Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1908 | 1909 | (Page 1910) | 1911 | 1912 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Kupata magazeti yote BOFYA HAPA

  0 0  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewapongeza Wajasiriamali wa Tanzania kwa ushiriki wao katika Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki maarufu kama JAMAFEST.

  Dkt. Mwakyembe ametoa pongezi hizo leo mjini Kampala nchini Uganda katika viwanja vya Mashujaa Kololo alipotembelea kujionea namna tamasha hilo lilivyopokelewa na wadau wake walioiwakilisha Tanzania wakiwemo wajasiriamali toka vikundi mbalimbali, vikundi vya ngoma, vikundi vya sanaa ya maigizo pamoja na baadhi ya wasanii.

  Katika tamasha hilo, Dkt. Mwakyembe pia alipata fursa ya kutembelea baadhi ya mabanda ya wajasiriamali hao pamoja na kuongea nao huku akijionea bidhaa mbalimbali zinazouzwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jambo ambalo limemfurahisha sana hususani kwa upande wa watu kutoka Tanzania kwakuwa wamejaza mabanda yao kwa bidhaa kadha wa kadha.

  “Tamasha hili linaonyesha utajiri mkubwa wa sanaa, utamaduni pamoja na bidhaa tulizonazo kama nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na hapa tumekutana kwasababu tunabadilishana mawazo na kuonyeshana bidhaa mbalimbali za nchi zetu”, alisema Dkt. Mwakyembe.

  Aidha, katika ziara hiyo, Dkt. Mwakyembe amewatoa wasiwasi wajasiriamali hao kuhusu suala la upatikanaji wa masoko huku akiwaahidi kuwatafutia fursa ya kuwapeleka wajasiriamali hao pamoja na bidhaa zao Bungeni mjini Dodoma ili ziweze kupata soko kwa urahisi kupitia wabunge.

  “Niwatoe wasiwasi wajasiriamali wote wa Tanzania mliohudhuria hapa, nitahakikisha kuwa pindi tunaporudi nyumbani nitatafuta wasaa wa kulishawishi Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili nyie mpate nafasi ya kuleta bidhaa zenu katika viwanja vya Bunge ili basi Wabunge wapate kujua haswa vitu vizuri mlivyonavyo nah ii itawasaidia kuviuza kwa urahisi zaidi na kujipatia vipato vyenu”, aliongeza Dkt. Mwakyembe.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia ngoma ya kiutamaduni iliyokuwa ikipigwa na Kikundi cha Sanaa na Utamaduni Tanzania (TaSUBA) katika banda lao wakati wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika mjini Kampala, Uganda 13 Septemba, 2017.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimsikiliza mjasiriamali wa Tanzania kuhusu baadhi ya bidhaa zilizopo katika banda lao wakati wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika mjini Kampala, Uganda 13 Septemba, 2017.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea zawadi ya shati toka kwa mjasiriamali wa Tanzania mara alipotembelea banda lao wakati wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika mjini Kampala, Uganda 13 Septemba, 2017.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Utamaduni, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu) akiangalia moja ya ubunifu wa picha iliyochongwa na mjasiriamali wa Tanzania wakati wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika mjini Kampala, Uganda 13 Septemba, 2017.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Mahenge amewataka viongozi hao kuongeza ulinzi katika maeneo hayo, kwa kuwashirikisha viongozi wa mitaa waozungukwa na vyanzo hivyo.  

  0 0

  Wamiliki wote wa migodi inayofanya shughuli za uchimbaji wa madini Mkoani Singida wameagizwa kuhakikisha kuwa hakuna vifo wa majeruhi katika maeneo yao kutokana na uwepo wa miundombinu mibovu au uzembe wowote.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa agizo hilo alipotembelea mgodi wa madini katika Kijiji cha Konkilangi, Kata ya Ntwike, Tarafa ya Shelui, Wilaya ya Iramba kuona shughuli za uokoaji mara baada ya mgodi huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa kufariki.

  Dkt Nchimbi amesema wamiliki wa migodi wanatakiwa kuwekeza katika kuboreha miundombinu ya migodi ili wachimbaji waweze kufanya kazi katika mazingira ambayo si hatarishi.“Madini yanatakiwa kuleta neema na kukuza uchumi wa taifa letu na sio kuangamiza nguvu kazi na kuleta majonzi, serikali haiwezi kukubali kupoteza vijana kutokana na uzembe wa baadhi ya watu”, amesema.

  Ameongeza kwa kumtaka Kamishna Msaidizi wa madini kanda ya kati Sostenes Masolla kuweka ratiba ya kutoa mafunzo kila wiki huku akitakiwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili wachimbaji wapewe semina na mafunzo ya juu ya usalama wao wawapo migodini.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na wachimbaji alipotembelea mgodi wa madini katika Kijiji cha Konkilangi, Wilayani Iramba kuona shughuli za uokoaji mara baada ya mgodi huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa kufariki. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula.
  Wachimbaji wakiendelea na shughuli za uokoaji katika Kijiji cha Konkilangi, Wilayani Iramba mara baada ya mgodi huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa kufariki.
  Wachimbaji wakiwa wanatazama shughuli za uokoaji zikiendelea katika Kijiji cha Konkilangi, Wilayani Iramba mara baada ya mgodi huo kutitia huku watu wawili wakihofiwa kufariki.


  0 0


  0 0


  Na Bashir Yakub. 

  Tumegusa uchumi wa bepari. Mara zote, na kote duniani bepari alipoguswa kwenye uchumi wake basi ametumia mbinu hizi hapa chini kuhakikisha anapambana na waliomzuia.

  [a] Kumwita kiongozi anayeongoza vita ya uchumi Mvunjaji wa haki za binadamu na asiyefaa. Imetokea kwa Gaddafi baada ya kumnyima bepari mafuta, halikadhalika kwa Saddam Hussein.Pia ndilo tatizo la Mugabe na bepari baada ya kurudisha mashamba kwa wazawa ili wafaidi uchumi wao.

  [b] Kuratibu na kufanikisha matukio ya ajabu kwenye jamii ili kuleta faraka,taharuki, chuki, uadui, na sintofahamu.Bepari analiweza sana hili hasa nchi za Afrika kutokana na uwezo wake mkubwa wa fedha na teknolojia.

  Lengo la mbinu hii ni :
  Mosi,kuwatoa kwenye ajenda ya vita dhidi yake na kuwaelekeza kwenye mijadala mingine.
  Pili, kuchonganisha watu, serikali na viongozi wao.
  Tatu, kupeleka ujumbe duniani kuwa kiongozi fulani na serikali yake hawafai tena.
  Nne, kuligawa taifa kati ya upande unaoamini matukio kutekelezwa na fulani na upande unaoamini vingine.


  0 0

   Jalada la kitabu cha ‘MIFUPA YA ALBINO’.
  Mwandishi Daniel Mbega, akiwa ameshikilia Karunguyeye waliokaushwa nyumbani kwa mganga wa jadi.


  MWANDISHI wa habari mwandamizi nchini, Daniel Mbega, amekamilisha kuandika kitabu kinachofichua siri zilizo nyuma ya pazia kuhusiana na mauaji ya vikongwe na albino nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.


  Mwandishi huyo, ambaye alifanya utafiti kwa kipindi cha miezi nane mfululizo katika mikoa 10 ya Kanda ya Maziwa Makuu, amesema kitabu hiyo alichokipa jina la ‘MIFUPA YA ALBINO’ kinatarajiwa kuwaingia kiwandani wakati wowote na kwa sasa anatafuta msaada wa fedha za kuchapia.


  “Nimekamilisha, lakini nimekwama kidogo kuhusu fedha za uchapaji na kama kuna taasisi yoyote au mtu anayeweza kunisaidia nitashukuru sana,” amesema mwanahabari huyo.“Yeyote mwenye nia njema na jamii ya Watanzania na anaguswa kusaidia uchapaji wa kitabu hiki, ninaomba awasiliane nami kwa namba hii 0656-331974, kwani naamini kitabu hiki kitakuwa msaada pia wa kiroho baada ya kujua mambo yanayofanywa hata na baadhi ya viongozi wa dini wanaotumia ushirikina,” aliongeza.

  Bw. Mbega amesema kwamba, katika utafiti wake huo alifanikiwa kukutana na waganga wa jadi, wachawi na matapeli katika mikoa ya Shinyanga, Geita, Simiyu, Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa, ambako alikaa kwa miezi miwili akifanya uchunguzi.  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi ametangaza rasmi kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli ameivunja rasmi Wakala wa Uendelezaji Mji wa Kigamboni (KDA) kuanzia leo.

  Aidha Mheshimiwa Rais ameelekeza kwamba shughuli zote zilizokuwa zinafanywa na KDA sasa zifanywe na manispaa ya kigamboni kwa mujibu wa sheria.

  Na kuanzia sasa manispaa ya Kigamboni itahusika kupanga na kusimamia ardhi yake kama manispaa nyingine zinavyofanya, na Wizara ya Ardhi itaendelea kusimamia masuala yote yahusuyo ardhi kwa ujumla wake kama inavyofanya katika manispaa zote nchini.

  Waziri wa Ardhi pia akatangaza kwamba kuanzia sasa wakazi wa mji wa Kigamboni wasizuiliwe kupewa hati zao za umiliki wa ardhi na wasizuiliwe kupewa vibali vya ujenzi.

  Mheshimiwa Lukuvi pia amefuta mashamba mawili yalioko wilayani kigamboni jijini Dar es salaam na kurudisha mashamba hayo kwa serikali ya wilaya ya kigamboni.

  Ufutaji hu ni baada ya wamiliki hao kushindwa kuyaendeleza na kuwanyima fulsa wananchi kufanya shughili zingine na kuinyima wilaya kufanya shuguli za viwanda na uwekezaji mwingine kutokana na kuhodhi kwa maeneo hayo.

  Nae mbuge wa wa Kigamboni Dr. Faustine Ndugulile ametoa shukrani zake kwa Rais kwani Muingiliano wa  majukumu wa mamlaka hizo ulikuwa ukiwabana wananchi hivyo kuwasababishia  kushindwa kufanya shuguli za maendeleo.

  Nao baadhi ya wananchi wa Kigamboni wamefurahishwa sana na maamuzi ya Rais kuhusu kuvunjwa kwa Wakala wa Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA) kwani ulikuwa unawapa wakati mgumu katika kuendeleza maeneo yao na kuleta urasimu.

  0 0

  Na Jumbe Ismailly SINGIDA 

  SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la Empower Society Transform Lives (ESTL) la Mkoani Singida limesema kwamba ukeketaji wa wanawake na watoto ni tatizo kubwa Afrika,Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi 28 zinazotajwa kuendeleza mila hiyo mbaya.

  Hayo yalisemwa na Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Mkoani Singida,Joshua Ntandu kwenye risala aliyosoma wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukeketaji katika vijiji 14 vilivyopo katika kata za Itaja,Mgori,Ntonge na Ughandi,uliofadhiliwa na The Foundation For Civil Society na kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Singida.

  Aidha Ntandu alifafanua kwamba inakadiriwa kuwa Tanzania ina zaidi ya wanawake milioni 7.9 waliogundulika kuwa wamekeketwa huku Mkoa wa Singida ukishika nafasi tano za juu za mikoa inayoongoza kwa ukeketaji hapa nchini.

  Alisema tafiti zinaonyesha pia kwamba vitendo hivyo vinaendelea kuongezeka katika Mkoa wa Singida na sababu kubwa zinazotajwa ni pamoja na imani kwamba ukeketaji ni sehemu ya makuzi ya mtoto wa kike na kwamba humzuia mtoto wa kike asiingie katika mahusiano ya mapenzi kabla ya kuolewa.Hata hivyo Ntandu alisisitiza kuwa jamii pia huamini kwamba ukeketaji ni tiba ya ugonjwa unaojulikana kama lawalawa kwa watoto wa kike (Vaginal or Urinary Tract Infection (UTI).

  “Kadhalika kuna mbinu mpya ambayo imeshamiri ya ukeketaji wa watoto wachanga mara tu wanapozaliwa na kabla ya kufikia umri wa mwaka mmoja,na hii hufanywa ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola”alisisitiza Mtendaji mkuu huyo wa ESTL.

  Akizindua mradi huo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida,Afisa Ustawi wa jamii wa Mkoa wa Singida,Shukurani Mbago,pamoja na kusikitishwa na mbinu mpya iliyoshamiri ya ukeketaji wa watoto wachanga,alizitaja baadhi ya sababu za kuongezeka kwa vitendo hivyo kuwa ni imani kuwa ukeketaji ni sehemu ya makuzi ya mtoto wa kike na kwamba kumzuia mtoto wa kike asiingie katika mahusiano ya mapenzi kabla ya ndoa.

  “Jamii pia huamini kuwa ukeketaji ni tiba ya ugonjwa ujulikanao kwa jina la lawalawa kwa watoto wa kike mara tu wanapozaliwa na kabla ya kufikia umri wa mwaka mmoja.”alifafanua Katibu tawala huyo wa Mkoa.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ESTL Mkoa wa Singida,Rose Mjema aliweka bayana kwamba mpaka sasa wameshaunda kamati za kutokomeza ukeketaji katika ngazi za vijiji na kata kutokana na watu waliopo katika ngazi hizo kuonyesha utayari wa kufanyakazi na wao.

  Kwa mujibu wa Mjema wajumbe waliopo katika kamati hizo ni ni vijana tu kwa ngazi ya kata na vijiji,viongozi wa jadi,wakunga wa tiba asilia na wakunga wa jadi kwa kuwaandalia vikundi vya kupiga vita masuala ya ukeketaji kwenye maeneo yao.

  Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Singida,Elia Digha akizungumza na washiriki wa semina hiyo alishauri kwamba ili kukabiliana na vitendo hivyo kuanzia ngazi za serikali za vijiji pamoja na Halmashauri waanze kuandaa sheria ndogo itakayosimamia udhibiti wa ukeketaji katika Halmashauri ya wilaya hiyo.
  Ni Mwenyekiti wa Bodi ya ESTL,Bi Rose Mjema akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya kupinga vitendo vya ukeketaji huku akitoa tahadhari juu ya madhara yatokanayo na vitendo hivyo vya ukeketaji.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).
  Ni baadhi ya Mangariba na wakunga wa jadi kutoka katika Tarafa ya Mgori,wilayani Singida ambao wameamua kuachana na shughuli za kukeketa baada ya kupatiwa elimu na Shirika lisilokuwa la kiserikali la ESTL la Mkoani Singida,wakitoa ushuhuda kwenye uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukeketaji kwa wanawake katika Mkoa wa Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Singida.

  0 0


  Na Ramadhani Ali – Maelezo 13.9.2017

  Makamu wa Raiswa Hospitali ya watoto ya Hunan Chini China Zhu Lihui ameahidi kuwa Hospitali hiyo itaendelea kushirikiana na Hospitali ya Mnazimmoja ya Zanzibar kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuimarisha Utawala wa Hospitali.

  Zhu ameeleza hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku kumi yanayowashirikisha madaktari na wauguzi 25 wanaoshughulikia watoto kutoka Hospitali ya Mnazimmoja, Kivunge na Makunduchi.

  Amesema Hospitali ya watoto ya Hunan imewahi kutoa mafunzo kwa wafanyakazi 26 katika vipindi tofauti nchini China imeamua kufanya mafunzo Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Afya iliwafanya kazi wengi waweze kufaidika.Ameeleza matarajio yake kuwa wafanyakazi waliopata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo wataenda kuwaelimisha wafanyakazi wenzao ambao hawakubahatika kushiriki.

  Aidha amesema kuja kwamadaktari bingwa kutoka jimbo la Hunan kutoa mafunzo hapa Zanzibar kutaongeza mashirikiano kati ya Hospitali ya Mnazimmoja na kubadilishana uzoefu katika kuimarisha afya za wananchi na kuimarisha masuala ya utawala.Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiawu amesema ushirikiano baina ya China na Zanzibar niwamuda mrefu na nchi yake itaendelea kusaidia Zanzibar katika kuimarisha na kukuza maendeleo ya wananchi.

  Alisema mafunzo yatakayotolewa na wataalamu kutoka Hospitaliya watoto ya Hunan yatawajengea uwezo watendaji wa wodi za watoto na kuimarisha afya ya mama baada ya kujifungua na watoto wanaozaliwa.
  Akifungua mafunzo hayo yanayofanyika Hospitali mpya ya wazazi ya Mnazimmoja, Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman aliishukuru Hospitali ya watoto ya Hunan kwa kusaidia kuwaongezea ujuzi wafanyakazi wanaoshughulikia matatizo ya watoto na kuimarisha utawalawa Hospitali.

  Aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa wasikivu na kufuatilia kwa karibu masomo watakayo someshwa ili nao kuja kuwa walimu kwa wengine baada ya kumaliza na kuwawezesha wataalamu wa China kusomesha kada nyengine za afya.
    Makamu wa Rais wa Hospitali ya Watoto ya Hunan nchini China akizungumza na washiriki wa mafunzo ya siku 10 ya Madaktari na wauguzi wanaoshughulikia watoto katika Hospitali ya Kivunge, Makunduchi na Mnazimmoja mafunzo yanayofanyika Mnazimmoja Mjini Zanzibar. 
   Balozi mdogo wa china aliepo Zanzibar XieXiawu akitoa hutuba katika ufunguzi wa mafunzo ya siku 10 ya kuwajengea uwezo madaktari na wauguzi wanaofanyakazi wodi za watoto za Hospitali ya Kivunge, Makunduchi na Kivunge. 
   Naibu Waziri wa Afya Arusi Said Suleiman akifungua mafunzo ya madaktari na wauguzi wanaoshughulikia watoto na kuimarisha utawala wa Hospitali, mafunzo yanayofanyika Hospitali kuu ya Mnazimmoja.
  Washiriki wa mafunzo kutoka Hospitali ya Mnazimmoja, Kivunge na Makunduchi wakiwa pamoja na wakufunzi wao kutoka Hospitali ya Hunan China wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Naibu Waziri wa Afya Bi. Arusi Said Suleiman (hayupo pichani).Picha na Makame Mshenga. 

  0 0

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, mchana huu, imemuachia huru mfanyabiashara maarufu Yusuph Manji na wenzake watatu baada ya mkurugenzi wa mashtaka nchini DPP kuwasilisha hati ya kumuachia (Nole Prosequie) kuonyesha kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.  0 0

  Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali na uvumbuzi, Tigo Tanzania imetambulisha huduma mpya ya Tigo Business inayotoa bidhaa na huduma mahsusi kwa biashara na mashirika ya aina yote; ili kuongeza ufanisi, ukuaji na faida. 

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema Tigo Business inatoa huduma za kipekee zinazolenga mashirika ya umma, serikali, biashara binafsi, kampuni za usambazaji na usafirishaji, mashirika ya fedha, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, wachimbaji madini, viwanda na kadhalika; huku ikiwapa uhuru wa kufanya shughuli zao kwa ueledi zaidi na kuwawezesha kufanikisha miradi yao nchini na nje ya nchi. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu ya Tigo Tanzania, Simon Karikari akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.

  ‘Tigo Business ndio huduma ya mawasiliano ya biashara inayokuwa kwa kasi zaidi nchini. Inajumuisha biashara za aina zote bila kutegemea ukubwa wa biashara au bajeti, huku ikiwapa wafanyabiashara amani na uhuru wa kushugulikia masuala ya muhimu zaidi yanayohusu ukuaji wa biashara zao,’ Karikari alisema.

  Tigo Business itafanikisha mahitaji tofauti ya mawasilano ya biashara ikiwemo mawasiliano ya sauti, data na mifumo ya mitambo ya biashara kwa ufanisi wa juu na kwa gharama nafuu zaidi. Kwa kutumia uwekezaji mkubwa wa Tigo katika mkongo wa mawasiliano (fibre) na  kituo cha kuhifadhia kumbukumbu (data centre), Tigo business imejikita kuongoza soko la mawasiliano ya kisasa ya biashara huku ikiboresha jinsi wateja wanavyotumia mawasiliano ya kisasa kukuza biashara zao. 

  ‘Tigo Business inaelewa kuwa dunia ya sasa imeunganishwa kwa mtandao na hii inabadilisha jinsi biashara zinvyoendeshwa. Kwa kutumia mtandao wetu na bidhaa zetu,  Tigo inatumia uzoefu wetu wa maisha ya digitali kuleta mageuzi katika mifumo ya biashara,’ Karikari alisema.
  Tigo Business, kauli mbiu yetu ni biashara yako ni biashara yetu.
  Tigo Business ni ya kwanza kuletea ofa ya Business Day inayowapa wafanyabiashara muda wa maongezi na data kwenda mitandao yote bila kikomo, huduma ya simu nje ya nchi na huduma ya makundi maalum ya simu ambayo inawawezesha kupiga simu za biashara kwa bei nafuu zaidi huku wakiwa hewani kwa wakati wote.

  Tigo Business pia inaongoza soko kwa kuwa na kituo cha kisasa zaidi cha kuhifadhia kumbukumbu (Tier 3 Designed Data Center) ya kwanza hapa nchini Tanzania, inayowahakikishia wateja kuwa watakuwa hewani 99.99% ya muda, huku wakiwa na uhakika wa ulinzi wa kisasa na utendaji wa hali ya juu wa mitambo yao. 

  Tigo Business pia inatoa ofa ya Mtandao usiohamishika (Advanced Dedicated Fixed Internet) na Corporate Access Point Network Solutions (APN) ambazo zinaunganizha wafanyakazi, mitambo na mashine moja kwa moja kwa njia ya mtandao bila kuhitaji uangalizi wa binadamu. Corporate APN inawezesha wafanayabiasahra kufuatilia utendaji wa mifumo yao ya biashara na uwekezaji wao kwa muda wote na toka sehemu yoyote ile bila hitaji la wao kuwa ofisini. 

  Tigo Business pia inatoa huduma bora kwa wateja, masaa 24 kupitia mfumo wetu maridhawa wa huduma kwa wateja. Tunajitatiti kuwa mshirika wako wa karibu katika biashara.

  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akipokelewa na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda Bi. Asha Abdalla Mwelekwa mara baada ya kufika katika ofisi hizo ili kuonana na  Kaimu Balozi ambaye ni Naibu Balozi  Elibariki Nderimo Maleko.

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akiangalia ngoma ya Utamaduni ya Kikundi cha Taifa cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati alipofika katika uwanja wa Uhuru Kololo kuangalia maonesho ya bidhaa za wasanii wa nchi mbalimbali Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

    Mhe. Mwakyembe akiangnalia bidhaa za viatu vinavyozalishwa na wasanii wa Nchi ya Rwanda ambvyo vikanyagio vyake vimetengenezwa kwa matairi ya gari wakati alipotembelea banda la nchi hiyo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
  Wanafunzi 100  wahitimisha mafunzo ya sanaa ikiwa ni mara ya pili  kufanyika   katika halimashauri ya wilaya ya kisarawe Mkoani Pwani,ikishirikisha  shule 5 kutoka  katika wilaya hiyo ambazo ni Chanzige A,ChanzigeB,Kibasila,Kazimzumbwi  pamoja  na Sanze .

  Nae muwakilishi wa  mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Simon  Biginagwa amezungumza  hayo leo katika Halimashauri ya wilaya ya Kisarawe  Mkoa wa Pwani  amesema  kuwa sasa ni wakati wa kuendeleza utamaduni wetu wa kitanzania  badala  ya  tamaduni na mila za kizungu akiongezea kuwa  kupia tamaduni zetu hupata fursa ya kuweza  kupa ajira na amesisitiza pia kulinda amani  nchini  .

  Hata hivyo Mkurugenzi Ukuzaji  Sanaa na Masoko Basata  Vivian Shalua amemshukuru mkuu wa wilaya ya kisarawe kwa kuwapa kibali cha kuweza  kufanya mafunzo ya sanaa kwa  wanafunzi hao na  ;NIvizuri watoto  kufanya sanaa wakiwa mashuleni na Lengo ikiwa ni  kukuza viapaji vya watoto na kufufua ngoma zetu za utamaduni;  amesema Mkurugenzi huyo.

  Afisa  elimu  Halimashauri  ya kisarawe  Zipporah Daniel  Simwanza, amewapongeza basata kwa  kuweza kurudi tena katika Halmashauri hiyo  kuweza kufanya zoezi hilo la uandaaji wa kutoa mafunzo ya sanaa  kwa wanafunzi hao .

  Vilevile  Afisa maendeleo ya jamii  Halimashauri ya Kisarawe Wanchoke Juma ametoa wito kwa walimu kufundisha  watoto  mafuzo ya sanaa  mashuleni na kulichukulia somo la sanaa kama masomo mengine badala ya kulifanya kama la ziada.
  Mkurugenzi Ukuzaji  Sanaa na Masoko Basata  Vivian Shalua, akizungumza na wanafunzi wa shule  za Kisarawe juu ya umuhimu wa kuendeleza sanaa na  tamaduni za  kitanzania leo katika Halimauri ya Kisarawe Mkoani pwani.
  Afisa Elimu Halimashauri ya Kisarawe, Zipporah Daniel Simwanza akizungumza na wanafunzi wa  Halimashauri ya Kisarawe na kuwapongeza kwa kujitokeza kwa wingi katika  kupata mafunzo ya sanaa yalioandaliwa na Basata na kuwataaka wanafuzi hao kudumisha tamaduni zetu leo katika Halimashauri ya mji wa Kisarawe  Mkoa wa Pwani.
   Mwakilishi wa  mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Simon  Biginagwa, akizungumza na wanafunzi hao akiwataka  pia kuendeleza utamaduni wetu badala ya kuiga ule wa kizungu kwani sanaa ni chanzo cha ajira na kutoa wito kwa wazazi kuwaruhu watoto kushiriki mafunzo  hayo ya sanaa leo katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo  Halmashauri ya Kisarawe Mkoani Pwani
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule za msingi za Kisarawe wakitoa burudani ya kuimba na kucheza  ya ngoma za asaili  mojawapo kati ya mafunzo waliyopata kwa viongozi,  waandishi wa habari  pamoja na walimu wao leo katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo  Halmashauri ya Kisarawe Mkoani Pwani  .
  Picha ya pamoja wakiwepo viongozi wa Kisarawe waandaaji wa mafuzo hayo Basata pamoja na walimu waliofundisha saana hizo mbalimbali ikiwemo kuimba, kucheza nyimbo za tamaduni ya asili ya Mtanzania leo katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo  Halmashauri ya Kisarawe Mkoani Pwani. (Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii)

  0 0

  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akizungumza na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock (katikati) na Mshauri Mwandamizi wa Serikali hiyo, Ndg. Aran Corrington, pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akiagana na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock (kulia) pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (kulia)akiagana na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock (kushoto) pale ugeni kutoka ubalozi wa Ireland ulipotembelea Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma, ukioongozwa na Balozi huyo. (PICHA NA OFISI YA BUNGE).

  0 0


  Na Karama Kenyunko.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo imemuachia huru mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji na wenzake watatu baada ya Mkurugenzi wa mashtaka ya jinai nchini (DPP) kuwasilisha Nole proseque kuonesha kuwa hana nia ya kuendele kuwashtaki washtakiwa dhidi ya mashtaka yao ya uhujumu uchumi yanayowakabili.

  Hakimu   Mkazi   Huruma Shahidi amewaachia huru washtakiwa hao baada ya DPP kuwasilisha hati hiyo ya kuwafutia mashtaka chini ya kifungu cha sheria namba 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai (CPA)

  Manji na wenzake watatu, Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda (28), Mtunza stoo, Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43)  mkazi wa Chanika.   wamechiwa baada ya kufikishwa mahakamani hapo kwa hati ya wito ya kuwatoa mahabusu (remove order).

  Akizungumza mbeleya hakimu Mkazi Huruma Shaidi, wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amesema mahakamani, “tuliomba remove order kwa ajili ya kuwaleta washtakiwa mahakamani hapa kwani DPP kupitia Jamuhuri ameondoa mashtaka dhidi ya washtakiwa na hana nia ya kuendelea kuwashtaki”

  Wakili wa utetezi, Hajira Mungula alipoulizwa kama analolote la kusema juu ya hilo, alisema kuwa, “sheria inamruhusu DPP kufanya hayo”. Hakimu Shaidi aliwaambia washtakiwa kuwa wako huru wanaweza kuondoka. “Washtakiwa mko huru ondokeni”.

  Manji ameondoka mahakamani hapo akiwa huru bila ya ulinzi wowote akiwa ameongozana na washtakiwa wenzake ha kuingia kwenye gari aina ya Alteza yenye namba za usajili T 383 DFN

  Kwa mara ya kwanza Manji na wenzake walisomewa mashtaka hayo ya uhujumu uchumi, July 5 mwaka huu, akiwa kitandani katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitali ya taifa .

  Wote kwa pamoja wanadaikwa kuwa Juni 30, mwaka huu maeneo ya Chang’ombe A wilayani Temeke Dar es Salaam, washitakiwa wote kwa pamoja, walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea  sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vyenye thamani ya Sh milioni 192.5.

  Pia inadaiwa Julai Mosi mwaka huu, maeneo ya Chang’ombe A, wilayani Temeke, Dar es Salaam, washitakiwa  wote walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo nane ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za JWTZ vyenye thamani ya Sh milioni 44.

  Katika mashitaka ya tatu, inadaiwa Juni 30, mwaka huu maeneo  ya Chang’ombe A, washitakiwa walikutwa wakiwa na mhuri wa JWTZ ambao uliandikwa ‘’Mkuu wa Kikosi 121  Kikosi cha JWTZ’’ bila kuwa na uhalali kitendo kinachohatarisha usalama wan chi.

  Pia inadaiwa, terehe hiyohiyo maeneo ya Chang’ombe washitakiwa walikutwa na mhuri uliokuwa umeandikwa ‘’Kamanda Kikosi 834 KJ Makutupora Dodoma bila kuwa na uhalali kitendo kinachohatarisha usalama.

  Ilidaiwa  Juni 30, mwaka huu, maeneo hayo, washitakiwa kwa pamoja walikutwa na mhuri ulioandikwa ‘’Commanding Officer 835 KJ, Mgambo P.o.Box 224 Korogwe isivyo halali.

  Katika mashitaka ya sita, inadaiwa Julai Mosi mwaka huu, maeneo hayo ya Chang’ombe, washitakiwa walikutwa na gari lenye namba za usajili SU 383 mali waliyojipatia isivyo halali.

  Aidha, wanadaiwa kuwa Julai Mosi mwaka huu, maeneo ya Chang’ombe A wilayani Temeke, Dar es Salaam, washitakiwa wote walikutwa na gari lenye namba za usajili SM 8573 pasipo uhalali.

  Kabla ya uamuazi huu leo, wiki iliyopita Yusuf Manji na wenzake hao, walipelekwa polisi kuhojiwa kuhusiana na kesi hii ya uhujumu uchumi kwa lengo la kukamilisha upelelezi ambapo walirudishwa baada ya usiku mmoja.

  0 0

  Ofisa Mwandamizi Biashara wa Benki ya Azania, Victor Musendo (kulia) akimuelezea jambo mmoja wa wahandisi waliotembelea banda lao kuhusu huduma mbalimbali za benki ya Azania wakati wa Mkutano wa Mwaka wa wahandisi Tanzania uliofanyika Septemba 7-8, 2017 Mkoani Dodoma. Katikati ni Afisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea.
  Maofisa wa Benki ya Azania wakiongozwa na Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja binafsi, Jackson Lohay (watatu kushoto) wakizungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika banda la Azania Bank Limited wakati wa Mkutano wa mwaka wahandisi uliofanyika Dodoma Septemba 7-8, 2017 .
  Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo kutoka vyuo mbalimbali kitaifa wakipata maelezo kuhusiana na huduma za kibenki zitolewazo na Azania Bank Ltd.

  0 0

  Na Tiganya Vincent

  KAMATI ya Ulinzi na Usalama mkoani Tabora imezuia vifaa vya ujenzi vya Kampuni ya Ujenzi ya Ceytun iliyokuwa ikipanua Uwanja wa Ndege na kunyang’anywa Hati za kusafiria za viongozi wake wawili hadi watakapomalizia malipo ya waliokuwa wafanyakazi wao.

  Uamuzi huo umetolewa jana mjini hapa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alipokuwa akitoa maamuzi ya  wajumbe wake kwenye mkutano na viongozi wa Kampuni hiyo na wanaodai.

  Alisema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya Mhasibu wa Kampuni hiyo Bw. Mahmut Garik kukataa kutoa vielelezo vinavyoonyesha  jinsi alivyowalipa waliokuwa wafanyakazi wao ili kuona kama madai ya wafanyakazi hao ni halali au sio halali.
  Mwanri alisema kuwa zoezi la kushughulikia madai ya wafanyakazi hao ilikuwa ni sehemu ya utekelezaji maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelea Uwanja wa Ndege mkoani Tabora kuonyeshwa bango la kumdai mmiliki wa Kampuni na ndipo Rais aliagiza lishughulikiwe.

  Alisema kuwa wakati wa majadiliano baina ya pande zote tatu yakiendelea na ndipo Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora alipomwomba Mhasibu wa Kampuni hiyo kuwasilisha vielelezo vinavyoonyesha ushahidi wake kama kweli alisha walipa wafanyakazi wake na ndipo alipojibu kuwa hawezi kutoa labda waendee Mahakamani.

  “Kitendo hicho cha kuonyesha jeuri hakiwezi kukubalika…RPC hakikisha hatoi vifaa vyake na Uhamiaji chukua Hati zao za kusafiri …hadi ukweli ujulikane…maana wakishaondoka Tabora ..wananchi hawa hawawezi kuwapata” alisema Mwanri
  Kwa upande Meneja Mradi wa Kampuni ya Ujenzi ya Ceytun  Ercan Kavaic aliomba radhi kwa kauli ya Mhasibu wake ya kukataa kutoa nyaraka hizo ambazo ndio zingesaidia kuondoa mvutano huo.

  Aliahidi kukaa pamoja na wadai wake na watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa  Mkoa ili kupitia madai na kuna njia bora ya kutatua tatizo hilo. Kavaic alikubali vifaa vyake kuwa chini ya ulinzi na kutoa hati yake ya kusafiria hadi hapo watakapopata muafaka.

  Kwa upande wa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Tabora Damian Ndabalinze aliwashauri vijana wanaomba kazi katika Kampuni mbalimbali za ujenzi wakahakikisha wanapewa mikataba kabla mradi haujaanza ili wajue malipo na stahili wanazopaswa kupata ili  kuondoa migogoro wa malipo pindi wanapokuwa wamemaliza mkataba.

  Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa alimwakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa hakuna kifaa kitakachoondoa katika eneo la mradi hadi hapo wakapokuwa wamehakikishiwa kuwa mgogoro ulipo wa malipo umemalizika.

  0 0

  Na KaramaKenyunko, Glogu ya jamii
  MSHITAKIWA Herbinder Seth leo ameileza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, bado hajapelekwa Hospital ya Muhimbili kutibiwa kama amri ya mahakama ilivyoagiza.

   Mshtakiwa Seth ameyasema hayo leo baada ya wakili wake wa utetezi, Melchisedeck Lutema kuileza mahakama kuwa bado mteja wake huyo anayeshtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha inayomkabili yeye na mwenzake James Rugemalira bado hajapelekwa Hospital ya Muhimbili 

  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Lutema ameomba upande wa mashtaka ueleze kwanini mshtakiwa hapelekwi hospitali, kwani katika mashauri yaliyopita  mahakama imetoa amri mara kadhaa zote zikielekeza mshitakiwa huyo apelekwe Hospitali ya Muhimbili lakini haijatekelezwa.

  ameiomba mahakama itumie busara ili kuhakikisha mshtakiwa anapekwa hospitali na kwamba wakuthibitisha kama ametibiwa au la ni mshtakiwa mwenyewe.

  Habinder amedai hayo baada ya Wakili wa Serikali, Leonard Swai akisaidiana na Vitalis Peter kudai kuwa shauri limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

  akiongea kuhusu matibabu, alidai mshtakiwa alipelekwa hospital ya magereza na kwamba alitibiwa na mtaalamu Dotto Pakacha ambaye anampatia matibabu kila anapolalamika huwa wanamuona na kwamba yeye mwenyewe alifuatilia kupata uhakika kuwa anapatiwa matibabu kwani hata akipata shinikizo la damu huwa wanamuona.  "Tunaendelea na upelelezi kwasababu kuna mashtaka ya kugushi yanahusisha taasisi zaidi ya moja tunaomba mahakama itupe muda ili tukamilishe upelelezi"alidai

  Hata hivyo, Hakimu Shaidi amesisitiza mshitakiwa Seth apelekwe katika hospitali ya Muhimbili kama ilivyotoa maagizo awali na kwamba inaonyesha wazi amri ya mahakama haifuatwi, “ oda ya mahakama lazima ifuatwe, haiwezekani kila siku tukija hapa tunaongea kitu kimoja tu hii haipendezi" amesema hakimu Shaidi.


  Aidha, Wakili anayemtetea James Rugemarila, Pascal Kamala amedai kuwa washtakiwa walifikishwa mahakamani hapo juni 19 mwaka huu hadi leo ni siku 87 wako ndani na makosa wanayoshtakiwa nayo hayana dhamana na upelelezi haujakamilika, ili haki iweze kutendeka kwa pande zote mbili wanaomba upelelezi ukamilike mapema na haki iweze kutendeka.

  Kesi hiyo itatajwa Septemba 29 mwaka huu. 
  Seth  na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kighushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

older | 1 | .... | 1908 | 1909 | (Page 1910) | 1911 | 1912 | .... | 3270 | newer