Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1899 | 1900 | (Page 1901) | 1902 | 1903 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (kulia) akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania, Andrew Kashangaki (katikati) katika hafla ya kukabidhi jengo maalum la mama ngojea ‘maternity waiting home’ yaani kwa kina mama wajawazito watakaokua wakisubiri kujifungua katika hospitali ya Kinyonga – Kilwa Kivinje, mradi uliogharimu shilingi 220m/-. kushoto kwake ni Mratibu wa shughli za Uwajibika kwa jamii -PANAFRICAN ENERGY Tanzania, Yvonne Abba.
  Meneja Uwajibikaji kwa jamii kampuni ya PAN AFRICA energy, Andrew Kashangaki akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai baada ya Kumkabidhi jengo la mama ngojea na vifaa vya kupumzikia iliyogharimu shilingi milioni 220.
  Baadhi ya wananchii wa wilaya ya Kilwa wakimsikiliza mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai akitoa hotuba yake katika Hafla ya Uzinduzi wa Jengo la Mama wajawazito iliyofanyika katika Hospital Kinyonga wilaya ya Kilwa .
  Mratibu wa uwajibikaji kwa Jamii-PANAFRICA ENERGY, Yvone K Abba akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai katika Hafla ya kukabidhi jengo la kusubiri la mama Mjamzioto-Kilwa Lindi


  0 0

  Na Tiganya Vincent
  Sikonge

  SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kutolipa malipo ya kiasi cha zaidi ya milioni 300 kwa ajili ya miradi miwili ya maendeleo ambayo imebainika kuwa na kasoro mbalimbali.
  Agizo hilo limetolewa jana mjini Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kikungi Kata ya Chabutwa na ujenzi wa barabara ya lami mjini Sikonge.
  Alisema katika mradi wa Zahanati  maelezo Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge yanaonyesha kuwa mjenzi wa Zahanati huo amekiuka makubaliano ya mpango wa ujenzi na vifaa vitakavyotumika katika (BOQ).
  Mwanri alisema kuwa mjenzi wa Zahanati hiyo amekuwa akitumia vifaa zaidi au pungufu na wakati mwingine ametumia vifaa katika ujenzi wa majengo ya ZAhanati hiyo ambavyo havikuonyeshwa katika BOQ bila makubaliano na Halmashauri hiyo.
  Kwa mujibu wa makubaliano mradi huo wa Zahanati unapaswa kugharimu shilingi milioni 170 ikiwa ni gharama za vifaa shilingi milioni 130 na gharama za mjenzi milioni 40 lakini kwa sababu ya mjenzi wake kutofuata maelezo ya BOQ zinaweza kuzidi.
  Katika mradi wa pili ambao ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa urefu kilometa moja kwa gharama za shilingi milioni 220.
  Mkuu huyo wa Mkoa alisema mradi huo unaonekana kujengwa chini ya kiwango na muda ambao mkandarasi alipaswa ameameashamaliza umeshapita.
  Kufuatia kasoro hizo katika miradi hiyo miwili Mkuu huyo wa Mkoa amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Sikonge kutoidhinisha malipo ambayo yalikuwa hayajafanyika kwa mjenzi wa Zahanati ya Kikungi ya shilingi milioni 170 na yale yaliyokuwa yamebaki ya zaidi shilingi milioni 70 zilizokuwa zimebaki kwa mradi wa barabara.
  Alisema kuwa wajenzi wote wa miradi hiyo watalipwa baada ya timu ya wataalamu kutoka Mkaguzi wa Hesabu Serikali za Mitaa  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Wakala wa Barabara Tanzania mkoa wa Tabora, Taasisi ya Kupambana na kudhibiti Rushwa(PCCB) na Wakala wa Majengo Tanzania(TBA).
  Mwanri alisema timu hiyo inalenga kutafuta ukweli kama taratibu za kutoa zabuni kwa wajenzi zilifuatwa na ikiwa vifaa vilivyotumika vinalingana na thamani halisi ya fedha na makubaliano katika BOQ.
  Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sikonge Simon Ngatunga alisema kuwa alisema katika mradi wa Zahanati mjenzi aliamua kutumia baadhi ya vifaa hata ambavyo havimo katika BOQ bila hata kuijulisha Ofisi yake.
  Alisema kuwa katika mradi wa barabara licha ya kutokwisha unaonyesha kuwa uko chini ya kiwango na kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuunda timu ya wataalamu kuchunguza miradi hiyo ili waone kama iko katika kiwango.
  Ngatunga alisisitiza kuwa hawezi kulipa hadi hapo timu ya wataalamu hapo itakapomuhakikishia kuwa taratibu zote zimezingatiwa.

  0 0


  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoa wa Kusini Unguja kutunza miradi na kuitumia kwa manufaa ya wote.

  Makamu wa Rais aliyasema hayo leo wakati wa Ufunguzi wa Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi ambao umefadhiliwa na Ubalozi wa Japan.

  Mhe. Samia aliwashukuru Ubalozi wa Japan kwa kufadhili ujenzi wa Uboreshaji wa Mazingira ya Elimu katika Wilaya ya Kusini ambao umegharimu dola za kimarekani laki moja na elfu kumi na mbili na mia nane na arobaini na tano (112,845) ambazo ni sawa na takribani ya shilingi milioni mia mbili arobaini na saba (247) .Awali Ubalozi wa Japan ulitoa dola za Kimarekani elfu ishirini na nane mia nane na sitini (28,860) takribani shilingi milioni sitini na moja za kitanzania kujenga uzio wa shule ya Msingi Muyuni .

  Makamu wa Rais alimshukuru sana Balozi wa Japan kwa ufadhili huo ambao umeendelea kuimarisha urafiki na mahusiano kati ya nchi mbili hizi, aliwataka wananchi wa Wilaya ya Kusini kutilia mkazo masuala ya elimu na kutunza miradi yote ili inufaishe na vizazi vijavyo.

  Makamu wa Rais pia aliwapongeza viongozi wa halmashauri ya wilaya ya kusini kwa kusimamia vizuri fedha za ufadhili na kufanikisha kukamika kwa ujenzi wa miradi kama ilivyopangwa na kukamilika mapema zaidi .
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki lililobeba mada isemayo Kuleta Mabadiliko katika jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutumia Kiswahili lilianza leo mjini Unguja, Zanzibar.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa ofisi ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mjini Zanzibar
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida wakipeana ishara ya kushukuru mara baada ya Balozi wa Japan kukabidhi miradi miwili mikubwa,mmoja ukiwa ni ujenzi wa uzio wa shule ya Msingi ya Muyuni na wa pili ni mradi wa uboreshaji wa mazingira ya elimu katika wilaya ya ya kusini uliojumuisha ujenzi wa shule ya awali katika kijiji cha Kajengwa na Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida wakikata utepe kama ishara ya kufungua Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuelezea Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida namna Pomboo wanavyovutia utalii katika mkoa wa kusini wakati akimkabidhi zawadi ya sanamu ya Pomboo mara baada ya ufunguzi wa Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais  0 0


  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amepewa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) ikiwa ni alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.

  Akikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa AWAMATA Taifa, Mwenyekiti wa AWAMATA Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo amesema Asasi hiyo imehamasika kutoa tuzo ya cheti kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa sababu ni mzalendo na amekuwa akifikiri juu ya maendeleo ya wananchi na namna mbalimbali za kuzalisha ajira kwa vijana.

  Amesema Mhe.Mtaka ni moja ya viongozi wabunifu sana na kama kiongozi kijana amekuwa na maono makubwa yenye manufaa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Taifa kwa ujumla, ambapo amehamasisha uanzishwaji wa viwanda katika Mkoa kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” na Kilimo cha Umwagiliaji wilayani Busega.

  “Mhe.Mtaka tumeanza kumfuatilia toka akiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Wilaya ya Hai mpaka na baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, tumekaa kama asasi tukashawishika kumpa tuzo hii, kwa sababu amekuwa anafanya kazi ya kizalendo na maendeleo hasa anapoumiza kichwa kwa ajili ya kutengeneza ajira; tena kila wilaya kwenye mkoa wake ina kitu cha kufanya” alisema Golyo.

  Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka, tuzo ya cheti kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWAMATA Taifa, ambayo imetolewa kwa Mkuu huyu wa mkoa kama alama ya kutambua kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akionesha tuzo ya cheti aliyokabidhiwa na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
  Kutoka kulia Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka, Katibu wa AMAWATA mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Millensasha Mneo na Afisa Uhusiano wa AWAMATA, Ndg Shushu Joel wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi tuzo ya cheti iliyotolewa kwa Mhe.Mtaka kama alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa AWAMATA na wadau wengine wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.


  0 0
  0 0

  Wakurugenzi wameagizwa kuhakikisha wanafuatilia watumishi wa afya waliojiriwa kwa ufadhili wa mfuko wa dharura wa rais wa marekani ( PEPFAR) kupitia THPS katika vituo mbalimbali mkoani Pwani wanalipwa mishahara yao kwa wakati.

  Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alipokuwa mgeni rasmi akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo, katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS).

  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alilipongeza shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS) katika juhudi wanazofanya katika sekta ya afya hususani mapambano dhidi ya ukimwi mkoani humo na kuwataka watumishi wa afya kuhakikisha wana wanatoa huduma ya vvu kila mahali katika vituo vya kutolea huduma za afya , mawodini, kliniki maalumu, kwenye mikusanyiko ya watu, na maeneo mengine maalumu ili malengo ya serikali ya 90 ya tatu yatimie ifikapo mwaka 2020 .

  Mshama alisema serikali iliridhia maazimio ya shirika la umoja wa mataifa ya kupambana na ukimwi ya tisini ya tatu ambapo alifafanua azimio hilo ni ifikapo 2020 asilimia 90 ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wawe wanatambua hali zao za maambukizi, asilimia 90 ya hao wawe wanatumia dawa na asilimia 90 ya walioko kwenye dawa wafubaze virusi kwa kiwango kinachotakiwa cha kopi 1000 za virusi kwa milimita moja ya damu.
  Mkuu wa Wilaya Kibaha, Assumpter Mshama akizungumza katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS). Mkuu wa Wilaya Kibaha Assumpter Mshama alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo.
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Maggid Mwanga akizungumza jambo katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS). 
  Mkurugenzi wa THPS Dk. Mbatia akimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo na kumwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Everist Ndikilo
  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akimkabidhi zawadi Dk. Beatrice (RMO PWANI) iliyotolewa na wafanyakazi wa THPC kutokana na mchango wake katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS). 
  Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akipatiwa maelezo juu ya upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi kwa kina kutoka kwa mtaalamu wa THPS.
  Mgeni rasmi Assumpter Mshama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya wenzake wa mkoa wa Pwani pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa THPS.


  0 0


  Na  Bashir  Yakub.


  1.UKOROFI  WA  WASIMAMIZI  WA  MIRATHI.


  Baadhi  ya wasimamizi  wa  mirathi  ni  wakorofi.  Baada   ya  kuteuliwa  kwa  jukumu  hilo   hawapendi  kugawa  mali  ili  kila  mtu  achukue  chake. Inapaswa  kufahamika  kuwa  mali  si  za  msimamizi  wa  mirathi .  Mali  ni  za  warithi  halali  isipokuwa  msimamizi  ni  kiongozi  tu.  Kwa  maana  hii  anawajibika  kusikiliza  warithi  wanasema  nini  ili  mradi  kile  wanachosema  kisipingane na  sheria.


  Wakati  mwingine  warithi  wanataka  wagawiwe  mali  zao   ili  kila  mtu  endelee  na  maisha  yake lakini  msimamizi  hataki  tena  bila  sababu  za  msingi. Hili  linakuwa  si  sawa  isipokuwa  kama  kuna sababu  za  msingi  za kufanya  hivyo.


  Sababu zaweza kuwa labda   anayetaka kugawiwa mali  ni  mtoto  mdogo asiyeweza  kumiliki  mali kwa wakati  huo, ni  mtu  asiye na  akili  timamu kwa  muda  huo,  kuna  shauri  mahakamani kuhusu  hiyo  mirathi  linaendelea, mali hazijakusanywa  zote, kuna  ugomvi  kwa  warithi  kuhusu  mali  ambao  utaathiri  mgao  nk.                      


  2. WAJIBU  MKUU  WA  MSIMAMIZI   WA  MIRATHI.      
                                   

  Kifungu  cha 108(1)  cha  Sheria  ya  Usimamizi  na  Uendeshaji  wa  Mirathi,  Sura  ya  352  kinaeleza  wajibu  wa  jumla  wa msimamia  mirathi. Kifungu  kinasema  kuwa  kazi  kubwa  ya  msimamizi  wa  mirathi  ni  kukusanya, mali  na  madeni  ya marehemu,kutunza  mali  hizo, kusimamia  gharama  za  mazishi  na  msiba, na  kugawa  mali kwa  wanaostahili. Na  kazi  hii yote  ifanyike  kwa  uadilifu  mkubwa.


  Kwahiyo  kumbe  moja  ya  kazi  ya lazima  na ya  kisheria  ya  msimamizi wa  mirathi  ni  kugawa mali  kwa  warithi.  Huu  ni  wajibu  ambao  msimamizi  anawajibika  kuutekeleza. Na  atagawa  kwa  mujibu  wa  wosia  au sheria  husika kama  hakuna  wosia. Hagawi  anavyotaka  yeye. Nani  apate  nini  halipo  katika  hiari  yake.

                  
     KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com
  0 0


  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini – Thobias Andengenye anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna wa Operesheni Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CF (OPS) Rogatius Peter Kipali, kilichotokea mapema leo Semptemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Mombasa, Ukonga jijini Dar es Salaam.

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatoa pole kwa Maafisa, Askari na Watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.

  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba huo na taarifa za Mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.

  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi

  Amina.
  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.

  0 0


  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inalaani vikali mauaji ya watoto wawili ambao walitekwa na kukutwa wameuawa katika mkoa wa Arusha.
   
  Wizara imepokea taarifa ya vifo hivyo kwa simanzi kubwa na inalaani vikali mauaji hayo ambayo yamekatisha uhai wa watoto hao katika umri huo mdogo. Mauaji na utekaji waliofanyiwa watoto hawa ni ukiukwaji mkubwa wa Haki za Mtoto ikiwemo haki ya Kuishi ambayo ndiyo haki kuu kati ya haki zote. 

  Wizara inawaasa wazazi, walezi na jamii kuimarisha mifumo ya ulinzi wa watoto katika ngazi ya mitaa, vijiji  na jamii ili kuwa na mifumo madhubuti katika kudhibiti ukatili unaofanywa dhidi ya watoto na kusababisha majonzi makubwa kwa wazazi, familia na jamii kwa ujumla.

  Jamii inakumbushwa kuwa tatizo la utekaji wa watoto linahitaji juhudi za pamoja katika kupambana nalo ili kuzifanya jamii zetu kuwa mahala salama kwa watoto wetu kuishi. Wizara itaendelea kuimarisha Kamati za ulinzi na usalama wa Mtoto katika ngazi za kata, vijiji na mitaa ili kuboresha huduma za ulinzi wa watoto wetu. 

  Aidha, Wizara inalipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zilizofanyika za kutaka kuwaokoa watoto hao  wakiwa hai, ingawa juhudi hizo hazikufanikiwa.  

  Wizara inaomba wazazi, walezi, familia, walimu na marafiki kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
  07/09/2017.

  0 0

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Septemba 7, 2017 amepokea ripoti za uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, zilizotokana na kamati mbili (Kamati ya Tanzanite iliongozwa na Mwenyekiti Dotto Biteko na Kamati ya Almas ilikuwa chini ya Mwenyekiti Mussa Azzan Zungu) zilizoundwa na spika wa Bunge, Job Ndugai . Muda mfupi baada ya kupokea ripoti hizo, Rais Dkt. Magufuli alisema kuwa ametengua uteuzi wa wateule wote waliotajwa katika ripoti hizo.
  Miongoni mwa wateule wa Rais waliotajwa katika ripoti hiyo ni pamoja na Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Edwin Ngonyani. Wengine waliotajwa katika taarifa hizo ni pamoja na Katibu Tawala Eliakim Maswi, wabunge Willium Ngeleja na Andrew Chenge.

  Katika hotuba yake aliyoitoa baada ya kupikea ripoti hiyo, Rais Dkt. Magufuli alisema "uwe RC,Waziri wau Mkurugenzi na umetajwa kwenye ripoti ya uchunguzi hauwezi kuendelea na wewe upo kwenye Serikali, Utupishe".

  "Kuna baadhi ya wabunge kama ulivyosema mheshimiwa Spika, kila mahali yupo, katika kashfa fulani yupo, katika hili yupo, katika lile yupo. Tena wengine bado wapo bungeni na wakati mwingine wanachangia mpaka mishipa inawatoka, taratibu zifanyike kuwachukulia hatua" Rais Magufuli Rais Magufuli amewasifu watanzania wazalendo ambao wako tayari kutoa uhai wao kwa ajili ya Taifa lao.

  "Tunawatumia watanzania wazalendo kupata taarifa za kizalendo kwa Taifa letu, wapo watanzania wanaorubuniwa na kuisaliti nchi yao, hao hawafai" Rais Dk John Pombe Magufuli, Ikulu. Dar es Salaam.

  Katika maelezo yake kabla ya kumkabidhi Rais ripoti hizo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kwa muda mrefu watanzania wamekuwa wakilalamika serikali kutowajali na kuwasikiliza. Amesema kupitia serikali ya Awamu ya Tano sasa watanzania wote watakuwa na haki sawa na wote watasikilizwa.

  "Watanzania ambao kwa miaka mingi wamejihisi hawasikilizwi na hawahurumiwi sasa ni wakati wao kujihisi kuwa ni watanzania na wanastahili haki zote kama watanzania kupitia serikali yako mheshimiwa Rais" Kassim Majaliwa

  Rais Magufuli amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kwa ripoti hizo za madini kwa ajili ya kufanyiwa kazi mara moja.

  0 0


   
  Mkuuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mhe.Jabir Shekimweri, (kushoto), akifungua pazia ikiwa ni ishara ya kuzindua nyumba mpya ya Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Kituo cha Kufua Umeme wa maji, Mtera, katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa, Septemba 6, 2017. Nyumba hiyo na nyingine iliyokarabatiwa zimejengwa kwa msada wa TANESCO kwa thamani ya shilingi milioni 35. Wengine pichani, ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja mama Joyce Ngahyoma,(wakwanza kulia), aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, , (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Ufuaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa. (kushoto), na Mkuu wa shule hiyo, Bw. Simon Dissa.


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi majengo mawili ya nyumba za walimu, shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Bwawa la kufua umeme wa maji Mtera, (Mtera Hydro Power Plant), lililoko katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa.

  Nyumba hizo zilizogharimu shilingi milioni 35, moja ikiwa mpya na nyingine imekarabatiwa, zimekabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa Septemba 6, 2017 na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja, Bi. Joyce Ngahyoma, ambaye alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Dkt. Tito Mwinuka.

  Akizungumza kabla ya kukabidhi nyumba hizo, Bi. Joyce Ngahyoma alisema, wakazi wa kata ya Mtera ni wadau na washirika wakubwa wa TANESCO katika kulinda miundombinu ya umeme ya kituo cha kufua umeme cha Mtera ambayo ina gharama kubwa kwa hivyo walipowasilisha maombi ya kujengewa nyumba ya mwalimu Mkuu, TANESCO ilikubali ombo hilo bila kusita.

  Alisema, uongozi wa TANESCO baada ya kupokea maombi hayo ulifanya tathmini na kutoa kiasi cha fedha shilingi Milioni 35 ambazo zilitumika kujenga nyumba jipya na kukarabati nyumba nyingine.

  Nyumba mpya iliyojengwa na TANESCO kwa ajili ya makazi ya Mwalimu Mkuu, ina vyumba vinne, choo, bafu na jiko, alisema.

  “Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia na niwaahidi tu kwamba Shirika litaendelea kushirikiana na serikali na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha sekta ya elimu, afya na huduma nyingine zinaimarika kwa kutoa michango ya hali na mali.” Alisema Bi. Ngahyoma.

  Alisema, sambamba na msada huo, TANESCO imekuwa ikisaidia jamii ya wana Mtera, katika kuwapatia huduma ya afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, huduma ya elimu ya awali(chekechea), kwenye shule ya chekechea iliyojengwa kuhudumia watotot wa wafanyakazi, na pia usafiri, ambapo mabasi yanayochukua wafanyakazi kwenda na kutoka kazini, huwasaidia pia wananchi.


  0 0

  MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanya uwekezaji wa Dola za kimarekani  Milioni 3.90 katika kiwanda cha machinjio  na usindikaji nyama cha Nguru ‘Nguru Hills Ranch Limited’ kilichoko nje kidogo ya Morogoro Wilaya ya Mvomero.

  Akizunguza katika  uwekaji wa saini kwenye mkataba wa uwekezaji, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga, alisema uwekaji wa saini umefikiwa baada ya tathini ya kina iliyofanywa na mfuko huo.Alisema mfuko umejiridhisha  kuhusu usalama wa rasilimali za wanachama kwenye uwekezaji huo.

  “Tunatambua kuwa Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji katika viwanda lakini LAPF imeona fursa hii ni moja wapo ambayo inakidhi vigezo vyote vya ajenda ya uwekezaji”alisema Sanga.

  Alisema LAPF imewekeza kwenye kiwanda hicho kwa ubia na kampuni ya ‘Eclipse Investments LLC’ inayotokana na kampuni tanzu ya Zubair Corporation ya Oman na kampuni ya ‘Busara Investments LLP’ na kufanya wabia kuwa watatu.

  “Kiwango cha uwekezaji kilichofanywa na LAPF ni USD 3.9 Milion ambayo ni sawa na asilimia 39 ya hisa za kampuni,ambapo Eclipse Investments LLC inaa hisa asilimia 46 na Busara Investments LLP ina hisa asilimia 15”alisema  Sanga.

  Alisema kiwanda hicho kina ukubwa wa ekari 6,000 ambapo ekari 1,200 zimejengwa miundombinu ya malisho ya mifugo kwa kipindi kisichopungua siku 90 kwaajili ya kuwanenepesha na kuwapa ubora kabla ya kuchinjwa.

  Sanga alisema kiwanda hicho kitakuwa na uwezo kuchinja na kuchakata ng’ombe 300 na mbuzi 2,000 kwa siku na kusafirishwa mara moja.

  “Nyama itakayozalishwa kwa kiwango kikubwa itasafirishwa nje kwenye nchi za mashariki ya kati na mashariki ya mbali ambako soko ni kubwa na Oman”alisema Sanga.

  Alisema kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 500 na nyingine zisizo za moja kwa moja na kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya viwanda vingine.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga (wa pili kushoto), akisaini mkataba wa makubaliano ya uwekezaji katika Kiwanda cha Machinjio ya kisasa na Usindikaji Nyama cha Nguru Wilayani Mvomero.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga (wa pili kushoto), akibadilishana hati na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zubair Corporation ya Oman, C.S. Badrinath, baada ya kusaini makubaliano ya uwekezaji katika machinjio ya kisasa ya Nguru.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Clliford Tandari (katikati), akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni wa LAPF, Eliud Sanga, baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya uwekezaji katika Kiwanda Machinjio ya kisasa na Usindikaji Nyama.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliud Sanga akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa Uwekezaji katika Kiwanda cha Machinjio ya kisasa na Usindikaji wa Nyama cha Nguru 'Nguru Hill Ranch Ltd' kilichopo Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Zubair Corporation ya Oman, C.S.Badrinath na katikati ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Clliford Tandari.
   Baadhi ya wadau walioshiriki katika hafla hiyo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  NEC -  Dar es salaam.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteua Ndugu Rehema Juma Migilla kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) ,kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Hindu Hamisi Mwenda aliyefariki  dunia Septemba 1, 2017.


  Akizungumzia uteuzi huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amesema kuwa Tume imemteua Ndugu Rehema Juma Migilla mara baada ya kupokea taarifa ya kuwepo kwa nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kutoka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Amesema kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 Mhe. Spika aliitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu kuwepo kwa nafasi wazi ya mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi CUF baada ya aliyeteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Malum kupitia chama cha CUF Ndugu Hindu Hamis Mwenda kufariki dunia.


  Katika hatua nyingine Mkurugenzi  huyo amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 86 A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa imewateua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum watatu (3) kujaza nafasi wazi za madiwani katika Halmashauri tatu za Tanzania Bara.


  Madiwani walioteuliwa ni Ndugu Jane I. Chungwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Rosana S. Mwinyi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Ndugu Pili M.Mfaume kupitia Chama Cha Wananchi CUF kutoka Halmashauri ya Temeke.


  Amesema uteuzi huo umefanyika baada ya Tume kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 aliitarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu uwepo wa nafasi wazi za madiwani.


  0 0  0 0

  Taarifa iliyotufikia hivi punde, inaeleza kuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Mawakili cha Tanganyika (TLS), Tundu Antipus Lissu ameshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa akitoka nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu. 

  Taarifa zaidi zitawafikia kadri tutakavyokuwa tukizipa.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt.Jose Graziano da Silva alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt.Jose Graziano da Silva alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).Dkt.Jose Graziano da Silva baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo alipofika Ikulu Mjini Unguja. Picha na Ikulu, Zanzibar.

  0 0

  Efm redio inatarajia kuzima kiki zote kwa kuwasha muziki wilaya ya Kigamboni, siku ya Jumamosi ya tarehe 9/9/2017 katika Bar ya G5 ikiwa ni muendelezo wa tamasha la Mziki Mnene lililoanza wiki mbili zilizopita ambapo burudani ya muziki kutoka kwa RDJs wa EFM na wasanii mbalimbali akiwemo Sholo Mwamba, Yuda msaliti, Daina Nyange, Timbulo na wengine wengi watakiamsha katika Bar hiyo.

  Na katika kuipa kipaumbele michezo, na kuinua vipaji vya vijana katika uimbaji, Efm itatafuta vipaji vya muziki wa Singeli “Singeli Michano” katika Kiwanja cha Machava ambapo mshindi katika kila wilaya atapata fursa ya kurekodi nyimbo bure, Ikifuatiwa na mechi ya kirafiki kuanzia saa 10:00 Jioni baina ya timu ya EFM na KOC Veterans katika uwanja wa Kibugumo –Kigamboni na Asubuhi Efm jogging itajumuika na jogging club za Kigamboni kukata wese na kuweka mwili fresh kwa mbio za mwendo pole.

  Vilevile wakazi wa Kigamboni watapata nafasi ya kujumuika, kujadili mambo kadha wa kadha na watangazaji mahiri wa kipindi cha Joto la Asubuhi, Sports Headquarters, Uhondo, na Ladha 3600 katika kiwanja cha MACHAVA siku ya Ijumaa tarehe 8/9/2017 kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 9:00 Alasiri ambapo vipindi hivyo vitarushwa live kutoka uwanjani hapo.
  Efm mziki mnene, zima kiki washa muziki.

  0 0

  Na Tiganya Vincent, Sikonge.

  MKUU wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Sikonge ameagizwa kuchunguza tukio la Polisi mmoja wilayani humo kumtolea lugha ya kejeli mwananchi akimhusisha na  Mkuu wa Wilaya hiyo mapema mwezi Aprili mwaka huu.

  Uamuzi huo umetolewa leo mjini Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri baada ya Mkazi mmoja wa Sikonge Hidaya Hussein kumweleza kiongozi huyo wakati akisikiliza kero mbalimbali za wananchi.

  Hidaya alisema kuwa mnamo Aprili 26 mwaka huu alitoka kwake kwenda katika kibanda kuangalia Sherehe za Muungano kwenye runinga na aliporejea alikuta Polisi wamevunja mlango wake na kuingia ndani ya nyumba yake bila ya yeye kuwepo na kupekua bila kuona kitu kibaya.

  Alisema kuwa baada ya kukuta tukio hilo aliamua kwenda katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya lakini akiwa njiani kuna mtu akamshauri aanzie kwa OCD na ndipo alipofika Polisi na kumkutana Mkuu huyo wa Polisi aliyempangia mtu wa kumsaidia. Hidaya alisema kuwa wakati akiwa anaendelea na mahojiano ndipo Polisi aliyepangiwa kumsaidia alitoa kauli ya kumkejeli yeye na  DC jambo lililomuuma sana kwa sababu alikuwa akidai haki yake.

  Mkazi huyo alinukuu baadhi ya maneno aliyomtamkia “Ulitaka kwenda kwa Mkuu wa Wilaya kushitaki …unadhani tunamuogopa Mkuu wa Wilaya…kwanza ujui na wewe tunaweza kukuwekea bangi kisha tukukamate”
  Hidaya alisema kuwa nia yake ya kwenda Polisi ilikuwa ni kutaka kujua kwanini waliendesha upekuzi wakati hayupo na kama walihisi kuna shida wangeweza kuwatuma watoto wamfuate alipo. Alisema kauli hiyo ilimuuma sana na baada ya kusikia Mkuu wa Mkoa wa Tabora anakuja kuwasilikiza akamua kwenda kufikishia kilio chake.

  Akijibu hoja hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya kumtafuta Polisi aliyetoa lugha hiyo na kumchukulia hatua na kuongeza kuwa kwa sababu mwananchi anamjua mhusika gwaride la utambuzi lifanyike. Alisema kuwa hawezi kuacha tabia hiyo iendelee kwani mtumishi kama ameonyesha dharau kwa Mkuu wa Wilaya ni sehemu ya kuelekea kumdharua yeye (RC).

  "Kama askari huyo au hawa wametoa lugha hiyo ya kumdharau Mkuu wa Wilaya , hiyo ni njia ya kuelekea kunidharau mimi ... siwezi kukubali ni lazima askari hao watafutwe na wachukuliwe hatua" alisema Mwanri.
  Aidha alisema kuwa alimwagiza OCD kuhakikisha Hidaya na wananchi waliojitokeza kueleza kero wanazofanyiwa na baadhi ya watumishi walindwe.

  Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri alisema hawezi kuvumilia kuona kuna watumishi watoa matamshi yanayonyesha dharua kwake na kwa wananchi. Alisema kuwa watakaobaika atamuchukulia hatua ikiwa ni pamoja na kumuondoa katika wilaya anayoingoza mwenyewe.

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora baada ya kumaliza zoezi la kusikiliza kero za wakazi wa Sikonge anatarajia kuendelea na Wilaya nyingine.

  0 0

  Mshindi wa Promosheni ya Tusua Mapene, Abdallah Mwalemba ambaye ni dereva wa magari makubwa, akipokea kitita cha Shilingi Milioni 7/- toka kwa Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu (kulia)wakati wa hafla fupi iliyofanyika Dar es Salaam leo.Katikati ni Meneja wa Vodashop Tawi la Mlimani City, Vanessa Mlawi, Ili Mteja aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu (kulia) akimkabidhi mshindi wa Promosheni ya Tusua Mapene, Octavian Ngosongo ambaye ni fundi magari wa Mabibo jijini Dares Salaam, kiasi cha fedha taslimu Sh. milioni 2/- alizojishindia kupitia promosheni hiyo, Dar es Salaam leo.Katikati ni Meneja wa Vodashop Tawi la Mlimani City, Vanessa Mlawi,Ili Mteja aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.
  Washindi wa Promosheni ya Tusua Mapene inayoendeshwa na Vodacom Tnzania PLC, Octavian Ngosongo (kushoto) na Abdallah Mwalemba,wakipongezwa kwa kupigiwa makofi na Meneja wa Vodashop Tawi la Mlimani City,Vanessa Mlawi(katikati)baada ya kukabidhiwa vitita vyao na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Matina Nkurlu (kulia), Dar es Salaam leo walivyojishindia kupitia promosheni hiyo, Ili Mteja aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.

older | 1 | .... | 1899 | 1900 | (Page 1901) | 1902 | 1903 | .... | 3272 | newer