Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110082 articles
Browse latest View live

UINGIZAJI WA MIFUGO KWENYE PORI LA AKIBA LA MKUNGUNERO UMEADHIRI UHIFADHI

$
0
0
Na mwandishi wetu, Kondoa.

Uingizaji wa mifugo kwenye pori la akiba la Mkungunero lililoko wilayani Kondoa mkoani Dodoma umeathiri uhifadhi wa pori hilo na kusababisha kukauka kwa baadhi ya vyanzo vya maji na kutoweka kwa baadhi ya wanyamapori adimu.


Meneja wa Pori la akiba la Mkungunero, Emmanuel Bilaso akizungumza na a waandishi wa habari waliotembelea pori hilo hivi karibuni amesema pori hilo linalopakana na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire lina vyanzo muhimu vya maji ambayo yanayotegemewa na wananchi wengi kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.



Bilaso amesema pori hilo la Mkungunero pia lina vyanzo vya maji ya mto Tarangire ambao ndiyo uhai wa Hifadhi ya taifa ya Tarangire na akatoa wito kwa wananchi kutilia mkazo uhifadhi ambao una umuhimu mkubwa kwa jamii na maendeleo ya taifa.



Amesema operesheni inayoendelea katika pori hilo imefanikisha kukamata kwa mifugo mingi katika pori hilo ambayo inachunga humo kinyume na sheria ya uhifadhi ambayo inakataza shughuli za binadamu kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.



“Tumekamata ng’ombe zaidi ya 230 ambao waliingizwa na wananchi kinyume cha sheria na wamefikishwa mahakamani na kutozwa faini ya zaidi ya shilingi milioni 6” alisema bwana Bilaso.



Aliongeza kuwa kuingiza ng’ombe ndani ya hifadhi ni kinyume cha sheria ya uhifadhi ambayo inatoa adhabu kali ikiwemo kutaifisha mifugo inayokamatwa ili iwe fundisho kwa watu wanaovunja sheria za uhifadhi.





WANANCHI WA KATA YA MONDO WILAYANI MISUNGWI MKOANI MWANZA WAELEZEA UMUHIMU WA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI MJINI DODOMA LEO SEPTEMBA 14,2017

$
0
0
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akiwasilisha muswada wa sheria ya madaktari, madaktari wa meno na wataalamu wa Afya shirikikishi (The medical, Dental and Allied Heath Professional) leo Bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo kuhusu muswada wa sheria ya madaktari, madaktari wa meno na wataalamu wa Afya shirikikishi (The medical, Dental and Allied Heath Professional) leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuimarisha zao la tangawizi pamoja na Kiwanda cha kuchakata Tangawizi ili iweze kuuzwa katika soko la Kimataifa.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Genista Mhagama akizungumzia hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kutatua changamoto zilizobainishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo kuhusu uchambuzi wa Sheria ndogo zilizowasilishwa katika mkutano wa sita na wa saba wa Bunge.
Baadhi ya Wabunge wakiwasili katika viwanja vya Bunge leo Asubuhi kushiriki kikao cha bunge.Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma

AFRIKA IANDAE RASILIMALI WATU KUSIMAMIA SEKTA YA MADINI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mataifa ya Afrika yanatakiwa yaandae maarifa, vitendea kazi na rasilimali watu watakaoweza kusimamia na kuendeleza ipasavyo sekta ya madini na kuleta tija kwa Taifa husika na wananchi kwa ujumla.
Amesema taarifa za kijiolojia zinaonesha kuwa Afrika ni Bara lenye utajiri mkubwa wa rasilimali madini huku sehemu kubwa ya madini hayo yakiwa bado hayajaanza au yako kwenye hatua mbalimbali za uendelezaji.
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Septemba 14, 2017) alipofungua mkutano wa 37 wa Baraza la Uongozi wa Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kituo hicho mkoani Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amesema rasilimali za madini ilizopo Barani Afrika inaweza kuwa ni chanzo kikubwa cha kusukuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi nyingi iwapo itasimamiwa vizuri. 
Ametolea mfano Tanzania ambayo licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu, almasi, chuma, madini ya vito kama tanzanite lakini mchango wa sekta ya madini ni asilimia 4.8 ya pato ghafi la Taifa.
“Changamoto kuu kwa sasa ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa na sekta ya madini inayotoa mchango stahiki katika nchi husika pamoja na kusimamia sekta hii kwa kuwafanya wananchi wetu hususan katika maeneo yenye rasilimali wakanufaika na kuona fahari badala ya kuacha mashimo, umasikini na mateso kwa wananchi.”
Amesema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ambacho leo kimetimiza miaka 40 ni kuhakikisha sekta ya madini inawajibika kuleta maendeleo ya kijamii na uchumi pia ikijali masuala ya mazingira, hivyo ni vema kikatumika kama ilivyokusudiwa.

Waziri Mkuu amesema kituo hicho kikitumika vema kwa mujibu wa kusudia la uanzishwaji wake kinaweza kuleta tija kubwa kwenye sekta ya uchumbaji wa madini, uongezaji wa thamani na usimamizi wa sekta.
Amesema kituo hicho ni moja kati ya taasisi chache duniani yenye teknolojia za kisasa ambazo zinaweza kusaidia kufanya uchambuzi wa miamba na madini yaliyimo. “Pia ni sehemu ambayo unaweza kupata huduma za ushauri na kusaidia teknolojia utakayoweza kutumia ili kufanya uzalishaji wa madini mbalimbali.”
Hivyo amewakumbusha wajumbe na wanachama wa AMGC kuwa kituo hicho hawajakitumia ipasavyo ni vema kikatumika ili kupata tija kwenye uendelezaji na usimamizi wa madini, ambapo ameiagiza Bodi iandae mpango utakaoziwezesha nchi wasnachama kukitumia.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amesema kwa sasa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ya kwanza ni kwa wanachama kutolipa ada kwa wakati.
Dkt. Kalemani ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Kituo cha AMGC amesema changamoto ya pili ni wanachama wa kituo hicho kutokitafutia wateja na masoko. Pia miundombinu mingi ya kutuo ni chakavu.
Akizungumzia changamoto hizo Waziri Mkuu ameziagiza nchi zote zinazodaiwa ada ikiwemo Tanzania zilipe ada stahiki kwa wakati na kuweka mkakati wa kukitangaza kituo hicho ili kukiwezesha kupata wateja kwa ajili ya kutumia huduma zitolewazo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
ALHAMISI, SEPTEMBA 14, 2017.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Vitu vilivyo tengenezwa na kituo cha Madini.Wakati alipo fika kwa ajili ya Ufunguzi wa Mkutano wa 37 wa Baraza la Uongozi wa Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika(AMGC) uliofanyika leo Septemba 14/2017 Mkoani Dar es salaam kulia kwake ni Naibu wa Nishati na Madini DR Kaliman .Picha na Ofisi y Waziri Mkuu

Uhamiaji yapata msaada wa vitendea kazi toka Shirika la IOM

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala akipokea msaada wa vifaa mbalimbali uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM. Anayekabidhi vifaa hivyo ni, Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania Dkt. Qassim Sufi. Vifaa hivyo vinajumuisha Kompyuta, mashine za kutolea nakala na kuchapishia vyenye thamani ya Dola za Kimarekani elfu arobaini.

Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na wana habari Limefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala akibadilishana nyaraka za makabidhiano ya msaada wa vifaa mbalimbali uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM. Anayebadilishana naye ni Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania Dkt. Qassim Sufi. Vifaa hivyo vinajumuisha Kompyuta, mashine za kutolea nakala na kuchapishia vyenye thamani ya Dola za Kimarekani elfu arobaini. Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na wanahabari Limefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu yaUhamiaji, Kurasini, Dar es Salaam. 

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 15, 2017

Kukamata na kuchoma nyavu haitoshi, tuwachome wahalifu- RC Rukwa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafi Zelote Stephen ameionya idara ya uvuvi iliyo chini ya wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini kuhakikisha wanawachukulia hatua wale wote wanaokamatwa na zana haramu za uvuvi na kutangaza hukumu zao na si kuishia kwenye kuchoma zana zao tu.

Ameyasema hayo wakati akijiandaa kushiriki zoezi la kuteketeza zana haramu zilizokamatwa kupitia doria katika vijiji vya Kabwe, Isaba, Chongokatete, mandakerenge, kolwe, lupata na kisenga katika wilaya ya Nkasi Mkoani humo. zoezi lililofanyika katika mwalo wa kijiji cha Kirando. 

“Kukamata na kuchoma haitoshi, kwasababu hii inaungua tu, nataka tuwachome wahalifu kwa kutumia sheria, nimechoma sana nyavu hizi na huu mtindo bado unaendelea, hii haina tija, kila tukichoma madhara yanatokea, mazingira yanaharibika, sasa tuseme basi, ningependa kusikia mhalifu kakamatwa kapelekwa mahakamani na kupewa adhabu,” Amesema

Katika kuhakikisha wahalifu hao wanapatika Mh. Zelote amewaasa watumishi wa idara hiyo kuachana na kupokea rushwa, jambo ambalo linaonekana kukwamisha juhudi za serikali katika kulinda rasilimali zake kwaajili ya faida ya kizazi hiki na kijacho.

Amesisitiza kuwa wananchi bado wanahitaji kuendelea kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa rasilimali hizo na wajulishwe kuwa rasilimali hizo ni za watanzania wote na hatimae kuacha tabia kuvua samaki hao kwa zana zisizokubalika na sheria za serikali.

Mh. Zelote aliishauri idara hiyo kuwa panapokuwa na zoezi hilo linalofanyika mbele ya wananchi wahakikishe kunakuwa na nyavu halali zinazokidhi viwango vya serikali na kuwaelimisha wananchi tofauti iliyopo ili wasiojua nao wapate kufahamu matakwa ya serikali katika kuhifadhi mazingira.

Kutokana na doria hiyo iliyofanywa na kikosi cha usimamizi wa rasilimali za uvuvi Kijiji cha Kipili kwa kushirikiana na polisi pakmoja na kikosi cha jeshi la wanamaji wote wa kipili kuanzia Juni hadi September 2017 waliweza kukamatanyavu zisizokidhi viwango vya serikali zenye thamani ya shilingi milioni 57.6.

Miongoni mwa nyavu zilizokamatwa ni nyavu 32 za Makira (gilinets) zenye thamani ya shilingi milioni 38.4, nyavu za dagaa zenye macho chini ya 8mm zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 na makokoro ya vyandarua yenye thamani ya shilingi milioni 2.7.

Awali akisoma taarifa hiyo fupi ya uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwa mgeni rasmi Afisa mfawidhi idara ya uvuvi kanda ya Rukwa Juma Makongoro alitaja kuwa kuna manufaa mengi yanayopatikana kutokana na rasilimali hiyo ikiwa ni pamoja na watu kujipatia ajira, kitoweo, fedha za kigeni na kuingizia serikali kodi ambayo hutumika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mtaaafu Zelote Stephen (Kulia)akitoa maelekezo namna ya kuziteketeza nyavu haramu (hazimo kwenye picha) mbele ya maafisa aliongozana nao kushiriki uteketezaji wa zana hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mtaaafu Zelote Stephen (Katikati Mwenye suti ya ugoro) akiwasha moto tayari kwaajili ya kuzitekezeteza zana haramu, kulia ni Juma Makongoro Afisa Mfawidhi Idara ya Uvuvi kanda ya Rukwa kushoto ni diwani wa kata ya kirando Kessy Sood


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mtaaafu Zelote Stephen kwa pamoja na Mfawidhi Idara ya Uvuvi kanda ya Rukwa Juma makongoro pamoja na Diwani wa Kata ya Kirando Mh. Kessy Sood wakiteketeza zana haramu.
Nyavu zenye thamani ya shilingi milioni 57.6 zikiteketea kwa moto mbele ya wananchi, katika mwalo wa kijiji cha kirando, Ziwa Tanganyika, Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.

Tanzania iko Tayari kuwa Mwenyeji wa Tamasha la JAMAFEST 2019-Dkt. Harrison Mwakyembe:

$
0
0

Na Benedict Liwenga-WHUSM, Kampala-Uganda.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kwamba, Tanzania iko tayari kuwa wenyeji wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki maarufu kama JAMAFEST kwa mwaka 2019.

Kauli hiyo ameitoa jana Mjini Kampala nchini Uganda wakati wa Ufungaji wa Tamasha hilo kwa mwaka 2017 ambapo wenyeji kwa mwaka huu walikuwa ni nchi ya Uganda.

Mhe. Mwakyembe amezipongeza nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo zimehudhuria tamasha hilo kwa ushirikiano wa hali ya juu katika kubadilishana uzoefu na ujuzi juu ya masuala mbalimbali yanayohusu utamaduni na sanaa kwakuwa yameongeza mahusiano mapya ya karibu baina ya nchi hizo.

Waziri Mwakyembe aliezea kufurahishwa kwake kwa kujionea ngoma mbalimbali za kitamaduni toka kwa nchi wanachama ambazo zinaakisi uhalisia wa utamaduni wa nchi hizo, pia amefurahishwa na kwa kujionea bidhaa mbalimbali adimu toka kwa nchi hizo jambo ambalo amesisitiza kwamba nchi wanachama hazinabudi kuendelea kushirikiana katika kuzilinda tamaduni hizo na kuendelea kujifunza ujuzi mbalimbali wa kazi za sanaa.

“Nilipotembelea Maonyesho ya Tamasha hili pale katika viwanja vya Kololo nilifurahi sana kujionea ngoma za kitamaduni toka kwa vikundi mbalimbali vya nchi wanachama wa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki, hakika inapendeza sana, kwakweli tuzidi kuzilinda tamaduni zetu na kushirikiana kwa karibu zaidi”, alisema Mhe. Mwakyembe.

Akiongea kuhusu suala la Tanzania kukubali kuwa wenyeji wa Tamasha lijalo litakalofanyika mwaka 2019, Dkt. Mwakyembe alisema kwamba, Tanzania iko tayari kuwa wenyeji katika tamasha hilo lijalo na amezitaka nchi wanachama kujitahidi kushiriki pasipo kukosa wakiwa na bidhaa zao za kutosha huku akiwaahidi kuwa pindi wajapo Tanzania watafurahia mambo mengi na kujionea namna Watanzania wanavyo chapa kazi kutokana na kaulimbiu ya ‘HAPA KAZI TU’ iliyoasisiwa na Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

“Kwakuwa mwaka 2019 ni mzunguko wa Tamasha kama hili niwaambie kwamba, Tanzania iko tayari kuwa mwenyeji wa Tamasha hili na nawakaribisheni kwa dhati kabisa mje kujionea nchi yetu na namna tunavyofanya kazi kwa bidii, lakini pia mje na bidhaa nyingi zaidi kwa ajili ya kuwaonyesha Watanzania”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Tamasha la JAMAFEST lilianzishwa mwaka 2013 nchini Rwanda na baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kwa mwaka huu tamasha hilo linafanyika mjini Kampala nchini Uganda ambapo kwa mwaka 2019 linatarajiwa kufanyika nchini Tanzania.
Naibu Waziri Mkuu ambaye ni Waziri wa Wizara ya Mambo ya Afrika Mashariki ya Uganda Mhe. Ali Kirunda Kivejinja akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe kabla ya kumkabidhi Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuashiria kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni zamu yake kukabidhiwa dhamana ya kuandaa Tamasha la Nne (4) la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) litakalofanyika mwaka 2019.
Naibu Waziri Mkuu ambaye ni Waziri wa Wizara ya Mambo ya Afrika Mashariki ya Uganda Mhe. Ali Kirunda Kivejinja akabidhi Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe ikiashiria kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni zamu yake kukabidhiwa dhamana ya kuandaa Tamasha la Nne (4) la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) litakalofanyika mwaka 2019 jana usiku hafla hyo ilifanyika katika Jumba la Sanaa la Taifa jijini Kampala Nchini Uganda.
Kaimu Balozi ambaye pia Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Balozi Elibariki Nderimo Maleko aliyevaa shati la kitenge akiwaongoza Washiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika Mashariki pamoja na Watanzania wanaishi Uganda kusherehekea kupokea bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukabidhiwa kutoka kwa Nchi ya Uganda


PPRA NA NEEC ZAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA MIAKA MITANO

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk. Laurent Shirima(kulia)pamoja na Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa wakisaini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano, wanaoshuhudia (kulia )ni Mwanasheria Mwandamizi wa PPRA, Agnes Sayi na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji, Esther Mmbaga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk. Laurent Shirima, pamoja na Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa wakibadilisha hati za mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano mapema jana  jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk. Laurent Shirima,akizugumza wakati wa hafla ya utiliaji saini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) mapema jana jijini Dar es Salaam.(kushoto)ni Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’I Issa. 
.Sehemu ya watendaji na waandishi wa habari wakiwa katika hafla hiyo.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

BREAKING NYUZZZZZ.....: WATUHUMIWA WAWILI KIZIMBANI KWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Mkurugenzi wa Tathmini Archad Alphonce Karugendo na Mthamini Wa Serikali Wa Madini, Edward Joseph Rweyemamu, mapema asubuhi hii, wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, jijini Dar es salaam kujibu shtaka moja la kuisababishia serikali ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania hasara ya zaidi ya bilioni 2.

Washtakiwa hao wawili wamesomewa shtaka la uhujumu uchumi mbele ya Hakimu Mkazi Respicious Mwijage, ambapo hawakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kisikiliza kesi za namna hiyo. Wamerudishwa rumande.

JAMBO LA AIBU LILILONITOKEA USIKU MBELE YA MKE WANGU.

$
0
0
Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 42 na mkaazi wa jijila Dar Es Salaam. Usiku wa kuamkia tarehe 02 Septemba ya mwaka huu wa 2017, nilipatwa na jambo la kutweza, kufedhehesha na kutia aibu mbele ya mke wangu.
Jambo hili mbali na kunitweza, kunifedhehesha na kunitia aibu, lakini pia limeyabadilisha maisha yangu juu chini na kuweka doa la milele ambalo ninaamini halitafutika kwenye akili na nafsi yangu mpaka siku nitakayo rejea kwa Muumba wangu. 
NI JAMBO GANI HILO ? 

IGP SIRRO ASHIRIKI MKUTANO WA 19 WA SHIRIKISHO LA WAKUU WA MAJESHI YA POLISI YA NCHI ZA MASHARIKI MWA AFRIKA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, yupo Kampala nchini Uganda, kushiriki Mkutano wa 19 wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi ya Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO) ulioanza 13-15 Septemba 2017 ukiwa na malengo ya kujadiliana kwa pamoja namna ya kupambana na uhalifu unaovuka mipaka (Cross Border Organized Crimes) na kubadilishana uzoefu wa kiutendaji pamoja na kuimarisha Ushirikiano miongoni mwa Majeshi ya Polisi.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 19 wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi ya Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO) unaofanyika Kampala nchini Uganda, wakifuatilia mada inayowasilishwa mbele yao katika mkuatano ulioanza 13-15 Septemba 2017 ukiwa na malengo ya kujadiliana kwa pamoja namna ya kupambana na uhalifu unaovuka mipaka (Cross Border Organized Crimes) na kubadilishana uzoefu wa kiutendaji pamoja na kuimarisha Ushirikiano miongoni mwa Majeshi ya Polisi, katika mkuatano huo yupo pia Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro. Picha na Jeshi la Polisi Tanzania.

News Alert: Mahakama yamwachia huru Askofu Gwajima na wenzake watatu

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat gwajima na wenzake watatu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha maahtaka dhidi yao.

Mbali na Gwajima, washtakiwa wengine walioachiwa huru ni Askofu msaidizi Yekonia Bihagaze  (39) mkazi wa Kimara Stop Over, George Mzavaa (43)  anaishi Ilala mabHeofrey Milulu (31) mchungaji mkazi Wa Kumara Baruti.
Askofu Gwajima alikuwa akikabiliwa na shtaka la kushindwa kutunza mahali pa usalama bastora na risasi wakati wenzake wakikabikiwa na tuhuma za kukutwa na bastola hiyo pamoja na risasi 20
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha ambaye amesema upande Wa mashtaka kupitia mashahidi wake wameshindwa kuthibitisha kuwa washtakiwa wametenda kosa hilo. 

alisema kuwa kesi hiyo haijathibitika kwa viwango vinavyotakiwa na kwamba begi lililokuwa na bunduki na risasi virudishwe kwa Askofu Gwajima.

Alisema kuwa hakuna uthibitisho kwamba Gwajima alizembea kusalimisha silaha hizo Polisi na pia hakuna ubishani kwamba alikubali kuripoti katika Ofisi ya  Mpelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO) ambapo alifika akiwa na begi hilo lenye bunduki na risasi 20. 

Ameongeza kuwa hakuna ushahidi kama mshitakiwa hakukaguliwa na polisi yeyote hadi alipokutana na ZCO na kwamba wakati anahojiwa alipoteza fahamu akiwa na begi lake hadi alipozinduka akiwa Hospitali ya TMJ, 

Hakimu Mkeha ameongeza kuwa, uteetezi uliotolewa  unaonyesha wazi mshitakiwa huyo alikuwa makini nyakati zote akiwa na silaha zake kwani hata alipokuwa kitandani alililinda.

"Ingawa sheria kwa namna yoyote haielezi ni lazima shahidi fulani aje lakini kwa mazingira yaliyokuwepo hospitali ambayo kulikuwa na walinzi hawa wangeweza kuletwa kama mashahidi wa upande wa mashitaka lakini hawakuletwa na hawakuingizwa kama wazembe katika kesi hii kitendo ambacho kinaongeza shaka kwa upande wa mashitaka,

Ameongeza kuwa kutokana na mashaka hayo, hakuweza kupata sababu za msingi za kutoamini ushahidi wa nesi ambae alikuwa ni shahidi wa utetezi aliyeeleza namna mambo yote yalivyotokea.

"Nimelazimika kuwaachia huru washtakiwa wote kwani upande wa mashtaka hawajaweza kuthibitisha kesi kwa kiwango kilichotakiwa" amesema Mkeha

Katika hati ya mashtaka ilidaiwa, kati ya Machi 27 na 29, mwaka 2015 jijini Dar ea Salaam, Gwajima akiwa mmiliki na aliyesajiliwa kutunza bastola aina ya berreta yenye namba za usajili CAT 5802 pamoja na risasi zake tatu na risasi 17 za bastola aina yabshortgun alishindwa kuitunza silaha hiyo na kuiacha mikononi mwa Bihagaze, Mzava na Milulu ambao hawatambuliki kisheria.
Aidha washtakiwa hao wakiwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni walikutwa na silaha pamoja na risasi hizo bila ya kuwa na kibali kutoka mamlaka husika.

WASANII na wanamichezo mbali mbali, wazidi kujiunga Uzalendo Kwanza

$
0
0
WASANII na wanamichezo mbali mbali nchini, wameendelea kujiunga na kundi Uzalendo Kwanza lenye nia ya kuurudisha uzalendo wa Mtanzania.

Akizungumza jiji jana, Mwenyekiti wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza  Steve Nyerere alisema wasanii hao wapya na wanamichezo watatambulishwa rasmi kesho.

"Kipindi cha kampeni za uchaguzi kama taifa tuligawanyika, wapo waliokuwa CCM na wapo waliokuwa Ukawa, ni muda muafaka sasa kuacha tofauti zetu za itikadi na kumuunga mkono muheshimiwa rais." alisema Nyerere

Nyerere alisema kampeni ya 'Uzalendo kwanza' ambayo itafanyika mikoa mbali mbali  itaenda sambamba na kutoa misaada  kwa jamii.

Kampeni hiyo  ilizinduliwa hivi karibuni inalengo la kuhamasisha wananchi, taasisi na mashirika mbali mbali kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli katika jitihada za kuleta maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuwa wazalendo kwa kulinda rasilimali za nchi.

UJUMBE WA WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKIWA KATIKA ZIARA YA MAFUNZO NCHINI CHINA.

$
0
0
Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiongozwa na Mhe. Augustino Manyanda Masele (wa pili kulia waliokaa) wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wabunge iliyofanyika jana katika Jiji la Fuzhou nchini China. Ujumbe huo uko nchini China kwa wiki mbili kwenye ziara ya mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya nchi hiyo. 

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

EXIM BANK TANZANIA DONTES 50 BEDS AND MATTRESSES TO MNAZI MOJA HOSPITAL IN ZANZIBAR

$
0
0
 Ambassador Seif Ali Iddi speaking during Exim Bank Tanzania donates 50 beds and mattresses worth TZS 20M/- to Mnazi Mmoja Hospital in Unguja Zanzibar Today.
 Ambassador Seif Ali Iddi 
Group photo of Exim Members  with Ambassador Seif Ali Iddi during Exim Bank Tanzania donates 50 beds and mattresses worth TZS 20M/- to Mnazi Mmoja Hospital in Unguja Zanzibar Today.

EXIM Bank Tanzania has donated 50 beds and mattresses worth TZS 20M/- to Mnazi Mmoja Hospital in Unguja Zanzibar, in its ongoing year-long corporate social campaign aimed at celebrating 20 years of serving the Tanzanian community.

In an attempt to address the chronic bed capacity problem plaguing the nation, Exim Bank launched the campaign dubbed “20 years of taking care of the community” last month during the banks 20th anniversary. In total, the bank is investing TZS 200M/- into the Tanzanian health care by donating 500 mattresses and beds to public hospitals in 13 regions across the country. 

Mnazi Mmoja Hospital in Zanzibar is the second hospital to receive this donation, after Temeke Hospital in Dar es Salaam last month. The event was held at the hospital grounds and was honoured by the presence of Honorable Ambassador Seif Ali Iddi, the Second Vice President of the Revolutionary Government of Zanzibar.

UFAFANUZI JUU YA TUHUMA ZA USHIRIKIANO WA TANZANIA NA KOREA KASKAZINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Korea ya Kaskazini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Korea ya Kaskazini, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Aziz Mlima na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara hiyo Bi. Mindi Kasiga.
Mwandishi wa Habari toka kituo cha Televisheni cha Channel Ten, David Ramadhan akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (aliye kaa katikati) wakati Waziri huyo akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Korea ya Kaskazini.


Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

TAPIE wafanya Mkutano Mkuu wa mwaka Dodoma.

$
0
0
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika elimu (TAPIE), wakiendelea na majadiliano kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka uliofanyika kwa siku mbili mkoani Dodoma.
 WAJUMBE waliohudhuria Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Elimu (TAPIE), wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha mkutano huo wa siku mbili uliofanyika mkoani Dodoma.Mwanamke pekee anayeonakana mbele ni Rais wa chama hicho, Ester Mahawe ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM).
  Rais wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika elimu (TAPIE),  Ester Mahawe akimkabidhi cheti mshiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho, Imelda Haule mwishoni mwa mkutano huo uliofanyika jana mkoani Dodoma. Anayefuata pichani ni Makamu wa Rais wa TAPIE, Khalfan Swali na mshauri wa shule za Tusiime Laurent Gama.
Rais wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika elimu (TAPIE),  Ester Mahawe akimkabidhi cheti mshiriki  wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho, Mkurugenzi wa shule za Tusiime, Albert Katagira, mwishoni mwa mkutano huo uliofanyika jana mkoani Dodoma. Anayefuata pichani ni Makamu wa Rais wa TAPIE, Khalfan Swali na mshauri wa shule za Tusiime Laurent Gama.

RC MAKONDA APIGA MARUFUKU WAGONJWA KULALA CHINI

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amepokea Magodoro 1,000 yenye thamani ya Shillingi Million 100 kutoka Kiwanda cha utengenezaji wa Magodoro ya Dodoma Asili kwa kushirikiana na Wadau wanaopendezwa na kazi kubwa anayoifanya katika kutatua kero Wananchi.
Makonda amekabidhiwa Magodoro hayo Mjini Dodoma na Kiwanda hicho mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana.
Akizungumza baada ya Makabidhiano hayo Makonda amepiga Marufuku kitendo cha Wagonjwa kulazwa Chini Hospitalini kwakuwa Magodoro hayo yanaenda kutatua kero hiyo.
 Amesema kuwa Magodoro aliyopatiwa atayakabidhi kwenye Hospital zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwakuwa baadhi zimekuwa na upungufu wa Magodoro hali inayofanya Wagonjwa kulala juu ya Vyuma vya kitanda na wengine kutandika Kanga na Nguo kwenye Sakafu.
 Amesema idadi kubwa ya Wananchi wamekuwa wakitoka Mikoani kufuata huduma za Afya Dar es Salaam kutokana na Wingi wa Hospital za Kisasa za Umma na Binafsi hivyo kusababisha Hospital kuwa na Wagonjwa wengi.
Licha ya Changamoto hiyo Makonda amesema Sekta ya Afya jijini Dar es Salaam imeimarika kwa kiasi kikubwa ambapo lengo lake ni kuona Mkoa huo unakuwa kinara kwenye utoaji wa huduma Bora za Afya.

Ameshukuru Kiwanda hicho na Wadau waliomuunga Mkono na kuwasihi Wananchi kununua Magodoro ya Dodoma Asili yanayotengene
zwa na Kiwanda cha Wazawa ili kukuza Uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana amempongeza RC Makonda kwa kazi kubwa anayoifanya katika Sekta mbalimbali ikiwemo Maboresho ya Jeshi la Polis na kusema ataenda Dar es salaam kujifunza namna walivyofanikiwa kwenye Ulinzi na Usalama.
Nae Mkurugenzi wa Kiwanda cha Magodoro ya Dodoma Asili Bwana Haider Gulamali amesema wataendelea kutoa ushirikiano kwa RC Makonda kwakuwa kazi anayoifanya ni kubwa na inawagusa Wananchi wote hususani wanyonge.

Makamba: Kila Mtanzania Anajukumu la Kuhifadhi Tabaka la Ozoni

$
0
0
Na: Lilian Lundo,MAELEZO-Dodoma

Serikali imesema kila Mtanzania anajukumu la kuhifadhi Tabaka la Ozoni kwa kutotumia bidhaa zenye madhara kwa Tabaka hilo katika biashara na shughuli za kila siku za majumbani.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba kupitia taarifa aliyoitoa leo, kwa vyombo vya habari juu ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni inayofanyika kila mwaka, Septemba 16.

“Kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu ni muhimu tuzingatie kwamba juhudi za kila mmoja wetu zinatakiwa ili kupunguza na kuondosha madhara katika Tabaka la Ozoni yanayosababishwa na bidhaa tunazonunua na kutumia majumbani au sehemu za biashara ,” amefafanua Makamba kupitia taarifa hiyo.
Makamba amesema kuwa kila mwananchi anatakiwa kuepuka kuingiza nchini gesi zilizopigwa marufuku na vifaa vinavyotumia gesi haribifu kama vile majokofu na viyoyozi vilivyokwisha tumika (mitumba) na ambavyo vinatumia vipoozi aina ya Chlorofluorocarbons (R11 na R12).
Vile vile amewataka Watanzania kununua bidhaa zilizowekwa nembo rasmi isemayo “Ozone friendly” ikiashiria haina wala haikutengenezwa na kemikali zinazomong’onyoa Tabata la Ozoni.
Aidha amewaasa Watanzania kuepuka kutupa hovyo majokofu ya zamani ama vifaa vya kuzima moto vyenye kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni aina ya ” CFCs” na “halon”. Ila wanapotaka kutupa wanatakiwa kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa mafundi ama mamlaka zinazohusika.
Pia mafundi wa majokofu na viyoyozi wametakiwa kuhakikisha kuwa wananasa na kutumia tena vipoozi kutoka kwenye viyoyozi na majokofu wanayohudumia badala ya kuviacha huru visambae angani.Mafundi hao wanatakiwa kutoa elimu kwa wateja wao kuhusu njia rahisi ya kutambua uvujaji wa vipoozi kutoka katika majokofu na viyoyozi wavyotumia.
Kitaifa, maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni yatafanyika kwa njia ya uelimishaji Umma kuhusu Tabaka la Ozoni, faida zake, madhara ya kuharibika kwa Tabaka hilo na matumizi salama ya bidhaa zenye kemikali rafiki kwa Tabaka hilo.

Kauli mbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha siku hiyo ni “Kutunza na Kulinda Viumbe Hai Duniani” ( Caring for All Life Under the Sun).
Viewing all 110082 articles
Browse latest View live




Latest Images