Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

DKT. ASHATU KIJAJI AZINDUA KITABU CHA MWONGOZO KWA WANAMIPANGO

$
0
0

Benny Mwaipaja, Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezindua Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango Tanzania, kilichoandaliwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya nchini Uholanzi (ISS), na kuwataka wataalamu wa mipango hapa nchini kuandaa mipango yenye tija itakayoiwezesha jamii kuondokana na umasikini.

Dkt. Kijaji ameeleza kuwa nafasi ya wataalamu wa mipango katika kukuza uchumi wa nchi ni kubwa na kwamba kinachotakiwa ni kuandaa mipango shirikishi itakayochangia kuimarisha maisha ya wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi.

“Ni matumaini yangu makubwa kwamba kuzinduliwa kwa kitabu hiki cha mwongozo kwa wanamipango, kutakuwa chachu ya wataalamu wetu kuangalia namna ya kupeleka maendeleo vijijini na sehemu nyingine duniani kwa kutoa wataalamu waliobobea ili kuharakisha maendeleo ya nchi” alisistiza Dkt. Kijaji

Ameeleza kuwa maudhui ya kitabu hicho yapelekwe hadi ngazi za chini kupitia Serikali za Mitaa ili watu wengi waweze kukisoma na kuelekezwa namna bora ya kupanga mipango yao ya maendeleo.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijini, Prof. Hozen Mayaya, amesema kitabu hicho kimelenga kuwaongezea ujuzi wataalamu wa mipango kwa kuzingatia vitendo zaidi badala ya nadharia.

“Kitabu cha Mwongozo kwa wanamipango kitakuwa rejea ya nadharia nyingi na njia ambazo wataalamu wanapaswa kuzijua, namna ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuifanya mipango iweze kutekelezeka kama ilivyokusudiwa” alisema Prof. Mayaya.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (aliyeshika mkasi) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners handbook), Toleo la Pili, kilichoandikwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya nchini Uholanzi (ISS), tukio hilo limefanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kampasi ya Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (katikati), akionesha kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili,  baada ya kukizindua rasmi katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma. Wa pili kushoto ni Kaimu Balozi wa Uholanzi hapa nchini, Bi. Lianne Houben, na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo hicho Prof. Razack Lokina.
 Kaimu Balozi wa Uholanzi hapa Nchini, Bi. Lianne Hauben (kushoto), akifurahi wakati akikabidhiwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, mara baada ya kukizindua rasmi mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiwaongoza wadau mbalimbali kunyanyua nakala ya kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners handbook), Toleo la Pili, kilichoandikwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya nchini Uholanzi (ISS), tukio hilo limefanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kampasi ya Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JAFFO- “MABILIONI KWA AFYA ZA WATANZANIA”

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Seleman Jafo (Mb).

Na. Atley Kuni- TAMISEMI
SERIKALI imepanga kukarabati vituo vya afya 172 kutokana na fedha kutoka Benki ya Dunia na Ubalozi wa Canada ambapo wametoa jumla ya Dolla za Kimarekani Mil 88 sambamba na Bil.12 fedha za kitanzania zilizovuka katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Seleman Jafo (Mb) amesema lengo la serikali nikuhakikisha ifikapo Desemba 30, 2017 shughuli hiyo iwe imekamilika ipasavyo kwa kusimamiwa karibu na Waheshimwa Wakuu wa mikoa wakisaidiana na Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya.

Jafo amesema kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Serikali imepokea Dolla za kimarekani  Mil. 66 kutoka Benki ya Dunia ambapo vituo 103 vitakarabatiwa aidha pia Serikali  kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI, imepata Msaada kutoka Ubalozi wa Canada wa dolla za kimarekani Mil 22, ambapo vituo 44 vya afya vitakarabatiwa kwa fedha hizo. 

Naibu waziri huyo alisema,  fedha zingine zitakazo tumika katika zoezi hilo ni zile zilizo vuka katika mwaka wa fedha uliopita.

“Vituo 25 vitafanyiwa ukarabati kupitia fedha za Benki ya Dunia na mfuko wa afya wa pamoja zilizovuka mwaka wa 2016/2017, ambapo Bil.12 za kitanzania zitatumika,” alisema Jafo na kuongeza  kwamba kila  “kituo kitapatiwa shilingi Mil. 500 za kitanzania na baada ya ukarabati serikali itakuwa na jukumu lakupeka vifaa katika maeneo hayo”.

Waziri Jafo amesema, Maeneo ya kipaumbele wakati wa ukarabati huo ni pamoja na  Upasuaji (Theater), Wodi za mama na Mtoto (Martenity), Maabara(Laboratory), pamja na Nyumba za watumishi sambamba na maeneo mengine ya kipaumbele kutokana na fedha zilizopo.

Katika hatua nyingine Jafo amewagiza Makatibu Tawala wa mikoa kuwasilisha Taarifa ya kila mwezi ofisini kwake juu ya maendeleo ya ukarabati, huku akiwataka Wakurugenzi na watendaji wengine kusimamia kwa ufasaha zoezi hilo. 

Naibu Waziri hakusita kuonya juu wale wote watakao kwenda kinyume na maagizo na maelekezo ya serikali yaliyotolewa  
“Nawaomba Wah. Wabunge na Madiwani kushirikiana bega kwa bega na watendaji katika kufanikisha zoezi hili kwa ufanisi, alisema Jafo na kuongeza kwamba,  “ofisi yangu haita mvumilia Kiongozi au Mtendaji yeyote atakaye onekana kutumia fedha hizo vibaya au kushindwa kutimiza wajibu wake na kisha kukwamisha shughuli hii muhimu yenye nia njema kwa maisha ya watanzania.

Akihitimisha maagizo hayo  Naibu waziri Suleima Jafo, amezishukuru  Wizara zote za kisekta katika kusukuma gurudumu la maendeleo  na kwenda sambamba na kasi ya Rais  Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ya HAPA KAZI TU,  ikiwapo, Wizara ya Afya, Fedha na Mipango pamoja na watendaji wa Ofisi yake ambao walikuwa bega kwa bega katika mchakato wote wa kupatikana kwa fedha.

RC SHIGELA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA -UTPC MKOANI TANGA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela leo Ijumaa Septemba 15,2017 amefungua mkutano Mkuu wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs- UTPC) mwaka 2017. 

Mkutano huo uliokutanisha viongozi wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa 27 nchini unafanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort mkoani Tanga. 

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo ambao utafanyika kwa muda wa siku mbili (Septemba 15 na 16,2017),Shigela alisema serikali inatambua umuhimu wa vyombo vya habari katika maendeleo ya jamii. 

“Ukitaka maendeleo katika jamii lazima ushirikiane na vyombo vya habari,na hata tunapoelekea katika Tanzania ya viwanda ni vyema vyombo vya habari vihusike”,alieleza. Alitumia fursa hiyo kuwataka waandishi wa habari nchini kuzingatia maadili katika kazi yao ya uandishi wa habari huku akiwaasa kujiendeleza kielimu ili kufanya vizuri zaidi katika kazi yao. 

“Vyombo vya habari vinafundisha,vinaelimisha,vinahamasisha ,vinakosoa na kufichua maovu na ili kutimiza haya ni vyema mkazingatia maadili yenu,mfanye kazi kwa usawa bila upendeleo lakini pia ni vyema mkawa wazalendo”,aliongeza. Kwa Upande wake rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo alisema miongoni mwa changamoto zinazoikabili tasnia ya habari ni uwepo wa sera na sheria zinazobinya uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo sheria ya Habari ya habari ambayo baadhi ya vifungu vyake siyo rafiki kwa waandishi wa habari. “Tunaiomba serikali ifanye marekebisho katika baadhi ya vifungu kwenye sheria hii ambavyo siyo rafiki kwa vyombo vya habari”,aliongeza Nsokolo. 

Mkutano wa 37 wa AGMC wafanyika jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe akihutubia wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Kituo cha Madini na Kijiosayansi cha Afrika (AMGC) jijini Dar es Salaam baada ya Kituo hicho kutimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake. 
 Mwakilishi Mkazi wa Masuala ya Uchumi kutoka Ubalozi wa China, Lin Zhiyong mmoja wa wafadhili wa AMGC akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo, Ibrahim Shaddad kwa ushirikiano mwema uliopo kati yao.
 Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania, Monica Patricio Clemente akichangia hoja katika Mkutano wa Baraza la Uongozi wa AMGC jijini Dar es salaam.
Wajumbe mbalimbali wa Mkutano wa Baraza la Uongozi wa AMGC wakiwa katika kikao cha 37 nchini Tanzania.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILISHA HOTUBA YA KUAHIRISHA BUNGE

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasilisha hotuba ya kuahirisha Bunge mjini Dodoma Septemba 15, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Wabunge baada ya kuwasilisha hotuba ya kuahirisha Bunge mjini Dodoma Septemba 15, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwenye ukumbi wa Spika baada ya kuwasilisha hotuba ya kuahirisha Bunge mjini Dodoma Septemba 15, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA ZA MATUKIO YA OFISI YA WAZIRI MKUU BUNGENI.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akisalimiana na baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari ya Jamhuri walipotembelea Bungeni Septemba, 2017 Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari ya Jamhuri waliotembelea Bungeni Septemba, 2017 Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jamhuri waliotembelea Bungeni tarehe 13 Septemba, 2017 Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA)

MRADI WA KUZALISHA UMEME STIEGLER’S GORGE HYDROPOWER DAM WATARAJIWA KUWA MUARUBAINI WA UPUNGUFU WA UMEME -RC NDIKILO

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi ,Rufiji

Wakazi wa wilaya ya Rufiji ,Mkoani Pwani pamoja na watanzania kijumla wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (stiegler’s gorge hydropower dam project),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 .

Mradi huo utazalishwa kutoka chanzo hicho , katika pori la akiba la Selou Kanda ya Kaskazini (Matambwe ).Kwasasa nchi inazalisha megawatts 1,450 lakini Stiegler’s gorge itazalisha megawatts 2,100 hali itakayoleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi .

Akizungumza mara baada ya kwenda kukagua na kujiridhisha eneo utakapozalishwa mradi huo kabla ya utekelezaji kuanza,Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, alisema tangazo rasmi limeshatolewa na wizara ya nishati na madini tangu august 30 mwaka huu.

Aidha alifafanua ,tangazo hilo linawapa nafasi kwa makampuni ya ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme .Mhandisi Ndikilo,alibainisha kampuni yoyote iwe ya ndani ama nje ya nchi ikikidhidhi vigezo itatangazwa .
Alieleza endapo mradi utakamilika utawezesha kuwepo kwa umeme wa uhakika na kuvutia wawekezaji kwa wingi.Mhandisi Ndikilo ,alisema wilaya ya Kisarawe na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Kibiti na Rufiji umeme ukatikakatika hivyo kuna changamoto ya upungufu wa umeme hali inayokwamisha jitihada za kuinua sekta ya uwekezaji na viwanda .
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akionyesha eneo la mradi litakapozalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Dam),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 za umeme.(Picha na Mwamvua Mwinyi )
Eneo la mradi litakapozalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Dam),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 za umeme,linavyoonekana .
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mloka kilicho karibu na pori la akiba la Selou .
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,na ujumbe wake wakikagua eneo la mto huo.(Picha na Mwamvua Mwinyi ).



WANANCHI WA KILOLO MKOANI IRINGA WAJITOKEZA KWA WINGI KUJISAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa limeendelea mkoani Iringa ambapo mara hii linafanyika katika Wilaya ya Kilolo Kata za Kimala, Idete na Dabaga.

Kwa mujibu wa Afisa Usajili wa Wilaya hiyo Ndugu Kelfasi Walingozi utaratibu unaotumika ni wa kuwasajili Wananchi kwa Kata ambapo kwa kushirikiana na Viongozi wa Wilaya, Kata, Mitaa na Vijiji. Amesema mpaka sasa zoezi limeanza vizuri na mwitikio wa watu ni mkubwa sana.

“ Kwakweli umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa ni mkubwa kwa wananchi na wananchi wanatambua umuhimu wake ndiyo maana unaona wazee hawa wanajihimu kufika kwenye vituo kusajiliwa” Alisema .

Mkoa wa Iringa uko kwenye Wilaya ya mwisho kukamilisha usajili Vitambulisho vya taifa ambapo Wilaya zingine za Mufindi na Iringa tayari zilishakamilisha zoezi hilo na wananchi kwa sasa wanasubiri kukabidhiwa Vitambulisho vyao.
Wakazi wa Kijiji cha Itonya wakiwa wamekusanyika kwenye kituo cha Usajili kilichopo Wilaya ya Kilolo mkoa wa Lindi. Mbali na kujaza fomu za maombi ya Vitambulisho wakazi hao pia wanachukuliwa alama alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki.
Hawa ni baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kimala Kata ya Kimala wakiwa wamejumuika na baadhi ya wazee kupata huduma ya Usajili wakati zoezi la kuwasajili likiendelea kijijini hapo. 
Mkazi wa Kijiji cha Uluti Kata ya Kimala akiweka alama za vidole kwenye mashine ya kuchukua alama za kibaiolojia wakati wa Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kijijini hapo.
Kinamama wakikamilisha zoezi la Usajili linaloendelea katika Kijiji cha Uluti. Mpango wa Usajili katika Kijiji hicho umezingatia utaratibu wa kutoa kipaumbele kwa kina mama na watoto, wazee na wajawazito wanaofika kijijini hapo kupata huduma ya usajili.

UBALOZI WA MAREKANI WAENDESHA MAHAFALI YA WASHIRIKI WA PROGRAMU YA MAFUNZO YA KIINGEREZA DAR ES SALAAM

$
0
0
Afisa wa Ubalozi wa Marekani anayeshughulikia masuala ya umma Bi. Brinille Ellis aliwakaribisha wanafunzi, wazazi na walimu zaidi ya 100 katika Shule ya JOMAK School iliyopo huko  Bahari Beach katika mahafali ya washiriki wa programu ya mafunzo ya Kiingereza inayofadhiliwa na Ubalozi iitwayo “English Access Microscholarship Program”.  
Wanafunzi wapatao 25 wa vidato vya tatu, nne na tano walianza kuhudhuria mafunzo yao ya Kiingereza baada ya masomo ya kawaida shuleni katika shule ya JOMAK hapo mwezi Septemba mwaka 2015.  Hawa watakuwa kundi la kwanza la wahitimu wa programu hii jijini Dar es Salaam. Serikali ya Marekani inafadhili madarasa mengine matatu hapa nchini chini ya programu hii.  Hii ni pamoja na darasa la pili katika shule ya JOMAK na madarasa mawili mjini Moshi yanayoendeshwa na taasisi iitwayo Kilimanjaro Information Technology. Inatarajiwa kuwa madarasa mengine yataanza mwezi Januari 2018 katika miji ya Mwanza, Tanga and Zanzibar. 

Bi. Ellis aliwapongeza wanafunzi wa programu hii kwa kujitoa kwao kwa dhati na kushiriki kikamilifu katika mafunzo yao: “Kwa kupitia programu ya Access mmepata mambo mengi zaidi ya ujuzi wa lugha ya Kiingereza. Mmekuwa viongozi wa jamii na mfano wa kuigwa katika jamii zenu.” Wakati wa hafla hii, wanafunzi walifanya maonyesho na kutambulisha kwa Kiingereza miradi na kazi mbalimbali za kuhudumia jamii walizozifanya wakati wa mafunzo yao katika programu hii. 

Programu ya Access hutoa mafunzo ya msingi ya lugha ya Kiingereza kwa watoto na vijana wenye vipaji wa kuanzia miaka 13 hadi 20 kutoka jamii zenye hali duni kiuchumi kupitia madarasa yanayoendeshwa baada ya muda wa shule na yanayotoa mafunzo ya kina.  Programu ya Access huwapatia washiriki wake stadi za lugha ya Kiingereza jambo ambalo huwapa fursa zaidi za kielimu na ajira.  Toka mwaka 2004, zaidi ya wanafunzi 200 kutoka Tanzania na 100,000 kutoka zaidi ya nchi  85 wameshiriki katika programu hii. 

SESEA yahitimisha mufunzo ya kitaalamu Halmashauri ya kilwa

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

Mradi wa kuimarisha  mifumo ya elimu   katika nchi za Afrika mashariki  (SESEA)  ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda imehitimisha mafunzo yake kupitia chuo kikuu cha  Agha Khan katika wilaya ya Kilwa  mkoani Lindi.
Hafla hiyo iliofanyika katika Halmashauri ya Kilwa mkoani Lindi ambao mradi huo unoafadhiliwa  na Global Affairs Cannada pamoja na Agha Khan Foundation unaolenga kuongeza  taaluma  kwa walimu wa shule za awali  na za msingi  ili kufikia idadi kubwa ya wasomi nchini.

Akizungumza  Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu, Sayansi, teknolojia na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu katika  hafla hiyo ya kuhitimisha mafunzo hayo  amesema kuwa   ushirikishwaji  kwa wazazi na  jamii kwa njia ya warsha  na semina  umesaidia kuongeza ushiriki katika  kusaidia  kuleta matokeo chanya  ya elimu kwa watoto wa kike na wa kiume  na imesaidia  kuweza kutunga vitabu vya hadithi  kwa lugha ya Kiswahili, na kiingereza   na kaika nukta nundu kwa kuzingatia mazingira yao.

Hata hivyo  Slyvia Temu amesema kuwa  kupitia mbinu ya Education Community of Practice mradi umeshirikiana na Halmashauri  kuanzaisha jumuiya za kitaaluma  za walimu 1,200 kwenye shule zote 150, jumuiya hizi huwai hukutana shuleni na kwenye klasta zao kuimarisha utaalamu wa kufundishia mbinu mpya ya kusoma kwa kujifunza (Reading to learn) ikiwa miongoni mwa walimu zaidi 750 waliopata mafunzo  hayo  na mradi uliwaongezea maarifa walimu 307 wanaume wakiwa ni 179 na wanawake ni  128 ili kuwafanya walimu wawe imara zaidi.

Nae  mwakilishi wa mkuu wa chuo cha Agakhan, Mkurugenzi wa mradi  Nicolaus Washira  amesema kuwa SESEA  lengo lake ni kutaka kuinua  na kuimarisha Elimu nchini pamoja na  kuongeza wigo la wasomi  kwa kutembelea wilaya 4 ambazo ni Klwa, Nachingwea, Newala pamoja na Lindi Vijijni.

Vilevile Mkurugenzi wa mradi, Bernard Orimbo amesema kuwa ;bila kupata Elimu  huwezi kupata maendeleo na ili nchi iweze kupata  mafanikio  huwezi kutumia bunduki bali elimu ndio hupaswa kuwa stari wa mbele; amesema Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu, Sayansi, teknolojia na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu  akizungumza na walimu wa Shule za msingi  ambapo walimu walifanya maonesho ya zana  za vitendo ambazo hutumika katika kufundishia  wanafunzi pindi wanapokuwa masomoni katika Halmashauri ya Kilwa mkoani Lindi. Profesa Slyvia Temu alimwakilisha  wa Katibu mkuu Wizara elimu, sayansi na teknolojia,  Dkt Leonard  Akwilapo.
Wanafunzi wa Shule za msingi  waliojitokeza katika hafla hiyo wakisikiliza namna jinsi SESEA inavyotoa huduma ya  Elimu na umuhimu wake katika Halmashauri ya Kilwa  mkoani Lindi.

Mwenyekiti wa Bodi TanTrade Eng. Christopher Chiza atembele mipaka ya Tanzania na Burundi

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi TanTrade Eng. Christopher Chiza akiongea na Waandishi wa Habari katika Mpaka wa Mabamba Wilayani Kibondo, Kigoma baada ya kumaliza ziara ya siku nne ya kutembelea Mipaka mitano ya Tanzania na Burundi iliyopo Mkoani Kigoma. 
Lengo la ziara hii lilikuwa la kukutana na Taasisi za Serikali na Wafanyabiashara kujadili mpango wa kuwekeza miundombinu ya kurasimisha biashara ya Mpakani na kuhamasisha ushiriki katika Kongamano na Maonesho ya Tanzania Bujumbura Burundi yatakayofanyika kuanzia tarehe 27.09 mpaka tarehe 1.10.2017. Karibuni sana tushiriki katika matukio haya ya muhimu ya kihistoria.

DAWASCO YAWASHAURI WANANCHI KUHIFADHI MAJI KUPISHA MABORESHO YA MTAMBO WA MAJI RUVU CHINI

VOA inakuletea Zulia Jekundu S1 Ep 140: Nicki Minaj, Rihanna, Taylor Swift, Janet Jackson na Sloane Stephens

MICHUZI BEAT: KUTANA NA MCHEKESHAJI NASSOR BACHO

KAMPUNI MPYA YA USAMBAZAJI WA KAZI ZA WASANII YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Jengo la Kampuni mpya ya usambazaji wa kazi za wasanii wa Bongo Movie, lililopo Kinondoni Hananasifu, Jijini Dar es salaam. Uongozi wa Kampuni hiyo umefanya Uzinduzi wake rasmi jioni hii na kuhudhuliwa na Wasanii mbalimbali pamoja na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Muonekani wa Jengo hilo kwa mbele.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Treeo Tabasamu, Ritchie Mtambalike akizungumza katika Uzinduzi rasmi wa Kampuni hiyo, jioni hii katika ofisi zao, Kinondoni Hananasifu, Jijini Dar es salaam. 
Mkuu wa Kitengo za Masoko wa Kampuni ya Treeo Tabasamu, Jacob Steven (JB) akizungumza katika Uzinduzi rasmi wa Kampuni hiyo, jioni hii katika ofisi zao, Kinondoni Hananasifu, Jijini Dar es salaam. 

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 15.09.2017

MAJAJI WAFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA WAKUTANA JIJINI ARUSHA KUJADILI USIKILIZAJI MASHAURI KWA HARAKA NA KUONDOSHA MLUNDIKANO WA MASHAURI

$
0
0
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akitoa neno katika kikao cha Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kikao hicho cha siku mbili kimeanza kufanyika mapema Septemba 15 katika UkumbiwaMikutano wa Kimataifa (AICC) uliopo jijini Arusha

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akiendesha kikao cha Majaji Wajaji kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano (AICC) jijini Arusha, wanaoonekana katika picha (wa pili kushoto) ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda Iringa, Mhe. Mary Shangali, wa pili kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein A. Kattanga na wa kwanza kushoto ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati.

 Waheshimiwa Majaji Wafawidhi wakiwa katika kikao hicho,wa kwanza kulia ni Mhe. Salvatory Bongole, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Bukoba, katikati ni Mhe. David Mrango, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu-Kanda ya Songea, na wa kwanza kushoto, ni Mhe. Firmin Matogolo, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu-Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

 Baadhi ya Waheshimiwa Majaji Wafawidhi wakiwa katika kikao hicho.
 1.      Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Makaramba akichangia katika Mkutano wa Majaji Wafawidhi unaofanyika jijini Arusha, lengo la Mkutano huo ni kujadiliana kwa pamoja juu usikilizaji wa kesi wa haraka na kuondoa mlundikano wa mashauri na hatimaye wananchi waweze kupata haki zao kwa wakati na hatimaye nguzo namba mbili ya  Mpango Mkakati wa Mahakama ya Upatikanaji na utoaji wa Haki kwa wakati kutekelezeka ipasavyo.

Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ilvin Mugeta akiwasilisha mada mbele ya Wahe. Majaji Wafawidhi (hawapo  pichani)

filamu mpya ya NDOTO YA wana Diaspora wa Kitanzania waishio Ufaransa

$
0
0
Bango la pili la filamu mpya ya NDOTO YA wana Diaspora wa Kitanzania waishio Ufaransa limeachiwa rasmi kusisitiza ujio wa filamu hiyo inayosubiriwa kwa hamu kila kona ya dunia. Yaani baada ya kupasha kwa bango la kwanza kuonyesha baadhi ya waigizaji nyota, mara hii bango linaonyesha wahusika wapya na waandaaji wakikwambia  kaa mkao wa kula na tegemea mazuri!

IGP SIRRO- NCHINI UGANDA kushiriki Mkutano wa 19 wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi ya Nchi za Mashariki

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, yupo Kampala nchini Uganda, kushiriki Mkutano wa 19 wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi ya Nchi za Mashariki (EAPCCO) ulioanza 13-15 Septemba 2017 ukiwa na malengo ya kujadiliana kwa pamoja namna ya kupambana na uhalifu unaovuka mipaka (Cross Border Organized Crimes) na kubadilishana uzoefu wa kiutendaji pamoja na kuimarisha Ushirikiano miongoni mwa Majeshi ya Polisi. Picha na Jeshi la Polisi Tanzania.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 19 wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi ya Nchi za Mashariki (EAPCCO) unaofanyika Kampala nchini Uganda, wakifuatilia mada inayowasilishwa mbele yao katika mkuatano ulioanza 13-15 Septemba 2017 ukiwa na malengo ya kujadiliana kwa pamoja namna ya kupambana na uhalifu unaovuka mipaka (Cross Border Organized Crimes) na kubadilishana uzoefu wa kiutendaji pamoja na kuimarisha Ushirikiano miongoni mwa Majeshi ya Polisi, katika mkuatano huo yupo pia Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro. Picha na Jeshi la Polisi Tanzania.

MKURUGENZI WA MAENDELEO YA JAMII AONGOZA UCHIMBAJI WA LAMBO KATIKA KIJIJI CHA MANGHANGU, MPWAPWA DODOMA

$
0
0

Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Serikali imeadhimia kuwa Sera ya Maendeleo ya Jamii ya mwaka 1996, inatekelezwa kikamilifu na inafuatilia utekelezaji wa Sera hiyo katika ngazi ya mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji mbalimbali hapa nchini.

Akiongea na wananchi wa Kijiji cha Manghangu, kilichoko Kata ya Vinghawe Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amesema Sera hiyo imeweka wazi kuwa wananchi ndiyo kitovu cha maendeleo maana ushiriki wao unatoa dhamana thabiti ya maendeleo na ustawi wa wananchi katika ngazi mbalimbali.

Bw. Patrick Golwike ametanabaisha kuwa lengo la kufika katika Kijiji hicho ni kushirikiana na wananchi kufanya kazi za maendeleo kwa vitendo.

“Kazi ya kuhamsha ari iliyobuniwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inalenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika kuibua miradi, kupanga, kutekeleza na kusimamia shughuli za maendeleo kwa kutumia rasilimali zilipo katika mazingira yao ili kujiletea maendeleo yao” alisema Bw. Golwike.

Kwa upande wake Mratibu wa masuala ya Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI Bibi Mwajina Lipinga, alisema kuwa mradi wa ujenzi wa lambo la maji, na ushiriki wa wananchi katika kazi za kujitolea utakuwa chachu kwa vijana kuhamsha ari ya kujitolea na kuchangia maendeleo ya vijiji na Taifa.
Sehemu ya vijana wa Kijiji cha Manghungu, Kata ya Vinghawe Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma wakishiriki kazi ya kuchimba Lambo kwa kutumia nguvu zao wenyewe. 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akishiriki kuchimbua eneo la Lambo la Kijiji cha Manghungu, Kata ya Vinghawe Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bw. Mohamed Maje akiweka mchanga kwenye ndoo katika zoezi la uchimbaji wa Lambo Kijijini cha Manghungu.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Manghungu, kata ya Vinghawe Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma wakishiriki kazi ya kuchimba Lambo kwa kutumia nguvu zao wenyewe.

Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images