Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MAKAMPUNI YA BIASHARA YATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Bagamoyo: Makampuni ya Kimataifa na Kitaifa yanayoendesha shughuli za kibiashara hapa nchi makubwa kwa madogo yanatakiwa kuendesha shughuli zao kwa kuheshimu haki za binadamu na kuwajibika pale yanapokiuka haki hizo.

Hayo yameelezwa leo mjini Bagamoayo na Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Obadia Kameya, wakati akifungua mafunzo ya uwezeshaji kwa Maafisa wa Serikali kuhusu Biashara na Haki za Binadamu. Bw. Kameya amesema, Makampuni ambayo yatabainika kukiuka haki za binadamu katika uendeshaji wa shughuli zao, yanapashwa kuchukuliwa hatua na kwamba mwenye wajibu huo ni Serikali ambayo ndiyo inayobeba dhamana kwa mujibu wa Katiba ya kuhakikisha kwamba haki za wananchi wake ndani ya mipaka yake zinalindwa, kusimamiwa na kutetewa.

Ni kwa sababu hiyo, Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema, Maafisa wa Serikali ambao kwa namna moja ama nyingine wanahusika na masuala ya Biashara na Haki za Binadamu wanapashwa kuwa na uelewa mkubwa kuhusu Kanuni na Miongozo inayohusu Haki za Binadamu na Biashara.

Akasema , suala la Biashara na Haki za Binadamu limekuwa ajenda ya ulimwengu katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kuhusishwa kwake na haki za binadamu na ni katika muktadha huo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Mshauri wa Serikali kuhusu mauala ya Sheria, imeamua kwa Kushirikiana na Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Kanda ya Afrika (OHCHR-EARO) kuandaa mafunzo ya kuwajenga uwezo Maafisa wa Serikali.

Bw. Kameya akasisitiza zaidi kwa kueleza kwamba, ni muhimu sana kwa Maafisa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Maafisa kutoka Wizara nyingine za Serikali na Taasisi kuwa na utambuzi wa masuala ya Biashara na Haki za Binadamu ambayo yaathari kwenye sera, sheria, mikataba na makubaliano ya kimataifa na katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali na hasa katika kipindi hiki ambacho nchi imejielekeza kuwa nchi ya Viwanda.

Naye Mwakilishi wa OHCHR EARO Madame Nwanneakolam Vwede-Obahor amesisitiza kwamba ingawa Maaofisa wa Serikali wanaowajibu wa msingi kabisa wakuhakikisha kwamba wanafuatilia kwa karibu na kuhakikisha kwamba Makapuni ya Kibashara yatekeleza na kuwajibika katika kuhakikisha kwamba hayakiuki misingi na kanuni za haki za binadamu na kwamba yajifanyia tathimini na kutoa taarifa kama inavyotakiwa.

Wawezeshwaji wa Mafunzo hayo wakiongozwa na Madame Nwanneakolam Vwede-Obahor ambaye ni Mwakilishi wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Kanda ya Afrika ( OHCHR-EARO) walifundisha kuhusu Mfumo wa Umoja wa Mataifa ulioridhiwa mwaka 2008 unaojulikana kama Zuia, Heshimu na Fidia kuhusu Biashara na Haki za Binadamu.

Mfumo huu wa Umoja wa Mataifa una Misingi Mikuu Mitatu. Wa Kwanza ni kuhusu wajibu wa serikali kwa kuzingatia sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ya kumlida kila mtu ndani ya mipaka yake na katika eneo la mamlaka yake kwa kuweka sheria madhubuti , kanuni , sera ikiwa ni pamoja na kuzuia na kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na Makampuni ya Kibiashara. Msingi wa Pili wa mfumo huu unazitaka Kampuni za Biashara kuwajibika katika kuheshimu haki za binadamu mahali popote zinakoendesha shughuli zao bila ya kujali ukubwa au udogo wa biashara hiyo ikiwa ni pamoja na kutambua madhara yatokanayo na shughuli zao na kuchukua hatua za kuzuia madhara hayo.

Msingi wa Tatu ni utoaji wa fidia kutokana na athari za ukiukwaji wa haki za binadamu unaotokana na shughuli za kibiashara zinazofanywa makampuni hayo. Baadhi ya athari hizo zinatajwa kuwa ni pamoja na uchafuzi wa mazingira, ajali kazini, malipo au ujira duni, uhamishwaji wa kutumia nguvu na usiozingatia sheria.

Washiriki wa Mafunzo hayo wametoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Biashara na Viwanda, Tume ya Kurekebisha Sheria , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kituo cha Uwekezaji, Nishani na Madini, na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Washiriki wa Mafunzo ya Uwezeshaji kuhusu Biashara na Haki za Binadamu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo. mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika mjini Bagamoyo na yameandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika (OHCHR EARO). Mafunzo hayo yalifunguliwa na Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Obadia Kameya aliyeketi katikati kushoto kwake ni Madame Nwanneakolam Vwede-Obahor na kulia ni Bi. Cecilia S. Shelly- Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Pwani.

JUMIA waja na mfumo wa malipo ya kulipa baada ya kupokea bidhaa

$
0
0

 Maneja Masoko wa Jumia Tanzania, Albany James akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi Kampuni ya Jumia Tanzania inavyoweza kurudisha imani kwa watanzania namna ya kununua bidhaa mtandaoni kwa kutumia mfumo wa malipo baada ya mteja kupokea bidhaa yake kwenye ofisi zao Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mkuu wa Biashara wa Jumia Tanzania, Mikolaj Kucia akizungumza na waandishi wa habari namna ya malipo yanavyofanyika hasa pale tu mtu anapopokea bidhaa wanzaouza mtandaoni pamoja na namna wanavyofikisha bidhaa kwa wateja wao kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi zao Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo.
Kampuni inayojihusisha na huduma za manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa njia ya mtandao nchini, Jumia Tanzania imewaondolea hofu wateja wake kwamba sasa wanaweza kulipia bidhaa pale zinapowafikia baada ya kufanya manunuzi kupitia tovuti yao.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Bw. Albany James amebainisha kwamba wameona ni vema kuutambulisha mfumo huo mpya kwa wateja wao ili kuwaondolea hofu na kuwajengea uaminifu kwa huduma zote za manunuzi wanazozifanya kwa njia ya mtandao.
Jumia Tanzania inayo furaha kuwajulisha wateja wao wote kwamba hivi sasa wanaweza kulipia bidhaa wanazozinunua kwa njia ya mtandao pindi zinapowafikia. Tumeona ni vema kuwapa wateja wetu chaguo hilo kwa kuzingatia mila na tamaduni tulizonazo watanzania kwamba tumezoea kununua bidhaa baada ya kujiridhisha kwa kuiona kwa macho. Mbali na hapo bado teknolojia ya huduma na manunuzi kwa njia ya mtandao ni ngeni miongoni mwa watanzania wengi hivyo wanakuwa na hofu kwamba wanaweza kuwa wanatapeliwa,” alisema Bw. James.
“Faida nyingine mbali na mteja kuiona bidhaa aliyoiagiza na kujiridhisha ndiyo alipie pia mteja atapata fursa ya kuweza kubadilisha kama hatoridhika. Tumekuwa tukipokea changamoto kwa baadhi ya wateja wetu kwamba wamekuwa wakipelekewa bidhaa ambazo zimekuwa tofauti kidogo na walivyoagiza. Ingawa tunawasisitiza sana kuwa makini na kuzingatia taarifa muhimu za bidhaa wananozitaka lakini katika kuwathibitishia kwamba Jumia Market sio wababaishaji tumeamua kuwajulisha kwamba wana chaguo la aidha kulipia kwa njia ya mtandao au pale bidhaa inapomfikia,” aliongezea Meneja Masoko huyo wa Jumia Tanzania.
Aliendelea mbele kwa kuongeza zaidi kwamba tofauti ya Jumia Tanzania na kampuni zingine zinazojihusisha na huduma za mauzo ya bidhaa kwa njia ya mtandao ni kwamba wao pekee ndio wanawapa wateja wao chaguo la kulipia bidhaa pale zinapowafikia. Na pale mteja asiporidhika na bidhaa aliyopelekewa anao uwezo wa kuomba kubadilishiwa na kuletewa bila ya kudaiwa malipo yoyote.
“Ningependa kutoa wito kwa watanzania kuchangamkia ofa mbalimbali za manunuzi ya bidhaa kwenye tovuti yetu na mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter na Instagram. Lakini pia kwa wafanyabiashara wa kitanzania kuhamia kwenye njia za mitandao ili kupanua wigo wa wateja wao. Kuna faida nyingi za kujiunga nasi zikiwemo kujiongezea wateja wengi tofauti na wale wanaotembelea maduka yao moja kwa moja lakini pia kutangazwa bure kabisa bila ya malipo yoyote kwenye mtandao wetu,” alihitimisha Bw. James.
Jumia Tanzania ina amini kuwa tekinolojia inavyokua kwa kasi inatubidi kwenda nayo sambamba hasa kwenye manunuzi ya bidhaa tajwa hapo juu ili kuepuka usumbufu wa kuzunguka duka hadi duka pamoja na kuokoa muda kwasababu bidhaa zote zinazoagizwa hupelekwa hadi pale mteja alipo.

BANK OF AFRICA – TANZANIA yazindua program mpya ya kibenki ya “SWAHIBA MOBILE APP”

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa BANK OF AFRICA – TANZANIA, Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah akizindua rasmi program ya SWAHIBA Mobile App. Kulia kwake ni mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa benki hiyo Ms. Mercy Msuya na Meneja Masoko, utafiti na maendeleo wa benki hiyo ndg. Muganyizi Bisheko.

 BANK OF AFRICA – TANZANIA imezindua programu yake mpya ya kibenki inayoitwa "SWAHIBA Mobile" kwenye soko la Tanzania. Huduma hii inakuja kama muendelezo wa programu ya B- Mobile, inayoruhusu watumiaji kufurahia huduma kamili za kibenki kupitia aina yoyote ya simu za mkononi, wakati wowote.

SWAHIBA Mobile App inawapa wateja urahisi wa kutumia huduma za kibenki katika simu kwani inakuja na muonekano mzuri Zaidi na sifa nyingi mpya zinanzowarahisishia wateja kufuatilia akaunti zao za binafsi na za kibiashara kwa wakati mmoja.

Huduma zipatikanazo kwenye programu hii ni: huduma za kuhamisha fedha, huduma za hundi, maombi ya mkopo wa papo hapo, malipo ya bili mbalimbali, huduma za utoaji fedha kwenye ATM bila kadi, kuongeza muda wa maongezi, usajili binafsi wa mobile banking na huduma za e-chama pamoja na nyingine nyingi.

  Emmanuel Mshindo, Mkuu wakitengo cha Huduma mbadala za kibenki akitoa maelezo juu ya huduma mbalimbali zipatikanazo katika program ya SWAHIBA Mobile, wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo mapema hii leo. 
Zaidi ya hayo, SWAHIBA Mobile APP inaweza kutumiwa na Mtanzania yoyote hata ambae si mteja wa BANK OF AFRICA. Hii ni kupitia huduma mbalimbali zinazopatikana kabla ya kuingia kwenye program yaani “without Log in services”. huduma hizi ni kama vile maelezo kuhusu Huduma mbalimbali zitolewazo na BANK OF AFRICA, Maombi ya Mikopo, maelekezo kuhusu yalipo Matawi ya BANK OF AFRICA na ATMs, pamoja na viwango vya ubadilishaji fedha za kigeni.

Mr. Ammishaddai Owusu-Amoah, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa BANK OF AFRICA - TANZANIA alisema Benki yake inajivunia kuanzisha programu hii mpya ya benki kiganjani katika wakati huu muhimu ambapo benki hiyo inaadhimisha miaka 10 ya biashara katika nchi ya Tanzania. "Uzinduzi wa SWAHIBA Mobile App ni namna ya kipekee ya kuwasilisha shukrani zetu kwa wateja, jamii, washirika, wamiliki na wadau wote, walio tupa ushirikiano wa kutosha katika kipindi cha miaka 10 ya kazi nchini ".

Naibu Mkurugenzi wa BANK OF AFRICA Bw. Wasia Mushi, akiongea na wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa program ya SWAHIBA Mobile mapema hii leo. 
"Huduma hii pia inakuja kutia msistizo wa ahadi yetu ya kuweka mapendekezo ya wateja wetu kwanza na kuwaongezea uzoefu wa kidigitli Zaidi katika ukuwaji wa sayansi na technologia. Mkurugenzi aliendelea kueleza “Pia inathibitisha uamuzi wa benki wa kujenga uwepo wake wa kidigitali na kukidhi mahitaji ya haraka ya wateja wetu "

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

PPRA NA NEEC ZAINGIIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA MIAKA MITANO.

$
0
0
MAMLAKA ya  Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na  Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), wametiliana saini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano.

Mkataba huo uliosainiwa leo Dar es Salaam, utawezesha PPRA na NEEC kushirikiana   kiutendaji  ili kuwawezesha  wajasiriamali wadogo  na wa kati   kushiriki   kwenye fursa   mbalimbali  zinazopatikana katika manunuzi ya umma.

Akizungumza wakati wa hafla ya utilianaji saini  mkataba huo,  Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk.  Laurent  Shirima, lengo linguine ni mamlaka  kuhakikisha  kigezo mojawapo  wakati wa  hatua ya tathimini kwenye zabuni za umma  cha  upendeleo kwa ajasiriamali  wadogo na kati kinazigatiwa.

“Pia  kila mwaka PPRA na NEEC kufanya tathimini ya pamoja ili  kujua namna taasisi nunuzi  zinavyotekeleza au kuzingatia ushiriki wa wajasiriamali wadogo na wakati,”alisema Dk. Shirima.

Malengo mengine ni PPRA na NEEC kufanya tafiti za pamoja  zitakazo jikita  zaidi  katika uwezeshaji  na ushiriki wa wajasiriamali  wadogo na kati  kwenye michakato ya  manunuzi  ya umma.

“Suala la kuwajengea wananchi uwezo  wa kupambana na umasikini kwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi limekuwa  kipaumbele kikubwa  cha serikali na hasa ya awamu ya tano.

Ili kufanikisha azma hiyo , serikali imekuwa ikiandaa sera  na sheria  mbalimbali  zinazoweka mazingira  mazuri  ya wananchi  kushiriki na kuitumia fursa za kibiashara,”lifafanua Dk. Shirima.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk.  Laurent  Shirima,akizugumza wakati  wa hafla ya utilianaji saini wa mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)  leo jijini Dar es Salaam.(kushoto)ni Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’I  Issa.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk.  Laurent  Shirima(kulia)pamoja na Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa wakisaini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano wanaoshuhudia  (kulia) ni  Mwanasheria Mwandamizi wa PPRA, Agnes Sayi  na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji, Esther Mmbaga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk.  Laurent  Shirima, pamoja na wakibadilisha hati za mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

MWENYEKITI WA BODI YA TPC AKUTANA NA MENEJIMENTI NA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI, DAR ES SALAAM

$
0
0
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa, akizungumza katika mkutano huo na kisha kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Harun Kondo (katikati), kuzungumza na Menejimenti na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa shirika hilo, jijini Dar es Salaam leo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Harun Kondo, akifafanua jambo wakati wa akizungumza na Menejimenti na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa TPC, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Harun Kondo (wa pili kulia), kuzungumza na Menejimenti na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wa TPC, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa na kulia ni Kaimu Katibu wa Shirika, Zuhuru Pinde. 
Baadhi ya viongozi wa Vyama vya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Harun Kondo, wakati akizungumza nao pamoja na Menejimenti ya TPC, jijini Dar es Salaam leo. 

Uhamiaji yapata msaada wa vitendea kazi toka Shirika la IOM

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala akipokea msaada wa vifaa mbalimbali uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM. Anayekabidhi vifaa hivyo ni, Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania Dkt. Qassim Sufi. Vifaa hivyo vina jumuisha Kompyuta, mashine za kutolea nakala na kuchapishia vyenye thamani ya Dola za Kimarekani elfu arobaini. Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na wana habari nimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala kwa pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini Tanzania, Dkt. Qassim Sufi wakisaini nyaraka za makabidhiano ya msaada wa vifaa mbalimbali uliotolewa na Shirika hilo, katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Dar es Salaam leo.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala akibadilishana nyaraka za makabidhiano ya msaada wa vifaa mbalimbali uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) na Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania, Dkt. Qassim Sufi, katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Dar es Salaam leo. Vifaa hivyo vina jumuisha Kompyuta, mashine za kutolea nakala na kuchapishia vyenye thamani ya Dola za Kimarekani elfu arobaini. 
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA AWAMU YA PILI YA MRADI WA KUUJENGEA UWEZO MHIMILI WA BUNGE, MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akitoa maelezo kabla ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzindua awamu ya pili ya mradi wa kuujengea uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua awamu ya pili ya mradi wa kuujengea uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017.Kushoto ni Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akizindua awamu ya pili ya Mradi wa kuujengea uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017. Kulia ni Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika Awamu ya Pili ya Mradi wa Kuujengea Uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Paul Sherlock (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. David Omozuafoh (kulia) baada ya kuzindua awamu ya pili ya mradi wa kuujengea uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

UJERUMANI YASHIKA NAMBA MOJA VIWANGO VYA SOKA DUNIANI, TANZANIA YASHUKA KWA NAFASI TANO

$
0
0
Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA limetoa viwango vipya vya soka duniani ambapo sasa Ujerumani wamerudi tena kuchukua nafasi yao ya kwanza ambayo hapo mwanzo ilienda kwa timu ya Brazil.

Brazil waliokuwa wakishika nafasi ya kwanza sasa wamekuwa nafasi ya pili huku Ureno waliokuwa nafasi ya sita sasa wako nafasi ya 3 na Argentina waliokuwa nafasi ya 3 wameshuka hadi 4.

Ubelgiji wamepanda hadi nafasi ya 5 kutoka 9 walipokuwa huku nafasi ya 6 ikienda kwa Poland, timu ya taifa ya Swiztrland wako katika nafasi ya 7 huku ya 8 ikikamatwa na Ufaransa.

Mabingwa wa Amerika Kusini timu ya taifa ya Chile wako nafasi ya 9 huku wanaofunga orodha ya 10 bora ni timu ya taifa kutoka bara la America timu ya Colombia.

Timu ya taifa ya Uingereza ambayo imeshuka hadi nafasi ya 15 ikiwa ni baada ya miaka 17 kufika katika hatua hiyo na wakipitwa na  Wales walioko 13.

Kwa upande wa kumi bora ya Africa, Misri wanaongoza wakifuatiwa na Tunisia huku Wasenegal wakiwa katika nafasi ya 3, ya 4 ikienda kwa DRC.

Nigeria wako nafasi ya 5, wakifuatiwa na mabingwa wa Africa timu ya taifa ya Cameroon huku Burkina Fasso wakishika namba 7, 8 ni Ghana, 9 Ivory Coast na 10 ni Morocco.Tanzania wameshuka kutoka nafasi 5 toka  120 hadi 125.

SERIKALI YAANZA JITIHADA ZA KUWAKABILI VIWAVIJESHI HATARI AINA YA FALL ARMYWORM (FAW)

$
0
0
Kiwavijeshi aina ya Fall Armyworm (FAW).

Na Mathias Canal, Dar es salaam 

Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi imeanza jitihada za kuwakabili Viwavijeshi wapya aina ya Fall Armyworm (FAW) wanaojulikana kitaalamu kama Spodoptera Frugiperda ambao wametajwa kuwa na uwezo mkubwa kuharibu mazao mbalimbali hususan mahindi ambayo ndio zao kuu la chakula nchini.

Imeelezwa kuwa Viwavijeshi hao wanapofika kwenye mazao hutoa kemikali ambayo huweza kudanganya mmea kuwa unashambuliwa na magonjwa kama ukungu au fangasi hivyo mmea unapohisi unashambuliwa na hayo magonjwa, hupunguza kinga dhidi ya wadudu hao hatari na kuwa rahisi kushambuliwa. 

Hayo yamebainishwa leo Septemba 14, 2017 na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bwana Beatus Malema wakati akifungua warsha ya siku moja mbele ya Wadau wa Kilimo ambao ni Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani USAD, ONE HACKER FUND, Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Ukanda wa Kitropiki (TPRI), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), na Mradi wa WEMA .
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bwana Beatus Malema akizungumza wakati akifungua warsha ya siku moja kujadili namna ya kukabiliana na mdudu aina ya Kiwavijeshi.

Mkutano ulikuwa na lengo la kujenga uelewa wa pamoja kwa ajili ya kumkabili mdudu huyo aina ya Fall Armyworm (FAW) ambaye anashambulia mazao mbalimbali nchini hususani zao la mahindi.

Alisema Athari ya viwavi jeshi haishii kuharibu majani ya mimea pekee, wadudu hao wanapokula majani na kutengeneza sumu aina ya ‘firenide’ inayodhuru mifugo inapokula majani yaliyoathiriwa.

Bwana Malema amesema tayari Serikali imechukua juhudi za awali kukabiliana na mdudu huyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya utambuzi wa mdudu huyo kwa kuwataka Wananchi kung’oa mazao na kuyachoma pindi wanapobaini uwepo wa mdudu huyo.

Pia tayari dawa tatu zimepitishwa na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kupitia Taasisi ya uchunguzi wa Viatilifu (TPRI) zinazoangamiza wadudu hao ambazo ni Duduba 450, Mupacrone 500 EC na Match Save kutoka Kampuni ya Syngenta hivyo Wananchi wametakiwa kuzitumia haraka pindi wanapoona dalili za kuwepo wa wadudu hao shambani.
Wadau wa kilimo kutoka Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, USAD, ONE HACKER FUND, Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Ukanda wa Kitropiki (TPRI), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), na Mradi wa WEMA wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bwana Beatus Malema akizungumza wakati akifungua warsha ya siku moja kujadili namna ya kukabiliana na mdudu aina ya Kiwavijeshi.


Bwana Malema amesema kuwa katika kipindi cha miaka mingi Tanzania imekuwa ikikumbwa na viwavijeshi aina ya African Armywarms ambapo mara zote imekuwa ikiwadhibiti wadudu hao wanapojitokeza kwa kuwapa kiuatilifu kinachosababaisha matumbo ya wadudu hao kujaa na hatimaye kuwasababishia vifo.

Kipanya ameamua kuishi maisha bila mawasiliano ya wasiwasi

$
0
0
Punguza ghasia zisizo na msingi linapokuja suala la mawasiliano, jiunge na #VodacomREDRLX  ufurahie mawasiliano bila wasi. Piga *149*01# na chagua RED

Jhpiego launches Project to scale up family planning solution in urban cities

$
0
0
By staff writer,
Jhpiego, in collaboration with the governments of Tanzania through the Ministry of Health, community development, Gender, elderly and Children, today has launched a bold initiative project called The Challenge Initiative- Tupange Pamoja Project to address the reproductive health needs of the urban poor population that will be implemented in Dar es Salaam, Arusha, Morogoro, Mwanza and Dodoma Regions to scale up family planning solutions.
Giving the overview of the project, the Jhpiego Country Director Jeremie Zoungrana  says the Initiative is built around the premise that will be putting municipalities in urban in the driver’s seat through an innovative, demand- driven approach by ensuring that they bring their own resources (cash or in-kind) to the table and the most promising proposals to have access to the Challenge Fund, which is seeded by the Bill & Melinda Gates Foundation.
“We are happy that Tanzania has been identified to be part of the TCI to scale up Family Planning in order to reach additional women and girls with voluntary Family Planning services over the next three to five years through the Tupange Pamoja Project. We sincerely thanks the Government of Tanzania for their strong commitment and leadership already observed at the decentralized level” says Jeremie.
 Jhpiego Tanzania Country Director Jeremie Zoungrana, giving his welcoming note during the National Launch of The Challenge Initiative (TCI) – Tupange Pamoja Project in Dar es Salaam today. The project is been implemented urban areas of Kenya, Tanzania and Uganda to scale up family planning solutions and in Tanzania it being implemented by Jhpiego in collaboration with the Ministry of Health, community development, Gender, elderly and Children.
 The Challenge Initiative (TCI) Project Director for East Africa, Nelson Keyonzo presenting his paper titled “Scaling up Family Planning in East Africa” during the National Launch of The Challenge Initaitive (TCI) – Tupange Pamoja Project in Dar es Salaam
 Zuhura Mkwizu from the Ministry of Health, community development, Gender, elderly and Children sharing the family planning status and progress in Tanzania during the National Launch of The Challenge Initiative (TCI) – Tupange Pamoja Project in Dar es Salaam
 The Dar es Salaam Regional Medical Officer Dr. Grace Maghembe elaborating the situation of the Family Planning in five municipal council in Dar es Salaam and their commitment toward the implementation of the Challenge Initiative (TCI) – Tupange Pamoja Project in the city during the National Launch of Project in Dar es Salaam.
 The Guest of Honor Dr. Janeth Mghamba, Acting Director of Preventive Services, Representing, Hon. Ummy Mwalimu, The Minister of Health Community Development Gender Elderly and Children and Jhpiego Tanzania Country Director Jeremie Zoungrana hold together  the TCI  package to mark the Official Launch of the Project in Tanzania.

MIKOA YA LINDI NA MTWARA YAPOKEA KWA KISHINDO MPANGO WA KUWAPATIA VYETI VYA KUZALIWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe Halima Dendego akizungumza na viongozi wote wa Mikoa ya Lindi na Mtwara juu ya kusimamia kikamilifu Mpango wa Kitaifa wa usajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano, uliofanyika mkoani humo leo.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe Halima Dendego amewaagiza viongozi wote wa Mkoa huo kujipanga na kusimamia kikamilifu Mpango wa Kitaifa wa usajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano kwa kufikia lengo la asilimia mia moja ndani ya kipindi kifupi cha  miezi mitatu.

Mhe Dendego ameyasema hayo hii leo Mkoani Mtwara alipokuwa akifungua mafunzo maalum yaliyoandaliwa na RITA kwa viongozi wa Mkoa  kuhusu utekelezaji wa mpango huo na kuwaagiza viongozi wote kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa mpango huo kwa Taifa kwani utawezesha upatikanaji wa takwimu sahihi zitakazosaidia katika mipango ya maendeleo na kufahamu  makundi mbalimbali katika utoaji wa huduma za elimu,afya pamoja na ajira.

Ameongeza kuwa,  Takwimu za Vizazi ni kichocheo cha maendeleo nchini kwani Serikali huhitaji takwimu hizi kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo ya muda mfupi na muda mrefu na  kwamba mipango mingi ya serikali huanzia katika ngazi ya Halmashauri hivyo  bila ya takwimu  itakuwa  vigumu kwa halmashauri  kuweza kujua kwa usahihi mahitaji ya kupeleka huduma muhimu kwenye jamii. 

“Kwa mfano ni muhimu kujua katika miaka mitano ijayo kutakuwa na wanafunzi wangapi wanaohitaji kuanza elimu ya msingi”. Amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe Shaibu Ndemanga kwa niaba ya Mkuu  wa Mkoa wa huo Mhe Godfrey Zambi, amesema mpango huo umeleta suluhisho la kudumu kwa Wananchi wanaoishi Vijijini ambao wamekuwa wakitumia gharama kubwa kufika makao Makuu ya Wilaya ili wapatiwe huduma hiyo.

Mhe Ndemanga ameongeza kuwa Mkoa wa Lindi umepokea kwa furaha na kuwahidi kutoa elimu zaidi kwa wananchi wake ili kuchangamkia fursa hiyo hasa ukizingatia umuhimu wa cheti cha kuzaliwa hasa kwa kipindi hiki ambapo ili Mwananchi aweze kupata huduma mbalimbali ni lazima atahitajika kuwasilisha nyaraka hiyo.

“tumeona wenzetu wa bima ya afya lazima uwe na cheti cha kuzaliwa cha mtoto na kwa sasa ili mtoto apate elimu itamlazimu awe na cheti cha kuzaliwa.

Naye Kaimu  Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson amesema kuwa Katika Mpango huo watoto watasajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa hapo hapo bila malipo (bure) katika vitu vya Tiba vinavyotoa huduma ya mama na Mtoto pamoja na Ofisi za watendaji kata tofauti na utaratibu uliozoeleka hapo awali ambapo iliwabidi kwenda katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya. 

Bi Hudson ameongeza  kwamba serikali imesogeza huduma za usajili karibu na maeneo ya makazi ya wananchi hivyo kuwaondolea wananchi changamoto ya kusafiri umbali mrefu na kutumia gharama nyingi kuweza kupata huduma hii. 

Tayari Mpango huu umeanza kutekelezwa katika Mikoa saba ya Mwanza, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Geita na Shinyanga na kote umeonesha mafanikio chanya na kwa  hivi  sasa maandalizi yanaendelea kufanyikakwa ajili ya  kuanza utekelezaji  katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.
 Kaimu  Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson akizungumza katika Mkutano na viongozi wote wa Mkoa mikoa ya Lindi na Mtwara juu ya kusimamia kikamilifu Mpango wa Kitaifa wa usajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano, uliofanyika mkoani humo leo.
 Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe Shaibu Ndemanga kwa niaba ya Mkuu  wa Mkoa wa huo Mhe Godfrey Zambi, akizungumza na viongozi wote wa Mikoa ya Lindi na Mtwara juu ya kusimamia kikamilifu Mpango wa Kitaifa wa usajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano, uliofanyika mkoani humo leo.
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe Halima Dendego akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya RITA.

Marehemu Mama Philberta Mapunda apumzishwa kwenye nyumba yake ya milele

$
0
0
Marehemu Mama Philberta Mapunda, mke wa aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali (Tanzania Standard Newspapers – TSN), Mzee Joseph Mapunda, amezikwa leo jioni Septemba 14, 2017 katika makaburi ya Luguluni, Kwembe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam,

Marehemu Mama Mapunda, aliyefariki dunia usiku wa Septemba 11, 2017 jijini Dar es salaam, alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo na shinikizo la damu. Alikuwa na umri wa miaka 62.

Mume wa Marehemu, Mzee Mapunda, pia ni mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Uongozi wa Michuzi Media Group na wafanyakazi wote wanatoa pole kwa familia ya Mzee Mapunda na kuwatakia uvumilivu katika wakati huu mgumu.

Mola na aiweke roho ya marehemu mahala pema Peponi – Amina.
Marehemu Mama Philberta Mapunda, mke wa aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali (Tanzania Standard Newspapers – TSN), Mzee Joseph Mapunda, ukiwasili nyumbani  kabla ya kwenda mazishini

Ibada  ya mazishi ya Marehemu Mama Philberta Mapunda

Aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali (Tanzania Standard Newspapers – TSN), Mzee Joseph Mapunda, akiweka shada la maua juu ya kaburi la mkewe Mama Philberta Mapunda wakati wa mazishi katika makaburi ya Luguluni, Kwembe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam,

TBC safari - TALII KISIWANI PEMBA NA FATMA MATULANGA

Wekeni Mazingira Rafiki katika Uwekezaji wa Madini- Waziri Mkuu

$
0
0
Jonas Kamaleki- MAELEZO

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amezitaka nchi wanachama wa Kituo cha Madini na Kijiosayansi cha Afrika (AMGC) kuweka mazingira rafiki kuvutia uwekezaji katika sekta ya madini, kuandaa raslimali watu na vitenda kazi ili kuifanya sekta kutoa tija.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa 37 wa Baraza la Uongozi wa Kituo cha Madini na Kijiosayansi cha Afrika.
Majaliwa amesema kuwa raslimali madini inaweza kuwa chanzo cha kusukuma maendelo ya uchumi katika nchi nyingi Barani Afrika kama ikisimamiwa vema.

“Changamoto kuu kwa sasa ni jinsi gani tunaweza kuwa na sekta ya madini inayotoa mchango stahiki katika nchi husika na Bara la Afrika kwa ujumla,” amesema Majaliwa.Aliongeza kuwa taarifa za kijiolojia zinaonyesha kuwa Afrika ni Bara lenye utajiri mkubwa wa raslimali madini na mengi kati yao bado hayajaanza au yako kwenye hatua mbalimbali za uendelezaji.

Aidha, Waziri Mkuu amesema lengo la uanzishwaji wa kituo hiki ni kuhakikisha sekta ya madini inawajibika kuleta maendeleo ya kijamii na uchumi pia ikijali masuala ya mazingira.Amezitaja kazi za AMGC kuwa ni kutafi,kufundisha wataalaam pia kusimamia maabara ya kisasa kwa ajili ya uhakiki na uongezaji thamani wa madini, hivyo amehimiza watanzania na nchi nyingine wanachama kukitumia kituo hicho.

Waziri Mkuu amesema kuwa kituo hiki kikitumika vema kinaweza kutoa tija kubwa kwenye sekta ya uchimbaji wa madini,uongezaji wa thamani na usimamizi wa sekta ambapo pia masuala ya usimamizi wa mazingira utazingatiwa.

“Tanzania licha ya kuwa na utajiri wa madini ya Dhahabu, Almasi,Shaba,Chuma, Madini ya vito kama Tanzanite na mengineyo, mchango wa sekta ya madini ni asilimia 4.8 ya pato ghafi la Taifa,” alisema Majaliwa na kuongeza kuwa kuna haja ya kuongeza usimamizi wa sekta hiyo ili kutoa tija kusudiwa kwa nchi ya Tanzania.

Waziri Mkuu pia amezitaka nchi wanachama kulipa ada zao kwa AMGC kwa wakati ili kuondoa changamoto ya raslimali fedha katika kituo hicho.Ameyasema hayo baada ya kupata taarifa kuwa zipo nchi nyingi ambazo hazilipi ada zao kwa wakati na nyingine kulimbikiza madeni.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa AMGC ni kituo muhimu kwa maendeleo ya Tanzania hususan katika sekta ya Madini.Ameongeza kuwa kituo hicho kitakuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania kwani kitaweka mitambo ya kuchenjua madini jambo ambalo linaunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli za kuzuia makinikia kusafirishwa nje.

Mtambo huo utaongeza ajira nchini kwa kuwa kituo hicho kipo Tanzania. Na amezisihi nchi nyingine za kiafrika kujiunga na AMGC na kuongeza kuwa nchi 36 za Afrika zimeonyesha nia ya kujiuinga.Mkutano huu umeenda sanjari na maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa AMGC mwaka 1977 ambapo Mhe Waziri Mkuu amekata keki kuashiria sherehe hizo.

Tanzania ndio Mwenyekiti wa Mkutano huu na wajumbe wameonyesha nia ya kuiomba Tanzania iwe Mwenyekiti kwa mwaka mwingine kutokana na msimamo imara wa Serikali ya Awamu ya Tano katika kusimamia raslimali za madini.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa nchi za Kituo cha Madini na Kijiosayansi cha Afrika (AMGC) leo tarehe 14/09/2017 baada ya kufungua Mkutano wa 37 wa Baraza la Uongozi wa kituo hicho.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata keki ikiwa ni ishara ya Maadhimisho ya miaka 40 ya Kituo cha AMGC tangu kuanzishwa kwake. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu kituo cha AMGC, Ibrahim Shaddad , kushoto ni Mwenyekiti wa AUC, Frank Mugenyi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea kwenye maabara mbalimbali katika kituo cha AMGC. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu kituo cha AMGC, Ibrahim Shaddad na kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani. Wengine ni washiriki wa mkutano huo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo cha AMGC.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam Mshauri wa kituo cha AMGC, Timo Gawronski kuhusu namna Maabara ya Kisasa ya Upimaji Madini ambayo inaonesha asili ya madini ya mahali yaliyochimbwa.

SPIKA JOB NDUGAI ATEMBELEWA NA BALOZI WA IRELAND NCHINI

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akizungumza na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock (katikati) na Mshauri Mwandamizi wa Serikali hiyo, Ndg. Aran Corrington,  pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akimsikiliza Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock (katikati) na kulia ni Mshauri mwandamizi wa serikali hiyo, Ndg. Aran Corrington,  pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. 

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akiagana na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock (kulia) pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (kulia)akiagana na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock (kushoto) pale ugeni kutoka ubalozi wa Ireland ulipotembelea Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma, ukioongozwa na Balozi huyo.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

WATU WA WILI WAMEUAWA NA POLISI MKOANI RUVUMA KATIKA MAJIBIZANO YA KURUSHIANA RISASI KATI YA POLISI NA WATU HAO.

$
0
0
Jeshi la polisi Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma limewaua watu wawili waisiojulikana kwa majina katika majibizano ya kurushiana risasi kati ya polisi na watu hao,Tukio hilo limetokea katika kijiji cha NANGURUKURU kata ya NANDEMBO tarafa ya NAMPUNGU .

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATIBABU YA MHE. LISSU

MKURUGENZI WA MAENDELEO YA JAMII NCHINI AUNGANA NA WANANCHI WA KATA YA MONDO KATIKA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

$
0
0
Attachments area Preview YouTube video MKURUGENZI WA MAENDELEO YA JAMII NCHINI ASHIRIKI KATIKA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA MONDO.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images