kuumia aliamua kutaja ovyo majina ya majirani zake na ndipo nao wakaunganishwa naye na kuendelea kupigwa na kuunguzwa katika sehemu za siri.

  Kufuatia vitendo hivyo vya kinyama Mkuu huyo wa Mkoa amemwagiza kuwasaka watu waliobaki ambao wamehusika katika kitendo hicho wakiwemo Makamanda wa sungusungu ili hatua kali ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

  Mmoja wa majeruhi wa tukio hilo la kinyama alisema kuwa alilazimika kutaja majirani zake ili kutaka kunusu roho yake baada ya kuona mashambulizi yanazidi na anasikia maumivu makali.

  Kwa upande wa ndugu wa waathiri wameomba wagonjwa wao watibiwe bure kwa sababu tukio hilo limetokea wakati wakiwa hawana kitu na hawajiandaa na kutokuwa na fedha ya kulipia matibabu

  Akijibu ombi la ndugu hao Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunin Kamba alisema wagonjwa wote walijeruhiwa na kuuguzwa moto watapewa matibabu kwa mkopo katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa ya Kitete ,malipo yatafanyika baadaye.

  Alisema kuwa lengo ni kutaka kwanza kuokoa maisha yao kutokana na unyama waliofanyiwa na kundi hilo la watu.

  Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kitete Dkt.Nassor Kaponta alisema kuwa wanaendelea kuwapatia huduma katika Hospitali hiyo na hakuna majeruhi ambaye atahamishiwa kwingine kwa sababu wanauwezo wa kuwasaidia wakiwa katika eneo hilo hilo.

  Aliwataja waliojeruhiwa ni Maria Sahani , Elizabeth Kashindye, Manugwa Lutema na Raheli Mikomangwa. Kabla ya kufariki marehemu ambaye alikuwa mganga wa kienyeji alikwenda kutoa matibabu kijiji cha jirani na baada ya kurejesha akaanza kuumwa na hatimaye usiku wake alifariki kwa sababu ya ugonjwa.

  Vitendo vya kinyama ikiwemo mauaji kwa wanawake Mkoani Tabora vinaanza kuonekana kama vya kawaida ambapo mapema mwezi Agosti mwaka huu wilayani Nzega wakinamama watano walipoteza maisha baada ya kushambuliwa na kisha kuchomwa moto na mwei huo huo wilayani Sikonge mtu mmoja alinusurika kifo baada ya kufungiwa nyumbani kwake na nyuma kuwekwa moto

  0 0


  0 0

  The Kigoma Joint Programme is an area-based UN joint programme that puts together the efforts of 16 different UN agencies in Tanzania to improve development and human security in Kigoma. Today, the United Nations met with Kigoma’s Regional Commissioner, members of the Development Partners Group, Civil Society Organizations and the media in Kigoma in order to brief them on the joint programme ensuring that the UN is set to effectively work with the government in implementing the issues that the joint programme aims to address.


  The Kigoma Joint Programme focuses on both the host population and refugees and migrants. Itlinks the UN’s current response to refugees and migrants with an increased focus on developing the host communities the UN will strengthenthe link between humanitarian and development initiatives in the region. The 16 UN agencies will work together across six themes which are sustainable energy and environment, youth and women’s economic empowerment, violence against women and children, education, agriculture and WASH (water, sanitation and hygiene).


  UN Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez, makes his opening remarks at the Soft Launch of the Kigoma Joint Programme highlighting the programme's focus on host communities in Kigoma.  Tanzania currently hosts over 300,000 refugees who reside in three camps in the districts of Kasulu, Kakonko, Kibondo which is why these are the three districts where the programme will operate. The programme aims to expand and increase support to host communities in these districts and the UN believes that partnering with the local government authorities is key to achieving this. “In order to have a sustainable and constructive dialogue between host communities and the refugees and migrants in the region we need to work together. The UN is here to support the government to ensure that humanitarian interventions do not prevent development,” said Mr. Alvaro Rodriguez, the UN Resident Coordinator during the press conference held immediately after the presentation of the joint program to the media.


  The UN Joint Program for Kigoma will be implemented for four years between 2017 and 2021.
  Ambassador of Belgium, H.E. Paul Carter, pointing out that development partners can complement the effort of the Kigoma Joint Programme  Commenting on the Program, Kigoma’s Regional Commissioner, Brig Gen Emmanuel Maganga said "Inception of this program has been at the right time because it is focusing at addressing the critical challenges that are facing community of Kigoma. The 6 areas of intervention that the program is focusing especially Sustainable Energy and Environment, Youth and Women Economic empowerment, Water Sanitation and Hygiene, Agriculture, addressing violence against women and children and education on girls and adolescent girls are the important economic aspect requiring special consideration for sustainable socio-economic growth of our people.


  Execution of UN Joint Program for Kigoma will accelerate the Regional Initiative towards poverty reduction. This program will significantly contribute in the attainment of the National Development Goals as stipulated in the Development vision 2025, The Second five years Development Plan as well as Sustainable Development Goals (SDG).
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

older | 1 | .... | 1916 | 1917 | (Page 1918) | 1919 | 1920 | .... | 3285 | newer